Battle of Agents: Gemu la kuchezwa na watu wawili au zaidi bila data/internet

Battle Of Agents ni moja kati ya magemu mzuri ya shooting ambayo ni madogo ki-size. Gemu hili hutoa nafasi ya watu zaidi ya mmoja kucheza gemu kwa pamoja kwa kutumia simu tofauti. Halina ukubwa wa kutisha sana kama magemu mengine yenye uwezo huu yaani unaweza lipakua kwa MB chache tu na ukawa unafurahia kulicheza na marafiki bila kutumia data tena. Kwaiyo ni offline multiplayer game.

Muonekano wa gemu hili upo vizuri japo sio bora kama magame mengine Ila uzuri sifa yake nzuri ni kwamba huchezwa hata katika simu zenye uwezo ndogo bila matatizo hivyo kama ulikua na simu yenye uwezo mdogo na ulikua unatamani magame ya kucheza wawili au watatu hili linaweza kuwa gemu ambalo hutakiwi kulikosa.

Upatikanaji: Ninaweza sema hakuna ugumu wowote katika kulitafuta Gemu hili maana hupatikana sehemu ambayo kila mtumiaji wa simu ya Android huifahamu vema. Namaanisha gemu hili hupatikana playstore na pia unaweza lipata kitahisi kwa kugusa INSTALL

Uungaji: Ili kucheza game hili mukiwa wawili inatakiwa kilammoja wenu awe na game hili katika simu alafu muziunge simu zenu kwa Wi-Fi. Yaani mmoja awashe Hotspot na mwingine WiFi alafu muziunganishe. Mukisha maliza mufanye yafuatayo.

Simu iliowashwa Hotspot:
1. Fungua game na likifunguka chagua Multiplayer kwa kugusa Kama inavyooneswa katika picha.

2. Hatua ya pili ni kuchagua mahali mnakotaka kwenda kupigania au kushindana. Kuna sehemu moja ukiichagua munapelekwa kijiji kilichojaa Zombies na sehemu 3 nyingine za kawaida tu. Chagua sehemu uipendayo kwa kuigusa kama nilivyochagua katika picha. 

3. Ukichagua sehemu, utaletewa ukurasa uliopo hapa chini katika picha. Kwakua wewe ndie uliewasha Hotspot, gusa neno Host game baada ya kugusa tu utapelekwa katika sehemu ulioichagua ili ukamsubiri mwenzako.

Simu iliowashwa FiWi:

1. Fungua game alafu chagua Multiplayer Kama kawaida.

2. Chagua sehemu ya kwenda. Itakubidi muchague sehemu moja na alietangulia ili mukutane kwenye sehemu hiyo.

3. Baada ya kuchagua sehemu, itakuletea ukurasa uliopo hapa chini katika picha. Chagua neno Find game.


4. Ukifanya uchaguzi huo utaletewa ukurasa uliopo hapa chini katika picha. Chagua sehemu ya kwanza kabisa ili kuunganisha game lako na lamwenzako. Ukigusa hapo tu utapelekwa moja kwa moja katika sehemu mulioichagua mukapigane.

3 thoughts on “Battle of Agents: Gemu la kuchezwa na watu wawili au zaidi bila data/internet”

Leave a comment