Tag Archives: UTAMU WA JUMLA

UTAMU WA JUMLA 02 (Simulizi ya Maandishi)


Wakati nakusanya nguo ghafla mlango ukagongwa “Ngo ngo ngo” na sauti ya Jimmy akisema “Oi wewe”.
Niligundua ni Jimmy nikasema “Oya… Umerudi sasa haha” akawa anasukuma malango huku anasema “Ahaha
nimekuja na shemeji yako huyu” huku akimruhusu mtu aingie. Mimi nikatupa macho kuangalia mtu anaeingia ni
nani, nikakuta ni Zuwena amevaa nguo nyeusi fupi alafu inaangaza kiasi ambacho baadhi ya sehemu zake za mwili
zinaonekana na Jimmy alikua anamshika kiuno alipokua akiingia ndani. Nilipomuona Moyo wangu ulidunda kwa
mshtuko “Nduh” na nikahisi kama kuishuwiwa nguvu hivi…
Nikaona bora nijikaze tu ila nisiwe na maneno mengi hapo maana nawezajikuta nimesema kitu kibaya. Nakumbuka
nilimsalimia Zuu kama ndio mara ya kwanza nakutana nae hapo. Na yeye alikua ananisalimia kama sijawahi ongea
nae kwa ukaribu. Baada ya kuwasalimia nikatoka nje na nguo nilizokusanya ili kuzifua na kuwaacha mule ndani.
Nilivyotoka tu, Jimmy aliufunga mlango ili mtu yoyote asiingie mule ndani na mimi sikua na hofu juu ya hilo
maana vitu vyote ambavyo vilikua vinahitajika ili nifue vilikua vinapatikana nje.
Nilichukua ndoo nikachota maji, nikavuta kiti pembeni ya chumba nilichukua nakaa alafu nikaanza kufua. Kichwa
changu muda huo kilikua hakipo sawa kabisa maana nilikua naona rafiki yangu Jimmy anaenda kula tunda la mtu
ninaempenda na kwakua sikumwambia basi nikaona acha niendelee kuumia moyoni tu kimya kimya huku nikifua
japo bado kichwani nilikua najiuliza “Amempataje huyu kiiumbe? Mbona sijawahi waona wakiwa karibu? Dah yani
Zuu nae inaonekana hanikubali kabisa maana aliponiona hata hakushtuka.ila namtamani sana huyu mwanamke”.
Wakati naendelea kufua ghafla nikaanza kusikia visauti toka ndani kupitia kidilisha kilichokua karibu na nilipokua
nafua. Mara ya kwanza nilikua nimevipuuza visauti hivyo nikawa nahisi ni Jimmy na Zuu wanaongea kawaida
kimahaba lakini baadae nikaanza kusikia sauti inaongezeka na inakua kama Zuu anabishana na Jimmy mule ndani.
Hali hiyo ilinifanya niache kufua nisogee zaidi kwenye dilisha nijue wanabishana nini humo ndani badala ya kuanza
mambo yao. Nilipotega sikio nikasikia Zuu akiwa na sauti kama amechukia hivi akisema “Usiniguse kwanza, Mimi
nataka uniambie ukweli kwanza… umesema hapa ni kwa nani?” Jimmy akawa anajibu “Kama nilivyokwambia
Zuwena, kwa rafiki yangu hapa… Kwanini unakua mgumu kunielewa” Zuu akajibu “We endelea kunidanganya tu, si
umeniona mimi mtoto mdogo? hiyo michezo naijua, usiniguse”. Nilimsikia Jimmy akisema “Tatizo huniamini…
Kama nilivyokwambia, mimi nakaa kule ila funguo kuna mtu ameondoka nayo ndio maana nimekuja kwa rafiki
yangu huku. Hata kodi ya hapa huwa nalipa mimi, huyo jamaa alietoka hapo nje huwa ni kama namsaidia tu maana
hayupo vizuri kipesa. Alafu nilishakwambia habari ya huyo jamaa hapo… Sasa kinachokufanya ubadilike sijui ni kitu
gani”. Nikakuta Zuu anamuuliza Jimmy “Yani umeniona mimi mjinga sana bora hata ungekua mkweli tu… Mimi
naona humu ndani kuna nguo zako ninazo zijua na hata viatu alafu bado unasema hapa sio pako. Sawa, kwasasa
naomba uniache niondoke maana nimekuchoka”. Mimi hadi hapo nikaanza kupata picha kidogo ya kinachoendelea
