Kwasasa katika dunia matumizi ya internet yameongezeka. Na inaonesha yatazidikuongezeka zaidi ya hapa maana baadhi ya huduma na vitu vilivyokua havihusiani na internet vimekua vinategema internet Kwa sasa. Mfano mzuri ni magari ya kisasa yanayotoka kipindi hiki. Mengine yanatumia internet kukupa huduma ya redio na vitu vingine. Yani huwezi sikiliza redio ya gari bila internet. Hebu tuachane na ulimwengu na tuingie Tanzania Sasa.
Ni wazi kuwa Kuna watu wanatumia sana internet na vifurushi vya internet Kwa hapa Tanzania vinaweza kukughalimu hata za zaidi ya 2000 Kwa GB 1(inategemea na kifurushi). Katika kununua vifurushi na kutumia internet, Kuna baadhi ya watu hununua vifurushi vya internet vya wiki lakini huvimaliza kabla ya wiki na hawajui ni Kwanini. Hiki sio kitu kukubwa kama hakikuumizi kwenye sawala la pesa lakini kama kinakuumiza basi hapa ntakujuza ni kwanini ipo hivyo na hatua gani unaweza kuchukua.
Jinsi ya kufanya simu isiishe chaji haraka GUSA HAPA>>>
Pata bando za internet Kwa Bei rahisi (Tigo & Halotel) GUSA HAPA>>>>
Kwanini bando la wiki la internet linawahi kuisha kabla ya wiki?
Kiufupi ni kwamba kitu kinacho maliza bando mara nyingi ni “matumizi”. Ukiwa na Mb 50 ikiingia kwenye internet na kutumia au zikatumika Mb 50, utabakiwa na Mb 0 hata kama ulipewa zikae mwezi. Ni mahesabu tu.
Ukiwa unamatuzi ya internet yanayotumia Mb nyingi basi utahitaji Mb nyingi ili uzitumie sio sinazokaa sana. Hata ununue bando la mwaka mzima, kama matumizi yako ni makubwa kuliko hilo bando au Mbs ulizonazo, utamaliza kabla ya huo mwaka kuisha.
Jinsi ya kufanya simu ijinunulie bando la internet (usichome pesa zako kununua bando) GUSA HAPA>>>
Kwani watu hutumia bando kiasi gani?
Kwa watumiaji wa Smartphone (Tz) wengine wanaweza kutumia Mb 200 kwa siku na kunawatu hufia hadi Gb 1, G 2 au zaidi. Hii hii pia hutegeana na “matumizi” ya mtu.
Kuna watu ambao hutumia internet kuangalia movies, kucheza magemu (cloud games) au wapo internet kikazi. Watu hawa hata GB 2 mbili zinaweza kuwa ndogo kwao Kwa siku.
Mbali na watu hao kunawatu wanamatumizi ya kawaida tu. Inawezakua wanatumia kupata nyimbo mpya, habari, matokeo ya michezo na vitu vingine kama hivyo. Watu wanye matumizi haya wanaweza kutumia chini ya Mb 500 japo wanaweza vuka hapo pia.
Nifanye nini ili kutomaliza bando la internet Kwa haraka?
Kama unataka usimalize bando lako la internet Kwa haraka basi inabidi uanze kujichunga kwenye matumizi maana maranyingi matumizi ndio hulimaliza bando.
Kama ni mtu wa movies basi punguza kuangalia movies au videos unazoangalia kwa siku.
Jizuie kutumia internet sana kama bando linaumiza pesa yako.
Ingiza vitu kama offline games au vichekesho na vitu vingine ambayo vitakua vinakufurahisha kwenye simu yako bila kuwasha data. Mfano wa vitu vingine ni Simulizi. Unaweza ukawa unanunua simulizi za kusoma kwenye simu yako alafu unakua unasoma kidogo kidogo ukiwa na muda.
Hayo ni machache niliokuandalia kwenye makala hii inayohusu internet. Tutakutana kwenye makala nyingine Lakini usiache kufuatilia The Bestgalaxy ili kujifunza mengi zaidi.
















