All posts by Admin

Jinsi ya kuongeza speed ya internet kwenye simu

Unasumbuliwa na speed ndogo ya internet? Usiwe na wasi tena! Hapa The Bestgalaxy tunakufungua juu ya nini unachoweza kukifanya kufurahia internet nyenye kasi kwenye simu yako ya smartphone.


Moja ya vitu ambavyo huudhi katika katika matumizi ya internet ni speed/ kasi ndogo. Speed ndogo ya internet sio tu huudhi bali pia hupoteza muda wa mtu anaetumia internet kwasababu kitu ambacho alitaka kukifanya kwa dakika 1 kwenye internet kinaweza mchukua mpaka dakika 5 ikiwa speed ya internet itakua ni ndogo. Watu wengi wanao thamini muda huchukizwa na swala hili.


Lakini tukirudi kufikilia kahusu historia ya internet utagundua internet imebadilika Sana na huwezi fanananisha na kipindi cha nyuma. Hata internet ya sasa isumbue vipi kwenye speed lakini huwezi ilinganisha na zamani maana huko nyuma internet ilikua haina kasi kabisa kama ya sasa. Kudownload nyimbo Moja tu yenye Mb 5 ilikua inaweza kukuchukua mpaka saa 1. Kama ni mtumiaji wa muda mrefu wa internet unaweza kuwa unajua kuhusu hili.

Yafuatayo ni mambo ambavyo Unaweza fanya kuongeza speed ya internet kwenye simu yako (hayahusishi matumizi ya WiFi)

WhatsApp yako inatatizo? Jifunze jinsi ya kutatua hapa>>>>

Namna ya kuongeza speed ya internet kwenye simu

1. Hakikisha unatumia laini ya 4G au 5G na Simu 4G au 5G

Kwasasa ukitaka kufurahia kasi nzuri ya internet basi inatakiwa iwe ni kuanzia kasi ya 4G. Ukitaka kufurahia kasi hii ya internet kwenye simu yako ya smartphone inatakiwa iwe na laini ya 4G na pia simu yako iwe ni ya 4G au 5G. Mbali na havyo pia ni vema “preferred network type” yako ikaiseti kwenye “Auto“. Kuiset preferred network type kwenye simu yako nenda kwenye “settings” ingia kwenye na uende katika “Network & internet” alafu ingia kwenye “SIM cards” kisha ingia kwenye “Mobile network“. Baada ya hapo gusa “Preferred network type” na uchague “Auto“.

2. Hamia kwenye mtandao wa simu wenye huduma ya internet yenye kasi.

Kuna muda mtu anaweza kuwa unakumbana na changamoto ya kasi ndogo ya internet katika matumizi ya internet kutokana na mtandao wa simu unaokupa huduma ya internet kutokua vizuri katika maeneo uliopo. Jaribu kufanya utafiti kwa watu uwalio kuzunguka ili kujua mtandao wanotumia kupata internet na speed yake ya internet iko vipi. Unaweza tu kuwaambia watu “Mimi ninatumia mtandao flani kupata huduma ya internet lakini naona Kama haupo vizuri Sana katika speed kwenye maeneo haya… Ivi ni mtandao gani nyinyi mnautumia na upo vizuri?”

Fanya haya kabla simu yako haijaibiwa ili kuipata ikiibiwa GUSA HAPA>>>


Kama kutakua na mtandao wanao sema upo vizuri basi jaribu na uangalie kama utakua vizuri kwako pia. Unaweza pia wasiana na watu wanao husika na mtandao wako wa simu na kuwataalifu kuhusu Jambo unalopitia kwenye eneo lako ili warekebishe. Tena bahati nzuri ni kwamba sikuizi makampuni ya mitandao ya simu ina kurasa zake katika mitandao ya kijamii na Unaweza watumia ujumbe kule na wakakujibu.

3. Boost speed ya internet kwa kuwasha “Flight mode” na kuizima.

Kama speed yako ya internet inasubua subua wakati unaitumia unaweza kuwa unaiboost kwa kuwasha “Flight mode” na kuizima. Flight mode huwakilishwa na kialama Cha “ndege ya usafiri” na hupatikana katika kisehemu Cha simu unachokifuata pindi unapo washa Data kwaajili ya kuanzia kutumia internet.

