Tag Archives: Swahili tech

Sehemu za kuuza bidhaa zako zilizotumika Mtandaoni (Vitu used)

Unaweza kuwa hata sio mtu unaefanya bishara kama sehemu kuu ya kupata pesa lakini ukawa na vitu vyako unavyotamani kuuza. Vitu hivi vinaweza kuwa ni Simu yako ya zamani, PC, Tv, Redio na hata magari. Watu wengi wana vitu kama hivyo na wanatamani kuviuza lakini kwakua sio watu waliojikita kwenye bishara basi wanashindwa kupata sehemu ya kuviuza hivyo vitu na hata muda wa kufanya hivyo wanaweza kosa.


Teknolojia kupitia mtandao (internet), unamuwezesha kila mtu mwenye bidhaa anayotaka kuiuza akutane na watu wanaweza kununua bidhaa mtandaoni. Kupitia simu yako yenye uwezo wa internet au kifaa kingine cha internet, utaweza ukauza vitu vyako used kwa watu wengine. Njia ya kuuza vitu used kupitia mtandao, inaweza kuokoa muda wako muuzaji kwa kufanya kitu au bidhaa used unayouza ionekane kwa watu wengi wanaweza kuinunua huku ukiwa unaendelea na shudhuli zako nyingine.

Kwenye ukurasa huu, The bestgalaxy tumekuandalia orodha ya app chache zinazokuwezesha kuuza vitu used mtandaoni kupitia simu yako. Katika orodha hii, hatujaangalia upande wa Dunia, ila tumengalia katika upande wetu huu tu hivyo usishangae kutoziona platform kama eBay na Amazon.

Mambo ya kuzingatia unaponunua bidhaa mtandaoni (Online) BONYEZA HAPA>>>

App za kuuza bidhaa zako zilizotumika Mtandaoni (Vitu used)

Facebook

Kuna mtu anaweza jiuliza “Facebook inakujaje kwenye orodha ya app za kuuzia vitu used?” hebu tuanze na hili. Facebook inaingizwa kwenye orodha ya app za kuuzia vitu used kwasababu inakipengele kiitwacho “marketplace”. Kipengele cha Facebook marketplace kinakuruhusu mtumiaji wa Facebook kuuza na kununua bidhaa, ikiwemo used. Ukiwa na akaunti ya Facebook, utaweza kuweka picha na maelezo ya kitu unachouza pale alafu wanunuzi wakakutafuta kwaajili ya kununua. Zamani walikua wanaruhusu kuweka hadi namba ya simu lakini kwasasa hawaruhusu kwasababu za kiusalama.

Kupatana

Kupatana ni app rasmi kwaajili ya kuuza na kununua bidhaa mtandaoni. Mtu unaweza itumia kuuza vitu na pia unaweza itumia kununua vitu kutoka kwa wengine. Inatumika na watu wengi hivyo inaweza kuwa rahisi kumpata mnunuzi wa bidhaa yako used au kupata mtu anaeuza bidhaa unayohitaji. Inaruhusu kuweka picha na maelezo ya bidhaa yako ili anahitaji aelewe vizuri unachouza kabla hajakutafuta.

Jiji

Hii JiJi ni app nyingine kubwa ya kuuza na kununua bidhaa ambayo unaweza itumia kuuza vitu vyako used. Haina watumiaji wachache, wengi tu huuza na kununua vitu used kupitia app hii hivyo utakua sio mtu wa kwanza kuuza vitu used ndani yake. Ukiweka picha, maelezo ya bidhaa yako na mawasiliano yako vizuri, unaweza pata mnunuzi ndani ya app hii bila kupoteza muda sana maana watumiaji wapo wengi. Ni nzuri zaidi kwenye bidhaa za kielekroniki na magari alafu pia imepewa nyota 4.5 kati ya nyota 5 katika playstore.

Tisitano

Tisitano pia ni app kwaajili ya kuuza na kununua bidhaa. Inawakutanisha wauzaji wa vitu au bidhaa na wanunuzi wa vitu au bidhaa hizo. Inaweza tumika kuuza vitu vyako used kupitia simu yako ya mkononi bila kupoteza muda wako sana. Unaweza iweka bidhaa yako ndani ya app hii na ikaonwa na watu wengi kama app ya Kupatana au JiJi. Kuna maelfu ya watu huitumia app kwenye maswala ya kuuza na kununua vitu mtandaoni.

