Tag Archives: Facebook

Content monetization: Mambo ya kuepuka ili kutengeneza Pesa katika Facebook

Toka Facebook imefungua zaidi mlango wa watu kuingiza pesa kupitia content zao, watu wamekuwa wakihitaji kujua vitu vingi sana kuhusu mchakato mzima. Kuwasaidia, hapa The Bestgalaxy tumekuwa tukitoa makala mbalimbali ikiwemo hii.


Kwenye makala hii, hebu tuzungumzie mambo ambayo unatakiwa kuepuka katika kuingiza pesa kupitia Facebook Content monetization.

Nadhani wote tumeisha jua Facebook Content monetization ni program inayohusu kuingiza pesa katika Facebook.
Sasa hebu tuangalie mambo ambayo anatakiwa kujua mtu aliyefanikiwa kuanza kuingiza pesa, na hata yule anayewinda nafasi ya kufikia katika hatua hiyo.

Facebook wanalipa kiasi gani kwa 1000 views? BONYEZA HAPA>>>

Mambo 5 ya kuepuka ili kutengeneza Pesa katika Facebook

1. Kushare link zisizoaminika

Facebook ni platform inayoruhusu kushare vitu mbalimbali ikiwemo link.
Lakini kwenye suala la kushare link, unatakiwa kuwa muangalifu sana ukiwa kama content creator. Link zinaweza kufanya post zako zizuiwe kuwafikia watu wengi.

Kuweka link kwenye captions au kuzituma kama zilivyo, kunaweza kuathiri hata ukuaji wa akaunti yako.
Mbali na kuathiri ukuaji, link zikiwa si salama zinaweza kufanya ukaondolewa kwenye Content monetization program na kufutiwa akaunti kabisa.

2. Kuweka video au picha toka kwa watu wengine

Facebook wanataka mtu atengeneze content ambazo ni “Original”.
Kama content unazoweka kwenye akaunti yako zimetolewa kwenye akaunti za watu wengine na kuwekwa kwako bila utofauti wowote, basi huwezi kuingizwa kwenye Content monetization program.

Na hata kama utafanikiwa kuingiza pesa, mapato yako yanakuwa madogo ukilinganisha na Original.
Kwa hiyo, ukitaka kufurahia kuingiza pesa Facebook bila matatizo, hakikisha unawekeza muda kutengeneza content zako, si kuchukua za watu kama zilivyo.
Na hata ukichukua, unatakiwa kuongeza thamani ili uonekane kuwa umefanya kazi ya kutengeneza kitu. (Mfano mzuri wa hili ni kufanya content za reaction).

3. Kutumia nyimbo za watu kwenye video zako kupita kiasi

Kwenye content, ni vizuri kutumia nyimbo za watu zinazofanya vizuri katika ulimwengu wa music.
Lakini suala hili huwa linakuja kuleta matatizo katika upande wa copyright ya ayoweza athiri monetization.

Kuna baadhi ya nyimbo ukiziweka kwenye video yako, zinakupa tatizo la “Copyright”.
Tatizo hili linaweza kuja kwa namna mbili; Mbaya sana na Nzuri kiasi.

  • Namna ya kwanza (Mbaya sana) ni utapata maonyo na vizuizi kwenye akaunti yako.
  • Namna ya pili (Nzuri kiasi) ni kukatwa mapato yako kwa ajili ya loyalty.

4. Kupost video za AI bila kuweka wazi

Mwaka 2025, baada ya ongezeko la content zinazozalishwa na AI mtandaoni, kampuni ya Meta iliamua kuweka utaratibu wa kuziwekea alama content zilizozalishwa na AI.

Ukiwa kama content creator, unatakiwa kuweka wazi content za AI unazopost ili kuepuka matatizo kwenye Content monetization.
Hapa naongelea kuweka post zako za AI katika kipengele ambacho huwa kinaandikwa AI label kila unapo post.

Kipengele cha “Ai label” katika Facebook

5. Kukomenti au kushare zaidi ya kawaida

Kukomenti, katika Facebook kuna namna mtu anaweza kupata matatizo kwa kufanya mambo kupitia kiasi.
Kukomenti na kushare vitu kupita kawaida ni kati ya mambo yanayoweza kukuletea matatizo.

