Call of Duty Warzone Mobile: Mambo ya kujua kuhusu game hili

Kuna muda Activision ilituacha na game moja tu zuri la Call of Duty ambalo tunaweza kulicheza kwenye simu. Game hilo linaitwa “Call of Duty mobile” na Activision walilitoa katika mwaka 2019. Katika mwaka wa 5 toka game hilo litoke na kuwa na mafanikio makubwa duniani, wakaamua kuongeza game lingine la Call of Duty iitwalo “Call of Duty warzone Mobile”. Game hili kilikua likisubiriwa na watu wengi sana maana lilikua linapatikana katika platform nyingine za game. Lilikua rasimu kwenye vifaa vingine vya games lakini halikua rasimi kwa simu/mobile. Activision walilitoa game hili rasimi tarehe 21 mwezi wa 3 mwaka 2024.

Call of Duty Warzone Mobile

Call of duty warzone Mobile ni First-person shooter game ambalo lina mode ya Battle Royale ambayo inawakusanya watu au wachezaji zaidi ya 120 katika eneo moja wapambane kubaki hai. Ni game la kivita la mtandaoni(online) unaloweza cheza kama timu au peke yako(solo). Kama ilivyo kwenye mechi za magame mengine ya Battle Royale, mshindi ni anaebaki hai peke yake au timu inayobaki hai pekee.

Sasa ukitaka kuona raha ya Mode hii, anza na kujiuliza kama unaweza kuwekwa sehemu moja na zaidi ya watu 120 wanaopambana alafu ukabaki mzima peke yako au na timu yako? Ukihisi unaweza, pakua na kujaribu katika game hili.

Kulipakua na kulicheza

Ili kulipakua/kudownload game la Call of Duty warzone Mobile kwenye simu yako ni lazima simu ikidhi vigezo. Simu inahitajika kuwa na GB 4 hadi 8 za RAM alafu pia Adreno 618 GPU au GPU nyenye uwezo zaidi ndio zanaweza kukuwezesha kulicheza. Hayo ni kwaajili ya simu za Android tu tena Android 13 na kuendelea.
Kwenye iOS huku, kifaa chako kinatakiwa kuwa na iOS 17.0 au zaidi na GB 3 za RAM.

Simu yako ikiwa na uwezo huo ndio utaweza kulipakua gemu la Call of Duty warzone Mobile na kulicheza. Linapatikana katika Play store kwaajili ya mtu wa Android na pia inapatika kwenye Appstore kwa watu wa iOS. Lakini kabla ya yote unakiwa kujua kuwa game hili linaweza kuchukua kama GB 5 hivi katika nafasi ya simu yako. Kwaiyo hakikisha unanafasi ya kutosha na hata kwenye internet pia uko vizuri.

Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy na usisahau kusoma na kujifunza vitu vingine vingi katika sehemu hii.

Kutatua tatizo la “CONNECTING TO ONLINE SERVICES” kwenye Warzone mobile BONYEZA HAPA>>>

3 thoughts on “Call of Duty Warzone Mobile: Mambo ya kujua kuhusu game hili”

Leave a reply to Jaka Cancel reply