Tag Archives: YouTube

YouTube channel za kuangalia Movie (Bure)

Watumiaji wa internet wana njia nyingi za kufurahia burudani, mojawapo ikiwa ni kupitia YouTube. YouTube ni platform iliopo chini ya Google na watu wengi duniani hutumia kuangalia video mbalimbali kwakutumia vifaa kama simu, smart Tv na PC.


Katika mambo mtumiaji wa YouTube anaweza furahia kwenye YouTube ni kuangalia Movie. Platform hii ni moja ya sehemu movie hupatikana katika mtandao. YouTube hujihusisha na Movie/Filamu pia video za vichekesho, masomo and mambo mengine.


Unaweza angalia movie YouTube kupitia kipengele cha “Movies and Tv” ambacho tumeisha kizungumzia kwa undani kwenye makala nyingine. Ukiachilia mbali kipengele hicho, unaweza pia kuangalia Movie kwenye channel za YouTube zinazojihusisha na movie.


Katika mtandao wa YouTube Kuna channel ambazo hujihusisha na Movie ambazo unaweza angalia Bure. Kupitia channel hizi unaweza pata movie za kuangalia na kufurahia muda wako bila kulipia chochote zaidi ya bando lako la internet.

Hapa chini The bestgalaxy tunaenda kukupa orodha ya hizi channel za YouTube za movie. Lakini unapaswa kujua baadhi ya movie za Bure huwa zinakua hazina ubora sana au zinaweza kuwa za zamani. Nyingine huwa nzuri na unaweza zifurahia bila kujutia muda uliotumia kuangalia.

Kuangalia movie katika kipengele cha movie Cha YouTube BONYEZA HAPA>>>

Channel za YouTube za kuangalia Movie bure

Popcornflix

Popcornflix ni mojawapo ya Channel maarufu za YouTube zinazotoa movie za bure duniani. Popcornflix imejipatia sifa kwa kutoa movie za kiwango cha juu na maalufu ambazo zinawafikia watazamaji kwa urahisi na bila gharama yoyote kwenye YouTube. Kwa wale wanaotafuta movie ya haraka na ya kusisimua YouTube, channel ya Popcornflix ni chaguo zuri sana. Channel hii inafikisha zaidi ya Subscriber Milioni 3 kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni. Kuna tuvuti yake pia ambayo unaweza tembelea kuangalia maelfu ya movie Bure kabisa.

Movies Central

Movies Central ni Channel maarufu ya YouTube inayotoa movie mbalimbali kwa watazamaji wanaotafuta burudani ya Filamu katika YouTube. Channel hii imekuwa ikijizolea wafuasi wengi kutokana na kuwa na movie nyingi za kutisha. Kwa wale wanaopenda kuangalia movie za kutisha, Movies Central ni sehemu nzuri ya Bure kufurahia movie hizo. Katika subscribers, channel ya Movies central inakusanya zawadi yako subscribers milioni 5 na unapata Views za kutosha..

Mr Bean

Mr Bean ni YouTube channel ya vituo vinavyopendwa zaidi duniani kuhusu Mr. Bean. Channel hii inajumuisha movie za Mr. Bean zilizoigizwa na Rowan Atkinson, pamoja na video za katuni ambazo ni kuhusu Mr bean. Kama ni moja wa watu wanao fahamu uwezo wa Mr bean na bado unapenda kuangalia kazi zake basi channel hii inaweza kuwa nzuri kwako. Ina video zinazoweza kukuchekesha na imevutia watazamaji wengi sana katika mtandao wa YouTube. Inaweza kukaa katika nafasi za juu katika orodha ya channel za vichekesho katika YouTube kwa kupata zaidi ya Subscriber Milioni 3 3.

Ni hizi tu tulizokuandalia hapa lakini Kuna channel nyingi zaidi ya hizi ambazo hujihusisha na Movie. Baadhi ya channel za YouTube zilizokua zikitoa huduma ya movie zamani, kwasasa hazijihusishi tena na movie kutokana na sheria content.

Jinsi ya kuangalia video Youtube  bila kutumia bando sana(Okoa data)

Uangaliaji wa video online kupitia app  kama Youtube,Tiktok na Instagram unaweza kua ni moja ya vitu ambayo hupelekea bando la internet kutumika sana kwenye simu. Kiufupi kama mtu anapenda kuangalia video sana mtandaoni basi hata matamizi yake ya data yanaweza kuwa ni makubwa na kupelekea bondo kuisha haraka. Hii inweza kuwa kawaida au ikawa tatizo kwa baadhi ya watu.