humondani. Kwa maongezi yale nilio yasikia nikajua tu huenda Jimmy hadi amemfikisha hapo huyo mwanamke ni
baada ya kumdanganya sana na muda huo uongo wake uligundulika na jambo hilo lilpelekea mpaka huyo
mwanamke kutaka kutoka humo ndani.
Basi nikatoka pale dilishani nikarudi nilipokua nafua ili kama wanatoka wasijenikuta pale na kugundua nilikua
nawasikiliza. Baada ya dakika kama tano hivi nikasikia mlango unafunguliwa, wakatoka kama wapo vizuri tu japo
Zuu alikua na sura inayoonesha amekasirika na Jimmy alikua ni kama anaaibu kiasi kutokana na kilicho mtokea.
Nakumbuka waliniaga pale alafu wakawa wanaondoka na kuniacha nikwa nafua. Kiukweli siku walivyokua
wanaondoka waliniacha nikiwa na furaha sana moyoni kwangu kutokana na kutofanikiwa kufanya mambo yao
humo ndani. Nilikua napenda sana Jimmy afanikiwe kwenye mipango yake kwasababu ni rafiki yangu lakini kwenye
Suala la kumkamata Zuu, sikulipenda maana mimi pia nilikua nampenda sana Zuu japo sikumwambia.
Nilipokua nikiendelea kufua na kufurahia tukio lililotokea, gafla nikaanza kufikilia tena yale maneno nilioyasikia
dilishani na kuanza kuwaza “Inamana Jimmy amemwambia Zuu mambo mengi kuhusu mimi alafu mimi sijui… Dah
na najua hawezi kuongea ukweli au jambo la kunisifu, lazima alikua ananiponda ili aonekane ni mtu wa juu”. Na kweli baada ya tukio hilo chuoni kulikua na watu wengi wajua juu ya Jimmy na Zuu. Zuu alimchafua sana jimmy
hapo chuoni kwa kuwaambia watu vitu alivyokua anaambiwa na Jimmy. Kulikua na maneno mengi ya Jimmy
kujigamba kwa Zuu ambayo yalienea kwa watu pale chuoni ila moja ya vitu nilivyosikia mwenyewe Jimmy
alimwambia Zuu ni kwamba ananilipia kodi tu lakini hakai na mimi. Jambo hili liliniumiza sana maana nilihisi
huenda ndio chanzo cha Zuwena kunipuuza nilipokua namtafuta. Lakini kwakua Jimmy alikua ni rafiki yangu,
nilipuuzia na tukaendelea kuwa pamoja hapo chuo.
Pamoja na yote yaliotokea, sikuwahi mtafuta tena Zuu. Nilikua nimetulia na mpenzi wangu sara na alikua anasema
ananipenda kweli. Niliweka moyo wangu wote hapo huku nikiwa na soma sana lakini nilivyozama sana katika penzi
lake, nikakuta Sara anaanza kunibadilikia tena. Ghafla tu alianza tabia ya kutonitafuta mpaka nimtafute na hata
nikimtafuta anaweza sema atanitafuta lakini hafanyi hivyo. Hali hii iliniumiza sana maana nilikua najua kwamba ni
dalili ya kuwa Sara amepata mwanaume mwingine. Nilichanganyikiwa sana kipindi hicho mpaka masomo nilikua
naona hayaeleweki. Hakuniambia kwamba tuachane ila tabia yake ilionesha kuwa tayari ameishaniacha ila ni mmi
tu ndio sijui. Nilifuatilia nikakuta kumbe kapata Mwanaume mfanyakazi na anamiliki mpaka gari. Niliwahi shuhudia
kwa macho yangu Sara akiingia kwenye gari baada ya kutoka chuoni. Niliumia sana na nikaamua kukubaliana na
uhalisia kuwa nimeachwa ila moyoni nikajisemea “Siku nikipata ajira na kuwa na hela nitawakamata sana
wanawake… yani nitawala sana. Ntanunua gari na ntakuwa na wanawake kila kona… Siwezi mpa moyo wangu
mwanamke auchezee kama hivi, ntakuwa nao wengi ili niwachezee wao… Pesa nyingine nitakua natumia na
marafiki tu maana ni bora marafiki kuliko kuwa na mpenzi”.