4. Tumia app zinaweza ongeza Speed ya internet.

Kuna baadhi ya app za VPN zinaweza ongeza speed ya internet. Hii inaweza onekana zaidi unapo download vitu au ku-stream vitu online ukiwa unatumia VPN. Lakini app za VPN zipo maalum kwaajili ya kuufanya muunganiko wako wa internet uwe salama na si kuongeza speed. Na pia sio kila unapotumia VPN utapata internet yenye kasi, VPN zinaweza pia kupunguza kasi kabisaa.

Mbali na app za VPN pia Kuna app zinazohusisha zaidi DNS zinaweza kuongeza kikasi Cha internet unapotumia. Mfano mzuri ni app iitwayo WARP… Unaweza ijaribu kwuingiza kwenye simu yako ya Android kwa lugusa hapa au iPhone kwa kugusa hapa

SMS za mchana mwema kwa mpenzi wako

Ukiwa kwenye mahusiano Unaweza kufanyia vitu vingi kwema kwa mweza wako ili kuonesha unamjali. Kutumia ujumbe wa mapenzi mpenzi wako ni Moja ya Jambo linaloonesha kujali pia… Mukiwa ni wapenzi mulio mbali hii inaweza kuwa ni kitu muhimu kinachojenga mahusiano kuliko hata kutuma tuma pesa.

Zifuatazo ni SMS au meseji za kumtakia mchana mwema mpenzi wako. Kama unahitaji Unaweza chagua zinazoendana na mahusiano yako kwa sasa kisha ukazitumia kwa umpendae. Endelea kuwa karibu na The Bestgalaxy kwa mambo mengine mazuri zaidi.

SMS za mchana mwema kwa mpenzi wako

Upendo wangu kwako huongezeka kila wakati ninapokutazama. Hautafifia wala kuisha kwa sababu hauna mwisho. Kila mara kumbuka kuwa Nakupenda sana na kwa muda huu nakutakia mchana mwema kipenzi changu.



Mpenzi, muda huu nakukumbusha tu kuwa wewe ndio chaguo langu. Yaani naomba ujue kuwa wewe ni Mfalme wa kasri langu na kwamba moyo uliokaa kifuani mwangu utalidunda jina lako. Ninakupenda zaidi ya ninavyoweza kusema nakupenda. Mchana mwema mpenzi wangu.






Nakutakia mume/mke mtamu zaidi ulimwenguni siku njema. Hakuna mtu katika ulimwengu mzima anaweza kuwa mpenzi wa maisha yangu kwa sababu nafasi hiyo tayari imechukuliwa na wewe, mume/mke wangu mpendwa. Nakupenda Saana na napenda kukupenda.



Asante kwa kupenda kila kitu changu, pamoja na kutokamilika kwangu. Mungu alinipa zawadi isiyo na kifani maishani mwangu pale alipokuumba wewe mpenzi wangu. Nakupenda sana kuliko ujuavyo.




Tambua kuwa wewe ni mtu pekee katika ulimwengu wote ambaye hufanya maisha yangu kuwa kamili kabisa na maridadi. Mpendwa, asante kwa kuleta joto na mwangaza katika maisha yangu. Sijawahi jutia kukupenda.





Nina nafasi moyoni mwangu ambayo hakuna mtu anayeweza kuchukua kwa sababu hakuna mtu mwingine anayeweza kunifanya nifurahi kama unavyonifanya. Nakutakia mchana mwema.




Wewe ni damu ambayo hupitia mishipa yangu. Wewe ndiye kipande muhimu ambacho hufanya roho yangu ikamilike. Siwezi kamwe kuishi katika ulimwengu huu bila wewe, mpenzi wangu wa thamani. Kuwa na siku mchana mwema huko uliko!


SMS za kumtakia mpenzi wako usiku mwema GUSA HAPA>>>




Kuangalia machoni pako kunanipeleka kwenye ulimwengu wenye zaidi ya maelfu ya furaha. Penzi lako hufanya nijihisi Niko paradiso. Umeniweza sasa, naomba kokote uendako usisahau kuwa nakupenda mpenzi wangu. Mchana mwema kwako.

Kila nikiona simu au SMS toka kwako moyo wangu hudunda kwa furaha… Kiufupi nakupenda na natamani kuelezea upendo wangu zaidi ya kukuambia “nakupenda” ili tu utambue na usije kuniumiza. Tambua hilo kipenzi changu… Nakutakia mchana mwema.

