Tag Archives: Swahili tech

Jinsi ya kuona sms za WhatsApp kwenye simu nyingine (Bila Kuigusa)

WhatsApp inatuwezesha watu kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki mtandaoni. App hii ina vipegele vingi na moja kati ya vipengele vyake kuna kipengele kinaitwa “Link a device”. Kipengele hiki kinamuwezesha mtumiaji wa Whatsapp kuunganisha akaunti ya WhatsApp kwenye vifaa viwili mpaka vinne. Baada ya kuunganisha WhatsApp kwenye vifaa hivyo sms na vitu vingine vingi vitakua vinaonekana kwenye simu zote hata zikiwa mbali. Na kila kifaa kitakua na uwezo wa kutumika kujibu na hata kufuta sms.

Kama ni mtu mwenye simu mbili na unahitaji kuona sms zako za Whatsapp kwenye simu nyingine bila kuigusa unaweza fanya hivyo kwa kutumia kipengele cha Whatsapp kiitwacho “Link a devices”. Hapa chini tunakupa mwanga juu ya jinsi unavyoweza kufanya kuungalisha na kuanza kuona sms za Whatsapp kwenye simu nyingine bila kuigusa. Hakikisha hautumii kipengele hiki kialifu.

Jinsi ya kuunganisha na kuona sms za WhatsApp kwenye simu nyingine bila kuigusa

Chukua simu zote mbili za smartphone na uziunganishe kwenye internet(ziwe na bando). Simu yenyewe unataka kuangalizia sms tutaiita simu ya pili, simu ambayo ina sms unazotaka uwe unaziona tutaiita simu ya kwanza. Baada ya kuziweka sawa simu hizo, fuata yafuatayo:

  • Chukua simu yenyewe unataka kuangalizia sms kwenye simu nyingine(simu ya pili) alafu ufungue web browser (Chrome) na kwenda katika website ya WhatsApp web ambayo ni https://web.whatsapp.com/
  • Baada ya kufanya hivyo, washa “Desktop site” kwenye hiyo web browser.
  • Baada ya kufanya hivyo, refresh ukurasa wa WhatsApp web alafu utaona kibox Cha QR code kimetokea kwenye ukurasa huo.
  • Baada ya kufanya hayo kwenye simu yako ya pili, sasa uchukue simu yenyewe itakua na sms unazotaka kuziona(simu ya kwanza) kisha fungua app ya WhatsApp.
  • Ukishafungua app ya WhatsApp, bonyeza vidoti vitatu vilivyo upande wa juu alafu chagua “Linked devices”.
  • Baada ya hapo utatupwa kwenye ukurasa wenye kitufe kilichoandikwa “Link a device”. Kibonyeze hicho kitufe alafu kamera ya simu hiyo itafunguka na utatakiwa kuitumia kamera hiyo kuscan QR code zinazooneshwa kwenye kile kibox kwenye simu nyingine. Ninaposema kuscan nnamaana elekeza hiyo kamera kwenye kibox kilichopo kwenye ukurasa wa WhatsApp web uliufungua kwenye ile simu nyingine.
  • Ukisha scan itaunganisha akaunti hiyo ya Whatsapp alafu utaandika jina lolote la kwenye sehemu ya device name itakayo jitokeza uijaze na kusave.
  • Baada ya hapo, utaanza kuona sms za Whatsapp kwenye simu zote mbili hata ukiwa mbali. Kiufupi utakua umefanikiwa kuziunganisha na utakua na uwezo wa kuangalia sms za Whatsapp za simu ya kwanza kwenye simu ya pili kupitia https://web.whatsapp.com/ ambayo ambayo inaitwa “WhatsApp web”.
  • Yani ukitaka kuangalia sms za WhatsApp za simu nyingine bila kuigusa, utaingia https://web.whatsapp.com/ kupitia Web browser yako na kuwasha “Desktop site” kwenye hiyo web browser ( Chrome) bila kuscan tena mara ya pili.
  • Ukifanya hivyo tu, moja kwa moja sms za simu ya kwanza utaziona kwenye simu ya pili kwa muonekano huu chini.

Hatua hizi zinaweza kuwa ngumu kama sio mtu unaejua sana vipengele vya simu. Lakini nadhani wengi wanaekewa vipengele vyote nilivyoelezea.


Mwisho; muunganiko huo utakatika endapo simu ya kwanza yenye sms itakua haijawa online kwa siku ya 14, ambazo ni sawa na wiki mbili.