Mwisho, tunapenda kukukumbusha umakini unapouza na kununua bidhaa mtandaoni kupitia app hizi. Fahamu kuwa unaweza kutana na matapeli au watu wenye nia mbaya pia. Lakini hii isikuzuie kufurahia njia hii ya kuuza vitu used mtandaoni maana watu kama hawa wapo pia kwenye maisha yetu ya kila siku. Endelea kufuatilia The bestgalaxy kwa mambo mengine zaidi.

Jinsi ya kuongeza ubora wa picha zako za zamani kwenye simu

Unaweza piga picha yenye ubora kwenye simu yenye kamera nzuri lakini baada ya muda au kipindi flani ukawa na picha hiyo uliopiga ikiwa inaonekana haina ubora. Picha hiyo ya zamani unawezaona haina ubora baada ya kupitia kwenye mitandao ya kijamii na michakato mingine inayopunguza ubora wa picha. Mbali na hayo, baada ya kupata simu yenye kamera inayotoa picha zenye ubora zaidi, unaweza anza kuona picha ya zamani haina ubora.

Nikawaida watu kuwa na picha zao wanazoziona hazina ubora na kama ni mmoja watu hawa, hapa The bestgalaxy tunakupa mwanga kuhusu kuziongeza ubora. Unapokua na picha zisizo na ubora, kumbuka kuna huduma zinazokuwezesha kuongeza ubora wa picha. Huduma hizi ni software ambazo nyingi huiongezea picha ubora bila kukuhitaji ufanye vitu vingi. Zimewezeshwa na AI hivyo ni rahisi kutumia kiasi ambacho mtu yoyote anaweza tumia kuongeza ubora wa picha zake.

AI ni nini na inaleta matokeo gani katika Ulimwengu? BONYEZA HAPA>>>>

Jinsi ya kuongeza ubora wa picha zako za zamani kwenye simu za Android

Kwenye simu za Andoid kupata huduma ya kuongeza ubora wa picha, unaweza tumia app iitwayo UpFoto. App hii inatumia internet ila inaweza pandisha ubora wa picha yako bure na rahisi sana kuitumia. Ukihitaji kujaribu kwenye picha zako zilizopoteza ubora, fuata maelezo yafuatayo;

 

  • Nenda katika Playstore na uipakue app iitwayo UpFoto kwenye simu yako.
  • Fungua, chagua Lugha ya “English” alafu bonyeza “Start” kwenye ukurasa utaopelekwa.
  • Baada ya hapo bonyeza kitufe cha “Try now” kwenye sehemu ilioandikwa “Enhance” kisha uchague picha unayotaka kuiboresha.
  • Baada ya kuchagua, Bonyeza kitufe kilicho andikwa “Enhance” ili kuanzisha mchakato wa kuboresha hiyo picha.  
  • App ikimaliza mchakato, utaletewa picha ilioboreshwa alafu utatakiwa kubonyeza kitufe kilichoandikwa “Save” ili kuiweka picha hiyo kwenye simu yako.

Kwa kufanya hayo utakua umefanikiwa. Lakini unapaswa kujua kwamba app ya UpFoto inamatangazo ambayo utakua unakutana nayo katika kufuata hatua hizo. Mbali na matangazo, app hii itakuomba access chache kwenye simu yako na utakua unabonyeza “Allow” kuiruhusu.

Kama ubora utakua haujakulidhisha unaweza chukua picha iliotoka kwenye app hiyo, alafu ukairudisha kwenye app kuiongeza ubora kwa mara ya pili.

Jinsi ya kutengeneza au kurekodi Nyimbo kwa kutumia Simu

Kutengeneza nyimbo kwa kutumia simu inawezekana? Ndio, inawezekana na nyimbo unayotengeneza kwa kutumia simu inaweza kuwa na mafanikio makubwa tu kama nyimbo za Studio rasmi. Kipindi cha nyuma, ukiwa kama msanii wa Muziki ilikua ni lazima uhusishe vyumba vya Studio rasmi vinavyomilikiwa na maproduser ili kufanya mazoezi ya nyimbo na kurekodi nyimbo zako. Lakini kwa sasa, hakuna ulazima sana wa kwenda huko kama hauna uwezo. Unaweza tumia simu yako ya mkononi kufanya mazoezi ya kurekodi nyimbo zako na hata kurekodi kabisa ukiwa nyumbani tu.