Ukiona dalili hizi Jua Account yako ya Facebook  imedukuliwa na si salama GUSA HAPA>>>>

Magroup ya WhatsApp ya kujiunga BURE

Hapa tutaangalia vikundi vya WhatsApp ambavyo unaweza kujiunga. Sote tunajua kuwa vikundi vya WhatsApp ni muhimu sana kwa sababu watu huvitumia kuungana na wengine na kushiriki habari fulani au kujadili mambo mengi. Lakini unahitaji kujua kwamba kila mtumiaji wa WhatsApp anaweza kuunda kikundi cha WhatsApp na kuongeza watumiaji wengine kwenye kikundi. Hii inamaanisha kuwa unaweza pia kuwa na kikundi chako mwenyewe cha WhatsApp na kukifanya kama Msimamizi.

WhatsApp yako inatatizo? Jifunze jinsi ya kutatua hapa>>>>

Jinsi ya kuunda kikundi chako cha WhatsApp?


Ni rahisi sana, unachohitaji kufanya ni kufungua programu yako ya WhatsApp kisha uguse nukta tatu. Baada ya kugonga nukta Tatu, utapata orodha ya chaguo chache. Chagua “New group” ili kuanza kuunda kikundi chako mwenyewe. Kwenye kuliunda utatakiwa kuwachagua watu watu unaotaka wawe kwenye group. Unaweza kuchagua wale watu wote unahitaji wawekwenye group lako lakini tambua kuwa sio mtu anapenda kuungwa kwenye group bila tahalifa. Hivyo ni vema ukawatahalifu watu unaotaka kuwaweka kwenye group juu ya group unalotaka kuwaweka kwanza.

Yafuatayo ni magroup ya WhatsApp ambayo unaweza kujiunga nayo

Hapa nakupa orodha za vikundi vya WhatsApp ambavyo unaweza kujiunga badala ya kuunda kikundi chako cha WhatsApp. Hivi ni vikundi ambavyo unaweza kujiunga na kutumia lugha ya Kiswahili katika kuchati.

Magroup ya Marafiki/Mahusiano

Magroup ya Biashara

Magroup ya Ajira/Kazi

Magroup ya Michezo & Burudani

Unapaswa kujua kuwa, vikundi vyote vilivyoorodheshwa hapa vina watu kutoka sehemu tofauti na hatuna uhusiano wowote nao. Kwa hivyo hakikisha kuwa kila wakati unakuwa mwangalifu na walaghai au wanachama wengine ambao wanaweza kukosa nidhamu.

Njia 3 za kutumia intaneti bila malipo kwenye simu ya Android au iPhone

Katika mabilioni ya watu wanaotumia internet ama mtandao kila mwaka na watu wengi kati yao wanaotumia Simu. Na siku hizi, watumiaji wengi wa simu wanatumia simu za Android na iOS. Mambo mengi ambayo watumiaji wa simu za Android au iOS wanapenda kufanya kwenye simu zao yanahusisha kutumia intaneti.

Wanatumia intaneti kwenye mambo kama vile kushiriki habari, kujifunza, kuendesha biashara zao, kupata burudani na zaidi. Kwa vile sote tunajua kwamba mtandao sio bure, inagharimu watumiaji kiasi cha pesa kununua bando za internet au kulipia huduma za internet. Lakini bado kuna nini cha kufanya ili kutumia wa internet bure kwenye simu.

Ukiona dalili hizi Jua Account yako ya Facebook  imedukuliwa na si salama GUSA HAPA>>>>

Pata BAND0 kubwa la internet Kwa Bei rahisi GUSA HAPA>>>

Ikiwa wewe ni mmoja wa watu wanaotumia simu yoyote ya Android au iPhone na unahitaji kutumia intaneti bila malipo basi hapa chini kuna kinachoweza kufanya ili kupata intaneti bila malipo.

