Dalili za mahusiano ya mapenzi yanayo taka kuvunjika na jinsi ya kuokoa

Tulisha angalia vitu au mambo muhimu katika mahusiano ya mbali yanayoweza pelekea mahusiano ya mapenzi kudumu. Kama haukusoma, unaweza BONYEZA HAPA kusoma juu ya hili.
Hapa the bestgalaxy, tunaenda kukujuza juu ya dalili za mahusiano ya mapenzi yanayo taka kuvunjika bila kujali ni ya mbali au karibu. Inaweza kuwa ni ngumu moja kwa moja kueleza mambo yanayo ashiria kuwa mahusiano ya mapenzi yanataka kuvunjika maana kuna mahusiano ya mapenzi hupitia vitu vingi vibaya na bado hudumu. Mahusiano haya ya mapenzi huwa yanafikia hatua ambayo unaweza sema yanaenda kuvunjika lakini yanarudi katika mstari na kuwa poa tena.


Lakini mbali na yote, sisi tumekukusanyia dalili ambazo mara nyingi huwa zinaashiria kuwa mahusiano yanaenda kuvunjika. Pia utapata na mwanga mdogo wa namna mtu unaweza fanya kuyarudisha mambo kwenye mstari.

Kama umeona dalili hizi kwenye mahusiano yako ni vema akazishughulikia maana hatakama mnapendana sana bado huwa zikionekana inamaana mahusiano yapo kwenye hali mbaya kidogo.

Maneno ya kumwambia mpenzi wako usiku  BONYEZA HAPA>>>

Dalili za mahusiano ya mapenzi yanayo taka kuvunjika na jinsi ya kuokoa

Kufifia kwa mawasiliano

Inaweza kuwa sio mara ya kwanza kuambiwa kuwa “Mawasiliano ni kitu cha msingi sana katika mahusiano”. Mawasiliano yakiwa sio mazuri au yamefifia kwenye mahusiano ya mapenzi ni jambo hatari sana maana huashilia mahusiano yanataka kuvunjika au yanaweza kuvunjika kirahisi.

Hali hii inaweza kuwa ni hamuwasiliani kwenye simu au muko sehemu moja lakini hamna muda mnakaa na kuzungumza vizuri.
Ukikusa mahusiano yako yapo kwenye hali hii jaribu kumgeukia mpenzi wako na kutengeneza muda mtaokaa pamoja na kufanya mazungumzo. Usizidishe kuwa buzy kiasi cha kushindwa kumjulia hali mpenzi wako au kutenga muda wa kuongea nae ujue anataka nini, anawaza nini au amepanga kufanya nini.

Mara nyingi ukipambana na kuanza kuongea na mtu, hatakama alikua hataki inaweza fika wakati mnajikuta mnapenda kuwasiliana tena.

Kutojali

Ikifika wakati wapenzi mupo kwenye mahusiano na hakuna tena kujaliana au mmepenguza kujaliana inaweza kuwa ishara mbaya. Katika mahusiano kila mmoja anatakiwa kumjali mwenza wake. Mwanaume anatakiwa kumjali mwanamke na mwanamke pia anatakiwa kumjali mwanaume.

Endapo kujali kutapungua katika upande mmoja au pande zote inaweza kuwa ndio mwanzo wa mahusiano kuvunjika. Hali hii inaweza weka hata urahisi wa mtu kuanzisha mahusiano mengine mapya na mtu ambae anaona atamjali zaidi.
Unapona hali hii katika mahusiano ni vema kumgeukia mwenza wako na kuonesha jinsi gani unamjali. Usiishie kuongea, uoneshe kwa vitendo pia kuwa yeye ana umuhimu kwako, unampenda na unapenda anavyokupenda. Usisahau kujali hisia zake, kumsikiliza, kumsaidia kwenye shida na kuwa upande wake unapoona anakuhitaji.

Mambo muhimu kufanya kwa mpenzi mwenye hasira au ukorofI BONYEZA HAPA>>>

Kupungua kwa hisia au msukumo wa kuwa pamoja

Hisia za upendo na msukumo wa kuwa pamoja ndio mara nyingi hutuendesha kwenye mahusiano. Hisia na misukumo hii huwafanya watu waingie kwenye mahusiano ya mapenzi bila hata ya kuambiana neno “Nakupenda”. Lakini msukumo wa kuwa pamoja na hisia hizi zinaweza pungua watu wakishaingia kwenye mahusiano. Hili hii inaweza pelekea mahusiano kuyumba au kuvunjika kabisa.


Kuna mambo mengi hupelekea jambo hili na kabla ya kuangalia utaokoa vipi, ni vema ukajiuliza chanzo ni kipi. Hili ya kukosa msukumo wa kuwa pamoja au hisia za upendo inaweza tokea kutokana na mambo kama Msongo wa mawazo, mazoea au kukosa malengo na mtu ulienae kwenye mahusiano.

Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze Kila mala BONYEZA HAPA>>>

Malumbano ya mara kwa mara

Mahusiano nyenye Malumbano ya mara kwa mara yanaweza kuwa ndio yanatoa ishara ya kufikia mwisho japo mengine huendelea. Baadhi ya mahusiano hupitia kwenye malumbano na misukosuko kibao lakini huendelea kusonga. Lakini bado malumbano katika mahusiano yakizidi ni jambo baya linaloweza pelekea mahusiano kuvunjika.


Mukiwa kama wapenzi mukiona malumbano yamezidi inafaa mbanane, mkae pamoja, muweke hasira pembani na kuulizana “kwanini muko hivyo? Na unatakiwa kufanya nini ili kuyashinda kisha muendelee kuwa pamoja kwa amani?”.

Kupotea kwa malengo yenu ya pamoja

Mahusiano bila malengo ya pamoja tunaweza sema ni safari bila muelekeo. Mnapokua kwenye mahusiano, kuongelea mambo yenu ya mbele mtayofanya pamoja au kutimiza ni jambo muhimu. Ni muhimu kuwa na vitu ambavyo hata mkikosana mkikumbuka kuwa mmepanga kuvitimiza kwa pamoja, inakua rahisi kupatana. Endapo mambo au malengo yenu ya pamoja yataanza kukosa uzito kwenu au yatapotea kabisa, inaweza kuwa dalili ya kuwa mahusiano pia yanaenda kupotea.

Ukiona dalili hii ni vema ukazidisha upendo na kuwa karibu na mwenza wako sana alafu mkiongea, mazungumzo yenu yawe yanajumuisha malengo au vitu vya kufanya pamoja.

Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze kila mara BONYEZA HAPA>>>

Usianze na mambo makubwa kama ndoa, Anza na madogo ambayo unaweza mtimizia au mkafanya pamoja baada ya wiki toka muongee tu. Mfano; kwenda nae sehemu nzuri, kununuliana vitu au kusaidiana mambo mengine yajayo.

Ni hayo tu katika ukurasa huu tumekuandalia. Lakini kabla ya kuondoka nakukumbusha kuwa mambo haya yanaweza tokea kwenye mahusiano na bado safari ya mapenzi ikaendelea japo mara nyingi huashiria mahusiano yanataka kuvunjika.

Kuwa mjanja! Tufuate kwenye akaunti zetu mpya za kijamii ; Instagram na Facebook

Leave a comment