Jinsi ya kutengeneza au kurekodi nyimbo kwa kutumia simu

Unaweza tengeneza au kurekodi nyimbo iliokamilika kwenye simu ila utatakiwa kuwa na app maalumu kwa kazi hiyo. App zipo nyingi na kati ya app hizo kuna app ngumu kutumia, pia kuna app rahisi kidogo zisizo hitaji mambo mengi kwenye kuzitumia. Moja ya app ambazo ni rahisi kutumia ni app iitwayo “Voloco”. Inapatikana katika Playstore kwa simu za Android na hata Appstore kwaajili ya watu wa iPhone au vifaa vya iOS kwa ujumla.

App ya Voloco inahusiana zaidi na kuweka Voco kwenye Beat. Unaweza ingiza Beat lako mwenyewe au ukadownload humo humo ndani Beat zilizotengenezwa na watu wengine. Ni ngumu kukuelezea kila kipengele cha app hii kwa maandishi ili uweze kuitumia ila tumejaribu kukuelezea hapa chini kwa msaada wa picha vitu vya muhimu kuvijua utakapo fungua app hii.

Kutengeneza nyimbo ni project na kwenye app hii kitu cha kwanza utakachotakiwa kukifanya ni kutengeneza au kufungua project mpya. Ukisha fungua project mpya unaweza weka Beat unalotaka kuliimbia kwenye project hiyo alafu ukaanza kurekodi sauti au voco zako. Uzuri ni kwamba Ina Autotune hivyo kunajinsi sauti au voco zako zinaboreshwa.

Unashauriwa kuvaa Earphone unaporekodi voco zako. Baada ya kumaliza kila kitu kwenye project hiyo, unaweza itunza project yako kwenye app hiyo.


Ukihitaji kuitoka kama audio za kawaida unaweza ingia kwenye project ulizo tunza alafu ukabonyeza vidoti vitatu vilivyo kwenye project yoyote unayoyahitaji alafu ukaugusa “Download” ili kuidownload nyimbo uliotengeneza iwe kwenye simu yako. Utakua na chaguo la kutunza iyo nyimbo kama Audio au video. Nyimbo yoko itakua tayari lkuisikiliza japo unaweza pia kuipitisha kwenye software nyingine ili kuiweka kwenye ubora zaidi au kuibadilisha kuwa mp3 kama utahitaji.

Jinsi ya kujiondoa kwenye post mbaya ulizoshirikishwa Facebook

Facebook inaruhusu kushirikisha mtu kwenye picha au post yako na huwa tunaita ku “Tag”. Mtu unaemshirikisha kwenye post yako anatakiwa kuwa ni rafiki yako wa Facebook. Kumshirikisha mtu ambae hamna urafiki kwenye Facebook haiwezekani kwa kumtag ila unaweza tumia kipengele cha kutaja (mention) kama njia ya kumshirikisha mtu.


Mtu unapo shirikishwa kwenye post kwa kipengele cha “Tag” na rafiki yako mmoja, marafiki zako wengine wanaweza pata taharifa kuwa umeshirikishwa kwenye post hiyo. Na endapo picha ulioshirikishwa itakua ni picha mbaya au usio taka kushirikiswa, Bado unauwezo wa kujiondoa.

Jinsi ya kujua kama akaunti yako ya Facebook ni Salama BONYEZA HAPA>>>

Jinsi ya kujiondoa kwenye post mbaya ulizoshirikishwa Facebook

Hapa chini tunaenda kukuelekeza hatua kwa hatua jinsi ya kujiondoa kwenye post waliokutag katika Facebook lakini hautaki kuhusishwa. Jambo zuri ni kwamba ukijiondoa, aliekutag hawezi pokea taharifa kuwa umejiondoa.
Ili mtu kugundua kuwa umejiondoa kwenye post aliokushirikisha itambidi azingatie vitu viwili. Cha kwanza ni idadi ya watu aliowashirikisha na Cha pili ni kuzingatia uwepo wa jina lako kwenye orodha ya watu aliowashirikisha. Watu wengi hawazingati jambo hili wanapo post picha na kushirikisha wengine katika Facebook japo.
Unaweza fuata hatua hii kuondoa Tag

  • Ingia katika Facebook na uende Katika post waliokutag
  • Bonyeza vidoti vitatu vilivyo upande wa pembeni katika post hiyo.
  • Chagua “Remove Tag” kwenye orodha ya chaguzi utazoziona.
  • Bonyeza”CONFIRM” ili kuthibitisha maamuzi yako ya kujiondoa kwenye post hiyo.

