WhatsApp ni mtandao unaoleta pamoja watu kupitia groups, channels na kurahisisha sana mawasiliano. Ni moja ya mitandao mkubwa ulimwenguni milikiwa na Meta. Unatumiwa na watu kuwasiliana na watu wengine walio ndani na nje ya nchi.
Kwenye mtandao wa WhatsApp Kuna vipengele vingi sana mtu unaweza tumia katika kuungana au kuwasiliana na watu wengine. Katika vipengele hivyo, Kuna kipengele kinaitwa “WhatsApp screen share”.
WhatsApp screen share ni kipengele cha WhatsApp kinachowawezesha watumiaji wa WhatsApp kuoneshana Screen za simu zao. Kupitia kipengele cha hiki cha WhatsApp, unaweza kumuonesha mambo yalio katika kioo cha simu yako mtumiaji mwingine wa WhatsApp. Lakini hii inafanyika pindi mnapopigiana video call.
WhatsApp ilikuja na kipengele hiki cha WhatsApp screen share rasimi mwaka 2023 lakini huduma kama Google meet na Zoom zina uwezo kama huu pia. Katika makala hii, tutajikita katika huduma ambayo inapatikana kwenye mtandao wa WhatsApp.
Jinsi ya kutumia kipengele cha “WhatsApp screen share”
Ukiwa unataka kumuonesha mambo yalio kwenye screen ya simu yako mtu mwingine kwa kutumia WhatsApp Screen share, fuata hatuna zifuatazo;
Mpigie au akupigie Video call
Mukianza video call, bonyeza Vidoti vitatu
Changua “Share screen” kwenye chaguzi zitakazotokea.
Baada ya hapo, utatakiwa kukubali kuwa Kila kinachofanyika kwenye screen ya simu yako, kionekane kwa yule mtu ulienae kwenye video call.
Ukikubari tu, WhatsApp wataanza kuionesha screen yako kwa yule mtu ulienae kwenye video call.
Kupitia kipengele hiki, unaweza kumuonesha mtu movie/video zililopo kwenye simu yako, kumfundisha Baadhi ya vitu kupitia simu yako na hata rekebisha matatizo kwa kufuata muongozo wake.
Baadhi ya watu hutumia WhatsApp bila kujali usalama wa akaunti zao. Kujali usalama wa akaunti ya WhatsApp ni jambo muhimu sana maana kunaweka mambo yako katika hali ya usalama na vile vile unakua unawakinga watu unaowasiliana nao wasipate matatizo kupitia namba yako.
Akaunti ya WhatsApp inatakiwa kulindwa maana inaweza vamiwa na watu wabaya katika mitandao waitwao “hackers” au “Wadukuzi”. Baada ya akaunti yako kuvamiwa na watu hawa, unaweza kuwa unaendelea kuitumia bila kujua au unaweza ipoteza ghafla kwa kushindwa kuingia kwenye akaunti hiyo. Kiufupi hii inategemeana na njia waliotumia kuivamia akaunti yako na kufanikiwa kuingia.
Kwaiyo moja ya dalili kubwa ya kuwa imevamiwa, ni kukuta akaunti yako inafanya mambo ambayo haufanyi. Mfano unaweza kuta sms zimetumwa kwa watu lakini binafsi wewe haukuzituma. Mbali na dalili za mtindo huo, kukuta unashindwa kuingia kwenye akaunti ghafla ni moja dalili za kwamba akaunti yako inaweza kuwa imedukuliwa.
Lakini haya maswala hayatakiwi kukuogopesha ila unatakiwa kuwa makini katika kuzingatia usalama wa akaunti yako. Kuna mambo mengi tuliyajadili katika makala ilioelezea jinsi ya kuangalia kama akaunti ya WhatsApp ni salama au laa. Kama haukusoma makala hii, unaweza ipitia ukaelewa zaidi juu ya hilo.
Kuvamiwa na kuilinda akaunti yako ya Whatsapp kwa sasa
Hapa tuzungumzie namna ambayo watu wengi hupoteza akaunti zao za WhatsApp Katika kipindi hiki.
Katika mitandao, kuna link ambozo unaweza bonyeza ukapelekwa kwenye kurasa, zikakudai namba ya simu ya WhatsApp na baada ya kuweka namba, unapokea sms kwenye simu yako ambayo ina Code ambazo wanasema uwape ili kuthibitisha. Ukiwapa hizo code tu, akaunti yako ya WhatsApp inakuzuia usiingie na hata ukifanikiwa kuingia unaweza kuta mambo wengi ambayo hauja yafanya wewe yamefanyika au yanaendelea kufanyika.
