Karibu The bestgalaxy. Hapa unaenda kupata maaelezo yatakayo kufungua kidogo ubongo juu ya “Uzazi wa mpango. Uzazi wa mpango ni mpango au uamuzi wa mtu au watu katika kuzaa watoto .Lengo kuu la uzazi wa mpango ni kuruhusu wazazi kuchagua ni lini na idadi gani ya watoto wanataka kuwa nayo, kwa kuzingatia rasilimali walizo nazo zao, hali ya maisha, na malengo yao katika maisha. Kuna njia au hatua zinazochukuliwa na watu au jamii ili kudhibiti idadi ya watoto wanazozaa au kuepuka mimba zisizo tarajiwa.
Kuna njia mbalimbali za uzazi wa mpango na hapa chini tunaenda kuangalia njia 6:
Njia za uzazi wa mpango
1. Dawa za Kuzuia Mimba(Njia ya kisasa): Hizi zinaweza kuwa dawa za kumeza au sindano ambazo zinaweza kuzuia ujauzito. Mwanamke anaweza kwenda kwenye kituo cha afya akachomwa sindano ya kuzuia mimba au akameza vidonge vya kuzuia mimba.
2. Kondomu(Njia ya kisasa): Kondomu ni mipira amayo huvaliwa katika tendo kuzuia mimba na kujikinga dhidi ya magonjwa ya zinaa. Mwanaume kuvaa kondomu katika tendo kunaweza fanya mwanamke asipate mimba. Lakini pia kuna kondomu za kike ambazo mwanamke anaweza vaa kumsaidia asipate mimba.
3. Vitanzi(Njia ya kisasa): Hivi ni vifaa vinavyowekwa ndani ya mfuko wa uzazi na huweza kuzuia mimba kwa muda mrefu.
4. Vipandikizi(Njia ya kisasa): Hivi ni vijiti vyenye ukumbwa kama njiti ya kiberiti ambavyo huwekwa katika mkono wa mwanamke kwa lengo la kuzuia mimba.
5. Upasuaji wa Kuzuia Mimba(Njia ya kisasa): Kwa wanaume, upasuaji wa kufunga mirija ya uzazi (vasectomy) unaweza kutumika kuzuia mimba. Kwa wanawake, upasuaji wa kufunga mirija ya fallopian (tubal ligation) ni njia nyingine.
6. Kufuatilia mzunguko wa hedhi au kutumia kalenda(Njia ya asili): Pia unaweza zuia mimba zisizotarajiwa kwa kufuatilia mzuguko wa hedhi kisha kuepuka kufanya tendo katika siku za hatari.
Uzazi wa mpango unaweza kusaidia kudhibiti idadi ya watoto na kuboresha afya na ustawi wa wazazi na familia kwa kutoa fursa ya kuchagua lini na jinsi ya kupata watoto. Lakini unapawa kutambua kuwa njia nyingi za uzazi wampango za kisasa zimekuwa zilieta madhara kwa watumiaji. Ni vema kufika katika kitua cha afya na kupewa muongozo zaidi juu ya njia za kisasa za uzazi wa mpango. Njia ya Kufuatilia mzunguko wa hedhi au kutumia kalenda ni njia ya asili isio na madhara kwa mtumiaji ila ina hitaji umakini sana.