Kwa sasa watu wengi wanatumia AI kama ChatGPT kuedit picha. Sababu kubwa ni kwamba AI imefanya mchakato huu kuwa rahisi, wa haraka, na hauhitaji utaalamu wowote wa picha. Kwa kutoa maelezo tu, mtu anaweza kubadilisha picha yake kwa namna yoyote anayotaka.
Lakini pamoja na urahisi wake, si huduma za AI zote zinapatikana bure bila kikomo. Kwa mfano, ChatGPT hukupa nafasi chache za kuedit picha bure; baada ya hapo unatakiwa kulipia ili kuendelea kutumia kipengele hiki bila mipaka.
Watu wengi wanalipia huduma ya ChatGPT kwa sababu inaonesha uwezo mkubwa wa picha, video na uandishi. Kwaiyo kulipia ni jambo jema kama unaweza. Lakini kama huwezi kulipia na bado unahitaji kuedit picha zako mara kwa mara, kuna cha kufanya ili kufanikisha hilo bure bila kikomo.
Njia ya Kuedit Picha Bure Bila Kikomo: Microsoft Copilot
Ikiwa unataka kuedit picha kwa ChatGPT bila kikomo, njia rasmi ni kununua vifurushi vyake kama Plus, Pro, Business, au Enterprise. Lakini kama kulipia ni changamoto, suluhisho rahisi ni kutumia Microsoft Copilot.
Copilot ni AI ya Microsoft, inayotumia teknolojia ile ile ya “OpenAI” kama ChatGPT (mfano GPT-4 na GPT-5). Ina uwezo sawa wa kuedit picha, kuandika, kutafsiri, kutoa majibu na kufanya kazi nyingi kama ilivyo ChatGPT. Tofauti kubwa ni kwamba Copilot hukuruhusu kutengeneza na kuedit picha bure bila kikomo.
App ya Copilot Ai ikibadilisha muonekano wa nyuma wa picha(Background)
Kwanini Copilot?
Inatumia injini sawa na ChatGPT
Inakupa uwezo wa kuedit picha bure
Haina kikomo kama ChatGPT ya bure
Kwa kifupi, kama huwezi kulipia ChatGPT lakini unahitaji uwezo wa kuedit picha kama vile ChatGPT, basi CopilotAI ni chaguo sahihi kwako. Inapatikana kwenye simu (Play Store & App Store). Mbali na simu, inapatikana kwenye PC na kupitia website pia.
Cryptocurrency ni aina ya sarafu ya kidijitali (digital currency) ambayo hutumika kama njia ya malipo au uwekezaji mtandaoni. Mfano wa cryptocurrency ni Bitcoin (BTC), Ethereum (ETH), Binance Coin (BNB), Solana (SOL), na Tether (USDT). Tofauti na pesa tulizozoea kama Shilingi au Dola, cryptocurrency haipo katika mfumo wa karatasi (yote ipo kidigitali).
Njia ya haraka zaidi ya kupata cryptocurrency ni kununua au kubadilisha (exchange) kwa kutumia pesa zako za kawaida. Thamani ya sarafu hizi hubadilika kulingana na soko. Kwa mfano, USDT (Tether) ni moja ya cryptocurrency zenye thamani inayofanana na Dola ya Marekani. 1 USDT ≈ Tsh 2,400, kwa hiyo ukiwa na 100 USDT unakua na thamani ya takriban Tsh 240,000.
Lakini je, unaweza kupata zaidi ya 100 USDT bila kutoa hata senti kutoka mfukoni mwako?
Habari njema ni kwamba, inawezekana!
Jinsi ya Kupata Zaidi ya “100 USDT” Bila Kutoa Pesa Zako
Njia rahisi na halali ya kupata USDT bila kutumia pesa yako ni kupitia platform zinazokupa USDT kwa kufanya jambo fulani. Mfano mzuri kwa sasa ni Opera News Hub, ambayo ni platform/jukwaa linalomilikiwa na kampuni ya Opera.
Kwenye Opera News Hub:
Unaandika au kutengeneza content (habari au makala).
Baada ya hapo unaweza kuamua kutunza USDT kama mali (asset) au kuibadilisha kuwa pesa za kawaida.
Kwa kifupi:
Tafuta platform inayolipa kwa kukupa USDT (mfano: Opera News Hub).
Fanya kazi inayohitajika (andika au tengeneza content bora).
Pokea USDT wanazokupa kwenye wallet yako.