Mbali na kubonyeza Link za mtandaoni, unaweza fuatwa na mtu tatika mitandao na akakuomba umpe Code ulizopokea kwenye simu yako alafu ukimpa tu, unapoteza akaunti.
Kuilinda akaunti yako dhidi ya njia hii ya uvamizi
Kuepuka kuvamiwa kwa akaunti yako kupitia njia hii, hakikisha hauweki namba yako ya simu kwenye tuvuti au kurasa ambazo haujazijua kiundani. Ukibonyeza Link ambayo hauimani na ikakudai namba yako, usiweke maana unaweza kuwa ni mtego wa kupoteza akaunti yako. Mara nyingi huwa wanadanganya kupata pesa za bure au vitu vingine vya Bure.
Pia kujiweka salama zaidi, hakikisha unakua makini na akaunti za rafiki zako unaochati nao. Kama utaona akaunti ya rafiki yako inafanya vitu ambayo sio kawaida yake kufanya, fahamu kuwa anaweza kuwa amevamiwa.
Mbali na hayo, unasisitizwa kutumia WhatsApp zilizo rasimi ili kujihakikishia usalama zaidi. Whatsapp nyingi zisizorasmi huwa sio salama kwa akaunti yako.
Jambo la kufanya ili kuirudisha akaunti ya WhatsApp iliochukuliwa.
Uzuri wa WhatsApp ni kwamba unaweza irudisha akaunti yako kwa kutumia namba ya simu. Hakikisha unaiingiza namba yako ya simu kwenye WhatsApp yako ili utumiwe tena Code alafu baada ya hapo utazijaza Code walizokutumia kisha utafanikiwa kuingia kwenye akaunti yako tena.
Ukikuta akaunti yako imezuiwa na WhatsApp (banned), unaweza toa maelezo kwenye kisanduku cha ku-request review. Utaeleza kuwa akaunti yako ilidukuliwa, umepambana kuirudisha lakini umeikuta banned (ni vizuri ukiandika maelezo hayo kwa kiingereza). Wakiangalia vizuri maelezo yako na kulinganisha mambo yaliotokea kwenye akaunti yako, wataondoa ban na kuruhusu uitumie kama kawaida.
WhatsApp Status views tunaweza sema ni idadi ya watu walioangalia au kuona status ya WhatsApp. Kipengele cha stutus katika WhatsApp kinakuruhusu mtumiaji wa WhatsApp kushiriki vitu na watu wengine kama vile picha, video au Audio.
Ili mtu kuona vitu ulivyoweka kwenye kipengele cha WhatsApp status ni lazima uwe umetunza namba yake kwenye simu yako na yeye pia we ameitunza namba yako. Ikiwa mmoja wenu atakua hajatunza namba ya simu, status hazitaonekana kwa yoyote kati yenu.
Lakini usipoona status ya mtu au asipoonekana kuwa ameangalia stutus, haina maana hajatunza namba yako. Anaweza kuwa mtu huyo hajaposti status ndio maana haujaiona status yake. Pia anaweza kuwa anatumia kipengele cha WhatsApp cha kuzuia usijue anapoangalia status zako. Kipengele hii wemewahi zungumzia katika ukurasa mwingine wa The bestgalaxy.
Kumekua na maswali mengi watu huuliza juu ya jinsi au namna ya kuongeza Stutus views. Jambo hili kwa sasa ni rahisi sana maana kila mtu anajua kuwa kadri jinsi unavyoongeza namba za watu kwenye simu yako ndivyo unaweza pata watu wa kuangalia status zako na pia utakua na uwezo wa kuangalia status zao. Kwaiyo kitu muhimu hapa ni kuungana na watu wengine wanaotumia WhatsApp.
Hapa chini, The Bestgalaxy tunaenda kukupata mambo machache yanayoweza kukusaidia katika safari yako ya kupata views nyingi katika WhatsApp status.