Ukisha fanya hivyo tu, post itakua uhusiano na wewe tena. Utakua umefanikiwa kujiondoa kwenye post hiyo na kama ilikua inaonekana kwenye orodha ya post zako, itaondolewa. Lakini kama ikitokea watu wengine au post mpya unaweza shirikishwa tena kama kawaida.

Akili bandia (AI) ni nini na inaleta matokeo gani katika Ulimwengu?

Katika vitu vikubwa na muhumu sana kwa binadamu wa sasa kuvijua na kufuatilia ni AI. “AI” ni kufupi cha “Artificial intelligence” na kwa kiswahili huitwa Akili bandia.

Akili bandia (AI) ni mfumo wa kompyuta kutumia algorithms na data ili kufanya maamuzi na kutatua matatizo kama vile binadamu. Kuna jinsi AI zinafanya kazi kama Akili ya banadamu japo hazipo sawa kufikia kiasi cha asilimia 100. AI ni kama ubongo au akili katika kompyuta kubwa.
Ai ni zao la Teknolojia ya mwanadamu. Upande mwingine tunaweza sema binadamu katika kukuza Teknolojia yake na kumfanya arahisishe maisha yake, ameweza kutengeneza kitu kinachofanya kazi kama Akili yake.

Teknolojia hii ya akili bandia kwasasa inawezesha magari kujiendesha bila dereva, robot kuwa na uwezo mkubwa wa kufanya baadhi ya mambo kama binadamu.

Mbali na hayo pia imefanya baadhi ya mambo yawe rahisi kwenye simu na vifaa vingine tunavotumia. Baadhi ya upande ambao Ai imehushwa sana kwenye simu zetu ni upande wa kupata taharifa, kuedit picha, video na kuiandika. Mambo yamekua marahisi sana kwenye upande huu kutokana Teknolojia ya AI. Vitu vingi vinavyo wezeshwa na Ai huwa vinakua ni virahisi kwa binadamu anaevitumia.

AI za kutengeneza picha kwa kuandika maneno BONYEZA HAPA>>>

Lakini jambo muhimu kutambua hapa ni kwamba AI au Akili bandia kwa sasa inamapungufu mengi sana japo bado imeizidi akili ya binadamu kwenye pande chache ikiwemo upande wa hesabu. Inasemekana kuwa Akili hii bandia itafika wakati itaizidi akili ya banadamu kwenye kila kitu. Jambo hili limezua mijadala mingi sana ikiwemo jambo la Ai kutugeuka binadamu ambalo tutaizungumzia kwenye makala ya “Miaka ijayo”.

Hapa chini the bestgalaxy tumekupa mwanga zaidi juu ya Teknolojia hii ya Ai inavyoleta matokeo chanya katika ulimwengu wetu.

Akili bandia (AI) inaleta matokeo haya chanya katika Ulimwengu

Ai katika Utafiti na Maendeleo.

AI inawezesha na kuongeza kazi kasi ya uvumbuzi na maendeleo katika sekta mbalimbali kama vile, nishati, na teknolojia mpya. Kuna mambo mengie ambayo IA inaweza kuyafanya kwa haraka na jambo hili ni zuri maana tunaweza ongeza Kasi ya mambo tunayofanya katika Utafiti na maendeleo kwa kusaidiwa Ai.

Akili bandia katika uchumi na Biashara.

Kwa sasa, Kampuni zinatumia AI kuboresha mchakato wa uzalishaji, kuboresha huduma kwa wateja, na kufanya maamuzi ya biashara kulingana na data sahihi wanazo pata kupitia AI.

AI katika Afya.

AI inaweza kutumika kuboresha na kirahisisha uwezo wa utambuzi wa magonjwa na kutoa matibabu. Kuna projeti za robot zilizowezeshwa na ia kutoa ushauri juu ya magonjwa au kutumia kwenye mambo mengine ya kiafya. Inasemekana kuwa AI inaweza fikia mpaka kipindi ambacho mtu hataitahi kuonana na daktari moja kwa moja maana mambo mengi madogo madogo ya kiafya yatakua yanaweza shugulikiwa na AI.

Usalama.

Katika upande au sekta ya usalama, AI inaweza kutumika kwa kuimarisha usalama ulimwenguni. AI inaweza rahisiha zaidi katika kufanya ulizi wa maeneno mbali mbali yanayo yenye kamera kwa kutambua na kutoa halifa pale mambo mabaya yanapotokea. Mbali na jambo hilo, kugundua vitisho au uhalifu mtandaoni, na kuboresha mifumo ya usalama wa kitaifa ni katika ya matokeo ya AI.

