Total football ni game la mpira ambalo unaweza cheza kwenye simu ya mkononi. Ni game la mpira wa miguu kama lilivyo game la eSports football, FIFA mobile (EA SPORTS FC) au Dream League soccer.
Game la Total football limetengenezwa na GALA Sports kisha kutolewa na Studio Vegas private Limited pamoja na GALA Sports pia. Limetolewa katika platform mbili tu kwasasa ambazo ni Android na iOS. Hiyo kwasasa watu wanaweza cheza kwenye simu za Android or iOS(iPhone). Ni game la Bure kabisa na lina mode zaidi ya moja unaweza furahia kucheza na kitu kizuri zaidi ni kwamba linaruhusu kucheza offline pamoja na online.
Yani ukiwa una data au bando unaweza cheza game hili online alafu ukiwa hauna data, unaweza cheza bila ya kuwa na muunganiko wa internet. Ukiachana na hayo, Total football lina muonekano au graphics nzuri japo linaeweza zidiwa na baadhi ya magemu mengine ya mpira, lakini bado lipo vizuri kimuonekano.
Linakuruhusu kuunda timu ya ndoto yako kutoka kwa machezaji zaidi ya 4000 ulimwenguni, kuitengenezea jezi na Logo kisha kuonesha jinsi gani timu yako ni Bora kwa kucheza na timu nyingine. Linakupeleka katika ulimwengu wa bosi halisi wa timu ya mpira wa mguu kama DSL na magemu mengine kama hilo.

Kudownload na kucheza game la Total football (Android)
Total football kabla ya kutolewa rasmi Kuna baadhi ya watu walikua wanacheza likiwa kwenye maboresho na lilikua likisubiriwa sana na watu litolewe rasimi. Katika kulitoa napo halikutoka katika nchi au maeneno yote. Baadhi ya nchi au maeneno, hauwezi kucheza game hili kirahisi maana bado halipo rasimi kwenye maneno hayo.
Kwa hizi pande zetu, ukiingia playstore kwenye game hili (Android) unaweza kuta ujumbe ulioandikwa “This item isn’t available in your country”. Ujumbe huu unamaana sehemu ulipo game hili halipatikani. Sijajua ni lini wanaweza fanya game hili kuwa rasimi katika pande za huku kwetu lakini nisieme tu kuwa ni muda wowote kwanzia sasa linaeweza patikana. Unaweza BONYEZA HAPA kuangalia muda huu katika playstore kama limeishaachiliwa rasimi lichezwe pande za huku kwetu au bado.
Kama Bado, basi jaribu kupakua au kudownload APK file yake nje ya playstore alafu install kwenye simu yako ya Android. Baada ya kuinstall kwenye simu yako, lifungue na uanze kulicheza. Ukitaka uianza safari ya Kudownload APK file ya game la Total football unaweza BONYEZA HAPA.