Category Archives: Love

Jinsi ya kumueleza hisia zako Mwanaume bila kusema unampenda

Kuna mtaalam mmoja wa mambo haya alisema hivi…

Mara nyingi kuwa na aibu ndio chanzo cha wanawake wengi kushindwa kuwaeleza hisia zao kwa wanaume wanao wahitaji na kibaya zaidi wanawake tunaweza kutunza siri zetu kwa muda mrefu hivyo, hutunza pia hizo hisia kama siri nyingine japo hutuumiza sana pale wanaume tunaowapenda  wanapoenda kwa wanawake wengine.

Wapo baadhi ya wanawake ambao hawana uoga katika kueleza hisia zao kwa wanaume na pia huwa huru pindi wanapokuwa karibu na wanaume. Lakini wanawake wengi ni sisi ambao tunashindwa hata kuongea pindi tunapo wakaribia wanaume tunaowapenda.

Sio kwamba tunakosa ustadi wa kimapenzi wa kimapenzi au hatujui kutamka maneno ya kueleza hisia zetu ila ni tunasikia raha na furaha inayotuzidi mpaka tunaogopa maana mapigo ya moyo hupiga kwa kasi na maneno yote hupotea na hurejea baada ya mwanaume uondoka.

Kuwa na aibu hakupaswi kukuzuia kumueleza mwanaume unayempenda hisia zako. Kuna mambo madogo madogo ambayo unaweza kuyafanya na ukafanikiwa kufikisha ujumbe wa hisia zako kwa mwanaume unayempenda lakini kitu cha msingi inatakiwa kujiamini tu.

Badala ya kumfuata na kumwambia mwanaume vile unajiskia juu yake unaweza tumia njia ya vitendo itakayo mfanya kukuzingatia na kuelewa kuwa unamuhitaji na utamfanya akuhitaji pia.

1.Wasiliana nae kwa macho.

Kuwasiliana kwa macho ni moja wapo ya njia rahisi na ya hila zaidi ya kumruhusu mwanaume ajue kuwa unavutiwa naye. Wakati mwingine wazo la kuwasiliana na mtu usiempenda linaonekana kuwa la kichefuchefu, lakini ikiwa unafikiria ni mzuri, muangalie. Kama ni muoga sana basi jaribu kuangaliana na picha yake kwenye simu yako. Usimtazame kama wewe ni polisi na yuko kwenye orodha ya watu wanaotafutwa. Mtazamo mfupi ndio unahitajika yaani muangalia mpaka ugonganenae macho na agundue ulikua unamungalia kisha acha kumuangalia na uiangalie sehemu nyingine (ila usingalie chini kamwe) huku ukiendelea na shughuli zako. Kitendo hiki ukiwa unakifanya kitamfanya ahisi kitu juu yako na anaweza kuanza mawazo ya upendo juu yako.

Katika Matumizi yako ya simu usifanye vitu hivi (Unaweza juta!) GUSA HAPA>>>

2. Weka tabasamu.

Pindi unapomuangalia hakikisha anakukuta na tabasamu zuri la kupendeza. Sio anakukuta unamuangalia huku umeweka sura ya kawaida tu utamfanya asihisi chochote juu yako na akakuona ni mtu unaemfuatilia mambo yake hivyo hakikisha unaweka tabasamu zuri litalomuonesha kufurahishwa na yeye. Akikukuta katika hali hii moja kwa moja atagundua umevutiwa nae.

3. Muulize swali kuhusu jambo flani.

Hii ni njia nzuri sana kwaajili ya kuanzisha mahusiano kati yenu.

Kuuliza swali kuhusu jambo flani au kuomba usaidizi juu ya jambo flani. Unaweza muuliza mwaswali ambayo yatamfanta ajibu kwa urefu au atumie muda wake kukuelekeza.

Mfano: Eliy, nimependa wallpaper ya simu yako, naomba nielekeze jinsi ya kuweka wallpaper kama yako?

Naomba nielekeze jinsi ya kufanya kitu hiki?

Njia hii pia utakusaidia kuanzisha mazungumzo nae yaani pale unapokosa neno la kuongea au kuanza mazungumzo basi unaweza uuliza kuhusu kitu flani.

Mbinu 6 zitakazo kusaidia katika mapishi yako GUSA HAPA>>

4. Mtege kwa kujichezesha.

Kila mwanamke anavitu ambavyo anajua vinamshawishi zaidi mwanaume katika mwili wake. Vitu hivi vinaweza kuwa ni lips nzuri, macho na vinginevyo. Vitu hivi unaweza vitumia pale ambapo unakuambele ya macho yake au unapogundua anakuangalia. Kuvitumia vitu hivi kunaweza kumchanganya mwanaume kisawa sawa mpaka akashindwa kuongea na kumfanya avutiwe na wewe zaidi.

 Mfano, unaweza zichezesha lips zako pindi anapokuangalia na kukuelekeza kitu fulani ulicho omba akuelekeze.

Kwakufanya vitendo Kama hivi kutachochea hisia zake kwako.

