Kampuni ya Sony ni kampuni kubwa sana katika upande wa games kutokana na sababu nyingi ikiwemo kuleta vifaa vya games vyenye mafanikio makubwa ulimwenguni. Katika Miaka ya nyuma Sony ilitengeneza kifaa kidogo cha mkononi kiitwacho PSP (PlayStation Portable) kama moja ya vifaa vya games ambacho kinamuwezesha mtu kucheza games popote kama vile inavyotumika simu siku hizi. Hii PSP ilitolewa rasmi na Sony mwaka 2005 na ilikua ni bidhaa iliopokelewa vizuri sana na watu.
Kulikua kuna magemu/gemes kama 1900 hivi na zaidi ambayo mtu ukinunua PSP, unaweza kuyacheza. Lakini Baada ya muda Sony walitangaza kusitisha projekti yao ya PSP. Baada ya Sony kufanya hivyo Games za PSP na vifaa vya PSP vikaacha kuzalishwa mpaka leo. Lakini kutokana na ubora wa vifaa vya PSP na game zake kwa kipindi kile, watu mpaka sasa hawajaisahau PSP. Kuna watu mpaka sasa wana vifaa vya PSP, wengine wanaiga kutengeneza vifaa vya PSP na wengine wametafuta njia ya kuyacheza magemu ya PSP kwenye PC na Simu.
Ukitaka kucheza magame ya PSP kwenye simu au PC, utahitajika kutumia app au software ziitwazo Emulators. Moja ya Emulators za magame ya psp zinazotumika sana inaitwa “PPSPPP PSP Emulator“. Hii inafanya mpaka baadhi ya watu kuyafahamu magame ya PSP kama “Magame ya PPSPP”.
Magame ya mpira ya kucheza kwenye simu BONYEZA HAPA>>>
Game nzuri za psp za kucheza kwenye simu au PC
GTA Liberty City Stories

Liberty City Stories ni sehemu ya mfululizo maarufu wa magame ya Grand Theft Auto ambayo yapo chini ya Rockstar. Game hili katika upande wa PSP, ni kati ya game zuri sana kucheza katika PC na Simu pia. Unapo cheza game hili unacheza kama jamaa mmoja muhuni au muhalifu aitwae Toni Cipriani, ambaye anarudi mjini baada ya kukaa mbali kwa muda. Unaingia katika ulimwengu wa uhalifu wa Liberty City na kupambana kuwa juu katika mji huo.
God of War chain of Olympus

Game hili pia ni mfululizo wa magame ya God of War ambayo ni maarufu pia kwenye ulimwengu wa games. Humu unacheza kama Kratos ukipigana na miungu pamoja kutatua changamoto mbali kwa mtiririko wa simulizi ya God of War. Liliundwa SCE Santa Monica Studio na kuchapishwa na Sony Computer Entertainment kwaajili ya vifaa vya PSP. Ni game la PSP zuri kulicheza mpaka sasa.
Assassin’s Creed bloodlines

Assassin’s Creed: Bloodlines katika psp ni game ambalo ambao lilitoka mwaka 2009. Magemu ya Assassin’s Creed yapo mengi katika ulimwengu wa games na hili ni moja kati ya hayo. Katika Assassin’s Creed bloodlines hili unacheza kama mtu aitwae Altair Ibn-La’Ahad. Huyo ni muhusika mkuu katika game na yupo katika miji ya Kilatini wakati wa karne ya 12(Zamani). Game la Assassin’s Creed bloodlines bado linaweza kuwa chaguo zuri mpaka sasa unahitaji kucheza game za psp maana sina stori nzuri na muonekano mzuri pia.
NFS most wanted

Ukiwa unapenda magame ya magari na unataka kufurahia game hizi upande wa PSP, game NFS most wanted linaweza kuwa zuri kwako. Game hili linaitwa “Need For Speed Most” wanted lakini unaweza liita “NFS most wanted” kwa ufupi. Need For Speed ni moja majina makubwa kwenye video games na hili game tunaloliongelea hapa, lina jina hili Kwasababu ni sehemu ya game za Need For Speed. Lilichapishwa na Electronic Arts Katika PSP na unaweza furahia mpaka sasa maana bado lipo vizuri.
Spider man 3

Hili game la Spider man 3 la PSP la Spider-Man 3 ni sehemu ya mfululizo wa magame ya Spider-Man. Kuna magemu mengi ya spider man na hili ni moja ya magemu hayo lilichapichwa kwaajili ya PSP ambalo linafurahisha mpaka sasa. Humu ndani ukiwa kama spider man utapambana na maadui kama Sandman, Venom, na New Goblin.
Hapo juu tumeweka games chache TU lakini games za psp zipo nyingi sana nzuri mbali na hizo. Lakini unapaswa kujua games za psp zilisimama kutolewa hivyo hakuna games mpya za psp ambazo ni rasmi. Ila u aweza kutana na game za zamani za psp zilizo boreshwa lakini sio rasmi. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mambo kuhusu games na mengine.










