Tag Archives: SMS

Sms za kumwambia mpenzi wako kuwa unampenda

SMS inaweza kuwa njia nzuri ya kueleza hisia za upendo na mapenzi kwa mwanamke au mwanaume umpendae. Sms kama sms zinamchango mkubwa katika mahusiano ya sasa maana ndio mara nyingi huunganisha wapenzi wakiwa mbali.

Katika makala hii, tumekuangalia jumbe mbalimbali za SMS ambazo unaweza kumtumia mpenzi wako kumwambia kuwa unampenda. Kuonyesha upendo kupitia maneno kunaweza kuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha uhusiano na kuongeza ukaribu kati yenu. Kunaweza mkumbusha jinsi gani unampenda na unahitaji.

Kwenye mahusiano ya mapenzi, maneno ni kitu kikubwa sana. Maneno yanaweza yumbisha mapenzi na hata kuyaweka sawa pia. Soto tunajua kwamba wakati mwingine mnaweza kuwa kwenye mahusiano lakini yakawa yanayumba. Kumwambia maneno mpenzi wako ya jinsi gani unampenda kunaweza mkumbusha mpenzi wako kushikamana na kuwa pamoja kwenye mahusiano. Na pia kuna muda mpenzi anaweza kuwa na kiu ya maneno mazuri toka kwako lakini akashindwa kusema maana na yeye haelewi.

SMS za kumsifia mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

Sms za kumwambia mpenzi mwanamke/mwanaume unampenda

  • Yule mtu anaeweza ufurahisha au kuuvunja moyo wangu ni wewe. Kuwa nawe ni furaha ya moyo wangu, sitamani kuwa mbali na wewe.
  • Kama kukupenda ni ujinga basi nakubari kuwa hivyo. Penzi lako limeushika moyo wangu mpaka naogopa. Ukiona chozi langu la maumivu ya mapenzi limenidondoka jua ni wewe. Na ikitokea hivyo naomba usije sahau kuwa hata wakulifuta pia ni wewe. Nakupenda sana.
  • Nakupenda Toka moyoni, Ukaribu wako huichemsha damu. Kuwa na Wewe ni Ndoto yangu tamu, staki kukatishwa mpenzi maana hainiishi hamu.
  • Penzi lako limenipeleka kwenye ulimwengu wa mapenzi ambao sikuwahi jua upo. Unanipa Raha, nakua na furaha kama mtoto.
  • Zawadi kubwa ninayotamani kuendelea kupata toka kwako ni upendo wako. Moyo wangu umeisha lidhia kuwa na wewe maishani, na wewe ukibadilika tu, jua unaniumiza mwanzako.
  • Duniani karibu kila mtu ana anae mpenda kwa dhati toka moyoni na yupo akili kila mara. Katika Maisha yangu mtu huyo ni wewe!
  • Wanaweza kuwa wamekwambia au umesikia maneno mengi kuhusu mimi. Ila naomba upuuze na usikilize moyo wangu unasema nini sasaivi. Moyo wangu usema unakupenda wewe!
  • Nimekua nikipenda kuangalia vitu vizuri na vyakupendeza ili nifurahi. Tangu nilipokutia machoni sina haja ya kuangalia chochote kizuri mbali na wewe ili nifurahi. Macho na kila kitu toka kwako hunivutia.
  • Ninapomaliza kuongea na wewe kwenye simu hua nakata simu lakini natamani kuendelea kuisikia sauti yako tena. Sijawahi kuichoka sauti yako maana ni faraja ya moyo wangu. Nakupenda sana.
  • Sijawahi jihisi mpweke nikiwa karibu na wewe mpenzi. Naweza umia kwa kupoteza vingi maishani ila nitaumia zaidi nikikupoteza wewe kipenzi. Maana nanipa sababu ya kufurahia maisha.
  • Moyo wangu hupitia mambo mengi maishani. Lakini dawa yake kila mara huwa ni wewe. Unajua jua kuugusa bila kuushika. Unagusa sehemu wajinga hawawezi fika. Nitakupenda mpaka mwisho wa Maisha.
  • Siri ya furaha yangu ni kuwa na wewe. Najiona wa thamani kwasababu yako. Moyo wangu umenitoraka, upo kwako. Umeuvuta kwa Raha za penzi lako. Nakupenda sana Mpenzi.