5. Toa maoni juu ya kile unachokiona kwake na pia usisahau kumsifia na kusifu anavyovipenda.

Kila mtu anapenda kusifiwa na  sikuzote watu huwapenda watu wanaowasifu pia unachotakiwa kujua ni kwamba  wanaume wengi huongeza juhudi katika jambo fulani pale wanaposifiwa yaani kama ni mchezaji mpira alafu ukawa unamwabia kuhusu uchezaji wake mzuri wa mpira basi utamfanya ajiskie vizuri mpaka ataanza kukualika mazoezini ili tu umuone anachokifanya na umsifie tena. Hivyo basi kumsifu inaweza kuwa njia nzuri ya kufanya avutiwe na wewe.

6. Usichukue vitu kibinafsi.

Ikiwa umemfanyia yote hayo na bado haoneshi matokeo mazuri juu yako, Usihisi kuwa wewe ni mbaya au hunamvuto. Huenda haoneshi dalili nzuri juu yako kwasababu hataki kukuchezea hivyo unapaswa kuheshimu pia mawazo yake na kuendelea na maisha yako huku ukimtafauta anaekupenda kwa dhati. 

SMS za mchana mwema kwa mpenzi wako

Ukiwa kwenye mahusiano Unaweza kufanyia vitu vingi kwema kwa mweza wako ili kuonesha unamjali. Kutumia ujumbe wa mapenzi mpenzi wako ni Moja ya Jambo linaloonesha kujali pia… Mukiwa ni wapenzi mulio mbali hii inaweza kuwa ni kitu muhimu kinachojenga mahusiano kuliko hata kutuma tuma pesa.

Zifuatazo ni SMS au meseji za kumtakia mchana mwema mpenzi wako. Kama unahitaji Unaweza chagua zinazoendana na mahusiano yako kwa sasa kisha ukazitumia kwa umpendae. Endelea kuwa karibu na The Bestgalaxy kwa mambo mengine mazuri zaidi.

SMS za mchana mwema kwa mpenzi wako

Upendo wangu kwako huongezeka kila wakati ninapokutazama. Hautafifia wala kuisha kwa sababu hauna mwisho. Kila mara kumbuka kuwa Nakupenda sana na kwa muda huu nakutakia mchana mwema kipenzi changu.



Mpenzi, muda huu nakukumbusha tu kuwa wewe ndio chaguo langu. Yaani naomba ujue kuwa wewe ni Mfalme wa kasri langu na kwamba moyo uliokaa kifuani mwangu utalidunda jina lako. Ninakupenda zaidi ya ninavyoweza kusema nakupenda. Mchana mwema mpenzi wangu.






Nakutakia mume/mke mtamu zaidi ulimwenguni siku njema. Hakuna mtu katika ulimwengu mzima anaweza kuwa mpenzi wa maisha yangu kwa sababu nafasi hiyo tayari imechukuliwa na wewe, mume/mke wangu mpendwa. Nakupenda Saana na napenda kukupenda.



Asante kwa kupenda kila kitu changu, pamoja na kutokamilika kwangu. Mungu alinipa zawadi isiyo na kifani maishani mwangu pale alipokuumba wewe mpenzi wangu. Nakupenda sana kuliko ujuavyo.




Tambua kuwa wewe ni mtu pekee katika ulimwengu wote ambaye hufanya maisha yangu kuwa kamili kabisa na maridadi. Mpendwa, asante kwa kuleta joto na mwangaza katika maisha yangu. Sijawahi jutia kukupenda.





Nina nafasi moyoni mwangu ambayo hakuna mtu anayeweza kuchukua kwa sababu hakuna mtu mwingine anayeweza kunifanya nifurahi kama unavyonifanya. Nakutakia mchana mwema.




Wewe ni damu ambayo hupitia mishipa yangu. Wewe ndiye kipande muhimu ambacho hufanya roho yangu ikamilike. Siwezi kamwe kuishi katika ulimwengu huu bila wewe, mpenzi wangu wa thamani. Kuwa na siku mchana mwema huko uliko!


SMS za kumtakia mpenzi wako usiku mwema GUSA HAPA>>>




Kuangalia machoni pako kunanipeleka kwenye ulimwengu wenye zaidi ya maelfu ya furaha. Penzi lako hufanya nijihisi Niko paradiso. Umeniweza sasa, naomba kokote uendako usisahau kuwa nakupenda mpenzi wangu. Mchana mwema kwako.

Kila nikiona simu au SMS toka kwako moyo wangu hudunda kwa furaha… Kiufupi nakupenda na natamani kuelezea upendo wangu zaidi ya kukuambia “nakupenda” ili tu utambue na usije kuniumiza. Tambua hilo kipenzi changu… Nakutakia mchana mwema.

Ukiona dalili hizi Jua Account yako ya Facebook  imedukuliwa na si salama GUSA HAPA>>>>

Maneno ambayo hautakiwi kusema kwa mwenza wako

Endapo umekwisha ingia katika mahusiano au unatarajia kuingia katika mahusiano ya kimapenzi, yapo mambo yanyofaa ambayo unaweza kumwambia mpenzi wako naye akafurahi, lakini yapo mambo ambayo kimsingi hupaswi kabisa kumwambia mpenzi wako. Kwani endapo utaamua kumwambia utatengeneza njia ambayo itawafanya mahusiono yenu yafe mara moja.
Maneno yafuatayo ni hatari kwa kuwa yanaleta madhara makubwa moyoni mwa mlengwa na ni vyema kuzuia kuyatamka kwa namna yoyote ile.

Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze Kila mara BONYEZA HAPA>>>

Maneno ambayo hutakiwi kuyasema kwa mwenza wako


1. Nakuchukia

Chuki ni kitu kikubwa sana, kwa kweli huwezi kuishi na mtu ambaye unamchukia. Hutakiwi kumtamkia mwenza wako neno hili. Unaweza kuchukia tabia yake lakini si yeye mwenyewe. Njia nzuri ni kusema kuwa “Nachukia au sipendi tabia yako ya kuchelewa kurudi nyumbani” au maneno yanayofanana na hayo.


2. Maneno ya matusi

Maneno kama “mjinga” au “mpumbavu” yasitumike kwa mwenza wako hata kama yana ukweli ndani yake. Japo ujinga ni kutofahamu kitu fulani lakini neno hili linaleta majeraha kama likitoka kwa mwenza. Hasa kama linatoka wakati wa ugomvi au kutofautiana.
Usiseme maneno mabaya yanayomshusha mweza wako mfano kuhusu mwonekano mbaya wa mwenza wako kama “sura mbaya”,”Mnene kama nguruwe” na maneno mengine kama hayo.

Ukiona dalili hizi Jua Account yako ya Facebook  imedukuliwa na si salama GUSA HAPA>>>>


3. Kumfananisha tabia mbaya mwezi wako na wazazi wake.

“Tabia zako kama mama yako”, au “..kama baba yako” maneno yanayomfananisha mwenza wako na wazazi au familia anakotoka yanachokoza sana na huweka vidonga kwa muda mrefu moyoni na yaepukwe.


4. Acha! nitafanya mwenyewe

Katika mahusiano kusaidiana ni jambo la kawaida na muhimu, maneno mabaya ya namna hii yanamvunja moyo mweza wako kutaka kufanya jambo kwako siku nyingine na linaleta utengano na kuvunjika kwa upendo.


5. Maneno mabaya ya kukatisha tamaa

“Hutaweza” ,”Hutafanikiwa” n.k yanavunja moyo kwa mwenza wako na kurudisha nyuma maendeleo. Ni muhimu kwa wenza kupeana moyo na kusaidiana ili wote muende mbele kwa pamoja. Umoja ni nguvu.
Hivyo nikusihi ya kwamba kama kweli unataka kudumu katika mahusiano acha mara moja kumwambia maneno hayo, bali unatakiwa kumfariji kwa maneno mazuri yenye kuleta upendo wa kweli na kujenga hamasa ya kudumu

Magroup ya WhatsApp ya kujiunga bure GUSA HAPA>>>

Mazoezi ya mwili ambayo husaidia katika Mapenzi

Mazoezi ni kitu muhimu sana katika maisha ya mwanadamu kwa sababu huuweka mwili vizuri na huuepusha na baadhi ya magonjwa pia. Mazoezi pia yamethibitika kusaidia katika kuuweka mwili mwili vizuri katika upande wa tendo la kujamiiana/kufanya mapenzi kwa jinsia zote mbili. Lakini unatakiwa kujua kuwa si mazoezi yote huwa na faida katika upende wa kufanya mapenzi bali ni mazoezi ya Kigel ndio huwa na faida katika upande huu.


Kigel ni aina ya mazoezi rasmi yalioandaliwa kwaajili ya kuimarisha misuli ya nyonga na viungo vilivyopo chini kwa mwanaume na mwanamke. Mazoezi haya husaidia viungo vilivyopo chini ya nyonga kuboresha mawalisiliano, kuboresha udhibiti wa kibofu cha mkojo na pia huimarisha uwezo wa kufanya tendo/mapenzi

Ukiona dalili hizi Jua Account yako ya Facebook  imedukuliwa na si salama GUSA HAPA>>>>

Jinsi ya kufanya mazoezi ya kigel
Kitu kizuri kuhusu mazoezi haya ni hayahitaji gharama zaidi ya muda wako maana unaweza yafanya hata ukiwa nyumbani. Mazoezi haya hufanywa na wanaume au wanawake. Tafuta sehemu yenye hewa safi na nafasi ya kutosha pia iweinaruhusu wewe kulala chini (chini pawe pasafi au weka kitambaa), inaweza kuwa ni chumbani, sebleni na ikiwezekena nenda katika vyumba maalumu vya kufanyia mazoezi. Baada ya hapo unaweza fanya mazoezi yafuatayo;

Zoezi la kwanza;

Lala chali katika sakafu ilionyooka, kunja magoti kisha pandisha kiuno juu kabisa kama picha iliopo juu inavyoonesha. Baada ya kufanya hayo anza kupandisha kiuno hicho na kukishusha. Endelea kufanya hivyo kwa muda usiopungua dakika tano.

Zoezi la pili;



Jilaze katika sakafu ukiwa umenyooka na umeangalia chini, kisha unyanyue mwili wako kwa kutumia miguu yako na mikono yako kama jinsi picha inavyoonesha. Kaa kwa kuganda kama ulivyo na hakikisha wiliwako unanyooka kama rula kutoka miguuni hadi kichwani. Endelea kukaa kwa muda usiopungua dakika tano.