Unaweza kuwa haujafanya kosa kushare au kucomment, lakini kwa kuwa unafanya kupita kiasi, utapata matatizo.


Hii ni kwa sababu Facebook ina mifumo ya kuzuia vitu vibaya na hatari kwa watumiaji wake. Endapo akaunti yako itagundulika kufanya jambo lisilo la kawaida, huwa wanazuia akaunti na kuangalia kama unajihusisha na mambo mabaya.
Kitendo cha kukuzui kinaweza kukufanya uondolewe kwenye Content monetization au kufutiwa akaunti kabisa endapo hawatakuelewa.

Kama unataka kufanikiwa kwenye Facebook Content monetization, basi epuka makosa haya matano huku ukitengeneza content zako kwa ubunifu.

Usinunue followers kwenye akaunti yako ya Facebook au Instagram BONYEZA HAPA>>>

Mambo 5 ya kuzingatia katika safari ya kuanza kuingiza pesa na Facebook monetization

Baada ya Facebook kufungua rasmi njia ya kuingiza kipato kupitia program ya Content monetization, watu wengi wameanza safari ya kutafuta njia ya kufanikisha ndoto ya kupata kipato kupitia content/maudhui wanazopost.

Lakini pamoja na nafasi hiyo kubwa, sio kila mtu anafanikiwa kuipata. Wengi hushindwa kutokana na kutozingatia mambo ya msingi ambayo yanaweza kusababisha kuchelewa au hata kushindwa kabisa kufikia malengo yao.
Ili kuepuka changamoto hizo, haya chini ndio mambo 5 muhimu unayopaswa kuzingatia.

Jinsi ya kutengeneza Pesa na Facebook monetization BONYEZA HAPA>>>

Mambo 5 ya Kuzingatia unapotaka Content Monetization katika Facebook

  1. Sheria za Facebook

Unapoanza safari ya kutafuta Facebook monetization, jambo la kwanza ni kuhakikisha kuwa hauvunji sheria za Facebook. Kumbuka kuwa Facebook ina sheria na miongozo mingi ambayo ni lazima izingatiwe.

Kuvunja sheria kunaweza kukusababisha usikubaliwe kuingiza pesa hata kama una followers/wafuasi wengi. Wengine huenda mbali zaidi na kufungiwa kabisa akaunti zao. Hivyo, kabla hujapiga hatua kubwa, hakikisha unazisoma na kuelewa vizuri sheria hizo ili kukusaidia kubaki salama na kuepuka matatizo ya baadaye.

  1. Aina ya Content Unazojihusisha Nazo

Kabla ya kuanza, jiulize: “Nataka nitengeneze content gani au muundo gani?” Facebook inaruhusu content za aina nyingi kama video, picha na makala za maandishi. Lakini kwa sasa njia rahisi zaidi ya kupata monetization ni kupitia video fupi (Reels). Reels hukupa nafasi ya kuongeza Followers kwa haraka, kupata views nyingi na kuongeza uwezekano wa kulipwa.

Kwa hiyo, chagua aina ya content unayoamini utaweza kuifanya kwa ubora na kwa mtindo unaoleta matokeo mazuri kwenye upande wa views.

  1. Engagement Katika Post Zako

Engagement ni jinsi watu wanavyoshirikiana na post zako. Hii inajumuisha mambo kama; Likes, Comments, Shares, Saves na hata Followers wapya.

Kadri content zako zinavyopata engagement kubwa, ndivyo Facebook itakavyotambua thamani ya kazi zako. Engagement ya juu inarahisisha safari yako ya kufikia monetization kwa haraka na hata kukua.
Kiufupi, jitahidi kutoa maudhui yanayogusa hisia, kufundisha, kuburudisha au kusisimua ili kuwaleta watu karibu zaidi na kazi zako.

  1. Usalama wa Akaunti Yako

Akaunti za Facebook mara nyingi hulengwa na wadukuzi (hackers). Hebu Fikiria umepambana mpaka umefikia vigezo vya kulipwa katika Facebook, lakini ghafla akaunti yako imechukuliwa na hacker…. maumivu yake ni makubwa sana si ndio? Sasa hii inaweza kukukuta endapo akaunti yako haitakua salama alafu ukawa unaendelea kuitumia kutafuta monetization.