SMS hizi ni nzuri kwako? Kama ni nzuri unaweza tumia Bure kwa unaempenda. Usisahau kuangalia sms nyingine za mapenzi ndani ya The bestgalaxy na useache kuifuatilia pia. Asante sana kwa muda wako ulioutoa kusoma makala hii.

SMS za kumsifia mpenzi wako (Mwanamke au Mwanaume)

Karibu the bestgalaxy na hapa katika makala tunaenda kuangalia SMS za kumsifia mpenzi wako. Hakuna raha kama kusifiwa na mtu unaempenda. Mtu ukisifiwa na unaempenda toka moyoni unaweza hisi Duniani upo juu na wathamani sana. Kiufupi maneno mazuri ya kusifu yakitoka kwa wapenzi au watu tunao wapenda huwa yanaupasua moyo kwa furaha na kufanya tuhisi kuwa tunathamani. Hivyo ukitaka kuugusa moyo wa mpenzi wako kwa kiasi hicho si vibaya ukatumia sms nzuri za mapenzi za kumsifia mpenzi wako. Hii inaweza kufanya awe na furaha, aione thamani yake na kujua umetambua thamani yake pia.


Kupitia ujumbe mfupi wa SMS, unaweza kumwambia mpenzi wako jinsi unavyomheshimu, kumjali, kumkumbuka na kwanini upo hivyo kwake. Unaweza fungua moyo wako kwake na kumwagia sifa zake zote nzuri.
Makala hii imekukusanyia ujumbe au sms ambazo unaweza kutumia kumsifia mpenzi wako mwanaume au mwanamke ili ajisikie vizuri na kujua jinsi unavyomthamini. Kama utahitaji unaweza ziangalia hapa sms chini

Zawadi za kumpa mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

SMS za kumsifia mpenzi wako (mwanaume au mwanamke)