Mambo yanayokupa views nyingi kwenye status za WhatsApp
Kuungana na watu wengi kwenye WhatsApp
Ili kupata views nyingi, unatakiwa kuwa na watu wanaoangalia status. Sasa inamaana unatakiwa kwanza uungana na watu wako wa karibu kwenye WhatsApp. Yaani uchukue namba zao za simu na pia wachukue zako. Kama unamarafiki, ndugu, wateja au watu mnaojuana basi itakua vizuri ukichukua namba zao na kuwa nao pamoja kwenye WhatsApp. Jambo hili ni lakawaida kwa sasa, watu wengi wanapenda kuungana kwenye WhatsApp hivyo ni jambo rahisi.
Kupost mambo mazuri
Kwenye status za WhatsApp unaweza weka kitu chochote kisichovunja sheria za WhatsApp. Hivyo unaweza weka kitu chochote unachojiskia na watu wakakiangalia.
Lakini watu waoangalia status zako kunavitu ukiweka wanaweza wasivipende au visiwavutie kufungua status zako mara kwa mara. Kutokana na hili, kama unataka watu wengi wa view status zako ni vema ukawa unaposti vitu vizuri vitakavyo wafurahisha hata wao na sio kinacho kufurahisha wewe tu. Weka mbali majungu na matusi alafu jaribu kuposti mambo kama vichekesho, ushabiki wa mpira na vitu vingine vya kufurahisha.
Kuweka Video au Picha chache
Kuposti video nyingi au picha nyingi kwenye status za WhatsApp kunaweza punguza views. Unaweza fanya hivi mara chache isiwe na madhara lakini ukiweka kama ni tabia yako, kuna jinsi watu wanaweza anza kupuunza status zako Kwasababu ya kuokoa muda au bando.
Jaribu kuweka vitu vichache kwa siku kwenye WhatsApp status yako ili kuongeza status views. Watu wana status nyingi sana za kuview siku hizi. Hivyo jaribu kuweka stutus zitakazo wachukua dakika chache kuzimaliza.
Kujihusisha na WhatsApp stutus za watu wengine
Kama haupo kibiashara (upo kama mtu binafsi) jiwekee tabia ya kutoa maoni kwenye status nzuri za watu wengine. Jihusishe na status za WhatsApp za watu wengine alafu wakipenda, wanaweza anza kujihusisha na zako. Kama unawatu wengi inaweza kua ni ngumu, lakini ukiweza itakua ni jambo zuri pia.
Kwakufuata mambo haya unaweza kuwa ni mtu mwenyewe mafanikio katika kupata views nyingi kwenye status za WhatsApp. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy na usichoke kuitembelea.
Kubadilisha namba ya WhatsApp inaweza kuonekana kama kazi ngumu na yenye kuleta wasiwasi wa kupoteza mazungumzo yako muhimu, picha, video, groups na vitu vingine. Lakini, ukifuata hatua sahihi, unaweza kufanya mabadiliko ya namba kwa urahisi bila kupoteza chochote. Ni muhimu kwa kila mtumiaji wa WhatsApp kujua njia sahihi ya kubadili namba ili kuepuka kupoteza vitu muhumu.
Wapo watu ambao hubadilisha namba bila kutumia njia sahihi na huishia kupoteza vitu muhumu. Kwa kuliona hilo The bestgalaxy, tumeamua kuwasaidia watu hawa na watu wengine wasio jua njia sahihi.
Katika makala hii, tunakupa hatua za jinsi ya kubadilisha namba yako ya WhatsApp bila kupoteza data yako(Android). Kama hajui kuhusu hili na unataka kubadilisha namba, hapa utapata mwongozo wa kufanikisha unachohitaji. Lengo ni kuhakikisha unafanya mabadiliko haya kwa usalama, huku ukiendelea kufurahia matumizi yako ya WhatsApp.
Jinsi ya kubadilisha Namba ya WhatsApp bila kupoteza Vitu (Android)
Kwanza unatakiwa kujua kuwa Akaunti yako ya WhatsApp na namba yako ya simu ni vitu viwili tofauti. Unapotumia WhatsApp inamaana una Akaunti ya WhatsApp iliofungukiwa kwa namba ya simu. Na namba ya simu inaweza badilishwa bila kubadilisha akaunti yako ya WhatsApp. Hii itakufanya usipoteze vitu vyako(Chats, Groups, na vingine). Kufanya hivi, fuata hatua zifuatazo;
Ingia kwenye WhatsApp na ubonyeze Vidoti vitatu vilivyopembeni juu.
Chagua “Settings” kwenye orodha ya chaguzi utazoziona.