Ili kulinda mambo yako kwenye akaunti, hakikisha unafanya kuwasha, Two-factor authentication, Tumia Password ngumu alafu kuingia kwenye akaunti na vifaa visivyo salama.

Kwa kufanya hivyo, utaendelea kuwa salama na kufurahia matunda ya kazi zako bila hofu ya kupoteza kitu.

  1. Usikate Tamaa

Safari ya kufanikisha kitu mtandaoni mara nyingi si rahisi. Wakati mwingine utapost maudhui yako lakini matokeo hayataridhisha moyo wako. Hapo ndipo wengi hukata tamaa.

Lakini kumbuka: kutoacha kufanya ndio msingi wa kufanikiwa. Badala ya kukata tamaa, jifunze kutokana na changamoto, tafuta mbinu mpya, na endelea kusonga mbele. Mafanikio yanahitaji uvumilivu hata huku mtandaoni.

Facebook monetization ni nafasi nzuri sana unayoweza kuitumia kuingiza kipato kupitia content zako. Lakini ili kufanikisha safari ya kumfikia hapo, zingatia sheria za Facebook, chagua content sahihi, ongeza engagement, linda akaunti yako na usikate tamaa kwenye ufanyayo.

Facebook inalipa kiasi gani kwa kutazamwa mara 1000 (1k views)?



Facebook ni mtandao unaomilikiwa na kampuni ya meta. Katika Facebook kuna kipengele unachoweza kukiita “Facebook Ads” au “Meta Ads”. Kipengele hiki katika Facebook ni kwaajili ya makampuni au watu wanaohitaji kutangaza matangazo(Ads) kwenye mtandao wa Facebook. Kuna makampuni na watu wengi sana huwa wanailipa pesa hapo ili kuonesha matangazo kwenye mtandao wa Facebook.

Meta inatengeneza mabilioni ya pesa kwa mwaka kupitia watu wanaotangaza matangazo katika Facebook. Katika pesa hizo, huwa inachukua kiasi flani walizotengeneza na kuwalipa Content creator wa Facebook. Ili content creator kuanza kulipwa, anatakiwa kuingia katika program yao maalum kwanza(content monetization).


“Content creator” wa Facebook ni mtu ambaye huunda na kutoa maudhui (content) kwenye  Facebook ili kuwavutia, kuwaburudisha, kuwafundisha au kuhamasisha watazamaji. Na Maudhui au content zinazozungumziwa hapa ni Video, Picha na hata Makala za maandishi.

Ujuzi utakao kuwezesha kuingiza pesa mtandaoni BONYEZA HAPA>>>

Facebook inalipa kiasi gani kwa views 1000 za video?



Ukiwa kama content creator unaejihusisha na video katika Facebook, utalipwa pesa pale video zako zinapopata views (zinapoangaliwa na watu). Lakini fahamu kuwa Facebook haina kiwango maalum itakachokulipa kwa kupata views 1000 kwenye video zako. Facebook huwa inalipa kutokana na mfumo unaoitwa Cost Per Mille (CPM). Hii ina maana unalipwa kiasi kutokana na kiasi walicholipa watangazaji (watu walio lipa matangazo yanayooneshwa kwenye video zako). Yaani kama matangazo yanayooneshwa kwenye video zako hulipiwa pesa nyingi na watangazaji, basi unaweza kuingiza pesa nyingi pia ukiwa kama content creator.

Screenshot ukionesha jinsi Facebook ilivyomlipa moja ya Content creator wa India kwa video 1 fupi (Reel).


Lakini pia kiasi unacholipwa Facebook creator kinaweza kuathiliwa na mambo mengine kama nchi ya mtazamaji, sekta unayojihusisha nayo na hata tabia za watu wako katika Ads wanazoangalia.

  • Nchi ya watazamaji wako (mfano Marekani na Ulaya CPM huwa kubwa kuliko Afrika).
  • Mada/sekta ya content zako (mfano video za biashara, fedha, teknolojia hulipa zaidi kuliko utani au burudani tu).
  • Tabia za watazamaji kwenye Ads(watazamaji wakiwa wanajihusisha na Ads kwa kuziangalia au kubonyeza).

Muhimu kujua: katika Facebook kuna aina mbili za video. Video ndefu na video fupi ambazo huitwa “Reels”. Malipo hati ya aina hizo za video huwa yanatofatulia kabisa. Ukijihusisha na Reel unaweza ulipwe pesa ndogo sana kwa views 1000 ila uzuri ni kwamba huwa zinaweza kufika views milioni 1 kirahisi kuliko video ndefu.

Reels zinaweza kulipa $0.20 – $1.00+ kwa views 1000 (kutegemeana na nchi au mengineyo). Alafu video ndefu zinaweza kuwa $1 – $10+ kwa views 1000, hasa kwenye niche za biashara, fedha au teknolojia.

Una download vipi video za Facebook kwenye simu yako?

Facebook ni moja ya mitandao maarufu sana kwa kutazama na kushare video mbalimbali. Mara nyingi, unaweza kuona video nzuri unayotaka kuihifadhi kwenye simu yako ili uitazame baadaye bila intaneti. Lakini tatizo ni kwamba Facebook haina chaguo la moja kwa moja la kudownload video hizo ziingie kwenye kifaa chako. Kwa bahati nzuri, kuna njia rahisi unazoweza kutumia kupakua video kutoka Facebook bila shida.

Katika ukurasa huu, tutakuelekeza hatua kwa hatua jinsi ya kudownload video za Facebook moja kwa moja kwenye simu yako. Haijalishi unatumia simu ya Android au iPhone, kuna mbinu rahisi ambazo zinafanya kazi kwa wote. Utajifunza jinsi ya kutumia website/tovuti maalum au programu zinazoweza kukusaidia kupakua video hizo kwa urahisi.

Ikiwa umewahi kuona video inayokuvutia kwenye Facebook na ukashindwa kuipakua, basi makala hii ni kwa ajili yako. Fuata mwongozo huu kwa makini ili uweze kuhifadhi video zako unazopenda na kuzitazama wakati wowote bila kuwa na wasiwasi wa data au intaneti.

Jinsi ya kudownload video za Facebook katika simu yako

Kiufupi njia rahisi ya kudownload video za Facebook ni kutumia App au tuvuti maalum kwaajili ya kudownload video hizo. Kuna app na tuvuti nyingi hukuwezesha mtu kupakua video za Facebook. Huwa zanahitaji uzipatie link ya video ambayo unataka alafu baada ya hapo, zinakuwezesha kuchukua video na kuiweka kwenye simu yako.

Mfano wa app za mitindo hii ni app iitwayo Video downloader iliotolewa na Inshot inc. Na kama utahitaji website unaweza tumia tuvuti Fdown.net ikakuwezesha bila tatizo.

Hatua za kudownload ya Facebook kwenye simu

  • Copy link ya video ulioiona katika Facebook
  • Paste link ya video katika tuvuti au app  maalum (katika app ya Video downloader au tuvuti ya Fdown.net)
  • Iruhusu app au tufuti kufanya mchakato wake kisha bonyeza kitufe cha kudownload video kitakacho letwa baada ya mchakato.

Kwa kufanya hayo utakua umefanikiwa kupakua video ya Facebook kwenye simu yako. Ila kabla ya kuondoka katika ukurasa huu ni vema kufahamu kuwa upakuaji wa video za watu bira ruhusa ya wamiliki ni kosa ingawa unaweza kufanya ikiwa video ipo katika kundi la video zisizo na madhara.

Jinsi ya kutengeneza pesa na Facebook Content Monetization Program


Facebook ni mtandao mkubwa wa kijamii unaomilikiwa na kampuni ya Meta na unaunganisha watu wengi Duniani. Watumiaji wa mtandao wa Facebook wanaweza furahia kuwasiliana na wepandwa wao, kuangalia picha, video na kusoma mambo mbalimbali.


Katika kufurahia mambo hayo, Facebook nimekua ni moja ya mitandao muhimu kwa watu wanaojiajiri. Ina vipengele vingi sana vinavyoweza msaidia mtu aliejiajiri, kukuza hudama yake. Mfano mzuri ni kile kipangele kutangaza biashara; mtu anaweza kutumia upande huo kutangaza biashara au huduma yake.


Mbali na upande huo, Facebook wana program iitwayo “Facebook Content monetization” ambayo inawawezesha watu kutengeneza pesa kwa content zao. Yani hapa unaweza lipwa kwa vitu unavyoandika na kupost, video na picha unazopost. Na unaweza fanya hivyo kupitia akaunti unayoitumia kila siku au Facebook page kama unayo. Ila kama unatumia akaunti ya kawaida utatakiwa kuweka kwenye “Professional mode” kwanza.

Jinsi ya kutengeneza video za katuni kwa simu ili kutengeneza pesa BONYEZA HAPA>>>

kuanza kulipwa katika Facebook Content monetization



Ili uanze kulipwa katika Facebook utatakiwa kuanza kujiunga na hiyo Facebook monetization. Na kabla haujajiunga, utatakiwa kutimiza vigezo vyao lakini vigezo vyao huwa vimetofautiana na hubadilika kutokana na kwamba mfumo wao kwa sasa upo kwenye maboresho.


Ukihitaji kuwavutia kwa kipindi hiki ili uingizwe kwenye program yao, ni vema ukawa na kuanzia followers 5000 na video zilizoangaliwa zikawa na jumla ya dakika 60000.

Pia ni vema ukatengeza video zako mwenyewe maana kuchukua video za watu bila maboresho yoyote ni kosa litakalokupunguzia nafasi ya kutengeneza Pesa.

Mambo ya kuepuka ili kutengeneza Pesa katika Facebook BONYEZA HAPA>>>

Jinsi ya Kuangalia kama upo tayari kulipwa na Facebook

Ukitaka kuangalia kama tayari umekidhi vigezo vya kuingia kwenye Facebook Monetization program, nenda kwenye Dashboard ya akaunti yako alafu ingia kwenye kipengele cha “Monetization”. Ikiwa utakutana na neno “eligible” au kipengele cha “Content monetization ” kimefunguka, basi fahamu kuwa akaunti yako inaweza ingizwa kwenye Facebook monetization program.


Baada ya kuwa vizuri sehemu hiyo, unaweza pokea ujumbe kwenye email yako kuwa wamekuarika kwenye program ya Content monetization program bila hata kufanya Chochote au ukakuta to vipengele vya kutengeneza pesa vimejifungua kwenye Dashboard. Unaweza pata hata notification kwenye Facebook ikikwambia umekua “eligible” hivyo set taalifa muhimu ili ulipewe.



Zingatia: kwasasa Facebook content monetization program ipo kwenye marekebisho hivyo kuna namna utaratibu wake haupo sawa. Hasa kwa nchi za huku Afrika mashiriki. Unaweza kuchati na sisi kwa kugusa HAPA.

Jinsi ya kutengeneza Pesa katika channel za WhatsApp BONYEZA HAPA>>>

Tofauti kati ya Facebook Lite na Facebook ya kawaida kwenye simu yako

Ukihitaji kutumia mtandao wa kijamii wa Facebook kwenye simu, unaweza tumia kupitia njia mbili. Njia ya kwanza kabisa ni kutumia mtandao wa Facebook moja kwa moja katika tuvuti/website ya facebook. Njia ya pili ni kutumia Facebook kupitia app maalumu ambazo ni “Facebook lite” and “Facebook ya kawaida”.
Njia nzuri na rahisi ya kutumia mtandao wa Facebook ni njia ya app. App rasmi za Facebook zipo mbili, unaweza tumia app ya kawaida ya Facebook au ukatumia app ya Facebook lite ila kikubwa ni utambue tofauti ya app hizi. App hizi zinautofauti na hapa chini tumeweka tofauti chache kati ya Facebook lite na Facebook ya kawaida.

Tofauti kati ya Facebook Lite na Facebook ya kawaida kwenye simu yako

Matangazo mengi

Mtu unapotumia mtandao wa Facebook kupitia app ya Facebook lite hua unaoneshwa matangazo machache kuliko akitumia Facebook ya kawaida.
Unapotumia mtandao wa Facebook huwa kuna matangazo ambayo hujitokeza. Matangazo haya huioneshwa na kampuni ya Meta kwa kila mtu anaetumia mtandao wa Facebook Bure. Kuna watu hua wanalipia pesa Facebook ili kuyaondoa matangazo haya kwenye akaunti zao.

Kutumia data sana


Katika mtandao wa Facebook, Kuna vitu vingi sana ambayo mtu unaweza tumia bando lako kuvifurahia. Lakini unapaswa kufahamu huwa unapotumia app ya Facebook lite bando lako litatumika kidogo ukilinganisha na ukitumia Facebook ya kawaida.
App ya Facebook lite imeundwa kutumia data kidogo na inafanya vizuri hata kama upo kwenye mazingira ambayo mtandao unasumbua.

Kuchukua nafasi kubwa kwenye simu


Ukiingiza Facebook ya kawaida pamoja na Facebook lite kwenye simu yako kisha ukaangalia nafasi zilizochukua kwenye simu yako, utagundua Facebook ya kawaida imechukua nafasi kubwa sana kwenye simu yako kuliko Facebook lite.
Facebook lite ni app ndogo isiochukua nafasi kubwa sana kwenye Storage ya simu yako.

Ubora wa picha na video


Facebook lite ni app inayoonesha ubora wa chini wa picha ukilinganisha na app ya Facebook ya kawaida. Ukihitaji kuona ubora katika video na picha katika mtandao wa Facebook, tumia Facebook ya kawaida na sio Facebook lite. Facebook lite inawezapunguza ubora wa picha au video unapoziingiza au unapozitoa mtandaoni.

Katika video na picha za 360°

Kama ni mpenzi wa video na picha za 360° unatakiwa kufahamu huwa huwezi angalia video na picha za 360° ukiwa unatumia Facebook lite. Video na picha za 360° zinapatikana katika mtandao wa Facebook lakini unahitaji kuwa na app ya Facebook ya kawaida ili kuangalia kwenye kifaa chako.

Ni vema kufahamu tofauti ya app ya Facebook lite na Facebook ya kawaida ili uweza chagua unahitaji kutumia ipi, kwanini na wakati gani. Endelea kuwa karibu zaidi na The bestgalaxy.

Ukiona dalili hizi Jua Account yako ya Facebook imedukuliwa na si salama (hacked)

Account za mitandao ya kijamii huwa zinawindwa na kudukuliwa na hackers. Katika Facebook muda mwingine unawezakua unatumia account iliodukuliwa na haujui kuwa imedukuliwa. Madhara ya kutumia account ya Facebook iliodukuliwa ni kwamba hacker anaweza itumia account yako ya Facebook kufanya uhalifu kwa watu Wengine na hao watu wakajua wewe ndiye umewafanyia hivyo. Kwaiyo ni muhimu kujua hali ya account yako ya Facebook ili kuepukana na mambo kama hayo.

WhatsApp yako inatatizo? Jifunze jinsi ya kutatua hapa>>>>

Kwenye audio nimezungunzia jinsi unavyoweza tambua kama account yako ya Facebook imedukuliwa/hakiwa na hackers. Kama imekufungua wewe basi usiache kuwa kuwajulisha na watu wako wengine wa karibu juu ya hili ili waweke account zao salama sisijetumika kukutapeli na vitu vingine kama hivyo. Unaweza gusa kitufe cha kijani hapo chini kuwasamazia watu ujumbe huu kwenye WhatsApp.

Kuangalia vifaa vilivyotumika kuingia kwenye Akaunti yako ya Facebook

  • Ingia kwenye account yako ya Facebook na uguse vimistari vitatu(menu)
  • Baada ya hapo chagua “Settings” ingia kwenye “Security and Login
  • Ukisha fanya hivyo utatupwa kwenye ukulasa ambao unakipengele kilichoandiwa “Where you Logged in“. Kwenye kipengele hiki unakutana na list ya vifaa ulivyotumia kuingilia kwenye account yako ya na taalifa nyingine kuhusiana uingiaji.