Ai katika Usafiri.


Maendeleo katika AI yameleta mambo mkubwa katika upande wa teknolojia ya gari. Kuna magari yanayojiendesha na yanatarajiwa kuboresha usalama barabarani na kusafirisha watu kwa ufanisi zaidi. Lakini gari hizi zinahitaji miundombinu ya kisasa ili kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Kwasasa unaweza kuwa umepata picha ya matokeo ya akili bandia katika Ulimwengu. Lakini jambo la muhimu kujua ni kwamba AI ina athari katika ajira. Kuna ajira ambazo zinaweza poteza kutokana na Al na pia kuna ajira zinaweza zaliwa. Usisahau fuatilia makala ya “Miaka Ijayo” inayoweza kukupa picha zaidi juu ya hili. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy.

Tofauti kati ya Simu za Waterproof na simu za Water resistance

Linapokuja swala la simu kuingia maji, inaweza kuwa ni moja ya vitu watu hawapendi litoke hata kidogo. Ila kutokana na kazi tunazofanya au mazingira ambayo mtu upo, jambo hili linaweza tokea. Na simu ikiingia maji wote tunajua kinachoweza kutokea ni kuharibika kwa simu pamoja na kupoteza vitu vya muhimu vilivyo kwenye simu.
Ili kuzuia jambo hilo lisitoke, Makampuni ya simu huwa yanatoa simu ambozo zinasifa ya kuzuia maji kuingia kwenye simu. Simu hizi mara nyingi hutangazwa kuwa ni “Waterproof” au “Water resistance”. Na watu wengi wakiwa wanataka kununua simu wakiona imetajwa kuwa ni “Waterproof” au “Water resistance” huwa wanajua ni simu zisizo ingia maji.

Kitu muhimu kujua hapa ni kwamba kuna utofauti kati ya Simu zinazosemwa kuwa ni “Waterproof” na simu zinazosemwa kuwa ni “Water resistance”. Na hapa chini The bestgalaxy tunaenda kukufungua kitu muhimu juu ya utofauti huo.

Tofauti kati ya Simu za Waterproof na simu za Water resistance

Simu za waterproof na simu za water resistance zina tofauti katika jinsi zinavyozuia maji. Simu za waterproof zina uwezo wa kuzuia maji kuingia ndani yake kabisa. Lakini simu za water resistance zinakua na kiwango cha kuzuia maji kwa kiasi flani au namna flani.

Kiufupi simu hadi imeitwa “Waterproof” ni haiwezi ruhusu maji kupenya ndani kabisa. Lakini simu ikiitwa “Water resistance” huwa inaweza kuzuia maji lakini inategemeana na wingi wa maji, joto la maji, aina ya maji, muda iliokaa ndani ya maji au kina cha maji. Na unapotumia simu za Water resistance haushauliwi kuziweka kwenye maji makusudi maana zinaweza kuingia maji. Kuzuia maji kwake kuna kunailinda simu yako isiharibike pale unapo idondosha kwa bahati mbaya kwenye maji au sababu nyingine zisizo za makusudi.

Inasemekana kwamba simu nyingi huwa ni Water resistance na sio Waterproof. Na Kuna Makampuni yanaweza kuziita simu zao Waterproof kwa lengo la kibiashara lakini zikawa zinastahili kuitwa Water resistance na sio Waterproof. Kutokana na jambo hili, haushauriwi kujiamini sana kiasi cha kuiweka weka kwenye maji simu yako hovyo baada ya kuambiwa ni Waterproof.

Simu za Waterproof na Water resistance huwa zinawekwa vimipira na gundi kwenye nafasi ambazo maji yanaweza kupita. Mara nyingi simu za muundo huu huwa ni ngumu kuzifungua zinapotaka kurekebishwa kifundi na pia zikifunguliwa tu, huwa zinapoteza uwezo wake wa kuzuia maji. Mbali na jambo hil, simu hizi zinaweza poteza uwezo wa kuzuia maji baada ya kudondoshwa chini na kujigonga au kutumia kwa muda mrefu.