Zoezi la tatu;

Lala chali ukiwa umeinyoosha miguu alafu nyanyua mikono na miguu juu kisha kunja magoti miguu ikiwa bado ipo hewani. Anza kuushusha mguu wa upande mmoja wakati huohuo hukishusha mkono wa upende tofauti na uliopo mguu kisha rudisha tena mguu na mkono juu. Rudia kitendo hicho kwa mguu na mkono mwingine. Endelea kurudia rudia tena tendo hilo kama picha inavyooneshwa katika picha inavyooneshwa hapo juu kwa muda usiopungua dakika tano.

Maneno ambayo hutakiwi kuyasema kwa mwenza wako GUSA HAPA>>>

Hayo ni baadhi tu ya mazoezi ya kigel ambayo unaweza fanya kila siku ili kuuweka mwili wako uwe vizuri katika tendo la kujamiiana. Sasa tuangalie baadhi ya faida ambazo mtu anaefanya mazoezi haya huzipata.


Faida kwa mwanaume

  • Huongeza uwezo wa kujizui kumaliza tendo kwa haraka
  • Huimarisha misuli katika sehemu zake
  • Huongeza uwezo wa kubana mkojo

Faida kwa mwanamke

  • Huimarisha misuri ya nyonga na kuifanya iwe fanisi
  • Huongeza hamu ya kufanya mapenzi
  • Hufanya mzunguko wa damu ufanyike vizuri katika sehemu zake.

Natumaini mpaka hapa umejifunza kitu na nakusihi endelea kuwa na The Bestgalaxy hakikisha upo na sisi kila wakati ili uendele kupata vitu vizuri.

Ujumbe mzuri kwa mpenzi wako katika kipindi cha Krismasi

Kipindi cha mwisho wa mwaka ni kipindi kizuri sana cha wapenzi kutumia muda wao pamoja. Sasa kama unampenzi basi katika ukaribu wenu wa kipindi hiki unaweza kumtumia mpenzi wako ujumbe mzuri utakao mfurahisha na kujiona wa peke katika maisha yake. Hapa tume kuandalia jumbe nzuri unazoweza mtumia mpenzi wako katika kipindi cha Krismasi. jumbe hizo ni zifuatazo;


~~~~Tulikutana, tukapambana ili tubaki pamoja, tukashinda na tulikua na nguvu katika changamoto zote tulizokabiliana nazo mpaka kufika hapa. Nafikili penzi letu litazidi kuwa imara zaidi. Nimependa kutumia Christmas hii kukukumbusha kuwa, nakupenda sana mpenzi wangu.~~~~

~~~~~~Penzi lako ni zawadi bora ambayo ninaweza kuifurahia zaidi! Krismasi njema, mpenzi!~~~~

~~~~Siku zinakwenda, masaa yana kwenda mimi bado nipo na wewe. Unaona naishi kwa furaha, naona kuishi ni raha lakini tambua sababubu kubwa ni wewe. Tafadhari usije sahau kuwa nakupenda na moyo wangu umetekwa na wewe.~~~~~~

~~~~~Krismasi inakuja mara moja kwa mwaka, lakini tafadhali jua kwamba ninakuenzi kila siku, bila kujali umbali kati yetu. Christmas njema mapenzi wangu.~~~~~

~~~~Nakutakia Christmas njema mme/mke wangu… Nakupenda Sana na ningependa popote ulipo utambue una nusu ya moyo wangu na nusu niliobakinayo yote inakupenda wewe.~~~~

~~~~Penzi letu ni changa bado lakini upendo wangu kwako upo zaidi ya unavyoweza kufikilika, nakupenda Sana na nafurahi kila nikikuona mbele ya macho yangu hakika umeteka hisia zangu. Nakutakia furaha msimu huu wa sikukuu na nitafurahi zaidi tukitumia wote siku ya Christmas.~~~

~~~~~Wewe ni ua zuuri lililoota katika bustani ya moyo wangu, tena ni ua pekee la thamani, linalonipa furaha katika maisha yangu. Nakupenda Sana na najivunia kuwa na wewe malaika wangu. Kuwa na furaha tele katika msimu huu wa sikukuu, kipenzi changu!~~~~~~

~~~~~Hakuna raha kama kupendwa na wewe na sijawahiona karaha kuwa na we. Kama moyo wangu ungekuwa wazi, ungejiona ukiwa peke yako na ukobusy kunipa furaha. Nakupenda Sana na nakutakia furaha katika msimu huu!~~~~~

~~~~Katika Christmas hii nitapenda niwe na furaha, na nikae na mtu ninaempenda na anipae furaha. Vyote hivyo vitakamilika endapo tutatumia siku hiyo pamoja maana utanipa furaha na vile vile nitakuwa na wewe nikupendae na unapae furaha. Mpenzi, tutakua wote si ndio?~~~~

~~~~~Wanasema furaha haiwezi kupimwa kwa maneno halisi, Ni kweli. Tambua kuwa Krismasi hii inatukumbusha kwamba upendo, furaha, na nia njema ndio vitu halisi vinavyoinua maisha yetu. Asante kwa furaha unayoniletea tangu nilipokutana na wewe, mpenzi wangu.~~~~~

Jinsi ya kupata mkopo kwa njia ya simu tanzania (Watu Million 10+ wanaitumia njia hii halali ya kukopa)

Unaambiwa, zaidi ya watu milioni 100 duniani wanatumia simu zao kupata mkopo kwa haraka. Na Kwa hapa Tanzania kuna watu wengi sana ambao tayari wanatumia simu zao kupata mikopo inayowazaidia kuwasukuma katika mambo mbali mbali kimaisha.
Kutumia simu kupata mkopo ni moja ya matumizi chanya ya simu hizi za Smartphone. Ni matumizi chanya kwasababu mkopo ambao watu hupata kupita simu zao, unawasaidia katika maisha halisi. Maana wanaweza kupata mkopo ili kurekebisha mambo yanapoenda vibaya katika biashara and maisha Kwa ujumla.