  • Ninafuraha kwakua nina Bahati sana. Bahati ya kwanza ni kufikia siku ya Leo na bahati ya pili ni kuwa na wewe mpaka leo. Nitakupenda Milele mpenzi wangu, wewe ni mtu muhimu kwangu.
  • Ivi ni nani alikufundisha Mapenzi? Yani hata kukuchiti siwezi, naona ushenzi. Nanenepa kwa Mahaba yako na chini ya shuka nakula mpaka mfupa, sitemi.
  • Najua huwenda kunasiku unahisi umewahi niudhi na kuna pia siku unahisi unanifurahisha. Lakini ukweli ni kwamba nazifurahia siku zote nilizokua na ntazokua na wewe. Nakupenda sana furaha yangu.
  • Hapo zamani nilikua naomba mungu nikutane na mwanaume jasiri, anaenipenda, anae nijali na kunithamini. Nashukuru mungu kwa kunileta karibu nawe. Mwanaume upo moyoni, unazunguka kwenye damu mpaka akilini. Nakupenda honey.
  • Wanasema “mapenzi ni matamu” ni kweli, umenipa nikaamini. Wanasema “Raha ya mapenzi umpate anae kupenda na kuyajua” hata siwezi pinga maana Raha naiona tangu ulivyoungana na mimi. Nakupenda na sihitaji kutoka penzini.
  • Mapenzi unayonipa yamenifanya nione maajabu. Siku hizi nikifumba macho sioni giza, nakuona wewe. Moyo unajawa na furaha, najikuta natabasamu kila nikikuwaza wewe. Yani naishi maisha ya furaha kwasababu nimekuchagua wewe.
  • Kila siku nikikutazama nakuona mpya katika uzuri wako. Na unanivutia kiasi ambacho tukiwa karibu natamani kugusisha moyo wangu na wako. Nimeisha kuwa teja wa penzi lako.
  • Nilikua natamani kupata na kumpenda mtu mwenyewe sifa nyingi nzuri. Nashukuru mungu kunikutanisha na wewe. Nimekupata sasa, nakupenda na napenda jinsi ulivyo.
  • Nilipokua mdogo nilikua napenda sana kuangalia mwezi na nyota angani. Zilikua zinanivutia sana kila nikizitizama. Siku hizi napenda kuangalia macho yako. Ni mazuri zaidi sana.
  • Lips tu ni tamu zaidi ya pipi, na vingine vitamu havielezeki, nitavitoa wapi kama si kwako? Huniishi hamu na wala wewe si bigG, hivyo sahau swala la mimi kuondoa moyo wangu kwako.
  • Huwa napenda vile unavyo vaa, unajipatia wewe malaika. Ni msafi unaependeza. Unakua kama nyota inayong’aa angani ambayo mungu ameichukua amenipa.
  • Ndoto yangu ya kuwa na mtu ninaempenda maishani, ilianza kutimia nilipokutana na wewe kipenzi changu. Kwasasa nipo pamoja na wewe, najiona naishi kwenye ndoto yangu, Nakupenda sana.
  • Macho yangu yakikutana na yako, moyo wangu hulipuka kwa furaha. Wewe ni mzuri kama malaika ulieshushwa kwangu, namuomba mungu, usiote mbawa.
  • Hakuna njia ya kuachana na mimi isio niumiza. Siwezi kukupoteza alafu nikwa na furaha au bila kuumia. Nimekuweka moyoni mpenzi, wewe ni muhimu kwangu . Nahisi nakupenda.
  • Mambo mazuri yote nilianza kuyaona maishani nilipokupata wewe. Umekua ni mwanamke mzuri unaevutia mambo mazuri kama ulivyo wewe.
  • Maua hufanya bustani ipendeze na kuvutia. Upendo wako wewe, hufanya nijione wa thamani kwenye hii Duniani. Nakupenda sana.
  • Uwezo wako wa kunitambua na kuelewa ninachohitaji bila kusemwa, hufanya mahusiano yetu kuwa ya kipekee sana. Unanipenda sana, najua. Na Mimi nakupenda kuliko unanyojua. Nitaishi nikiwa nawe moyoni mpaka mwisho wa Dunia.
  • Unajua kupenda malaika wangu. Penzi lako hufanya nione bahati kuwa na wewe. Sauti yako, hunibembeleza. Najihisi kuishi mbingu ya saba na upendo wako ndio umenileta.

Sms hizi zimewekwa hapa kwaajili ya watu wa Jinsi zote. Kama ni mwanaume unataka kumtumia mwanamke/mke unaempenda, unaweza pata sms inayofaa. Na hata ukiwa mwanamke pia unaweza pata sms kwaajili ya Mwanaume/mme. Wakati ukifurahia hayo, endelea kuwa karibu na The bestgalaxy.

SMS za mafumbo ya Mapenzi kwa umpendae

Kama umezoea kumtumia sms za kawaida za mapenzi mwenza wako ni jambo zuri lakini tambua kuwa kuna sms za mafumbo za mapenzi ambazo ni nzuri pia kumtumia mtu unaempenda. Sms za mafumbo ya mapenzi ni sms ambazo nyingi ujumbe au maana ya sms huwa inajificha kidogo. Sms hizi  zanafanya mpenzi wako ahusishe ubongo wake kidogo kutambua maana sahihi ya kilicho maanishwa katika ujumbe wa mapenzi anao usoma.

Ni SMS nzuri sana kwa mpenzi na hapa The bestgalaxy tumekuandalia jumbe au SMS za mapenzi zilizochangamana na sms chache za mafumbo unayoweza kutumia kwa mapenzi wako. Kikubwa ukumbuke kuchagua sms inayoendana na hali yenu.