Basi siku zilisonga hapo chuo mpaka tukamaliza na kurudi nyumbani Tabora. Nakumbuka mimi na Jimmy tulirudi
nyumbani na tulikua tunaishi kwa wazazi wetu. Kwetu na kwakina Jimmy ni karibu sana. Kwao ni nyumba ya tatu
kutoka kwetu. Tulivyokua wadogo hatukua pamoja, familia yake ilihamia hapo kipindi nipo sekondari na yeye
alikua sekondari na tulipokutana tukawa marafiki mpaka tulipoenda chuo pamoja na kurudi pamoja. Tulivyorudi
tulikua mabishoo sana na tunapendeza juu mpaka chini kila muda na masimu yetu makubwa ya kupalasa.
Baada ya miezi kadhaa ishu ya chuo tukawa tumeimaliza kabisa tukawa tunamawazo ya kupata Ajira kichwani
mwetu kutokana na vyeti tulivyopata. Lakini tulianza kuona kama neno “ajira” linaongelewa kwenye ma TV alafu
hatuzioni mtaani na hata wakiziongelea kwenye TV mara nyingi wanasema “changamoto ya upungufu wa ajira”.
Jambo hili lilinifanya nijiulize “Inamaana pamoja nakuwa na vyeti Ajira naweza kupata au nisipate? Duh!”. Siku moja
nikakuta tu ghafla jamaa yangu Jimmy kasafili. Na hakuniambia kwamba anasafiri mpaka nilipomcheki kwenye simu
“Wewe uko wapi mwanangu, mbona haujaonekana leo” ndio akaniambia amerudi Dar. Mimi nikamuliza “Mbona
hukuniambia rafiki yangu?” akasema “Hahaha ilikua ni ghafla mzee, Nitakucheki tutaongea vizuri”. Mh Mimi
nikajua atanicheki kweli lakini haikua hivyo, siku zilizidi kusongea tu hanicheki na hata nikimcheki ananiambia
“ntakucheki”. Baadae nikakata tamaa kabisa ya kumtafuta maana nilikua najua nimuongo hivyo ukimsikiliza
unapoteza muda nikakata mawasiliano nae. Kiukweli baada ya Jimmy kuniacha kule Tabora nilianza kuwa na
mtizamo tofauti kidogo juu ya Marafiki, nilikua kama nimegundua kuwa marafiki hawajashikana na maisha yangu,
wanaweza ondoka muda wowote.
Nikaendelea kukaa pale nyumbani bila mafanikio ya kupata ajira na wazazi nilikua naona hawaniwazi tena kwenye
mambo ya pesa, wao walikua wapo tayari walipie mamilioni sehemu nisome au nipate kazi kuliko kunipa mimi pesa
ya hivi hivi tu. Kadri siku zilivyo zidi kusonga nilianza kuchakaa kimuonekano kutokana na kukosa hela. Wakati
nakuja kutoka chuo nilikua napendeza kiasi kwamba nikikutana na mtu ananiuliza “Hiyo sendo uliovaa mguuni
shingapi?” nikimwambia bei anasifia “Dah nzuri sana hiyo sendo!” lakini mambo yalibadilika kiasi kwamba
nakutana na mtu ananiangalia juu mpaka chini alafu anauliza “Hiyo gundi ni supagruu?” namuuliza “Wapi? hapa
kwenye sendo?” Anajibu ” ndio, hapo mguuni” namwambia “Ndio ni yenyewe” ananijibu “Gundi nzuri sana
hiyo!”. Kiukweli nilichakaa sana na hali hiyo ilinifanya niwe na kiu ya kufanya chochote nipate ajira na ilikua kama
bahati hivi nilikutana na tangazo ambalo liliingia kwenye simu yangu kama ujumbe. Ujumbe huo niiliona kama fulsa
hivi kwasababu ulikua unaeleza kwamba kuna kampuni inaenda kuanzishwa na kabla ya kuanzishwa Dar inatoa
mafunzo kama miezi sita hivi na waliopata mafunzo ndio wataajiriwa. Kulikua kuna namba zao pale kwenye ujumbe
ili kupata maelezo zaidi…

INAENDELEA….

Hii ni simulizi ya UTAMU WA JUMLA ilio katika maandishi. Ina uhusiano kidogo na Simulizi ya SUKARI YA DADA na MZIGO WA WAKUBWA. Inapatikana katika Sauti pia. Inavipande 11.