Kwa mfano; Kuna dada flani mzuri sana sitomtaja jina. alikua anasafiri alipanda gari alafu alipokua ndani ya gari na wakati gari limeanza safari akagundua sehemu alioweka pesa zake ikiwemo nauli ipowazi na hakuna pesa… Basi moja Kwa moja akajua ameibiwa pesa na hana pesa yoyote. Dada yele alikua mpole kama amemwagiwa maji ya baridi kwenye gari hilo huku akiwaza ni jinsi gani konda atamuelewa, ukizingatia maneno ya makonda wengi huwa ni mabaya kwenye maswala ya hela.
Lakini Kwa bahati nzuri alikumbuka kuwa kwenye simu yake huwa anatumia huduma flani inayo mruhusu kukopa hadi 100,000 ndani ya dakika 5 tano tu. Alikua hadaiwi kwenye hiyo huduma na alikua ni Moja ya watu wanalipa mikopo Kwa wakati ndio maana alipewa uwezo wa kukopa kiasi kikubwa kidogo.


Basi bila kupoteza muda yule dada akatumia huduma hiyo kukopa kiasi cha pesa Cha kutosha nauli na mambo mengine. Pesa aliokopa ilitumwa kwenye laini yake ya simu (Tsh 70,000). Alipoingia tu kwenye simu akapatanguvu, akamuita konda na kumwambia “Samahani kaka, nimedondosha pesa ya nauli lakini ninapesa kwenye simu naomba uniruhusu nikutumie nauli kwenye simu yako au nikifika stendi tukatoe Kwa wakala…”. Konda akampa pole yele dada kisha akamwambia atume tu kwenye simu ila utume na yakutotea. Basi yele dada alipona kiivyo.

Sasa huo ni kama mfano mzuri unaoonesha umuhimu wa watu kujua na kua na huduma za kukopa kwenye simu. Ikiwa wewe ni moja wa watu wanaohitaji kuwa na huduma za kukopa kwenye simu basi hapa tunakujuza juu ya njia moja ya haraka na halali ya kupata mkopo kwenye simu Tanzania. Soma maelezo yafuatayo hadi mwisho ili kuelewa zaidi njia hii.

Jinsi ya kupata mkopo kwa njia ya simu tanzania.

Kama unahitaji kupata huduma ya mkopo kwa njia ya simu, basi tumia app iitwayo Branch. App ya branch ni moja ya app halali ambayo ukiwanayo kwenye simu yako inakupa uwezo wa kukopa Tsh 5,000 na kuandelea ndani ya dakika chache tu. Tena mkopo unatumwa kwenye laini yako hapo hapo na utakuja kulipa kwa gharama nafuu.
App ya Branch unaweza kuipata na kuiingiza kwenye simu yako kirahisi kwa kugusa HAPA. Lakini kabla haujaiingiza kwenye simu yako ningepeda ufahamu mambo ya fuatayo;

Ukishaiingiza app hii kwenye simu yako, jisajili na ujaze taalifa zako za ukweli kabisa alafu ndio uombe mkopo. Na kwa mara ya kwanza unavyokopa, kopa kiasi kidogo tu (Tsh 5000) na urudishe kwa wakati. Kurudisha kwa wakati kutafanya wakuamini na upadate uwezo wa kukopa kiasi kikubwa kirahisi mbeleni. Unapokopa Kwa mara ya kwanza wanaweza wakachelewa kidogo kukupa. Ila mkopo utakao omba baadaya kurudisha mkopo wa kwanza unaweza upata hata ndani ya dakika moja. Maana wanakua wanajua wewe ni mwaminifu.

Zawadi ya Tsh 5750 BURE Utayopewa na Branch (USISAHAU HII)

App ya Branch pia huwa wanatoa Zawadi ya Tsh ,5750 BURE unaporudisha mkopo wa kwanza. Lakini ni lazima uwe umeandika namba za mualiko. Hii ni kwaajili ya uaminifu wako maana wanaotangulia kukupa pesa ni mwenye.


Kama unahitaji kupata zawadi hiyo basi ingize app kwenye simu yako Kisha jisajili. Ukijisajili Gusa sehemu ilioandikwa “Alika” alafu chagua “Ingiza Nambari ya promosheni” kama unavyoona hapa chini.

Baada ya hapo, unaletewa kibox, jaza nano hili “””elia04c93“”” katika kibox kama inavyo onekana katika picha ya hapa chini. Usisahau kunandika namba hiyo ya mualiko ili upate zawadi.

Ukishajaza tu na kugusa kitufe cha blue, siku yoyoye utakayoomba mkopo alfu ukarejesha, utapata Tsh 5750 BURE.