Wallet ya MiniPay
Kuna maplatform mengi duniani yanayolipa kwa kwa kukupa cryptocurrency, lakini Opera News Hub ni rahisi zaidi kuelewa na kutumia ukiwa Afrika Mashariki. Hata kama utakua ukipata kiasi kidogo, ukijituma na kutunza USDT zako, unaweza kufikisha zaidi ya 100 USDT baada ya muda bila kutumia pesa zako za kawaida.
Disclaimer: This article is for education only and is not financial advice. Always do your own research before making any decisions.
Miaka michache iliyopita, ilikua rahisi sana kutambua video au picha zilizotengenezwa na AI (Artificial Intelligence). Mara nyingi, picha au video hizo zilikuwa na makosa mengi ya wazi. Kwa mfano, mtu kwenye picha angeweza kuonekana na vidole saba, au mikono mitatu, jambo lililofanya iwe rahisi kuelewa kuwa hiyo ni kazi ya AI.
Lakini siku hizi mambo yamebadilika. AI imekua ya kisasa zaidi na makosa yake yamepungua sana. Kwa sasa, ni vigumu sana kutofautisha picha au video halisi na zile zilizoundwa na AI. Kutokana na hilo, mitandao mingi ya kijamii imeanza kuweka alama maalum (label) kwenye maudhui (picha au video) yaliyotengenezwa na AI, ili kuwasaidia watumiaji kutambua kwa urahisi.
Pamoja na hayo, bado kuna ugumu kwa watu wengi katika kutofautisha picha au video halisi na zile za AI; hasa kama zimeundwa vizuri.
Hapa The Bestgalaxy, tumekuandalia njia rahisi za kuitambua picha au video iliyotengenezwa na AI, ili usipoteze muda au kudanganywa mtandaoni. Pia ni njia ya kujilinda dhidi ya matapeli wanaotumia maudhui ya AI kwa udanganyifu.
Jinsi ya kuitambua Picha au video iliotengenezwa na Ai
1. Tumia Platform Maalum Kutambua Kazi za AI
Njia ya haraka na rahisi zaidi ni kutumia tovuti maalum zilizoundwa kwa ajili ya kutambua kama picha au video imetengenezwa na AI. Mfano wa tuvuti kama hii ni Ai or Not. Hii tuvuti inakuruhusu kuweka picha au video, kisha inakupa matokeo ikiwa ni ya AI au halisi.
Hii ni njia nzuri sana lakini kuna baadhi ya picha halisi huwa zinaweza kuonekana ni kazi za Ai kwenye njia hii. Hili linaweza kutokea endapo picha au video halisi itapitishwa kwenye michakato inayohusisha Ai. Michakato hii inaweza kuwa hata kuongeza ubora kwa kutumia Ai tu.
Kwaiyo kiufupi kuna Picha au Video halisi huwa zinaweza kuonekana kama sio halisi(za Ai) kwasababu zimeongeza ubora tu kwa kutumia Ai.
Hii ni website ya Ai or Not ikitoa majibu juu picha. Majibu ya picha hii yamesomeka “Likely AI Generated” ikiwa ni ishara yakwamba picha imetengenezwa na AI.
2. Angalia Vitu Hivi Kwa Macho Yako
Kama hutaki kutumia tovuti au programu maalum, unaweza kutambua mwenyewe kupitia dalili ndogo zifuatazo:
Rangi zilizokolea kupita kawaida: Video/Picha za AI mara nyingi huwa na rangi ang’avu kupita kiasi, zisizo za kawaida kuwepo kwenye picha halisi.
Mabadiliko madogo kwenye video: Wakati mwingine vitu vidogo hubadilika ghafla, kama sura, madoa ya nguo, macho, au mwanga. Hii ni ishara ya AI.
Sauti yenye uroboti: Video za AI (hasa deepfake) mara nyingi zinakuwa na sauti nyepesi au zenye mwangwi kama sauti za roboti (robotic tone).
AI imefika mbali sana lakini bado unaweza kuitambua ukitumia umakini. Ingawa zinatambulika ila kumbuka kuwa sio kila kitu kinachoonekana halisi mtandaoni ni cha kweli. Baadhi ya video au picha zinawezakuwa ni ngumu kutambua mpaka alietengeneza aweke wazi.
Toka Facebook imefungua zaidi mlango wa watu kuingiza pesa kupitia content zao, watu wamekuwa wakihitaji kujua vitu vingi sana kuhusu mchakato mzima. Kuwasaidia, hapa The Bestgalaxy tumekuwa tukitoa makala mbalimbali ikiwemo hii.