Njia za kupata intaneti ya Bure kwenye simu ya Android na iPhone


  1. Unaweza unganisha simu yako Kwenye huduma za Wifi za bure zinazopatikana kwenye mazingira yako… unaweza tafuta sehemu zilizio na huduma ya WiFi kitahisi kwa kutumia App yako ya Facebook. App ya Facebook inakipengele kinachokuonesha maeneo yenye huduma za WiFi katika eneo ulilopo.
  2. Unaweza pata ofa au zawadi za interneti ambazo hutolewa bure na kampuni inayokupatia huduma ya internet (mfano Tigo: Ukituma neno “BURE” au “Social bonus” kwenda Namba 15166 unaweza zawadiwa Mb za internet BURE..
  3. VPN pia inaweza tumika kupata internet bila malipo… lakini njia hii imewekwa hapa Kwa lengo la elimu tu na si vinginenyo. Unaweza soma moja ya makala zetu zinazohusisha njia hii HAPA>>>>>

Magroup ya WhatsApp ya kujiunga bure GUSA HAPA>>>

Maneno ambayo hautakiwi kusema kwa mwenza wako

Endapo umekwisha ingia katika mahusiano au unatarajia kuingia katika mahusiano ya kimapenzi, yapo mambo yanyofaa ambayo unaweza kumwambia mpenzi wako naye akafurahi, lakini yapo mambo ambayo kimsingi hupaswi kabisa kumwambia mpenzi wako. Kwani endapo utaamua kumwambia utatengeneza njia ambayo itawafanya mahusiono yenu yafe mara moja.
Maneno yafuatayo ni hatari kwa kuwa yanaleta madhara makubwa moyoni mwa mlengwa na ni vyema kuzuia kuyatamka kwa namna yoyote ile.

Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze Kila mara BONYEZA HAPA>>>

Maneno ambayo hutakiwi kuyasema kwa mwenza wako


1. Nakuchukia

Chuki ni kitu kikubwa sana, kwa kweli huwezi kuishi na mtu ambaye unamchukia. Hutakiwi kumtamkia mwenza wako neno hili. Unaweza kuchukia tabia yake lakini si yeye mwenyewe. Njia nzuri ni kusema kuwa “Nachukia au sipendi tabia yako ya kuchelewa kurudi nyumbani” au maneno yanayofanana na hayo.


2. Maneno ya matusi

Maneno kama “mjinga” au “mpumbavu” yasitumike kwa mwenza wako hata kama yana ukweli ndani yake. Japo ujinga ni kutofahamu kitu fulani lakini neno hili linaleta majeraha kama likitoka kwa mwenza. Hasa kama linatoka wakati wa ugomvi au kutofautiana.
Usiseme maneno mabaya yanayomshusha mweza wako mfano kuhusu mwonekano mbaya wa mwenza wako kama “sura mbaya”,”Mnene kama nguruwe” na maneno mengine kama hayo.

Ukiona dalili hizi Jua Account yako ya Facebook  imedukuliwa na si salama GUSA HAPA>>>>


3. Kumfananisha tabia mbaya mwezi wako na wazazi wake.

“Tabia zako kama mama yako”, au “..kama baba yako” maneno yanayomfananisha mwenza wako na wazazi au familia anakotoka yanachokoza sana na huweka vidonga kwa muda mrefu moyoni na yaepukwe.


4. Acha! nitafanya mwenyewe

Katika mahusiano kusaidiana ni jambo la kawaida na muhimu, maneno mabaya ya namna hii yanamvunja moyo mweza wako kutaka kufanya jambo kwako siku nyingine na linaleta utengano na kuvunjika kwa upendo.


5. Maneno mabaya ya kukatisha tamaa

“Hutaweza” ,”Hutafanikiwa” n.k yanavunja moyo kwa mwenza wako na kurudisha nyuma maendeleo. Ni muhimu kwa wenza kupeana moyo na kusaidiana ili wote muende mbele kwa pamoja. Umoja ni nguvu.
Hivyo nikusihi ya kwamba kama kweli unataka kudumu katika mahusiano acha mara moja kumwambia maneno hayo, bali unatakiwa kumfariji kwa maneno mazuri yenye kuleta upendo wa kweli na kujenga hamasa ya kudumu

Magroup ya WhatsApp ya kujiunga bure GUSA HAPA>>>

Battle of Agents: Gemu la kuchezwa na watu wawili au zaidi bila data/internet

Battle Of Agents ni moja kati ya magemu mzuri ya shooting ambayo ni madogo ki-size. Gemu hili hutoa nafasi ya watu zaidi ya mmoja kucheza gemu kwa pamoja kwa kutumia simu tofauti. Halina ukubwa wa kutisha sana kama magemu mengine yenye uwezo huu yaani unaweza lipakua kwa MB chache tu na ukawa unafurahia kulicheza na marafiki bila kutumia data tena. Kwaiyo ni offline multiplayer game.