Kama utakua na tatizo, njoo uulize maswali WhatsApp kwa kugusa HAPA>>>

App hii itakusaidia kuomba mkopo kwa Simu Tanzania. Na ukiwa mwaminifu basi unaweza kuitumia kupata mikopo ya haraka kupitia simu yako Kila unapohitaji. Utakuaunaomba mkopo online kirahisi sana.

Fanya haya kabla simu yako haijaibiwa ili kuipata ikiibiwa GUSA HAPA>>>

Jinsi ya kuingia katika Akili ya mwanamke umpendae

Je uko tayari kufahamu jinsi ya kuingia katika akili ya mwanamke na kufanya mapinduzi ya njia ya kawaida unayotumia kuapproach mwanamke? Kama jawabu lako ni ndio, basi zama nami kusoma hizi mbinu ambazo zimethibitishwa kufanya kazi.

1. Anza approach ya mbali

Kabla ya kumuapproach mwanamke, hakikisha ya kuwa unamsoma kwa umbali mambo anayofanya kwanza. Halafu ukiona kama umepata kile unachoweza kutumia kutoka kwake unaweza kumuaproach. Ukiwa unaongea nayeye mwambie kuwa una uwezo wa kusoma nyota yake. Wanawake wengi watakubaliana na hili ili kuona ucheshi wako. Halafu ukirudilia na vitu ambavyo ulimsoma awali, utakuwa umemfunga. Mwanzo kama umejaribu kumtabiria vitu ambavyo viko sawa kwake ama vinahusiana na yeye, una nafasi kuu ya kumfanya kukutaka kukufahamu zaidi. Pia ni vizuri kufahamu miondoko ya wanawake na mapema ili kuelewa kama anakubaliana na utabiri wako kwake. [soma; Jinsi ya kuapproach demu usiyemjua]

Gusa hapa>> USOME JAMBO ZURI ZAIDI KWAAJILI YAKO

Pia unaweza kuwambia unaweza kusoma nyota yake kupitia kwa maganja yake. Hii itakupa nafasi ya rahisi kuweza kupata kumgusa bila kukushuku ajenda yako nzima iliyo akilini mwako. Mbinu hii itamfanya yeye kuvutiwa na wewe kwa urahisi.

2. Leta shangwe

Wanawake wanapenda wanaume ambao hawayachukulii maisha serious vile, so hakikisha kuwa unajua jinsi ya kuchat na wanawake. Unaweza kutumia mbinu ya kutumia kuwa mcheshi na kutoa mizaha ukiwa kando yake. Kufanya hivi kutamfanya yeye kucheka na kutabasamu, jambo ambalo automatic litamfanya yeye kuvutiwa na wewe. Usitumie mbinu ya kumtesa sana na mizaha yako ama utaonekana kuwa na utoto mwingi ama anaweza kukasirishwa. Uzuri wa kutumia ucheshi ni kuwa kunamfanya mwanamke kujihisi bado ana ujana. [soma: Dalili za kuonyesha kama mwanamke anakutaka kimapenzi]

3. Ichokore akili yake

Hii ni mbinu ya sanaa ya kutongoza ambayo itamfanya mwanamke yeyote kuathirika kihisia na wewe. Itamfanya akutamani na kuifanya akili kukufikiria wewe tu.

Njia moja kama hii ni kumfanya mwanamke kuingiwa na furaha dakika moja na kukasirika dakika ya pili. Wanawake inaonekana mara nyingi hupenda vioja katika maisha yao, kama vile katika vipindi vya tamthilia ama soap opera. Hoja ya vioja ni nzuri pia kwa kuwa inatoa ile dhana ya kubandikwa jina kuwa unaboa.

Gusa hapa>> USOME JAMBO ZURI ZAIDI KWAAJILI YAKO

Kama unaweza kuyafanya maisha yako kuwa na vioja vya mara kwa mara wanawake watakupenda automatically bila wao kujifahamu. Ukishafanikiwa kuteka hisia zao, inakuwa rahisi kwako kuingia katika akili yao. Unafaa kuonywa ya kuwa kutumia mbinu hii sana inaweza kuwafanya baadhi ya wanawake kuchunguza maisha yako wakitaka kuwa karibu yako kila wakati.

Pia fahamu ya kuwa usimchangaye akili kihisia mwanamke yeyote kwa kutumia mbinu hii kwani mwishowe inaweza kukujeukia.

Hebu jifunze kummiss mpenzi wako ili kuongeza upendo

Ni lazima uipe pumzi penzi lenu kama mnafanya kazi ambayo inawafanya wewe na mke wako kuwa pamoja kila wakati, basi kila mmoja anahitaji muda wa peke yake awe na muda wa kummiss mwenzake.

Gusa hapa>> USOME JAMBO ZURI ZAIDI KWAAJILI YAKO

Huwezi kummiss mtu ambaye kila dakika unamuona, sana sana utaishia kuona mapungufu yake na kugombana tu. Utammiss vipi wakati kila wakati uko naye, kila mmoja anahitaji kummiss mwenza wake ili mapenzi yawe na raha.

Mume/mke wako anahitaji maisha mbali na wewe, anahitaji angalau nusu saa kwa siku ambayo hataona sura yako, atakuwa na watu wengine, atakuwa na marafiki au atakuwa anafanya kitu kingine bila wewe.

