Kutuma pesa nje ya nchi ilikua ni jambo gumu sana katika miaka ya nyuma, lakini wakati huu jambo hili ni jambo jepesi kiasi kiasi kwamba unaweza fanya kiganjani pako ndani ya dakika mbili. Hii yote ni kwasababu ya Teknolojia ambayo lengo lake ni kurahisisha maisha ya Binadamu.
Hapa The bestgalaxy tunaenda kuangalia jinsi ya kutuma pesa Kenya na Tanzania kwakuhusisha Safaricom Kenya na Vodacom Tanzania. Kama upo nchi ya Tanzania, unaweza tumia mtandao wa Vodacom kumtumia pesa mtu kwa Mpesa akiwa kenya anatumia mtandao wa Safaricom. Pia ukiwa kenya unatumia Safaricom unaweza mtumia pesa mtu kwa Mpesa akiwa anatumia mtandao wa Vodacom Tanzania.
Jinsi ya kutengeneza Logo ya biashara au Binafsi BONYEZA HAPA>>>
Kutuma pesa Kenya na Tanzania (Vodacom/Safaricom)
Unataka kujua jinsi ya kutuma? Usijali, hapa chini kuna maelezo juu ya hatua unazoweza kufuata pale unapotaka kutuma pesa ukiwa Tanzania na kenya kwakutumia mtandao wa Vodacom au Safaricom.
Kutuma pesa toka Tanzania kwenda Safaricom Kenya kwa kutumia Mpesa(Vodacom)
- Fungua App ya Mpesa na uguse sehemu ilioandikwa “Services” alafu utaletewa orodha ya huduma.
- Chagua huduma ilioandikwa “International Transfers” kwenye orodha hiyo.
- Baada ya kufanya hiyo utapelekwa kwenye ukurasa utakao takiwa kuchagua nchi unayotaka pesa iende. Utachagua Kenya kwakua ndiko unataka kutuma pesa.
- Baada ya kuchagua nchi utaletewa ukurasa wa kuchagua mtandao. Wewe utachagua mtandao wa Safaricom kwakua mtu unaemtumia anatumia Safaricom.
- Baada ya kuchagua, utapelekwa kwenye ukurasa utakao takiwa kujaza namba ya simu ya mtu unaemtumia pesa kwa mfumo wa kimataifa (254xxxx) kisha andika kiasi unachotaka kutuma. Na ukishajaza utabonyeza kitufe kilichoandikwa “Endelea” ili kuendelea na hatua nyingine za uthibisho wa kutuma pesa yako.
Sending money from Kenya to Tanzania with Mpesa (Safaricom)
- Dial *334# to open Mpesa Global.
- Select “Send Money Abroad”.
- Select “Send to Mobile Number”
- Select “Tanzania” as a county you want to send money.
- Enter Recipient Mobile Number in International Format (255xxxxxx)
- Enter Amount of Money you want to send.
- Select source of fund and purpose of Funds then confirm.
Mwisho ningependa kukukumbusha kuwa makini katika kutuma pesa yako ili kuepuka kutuma pesa kimakosa. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy na usiache kufuatilia The bestgalaxy.
kunandugu ana line ya safaricom anataka kutuma pesa Tanzania kutumia *334#
inakataa shida nini leo
LikeLiked by 1 person
Ingia Katika Facebook page alafu tafuta page/ukurasa wa Safaricom. Hakikisha ukurasa huo ni official (unatiki). Baada ya hapo, watumie ujumbe ukielezea tatizo lako. Watakujibu na kukusaidia ikiwezekana. Haijalishi upo nchi gani, huwa wanajibu japo kwa kuchelewa kidogo
LikeLike