KUMBUKA: Hairuhusiwi kusomwa na mtu mwenye umri chini ya miaka 18.

Ukihitaji simulizi zote 3, Njoo WhatsApp

UTAMU WA JUMLA 01 (Simulizi ya maandishi)

Tulikua tunakaa na wazazi wangu Tabora na nilimaliza shule ya sekondari kule alafu nikaja kusoma mpaka chuo Dar es salama. Nilikua nasomea mambo ya biashara huko chuo na nilienda chuo baada tu ya kumaliza sekondari. Nilipokua chuo nilikua na rafiki yangu mmoja anaitwa Jimmy. Huyu jamaa tulikua marafiki sana kwasababu tulikua tumetokea sehemu moja. Na yeye alikua ametokea Tabora. Alikua ni muongo jamaa huyu ingawa mimi nilimzoea lakini alikua muongo sana. Pamoja na kwamba nilikua rafiki yake lakini alikua hawezi kuniambia vitu vya ukweli. Ilikua ni kawaida kwake kukwambia “Nisubiri nakuja” na hasije, “Niazime hela nitakurudishia” na asirudishe au “Nipo Sehemu flani” na asiwepo hiyo sehemu. Lakini alikua bado ni rafiki yangu na tulikua tunakaa chumba kimoja kilichokua pembezoni kidogo ya chuo. Uongo wa Jimmy ulikua kunamda unaniudhi mimi na hata watu wengine lakini kwake ulikua na faida. Alikua na anakamata sana madada wa pale chuoni. Alikua anapendeza kwa nguo za kuazima azima kwa watu na watu wengi hapo chuoni walikua wanahisi anatoka sehemu yenye hela sana lakini kiukweli alikua ananitegea sana kwenye swala la pesa maana kwao walikua hamampi hela sana kama ninavyopewa mimi. Kwakua alikua ni rafiki ilikua sio shida.

Wakati naanza chuo nilijikuta navutiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na dada mmoja mzuri na alikua anafahamika sana kwa uzuri hapo chuo. Moyo wangu ulimpenda huyo dada na sikuwahi mwambia hata rafiki yangu Jimmy kuhusu huyo dada. Alikua anaitwa Zuwena na watu wanamuita “Zuu” badala ya kulitaja jina lake lote. Alikua ni dada flani hivi mweusi alafu anaumbo zuri sana. Alikua amebalikiwa sura nzuri na nyuma alikua amejaza sana kiasikwamba alikua akitembea unajikuta unavutiwa kumuangalia jinsi mizigo inavyojitikisa.

Nilitamani sana kumwambia hisia nilizo nazo juu yake lakini tulikua hatuna ukaribu nae kabisa na pia nilikua na uwoga. Zuu alikuana marafiki wengi warembo kama yeye wanaomzunguka mara kwa mara na mmoja ya marafiki zake alikua anaukaribu kidogo na mimi. Huyo rafiki yake alikua anaitwa Sara na alikua ni mpole kidogo kuliko marafiki wengine wa Zuu. Ukaribu wangu na Sara ulikua wakusalimiana na kuongea maneno mawili au matatu tu kutokana na kwamba tuliwahi kaa karibu kwenye mthihani wa kujipima akaniomba nimsaidie kidogo, nikamsaidia.