Kama uko kwenye ndoa au mahusiano ambayo kila kitu mnafanya pamoja, kila wakati mko pamoja, kila muda wa ziada mko pamoja basi suala la kugombana kwenu ni la muda tu.

Jifunze kuwa na furaha nje ya mwenza wako, si kuchepuka hapana, hata kucheza tu karata na majirani inatosha kukufanya ummiss mwenza wako.

Kama kila wakati mko pamoja, hata kama hamfanyi kazi pamoja lakini kama ule muda wa zaida kila siku mpo pamoja basi mtaanza kuboana, utaanza kuona mapungufu ya mwenza wako, utaanza kuona ubaya wake na mtagombana tu.

Gusa hapa>> USOME JAMBO ZURI ZAIDI KWAAJILI YAKO

Yes kuna watu wanalalamika kuwa waume zao wanawaganda hawatoki nyumbani, kuna wanaume hulalamika wake zao wanawaganda.

Kama mnagandana kama mapacha halisi jua tu mtaboana.

Mahusiano ya mapenzi huitaji vitu hivi

1. Ujasiri
Upendo unahitaji uwe jasiri katika hali zote ujasiri katika kunena ,ujasiri kutenda, ujasiri katika kuuzungumzia upendo kwa mwenzi wako upendo unamhitaji mtu jasiri sio kitu rahisi kama wengine wanavyozungumzia.

2. Uvumilivu
Upendo unahitaji uvumilivu kuvumiliana. Hakuna mwanadamu aliyekamilika katika mambo yote, unajua Waswahili wanasema “mvumilivu hula mbivu “ mvumilivu katika upendo maana yake hii ni shule ya kila siku, tunajifunza kutokana na makosa. Uvumilivu unatakiwa sana katika upendo – unajua kumfanya mwenzi wako kuwa kama wewe unavyotaka awe inahitaji uvumilivu. Hilo ni kweli, maana mmetoka mazingira tofauti na malezi tofauti; hivyo kumbadilisha inahitaji uvumilivu.

3. Kiasi
Kiasi ni kitu muhimu. Chochote kinachofinywa zaidi ni hatari, unatakiwa uwe na kiasi katika mambo yako ili uweze kudumu katika upendo maana upendo unahitaji kiasi. Usijifanye uko (busy) sana unakosa hata nafasi/muda wa kukaa na mwenzi wako, lakini wewe unarudi usiku, huo sio upendo. Nakuombea uwe na kiasi ili uenzi katika maisha yako.

4. Kutiwa moyo
Upendo unahitaji kutiwa moyo. Mtie moyo mwenzi wako ukimwambia pole asali wangu wa moyo, Unafanya vizuri sana, umefanya vizuri sana, unapoweza kumtia moyo mwenzi wako kwa yale anayofanya yanamuhamasisha kutenda zaidi na kukupenda zaidi. Kutiwa moyo ni kufarijiwa, moyo unahitaji kutiwa moyo, kuthaminiwa. Hivyo katika upendo unahitaji kumtia moyo mwenzi wako ili upendo huo udumu maishani mwako. Ikiwa hauna tabia ya kumtia moyo mwenzi wako ipo siku utampoteza, akipata watu wanaothamini mambo anayoyafanya na kumfariji. Atulie badilika uuteke upendo kwa kufuata masharti yake.

Gusa hapa>> USOME JAMBO ZURI ZAIDI KWAAJILI YAKO

5. Kutambuliwa
Upendo unahitaji kutambuliwa katika maisha yako na kujua umuhimu wake. Kutambuliwa ni kitu muhimu sana katika maisha, kumtambua mpenzi wako na umuhimu wake kwako. Atambulike toka moyoni mwako kuwa anafaa kuwa mumeo au mke wako, hivyo upendo unahitaji sana utambuliwe na wewe mwenyewe. Umfahamu na umuelewe kiundani.

6. Uaminifu
Upendo unahitaji uaminifu kwa mwenzio sio msaliti wenye kujitunza na kujiheshimu mtu asiye na hila ndani yake uaminifu ni dawa ya upendo katika maisha yetu tukikosa uaminifu sisi kwa sisi upendo hautaweza kukaa pamoja nasi.

Gusa Hapa>> USOME JAMBO ZURI ZAIDI KWAAJILI YAKO

7. Usawa
Upendo unahitaji usawa unajua mapenzi ni kusaidiana hakuna kiongozi wa mapenzi bali tunasaidiana hivyo huo ndio usawa katika mapenzi upendo unahitaji usawa huo wewe unawajibu kwa mwenzi wako na mwenzi wako anawajibu kwako.

8. Urafiki
Upendo unahitaji urafiki upendo hujenga urafiki mwenzi wako ni rafiki yako kuliko marafiki ulionao katika maisha yako- Mapenzi wako sio adui yako mficha siri wako usimuogope maana upendo hauna hofu unatakiwa kuzungumza na rafiki yako kirafiki ili upendo uwezo kudumu na kushamili.

9. Kukubalika
Upendo unahitaji kukubalika, kupokelewa toka moyoni mkubali mwenzi wako apate kibali moyoni na maishani mwako ukimkubali hautamuumiza hivyo upendo unataka kukubalika hapo utafurahia maisha yako.