Muonekano wa gemu hili upo vizuri japo sio bora kama magame mengine Ila uzuri sifa yake nzuri ni kwamba huchezwa hata katika simu zenye uwezo ndogo bila matatizo hivyo kama ulikua na simu yenye uwezo mdogo na ulikua unatamani magame ya kucheza wawili au watatu hili linaweza kuwa gemu ambalo hutakiwi kulikosa.

Upatikanaji: Ninaweza sema hakuna ugumu wowote katika kulitafuta Gemu hili maana hupatikana sehemu ambayo kila mtumiaji wa simu ya Android huifahamu vema. Namaanisha gemu hili hupatikana playstore na pia unaweza lipata kitahisi kwa kugusa INSTALL

Uungaji: Ili kucheza game hili mukiwa wawili inatakiwa kilammoja wenu awe na game hili katika simu alafu muziunge simu zenu kwa Wi-Fi. Yaani mmoja awashe Hotspot na mwingine WiFi alafu muziunganishe. Mukisha maliza mufanye yafuatayo.

Simu iliowashwa Hotspot:
1. Fungua game na likifunguka chagua Multiplayer kwa kugusa Kama inavyooneswa katika picha.

2. Hatua ya pili ni kuchagua mahali mnakotaka kwenda kupigania au kushindana. Kuna sehemu moja ukiichagua munapelekwa kijiji kilichojaa Zombies na sehemu 3 nyingine za kawaida tu. Chagua sehemu uipendayo kwa kuigusa kama nilivyochagua katika picha. 

3. Ukichagua sehemu, utaletewa ukurasa uliopo hapa chini katika picha. Kwakua wewe ndie uliewasha Hotspot, gusa neno Host game baada ya kugusa tu utapelekwa katika sehemu ulioichagua ili ukamsubiri mwenzako.

Simu iliowashwa FiWi:

1. Fungua game alafu chagua Multiplayer Kama kawaida.

2. Chagua sehemu ya kwenda. Itakubidi muchague sehemu moja na alietangulia ili mukutane kwenye sehemu hiyo.

3. Baada ya kuchagua sehemu, itakuletea ukurasa uliopo hapa chini katika picha. Chagua neno Find game.


4. Ukifanya uchaguzi huo utaletewa ukurasa uliopo hapa chini katika picha. Chagua sehemu ya kwanza kabisa ili kuunganisha game lako na lamwenzako. Ukigusa hapo tu utapelekwa moja kwa moja katika sehemu mulioichagua mukapigane.

Ukiona dalili hizi Jua Account yako ya Facebook imedukuliwa na si salama (hacked)

Account za mitandao ya kijamii huwa zinawindwa na kudukuliwa na hackers. Katika Facebook muda mwingine unawezakua unatumia account iliodukuliwa na haujui kuwa imedukuliwa. Madhara ya kutumia account ya Facebook iliodukuliwa ni kwamba hacker anaweza itumia account yako ya Facebook kufanya uhalifu kwa watu Wengine na hao watu wakajua wewe ndiye umewafanyia hivyo. Kwaiyo ni muhimu kujua hali ya account yako ya Facebook ili kuepukana na mambo kama hayo.

WhatsApp yako inatatizo? Jifunze jinsi ya kutatua hapa>>>>

Kwenye audio nimezungunzia jinsi unavyoweza tambua kama account yako ya Facebook imedukuliwa/hakiwa na hackers. Kama imekufungua wewe basi usiache kuwa kuwajulisha na watu wako wengine wa karibu juu ya hili ili waweke account zao salama sisijetumika kukutapeli na vitu vingine kama hivyo. Unaweza gusa kitufe cha kijani hapo chini kuwasamazia watu ujumbe huu kwenye WhatsApp.

Kuangalia vifaa vilivyotumika kuingia kwenye Akaunti yako ya Facebook

  • Ingia kwenye account yako ya Facebook na uguse vimistari vitatu(menu)
  • Baada ya hapo chagua “Settings” ingia kwenye “Security and Login
  • Ukisha fanya hivyo utatupwa kwenye ukulasa ambao unakipengele kilichoandiwa “Where you Logged in“. Kwenye kipengele hiki unakutana na list ya vifaa ulivyotumia kuingilia kwenye account yako ya na taalifa nyingine kuhusiana uingiaji.