Chagua “Account” kwenye chaguzi zitazokuja tena Kisha bonyeza “Change number”.
Bonyeza kitufe kilichoandikwa “Next” Kisha andika namba mpya na namba ya zamani kwenye ukurasa utaoletewa.
Baada ya kuandika namba kwa usahihi utatakiwa kubonyeza “Next” ili kuendelea na uthibitisho namba hizo. Utatakiwa kuthibitisha namba hizo kwa kupokea code watakazozituma. Ukiweza kuthibitisha, WhatsApp wataweza kubadilisha Namba yako na kama utashindwa kuthibitisha, hautaweza kubadili namba.
Uzuri wa kubadilisha Namba kwa njia hii ni kwamba, Rafiki zako na watu wengine ulioungana nao kwenye WhatsApp watajulishwa. Wataambiwa kuwa umebahatisha namba alafu watapewa na namba yako mpya ya WhatsApp. Epuka kufanya mabadiliko kama haya kama hutumii WhatsApp rasimi.
WhatsApp inatuwezesha watu kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki mtandaoni. App hii ina vipegele vingi na moja kati ya vipengele vyake kuna kipengele kinaitwa “Link a device”. Kipengele hiki kinamuwezesha mtumiaji wa Whatsapp kuunganisha akaunti ya WhatsApp kwenye vifaa viwili mpaka vinne. Baada ya kuunganisha WhatsApp kwenye vifaa hivyo sms na vitu vingine vingi vitakua vinaonekana kwenye simu zote hata zikiwa mbali. Na kila kifaa kitakua na uwezo wa kutumika kujibu na hata kufuta sms.
Kama ni mtu mwenye simu mbili na unahitaji kuona sms zako za Whatsapp kwenye simu nyingine bila kuigusa unaweza fanya hivyo kwa kutumia kipengele cha Whatsapp kiitwacho “Link a devices”. Hapa chini tunakupa mwanga juu ya jinsi unavyoweza kufanya kuungalisha na kuanza kuona sms za Whatsapp kwenye simu nyingine bila kuigusa. Hakikisha hautumii kipengele hiki kialifu.
Jinsi ya kuunganisha na kuona sms za WhatsApp kwenye simu nyingine bila kuigusa
Chukua simu zote mbili za smartphone na uziunganishe kwenye internet(ziwe na bando). Simu yenyewe unataka kuangalizia sms tutaiita simu ya pili, simu ambayo ina sms unazotaka uwe unaziona tutaiita simu ya kwanza. Baada ya kuziweka sawa simu hizo, fuata yafuatayo:
Chukua simu yenyewe unataka kuangalizia sms kwenye simu nyingine(simu ya pili) alafu ufungue web browser (Chrome) na kwenda katika website ya WhatsApp web ambayo ni https://web.whatsapp.com/
Baada ya kufanya hivyo, washa “Desktop site” kwenye hiyo web browser.
Baada ya kufanya hivyo, refresh ukurasa wa WhatsApp web alafu utaona kibox Cha QR code kimetokea kwenye ukurasa huo.
Baada ya kufanya hayo kwenye simu yako ya pili, sasa uchukue simu yenyewe itakua na sms unazotaka kuziona(simu ya kwanza) kisha fungua app ya WhatsApp.
Ukishafungua app ya WhatsApp, bonyeza vidoti vitatu vilivyo upande wa juu alafu chagua “Linked devices”.
Baada ya hapo utatupwa kwenye ukurasa wenye kitufe kilichoandikwa “Link a device”. Kibonyeze hicho kitufe alafu kamera ya simu hiyo itafunguka na utatakiwa kuitumia kamera hiyo kuscan QR code zinazooneshwa kwenye kile kibox kwenye simu nyingine. Ninaposema kuscan nnamaana elekeza hiyo kamera kwenye kibox kilichopo kwenye ukurasa wa WhatsApp web uliufungua kwenye ile simu nyingine.
Ukisha scan itaunganisha akaunti hiyo ya Whatsapp alafu utaandika jina lolote la kwenye sehemu ya device name itakayo jitokeza uijaze na kusave.
Baada ya hapo, utaanza kuona sms za Whatsapp kwenye simu zote mbili hata ukiwa mbali. Kiufupi utakua umefanikiwa kuziunganisha na utakua na uwezo wa kuangalia sms za Whatsapp za simu ya kwanza kwenye simu ya pili kupitia https://web.whatsapp.com/ ambayo ambayo inaitwa “WhatsApp web”.