10. Ukweli
Upendo unahitaji ukweli,upendo ni adui wa uongo unatakiwa uwe mkweli katika mapenzi yenu,ukweli hujenga upendo, ukweli huimarisha mahusiano,upendo unahitaji mtu ambaye ni mkweli kwa mwenzi wake,ukweli ndio upendo wenyewe unatakiwa uwe mkweli ili upendo uchukue nafasi moyoni mwako.

11. Imani
Upendo unahitaji imani na imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo ,ni bayana ya mambo yasio onekana. Unatakiwa kuwa na imani na mwenzi wako, imani katika mahusiano ni muhimu sana kuaminiana ,toa wasiwasi kwa mwenzi wako, mwamini kuwa amekuchagua wewe na hakuna mwinginen wewe uko peke yako.

Gusa hapa>> USOME JAMBO ZURI ZAIDI KWAAJILI YAKO

12. Penzi
Upendo unahitaji penzi la kweli linalotoka moyoni ,penzi kwa mpenzi wako ni muhimu sana kama litatumika kwa utaratibu na kwa uaminifu kabisa maana penzi linahitaji muda hivyo hivyo unatakiwa uwe na muda wa kutosha ili uweze kupata pendo la kweli.

Jinsi ya kumsifia mwanamke mrembo unempenda kwa dhati

maana msingi ya neno ‘wewe ni mrembo’ imepotea. Hii ni kwa sababu baadhi ya wanaume wasiojua kutongoza wanaishia kulitumia neno hili vibaya kiasi cha kuwa neno hili limepoteza uhalisia.

Je ulikuwa wajua kuwa wanawake hupenda kusifiwa? Na ulikuwa ukijua kuwa kumsifia mwanamke mara kwa mara ni njia moja wapo ya kutongoza?  leo tumekuja na mambo tofauti ambayo unapaswa kutumia ili umshawishi mwanamke kuwa ni mrembo, na wala hataona kama ni maneno unalompakizia ama maneno ambayo ameyazoea kuyaskiliza awali.

Twende pamoja:
Jambo la kwanza 
Wakati unapotaka kumsifia mwanamke kuwa ni mrembo, usimwambia, “Wewe ni mrembo” mara kwa mara kwa sababu itafikia mahali flani neno hilo litaisha ladha. Badala yake tafuta sehemu muhimu kutoka kwa mwili wake ambayo utaitumia kama kigezo cha kumsifia. Kwa mfano kama umependezwa na pua yake mwambia, “Nimependezwa na pua yako, kila mara nikiiona najiskia na furaha.” Ama kama umependezwa na mashavu yake unaweza kumwambia, “Mashavu yako ndio nuru ya macho yangu, yanapendeza.” Kumwambia mwanamke maneno kama haya yatamfanya atamani kuwa kando yako. Pia ataona kuwa unamwona anapendeza, unamakinika kuuona urembo wake kupitia kwa viungo vyake vya mwili.

Jambo la pili 
Kumsifia mwanamke urembo wake hakuhusishi ngozi yake ya nje pekee, bali pia sehemu yake ya ndani, yaani nafsi yake. Wanaume wengi huwa wanamakinika kumsifia mwanamke umbo, sura na shepu yake huku wakisahau kuwa nafsi ya mwanamke ina umuhimu. Kumsifia mwanamke kwa ujasiri wake, ubunifu wake, hekma, na ujanja kutakupa mkono wa mbele zaidi wakati unapomtongoza ama unapomshawishi. Jambo hili tulishawahi kulizungumzia katika moja ya hatua ya kumtongoza mwanamke ambaye hayuko ligi sawa na wewe. Kumshawishi na kumsifia mwanamke nafsi yake kutamfanya ajiunganishe na wewe zaidi kuliko mwanamke yeyote yule, hivyo hatua iko kwako sasa.

Jambo la tatu
Wakati ambapo umeamua kumsifia mwanamke kama huyu, hakikisha kuwa unamwangalia machoni. Kama ni mwanamke ambaye ndio unaanza kumfukuzia basi jenga confidence ya kumwangalia machoni. Usimsifie huku ukiangalia pembeni ama kuangalia kando. Kumbuka wewe ni Mwanaume Alpha, na wanaume alpha huwa hawatatiziki kama wanatoa hisia zao kuhusu wanawake wanaowapenda.

Gusa hapa>> USOME JAMBO ZURI ZAIDI KWAAJILI YAKO

Jambo la nne
Unapomsifia mwanamke usitumie maneno hayo kwa hayo. Yaani wewe kila siku ukikutana na yeye unamwambia, “Nakupenda, leo umeangaza nafsi yangu.” Matumizi ya neno moja siku nenda siku rudi kutamfanya mwanamke atilie shaka iwapo unasema maneno hayo ndani ya moyo wako ama unasema kumridhisha tu. Well, mbona usije na misamiati mipya? Ama mbona usije na maneno ambayo angetamani kuyaskia? Ukitumia maneno kama ‘hurulaini’, ‘malkia, leo nimekuja kwa milki yako’, ‘ua langu la waridi’ nk kutamfanya mwanamke akupende zaidi na zaidi. So anza kutafuta maneno ambayo anayapenda. Usiingiwe na uvivu wa kutumia maneno hayo kwa hayo kila siku. Kumbuka hapa unataka kuwa bora zaidi kati ya wanaume wale wengine. Chukua hatua sasa.