Tag Archives: Vichekesho

Vichekesho vya Maandishi unavyoweza kusoma

Kucheka ni njia bora ya kupunguza mawazo yanayotukumba kila siku. Katika maisha haya yenye changamoto nyingi, kila mtu anahitaji muda wa kupumzika na kufurahia vitu vidogo vinavyoweza kuleta tabasamu. Hakuna njia bora ya kufurahia muda wako wa kupumzika kama kuangalia video au kusoma vichekesho vya maandishi, vinavyoweza kukuchekesha na kukufanya usahau magumu ya maisha kwa muda.

Utafiti unaonyesha kwamba kucheka kuna faida kubwa kiafya, kama vile kupunguza msongo wa mawazo, kuongeza kinga ya mwili, na kuboresha hali ya moyo. Kicheko pia huimarisha mahusiano ya kijamii kwa sababu huleta furaha na mshikamano miongoni mwa watu unaocheka nao. Kwa hivyo, kama unatafuta kitu cha kukuchekesha na kukupa muda wa kuburudika, basi uko mahali sahihi.

Katika makala hii, tumekusanya orodha ya vichekesho vya maandishi vinavyovutia na kuchekesha, ambavyo unaweza kusoma popote ulipo. Jiandae kwa kucheka kupitia vichekesho hivi vya maandishi!

Soma Vunjambavu za vichekesho BONYEZA HAPA>>>

Vichekesho vya Maandishi vya kuvunja mbavu

  1. Mtoto katika maombi

Kila mara mtoto alikua akiambiwa kuwa anaeleta au kuwapa chakula ni Mungu. Siku moja, Mama yake alimwambia huyo mtoto aombee chakula kabla ya kula. Mtoto akaanza:
“Mungu, tunashukuru kwa chakula hiki. Naomba pia ulete chips na soda kesho maana ugali na mboga za majani kila siku zinachosha!”
Watu wote mezani walicheka sana.

  1. Mtoto na Mwalimu

Mwalimu alianza kuuliza kila mwanafuzi darasani “Kwa nini unahitaji kujifunza hesabu?”
Mtoto mmoja akajibu “Ili mama yangu asitumie hela zangu vibaya nikimpa anishikie”
Darasa zima likacheka

  1. Bibi na TikTok

Bibi Fatuma alikuwa sio mjanja na hakuielewa teknolojia ya TikTok. Wajukuu wake walimshawishi ajaribu. Alianza na video kutaka kutengeneza video akiwa anacheza live. Badala ya kubonyeza kitufe cha kuanza kurekodi, aliweka simu mfukoni na kuanza kucheza peke yake huku akipiga makelele ya nyimbo za zamani.
Baada ya muda mrefu, aliwauliza wajukuu:
“Mbona hakuna mtu ana-like video yangu?”
Wajukuu alipo fikilia kuwa bibi yake alichofanya, alicheka sana.

  1. Mtu na mpenzi wake wanaoongea kwenye simu

MKAKA: Hi uwapi swity?
MDADA: Niko home
MKAKA: Unafanya nini?
MDADA: Nakula
MKAKA: Unakula nini?
MDADA: Mama katengeneza macaroni, ambayo kanyunyizia chiizi na sausage fulani imported ambazo baba amenunua supermaketi Masaki, na saladi, kisha ntateremsha na Epo juisi…

Mara ghafla ikasikika sauti ya mama yake “Hivi we Gulo kaka yako atakula nini na we umemaliza ugali na maharage yote?”

  1. Ndoa nyingine

Mtaani kwetu kuna jamaa mmoja anaitwa chogo, ana mtoto mmoja anaitwa “emma” pamoja na mke wake.. leo bwana katoa kali; Alikua amekaa nje ya nyumba yake kwenye kibalaza, alikua ameshikilia cheti cha ndoa yake.. akanza kukitazama sana, ikafika kipindi mke wake ikabidi avunje ukimya na kumuuliza “Baba emma, mbona unakitazama sana hicho cheti..?” bwana chogo akajibu huku akilia, akitoa sauti ya upole “NATAFUTA EXPIRE DATE YA HIKI CHETI CHETU..” Mke wake hoi akazimia…!

