Kuna wanaume huwa wanaogopa wanawake wazuri kwao. Kuogopa huku tunakozungumzia sio kuogopa kuwaoa. Yani unakuta mwanaume akimuona mwanamke mzuri wa sura, muonekano au msafi sana, akili huwa inamuhama. Na haimuami kwa matamanio, inamuhama kwa woga.
Kwenye kuongoza ndio muoga kabisa kiasi cha kutojaribu. Anaweza kuwa anaogopa na kuona kwamba mwanamke huyo mzuri ni kiumbe ambacho hawezi hata kukigusa. Anaweza kujiona yupo kwenye wakati mgumu sana endapo atakua kwenye mazingira ambayo amezungukwa na wanawake wazuri. Hatakama atatakiwa kuongea na mwanamke mzuri kuhusu mambo yasio husiana na mapenzi, bado huwa ni mthihani kwake. Katika maisha ya mahusiano, ameisha jiwekea mipaka ya mwanamke wazuri asio weza kuwao nao kwenye mahusiano maana hua wanamchanganya hata akiwa nao karibu tu. Kiufupi ni mwanaume anaeogopa wanawake wazuri.
Kwanza kabisa ni vema kujua kuwa ni kawaida kwa wanaume kuogopa au kuwa na wasiwasi mbele ya wanawake wazuri. Ila kama hali hii imezidi sana inaitwa gynophobia. Gynophobia ni hali ya kuogopa wanawake kiujumla.
Katika upande wa wanawake wazuri, unaweza jaribu kuelewa na kufanya yafuatayo ili kuondoa au kupunguza uoga.
Mazoezi ya mwili ambayo husaidia katika tendo BONYEZA HAPA>>>
Sababu za Mwanaume kuogopa wanawake wazuri na jinsi ya kujiweka sawa
Mambo unayotarajia
Kuna watu hua wanaingiwa na woga au wasiwasi wanapokua mbele ya mwanamke wazuri. Kuna vitu huwa vinawajia kichwani mara tu ya kuwaona. Yani anaweza kuwa amemuona mwanamke mzuri lakini akili yake imempeleka mbele kiasi kwamba anapoteza umakini katika wakati aliopo. Mfano; anaweza kuwa ameonana ya mwanamke mzuri na anataka kumsalimia lakini kichwani ameisha waza kuwa “Huyu mwanamke mzuri sana. Huenda nikimsalimia hata jibu… Asipojibu itakuaje?”. Kwa kuwaza hayo tu unaweza poteza umakini na kuingiwa na woga.
Kama unajiona unaogopa wanawake wazuri kwasababu hii, jaribu kupunguza matarajio mbaya. Fanya kitu unachoona ni sahihi bila kujali atafikiliaje au kitakutokea kitu gani kibaya. Ukifanya kitu kizuri alafu akakutukana, akakuonesha dharau au kitu chochote kibaya, tatizo litakua kwake na sio kwako.
Pia tabia ya kuangalia video za ngono na kujichua inaweza fanya unapokutana na mwanamke mzuri ufikilie vitu vingi kichwani na kuingiwa na woga au wasiwasi kupita kiasi mbele yake. Kama unajihusisha na tabia hizi, unaweza ziacha au kupunguza ili kujiweka sawa.
Uzoefu
Kuna baadhi ya wanaume hawana mazoea ya kuwa karibu na wanawake wazuri na ndio sababu ya kuwaogopa. Hii inaweza kuwa ni kutokana na mazingira mwanaume uliokulia au aliopo.
Kama unahisi hili inaweza kuwa sababu ya kuogopa wanawake wazuri na unataka kubadilika, anza kwa kujizoesha kuwa nao karibu.
Unaweza anza na kujisukuma kuwasalimia unapokutana nao. Unapojiwekea uzoefu huu, usiwe unawaza kuwaweka kuwa wapenzi wako. Jizoeshe kuwa nao karibu tu na usiwe na lengo la moja kwa moja la kuingia nao kwenye mahusiano. Liweke pembeni kidogo wazo la kuwa nao kwenye mahusiano. Unapo msalimia, anapokuita, unapomuita, unapokua mbele yake au kongea nae, usifikilie moja kwa moja mambo ya mahusiano ya mapenzi.
Kwa kufanya hivyo unaweza zoea na kuwachukulia wanawake wazuri ni wakawaida kwenye maisha yako alafu baada ya hapo, maamuzi ya kuingia nao kwenye mahusiano yatakua ni yako sasa.
Kujiamini na kuijua thamani yako
Kuna watu huwa wanaogopa wanawake na tatizo kubwa ni kushindwa kujiamini tu. Yani wanajiona hawana thamani mbele ya mwanamke wazuri kwao.
Kujiamini sio lazima uwe na pesa. Kujithamini au kutambua thamani yako sio lazima uwe na pesa. Kuna mpka watu kwenye maisha waliaza kujiamini au kujithamini ndipo wakapata pesa.
Popote ulipo kama mwanaume, jiamini na kujithamini pia. Usiionee aibu kazi yako, nguo zako, sura yako, sauti yako, mwendo wako au vitu unavyofanya hata kama unahisi mwanamke mzuri atakidharau. Ukifanya hivyo hata kama hauna pesa, unaweza mtetemesha mwanamke wazuri wenye pesa.
Asante kwa muda wako ndani ya The bestgalaxy. La kuongezea hapa mwisho ni kwamba mtazamo wako juu ya wanawake wazuri ni muhimu kuuweka vizuri ili usiwaogope. Watazame wanawake wazuri kama binadamu wa kawaida na sio malaika kama jinsi tunavyowasifu au wanavyojisifia. Na pia fahamu kuwa uzuri wa mwanamke au urembo anaoweka ni kwaajili yako wewe mwanaume hivyo hauna haja ya kuogopa, furahia kuwaona.