Kuwa mjanja! Tufuate kwenye akaunti zetu mpya za kijamii ; Instagram na Facebook

Apple vision pro: Fahamu kuhusu Miwani hii ya Apple

Miwani ya VR(VR headsets) ni vifaa vya kisasa ambayo huvaliwa na watu na hufanya watu kuanza kuona mazingira ya kisasa au yalioundwa tofauti na mazingira ya ulimwengu halisi. Ukivaa Miwani hii unaweza kuona upo kwenye ulimwengu mwingine kabisa na ulimwengu ulio uzoea alafu utakua na uwezo wa kufanya vitu katika ulimwengu huo.


Makampuni mengi hujihusisha na utengenezaji wa Miwani hii ya VR ikiwemo kampuni ya Apple inayotoa simu za iPhone. Katika February 2, 2024 huko US, kampuni ya Apple ilitoa Miwani ya VR itwayo Apple vision pro. Miwani hii ilikua ikisubiriwa sana na watu wanaofuatilia mambo ya VR maana ilikua ikiongelewa sifa na mambo ambayo itakua nayo kabla Apple hawajaitoa.

Mambo kuhusu Apple vision pro

Apple vision pro imebeba vingi vizuri

Kwasasa Miwani hii imeisha toka na unaweza ipata kama bidhaa nyingine za Apple tunazozifahamu kutoka kampuni Apple. Baada ya Miwani ya Apple vision pro kutoka kumekua na mambo mengine yameongelewa kuhusu badhaa hii ya Apple. Machache kati ya mambo hayo ni yafuatayo.

Apple vision pro Ina vitu vingi vizuri tunavyoweza viongelea. Kwanza kabisa Miwani hii ina “eye and hand tracking”. Kupitia hii unaweza ivaa na kugusa au kuchagua vitu unavyooneshwa na Miwani hiyo bila kutumia kifaa kingine. Unaweza kuchagua au kugusa vitu kwakutumia macho tu au mikono yako bila kuwa na kifaa kingine chochote mkononi.

Kwenye kioo, Apple vision pro Iko na micro-OLED displays zenye pixels milioni 23, ambazo zitafanya ufurahie ubora wa picha za 4k kwenye Kila jicho.
Kwa usaidizi wa kamera, Apple Vision Pro inaweza kuunda Avatar ambae ataonekana unapowapigia kupiga video call watu wengine kupitia Miwani hiyo.

Kiufupi, Apple vision pro ni bidhaa nzuri sana toka kampuni ya Apple na imetikisa ulimwengu wa bidhaa za VR katika mwanzo wa mwaka 2024. Angalia video hii hapa chini.

Video ya Apple vision pro

Bei


Moja katika ya vitu watu wameongelea sana baada ya Apple vision pro kutoka ni bei yake. Ukihitaji kununua bidhaa hii kutoka kampuni ya Apple kwasasa itakuhitaji uwe na $3,499. Hiyo ndio bei yake katika Dola za kimalekani, ukiigeuza kibongo bongo(Tsh) inaweza kuwa kama milioni 8 na laki 9 hivi.

Kuna baadhi ya watu ikiwemo CEO wa kampuni ya Meta, Mark Zuckerberg wamezungumza kuwa ni ghalama sana kuliko Miwani ya Meta Quest 3 inayofanya baadhi ya vitu kama Apple vision pro japo haina ubora sana kwenye baadhi ya vitu pia. Miwani ya Meta Quest 3 inapatikana kwa Dola 499.99 za kimalekani.

Lakini Kuna waataalamu wameeleza kuwa Apple vision pro imeundwa nah baadhi ya vitu vyenye gharama kuliko Meta Quest 3, hivyo inaweza kuwa ni sawa kuwa na gharama kubwa.

Credit: Apple

Haipo vizuri kwenye games

Baadhi ya watu wanonunua miwani ya VR huwa wanapenda kutumia zaidi upande wa games. Kucheza VR Games kwenye Miwani ya VR kunaweza huwa kunafurahisha sana. Sasa Apple vision pro bado haiko sawa katika upande huu.

Hand tracking yake haiko vizuri sana ukilinganisha na Meta Quest 3 na haina game nyingi za VR unazoweza furahia kuzicheza. Pia hand tracking haiko vizuri sana kiasi cha kukufanya ufurahie zaidi kucheza game za VR. Ila Meta Quest 3 ndio imetajwa kuwa vizuri katika upande huu wa games kuliko Apple vision pro.