Basi mimi bila kuwaza mbali nikaona bora niongeze ukaribu na Sara ili nipate nafasi ya kuwa karibu na Zuu na kwakua zuu ni rafiki wa Sara basi nikaona huenda nitakua najua mambo mengi ya Zuu kupitia kwa Sara. Niliongeza ukaribu na Sara kasikwamba tulikua tunawasiliana kila siku na ananitafuta kila muda tukiwa chouni, kwenye simu au nje ya chuo. Ukaribu huo ulileta matokeo ambayo sikuyatarajia maana ilifikia kipindi nataka kumuuliza Sara mambo ya Zuu lakini kila nikijaribu kuingizia mada za Zuu au mwanamke mwengine, anazutupilia mbali alafu anakua kama anachukia hivi. Hali hiyo iliendelea mpaka kunasiku moja hivi nilikua nimekaa chuoni nimejitenga najisomea nikakuta Sara amekuja kukaa na mimi. Ni kawaida yake kufanya hivyo. Tulipiga stori hapo za uongo na ukweli ila katikati ya stori nikashangaa kumuona Sara kaganda tu ananiangalia usoni kwa macho ya kulegea bila kuongea kitu. Mimi kuona hivyo nikasema kwa kisauti cha chini “We Sara… Ndo nini hivyo?… wewe unaniangaliaje hivyo?… wewe” nikakuta bila kuyayumbisha macho yake anasema “Niangalie vizuri machoni’. Nilivyosikia hivyo nikaacha kumuangalia macho, nikaangalia kulia na kushoto kwanza kama kunamtu anatuangalia muda huo maana macho ya Sara yanaonesha ni mtu aliechoka kuzificha hisia zake juu yangu na yupo hapo kunionesha jinsi anavyo hisi. Niliona amna mtu anaetuangalia muda huo, nikayarudisha macho kwa Sara nikasema “Macho yako mbona kama… Mbona kama yako vizuri tu ila yanakua kama unausingizi hivi”. Akaniambia “Endelea kuniangalia tena alafu niambie umegudua nini”. Mimi nikimuuliza “Macho yanakuuma?” akakataa kwa kutikisa kichwa. Nikatulia kidogo nikamuuliza “Unanipenda?” nikakuta anakubali kwa kutikisa kichwa chake huku akiwa na vimacho kama anataka kudondosha vimachozi hivi. Nikamwambia “Ah sasa kumbe ndio hicho kinakufanya uniangalie hivyo… Na mimi nakupenda… nipe mkono wako nikwambie kitu”. Basi nikaona Sura yake inatabasamu kubwa sana baada ya mimi kusema hivyo. Tulishikana mikono tukaanza kuongea vitu vya upendo upendo pale tukiwa na kauwoga uwoga maana sehemu hiyo ilikua sio sehemu sahihi kwa watu kushikana shikana. Tulitaka kukutanisha midomo lakini sehemu hiyo haikua inaruhusu sisi kufanya jambo hilo. Kwanzia siku hiyio mimi na Sara tulikua wapenzi ila kiukweli mimi moyoni mwangu bado nilikua nampenda Zuu na sio Sara. Pamoja na kwamba nilikua kwenye mahusiano na Sara na ananipa raha kila nikizihitaji lakini bado nilikua naiwinda nafasi ya kuwa na Zuu.

Kunasiku nilipata nafasi ya kuongea na Zuu kidogo akiwa pekeyake na nikaitumia kumuomba namba ya simu tu. Siku hiyo hiyo nikamcheki kwenye simu mida ya jioni. Nilijitambulisha kuwa ndie niliemuomba namba akasema amenikumbuka ila hatukuongea sana akasema “Subiri kidogo nitakushtua, kunakitu nafanya”. Nilisubiri sana nikaona mpaka naingia kulala hajanitafuta. Sana sana nilikua nikisumbuliwa na Sara tu kwenye simu akidai nimebadilika nimekua kama simpendi hivi. Nilimpuuza Sara nikaona nijaribu kumtumia ujumbe Zuu ili kama amesahau akumbuke lakini nikakuta hajibu mpaka asubui inafika.

Siku iliofuata nikaenda chuo na nikatafuta sana nafasi ya kuongeanae na bahati nzuri niliipata tena. Nakumbuka nilimuona amekaa pekeake sehemu anaandika. Nilivyomuona nikaangalia kulia na kushoto kuhakikisha Sara hayupo maeneo yale alafu nikamfuata. Alikua amependeza alafu nguo ya juu aliokua ameiva ilikua imeacha kinafasi kinachoonesha tunda za kifua chake zikiwa zimebanana kiasikwamba nilikua kila nikizitupia macho mapigo yangu ya moyo yalikua yanaongezeka. Nipofika nikasema “Mambo vipi Zuu” akaacha kuandika akaniangalia akanijibu “Safi tu, Mzima?” mimi nikamwambia “Nimekuona toka kule upo bize sana kuandika, unaandika nini?” akasema “Mh kunavitu nahamisha toka kwenye daftari hili hapa” nikasema “Anha sawa, nimekuja kukusaidia kuandika”. Kusikia hivyo akasema “Hahaha, namaliza mwenyewe hizi usihofu banaa… Nimeanza kuandika tangu jana, leo namalizia tu” mimi nikasema “Haya” alafu nikasema tena “Alafu jana nimekutafuta ukasema utanitafuta lakini hukunitafuta” nikakuta ananijibu “ah hahaha hivi nilikwambia nitakutafuta? dah nilisahau kabisa alafu jana tulivyoongea tu, nikaweka simu kwenye chaji… nimekuja kugusa leo wakati nakuja huku na nimekuta SMS nyingi bado sijasoma ila tutaongea vizuri leo, nitakutafuta”. Alivyoniambia hivyo nikamwambia “Sawa” tukapiga stori kidogo sana alafu nikamuacha pale aendelee kuandika.