Yani ukitaka kuangalia sms za WhatsApp za simu nyingine bila kuigusa, utaingia https://web.whatsapp.com/ kupitia Web browser yako na kuwasha “Desktop site” kwenye hiyo web browser ( Chrome) bila kuscan tena mara ya pili.
Ukifanya hivyo tu, moja kwa moja sms za simu ya kwanza utaziona kwenye simu ya pili kwa muonekano huu chini.
Hatua hizi zinaweza kuwa ngumu kama sio mtu unaejua sana vipengele vya simu. Lakini nadhani wengi wanaekewa vipengele vyote nilivyoelezea.
Mwisho; muunganiko huo utakatika endapo simu ya kwanza yenye sms itakua haijawa online kwa siku ya 14, ambazo ni sawa na wiki mbili.
Kuwa mjanja! Tufuate kwenye akaunti zetu mpya za kijamii ; Instagram na Facebook
WhatsApp ni app inayotumika na watu wengi na app hii inavipengele vingi ikiwemo kipengele cha status. Kipengele cha status huwezesha watu kushiriki hali zao na watu wengine. Kuiona status ya mtu kwenye WhatsApp utatakiwa kuwa na namba ya huyo mtu na yeye kuwa na namba yako. Na endapo ukiiangalia/ukiview status ya mtu, ataona kuwa umeangalia status yake.
Sasa Kuna baadhi ya watumiji wa WhatsApp huwa wanataka kujua jinsi ya kuview status ya mtu na isionekane kuwa wameona kwa aliepost. Hapa The bestgalaxy tunaenda kukufungua juu ya hili kwa kukupa njia nzuri na salama ya kuanaglia au kuview status ya mtu bila kuonekana umeona.
Jinsi ya kuview Whatsapps status bila kuonekana umeona
Kuview Whatsapp status ya mtu bila kuonekana kunawezekana kufanyika kwa njia zaidi ya moja lakini njia nyingi sio salama kwa akaunti yako ya WhatsApp maana zinaweza kufanya uzuiwe kutumia WhatsApp. Njia salama ya kuview Whatsapp status ya mtu bila kuonekana ni kuzima “Read receipts” kwenye app yako rasimi ya whatsApp. Fuata hatua zifuatazo kufanya hivyo.
Fungua App yako ya WhatsApp na uguse vidoti vitatu vilivyo juu kulia.
Chagua “Settings” kwenye orodha ya chaguzi zitakazo jitokeza.
Baada ya hapo ingia katika sehemu ilioandikwa “Privacy” na uzime kipengele kilichoandikwa“Read receipts”
Baada ya kuzima kipengele cha hicho utakua na uwezo wa kungalia status za watu bila wenyenazo kujua. Kwaiyo ukizima, unaweza kuview status bila kuacha nyayo.
Kipengele hiki ni kipengele salama na hakiwezi pelekea akaunti yako ya Whatsapp kufungwa na Whatsapp. Lakini ubaya wake ni kwamba ukikizima huwa kinafanya usijue watu wanapoangalia status zako au kujua kuwa wamesoma sms ulizowatumia. Na wala wewe hautaweza kuonekana kama umesoma sms zao.
Kutokana na jambo hili unashauriwa; ukisha maliza kuangalia status ya mtu ambae hutaki ajue umeangalia, kiwashe tena hicho kipengele cha “Read receipts”.
Njia hii ni njia nzuri kuliko kutumia app za WhatsApp zisizo rasimi zilioweka urahisi katika kuangalia status bila kuacha nyayo. App hizo zinazoweza pelekea WhatsApp kuzuia akauti yako na ndio maana hatupendekezi japo unaweza tumia pia.
Whatsapp ni mtandao mkubwa ulimwenguni ambao watu huutumia sana katika mawasiliano. Unaweza kuwa ni mtandao wako pendwa katika mawasilioano ndio maana upo hapa… Endelea kuwa karibu na The Bestgalaxy, utajifunza vingi kuhusu mtandao huu.