Inaendelea kuboreshwa

Apple vision pro ni bidhaa nzuri Toka apple lakini ni toleo la kwanza, yani “first-generation product”. Mara nyingi bidhaa toleo la kwanza huwa zinakuja na matatizo na madogo madogo madogo ambayo kampuni huwa inaangalia namna ya kutatua na kuboreshwa bidhaa yao hiyo au zijazo. Apple vision pro nayo ipo kuboreshwa na kampuni ya Apple ili iweze kuwa bora zaidi.

Ni hayo TU katika ukurasa huu, usiache kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mambo mengine zaidi.

Image credit: Apple

Mambo ya kuzingatia katika kununua bidhaa Mtandaoni (Online)

Kufanya manunuzi mtandaoni ni jambo watu hufanya sana katika miaka hii. Watu hununua vitu kwenye kwenye platfom maalumu za kuuza badhaa mtandaoni au kwenye mitandao ya kijamii.
Kununua vitu mtandaoni au online ni jambo zuri na huweza kufanyika kupitia vifaa kama simu au PC. Faida moja ya kununua vitu mtandaoni ni kuokoa pesa yako maana kuna bidhaa ambazo hupatikana kwa bei ya chini huku mtandaoni.

Ukiachilia mbali faida, kunachanga moto unaweza kutana nazo katika kufanya manunuzi mitandaoni. Hapa hatutazungumzia moja kwa moja changamoto hizi ila tunakupa mambo ya kuzingatia katika kununua bidhaa Mtandaoni. Mambo haya yanaweza kusaidia katika baadhi ya changamoto.

Mambo 5 ya kuzingatia katika kununua bidhaa Mtandaoni

Maelezo kuhusu badhaa

Bidhaa zinazouzwa mitandaoni huwa mara nyingi zinawekwa maelezo ambayo ukiwa kama mnunuzi unatakiwa kuyasoma ili kuielewa bidhaa. Unatakiwa usiishie kuangalia picha na bei tu, hakikisha unasoma na maelezo yaliowekwa kwenye hiyo bidhaa pia. Alafu usisahau kulisoma jina la hiyo bidhaa mara mbili mbili.
Ukiwa na tabia ya kununua vitu mtandaoni bila kusoma maelezo unaweza nunua kitu tofauti na ulichokusudia. Yani badala ya kununua simu, unaweza jikuta umelipia kupata kava la simu.

Angalia maoni toka kwa walionunua

Kabla ya kununua bidhaa Mtandaoni inashauriwa kuangalia maoni kabla ya kufanya maamuzi ya kununua. Mara nyingi watu huwa wanatoa maoni juu ya bidhaa walizonunua mtandaoni na kama bidhaa mbaya au nzuri huwa wanaweka wazi ili wengine wajue. Unaweza ingia YouTube, Facebook au ndani ya platfom unayotumia kununua bidhaa alafu ukaangalia maoni toka kwa walionunua katika kipengele cha “Reviews”.
Hii itakusaidia kujua kitu unachotaka kununua ni vizuri au kibaya. Ila unatakiwa kuwa makini na maoni ya uongo pia. Na fahamu kuwa baadhi ya vitu huwa vinakua vibaya kwa wengine ila ni vizuri kwako.

Utaratibu wa kurudisha bidhaa

Mambo mengi yanaweza tokea baada ya kulipia na kuletewa bidhaa ulioiona mtandaoni. Unaweza letewa bidhaa ikawa haina tatizo, ukaendelea kutumia au ikawa na tatizo, ukataka kurudisha.
Bidhaa ikiwa vizuri ni jambo zuri lakini ukiwa na matatizo alafu ukataka kuirudisha unapaswa kujua kuwa sio kila huduma huwa zinakuruhusu kurudisha bidhaa. Sasa ukiwa kama mnunuzi ambae unaona unaweza chukua bidhaa yenye matatizo kwa bahati mbaya, ni vema ukaangalia utaratibu wa kurudisha bidhaa zenye matatizo kabla hauja nunua hiyo bidhaa Mtandaoni.

Linganisha bei

Badhaa za mtandaoni huwa zinatofautiana bei. Unaweza kuta sehemu flani bidhaa inauzwa kwa bei kubwa kuliko sehemu nyinge lakini ni bidhaa moja. Kutokana na hili, inashauriwa kuwa mtu ambae ukiwa unataka bidhaa mtandaoni, uangalie hiyo badhaa katika sehemu tofauti tofauti na kulinganisha bei. Kwa kufanya hivyo, utapata sehemu ambazo bidhaa unayoihitaji inaizwa kwa bei rahisi.

