WhatsApp: kuview status ya mtu na isionekane umeona

WhatsApp ni app inayotumika na watu wengi na app hii inavipengele vingi ikiwemo kipengele cha status. Kipengele  cha status huwezesha watu kushiriki hali zao na watu wengine. Kuiona status ya mtu kwenye WhatsApp utatakiwa kuwa na namba ya huyo mtu na yeye kuwa na namba yako. Na endapo ukiiangalia/ukiview  status ya mtu, ataona kuwa umeangalia status yake.

Sasa Kuna baadhi ya watumiji wa WhatsApp huwa wanataka kujua jinsi ya kuview status ya mtu na isionekane kuwa wameona kwa aliepost. Hapa The bestgalaxy tunaenda kukufungua juu ya hili kwa kukupa njia nzuri na salama ya kuanaglia au kuview status ya mtu bila kuonekana umeona.

WhatsApp yako inatatizo? Jifunze jinsi ya kutatua BONYEZA HAPA>>>

Jinsi ya kuview Whatsapps status bila kuonekana umeona

Kuview Whatsapp status ya  mtu bila kuonekana kunawezekana kufanyika kwa njia zaidi ya moja lakini njia nyingi sio salama kwa akaunti yako ya WhatsApp maana zinaweza kufanya uzuiwe kutumia WhatsApp. Njia salama ya kuview Whatsapp status ya  mtu bila kuonekana ni kuzima “Read receipts” kwenye app yako rasimi ya whatsApp. Fuata hatua zifuatazo kufanya hivyo.

  • Fungua App yako ya WhatsApp na uguse vidoti vitatu vilivyo juu kulia.
  • Chagua “Settings” kwenye orodha ya chaguzi zitakazo jitokeza.
  • Baada ya hapo ingia katika sehemu ilioandikwa “Privacy” na uzime kipengele kilichoandikwa“Read receipts
  • Baada ya kuzima kipengele cha hicho utakua na uwezo wa kungalia status za watu bila wenyenazo kujua. Kwaiyo ukizima, unaweza kuview status bila kuacha nyayo.

Kipengele hiki ni kipengele salama na hakiwezi pelekea akaunti yako ya Whatsapp kufungwa na Whatsapp. Lakini ubaya wake ni kwamba ukikizima huwa kinafanya usijue watu wanapoangalia status zako au kujua kuwa wamesoma sms ulizowatumia. Na wala wewe hautaweza kuonekana kama umesoma sms zao.

Kutokana na jambo hili unashauriwa; ukisha maliza kuangalia status ya mtu ambae hutaki ajue umeangalia, kiwashe tena hicho kipengele cha “Read receipts”.

Njia hii ni njia nzuri kuliko kutumia app za WhatsApp zisizo rasimi zilioweka urahisi katika kuangalia status bila kuacha nyayo. App hizo zinazoweza pelekea WhatsApp kuzuia akauti yako na ndio maana hatupendekezi japo unaweza tumia pia.

Leave a comment