Mazoezi ya mwili ambayo husaidia katika Mapenzi

Mazoezi ni kitu muhimu sana katika maisha ya mwanadamu kwa sababu huuweka mwili vizuri na huuepusha na baadhi ya magonjwa pia. Mazoezi pia yamethibitika kusaidia katika kuuweka mwili mwili vizuri katika upande wa tendo la kujamiiana/kufanya mapenzi kwa jinsia zote mbili. Lakini unatakiwa kujua kuwa si mazoezi yote huwa na faida katika upende wa kufanya mapenzi bali ni mazoezi ya Kigel ndio huwa na faida katika upande huu.


Kigel ni aina ya mazoezi rasmi yalioandaliwa kwaajili ya kuimarisha misuli ya nyonga na viungo vilivyopo chini kwa mwanaume na mwanamke. Mazoezi haya husaidia viungo vilivyopo chini ya nyonga kuboresha mawalisiliano, kuboresha udhibiti wa kibofu cha mkojo na pia huimarisha uwezo wa kufanya tendo/mapenzi

Ukiona dalili hizi Jua Account yako ya Facebook  imedukuliwa na si salama GUSA HAPA>>>>

Jinsi ya kufanya mazoezi ya kigel
Kitu kizuri kuhusu mazoezi haya ni hayahitaji gharama zaidi ya muda wako maana unaweza yafanya hata ukiwa nyumbani. Mazoezi haya hufanywa na wanaume au wanawake. Tafuta sehemu yenye hewa safi na nafasi ya kutosha pia iweinaruhusu wewe kulala chini (chini pawe pasafi au weka kitambaa), inaweza kuwa ni chumbani, sebleni na ikiwezekena nenda katika vyumba maalumu vya kufanyia mazoezi. Baada ya hapo unaweza fanya mazoezi yafuatayo;

Zoezi la kwanza;

Lala chali katika sakafu ilionyooka, kunja magoti kisha pandisha kiuno juu kabisa kama picha iliopo juu inavyoonesha. Baada ya kufanya hayo anza kupandisha kiuno hicho na kukishusha. Endelea kufanya hivyo kwa muda usiopungua dakika tano.

Zoezi la pili;



Jilaze katika sakafu ukiwa umenyooka na umeangalia chini, kisha unyanyue mwili wako kwa kutumia miguu yako na mikono yako kama jinsi picha inavyoonesha. Kaa kwa kuganda kama ulivyo na hakikisha wiliwako unanyooka kama rula kutoka miguuni hadi kichwani. Endelea kukaa kwa muda usiopungua dakika tano.

Zoezi la tatu;

Lala chali ukiwa umeinyoosha miguu alafu nyanyua mikono na miguu juu kisha kunja magoti miguu ikiwa bado ipo hewani. Anza kuushusha mguu wa upande mmoja wakati huohuo hukishusha mkono wa upende tofauti na uliopo mguu kisha rudisha tena mguu na mkono juu. Rudia kitendo hicho kwa mguu na mkono mwingine. Endelea kurudia rudia tena tendo hilo kama picha inavyooneshwa katika picha inavyooneshwa hapo juu kwa muda usiopungua dakika tano.

Maneno ambayo hutakiwi kuyasema kwa mwenza wako GUSA HAPA>>>

Hayo ni baadhi tu ya mazoezi ya kigel ambayo unaweza fanya kila siku ili kuuweka mwili wako uwe vizuri katika tendo la kujamiiana. Sasa tuangalie baadhi ya faida ambazo mtu anaefanya mazoezi haya huzipata.


Faida kwa mwanaume

  • Huongeza uwezo wa kujizui kumaliza tendo kwa haraka
  • Huimarisha misuli katika sehemu zake
  • Huongeza uwezo wa kubana mkojo

Faida kwa mwanamke

  • Huimarisha misuri ya nyonga na kuifanya iwe fanisi
  • Huongeza hamu ya kufanya mapenzi
  • Hufanya mzunguko wa damu ufanyike vizuri katika sehemu zake.

Natumaini mpaka hapa umejifunza kitu na nakusihi endelea kuwa na The Bestgalaxy hakikisha upo na sisi kila wakati ili uendele kupata vitu vizuri.