Kwenye makala hii, hebu tuzungumzie mambo ambayo unatakiwa kuepuka katika kuingiza pesa kupitia Facebook Content monetization.
Nadhani wote tumeisha jua Facebook Content monetization ni program inayohusu kuingiza pesa katika Facebook. Sasa hebu tuangalie mambo ambayo anatakiwa kujua mtu aliyefanikiwa kuanza kuingiza pesa, na hata yule anayewinda nafasi ya kufikia katika hatua hiyo.
Mambo 5 ya kuepuka ili kutengeneza Pesa katika Facebook
1. Kushare link zisizoaminika
Facebook ni platform inayoruhusu kushare vitu mbalimbali ikiwemo link. Lakini kwenye suala la kushare link, unatakiwa kuwa muangalifu sana ukiwa kama content creator. Link zinaweza kufanya post zako zizuiwe kuwafikia watu wengi.
Kuweka link kwenye captions au kuzituma kama zilivyo, kunaweza kuathiri hata ukuaji wa akaunti yako. Mbali na kuathiri ukuaji, link zikiwa si salama zinaweza kufanya ukaondolewa kwenye Content monetization program na kufutiwa akaunti kabisa.
2. Kuweka video au picha toka kwa watu wengine
Facebook wanataka mtu atengeneze content ambazo ni “Original”. Kama content unazoweka kwenye akaunti yako zimetolewa kwenye akaunti za watu wengine na kuwekwa kwako bila utofauti wowote, basi huwezi kuingizwa kwenye Content monetization program.
Na hata kama utafanikiwa kuingiza pesa, mapato yako yanakuwa madogo ukilinganisha na Original. Kwa hiyo, ukitaka kufurahia kuingiza pesa Facebook bila matatizo, hakikisha unawekeza muda kutengeneza content zako, si kuchukua za watu kama zilivyo. Na hata ukichukua, unatakiwa kuongeza thamani ili uonekane kuwa umefanya kazi ya kutengeneza kitu. (Mfano mzuri wa hili ni kufanya content za reaction).
3. Kutumia nyimbo za watu kwenye video zako kupita kiasi
Kwenye content, ni vizuri kutumia nyimbo za watu zinazofanya vizuri katika ulimwengu wa music. Lakini suala hili huwa linakuja kuleta matatizo katika upande wa copyright ya ayoweza athiri monetization.
Kuna baadhi ya nyimbo ukiziweka kwenye video yako, zinakupa tatizo la “Copyright”. Tatizo hili linaweza kuja kwa namna mbili; Mbaya sana na Nzuri kiasi.
Namna ya kwanza (Mbaya sana) ni utapata maonyo na vizuizi kwenye akaunti yako.
Namna ya pili (Nzuri kiasi) ni kukatwa mapato yako kwa ajili ya loyalty.
4. Kupost video za AI bila kuweka wazi
Mwaka 2025, baada ya ongezeko la content zinazozalishwa na AI mtandaoni, kampuni ya Meta iliamua kuweka utaratibu wa kuziwekea alama content zilizozalishwa na AI.
Ukiwa kama content creator, unatakiwa kuweka wazi content za AI unazopost ili kuepuka matatizo kwenye Content monetization. Hapa naongelea kuweka post zako za AI katika kipengele ambacho huwa kinaandikwa “AI label” kila unapo post.
Kipengele cha “Ai label” katika Facebook
5. Kukomenti au kushare zaidi ya kawaida
Kukomenti, katika Facebook kuna namna mtu anaweza kupata matatizo kwa kufanya mambo kupitia kiasi. Kukomenti na kushare vitu kupita kawaida ni kati ya mambo yanayoweza kukuletea matatizo.
Unaweza kuwa haujafanya kosa kushare au kucomment, lakini kwa kuwa unafanya kupita kiasi, utapata matatizo.
Hii ni kwa sababu Facebook ina mifumo ya kuzuia vitu vibaya na hatari kwa watumiaji wake. Endapo akaunti yako itagundulika kufanya jambo lisilo la kawaida, huwa wanazuia akaunti na kuangalia kama unajihusisha na mambo mabaya. Kitendo cha kukuzui kinaweza kukufanya uondolewe kwenye Content monetization au kufutiwa akaunti kabisa endapo hawatakuelewa.
Kama unataka kufanikiwa kwenye Facebook Content monetization, basi epuka makosa haya matano huku ukitengeneza content zako kwa ubunifu.
Watu wengi wanaotuma na kupokea pesa kwenye simu zao hapa Tanzania huwa wanatumia huduma za kifedha za mitandao ya simu ikiwemo Mixx by yas kutoka Yas(Tigo). Mixx by yas imekua moja ya njia nzuri za kutuma na kupokea pesa toka miaka nyuma ambayo ilikua inaitwa “Tigo Pesa”.