Usalama wa pesa zako

Unapofanya manunuzi mitandaoni, usisahau kuzilinda pesa zako. Hakikisha unanunua bidhaa mtandaoni katika sehemu inayoaminika ili usiibiwe pesa zako. Hakikisha unajaza taalifa za malipo vizuri ili usije kosea kulipia. Hakikisha haudanganyiki katika kutoa taalifa za akaunti yako ya pesa.

Kama unatumia credit card katika kulipia, epuka kujaza taalifa za Credit card ukiwa umeunganisha kifaa chako na public WiFi bila VPN.

Mambo hayo machache yanaweza kusaidia katika kuepuka baadhi ya changamoto ambazo watu hukutana nazo. Hii inaweza kuwa kwenye platfom za kununua bidhaa kama; Alibaba, kikuu, Jiji na nyinginezo au mitandao ya jamii kama; Facebook na Instagram.

Tofauti kati ya Facebook Lite na Facebook ya kawaida kwenye simu yako

Ukihitaji kutumia mtandao wa kijamii wa Facebook kwenye simu, unaweza tumia kupitia njia mbili. Njia ya kwanza kabisa ni kutumia mtandao wa Facebook moja kwa moja katika tuvuti/website ya facebook. Njia ya pili ni kutumia Facebook kupitia app maalumu ambazo ni “Facebook lite” and “Facebook ya kawaida”.
Njia nzuri na rahisi ya kutumia mtandao wa Facebook ni njia ya app. App rasmi za Facebook zipo mbili, unaweza tumia app ya kawaida ya Facebook au ukatumia app ya Facebook lite ila kikubwa ni utambue tofauti ya app hizi. App hizi zinautofauti na hapa chini tumeweka tofauti chache kati ya Facebook lite na Facebook ya kawaida.

Tofauti kati ya Facebook Lite na Facebook ya kawaida kwenye simu yako

Matangazo mengi

Mtu unapotumia mtandao wa Facebook kupitia app ya Facebook lite hua unaoneshwa matangazo machache kuliko akitumia Facebook ya kawaida.
Unapotumia mtandao wa Facebook huwa kuna matangazo ambayo hujitokeza. Matangazo haya huioneshwa na kampuni ya Meta kwa kila mtu anaetumia mtandao wa Facebook Bure. Kuna watu hua wanalipia pesa Facebook ili kuyaondoa matangazo haya kwenye akaunti zao.

Kutumia data sana


Katika mtandao wa Facebook, Kuna vitu vingi sana ambayo mtu unaweza tumia bando lako kuvifurahia. Lakini unapaswa kufahamu huwa unapotumia app ya Facebook lite bando lako litatumika kidogo ukilinganisha na ukitumia Facebook ya kawaida.
App ya Facebook lite imeundwa kutumia data kidogo na inafanya vizuri hata kama upo kwenye mazingira ambayo mtandao unasumbua.

Kuchukua nafasi kubwa kwenye simu


Ukiingiza Facebook ya kawaida pamoja na Facebook lite kwenye simu yako kisha ukaangalia nafasi zilizochukua kwenye simu yako, utagundua Facebook ya kawaida imechukua nafasi kubwa sana kwenye simu yako kuliko Facebook lite.
Facebook lite ni app ndogo isiochukua nafasi kubwa sana kwenye Storage ya simu yako.

Ubora wa picha na video


Facebook lite ni app inayoonesha ubora wa chini wa picha ukilinganisha na app ya Facebook ya kawaida. Ukihitaji kuona ubora katika video na picha katika mtandao wa Facebook, tumia Facebook ya kawaida na sio Facebook lite. Facebook lite inawezapunguza ubora wa picha au video unapoziingiza au unapozitoa mtandaoni.

Katika video na picha za 360°

Kama ni mpenzi wa video na picha za 360° unatakiwa kufahamu huwa huwezi angalia video na picha za 360° ukiwa unatumia Facebook lite. Video na picha za 360° zinapatikana katika mtandao wa Facebook lakini unahitaji kuwa na app ya Facebook ya kawaida ili kuangalia kwenye kifaa chako.

Ni vema kufahamu tofauti ya app ya Facebook lite na Facebook ya kawaida ili uweza chagua unahitaji kutumia ipi, kwanini na wakati gani. Endelea kuwa karibu zaidi na The bestgalaxy.