Whatsapp ni mtandao mzuri kuutuumia katika kuwatumia watu Picha, Video, Audio au ujumbe wa maneno lakini unapofanya hivyo tambua kuwa kunajinsi ambavyo mtu mwingine anaweza kuona vitu vyote hivyo kwenye simu au kifaa chake bila wewe kutambua(kisiri). Kuna njia ambazo hata mtu asiebobea sana katika maswala ya Teknolojia anaweza tumia kuona sms au vitu unavyofanya kwenye Whatsapp. Lakini jambo hili lisikutishe maana hapa chini tunakwenda kukujuza jinsi ya kuangalia kama upo salama na jinsi ya kujilinda pia… Kwaiyo ondoa hofu na endelea kutumia Whatsapp yako kama kawaida.
Jinsi ya kujua mtu mwingine anaona sms na vitu unavyofanya WhatsApp kisiri
Whatsapp kwa sasa inakuruhusu mtumiaji wake kuunganisha akaunti yako moja ya Whatsapp kwenye kifaa zaidi ya kimoja. Unaweza fannya akaunti yako moja ya WhatsApp iwe inatumika kwenye simu mbili mpaka 4 na namba ikawa hiyo hiyo moja. Mtu mingine anaweza kuitumia hii kunganisha akauti yako kwenye simu yake au kifaa chake na kuanza kukuchunguza unachofanya bila wewe kujua. Na mtu akitumia ataweza kusoma sms zako, kujibu, kuona na kuchua audio,video na vitu vingine unavyotuma na kutumiwa bila wewe kujua.
Ukitaka kujua kama akaunti yako ya Whatsapp imeunganishwa fanya yafuatayo:
Fungua Whatsapp yako na uguse Vidoti Vitatu
Ukifanya hivyo, Chagua “Linked divices”
Baada ya kufanya hivyo utatupwa kwenye ukurasa ambao ukikuta kuna kifaa chochote kiorodheshwa basi jua whatsapp yako sio salama. Na kama hamna kifaa basi yawezekana upo salama. Unaweza angalia picha hapa chinikuelewa zaidi.
Endapo utakuta akaunti yako ya Whatsapp sio salama(hacked) unaweza gusa kifaa kilicho orodheshwa kwenye kwenye ukurasa huo alafu ukagusa vidoti vitatu itakavyoonekana juu kulia kisha utachagua “Remove device”.
Ili kuhakikisha kuwa WhatsApp yako iko salama kila mara, hakikisha unafanya kuangalia kama akaunti yako ya WhatsApp imeunganishwa mara kwa mara hasa baada ya kumruhusu mtu mwingine aishike simu yako bila uangalizi wako.
Whatsapp ni mtandao unaotumiwa na watu wengi sana na umekua na msaada mkubwa kwa watu katika swala la mawasiliano. Katika kutumia mtandao huu unaweza kupambana na changamoto au vitatizo vidogo vidogo, hasa katika app za simu. Changamoto au matatizo huwa hayatokei mara kwa mara lakini hapa The bestgalaxy tumekuandalia orodha ya matatizo au changamoto unazoweza kutananazo katika kutumia whatsapp na maelezo ya jisi ya kutatua. Hii inaweza kuwa msaada pindi mtu unapokumbana na changamoto hizo. Pia usisahau kuungana nasi kwenye WhatsApp namba 0622586399.
Changamoto au Matatizo kwenye kutumia Whatsapp na jinsi ya kutatua
Whatsapp ban
Kama upo banned/umezuiwa kwenye WhatsApp unaweza kuona hivi
Mtandao wa whatsapp unasheria zake ambazo ukikiuka katika kutuumia mtandao huu, wanazuia akaunti yako. Kutumia app za whatsapp zisizo rasimi ni moja ya jambo linaloweza kufanya akaunti yako izuiliwe Whatsapp. Nikizungumzia “Whatsapp zisizo rasmi” namaanisha app kama vile OG Whatsapp, GB Whatsapp au FM whatsapp. Mtandao wa Whatsapp una app rasmi mbili tu. App ya kwanza inaitwa “Whatsapp messenger” na ya pili inaitwa “Whatsapp business”… App yoyote mbali na hizo ni app isio rasmi na inaweza kufanya akaunti yako izuiwe/ifungwe na mtandao wa Whatsapp.