Sms za mafumbo ya mapenzi

  • Sioni ajabu Nzi kufia kwenye kidonda maana hata mimi najiona naweza kubari iwe hivyo nikipambania ninapopapenda. Milele nataka niwe kwako maana ni mahali nimependa.
  • Natamani ujue kuwa wewe ndie umenifanya niijue Radha halisi ya tunda la upendo. Sikuwahi fikilia kuwa siijui mpaka uliponipatia. Staki kukupoteza mpenzi, nimeridhika kuwa nawe, nataka kuendelea kufurahia.
  • Nilikua kila nikisikia simulizi juu ya watu waliopendana mpaka wakaamua kuanza kuishi pamoja, nawaza “wanapendana kiasi gani mpaka wanafikia mawazo hayo?”. Kwasasa nimewaelewa maana hali yangu kwako ni kama yao.
  • Nimezama kwenye penzi lako na staki mtu yoyote wa kuniopoa. Sipatishida, napata Raha. Hata nikitapatapa ni penzi tu limejaa. Sehemu nyingi nimepita ili kwako nije kukaa.
  • Siku Jua likichomoza jioni na kuzama asubuhi huenda labla ndio siku naweza kuwa nimebadilika kwako mpenzi wangu. Napo inaweza kuwa siko sawa. Lakini kama sio hivyo milele utakua wa muhimu kwangu kama pumzi. Nakupenda kipenzi.
  • Hata ungekua ni wewe; fikilia umekutana na mtu maishani anakupa furaha na anajua kujali pia. Mbali na mambo hayo, Bado moyo wako unampenda na hautaki uondoke maishani pia. Hivyo ndivyo jinsi ulivyo kwangu kwangu, Nakupenda my dear.
  • Penzi lako hunifanya ni hisi nipo juu sana. Ni Mbali linanifikisha tena ni zaidi ya usawa wa milima. Sijiwezi, nimeisha chizika sasa, napenda linako nipeleka na nampenda sana anaenipeleka.
  • Ukiziba vizuri masikio kwa mikono yako utagundua kelele zote pembeni hupotea na utulivu tu ndio hubakia. Hivyo ndio penzi letu linaweza kuwa endapo maneno ya watu tutayapuuzia. Nakupenda sana my love.
  • Umekuja kwangu kipindi ambacho nipo kwenye giza nene lakini umekuwa mwanga unaoangaza kila pande. Sasa sijui kitu gani unahisi kitafanya nisikupende? Tambua moyo wangu wote upo kwako na si kipande. Naomba usiniumize.
  • Nimekupatia moyo wangu kama zawadi yako kwa mapenzi matamu unayonipa. Naomba ushike taratibu mpenzi usije ukaniumiza.
  • Wewe ni lile ua ambalo limeota pekee kwaajili ya moyo wangu. Moyoni mwangu unahisi furaha nikikuwaza, nikikusikia na hata kukuona wewe. Pokea salamu Toka kwenye moyo wangu, unakupenda sana.

Unahitaji sms nyingine? Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy. Sms hizi ni moja ya sms nyingi ndani ya The bestgalaxy. Unaweza pitia kurasa nyingine za the bestgalaxy ili kupata mengine zaidi.

SMS za kumfanya mpenzi wako afurahi

Hapa kwenye ukurasa huu tunaenda tena kuangalia za sms za mapenzi unazoweza tumia kwa mpenzi wako. SMS tunazozingatia hapa ni kama ilivyoelezwa kwenye kichwa cha makala hii, yani tunaenda kuangalia sms zile zinazoweza mfurahisha mpenzi. Sio kila sms tutazoangalia hapa zinaweza mfurahisha mapenzi wako lakini kupitia orodha ya sms za mapenzi tulizoweka hapa chini unaweza pata sms nzuri inayoweza kumfurahisha mpenzi wako.