WhatsApp: kuview status ya mtu na isionekane umeona

WhatsApp ni app inayotumika na watu wengi na app hii inavipengele vingi ikiwemo kipengele cha status. Kipengele  cha status huwezesha watu kushiriki hali zao na watu wengine. Kuiona status ya mtu kwenye WhatsApp utatakiwa kuwa na namba ya huyo mtu na yeye kuwa na namba yako. Na endapo ukiiangalia/ukiview  status ya mtu, ataona kuwa umeangalia status yake.

Sasa Kuna baadhi ya watumiji wa WhatsApp huwa wanataka kujua jinsi ya kuview status ya mtu na isionekane kuwa wameona kwa aliepost. Hapa The bestgalaxy tunaenda kukufungua juu ya hili kwa kukupa njia nzuri na salama ya kuanaglia au kuview status ya mtu bila kuonekana umeona.

WhatsApp yako inatatizo? Jifunze jinsi ya kutatua BONYEZA HAPA>>>

Jinsi ya kuview Whatsapps status bila kuonekana umeona

Kuview Whatsapp status ya  mtu bila kuonekana kunawezekana kufanyika kwa njia zaidi ya moja lakini njia nyingi sio salama kwa akaunti yako ya WhatsApp maana zinaweza kufanya uzuiwe kutumia WhatsApp. Njia salama ya kuview Whatsapp status ya  mtu bila kuonekana ni kuzima “Read receipts” kwenye app yako rasimi ya whatsApp. Fuata hatua zifuatazo kufanya hivyo.

  • Fungua App yako ya WhatsApp na uguse vidoti vitatu vilivyo juu kulia.
  • Chagua “Settings” kwenye orodha ya chaguzi zitakazo jitokeza.
  • Baada ya hapo ingia katika sehemu ilioandikwa “Privacy” na uzime kipengele kilichoandikwa“Read receipts
  • Baada ya kuzima kipengele cha hicho utakua na uwezo wa kungalia status za watu bila wenyenazo kujua. Kwaiyo ukizima, unaweza kuview status bila kuacha nyayo.

Kipengele hiki ni kipengele salama na hakiwezi pelekea akaunti yako ya Whatsapp kufungwa na Whatsapp. Lakini ubaya wake ni kwamba ukikizima huwa kinafanya usijue watu wanapoangalia status zako au kujua kuwa wamesoma sms ulizowatumia. Na wala wewe hautaweza kuonekana kama umesoma sms zao.

Kutokana na jambo hili unashauriwa; ukisha maliza kuangalia status ya mtu ambae hutaki ajue umeangalia, kiwashe tena hicho kipengele cha “Read receipts”.

Njia hii ni njia nzuri kuliko kutumia app za WhatsApp zisizo rasimi zilioweka urahisi katika kuangalia status bila kuacha nyayo. App hizo zinazoweza pelekea WhatsApp kuzuia akauti yako na ndio maana hatupendekezi japo unaweza tumia pia.

Magari ya Umeme: Fahamu mambo 5 kuhusu magari haya

Magari ya umeme yameonekana kuwa ni future katika teknolojia ya magari.

Kumekua na mipango mikubwa ya kuwezesha magari kuifikia sehemu ambayo magari ya diesel na petrol yameifikia. Na sio kuyafikia tu, Magari ya umeme yaenda kuwa mbadala wa Magari hayo ili kusimamisha uchafuzi wa hali ya hewa unaotokana na uchomaji wa diesel na petrol hapa Duniani.

Hapa The bestgalaxy tumekuandalia mambo matano kuhusu magari haya ya umeme. Kama wewe ni mtu unaependa kujua mambo kuhusu magari ya umeme, basi chukua muda wako kuyasoma hapa chini.

Mambo 5 kuhusu magari ya umeme

Betri ni moja ya vitu vya gharama sana kwenye magari haya

Kama tunavyo fahamu, magari huwa yananunuliwa, yatumika na katika kutumika huwa tunabadilisha sehemu za magari zilizochoka na kuweka mpya. Karibu kila sehemu tunayobadilisha kwenye gari hughalimu pesa.  Sasa katika magari ya umeme ukihitaji kubadili betri, huwa inagharimu pesa nyingi kuliko sehemu zote. Betri ya sehemu ya gharama sana katika magari ya umeme.

Unashauriwa kuangalia vituo vya kuchaji kabla haujanunua

Kutokana na magari haya kuonekana future, unaweza kuwa na shauku ya kufanya kila liwezekanano ili kununua. Lakini unapaswa kujua kuwa, kumiliki magari haya ya umeme katika sehemu iso na miundombinu mizuri kwajili ya magari ya umeme ni kitu unachoweza jutia. Unashariwa kuangalia zaidi upatikanaji wa vituo vya kuchaji katika mazingira yako kabla ya kuchaji magari haya ili usiteseke kupata chaji unapoishiwa ukiwa njiani.