Ukiachana na kutumia app zisizo rasmi, unaweza fungiwa au kuzuiwa akaunti baada ya kufanya mambo mengine yasio faa katika Whatsapp au watu kutoa taarifa kwa Whatsapp kuhusu akaunti yako kujihusisha na jambo flani lisilo ruhusiwa kwenye Whatsapp.
kuna namna mbali za kuzuiwa; unaweza zuiwa na whatsapp kwa muda mfupi au kwa muda mrefu. Ukizuiwa kwa muda mfupi, baada ya muda flani akaunti yako itaondolewa kizuizi na mara nyingi huwa app inaonesha kabisa muda ambao akaunti itaachiliwa. Lakini ikizuiwa kwa muda mrefu huwa inachukua muda mrefu sana kuachiliwa… ukikumbana na kizuizi hiki unashauriwa kufungua akauti nyingine ya whatsapp kwa namba nyingine au kama unahisi wamekuonea, wasiliana nao kupitia Support@whatsapp.com tuma ujumbe wa kuelezea tatizo lako ili wakusaidie.
Backup katika whatsapp ni kipengele kinachokuwezesha kutunza sms za whatsapp na vitu vingine kwenye akaunti yako ya google drive ili iwe rahisi kupata au kurudisha sms na vitu hivyo pindi simu yako inapopotea au ukifuta app kwa bahati mbaya. Unaweza fungua whatsapp ukuta ghala tu wahatsapp imekuletea ujumbe unaoziba kioo kizima umeandikwa “Backup to Google drive” na kuna orodha ya chaguzi unazotakiwa kuzichagua pale. Kama hauelewi lolote kuhusu backup basi umaweza changua “Never” tu ili kuokeo muda na kuendelea kuitumia app yako ya Whatsapp.
Whatsapp kumaliza bando
Whatsapp ni moja ya app zisizotumia bando la internet sana ila kama wewe ni mtu unaetumia Whatsapp kwenye upande wa video sana basi app hii inaweza kutumia bando zaidi. Nikisema upande wa video namaanisha kutuma au kupokea video nyingi kwenye vikundi au watu wa kawaida, kutumia video call sana, kuangalia status za watu wengi wilio weka video kwenye status zao. Kuacha au kupunguza mambo hayo kutafanya Whatsapp isile bando lako sana.
Whatsapp inajaza picha na video nisizozitaka kwenye simu
Whatsapp inaweza kuwa inajaza picha na video usizozijua au usizozipenda kwenye simu yako. Kama hili ni tatizo, unaweza tatua tatizo hili kwa kuzima kipengele cha whatsapp kinacho iruhusu app ya whatsapp kuingiza kwenye simu video au picha zinazotumwa kwenye magroup au unazotumiwa. hii itafaya kila video au picha unayotumiwa kutojiingiza kwenye simu yako mpaka utakapo gusa kuidownload.
jinsi ya kufanya hivyo; fungua app yako ya whatsapp, gusa vidoti vitatu, chagua “Settings” kisha gusa “Storage and Data” alafu baada ya hapo ingia walipo andika “When using mobile data” na uondoe alama ya tiki kwenye vibox vyote au cha video na Photos tu. baada ya kufanya hivyo, bonyeza “Ok” na rudi nyuma kidogo kisha uingie kwenye “When connected on WiFi” alafu uondoe alama ya tiki katika vibox vyote au vibox vya “Photos” na “Videos” tu.
kama umekua unajikuta umeingizwa kwenye magroup ya Whatsapp na watu usio wajua bila hata taharifa na haupendi hali hiyo basi kunakitu unaweza fanya hapa. Kwenye Whatsapp kunakipengele kinakuruhusu kuzuia mtu ambae hauna namba yake kukuingiza kwenye group. Unaweza kutumia kipengele hiki kuzuia watu ambao hauna namba zao wasikuingize kwenye group lolote bila kukutaharifu.
jinsi ya kufanya hivi; Fungua Whatsapp, gusa vidoti vitatu, chagua “Settings” kisha gusa “Privacy”. Baada ya hapo, nenda eneo la chini kidogo uingie walipoandika “Groups” kisha chagua “My Contacts” alafu rudi nyumbani na uendelee kutumia app yako.
Nasumbuliwa na simu za watu nisio wajua
Whatsapp pia inakipengele cha kufanya watu watu ambano nambazao hazijawekwa kwenye simu yako wakikupigia usipate usumbufu. Mtu yoyote ambae anakupigia kwenye Whatsapp kwa namba ngeni, simu yako haita, itakua kimya tu bila kukusumbua. Kama ni mtu amabae huwa unapata simu nyingi kwenye Whatsapp toka kwa watu usio wajua na haupendi swala hiilo basi unaweza kutumia kipengele hicho kuondokana na jambo hilo.