Ingress protection ratings (IP ratings) ni kipimo cha uwezekano wa kifaa cha kielectric ikiwemo simu zuia maji(vimiminika) na vumbi. Mfano wa IP rating ni “IP68” na imetajwa kuwa samsung galaxy s24 ultra inauwezekano huo. Namba ya kushoto “6” ni uwezekano wa kuzuia vumbi alafu namba “8” ni uwezekano wa kuzuia maji. Simu hii inafahamika kama ni “Waterproof” kutokana na uwezekano huo japo bado haushauriwi kujiachia nayo kwenye maji au vimiminika. Mwisho ningependa ufahamu kuwa Samsung Galaxy S24 ultra ni simu ya kwanza toka Samsung iliojikita kwenye Ai (akili bandia).

Jinsi ya kupata Namba zilizofutika kwenye Simu

Kwenye simu huwa tunatuza namba na siku hizi Smartphone huturuhusu kutunza katika Email mbali na kuzitunza katika Laini na Simu yenyewe. Mara nyingi mtu unashariwa utunze namba za simu kwenye simu yako katika Email. Email ni sehemu nzuri ya kutunza namba zako maana huwa Inazitunza namba in cloud na kuzifanya iwe rahisi kuzipata hata utakapo ibiwa au kupoteza simu. Yani hata kama umeibiwa simu, ukiwa na taalifa za Email yako uliotunzia namba tu, unaweza ingiza email hiyo kwenye simu yako nyingine na ukapata namba za simu ulizotunza. Taalifa za Email tunazoziongelea ni Email yenyewe na Password yake tu.

Ukiona dalili hizi ujue akaunti yako ya Facebook si salama BONYEZA HAPA>>>


Katika ukurasa huu wa The bestgalaxy, hatuta zungumzia kuhusu utunzaji wa namba za simu zaidi ya hapa. Ila tunaenda kueleza jinsi ya kupata Namba za simu zilizofutika.

Jinsi ya kupata Namba za simu zilizofutika

Ikiwa umefuta namba yoyote kwenye simu yako na haipo tena kwenye Lain, Email na hata katika simu yenyewe, tambua bado unanafasi ya kuipata namba hiyo. Namba iliofutika kwenye simu inaweza kuwa katika akaunti yako ya Facebook iliopo kwenye app ya Facebook ya simu yako.

Ukiwa na app ya Facebook kwenye simu yako, huwa wanaomba ruhusa ya kuchukua namba za simu ulizotunza kwenye simu yako ili wazitumie kuiweka akaunti yako ya Facebook karibu na watu unaowajua. Hii ni moja ya sababu ambazo hupelekea kuwaona watu unaowajua kwenye Facebook.
Ukiruhusu ruhusu Facebook ichukue namba za simu kwenye simu yako, hata zikifutika kwenye simu, bado zitakuepo ndani ya akaunti yako ya Facebook. Kama uliiruhusu Facebook kuchukua namba za simu, unaweza fuata yafuatayo ili kupata Namba zilizofutika kwenye Simu yako.

  • Ingia katika Facebook na ubonyeze vimistari vitatu gusa “Settings”
  • Ingia kwenye settings alafu nenda kwenye “Accounts center”.
  • Ingia kwenye “Your Information and permissions” na ubonyeze kwenye “Upload contacts”
  • Chagua account yako ya Facebook utakayoiona Pele alafu utapelekwa kwenye ukurasa uliona orodha ya majina ya namba ambazo Facebook imeyatunza.
  • Baada ya hapo utakua ukigusa tu majina ili kuona namba. Kwenye orodha ya namba hizo unaweza kuziona namba ya simu iliofutika kwenye simu yako.

Kama haukuiruhusu Facebook kuchukua namba za simu kwenye simu yako, unaweza usiikute namba ambayo unaihitaji. Ni hayo tu tulio kuandalia hapa ila usiache kutembea The bestgalaxy.

WOWCube: Ni kifaa gani hiki na kinatumikaje?

Kama umewahi chezea “Rubik’s Cube” basi unaweza kuielewa zaidi WOWCube. “Rubik’s Cube” ni kifaa kilichoundwa na Ernő Rubik mnamo mwaka 1974. Ni kifaa chenye puzzle au fumbo ambalo linajumuisha kurejesha sura sita za maraba katika usawa baada ya kuvurugwa. Kuna Cube nyingine zanaubo mbali na mraba. Rubik’s Cube imekuwa maarufu zaidi ulimwenguni na inachezwa na mamilioni ya watu ulimwenguni.

