Jinsi ya kuachana na mtu asiyekupenda

Mapenzi au mahusiano yana mambo mengi sana ya kufurahisha na kuumiza pia. Kupenda usipo pendwa ni moja ya jambo la maumivu sana katika mapenzi. Jambo hili kama haujawahi pitia, basi unaweza kuwa umewahi ona kwenye filamu au kwa mtu mwingine wa karibu yako. Ni jambo linaloumiza sana na huwa linamuumiza aliependa tu, asiependa huwa haumii maana moyo yake unakua hauhisi au kujali chochote.

Ikiwa upo kwenye hali ya kumpenda mtu asiekupenda inaweza fikia wakati akakuelewa na kuanza kukupenda pia. Hivyo usiwe mwepesi sana wa kukata tamaa.
Ila ukiona hakuna dalili nzuri za kukugeukia na kukupenda, kuachana nae ni uamuzi mzuri pia maana maumivu ya mapenzi yakizidi sio mazuri. Ni rahisi sana kumfanya mtu anaekupenda, akuchukie kuliko kumfanya mtu asiyekupenda, akupende. Kuna watu hupata magonjwa na hata kupoteza maisha kutokana na maumivu wanayopata katika kulazimisha kupendwa wasipopedwa. Kama utapenda, unaweza fuata hatua zifuatazo katika kuachana na mtu asiyekupenda kabisa.

Mambo ya kuepuka baada ya kuachana na Mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

Hatua za kuachana na mtu asiyekupenda

Kuwa muwazi kwake

Moyo wako unaweza kuwa unakusukuma kusema Mambo mengi sana kuhusu pendo wako kwake. Unapotaka kuachana nae, ni vema ukaufungua moyo wako kwake kwa kusema Mambo yote unayotamani ajue. Tua Kila kitu kilichokua moyoni mwako ili moyo wako na akili yako iwe huru pindi utakapokua umemgeuzia mgongo. Unaweza fanya hivi kwenye simu lakini itakua vizuri zaidi kama mtaonana kabisa na kufanya mazungumzo. Kama ni mwanaume au mwanamke, kuwa huru kumwambia vitu ambavyo badae havita uvuta moyo na kukusumbua kuwa huku mwambia. Mwambie jinsi gani unapenda, unatamani aweje kwako na ikiwezekana mwambie na anakupa shida kiasi gani.

Kumbuka thamani yako

Kumpenda mtu kunaweza kusahaulisha thamani yako. Ukiwa unalazimisha sana kupendwa usipopendwa, kunajinsi unaweza jihisi hauna thamani. Lakini ukweli ni kwamba, thamani hua inakua pale pale. kila mtu ana thamani hapa Duniani haijalishi unapendwa au haupendwi. Kikubwa ukumbuke au utambue thamani yako tu alafu baada ya hapo unaweza anza kujiamini kwenye mambo yako na maamuzi yako.

Zingatia vitu vingine na kujiweka mbali nae

Kumzingatia mwanamke au mwanaume alietambua upendo wako kunaweza kukuyumbisha hata kimaisha au kiuchumi bila kukuletea faida yoyote mwishoni. Ni vema ukaanza kuzingatia vitu vingine vinavyoweza rahisiha maisha yako au kukuletea faida mwishoni. Wekeza muda wako kwenye kujifunza vitu vipya, kufanya mazoezi au kazi. Wakati ukifanya hayo hakikisha unajiweka mbali na mtu asiyekupenda.

Jipe muda wa kusahau

Tambua kuwa maumivu ya kumuacha mtu unaempenda hayawezi kuisha katika siku moja au mbili. Yanaweza kuchukua muda mrefu kidogo na ili uweze kufikia hatua ya kuto kuumia. Unapaswa kukubaliana na kila kitu alafu ujipe muda wa kusahau. Pamoja na maumivu unavyoweza pitia unapaswa pia kujikumbusha kuwa “Maumivu yote yataisha,utakua vizuri na utapenda mtu mwingine”. Kunasiku unaweza fanikiwa kumtoa moyoni au kupunguza maumivu aliokupatia.

Wakati unajipa muda wa kusahau usisahau kufuahi, fanya vitu salama vinavyokupa furaha huku ukipanga mipango mipya ya siku zijazo.

2 thoughts on “Jinsi ya kuachana na mtu asiyekupenda”

Leave a comment