Mbali na kutumika kutuma na kupokea pesa, Mixx by yas huwa ina huduma nyingine ndani yake zinahusisha fedha. Katika huduma hizo, kuna huduma ambazo zimelenga kumsaidia au kumuwezesha mtumiaji wao. Katika Makala hii, tutajikita katika huduma yao ya mikopo inayomuwezesha mtu kukopa pesa zinazoweza kumsaidia kwenye mambo mbalimbali. Ikiwa unahitaji kujua namna ya kukopa pesa katika akaunti yako ya Mixx by yas, basi hapa ndio mahali pake.
Kama unahitaji kukopa pesa katika akaunti ya Mixx by yas na uwe huru kuitumia kwenye mambo mbalimbali basi utatakiwa kutumia huduma yao ya “Nivushe plus“. Nivushe plus ni huduma ya Mixx by yas inayokuwezesha mtumiaji kukopa kiwango flani cha pesa na kukilipa katika muda uliochagua kurejesha. Unapewa uhuru wa kuchagua ni muda gani utarejesha(inaweza kuwa baada ya wiki kadha au mwezi mmoja kabisa).
Kama ilivyo mikopo mingine, Nivushe plus pia huwa ina riba ingawa ni kiwango kidogo sana ukilinganisha na baadhi ya huduma za mikopo. Ukiachilia mbali kuwa na riba kidogo, Nivushe plus ni huduma ya haraka sana ya Mkopo kwa watumiaji wa Yas (Tigo).
Jinsi ya kukopa pesa Nivushe plus
Njia rahisi ya kukopa pesa katika Nivushe plus ni kupitia app ya “Mixx by yas“. Kama una app hii kwenye simu yako, fanya yafuatayo:
Fungua app ya Mixx by yas
Chagua kipengele Cha “Mikopo” kinachoandikwa “Loans” kwa lugha ya kiingereza.
Baada ya hapo, chagua “Nivushe plus” kwenye chaguzi zitakazokuja.
Ukishachagua, utapelekwa kwenye ukurasa maalum wa kuchukua, kuangalia na kurejesha mikopo.
Ukurasa wa Nivushe plus katika app ya Mixx by yas
Kwenye ukurasa huo unaweza kukopa Mkopo na kuangalia taalifa nyingi za mikopo. Taalifa hizo ni pamoja na Salio la deni, kiwango chako Cha kukopa na hata historia ya malipo yako.
Kiwango unachoweza kukopa katika Nivushe plus huwa kinaongezeka kutoka na mambo kama miamala unavyofanya kwenye akaunti yako na uaminifu katika kurejesha mikopo. Mara nyingi mtu muaminifu na mwenye miamala mikubwa huwa anakua na kiwango kikubwa cha kukopa. Lakini kitu muhimu zaidi ni uaminifu. Ukiwa vizuri unaweza kukopa hadi milioni 2 (Tsh 2,000,000)
Katika miaka ya hivi karibuni, dunia imeingia kwenye kipindi kipya cha teknolojia ambacho hakijawahi kushuhudiwa hapo nyuma. Ujio wa Artificial Intelligence (AI) au Akili Bandia kwa Kiswahili umebadilisha kabisa dunia katika kila sekta. Tokea kampuni kubwa kama Google, OpenAI, Meta, na Microsoft zilipoanza kuwekeza nguvu kubwa katika utafiti wa AI, dunia imeanza kushuhudia mambo ya ajabu ambayo zamani yalionekana kama miujiza.
Leo hii, AI inaweza kuandika makala, kutengeneza picha au video, kuzungumza kama binadamu, na hata kufanya maamuzi kama vile ni akili inayofanana na ya mwanadamu. Imeingia katika pande za biashara, elimu, sanaa, uandishi, afya, michezo, na hata mahusiano ya binadamu. Wengine wanaiona ai kama ni neema kubwa ya karne hii, wakati wengine wanaiogopa wakihisi inaweza kuchukua nafasi za kazi, kubadilisha maisha, au hata kuvuruga mfumo wa kijamii tuliouzoea.
Lakini jambo moja ambalo halina ubishi ni kuwa AI imeleta mapinduzi makubwa. Imefanya mambo ambayo yalionekana hayawezekani miaka michache iliyopita. Hapa chini tutaangalia mambo kadhaa ya ajabu ambayo AI imeweza kufanya mpaka sasa kwenye ulimwengu ili ujue jinsi inavyoendelea kuathiri maisha yetu ya kila siku.
Mambo 5 ya Ajabu Yanayofanywa na AI Katika Ulimwengu wa Sasa
Inaleta ugumu wa Kutambua Kazi za AI
Miaka michache iliyopita, ilikuwa rahisi sana kutambua kama picha, video, au maandishi fulani yametengenezwa na AI. Lakini sasa, mambo yamebadilika sana! AI imeboreshwa kiasi kwamba ni vigumu kugundua kama kitu fulani kimeundwa na kompyuta au binadamu. Teknolojia kama Midjourney, Sora, Runway, na D-ID zimefikia hatua ya kuzalisha picha na video zenye uhalisia wa kushangaza. Makampuni haya yanazidi kuboresha mifumo yao kila siku, na matokeo yake ni video au picha ambazo zinaonekana kama zimetengenezwa na kamera ya kweli. Ingawa bado hazijakamilika kwa asilimia 100, ubora wake unafanya hata wataalamu waone ugumu kutofautisha kazi ya AI na halisi.
Inapunguza Thamani ya Baadhi ya Kazi
AI imeathiri baadhi ya ajira duniani. Kazi ambazo zamani zilihitaji muda na utaalamu, sasa zinaweza kufanywa kwa sekunde chache kupitia AI. Kwa mfano, watu wengi waliokuwa wakitegemea platform kama Fiverr au Upwork kupata kazi za Ubunifu kama utengenezaji wa logo au picha wameanza kupoteza wateja. Yote ni kwasababu kila mtu sasa anaweza kufanya hizo kazi mwenyewe kupitia programu za Ai kama Canva AI, ChatGPT, au Logo Creator AI. Hii imesababisha baadhi ya kazi kushuka thamani huku watu wengi wakiendelea kujifunza kutumia AI kufanya mambo ambayo zamani yalihitaji mtaalamu.
Imerudisha Wasanii Waliofariki
AI imeleta kitu cha ajabu kinachogusa hisia za watu wengi. Imefanya kuwarejesha wasanii waliokufa. Hapa namaanisha; Kupitia mifumo ya AI, sasa inawezekana kutengeneza nyimbo mpya, video, au hata picha za wasanii waliotutoka miaka mingi iliyopita. Kwa mfano, unaweza kuona video mpya ya msanii maarufu aliyefariki zamani, au kusikia wimbo mpya uliotengenezwa kwa kutumia sauti yake ya zamani. AI imeruhusu mashabiki kuendelea kufurahia kazi mpya kutoka kwa wasanii waliowapenda, kama bado wako hai. Ni jambo la ajabu, na lionaonesha kuongeza uwanja mkubwa wa watu wanaohitaji kutengeneza vitu vitakavyoishi moyoni mwa watu milele.
Hii ni video ya 2Pac akiwa na Kode pamoja na wengine waliokufa. Video hii imetengenezwa na AI
Imetajirisha Watu Wanaoitumia Vizuri
Kama ilivyo kwa teknolojia nyingine, wale wanaoitumia AI vizuri, wamepata mafanikio makubwa. Watu wengi duniani wameweza kujijenga kifedha kupitia AI, wengine wanauza huduma za ubunifu, wengine wanaunda biashara za kidigitali, na wengine wanatumia AI kuendesha matangazo ya biashara mtandaoni. Kwa mfano; baadhi ya vijana mpaka sasa wanaingiza pesa kwasababu wameunda brand za nguo, eBooks na hata video kwa nguvu ya AI. AI ni kama kifaa chenye thamani ya mamilioni, inayoweza kubadilisha maisha ya mtu yeyote anayeijua vizuri.
Pamoja na hofu nyingi zilizokuwepo mwanzoni, AI sasa imekubalika kote duniani. Watu wa rika zote, kuanzia wanafunzi, walimu, wafanyabiashara, hadi watoto wadogo, wanaitumia kila siku. Kwa mfano, watoto wengi hutumia ChatGPT kujifunza, kuuliza maswali, au hata kufanya kazi za shule. Hili ni jambo zuri lakini ni muhimu kukumbuka kuwa AI haiko sahihi kwa asilimia 100. Wakati mwingine inaweza kutoa taarifa zisizo sahihi au kukosea bila wewe kujua.
Mwisho; fahamu kuwa ai imeleta mabadiliko makubwa katika maisha ya kila siku. Inatengeneza fursa mpya na changamoto mpya kwa wakati mmoja. Lakini kikubwa kwa mtu ulie bahatika kuwa hai katika mapinduzi haya ya Teknolojia ni kujifunza namna nzuri ya kunufaika nayo.
Kama wewe ni mfuatiliaji wa teknolojia ya AI(Artificial Intelligence), basi unajua kuwa sasa hivi kuna njia nyingi za kutengeneza picha na video kwa kutumia AI. Changamoto kubwa ni kwamba karibu kila platform ya AI maarufu huhitaji malipo kabla hujaweza kufurahia huduma zake.
Kwa mfano, sehemu ya kutengeneza videoza AI mara nyingi ndiyo ghali zaidi. Kuna baadhi ya platform zikikugharimu hadi zaidi ya Tsh 200,000kwa mwezi ili upate uhuru wa kutengeneza video kwa uhuru mkubwa.
Lakini sio kila mtu ana uwezo wa kulipia gharama hizi. Wapo wanaolipia kwa sababu wanatambua thamani yake; hasa wale wanaotumia video au picha za AI kutengeneza brand zao na hata kuingiza pesa kama content creators.
Habari njema ni kwamba sio lazima ulipie! Kuna njia halali na rahisi kabisa ambayo unaweza kutumia kutengeneza picha na video za AI bure na bila kikomo.
Njia hii ni kupitia huduma ya Bing. Hii ni injini ya utafutaji (search engine) inayomilikiwa na kampuni ya Microsoft. Watu huitumia kutafuta vitu mbalimbali kama ilivyo “Google” lakini inamilikiwa na kampuni tofauti.
Ukiachilia mbali kutafuta vitu mbalimbali, katika Bing kuna sehemu ya kutengeneza Video na Picha za Ai bure(Bing Image Creator na Bing Video Creator.). Hii sehemu ndio unaweza kuitembelea ukihitaji kutengeneza video au picha bila kulipia chochote.
Bing Image Creator: Hii ni sehemu inayokuwezesha kutengeneza picha za AI bure kabisa. Unachotakiwa kufanya ni kutembelea tovuti ya Bing(au Google) na kisha kutafuta “Bing Image Creator”. Hapo utaweza kuandika maelezo ya aina ya picha unayoitaka na AI itakutengenezea papo hapo.
Bing Video Creator: Kama unataka video, unaweza kutumia “Bing Video Creator”. Hii pia inapatikana mtandaoni bure kupitia Bing. Unachotakiwa kufanya ni kutafuta jina hilo kwenye Bing au Google, kisha utaelekezwa kwenye sehemu ya huduma hiyo.
MUHIMU KUJUA: Ili kutumia huduma hizi, utahitaji kuwa na akaunti ya Microsoft. Kama tayari unayo, unaweza kuingia moja kwa moja. Kama huna, unaweza kufungua akaunti mpya bure kabisa.
Kwa hiyo, kama umekuwa ukitaka kutengeneza picha na video za AI bure bila kikomo, usihangaike tena na gharama kubwa. Bing imekuletea suluhisho kwenye hili.
Facebook ni mtandao unaomilikiwa na kampuni ya meta. Katika Facebook kuna kipengele unachoweza kukiita “Facebook Ads” au “Meta Ads”. Kipengele hiki katika Facebook ni kwaajili ya makampuni au watu wanaohitaji kutangaza matangazo(Ads) kwenye mtandao wa Facebook. Kuna makampuni na watu wengi sana huwa wanailipa pesa hapo ili kuonesha matangazo kwenye mtandao wa Facebook.
Meta inatengeneza mabilioni ya pesa kwa mwaka kupitia watu wanaotangaza matangazo katika Facebook. Katika pesa hizo, huwa inachukua kiasi flani walizotengeneza na kuwalipa Content creator wa Facebook. Ili content creator kuanza kulipwa, anatakiwa kuingia katika program yao maalum kwanza(content monetization).
“Content creator” wa Facebook ni mtu ambaye huunda na kutoa maudhui (content) kwenye Facebook ili kuwavutia, kuwaburudisha, kuwafundisha au kuhamasisha watazamaji. Na Maudhui au content zinazozungumziwa hapa ni Video, Picha na hata Makala za maandishi.
Facebook inalipa kiasi gani kwa views 1000 za video?
Ukiwa kama content creator unaejihusisha na video katika Facebook, utalipwa pesa pale video zako zinapopata views (zinapoangaliwa na watu). Lakini fahamu kuwa Facebook haina kiwango maalum itakachokulipa kwa kupata views 1000 kwenye video zako. Facebook huwa inalipa kutokana na mfumo unaoitwa Cost Per Mille (CPM). Hii ina maana unalipwa kiasi kutokana na kiasi walicholipa watangazaji (watu walio lipa matangazo yanayooneshwa kwenye video zako). Yaani kama matangazo yanayooneshwa kwenye video zako hulipiwa pesa nyingi na watangazaji, basi unaweza kuingiza pesa nyingi pia ukiwa kama content creator.
Screenshot ukionesha jinsi Facebook ilivyomlipa moja ya Content creator wa India kwa video 1 fupi (Reel).
Lakini pia kiasi unacholipwa Facebook creator kinaweza kuathiliwa na mambo mengine kama nchi ya mtazamaji, sekta unayojihusisha nayo na hata tabia za watu wako katika Ads wanazoangalia.
Nchi ya watazamaji wako (mfano Marekani na Ulaya CPM huwa kubwa kuliko Afrika).
Mada/sekta ya content zako (mfano video za biashara, fedha, teknolojia hulipa zaidi kuliko utani au burudani tu).
Tabia za watazamaji kwenye Ads(watazamaji wakiwa wanajihusisha na Ads kwa kuziangalia au kubonyeza).
Muhimu kujua: katika Facebook kuna aina mbili za video. Video ndefu na video fupi ambazo huitwa “Reels”. Malipo hati ya aina hizo za video huwa yanatofatulia kabisa. Ukijihusisha na Reel unaweza ulipwe pesa ndogo sana kwa views 1000 ila uzuri ni kwamba huwa zinaweza kufika views milioni 1 kirahisi kuliko video ndefu.
Reels zinaweza kulipa $0.20 – $1.00+ kwa views 1000 (kutegemeana na nchi au mengineyo). Alafu video ndefu zinaweza kuwa $1 – $10+ kwa views 1000, hasa kwenye niche za biashara, fedha au teknolojia.
Watu wengi(Music Producers) wana kipaji cha kutengeneza beats za muziki lakini changamoto kubwa inabaki kuwa jinsi ya kuziuza na kupata kipato. Kwa sasa, teknolojia imerahisisha sana upande huu, unaweza kuuza beats zako kwa wasanii bila hata kuwa na studio kubwa. Tena unaweza kuwafikia watu Toka nchi mbalimbali wakawa Wateja wako.
Hapa chini kuna njia tatu bora za kuuza beats zako mtandaoni. Unaweza zitumia ikiwa wewe ni producer unahitaji kutengeneza Pesa mtandaoni kupitia Beats zako.
Njia 3 za kuuza beats zako mtandaoni:
Tumia Platform Maalum kwa Uuzaji wa Beats
Kuna tovuti nyingi ambazo zimetengenezwa mahsusi kwa wauzaji wa beats. Hizi platform zinakuwezesha ku-uproad kazi zako na kuziuza moja kwa moja kwa wasanii kutoka sehemu mbalimbali duniani. Baadhi ya mifano ni:
Unachohitaji ni kufungua akaunti(inaweza kuhitaji kulipia ili kuanza kuitumia), kuweka bei zako, na ku-uproad beats zako. Hii ni njia rahisi na salama kwa sababu wateja wengine watatoka ndani ya hiyo hiyo platform ana watalipia kupitia mfumo wanaoujua, na wewe unapokea malipo yako.
Huu ni ukurasa wa tuvuti/website ya Beatstars ukionesha Beats zinazouzwa.
Kuwa na Website Yako ya Kuuza Beats
Kama unataka kuwa na brand yako binafsi, basi kuwa na website ni muhimu. Kupitia website yako, Wateja wataona beats zako zote kwa mpangilio mzuri. Unaweza kuweka mfumo wa malipo (Card, Crypto, Skrill, M-Pesa, n.k).
Inakusaidia kujenga jina lako kama producer professional.
Website yako inaweza pia kuwa sehemu ya kuonyesha huduma nyingine unazotoa kama mixing & mastering, au hata tutorials za muziki.
Uza Kupitia Mitandao ya Kijamii
Mitandao ya kijamii ni soko kubwa la bure. Tumia Instagram, TikTok na Facebook kuonyesha vipande vya beats zako. Unaweza ku-uproad video fupi za beats alafu wasanii watakao lipenda beat, wanakua wanakutafuta inbox kwaajili ya maelewano ya kibiasha.
Unaweza pia kutumia captions nzuri na kutoa challenge mbalimbali kwa wasanii juu ya Beats zako ili kupata Wateja zaidi.
Mitandao ya kijamii hukusaidia kufikia watu wengi bila gharama kubwa, ila unahitaji kuwa consistent na ubunifu kwenye content unayoshare.
Kuuza beats mtandaoni siyo kazi ngumu kama ukipanga vizuri mfumo wako. Unaweza kuanza na platform za kuuza beats, kisha kujenga website yako, na hatimaye kutumia nguvu ya mitandao ya kijamii kupata wateja zaidi. Yani mfumo wako ukiwa vizuri, unaweza tumia njia zote tatu kama ulimwengu wa kuuza beats zako.
Mchakato wa kuchambua timu na kusuka mikeka ya kubeti huwa unachukua muda sana kwa baadhi ya watu. Kuna watu huumiza akili zaidi ya saa 1 kufikilia mkeka uwake uwe vipi kabla hajaweka dau.
Kama wewe ni mmoja kati ya wanaotumia muda mwingi katika kusuka mikeka ya kubeti, fahamu kuwa unaweza okoa muda wako wa kusuka mikeka kwa kuchukua mikeka iliosukwa na watu wengine. Kuchukua mikeka iliosukwa na watu wengine na kuibetia, ni njia rahisi ya kubeti inayoweza kukufanya uwe unashinda baadhi ya mikeka bila kupoteza sana muda wako. Kitu kikubwa hapa ni kuhakikisha mkeka uliouchukua, Umetoka kwa mtu ambae anafikilia vizuri kabla ya kuutengeneza.
Kufanya hivi hakuna maana utakua ukishinda kila siku, lakini baadhi ya siku unaweza kushinda mpaka ukampongeza aliekupa mkeka.
Siku hizi katika makampuni ya kubeti, wamerahisisha maswala ya kuchukua mikeka iliosukwa na watu wengine. Kuna kipengele cha “Code za mikeka” ambacho kinakuwezesha kuchukua mikeka kwa wengine kwa kujaza code tu. Yani ukitaka mkeka wa mtu, unachukua Code ya mkeka huo na kuujaza katika akaunti yako kwaajili ya kubeti. Hizo code huitwa “Booking Code” pia. Na yote haya ni kuokoa muda wako tu.
Sehemu za kupata Code za mikeka bure (Booking Codes)
1. Katika tuvuti ya kampuni unalobetia
Baadhi ya makampuni makubwa ya kubeti huwa yanakipengele maalum kwa code za mikeka. Kwenye kipengele hicho unakutana na Codes za mikeka mbalimbali iliotengenezwa na watu wengine alafu unaweza kutumia kubeti mkeka kwa upande wako.
Mbali kuchukua Code, unaweza sambaza na code za mikeka yako ikiwa utahitaji. Betway ni kati ya makampuni ya kubeti yenye kipengele cha “Booking Code” kwenye tuvuti zao. Katika tuvuti ya Betway kipengele hiki kinajulikana kama “Booking Codes”.
2. Tuvuti maalum kwa code za mikeka
Kuna tuvuti maalum ambazo huwa zinajihusisha na code za mikeka. Katika tuvuti hizi unapata code za mikeka unayoweza kubeti katika makampuni mbalimbali. Humu unakutana na orodha kubwa sana ya code za mikeka na Odds zake pia. Naweza kusema katika tuvuti hizi unaweza kupata mkeka wa kila Odds unazohitaji.
Convertbetcodes ni moja ya tuvuti ambazo hujikita kwenye code za mikeka unayoweza kuitumia. Tuvuti hii inatumika ku-convert code za kampuni moja kwenda nyingine lakini pia ina orodha ya code nyingi sana za mikeka iliosukwa na watu wengine. Unaweza kupata hata code za mikeka ya Leo.
3. Katika mitandao ya kijamii
Unatumia mitandao ya kijamii kama Facebook, X na Instagram? Basi fahamu kuwa kuna namna unaweza kupata code za mikeka humohumo. Baadhi ya watu siku hizi hutumia muda wako kuunda mikeka na kutoa au kusambaza Code kwa wengine kupitia mitandao ya kijamii.
Kuchukua Code wanazosambaza na kuzitumia, kunaweza kuwa njia nzuri ya kukwepa kupoteza muda wa kuunda mikeka. Mfano wa watu wanaotoa code za mikeka yao mitandaoni ni Samkicheko.
Ni hayo tu katika Makala hii lakini nakukumbusha; Kabla haujafanya uamuzi wowote katika kubeti, fahamu kuwa kubeti kunahitaji ustaharabu pia. Zingatia hii kata kwenye kutafuta code za mikeka ya leo. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy!
Disclaimer: This article is for education only and is not financial advice. Always do your own research before making any decisions.