Hapa The bestgalaxy tunaendea kuangalia mambo machache ambayo mtu anaweza fanya kuangalia video Youtube  bila kutumia bando sana. Kama unataka kujua mambo yaha hebu chukua muda wako kusomaa hapa chini.

Fanya haya kuangalia video Youtube  bila kutumia bando sana

Washa Data saving mode

Youtube imejali matumizi ya data ya watumiaji wa app ya Youtube kwa kuweka kipendele kinachopunguza matumiza ya Data. Kuna kipegele  ambaacho ukikiwasha katika app ya youtube, unakua unatumia bando lako la internet kidogo. Kipengelea hii kinaitwa Data saving mode na ukikiwasha huwa kinapunguza na kuzima baadhi ya vipengele vingine vya app ya  Youtube vinavyotumia Data. Ni jambo zuri kutumia njia hii kuoa data lakini video hua zinaonekana hazina ubora. Kuwasha Data saving mode nenda katika app alafu gusa Profile yako kisha bonyeza alama ya settings iliojuu kulia alafu chagua “Data saving”. Baada ya hapo, washa sehemu ya juu ilioandikwa “Data saving mode”.

Chagua video fupi

Youtube inavideo fupi na ndefu. Kati ya video fupi na video ndefu katika kutumia data tunaweza sema  uangaliaji wa video ndefu unaweza kufanya utumie data zaidi endapo video hizo zitakua na ubora wa picha sawa. Hivyo kama unahitaji kuangalia video Youtube  bila kutumia bando sana unaweza angalia video fupi badala ya kuangalia video  ndefu. Na hatakama utamaliza bado lako kwa uangalia video fupi utakua umeangalia video nyingi.

Zima Autoplay

“Autoplay” ni kipengele ambacho hufaya video ziwe zinaendelea kujiplay Moja baada ya nyingine mfulilizo pale zinapoisha. Kipengele hiki ni kizuri lakini ubaya wake ni kwamba ukijisahau unaweza kuta video nyingi sana zimejiplay na kumaliza bado lako la internet. Kama unahitaji kuzima kipengele hiki, nenda kwenye app yako ya Youtube kisha ingia kwenye Profile alafu gusa alama ya Settings na uchague “Autoplay”. Baada ya kufanya hivyo, zima Autoplay kwa kugusa kitue kilicho upende wa kulia.

Endelea kuwa karibu na The Bestgalaxy na usiache kutembelea mara kwa mara The Bestgalaxy ili kusoma vitu vingine.

Jinsi ya kuangalia movie katika kipengele cha Movies cha YouTube

YouTube ni Moja ya app maharufu sana Duniani. Inatumiwa na ma billion ya watu toka nchi mbalimbali hapa ulimwenguni.
Hapa Tanzania kunabaadhi ya watu huisi YouTube inajihusisha na videos lakini sio “Movies”. Ukweli ni kwamba YouTube ni moja ya app ambazo zinajihusisha na movies kama app nyingine maharufu katika upande wa Movies.


YouTube inakipendele cha movies kiitwacho “Movies & Shows” kinachokuruhusu wewe kama mtumiaji wake kuangalia movies zozote unazozitaji. Lakini unachotakiwa kujua kuhusu kipengele hiki cha movies ni kwamba, zipo movie za bure na pia movie ambazo lazima ulipie au ununue ndio uziangalie.

Magemu ya kucheza kwenye simu (Android) GUSA HAPA>>>


Kwa bahati mbaya, ukiwa Tanzania uweza kunagalia movies za kulipia tu katika kipengele hiki. YouTube bado haijaruhusu kipengele hiki kitoe movie za bure kwenye baadhi ya nchi, ikiwemo Tanzania. Kwaiyo ukiwa Tanzania huwezi kuangalia movies za bure kwenye kipengele Cha movie YouTube.

Lakini hii haiwezi kukuzuia kabisa kukiona kipengele hiki na movies zake za bure. Unaweza Tumia VPN kukiona na kuangalia movies zake za bure bila tatizo. Unachotakiwa kufanya ni kufuata hatua zifuatazo:

  • Download VPN kwenye simu yako.
  • Ifungue VPN, chagua Server yoyote ya “USA” kisha iconnnet
  • Ingia YouTube Kisha gusa “Library” alafu chagua “Your Movies and Shows
  • Baada ya hapo gusa “Free with Ads

Ukishafanya hivyo utakua tayari upo kwenye movies za bure za kipengele Cha movies Cha YouTube. Itakua ni juu yako kuchagua ipi uiangalie.

Movies za kutafsiliwa GUSA HAPA>>>>