Sasa WOWCube(WOWCUBE® Entertainment System) ni kifaa ambacho ni kama “Rubik’s Cube” lakini kipo kidigitali zaidi. WOWCube ipo kisasa zaidi kiasi ambacho inaitwa kifaa cha kucheza games. Kina kuruhusu kucheza games nyingi na unakua unacheza kwa kukizungusha, kukitikisa na kugusa screen. Kifaa hiki kina screen ndogo 24 ambazo zinakufanya uone vitu au games unachocheza.
Unakua unakichaji kama unavyochaji vifaa vingine vya kuchaji vya kidigitali alafu unaweza kukiunganisha na simu ya smartphone kwakutumia Bluetooth. Haijali ni simu ya Android au iOS, zote zinaweza kufanya kazi na hiki kifaa.


Kuna app yake unatakiwa uiingize kwenye simu ya smartphone unayoiunganisha nacho. App hiyo inaitwa WOWCube connect na kazi yake kubwa ni kukupa uwezo wa kuendesha kifaa cha WOWCube. Kupitia app hiyo unaweza ingiza games pamoja na app mpya kwenye kifaa cha WOWCube na kurekebisha vitu kama mwanga ili kuwa vile wewe unapenda.

Mbali na hayo, WOWCube pia inauwezo wa kuonesha notifications za kwenye simu ukiunganisha, tarehe (kalenda kwa ujumla), unaweza soma comics na kujifunza mambo mengine. Ni kifaa kizuri kwa watoto na wakubwa pia. Pre order kwenye website ya WOWCube, imeandikwa unaweza pata kwa kama dora 549 za kimalekani hivi. Hiyo ni pre-order.

Moja ya stori kuhusu jina lake lilivyotokea; wanasema kabla hakijaitwa WOWCube, watu alipokua wakioneshwa walikua wanamshangao wa “Wow”. Basi baada ya mishangao hiyo kuwa mingi, wakaamua kukiita “WOWCube”.

Jinsi ya kutumia bando kidogo unapokua Instagram

Mtandao wa instagram ni moja ya mitandao huwa inatajwa sana katika upande wa mitandao yenye kutumia sana data au bando la internet kwenye simu. Katika uzoefu wako wa kutumia mtandao huu kutoka Meta, unahisi unatumia sana bando la internet? Mh sijui kwa upande wako unawazo gani lakini ukweli ni kwamba mitandao ukiwemo instagarm ambayo hujihusisha na video huwa inatumia sana bando.

Instagram ina video ambazo hua zinajiplay bila hata uamuzi wa mtumiaji na video hizi hua zinachukua bando zinapojiplay. Mbali na video, picha zenye ubora pia zipo katika Instagram na picha zenye ubora hua zinachukua bando kuliko zisizo na ubora. Lakini hatuwezi sema mambo hayo kwenye instagram ni mabaya maana ndio kati ya mambo hufanya mtu ufurahie kutumia mtandao huu. Kama jambo la bando linakuumiza sana unawezafanya yafuatayo kutumia bando kidogo unapokua Instagram.

WhatsApp yako inatatizo? Jifunze jinsi ya kutatua hapa>>>>

Jinsi ya kutumia bando kidogo unapokua Instagram

Njia rahisi na rasmi ya kupunguza matumizi ya data au bando lako la internet ni kutumia App ya Instagram Lite. App ya Instagam Lite ni app ambayo imeundwa tofauti na jinsi ilivyo App ya Instagram ya kawaida. App hii ni ndogo kuliko app ya kawaida na imepunguzwa baadhi ya mambo au vipengele ambavyo hutumia bando lako ikiwemo ubora wa picha na video . Hivyo, unapoitumia app ya  Instagram Lite unakua unatumia bando kidogo kuliko ambavyo ungetumia app ya Instagram ya kawaida. Haitumi bando lako sana app hii na inaweza fanya vizuri hata kama mtandao wa internet kwenye simu yako haupo vizuri.

Kama hautataka kutumia app ya Instagram lite basi ni unaweza punguza matumizi ya data kwa kuwasha kipengele cha Data saver ambacho hupatika kwenye app ya Instagram ya kawaida. Kuwasha kipengele hiki, gusa vimistari vitatu vilivyo juu upande wa profile yako ya Instagram. Baada ya hapo ingia kwenye “Data usage and media quality” na uwase sehemu ya Data saver utakayoiona hapo.

Mbali na njia hiyo, unaweza punguza pia idadi ya video unazoangalia au ukapunguza muda unaotumia katika mtandao huu ili kupunguza matumizi ya bando lako.