Kiukweli Zuu japokua ilikua tukikutana tunaongea lakini niligundua ni mtu anaenidharau sana na ananikwepa maana hata siku hiyo bado hakunitafuta na hata nilipomtafuta, nikawa sijibiwi chochote. Jambo hili lilinifanya mpaka niwaze “Huenda Zuu anajua ninachotaka kwake na anajua ninamahusiano na rafiki yake Sara au tu anaona simuwezi… kwanza kwa muonekano wake tu anaonekana anataka watu wakubwa wenye pesa za kutosha”. Nilivyoona ananisumbua sana akili yangu nikaona isiwe taabu, acha nitulie na Sara tu maana kipindi hicho Zuu alifanya nimpuuze sana Sara. Niliacha kumfuatilia Zuu, nikajikita zaidi kwa Sara lakini nilikua bado natamani niwe na Zuu kimapenzi kama ningepata nafasi.

Baada ya kama wiki moja hivi toka niache kumfuatilia Zuu nilikutana na kitu ambacho sikukitegemea kabisa. Ilikua ni jumamosi mida ya saa 9 mchana nilikua nipo kwenye chumba tunachokaa na rafiki yangu Jimmy. Muda huo Jimmy alikua hayupo, aliondoka toka asubui akiwa amependeza sana na hakuniambia anakoenda na wala sikumuuliza maana hata nikimuuliza huwa haongei ukweli. Kuliko kukaa tu humo nikaona bora nikusanye nguo zangu chafu zilizokua zimezagaa chini zimejichanganya na za jimmy nifue. Wakati nakusanya nguo ghafla mlango ukagongwa “Ngo ngo ngo” na sauti ya Jimmy akisema “Oi wewe”. Niligundua ni Jimmy nikasema “Oya… Umerudi sasa haha” akawa anasukuma malango huku anasema “Ahaha nimekuja na shemeji yako huyu” huku akimruhusu mtu aingie. Mimi nikatupa macho kuangalia mtu anaeingia ni nani, nikakuta ni Zuwena amevaa nguo nyeusi fupi alafu inaangaza kiasi ambacho baadhi ya sehemu zake za mwili zinaonekana na Jimmy alikua anamshika kiuno alipokua akiingia ndani. Nilipomuona Moyo wangu ulidunda kwa mshtuko “Nduh” na nikahisi kama kuishiwa nguvu hivi…

INAENDELEA…

Hii ni simulizi ya UTAMU WA JUMLA ilio katika maandishi. Ina uhusiano kidogo na Simulizi ya SUKARI YA DADA na MZIGO WA WAKUBWA. Inapatikana katika Sauti pia. Inavipande 11.

Tutumie ujumbe WhatsApp upate simulizi zote

UTAMU WA JUMLA 🔞 (Simulizi ya sauti)

Simulizi ya UTAMU WA JUMLA ni simulizi yenye uhusiano kidogo na simulizi ya SUKARI YA DADA. Unaweza sikiliza simulizi hii ukiwa ndani ya The Bestgalaxy Bure kabisa na pia unaweza ipakua na kufurahia kwenye simu au kifaa chako. Sikiliza simulizi hii katika mazingira tulivu yatakayo ruhusu kuielewa kirahisi.

Katika kuisikiliza ukiwa kama msikilizaji hakikisha unazingatia umri maana simulizi hii haitakiwi kusikilizwa na mtu mwenye umri chani ya miaka 18.

kama umebonyeza na inachelewa kuanza basi huenda ni tatizo la mtandao wako. Jaribu mara kadhaa kwa kusubiri.

Sehemu ya 1
Sehemu ya 2
Sehemu ya 3
Sehemu ya 4
Sehemu ya 5
Sehemu ya 6
Sehemu ya 7
Sehemu ya 8
Sehemu ya 9
Sehemu ya 10
Sehemu ya 11 (mwisho)

Kupata taharifa ya simulizi mpya na mambo mwengine, hakikisha unatembelea The bestaglaxy kila mara na pia unaweza jiunga kwenye group letu la Whatsapp Bure.