Jinsi ya kufanya simu isiishe chaji haraka

Hapa tumeelezea vitu vichache unavyoweza kufanya kwenye simu yako ya Smartphone (Android) ku refusha maisha ya chaji. Hii inaweza kuwa msaada mkubwa Kwa watu wenye simu zinazowahi kuisha chaji.

Lakini unachotakiwa kujua ni kwamba vitu vinne tulivyotaja katika Audio si vitu pekee vinavyorefusha maisha ya chaji. Kama utaka kaelezo zaidi ya kufanya vitu hivi kuandika ujumbe wako na kutumia Kwa njia ya WhatsApp kwa kugusa kitufe kilicho andikwa “Chati nasi WhatsApp” kwenye Home Page yetu.

Ukiona dalili hizi Jua Account yako ya Facebook  imedukuliwa na si salama GUSA HAPA>>>>

Magroup ya WhatsApp ya kujiunga bure GUSA HAPA>>>

Ujumbe mzuri kwa mpenzi wako katika kipindi cha Krismasi

Kipindi cha mwisho wa mwaka ni kipindi kizuri sana cha wapenzi kutumia muda wao pamoja. Sasa kama unampenzi basi katika ukaribu wenu wa kipindi hiki unaweza kumtumia mpenzi wako ujumbe mzuri utakao mfurahisha na kujiona wa peke katika maisha yake. Hapa tume kuandalia jumbe nzuri unazoweza mtumia mpenzi wako katika kipindi cha Krismasi. jumbe hizo ni zifuatazo;


~~~~Tulikutana, tukapambana ili tubaki pamoja, tukashinda na tulikua na nguvu katika changamoto zote tulizokabiliana nazo mpaka kufika hapa. Nafikili penzi letu litazidi kuwa imara zaidi. Nimependa kutumia Christmas hii kukukumbusha kuwa, nakupenda sana mpenzi wangu.~~~~

~~~~~~Penzi lako ni zawadi bora ambayo ninaweza kuifurahia zaidi! Krismasi njema, mpenzi!~~~~

~~~~Siku zinakwenda, masaa yana kwenda mimi bado nipo na wewe. Unaona naishi kwa furaha, naona kuishi ni raha lakini tambua sababubu kubwa ni wewe. Tafadhari usije sahau kuwa nakupenda na moyo wangu umetekwa na wewe.~~~~~~

~~~~~Krismasi inakuja mara moja kwa mwaka, lakini tafadhali jua kwamba ninakuenzi kila siku, bila kujali umbali kati yetu. Christmas njema mapenzi wangu.~~~~~

~~~~Nakutakia Christmas njema mme/mke wangu… Nakupenda Sana na ningependa popote ulipo utambue una nusu ya moyo wangu na nusu niliobakinayo yote inakupenda wewe.~~~~

~~~~Penzi letu ni changa bado lakini upendo wangu kwako upo zaidi ya unavyoweza kufikilika, nakupenda Sana na nafurahi kila nikikuona mbele ya macho yangu hakika umeteka hisia zangu. Nakutakia furaha msimu huu wa sikukuu na nitafurahi zaidi tukitumia wote siku ya Christmas.~~~

~~~~~Wewe ni ua zuuri lililoota katika bustani ya moyo wangu, tena ni ua pekee la thamani, linalonipa furaha katika maisha yangu. Nakupenda Sana na najivunia kuwa na wewe malaika wangu. Kuwa na furaha tele katika msimu huu wa sikukuu, kipenzi changu!~~~~~~

~~~~~Hakuna raha kama kupendwa na wewe na sijawahiona karaha kuwa na we. Kama moyo wangu ungekuwa wazi, ungejiona ukiwa peke yako na ukobusy kunipa furaha. Nakupenda Sana na nakutakia furaha katika msimu huu!~~~~~

~~~~Katika Christmas hii nitapenda niwe na furaha, na nikae na mtu ninaempenda na anipae furaha. Vyote hivyo vitakamilika endapo tutatumia siku hiyo pamoja maana utanipa furaha na vile vile nitakuwa na wewe nikupendae na unapae furaha. Mpenzi, tutakua wote si ndio?~~~~

~~~~~Wanasema furaha haiwezi kupimwa kwa maneno halisi, Ni kweli. Tambua kuwa Krismasi hii inatukumbusha kwamba upendo, furaha, na nia njema ndio vitu halisi vinavyoinua maisha yetu. Asante kwa furaha unayoniletea tangu nilipokutana na wewe, mpenzi wangu.~~~~~