Vichekesho vya kiswahili vunja mbavu




Karibu kwenye makala hii yenye vichekesho vya kusoma vinavyofurahisha! Katika ulimwengu wa hadithi za kuchekesha, tunakuletea mkusanyiko wa visa vya kufurahisha na kukuvunja mbavu. Kupitia makala hii, utaweza kufurahia na kucheka kwa kujitupa katika hadithi fupi zilizojaa kujifunza na kuchekesha pia.

Hadithi hizi za kuchekesha zimeandikwa na watu kwa ustadi na kubuniwa kwa kina ili kukuvutia wewe msomaji lakini hapa the bestgalaxy, zimekusanyawa tu. Hadithi inaweza kuja na mchanganyiko wa utani, kujikosoa, na vituko, kikubwa usiwe serious sana, lengo kubwa ni kucheka kufurahi hivyo jiachie.


Kucheka ni moja ya mambo muhimu katika maisha yetu ya kila siku. Kwanza kabisa, kucheka husaidia mtu kupunguza msongo wa mawazo na hali ya wasiwasi. Unapocheka, mwili wako huzalisha homoni za furaha kama vile endorphins, ambazo husaidia kupunguza mkazo na kuongeza hisia za nzuri.

Vichekesho vya kiswahili vunja mbavu

MUOKOTA MAKOPO:

Tamaa mbaya! Muokota makopo katika uokotaji wake wa makopo akaona chupa ambayo ndani kuna kikaratasi, alipoifungua chupa likatoka jitu la ajabu lisilo onekana na watu wengine. Lilikua likitetemeka na lilimwambia “kijana asante sana kwa kuniokoa omba vitu viwili sasa hivi”. Kijana kwa hofu akaomba pesa za kumiliki magari na majumba ya kifahari. Ghafla fuko liliojaa hela na pete ya dhahabu ya bahati vikadondoka mbele yake. Akaambiwa aseme ombi la pili, akasema “Nibadilishe niwe kivutio ili nipendwe sana nakina dada wazuri” Hapohapo jamaa akageuzwa akawa chipsi yai.!!

MTOTO MDOGO KATULIA NA BABA:

MTOTO: Hivi Baba ivi wewe umezaliwa wapi?
BABA: Nimezaliwa Mbeya
MTOTO: Mama nae kazaliwa Mbeya?
BABA: Hapana, amezaliwa Tanga
MTOTO: Na Mimi jee?
BABA: Dar
MTOTO: Mh Sasa tulikutanaje????
Baba akaangua kicheko

JAMAA BAADA YA KUCHELEWA KAZINI:

Boss: kwa nini umechelewa kazini

Juma: kuna mtu njiani alidondosha 5000 boss

Boss: anha kwahiyo ulikua unamsaidia kuitafuta

Juma: Hapana, bahati nzuri niliikanyaga nikawa nasuri aondoke.

MAWAZO YA VIKOBA:

(Mdada baada ya kufika kwa mpenzi wake akiwa na Mawazo mengi ya vikoba)

Mdada: Baby, naomba shilingi elufu kumi na tano nilipie taxi niliokua nayo.

(Mkaka kaingiza mkono mfukoni kutoa pesa lakini ghafla alipomuangalia mpenzi wake vizuri akashtuka!)

Mkaka: Unasema umekuja na Taxi? Mbona umejisahau umekuja na helmet ya Bodaboda?

Katika ukurasa huu, tuliokuandalia ni hayo tu lakini Kuna vichekesho vingi ndani ya The bestgalaxy ambayo unaweza furahia kuvisoma. Endelea kuwa karibu na sisi kwenye mambo mbalimbali tunayojihusisha nayo.

Stori za vichekesho vya kuvunja mbavu BONYEZA HAPA>>>

Vunja mbavu sms za vichekesho (soma hapa)

BANGE SIO CHAI..

Siku moja Nyani alikuwa kakaa kijiweni anavuta bangi,Mjusi(lizard) akaja akampa “Hi” akajiunga na kumuomba puff.

Nyani akamuonya kuwa ile bangi ilikuwa ni kali sana,ni kipisi cha kutoka Milimani huko. Mjusi akapokea wakaanza kuvuta bangi kwa raha zao…baada ya muda mjusi akawa hoi kwa stimu akamuambia nyani “Duh nasikia koo langu limekauka acha niende mtoni nikanywe maji!”