Unaweza kuyachaji magari ya umeme nyumbani

Kutokana na Magari haya kutumia umeme, kunauwezekano wa kuyachaji nyumbani tu kwa umeme wa nyumbani. Lakini unapaswa kufahamu kuwa chaji zinazoweza kuwekwa nyumbani huwa hazina nguvu ya kujaza betri kwa haraka ukilinganisha na chaji zinazopatikana kwenye vituo maalum. Hivyo umuhimu wa vituo vya kuchajia upo pale pale.

Wamiliki wameonekana kupata changamoto katika baridi

Katika msimu wa baridi,  watu wanaomiliki magari ya umeme waishio nchi ambazo hukumbwa na theluji wamekumbana na changamoto katika kutumia magari haya. Changamoto hizi ni pamoja na kuchelewa kujaa kwa betri za magari na kupungua kwa “Range” (Umbali ambao gari linaweza kutembea kabla haujalipeleka kuchaji tena).

Yanaendelea kushuka bei

Watu wengi wanaotupia macho magari ya umeme huwa wanaishia kuyatupia macho magari ya kifahari au Luxuly cars zinazouzwa ghari sana na kusahau kuwa kuna magari ya umeme ya kawaida yasio na bei ya juu sana japo ni bado inaweza kuwa dharama sana kwa baadhi ya watu. Ujio wa magari ya umeme ni mapinduzi yanayogusa watu wote na kila siku zinavyozidi kwenda kunajisi bei zinaenda kuwa rafiki.

Unawazo gani kuhusu mapinduzi haya ya magari? Sawa, asante sana kwa muda wako. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mambo mengine.

Jinsi ya kutuma pesa Kenya na Tanzania (Vodacom/Safaricom)

Kutuma pesa nje ya nchi ilikua ni jambo gumu sana katika miaka ya nyuma, lakini wakati huu jambo hili ni jambo jepesi kiasi kiasi kwamba unaweza fanya kiganjani pako ndani ya dakika mbili. Hii yote ni kwasababu ya Teknolojia ambayo lengo lake ni kurahisisha maisha ya Binadamu.

Hapa The bestgalaxy tunaenda kuangalia jinsi ya kutuma pesa Kenya na Tanzania kwakuhusisha Safaricom Kenya na Vodacom Tanzania. Kama upo nchi ya Tanzania, unaweza tumia mtandao wa Vodacom kumtumia pesa mtu kwa Mpesa akiwa kenya anatumia mtandao wa Safaricom. Pia ukiwa kenya unatumia Safaricom unaweza mtumia pesa mtu kwa Mpesa akiwa anatumia mtandao wa Vodacom Tanzania.

Jinsi ya kutengeneza Logo ya biashara au Binafsi BONYEZA HAPA>>>

Kutuma pesa Kenya na Tanzania (Vodacom/Safaricom)

Unataka kujua jinsi ya kutuma? Usijali, hapa chini kuna maelezo juu ya hatua unazoweza kufuata pale unapotaka kutuma pesa ukiwa Tanzania na kenya kwakutumia mtandao wa Vodacom au Safaricom.

Kutuma pesa toka Tanzania kwenda Safaricom Kenya kwa kutumia Mpesa(Vodacom)

  • Fungua App ya Mpesa na uguse sehemu ilioandikwa “Services” alafu utaletewa orodha ya huduma.
  • Chagua huduma ilioandikwa “International Transfers” kwenye orodha hiyo.
  • Baada ya kufanya hiyo utapelekwa kwenye ukurasa utakao takiwa kuchagua nchi unayotaka pesa iende. Utachagua Kenya kwakua ndiko unataka kutuma pesa.
  • Baada ya kuchagua nchi utaletewa ukurasa wa kuchagua mtandao. Wewe utachagua mtandao wa  Safaricom kwakua mtu unaemtumia anatumia Safaricom.
  • Baada ya kuchagua, utapelekwa kwenye ukurasa utakao takiwa kujaza namba ya simu ya mtu unaemtumia pesa kwa mfumo wa kimataifa (254xxxx) kisha andika kiasi unachotaka kutuma. Na ukishajaza utabonyeza kitufe kilichoandikwa “Endelea” ili kuendelea na hatua nyingine za uthibisho wa kutuma pesa yako.

