Ukiwa kwenye mahusiano Unaweza kufanyia vitu vingi kwema kwa mweza wako ili kuonesha unamjali. Kutumia ujumbe wa mapenzi mpenzi wako ni Moja ya Jambo linaloonesha kujali pia… Mukiwa ni wapenzi mulio mbali hii inaweza kuwa ni kitu muhimu kinachojenga mahusiano kuliko hata kutuma tuma pesa.
Zifuatazo ni SMS au meseji za kumtakia mchana mwema mpenzi wako. Kama unahitaji Unaweza chagua zinazoendana na mahusiano yako kwa sasa kisha ukazitumia kwa umpendae. Endelea kuwa karibu na The Bestgalaxy kwa mambo mengine mazuri zaidi.
SMS za mchana mwema kwa mpenzi wako
Upendo wangu kwako huongezeka kila wakati ninapokutazama. Hautafifia wala kuisha kwa sababu hauna mwisho. Kila mara kumbuka kuwa Nakupenda sana na kwa muda huu nakutakia mchana mwema kipenzi changu.
Mpenzi, muda huu nakukumbusha tu kuwa wewe ndio chaguo langu. Yaani naomba ujue kuwa wewe ni Mfalme wa kasri langu na kwamba moyo uliokaa kifuani mwangu utalidunda jina lako. Ninakupenda zaidi ya ninavyoweza kusema nakupenda. Mchana mwema mpenzi wangu.
Nakutakia mume/mke mtamu zaidi ulimwenguni siku njema. Hakuna mtu katika ulimwengu mzima anaweza kuwa mpenzi wa maisha yangu kwa sababu nafasi hiyo tayari imechukuliwa na wewe, mume/mke wangu mpendwa. Nakupenda Saana na napenda kukupenda.
Asante kwa kupenda kila kitu changu, pamoja na kutokamilika kwangu. Mungu alinipa zawadi isiyo na kifani maishani mwangu pale alipokuumba wewe mpenzi wangu. Nakupenda sana kuliko ujuavyo.
Tambua kuwa wewe ni mtu pekee katika ulimwengu wote ambaye hufanya maisha yangu kuwa kamili kabisa na maridadi. Mpendwa, asante kwa kuleta joto na mwangaza katika maisha yangu. Sijawahi jutia kukupenda.

Nina nafasi moyoni mwangu ambayo hakuna mtu anayeweza kuchukua kwa sababu hakuna mtu mwingine anayeweza kunifanya nifurahi kama unavyonifanya. Nakutakia mchana mwema.
Wewe ni damu ambayo hupitia mishipa yangu. Wewe ndiye kipande muhimu ambacho hufanya roho yangu ikamilike. Siwezi kamwe kuishi katika ulimwengu huu bila wewe, mpenzi wangu wa thamani. Kuwa na siku mchana mwema huko uliko!
SMS za kumtakia mpenzi wako usiku mwema GUSA HAPA>>>
Kuangalia machoni pako kunanipeleka kwenye ulimwengu wenye zaidi ya maelfu ya furaha. Penzi lako hufanya nijihisi Niko paradiso. Umeniweza sasa, naomba kokote uendako usisahau kuwa nakupenda mpenzi wangu. Mchana mwema kwako.
Kila nikiona simu au SMS toka kwako moyo wangu hudunda kwa furaha… Kiufupi nakupenda na natamani kuelezea upendo wangu zaidi ya kukuambia “nakupenda” ili tu utambue na usije kuniumiza. Tambua hilo kipenzi changu… Nakutakia mchana mwema.
Ukiona dalili hizi Jua Account yako ya Facebook imedukuliwa na si salama GUSA HAPA>>>>
Ni2mie hizi massege kwa hii no 0768839158 aky zinanibamba
LikeLike