Mjusi kufika mtoni kwa kuwa alikuwa na stimu nyingi akatumbukia mtoni. Bahati nzuri Mamba alikuwa pembeni, akawahi kumuokoa mjusi na kumtoa nje ya maji.

Baada ya kumuokoa, Mamba akamuuliza mjusi “Ina kuwaje bro mbona umetumbukia mtoni kipuuzi vile?” Mjusi akajibu “Nilikuwa na nyani tunavuta bangi nikasikia kiu ya ajabu nikajikuta kwenye maji bila kujua!” Mamba akasema “Aaah wacha niende huko kwa nyani nikamuone.”

Mamba kufika akamkuta nyani ndo anamalizia kipisi chake,kazidiwa hata macho ni tabu kufungua. Mamba akamuita “Oya” Nyani akafungua macho,kumuona Mamba akashtuka Et”Duh! Mshikaji kwani umekunywa maji yote mtoni! Mbona umerudi mkubwa hivyo!!”

SIPATI PICHA INGEKUAJE…

Jamaa yangu mmoja alikuja kunitembelea kule Mburahati Madoto. Sasa wakati namsindikiza tukafika kituo cha madoto mwisho

kusubiri daladala. Mara jamaa yangu akanyewa na kunguru kichwani. Jamaa akaangalia juu alivyogundua amenyewa akamuona

kungulu usawa wake, jamaa akaangua kicheko sana yaani. Mi nilikuwa naona yote yanayotokea nikamuuliza “sasa unacheka nini

ndugu yangu wakati umenyewa?” Jamaa akajibu “We acha tu, afadhali bata hawapai angani kama kunguru”

AMRI KUMI KWA WAPENDAO OFA

  1. Muheshimu anayekununulia
  2. Muamkie mtoa ofa kabla hujakaa kitini
  3. Uwe ndie mchekeshaji wa kikao, lakini usimkatishe mazungumzo anaetoa ofa
    . Mtoa ofa akikutuma popote usikatae
  4. Mtoa ofa akiupenda muziki fulani, we anza kucheza kwa bidii kabisa
  5. Usinywe kwa pupa, kunywa mafunda madogomadogo
  6. Mtoa ofa akitoa kichekesho cheka sana hata kama hakichekeshi

Soma Stori 2 Fupi za Vichekisho (Vunjambavu)

KIKUNDI CHA WATALII kilitembelea mto wa kufugia mamba na walikuwa wakielea kwenye meli ndogo katikati ya mamba wenye njaa. Ikasikika sauti ya mmiliki wa eneo hilo ikisema: “Atakaye ruka kwenye maji na kuogelea kutoka nje atazawadiwa dola milioni 10”. Kila mtu kimya, ghafla mwanaume mmoja akajirusha majini. Alikimbizwa na mamba kwa bahati nzuri alitoka salama. Akatangazwa mshindi. Wakati anarudi hotelini na mkewe akamwambia mkewe “Aisee sijajirusha mwenyewe majini, kuna mtu alinisukuma nikapambana niokoe maisha yangu”. Mke wake akatabasamu na kusema “Ni mie ndio nilikusukuma”. Wewe ungemfanyaje kama ni mkeo? Anyway, “Nyuma ya kila mwanaume mwenye mafanikio kuna mwanamke anayemsukuma kufikia mafanikio”.🤣🤣🤣

UMEMUAGA mkeo unaenda kazini, ukapita kwa mchepuko wako, wakati unajimwaya-mwaya na mchepuko, mume wa mchepuko akagonga mlango, ikabidi ufichwe uvunguni mwa kitanda.
Wakati bado upo uvunguni ka mchepuko kakamuaga mume wake kwamba, kanaenda saloon, mume wa ka-mchepuko naye akaona ndo muda wa kuita mchepuko wake, akauita ukaja, wakajimwayamwaya kwa sana muda huo wee bado upo uvunguni. Mara mchepuko wako akarudi kutoka saloon, akagonga mlango, ikabidi mume wa mchepuko wako aufiche uvunguni mchepuko wake.
Kucheki hivi kumbe mchepuko wenyewe ndo mke wako uliyemuaga unaenda kazini, kwa hiyo wewe na mke wako wote mkawa mmefichwa uvunguni…Ukisikia vita ya tatu ya dunia, ndo hii sasa.