Sending money from Kenya to Tanzania with Mpesa (Safaricom)

  •  Dial *334# to open Mpesa Global.
  • Select “Send Money Abroad”.
  • Select “Send to Mobile Number”
  • Select “Tanzania” as a county you want to send money.
  • Enter Recipient Mobile Number in International Format (255xxxxxx)
  • Enter Amount of Money you want to send.
  • Select  source of fund and purpose of Funds then confirm.

Mwisho ningependa kukukumbusha kuwa makini katika kutuma pesa yako ili kuepuka kutuma pesa kimakosa. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy na usiache kufuatilia The bestgalaxy.

Jinsi ya kuangalia video Youtube  bila kutumia bando sana(Okoa data)

Uangaliaji wa video online kupitia app  kama Youtube,Tiktok na Instagram unaweza kua ni moja ya vitu ambayo hupelekea bando la internet kutumika sana kwenye simu. Kiufupi kama mtu anapenda kuangalia video sana mtandaoni basi hata matamizi yake ya data yanaweza kuwa ni makubwa na kupelekea bondo kuisha haraka. Hii inweza kuwa kawaida au ikawa tatizo kwa baadhi ya watu.

Hapa The bestgalaxy tunaendea kuangalia mambo machache ambayo mtu anaweza fanya kuangalia video Youtube  bila kutumia bando sana. Kama unataka kujua mambo yaha hebu chukua muda wako kusomaa hapa chini.

Fanya haya kuangalia video Youtube  bila kutumia bando sana

Washa Data saving mode

Youtube imejali matumizi ya data ya watumiaji wa app ya Youtube kwa kuweka kipendele kinachopunguza matumiza ya Data. Kuna kipegele  ambaacho ukikiwasha katika app ya youtube, unakua unatumia bando lako la internet kidogo. Kipengelea hii kinaitwa Data saving mode na ukikiwasha huwa kinapunguza na kuzima baadhi ya vipengele vingine vya app ya  Youtube vinavyotumia Data. Ni jambo zuri kutumia njia hii kuoa data lakini video hua zinaonekana hazina ubora. Kuwasha Data saving mode nenda katika app alafu gusa Profile yako kisha bonyeza alama ya settings iliojuu kulia alafu chagua “Data saving”. Baada ya hapo, washa sehemu ya juu ilioandikwa “Data saving mode”.

Chagua video fupi

Youtube inavideo fupi na ndefu. Kati ya video fupi na video ndefu katika kutumia data tunaweza sema  uangaliaji wa video ndefu unaweza kufanya utumie data zaidi endapo video hizo zitakua na ubora wa picha sawa. Hivyo kama unahitaji kuangalia video Youtube  bila kutumia bando sana unaweza angalia video fupi badala ya kuangalia video  ndefu. Na hatakama utamaliza bado lako kwa uangalia video fupi utakua umeangalia video nyingi.

Zima Autoplay

“Autoplay” ni kipengele ambacho hufaya video ziwe zinaendelea kujiplay Moja baada ya nyingine mfulilizo pale zinapoisha. Kipengele hiki ni kizuri lakini ubaya wake ni kwamba ukijisahau unaweza kuta video nyingi sana zimejiplay na kumaliza bado lako la internet. Kama unahitaji kuzima kipengele hiki, nenda kwenye app yako ya Youtube kisha ingia kwenye Profile alafu gusa alama ya Settings na uchague “Autoplay”. Baada ya kufanya hivyo, zima Autoplay kwa kugusa kitue kilicho upende wa kulia.

Endelea kuwa karibu na The Bestgalaxy na usiache kutembelea mara kwa mara The Bestgalaxy ili kusoma vitu vingine.

Jinsi ya kucheza game la Fortnite online kwenye simu (bila kudownload)

Fortnite ni game lililotolewa na Epic Games katika  mwaka 2017. Epic games ni kampuni inayojihusisha na Games na imetengeneza magemu mengi tu, ikiwemo hili game linaloitwa Fortnite. Tangu game hili limetoka mpaka sasa kuna mamilioni ya watu wanalicheza na baadhi ya watu wanaotumia simu za Android ni miongoni mwa watu hao.

Hapa chini The bestgalaxy tunatoa maelezo juu ya jinsi ya kulicheza gemu kwenye simu za Android online bila kudownload. Game la Fortnite halipatikani katika Playstore hii ni baada ya kuondolewa kwa kutofuata sheria za Google Play store. Liliondolewa mwisho wa mwaka 2020 na game nyingi zikikiondelewa katika Playstore huwa zinakufa lakini Fortnite ni game ambalo lipo hai mpaka leo na unaweza cheza kwenye simu yako ya Android kwa kudownload nje ya Playstore na hata kujeza bila kudownlod pia.