Katika matumizi yako ya simu usifanye vitu hivi GUSA HAPA>>>

Matumizi ya simu ya zamani unaponunua mpya (usiiuze au kuidharau)

Mara nyingi watu, hutumia simu walizonunua alafu hununua nyingine mpya baada ya muda flani. Sababu za kununua hutofautiana maana kila mtu huwa na jambo lake liliomsukuma kutoa pesa yake na kunua simu mpya. Kuna watu hununua simu mpya baada ya kuona simu ya zamani imeharibika kabisa, wengine hununua baada ya kupoteza simu, pia kuna wengine huwa wananuanua simu mpya kutokana na kuichoka simu ya zamani au kutamani kubadilisha simu tu.

Kama unatabia ya kununua simu mpaya ili kubadilisha simu au kwenda na wakati ni jambo zuri. Simu mpya huwa zinakuja na maboresho pamoja vitu vingine vizuri kwa huo wakati zinaotolewa. Hivyo kwenda na wakati katika upande wa simu ni jambo zuri. Lakini unaponunua simu, mpya simu ya zamani huwa unafanya nini?
Kama haujui matumizi ya simu yako ya zamani unapo nunua simu mpya, soma hapa chini ili kufahamu jinsi wanavyoweza itumia.

Matumizi ya simu ya zamani unapo nunua mpya

Badili kuwa kifaa cha games

Simu yako ya zamani kama ipo vizuri na inaweza kuwekwa games za kucheza, basi ibadili kuwa kifaa cha games. Kuna games nzuri sana ambazo unaweza zijaza kwenye simu hiyo alafu ukitulia ukawa unazicheza. Sio lazima iwe wewe tu unacheza, hata ukiwapa watoto inaweza kuwa vizuri pia.

Ifanye WiFi ya nyumbani

Simu za smartphone huwa zina WiFi ambayo unaweza unganisha vifaa vingine vinavyotumia internet alafu vikatumia internet kupitia simu hiyo. Sasa endapo itakua na simu ya zamani na laini ya simu usioitumia, unaweza weka bando la kutosha kwenye hiyo laini alafu ukiingiza kwenye simu kisha ukawa unaitumia iyo simu kama WiFi ya nyumbani kwako. Kama unatumia internet kwenye PC au simu yako, hii inaweza kuwa nzuri kwako maana utakua unaiunganisha kifaa chako kwenye simu hiyo ya zamani ili kupata internet.

Iweke kuwa simu ya nyumbani

Unasimu ambayo ukiwa mbali na nyumbani ukiipiga mtu yoyote aliopo nyumbani anaweza ipokea? Mh sawa. Ni vema kuwa na simu ya nyumbani ili ukipata dharura au wakipata dharaura watu alioko nyumbani muwasiliane. Kama hauna simu ya zamani, unaweza ibadili kuwa simu ya nyumbani kwa kuiwekea laini na kuwaambia wanaoshinda nyumbani waitumie kama simu ya nyumbani tu.

Badili kuwa kifaa Cha Muziki na video

Kama unapenda kusikiliza nyimbo na kuangalia filamu, basi simu yako ya zamani inaweza kukufurahisha kwenye hilo. Unaweza ijaza nyimbo zote ambazo huwa ukitulia unazisikiliza sana bila kuchoka au ukajaza filamu unazozipenda sana. Baada ya kufanya hivyo ukipata muda utakua unachukua iyo simu na kusikiliza nyimbo au filamu zako bila Kuigusa simu yako mpya na kumaliza betri.

Tunzia file usizotaka kutembea nazo au zipotee

Simu yako ya zamani pia inaweza tumika kama kifaa cha kuhifadhia vitu vyako. Unaweza ingiza mafaili ambayo hautaki yapotee au hautaki yawe kwenye simu yako mpya. Ukishaingiza, unaweza ficha hiyo simu sehemu ambayo unahisi ni salama. Kama ni mtu unaekumbuka password, basi unaweza weka na password kwenye simu hiyo.

Unaponunua simu mpya, usisahau kuwa thamani ya simu ya zamani bado ipo. Kikubwa ujue jinsi gani utaitumia simu ya zamani baada ya kupata simu hiyo maana usipojua hautaiona thamani yake.

Mbali na yote, kuiuza au kuigawa ni jambo zuri pia maana unakua ni kama unawasaidia watu wengine kupata simu na kuwaonesha upendo.