Kuna wakati unaweza tulia na kuamua kumfurahisha mpenzi wako kupitia simu. Kuna mambo mengi sana unaweza mfanyia kupitia hiyo simu na akafurahi. Inaweza kuwa ni unampigia mnaongea mambo mazuri, unamtumia picha na hata ujumbe tu wa maandishi.
Na tena sio lazima muwe mnaishi mkiwa mbali mbali ndio mtumie simu kumfurahisha. Unaweza mfurahisha mpenzi wako kupitia simu hata kama mnaishi nyumba moja. Kumtumia ujumbe mzuri asio utarajia kwenye simu yake ni jambo unaloweza fanya kama utani ila linaweza kufanya afurahi sana hatakama mnaishi pamoja.

The bestgalaxy tumekua mstari wa mbele kuhakikisha hauumizi kichwa sana kwenye mambo ya mahusiano. Katika ukurasa huu, tumekuandalia orodha ya ujumbe mzuri kwa mpenzi wako. Kama unahitaji kumtumia mweza wako ujumbe unaoeleza hisia za upendo ulionao kwake, basi unaweza chukua itayokufaa hapa.
Sms za kumwambia mpenzi wako kuwa unampenda BONYEZA HAPA>>>
Ujumbe mzuri kwa mpenzi wako (Mwanaume au Mwanamke)
- Unahisi kuna mwanaume anaependa mwanamke mzuri hivyo amkukose kisa mimi? Au wanawake wengine wanapenda unavyo kuwa na mimi? Hapana, hawapendi kuona tukipendana hao. Kuwa pamoja ni pigo letu kwao.
- Penzi lako hunisukuma kutaka nikuulize “Nikupatie nini hapa Duniani ufurahi?” lakini nakumbuka siwezi kupa kila kitu. Ila ningekua na wezo, ningekupa tu kama nilivyokupa huu moyo wangu wa pekee uwe nao wewe mpenzi.
- Sauti tamu ninayopenda kuisikia masikioni mwangu bila kuchoka ni Sauti yako. Mtu pekee ninaempenda bila kuchoka ni wewe. Kitu pekee ninachoweza pokea bila kuchoka ni penzi lako.
- Waliopita walinifundisha kuwa mapenzi ni maumivu na nisiamini mtu. Wewe umenifundisha maana sahihi ya mapenzi na radha yake hadimu. Umenifanya niwasahau mazima, nimekupenda na nakukuona wewe tu.
- Umenizamisha kwenye hisia za mapenzi mpaka najiona mimi na wewe tu kwenye Dunia. Na naogopa ila kwasababu nakuamini, naendelea. Nakupenda na naamini popote nikwa na wewe, sijapotea.
- Nashindwa kuelezea jinsi nakupenda ila hebu fikiria; kila nyota angani ingekua inawakilisha jinsi ninavyokupenda. Unahisi ningekua nakupenda kiasi gani?
- Niende nikaombe nini kwa jirani? Nikaombe Maji ili nikate kiu? Hapana, wewe tayari umeiweza kiu yangu. Siwezi hata kuiomba Asali kwao maana natosheka na vitamu unavyonipa malkia wangu.
- Kuna muda huwa nakosa kabisa furaha na Sababu za kufurahia maisha yangu. Ila nikikumbuka nina wewe maishani, furaha humwagika kama maji ya mvua moyoni.
- Usijiuze nakupendea nini mpenzi wangu. Utauchosha bongo wako Bure. Ninasababu nyingi sana za kukupenda wewe. Na hata ukiziondoa, bado nahisi Moyo wangu uliumbwa kukupenda wewe.
- Kabla ya kukutana na wewe, nilitamani kukutana na mtu kama wewe nimpende maishani. Sasa nimekupata, nakupenda na kwenye maisha umekua kama Nuru gizani.
- Najua kunamuda tunagombana au hatuelewani. Lakini tambua sijutii kukupata Ila najutia kuwa nawe mapema hapa Duniani. Moyo wangu unakupenda na umejaa mpaka akilini.
Katika orodha hii, Kuna ujumbe unaoweza kutuma kwa mwanamke na hata Mwanaume pia. Kwaiyo hii ni kwa watu wa jinsi a zote. Kikubwa hakikisha unatambua muda amambao utakua mzuri kwa mpenzi wako kupokea. Angalia na maana sahihi ya ujumbe ili mpenzi wako aelewe unacho maanisha unapomtumia.
Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy