Category Archives: Uncategorized

Zawadi za kumpa mpenzi wako (Mwanaume/Mwanamke)

Mahusiano ya mapenzi huwa yana vitu ambavyo mnaweza fanyiana mukiwa wapenzi ili kufurahishana au kuoneshana jinsi mnavyopendana. Kutoa zawadi ni moja ya mambo ambayo mara nyingi watu hufanya ili kuwafurahisha wenza wao au uwaonesha jinsi wanavyo wapenda.

Lakini hii haimaanishi kuwa usipotoa au kupokea zawadi katika mahusiano yenu mtakua hampendani. Upendo ni zaidi ya kupeana zawadi na pia unaweza kuwa umetoa au kupokea zawadi bila kujua kama ni zawadi maana zawadi inaweza isiitwe “zawadi” moja kwa moja ila ikawa ni zawadi kwa mpokeaji.

Picha zenye maneno mazuri ya mapenzi BONYEZA HAPA>>

Zawadi za kwa mpenzi wako

Zawadi ni kitu kizuri katika mahusiano na haijalishi wewe ni mwanaume/mume au mwanamke/mke, unaweza pokea zawadi au kutoa zawadi kwa mpenzi wako bila tatizo. Unaweza toa kitu chochote kizuri kwa mpenzi wako kama zawadi, hijalishi ni kidogo au kikubwa. Kama unauhitaji wa kufungua ubongo na kujua zawadi gani ya kumpa mpenzi wako, unaweza angalia zawadi hizi chini kama zitakukua nzuri kwake.

Zawadi za kumpa mpenzi wako wa kike

  • Nguo nzuri za kuvaa nje
  • Nguo za Dani
  • Mkoba
  • Hereni
  • Bangili
  • Saa
  • Simu
  • Viatu
  • Mkufu

Zawadi za kumpa mpenzi wako wa kiume

  • Barua ulioandikwa maneno mazuri
  • Nguo nzuri za kuvaa nje
  • Nguo za Dani
  • Saa
  • Viatu

Hivyo juu ni kati ya vitu unavyoweza mpatia mtu kama zawadi mukiwa kwenye mahusiano. Lakini ni vema ukajaribu kufikilia ni kitu gani atakachokifurahia unapotaka kuchagua zawadi gani ni ya kumpatia mpenzi wako. Jiulize, kitu gani atakipenda kwa jinsi unavyomjua? Rangi gani anaipenda kwa jinsi unavyomjua? Kitu gani anatamani kwa jinsi unavyomjua? Anashida na nini kwa jinsi unavyomjua?. Maswali hayo na mengine kama hayo yatakufanya uchague kitu kizuri kitakacho mfurahisha zaidi mpenzi wako.

SMS za kumbembeleza mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

Inashauriwa kuweka harufu nzuri kwenye zawadi unazotoa kwa mpenzi wako. Harufu nzuri itafanya ahisi vizuri anapofungua zawadi yako. Na pia kisayansi; harufu huwa inasadia katika kukumbuka. Katika maisha yako kuna harufu nzuri hukukumbusha vitu, watu au matukio si ndio?

Tukiachilia mbali harufu nzuri, katika kumpatia zawadi mpenzi wako ubunifu ni kitu cha muhumu pia. Unaweza andaa tukio au ukasubiri tukio ndio ukampa zawadi uliomuandalia. Mbali na kusubiri matukio, unaweza mpa tu zawadi huku ukimpatia maneno mazuri toka moyoni mwako.

Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze kila mara BONYEZA HAPA>>>

Mambo 5 ya kuyajua unapotaka kumtongoza Mwanamke mtandaoni

Kutokana na teknolojia kuwaunganisha watu kupitia mitandao ya kijamii, watu wanaweza anzisha mahusiano ya mapenzi bila hata kuonana. Watu wengi tu hujikuta katika mahusiano ya mapenzi yalioanzia mitandaoni bila ya kuonana. Kuna mpaka ndoa ambazo zimefungwa zilizotokana na mahusiano yalioanzia mtandaoni bila kuonana.

Hapa kwenye ukurasa huu The bestgalaxy, tunaenda kukujuza mambo ya kuyajua mtu anapotaka mtongoza mwanamke mtandaoni. Hii ni kwaajili ya mwanaume ambae anataka kutupa kamba kwa mwanamke katika mitandao ya kijamii au app kama Facebook, WhatsApp, Instagram na Telegram. Unahitaji kujua mambo haya? Basi soma yafuatayo.

Jinsi ya kutunza mahusiano ya mbali BONYEZA HAPA>>>

Mambo ya kuyajua unapotaka kumtongoza mwanamke mtandaoni

Usitegeme kukufanyia mazuri maana hakujui.

Unapotaka kumtongoza mwanamke ambae hamjawahi kutana zaidi wewe kumuona mtandaoni, fahamu na kukubali kuwa hakujui. Kutokana na kutokukujua unaweza kutana na changamoto nyingi katika kuanzisha mahusiano. Anaweza kuwa hajibu ujumbe wako kwa wakati, anaweza kuwa mkali kwako, anaweza kuwa hajali hata kuondoka kwako kiasi kwamba anaweza kukublock muda wowote. Kiufupi usitegeme akufanyie mazuri maana hakujui sana kiasi cha kuzingatia au kujali hisia zako. Hii inaweza kuwa hata ni ishara ya kwamba unachati na mwanamke halisi na sio tapeli.

Unaweza kuwa si mmoja unaetuma ujumbe.

Kuna wanawake huwa ukiwatumia ujumbe kwenye mitandao ya kijamii, hawaonekani kusoma ujumbe kabisa. Kwa baadhi ya wanawake, hali hii inaweza sababishwa na kupokea ujumbe kutoka kwa watu wengi wasumbufu kiasi kwamba ujumbe wako haujaonekana au ameacha mazima kusoma jumbe zote zinatumwa na watu. Ukikutana na mwanamke wa namna hii, unaweza Endelea kumtumia ujumbe bila kukata tamaa au ukatafuta njia nyingine za kuwasiliana nae. Pia usisahau kuwa mbunifu ili kumvutia aendeleze maongezi na wewe.

SMS za kumbembeleza mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

Huangalia picha zako.

Ukifanikiwa kutumia ujumbe wa kwanza kwa mwanamke ulikutanane mtandaoni, unatakiwa kufahamu huwa akisha soma ujumbe wako, ataangalia picha zako kukujua. Kwa baadhi ya wanawake, picha zako zinaweza amua akujibu au asikijibu. Ukiwa na picha nzuri au unapost vitu vizuri, unaweza kuwa na nafasi kubwa ya kuanza mazungumzo nae. Endapo endapo ni mtu unaepost vitu vya hovyo kama matusi au picha zinazomtisha, unaweza ukakosa bahati ya kuchati nae kabisa.

Unaweza muona tofauti mtakapo kutana.

Kama unapendelea kuchangua mwanamke kwa kuangalia picha zake, basi fahamu kwanza kuwa siku hizi picha zanaweza kuwa tofauti na uhalisia wa mtu. Picha zinaweza kupitia michakato mingi inayoweza fanya mwanamke anaeonekana kwenye picha awe tofauti kidogo na jinsi anavyoonekana kwenye uhalisia. Mara nyingi utofauti unakua ni mdogo na unatakiwa kujiandaa nao ili ukianzisha mahusiano na kukutana nae, usishangae sana.

Anaweza kukupenda pia

Mapenzi ya mitandaoni yanaweza kujengwa na kufikia hatua za ndoa. Unaweza pata mwanamke unaempenda mtandaoni, ukapambana kujuana nae, mukaingia kwenye mahusiano na akawa anakupenda toka moyoni pia. Jambo hili linawezekana ila epuka kuwa msumbufu kwake na uwe makini pia na matapeli.

Mwisho; Kumtongoza mwanamke mtandaoni na kuanzisha mahusiano nae ni jambo zuri. Ila kuanzisha mahusiano kwa njia hii, unaweza kutana na changamoto ya mtu kukuigizia maisha na kukudanganya kwenye vitu vingi sana. Kiufupi ni ngumu kutambua maisha halisi ya baadhi ya watu kupitia picha zao.

Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze Kila mala BONYEZA HAPA>>>

Tofauti kati ya Facebook Lite na Facebook ya kawaida kwenye simu yako

Ukihitaji kutumia mtandao wa kijamii wa Facebook kwenye simu, unaweza tumia kupitia njia mbili. Njia ya kwanza kabisa ni kutumia mtandao wa Facebook moja kwa moja katika tuvuti/website ya facebook. Njia ya pili ni kutumia Facebook kupitia app maalumu ambazo ni “Facebook lite” and “Facebook ya kawaida”.
Njia nzuri na rahisi ya kutumia mtandao wa Facebook ni njia ya app. App rasmi za Facebook zipo mbili, unaweza tumia app ya kawaida ya Facebook au ukatumia app ya Facebook lite ila kikubwa ni utambue tofauti ya app hizi. App hizi zinautofauti na hapa chini tumeweka tofauti chache kati ya Facebook lite na Facebook ya kawaida.

Tofauti kati ya Facebook Lite na Facebook ya kawaida kwenye simu yako

Matangazo mengi

Mtu unapotumia mtandao wa Facebook kupitia app ya Facebook lite hua unaoneshwa matangazo machache kuliko akitumia Facebook ya kawaida.
Unapotumia mtandao wa Facebook huwa kuna matangazo ambayo hujitokeza. Matangazo haya huioneshwa na kampuni ya Meta kwa kila mtu anaetumia mtandao wa Facebook Bure. Kuna watu hua wanalipia pesa Facebook ili kuyaondoa matangazo haya kwenye akaunti zao.

Kutumia data sana


Katika mtandao wa Facebook, Kuna vitu vingi sana ambayo mtu unaweza tumia bando lako kuvifurahia. Lakini unapaswa kufahamu huwa unapotumia app ya Facebook lite bando lako litatumika kidogo ukilinganisha na ukitumia Facebook ya kawaida.
App ya Facebook lite imeundwa kutumia data kidogo na inafanya vizuri hata kama upo kwenye mazingira ambayo mtandao unasumbua.

Kuchukua nafasi kubwa kwenye simu


Ukiingiza Facebook ya kawaida pamoja na Facebook lite kwenye simu yako kisha ukaangalia nafasi zilizochukua kwenye simu yako, utagundua Facebook ya kawaida imechukua nafasi kubwa sana kwenye simu yako kuliko Facebook lite.
Facebook lite ni app ndogo isiochukua nafasi kubwa sana kwenye Storage ya simu yako.

Ubora wa picha na video


Facebook lite ni app inayoonesha ubora wa chini wa picha ukilinganisha na app ya Facebook ya kawaida. Ukihitaji kuona ubora katika video na picha katika mtandao wa Facebook, tumia Facebook ya kawaida na sio Facebook lite. Facebook lite inawezapunguza ubora wa picha au video unapoziingiza au unapozitoa mtandaoni.

Katika video na picha za 360°

Kama ni mpenzi wa video na picha za 360° unatakiwa kufahamu huwa huwezi angalia video na picha za 360° ukiwa unatumia Facebook lite. Video na picha za 360° zinapatikana katika mtandao wa Facebook lakini unahitaji kuwa na app ya Facebook ya kawaida ili kuangalia kwenye kifaa chako.

Ni vema kufahamu tofauti ya app ya Facebook lite na Facebook ya kawaida ili uweza chagua unahitaji kutumia ipi, kwanini na wakati gani. Endelea kuwa karibu zaidi na The bestgalaxy.

Faida za kufanya mapenzi(Tendo la ndoa)


Mapenzi tunaweza kusema ni hisia, lakini kufanya mapenzi ni Tendo ambalo pia tunaliita Tendo la ndoa. Tendo hili kikawada limekua likihusisha watu wa jinsi mbili tofauti ambao wanaweza kuwa wapo katika mahusiano ya kimapenzi. Kwa upande mwingine tunaweza alezea kuwa ni moja kati ya matendo ya asili ya binadamu.

Kumekua na tafiti nyingi kuhusu mwanadamu kushiliki Tendo la ndoa na kuna faida nyingi ambazo zimeonekana kwa watu kutokana kufanya Tendo hili. Hapa chini unaweza soma faida 5 za kufanya mapenzi (Tendo la ndoa).

Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze Kila mala BONYEZA HAPA>>>

Faida 5 za kufanya Tendo la ndoa (Mapenzi)

Kupunguza Msongo Wa Mawazo na Wasiwasi

Kufanya Tendo kunaweza changia mtu kupunguza Msongo Wa Mawazo na wasi wasi. Utolewaji wa oxytocin, endorphins, na homoni nyingine za kukufanya ujisike vizuri Katika tendo, unaweza sababisha mtu kupunguza msongo wa mawazo na wasi wasi.

Kumuweka mtu mbali na magonjwa ya moyo

Katika upande wa magonjwa ya moyo, Tendo la ndoa linaweza kumuweka mtu mbali na magonjwa haya. Kufanya mapenzi mara kwa mara kwa mwanaume au mwanamke kunaweza kusaidia kupunguza hatari ya mtu huyo kupata magonjwa ya moyo, kama vile kiharusi.

kupunguza maumivu

Kufanya Tendo pia huwa ni msaada katika kupungaza maumivu ya mwili kwa mwanaume au mwanamke. Kufanya mapenzi au Tendo la ndoa kunaweza fanya maumivu ya kichwa, maumivu ya misuli, au maumivu ya tumbo, yakapungua.

Kuongeza Kinga Za Mwili

Tendo la ndoa linachango wake katika Kinga za Mwili wa binadamu. Kufanya mapenzi kunaweza kusaidia kuongeza viwango vya kinga mwilini, na hivyo kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya baadhi ya magonjwa.

Kuongeza Ukaribu

Kushiliki Tendo pia huwa kuna umuhimu katika kuongeza mahusiano na ukaribu kati ya wapenzi. Tendo hili likifanywa na watu waliokatika mahusiano mazuri ya mapenzi kusaidia kuboresha uhusiano wao wa kimapenzi na kufanya wawe karibu zaidi.

Maneno ambayo hautakiwi kusema kwa mwenza wako BONYEZA HAPA>>>

Hizo ni faida Tano kati ya faida nyingi za Kushiliki Tendo la ndoa. Lakini unapaswa kufahamu huwa Tendo hili pia lina athari andapo litafanywa bila kujali usama maana kunamagonjwa huambukizwa kupitia Tendo hili.

WhatsApp: kuview status ya mtu na isionekane umeona

WhatsApp ni app inayotumika na watu wengi na app hii inavipengele vingi ikiwemo kipengele cha status. Kipengele  cha status huwezesha watu kushiriki hali zao na watu wengine. Kuiona status ya mtu kwenye WhatsApp utatakiwa kuwa na namba ya huyo mtu na yeye kuwa na namba yako. Na endapo ukiiangalia/ukiview  status ya mtu, ataona kuwa umeangalia status yake.

Sasa Kuna baadhi ya watumiji wa WhatsApp huwa wanataka kujua jinsi ya kuview status ya mtu na isionekane kuwa wameona kwa aliepost. Hapa The bestgalaxy tunaenda kukufungua juu ya hili kwa kukupa njia nzuri na salama ya kuanaglia au kuview status ya mtu bila kuonekana umeona.

WhatsApp yako inatatizo? Jifunze jinsi ya kutatua BONYEZA HAPA>>>

Jinsi ya kuview Whatsapps status bila kuonekana umeona

Kuview Whatsapp status ya  mtu bila kuonekana kunawezekana kufanyika kwa njia zaidi ya moja lakini njia nyingi sio salama kwa akaunti yako ya WhatsApp maana zinaweza kufanya uzuiwe kutumia WhatsApp. Njia salama ya kuview Whatsapp status ya  mtu bila kuonekana ni kuzima “Read receipts” kwenye app yako rasimi ya whatsApp. Fuata hatua zifuatazo kufanya hivyo.

  • Fungua App yako ya WhatsApp na uguse vidoti vitatu vilivyo juu kulia.
  • Chagua “Settings” kwenye orodha ya chaguzi zitakazo jitokeza.
  • Baada ya hapo ingia katika sehemu ilioandikwa “Privacy” na uzime kipengele kilichoandikwa“Read receipts
  • Baada ya kuzima kipengele cha hicho utakua na uwezo wa kungalia status za watu bila wenyenazo kujua. Kwaiyo ukizima, unaweza kuview status bila kuacha nyayo.

Kipengele hiki ni kipengele salama na hakiwezi pelekea akaunti yako ya Whatsapp kufungwa na Whatsapp. Lakini ubaya wake ni kwamba ukikizima huwa kinafanya usijue watu wanapoangalia status zako au kujua kuwa wamesoma sms ulizowatumia. Na wala wewe hautaweza kuonekana kama umesoma sms zao.

Kutokana na jambo hili unashauriwa; ukisha maliza kuangalia status ya mtu ambae hutaki ajue umeangalia, kiwashe tena hicho kipengele cha “Read receipts”.

Njia hii ni njia nzuri kuliko kutumia app za WhatsApp zisizo rasimi zilioweka urahisi katika kuangalia status bila kuacha nyayo. App hizo zinazoweza pelekea WhatsApp kuzuia akauti yako na ndio maana hatupendekezi japo unaweza tumia pia.

Picha zenye maneno mazuri ya mapenzi

Mawasiliano ni jambo la msingi katika mahusiano na siku hizi watu hutumia mitandao ya kijamii kuwasiliana na wapenzi wao. Mitandao hii ya kijamii itaweza kutumika kutuma jumbe za maandishi na sauti. Mbali na vitu hivyo, Video na picha ni kati ya vitu ambayo watu wanaweza tumiana kupitia mitandao ya kijamii.

Kutokana na mitandao ya kuwezesha watu kutumiana picha, kunawatu hupendelea kutuma picha zenye ujumbe au maneno mazuri kwa wapenzi wao katika mahusiano. Jambo hili ni zuri sana na linapendeza maana ni njia nzuri ya kuelezea upendo. Kama na wewe ni moja wa watu hawa, basi hapa kunaweza kuwa na kitu kizuri kwaajili yako.

Hapa chini tumeweka picha zenye maneno mazuri ya mapenzi ambazo unaweza zitumia ikiwa wewe ni moja wa watu waopenda kutumia picha hizi. Unaweza chagua inayoendana na hali yako ya mahusiano na kuitumia.

Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze Kila mala BONYEZA HAPA>>>

Picha zenye maneno mazuri ya mapenzi 

Ujumbe wa picha hii: Penzi lako hunifanya niwe ninafuraha kila nikikutazama na kutabasamu kila nikikuwaza… Nakupenda sana.

Ujumbe wa picha hii: Wewe ndio sababu ya mimi kujua upendo ni nini. Najifuza mengi toka kwako… Umekua kipenzi cha moyo stamani upunguze penzi lako.

Ujumbe wa picha hii: Katika Dunia hii nakupenda wewe.

Ujumbe wa picha hii: Neno nakupenda halitoshi kuelezea ninavyokupenda. Uwepo wako maishani mwangu ni kama mwanga… Nakuhitaji mpenzi nahisi bila wewe siwezi songa.

Ujumbe wa picha hii: Hakuna Penzi lililodumu kwa kusikiliza sana maneno ya watu. Ila kuna watu hudumu kwenye mapenzi kwa kusikilizana.

Nafikili katika picha hizi, unawezakua umepata unayoweza kutumia. Kama unatatizo katika kuidownload picha unayoitaka hapa, unaweza jaribu kuipakua kwa kugusa kwa muda wa sekunde chache alafu chagua “Download image” kwenye chaguzi zitakazojitokeza.

Kuwa mjanja! Tufuate kwenye akaunti zetu mpya za kijamii ; Instagram na Facebook

SMS za kumfanya mpenzi wako afurahi BONYEZA HAPA>>>

Magari ya Umeme: Fahamu mambo 5 kuhusu magari haya

Magari ya umeme yameonekana kuwa ni future katika teknolojia ya magari.

Kumekua na mipango mikubwa ya kuwezesha magari kuifikia sehemu ambayo magari ya diesel na petrol yameifikia. Na sio kuyafikia tu, Magari ya umeme yaenda kuwa mbadala wa Magari hayo ili kusimamisha uchafuzi wa hali ya hewa unaotokana na uchomaji wa diesel na petrol hapa Duniani.

Hapa The bestgalaxy tumekuandalia mambo matano kuhusu magari haya ya umeme. Kama wewe ni mtu unaependa kujua mambo kuhusu magari ya umeme, basi chukua muda wako kuyasoma hapa chini.

Mambo 5 kuhusu magari ya umeme

Betri ni moja ya vitu vya gharama sana kwenye magari haya

Kama tunavyo fahamu, magari huwa yananunuliwa, yatumika na katika kutumika huwa tunabadilisha sehemu za magari zilizochoka na kuweka mpya. Karibu kila sehemu tunayobadilisha kwenye gari hughalimu pesa.  Sasa katika magari ya umeme ukihitaji kubadili betri, huwa inagharimu pesa nyingi kuliko sehemu zote. Betri ya sehemu ya gharama sana katika magari ya umeme.

Unashauriwa kuangalia vituo vya kuchaji kabla haujanunua

Kutokana na magari haya kuonekana future, unaweza kuwa na shauku ya kufanya kila liwezekanano ili kununua. Lakini unapaswa kujua kuwa, kumiliki magari haya ya umeme katika sehemu iso na miundombinu mizuri kwajili ya magari ya umeme ni kitu unachoweza jutia. Unashariwa kuangalia zaidi upatikanaji wa vituo vya kuchaji katika mazingira yako kabla ya kuchaji magari haya ili usiteseke kupata chaji unapoishiwa ukiwa njiani.

Unaweza kuyachaji magari ya umeme nyumbani

Kutokana na Magari haya kutumia umeme, kunauwezekano wa kuyachaji nyumbani tu kwa umeme wa nyumbani. Lakini unapaswa kufahamu kuwa chaji zinazoweza kuwekwa nyumbani huwa hazina nguvu ya kujaza betri kwa haraka ukilinganisha na chaji zinazopatikana kwenye vituo maalum. Hivyo umuhimu wa vituo vya kuchajia upo pale pale.

Wamiliki wameonekana kupata changamoto katika baridi

Katika msimu wa baridi,  watu wanaomiliki magari ya umeme waishio nchi ambazo hukumbwa na theluji wamekumbana na changamoto katika kutumia magari haya. Changamoto hizi ni pamoja na kuchelewa kujaa kwa betri za magari na kupungua kwa “Range” (Umbali ambao gari linaweza kutembea kabla haujalipeleka kuchaji tena).

Yanaendelea kushuka bei

Watu wengi wanaotupia macho magari ya umeme huwa wanaishia kuyatupia macho magari ya kifahari au Luxuly cars zinazouzwa ghari sana na kusahau kuwa kuna magari ya umeme ya kawaida yasio na bei ya juu sana japo ni bado inaweza kuwa dharama sana kwa baadhi ya watu. Ujio wa magari ya umeme ni mapinduzi yanayogusa watu wote na kila siku zinavyozidi kwenda kunajisi bei zinaenda kuwa rafiki.

Unawazo gani kuhusu mapinduzi haya ya magari? Sawa, asante sana kwa muda wako. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mambo mengine.

Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze kila mara

Baadhi ya watu wamekua wakijiuliza ni jinsi gani wanaweza wafanya wapenzi wao wawawaze kila mara au mara kwa mara. Kuna muda wazo hili humjia mtu baada ya kuona anapuuzwa kiasi flani na mpenzi wake au akiwa na hitaji la kumuweka mpenzi wake karibu zaidi.

Kama ni moja kati ya watu ambao wanataka kujua juu ya hili kwasababu hiyo au sababu nyingine tofauti. The bestgalaxy inakupa mwanga kidogo juu ya hili hapa chini. Tunaenda kuangalia vitu vichache unavyoweza jaribu kumfanya mpenzi wako akuwaze mara kwa mara.

Sms za kumfanya mpenzi wako afurahi BONYEZA HAPA>>>

Mambo ya kufanya mpenzi wako akuwaze mara kwa mara (Mwanamke au mwanaume)

Uwe msaada na mshauri wake mzuri

Mukiwa kwenye mahusiano mpenzi wako anaweza kuwa na matatizo ambayo huitaji umshauli au umsaidie kwanjia nyingine. Endapo utakua msaada na mshauri mzuri kwake basi utakua kichwani mwake kila mara maana tukiwa kama binadamu hua mara nyingi tunahitaji msaada. Hakikisha haupuuzi matatizo yake na hata yakikushinda fanya kumshauri kwa maneno mazuri. Na usiwe msaada kwenye matatizo tu, hata kwenye nyakati za furaha kuwa nae. Kusaidia kunaweza jumuisha kumpa pesa maana vitu vingi kwenye maisha ya sasa huitaji pesa .

Uwe unampa ahadi

Katika mahusiano ahadi zinaweza fanya hata mahusiano yadumu maana mnakua mnajua mnakoelekea. Ni vema sana ukawa unampa ahadi mpenzi wako na ahadi hizi zinaweza kuwa kubwa au ndogo lakini tambua kuwa ahadi ni deni kwa mpenzi wako. Unaweza huahidi mpenzi wako kuhusu vitu vya kesho, mwezi ujao, mwakani na hata maishani. Mtu anaekudai atakua anakukumbuka hata ukisahau wewe.

Ila tambua tu ahadi ni deni na kuna baadhi ya ahadi huharibu mpaka maisha ya mtu. Mfano; unamuahidi mtu mtaoana alafu anazama kwenye penzi na kukupa moyo wote  mpaka maisha alafu unaanza kumuona mjinga kisa akili yote ipo kwako na hutaki muoane tena. Ivi nafikili maisha yake utakua umeyavuruga kiasi gani?. Unaweza kuwa umewahi pewa ahadi kubwa za uongo lakini jambo hilo likufuze kuwa mkweli na sio muongo.

Mambo muhimu kufanya kwa mpenzi mwenye hasira au ukorofI BONYEZA HAPA>>>

Ukiwa nae hakikisha mnakua na furaha

Kuna nyakati nyingine kwenye mahusiano mnaweza kuwa na hasira au maugovi lakini nyakati ambazo hata mkiachana au mkiwa mbali mnaziwaza ni nyakati zile za furaha. Ukiwa kwenye mahusianao hakikisha ukiwa na mpenzi wako unakua chanzo cha furaha na sio maugomvi. Mpenzi wako anaweza kua amekufanya uchukie lakini pamoja na kuchukia kwako hakikisha  unamaliza utata na unatengeneza hali ya furaha ukiwa nae maana nyakati za furaha ndio nyakati ambazo tunaziwaza sana.

Mfano; Kuna muda unaweza chati na mpenzi wako vizuri mpaka ukarudia kusoma sms mara kumi kwa siku huku ukimuwaza. Au umeongea nae vizuri muda uliopita lakini tukio zima la maongezi yenu lipokichwani unaliwaza kila mara huku ukitabasamu.  Hii inaweza kuwa ni kwasababu mulikua kwenye nyakati inayofurahisha na Kama tunavyofahamu, hakuna mtu asiependa kuziwaza nyakati zinazofurahisha.

Pia usisahau kutumia maneno ya upendo na kumsifu ili ajisikie vizuri na kupata furaha. Pambana kutengeneza nyakati za furaha mkiwa wote alafu hizi nyakati zitatengeneza historia nzuri ya mahusiano yenu ambayo mtakua mkivutiwa kuendelea kuiandika.

Usije tumia nguvu kubwa kufanya mtu akuwaze kila mara kama hauna mpango nae kimaisha maana siku utakapomuacha unaweza kuwa na deni kubwa katika moyo wake. Asante kwa kusoma na endelea kuwa karibu na The bestgalaxy.

Jinsi ya kutuma pesa Kenya na Tanzania (Vodacom/Safaricom)

Kutuma pesa nje ya nchi ilikua ni jambo gumu sana katika miaka ya nyuma, lakini wakati huu jambo hili ni jambo jepesi kiasi kiasi kwamba unaweza fanya kiganjani pako ndani ya dakika mbili. Hii yote ni kwasababu ya Teknolojia ambayo lengo lake ni kurahisisha maisha ya Binadamu.

Hapa The bestgalaxy tunaenda kuangalia jinsi ya kutuma pesa Kenya na Tanzania kwakuhusisha Safaricom Kenya na Vodacom Tanzania. Kama upo nchi ya Tanzania, unaweza tumia mtandao wa Vodacom kumtumia pesa mtu kwa Mpesa akiwa kenya anatumia mtandao wa Safaricom. Pia ukiwa kenya unatumia Safaricom unaweza mtumia pesa mtu kwa Mpesa akiwa anatumia mtandao wa Vodacom Tanzania.

Jinsi ya kutengeneza Logo ya biashara au Binafsi BONYEZA HAPA>>>

Kutuma pesa Kenya na Tanzania (Vodacom/Safaricom)

Unataka kujua jinsi ya kutuma? Usijali, hapa chini kuna maelezo juu ya hatua unazoweza kufuata pale unapotaka kutuma pesa ukiwa Tanzania na kenya kwakutumia mtandao wa Vodacom au Safaricom.

Kutuma pesa toka Tanzania kwenda Safaricom Kenya kwa kutumia Mpesa(Vodacom)

  • Fungua App ya Mpesa na uguse sehemu ilioandikwa “Services” alafu utaletewa orodha ya huduma.
  • Chagua huduma ilioandikwa “International Transfers” kwenye orodha hiyo.
  • Baada ya kufanya hiyo utapelekwa kwenye ukurasa utakao takiwa kuchagua nchi unayotaka pesa iende. Utachagua Kenya kwakua ndiko unataka kutuma pesa.
  • Baada ya kuchagua nchi utaletewa ukurasa wa kuchagua mtandao. Wewe utachagua mtandao wa  Safaricom kwakua mtu unaemtumia anatumia Safaricom.
  • Baada ya kuchagua, utapelekwa kwenye ukurasa utakao takiwa kujaza namba ya simu ya mtu unaemtumia pesa kwa mfumo wa kimataifa (254xxxx) kisha andika kiasi unachotaka kutuma. Na ukishajaza utabonyeza kitufe kilichoandikwa “Endelea” ili kuendelea na hatua nyingine za uthibisho wa kutuma pesa yako.

Sending money from Kenya to Tanzania with Mpesa (Safaricom)

  •  Dial *334# to open Mpesa Global.
  • Select “Send Money Abroad”.
  • Select “Send to Mobile Number”
  • Select “Tanzania” as a county you want to send money.
  • Enter Recipient Mobile Number in International Format (255xxxxxx)
  • Enter Amount of Money you want to send.
  • Select  source of fund and purpose of Funds then confirm.

Mwisho ningependa kukukumbusha kuwa makini katika kutuma pesa yako ili kuepuka kutuma pesa kimakosa. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy na usiache kufuatilia The bestgalaxy.

Mambo ya kuzingatia unapotaka kufanya Tendo (Wapenzi)

Kama ni mtu ambae upo katika mahusiano ya mapenzi na mmefikia hatua ya kutaka kucheza mchezo wa mapenzi, inaweza kuwa ni jambo zuri.
Mwanaume ikiwa umefika umri ambao unaruhurusu kufanya mchezo huu na mwanamke pia amefika umri, mnaweza kufanya mapenzi/tendo.
Lakini jambo hili linaweza kuwa zuri zaidi na salama kwenu kama mambo ambayo tunayaeleza hapa yatazingatiwa.

Mambo ya kuzingatia unapotaka kufanya tendo (mwanaume/mwanamke)

Usafi wa mwili

Usafi ni muhimu kuzingatia pale unapotaka kucheza mchezo wa mapenzi. Ikiwa wewe ni mwanaume au mwanamke, usafi unatakiwa kuuweka mbele maana uchafu unaweza mtoa mwenza wako raha ya mchezo. Hakikisha mdomo wako uko vizuri na hizo sehemu za mchezo husika siko safi pia. Epuka kuweka mdomoni vitu vyenye harufu mbaya na utumie vitu vinavyoleta harufu nzuri ili usimkere mwenza wako.

Kutumia kinga

Ikiwa mahusiano yenu yamewapeleka kucheza mchezo lakini hamjajuana vizuri, ni vema kuzingatia matumizi ya Kinga kwenye mchezo huo. Kinga ni muhimu maana huzuia mimba zisizotarajia na pia maambukizi ya baadhi ya magonjwa ikiwemo virusi vya Ukimwi. Ngono zembe inaweza kumpa mwenza wako au kukupatia wewe athari bila kujali wewe ni mwanaume au mwanamke. Ndio maana mtu anashauriwa kutumia mpira wa Kondom ambao ni Kinga unapokutana kimwili na mtu usiemjua kiundani.

Mazoezi ya mwili ambayo husaidia katika tendo BONYEZA HAPA>>>

Kuchukua tahadhari ya matukio mabaya

Kama mazingira ambayo mmekubaliana kucheza mchezo huu ni mageni kwako, ni vema ukachukua tahadhari. Hakikisha unakua makini ili vitu vyako visiibiwe, kuwa makini katika vitu unavyoweka mdomani ili usipewe dawa, kuwa makini pia usije kurekodiwa video na watu wabaya. Usiache kuzingatia jambo hili kama hata huyo mwenza wako hamjajuana vizuri maana baadhi ya watu huwa na nia mbaya tofauti na mapenzi.

Elewa mipaka yako na kuheshimu

Watu hucheza mchezo wa mapenzi na kila mtu huwa na mipaka yake katika mchezo huu. Sasa ni vema ukaelewa na wewe mipaka yako ni ipi na kuisimamia pale utakapokua ukicheza mchezo bila kumtoa mchezoni mwenza wako. Pia Kama mwenza wako atakua na mipaka, jiweke tayari kuiheshimu mipaka hiyo bila kutoka mchezoni. Na Kama mtavunja mipaka yenu basi ile kwa makubaliano.

Kuondoa woga wa kupita kiasi


Woga ukipita kiasi katika mchezo wa mapenzi, unaweza ushindwe hata kucheza mchezo vizuri. Baadhi ya wanaume wamekua wakishindwa kusimama uanaume wao kutokana na kuogopa. Ni vema kuondoa woga na kujiamini ukiwa Kama mwanaume au mwanamke ili ucheze katika nafasi yako vizuri na kumfurahisha mwenza wako.

Mambo hayo machache na yanaweza kuwa marahisi kuyapuuza, lakini ni mambo muhimu kuzingatia unapotaka kukutana kimchezo na mwenza wako hata ikiwa ni mara ya kwanza.