Jinsi ya kufanya hivi; Fungua app yako ya Whatsapp, gusa vidoti vitatu, chagua “Settings” alafu bofya “Privacy”. Baada ya hapo, nenda chini kidogo uingie katika “Call” alafu washa palipo andikwa “Silence unknown callers”.
Kama huwa unaambiwa umuweke status kitu lakini unashindwa kwasababu mbalimbali na kupelekea kutoelewana kati yenu au unakitu unahitaji kuiweka status bila watu au mtu flani kujua basi leo nakufundisha jinsi ya kufanya hivyo.
WhatsApp status ni kipengele cha WhatsApp ambacho mtu hutumia kupost vitu mbalimbali ambayo huonwa na watu wengine walio na namba yake kwenye simu kama alivyo nazo zao yeye kwenye simu yake. Lakini unachotakiwa kujua ni kwamba katika kipengele hiki unauhuru wa kuchagua mtu au watu gani waone status yako na watu gani wasione… Hii inamaanisha unaweza chagua watu au mtu pekee unahitaji aone status yako kisha ukapost kitu kwenye status yako na akakina yeyetu.
Unaweza fanya hivyo kwa kufunya yafuatayo;
Fungua app ya WhatsApp kisha gusa vidoti vitatu vilivyo juu kulia.
Utakuta orodha ya maneno machache, Chagua “Settings” Kwakuigusa.
Katika settings utakuta orodha pia, Chagua “Account” Kwakuigusa na itakuletea orodha tena chagua “privacy”
Ukisha chagua privacy, utakuta orodha tena,Chagua neno “Status” Kwakuigusa Hapo utaletewa orodha hii:
My Contact My Contact except.. Only share with…
orodha hii inakidoti ambacho wewe unachagua kiwe katika nenolipi kati ya hayo.Na kidoti hicho utakikua kwenye “My Contact” wewe inabidi upeleke kwenye “Only shere with..” ukikipeleka hapo itakuletea namba za watu wako kwenye simu,inabidi umchague yule unaetaka aione hiyo status alafu gusa “Ok” kisha “Done” ukisha maliza nenda kaposti hiyo status, nenda kapost kitu anachotaka kwenye status yako na atakiona yeye tu!
Hapa tutaangalia vikundi vya WhatsApp ambavyo unaweza kujiunga. Sote tunajua kuwa vikundi vya WhatsApp ni muhimu sana kwa sababu watu huvitumia kuungana na wengine na kushiriki habari fulani au kujadili mambo mengi. Lakini unahitaji kujua kwamba kila mtumiaji wa WhatsApp anaweza kuunda kikundi cha WhatsApp na kuongeza watumiaji wengine kwenye kikundi. Hii inamaanisha kuwa unaweza pia kuwa na kikundi chako mwenyewe cha WhatsApp na kukifanya kama Msimamizi.
Ni rahisi sana, unachohitaji kufanya ni kufungua programu yako ya WhatsApp kisha uguse nukta tatu. Baada ya kugonga nukta Tatu, utapata orodha ya chaguo chache. Chagua “New group” ili kuanza kuunda kikundi chako mwenyewe. Kwenye kuliunda utatakiwa kuwachagua watu watu unaotaka wawe kwenye group. Unaweza kuchagua wale watu wote unahitaji wawekwenye group lako lakini tambua kuwa sio mtu anapenda kuungwa kwenye group bila tahalifa. Hivyo ni vema ukawatahalifu watu unaotaka kuwaweka kwenye group juu ya group unalotaka kuwaweka kwanza.
Yafuatayo ni magroup ya WhatsApp ambayo unaweza kujiunga nayo
Hapa nakupa orodha za vikundi vya WhatsApp ambavyo unaweza kujiunga badala ya kuunda kikundi chako cha WhatsApp. Hivi ni vikundi ambavyo unaweza kujiunga na kutumia lugha ya Kiswahili katika kuchati.
Unapaswa kujua kuwa, vikundi vyote vilivyoorodheshwa hapa vina watu kutoka sehemu tofauti na hatuna uhusiano wowote nao. Kwa hivyo hakikisha kuwa kila wakati unakuwa mwangalifu na walaghai au wanachama wengine ambao wanaweza kukosa nidhamu.