Magemu ya mpira ya kucheza kwenye simu GUSA HAPA>>>

Jinsi ya kucheza game la Fortnite online kwenye simu (bila kudownload)

Kucheza gemu hili kwenye simu bila kulidownload ni rahisi tu japo utakitaji kuwa na internet yenye kasi, VPN pamoja na Accounti ya Microsoft. Kama hauna akaunti ya microsoft usihofu maana unaweza tengeneza  katika ya safari ya kulicheza gemu hili. Fuata hatua zifuatazo kucheza game la fortnite online kwenye simu bila kudownload.

  • Unganisha VPN na iwe kwenye server ya USA
  • Tumia web browser yako kuingia katika Xbox.com/play
  • Bonyeza kiduara cha upande wa kulia juu ya ukurasa wa kwanza wa Xbox.com/play
  • Bonyeza batani ya kijani ilioandikwa “SIGN IN” alafu jaza taharifa za akaunti ya Microsoft. Kama hauna akaunti utabonyeza neno “Create One” utakaloliona baada ya bonyeza hiyo batani ya kijani.
  • Baada ya kuweka sawa akaunti ya Microsoft utarudishwa kwenye ukurasa wa Xbox
  • Utatakiwa kutumia kisehemu ya tafuta cha ukurasa huo kutafuta game la “fortnite” alafu kuliona utalichagua na kubonyeza “Play” ili kuanza kulicheza.

Unapocheza gemu hili, hakikisha internet yako iko vizuri maana ikiwa iko vibaya unaweza kutofurahia kucheza gemu la fortnite kwa njia hii. Njia hii ya kucheza gemu huwa inaitwa “Cloud gaming” na huduma ya” Xbox cloud gaming” ndio inayotumika maana inaruhusu kucheza gemu hili bure.

Kama wewe ni mtu uliekua USA na upo kwenye sehemu ambayo game hili halikupi nafasi ya kucheza basi hizo hatua juu ukizifuata utaweza kucheza gemu lako pendwa ukiwa nje ya USA.

Unaweza book ndege kwa app ya MPesa?

Moja ya app zinazotupa uwezo wa kufanya miamala ya kifedha katika viganja vyetu ni app ya Mpesa. App hii ni kwaajili ya watumiaji wa Vodacom. Moja ya faida za kutumia app ya Mpesa kwa mtumiaji wa Vodacom ni kwamba hata laini voda ikiwa haipo hewani au imepotea, unakua umebaki na uwezo wa kufanya miamala kwenye app hiyo kwa kutumia internet ambayo haihusiani na laini yako ya voda.  

Kuna baadhi ya watu wamekua wakiuliza juu ya kubook ndege za usafiri kwenye app ya Mpesa na hapa tunaenda kuangalia kuhusu hilo. Kama na wewe unahitaji kujua juu ya hili basi hapa unaweza pata mwanga.

Kubook ndege kwa app ya MPesa

Unaweza book ndege kwa app ya MPesa?

Ndio, inawezekana. Precision Air na Vodacom waliungana na kukuletea uwezo wa kubook ndege kwenye simu yako kupitia app ya Mpesa. Kwa sasa app ya Mpesa inavipengele vingi ikiwemo kipengele cha kubook ndege za usafiri. Precision Air wamekiri kuwa huduma ya kubook ndege kwa app ya Mpesa ni huduma rahisi na haraka kwa watumiaji. Na pia moja ya kitu kizuri kuhusu kubook ndege kupitia app ya Mpesa ni kwamba unapata punguzo la asilimia 20  ambayo inaokoa karibu robo ya pesa yako. Kwaiyo tunaweza sema pia hii ni njia ya kupata tiketi za ndege kwa bei rahisi.

Kipengele cha kubook ndege kwenye app ya MPesa

Ukifungua app ya Mpesa unaweza kiona kipengele cha kubook ndege maeneo ya chini kikiwa kimeandikwa “Book Flights”. Kama umeangalia chini na haujakiona, mbonyeza sehemu ilioandikwa “Services” alafu ukisha fanya hivyo utapelekwa kwenye orodha ya huduma na utaona kipengele kinachoitwa Book Flights kwenye orodha hiyo. Ukifungua kipengele hicho utakutana na ukurasa huu chini kwaajili ya kutafuta na kubook ndege itakayofanikisha safari yako.

Asante kwa muda wako, Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy na usisahau kutembelea kila mara kupata vitu vipya.