Usimtumie sms bila kufikilia kama ataipenda kwa jinsi unavyo mjua mweza wako. Kiufupi unatakiwa kuchagua sms kulingana na hali ya mahusiano yenu au hali ya mpenzi wako wakati unamtumia.

Mazoezi ya mwili ambayo husaidia katika tendo BONYEZA HAPA>>>

Sms za kufanya mpenzi wako afurahi

  • Asubuhi njema mpenzi wa moyo wangu! Kila siku ninapoanza na wewe, moyo wangu hujaa furaha na upendo siku nzima. Nakutakia siku yenye neema na mafanikio.
  • Leo ni siku ya kipekee kwa sababu nakupenda zaidi ya jana. Na usiwaze kuhusu kesho maana uko moyoni mwangu milele na kesho ntakupenda zaidi ya leo.
  • Ninapopitia picha zetu za pamoja, nakumbuka jinsi kila wakati tunavyopendana na kusaidiana. Kiukweli wewe ni nguzo yangu, na nakushukuru kwa kunifanya niwe na wewe maishani, Nakupenda sana.
  • Nakupenda sana Mpenzi wangu. Unanifanya nihisi nipo kwenye bahari ya mapenzi ambayo kuzama kwenye maji ni Raha na kuibuka raha. Unajua kunisafisha nakuwa mweupe, stamani kwenda kwengine nikachafuke.
  • Ningependa kushare nawe furaha yangu, maumivu yangu, na kila wakati wa maisha yangu. Kila ujumbe toka kwako hunijaza nguvu na matumaini. Nakupenda sana.
  • Hakuna neno la kutosha kueleza jinsi unavyonifanya nijisikie. Kila wakati ninaiona picha yako mbele yangu, moyo wangu unagonga kwa furaha kiwaza kuhusu wewe. Nakupenda sana mpenzi wangu, usije niacha mwenyewe.
  • Nashukuru kwa uwepo wako katika ulimwengu yangu. Umejaza moyo wangu furaha, upendo, na kufanya nitambue maana mapenzi ni nini. Kwangu maana ya mapenzi ni wewe. Nimeridhika kuwa nawe, Nakupenda.
  • Unaponikumbatia, nahisi niko salama na nina amani. Hakuna mahali pengine napendelea kuwa zaidi ya mikononi mwako. Nakupenda na nipo tayari kula kiapo.
  • Nimefurahi sana kuwa nawe katika kila hatua ninayoipiga maishani mwangu. Najua kwamba si kila changamoto tutayokutananayo maishani ni rahisi lakini siwezi yumba nikiwa na wewe kipenzi wangu.
  • Nakupenda sana na napenda vile umejua kunipa ninachotaka na naridhika nikikipata. Nitataka nini tena wakati penzi lako tamu nimenikamata? penzi lako ni hadimu, mbali na wewe siwezi pata.

Ni hayo tu, tuliokuandalia hapa Kwenye ukurasa huu. Usiache kufuatilia The bestgalaxy ili kujifunza mambo mengine yanayoweza kuwa muhimu kwako.

Kuwa mjanja! Tufuate kwenye akaunti zetu mpya za kijamii ; Instagram na Facebook

Ujumbe wa siku ya kuzaliwa kwa Mpenzi au Rafiki

Moja ya siku au tarehe ambazo watu wanaweza ya ona zina umuhimu sana kuzijua kwenye maisha yao ni siku ya kuzaliwa. Na ni kweli zina umuhimu maana katika mambo mengi huwa watu wanahitajika kutaja siku au tarehe ya kuzaliwa. Mara nyingi hii inaweza kuwa ni kwaajili ya kudhibitisha umri maana mtu anaweza kujua umri wako kwa kujua siku uliozaliwa(tarehe,mwezi au mwaka). Umri wa mtu ni tofauti kati ya siku mtu aliozaliwa na siku aliopo.
Katika jamii zetu siku ya kuzaliwa imewekwa mbele sana kwa baadhi ya watu kiasi kwamba inakua inakumbukwa kila mwaka na kusherehekewa. Sio jambo la ajabu na sio jambo la lazima pia.

Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze kila mara BONYEZA HAPA>>>

Kama unampenzi au rafiki anaejali siku yake ya kuzaliwa, unaweza mfanyia jambo lolote la furaha katika siku yake ya kuzaliwa na akafurahi. Na inasemekana hata ambao hawazisherehekei na kuzijali siku zao za kuzaliwa, wanajiskia vizuri sana wakifanyiwa jambo lolote la furaha kuhusu siku yao hiyo. Hivyo ukiwa na rafiki au mpenzi hata ambae hajali kuhusu siku yake ya kuzaliwa, unaweza mfurahisha kwa kuonesha unaijali siku yake.

Katika birthday au siku ya kuzaliwa ya mtu, unaweza fanya mambo mengi kumfurahisha ikiwemo kumpa zawadi au kumtumia ujumbe kwenye simu. Hapa chini tumeweka baadhi ya jumbe au sms za kumtumia mpenzi au rafiki katika siku ya kuzaliwa.

SMS za kumbembeleza mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

Sms au Ujumbe wa siku ya kuzaliwa kwa mpenzi na rafiki

  • Mtu ambea ni mwanga wa maisha kwangu ni wewe. Napenda kila wakati ukumbuke kuwa furaha ya moyo wangu ni wewe. Nakutakia siku ya kuzaliwa yenye baraka tele.
  • Happy birthday rafiki yangu. Nakutakia maisha marefu na yenye furaha. Baraka na mafanikio ziwe katika Maisha yako na kila jema lisiache kukufuata.
  • Heri ya siku ya kuzaliwa rafiki yangu kipenzi. Natumai siku yako itakua nzuri na furaha. Napenda kukuona na furaha hivyo napenda kuona ukifurahia siku hii muhimu kipenzi.
  • Mpenzi wangu, Kuzaliwa kwako ni siku muhimu kwangu. Maana huo ni wakati zawadi yangu nzuri ililetwa toka kwa mungu. Nakupenda sana zawadi yangu, pia nakutakia maisha marefu yenye afya njema na furaha.
  • Happy birthday rafiki mpendwa! Nakutakia kila wakati kupata nguvu na msukumo wa kutimiza matamanio yako hapa Dunia. Maisha ni safari na nakutakia kila jema kwenye safari yako rafiki yangu.
  • Ninafuraha sana Leo maana ni siku mbayo malaika wangu ulizaliwa ili uje kuangaza maisha yangu. Kuwa na wewe na Raha sikufichi. Happy birthday my queen.
  • Nakupenda sana. Napenda jinsi unavyonifanyia katika Upendo na maisha kiujumla. Nafurahi kuwa na wewe. Tunapitia mengi ila daima nitakupenda wewe. Hicho ndio kitu natamani ujue katika siku hii, happy birthday mpenzi!
  • Nakutakia siku njema ya kuzaliwa rafiki yangu. Wewe ni mtu ambaye anamaanisha mengi kwangu na ambaye ninathamini sana wepo wako. Uishi maisha marefu rafiki yangu.
  • Kila siku ninapokuwa nawe ni zawadi kubwa. Siku ya kuzaliwa yako ni fursa kwangu ya kusherehekea upendo wetu. Heri ya siku ya kuzaliwa, mpenzi!
  • Upendo wangu kwako hauwezi kuelezwa kwa maneno yakatosha. Lakini katika siku hii ya kuzaliwa nataka nijaribu tu kwa kumwambia Nakupenda sana na uishi maisha marefu kipenzi changu. Happy birthday!
  • Ningekua na uwezo ningeiweka siku yako ya leo iwe ni siku ya kitaifa my love. Natamani Kila mtu ajue siku ya leo ndio siku mtu alieuweza mayo wangu na kunipa furaha maishani amezaliwa. Nakutakia siku njema na maisha marefu.

Sms hizi au jumbe hizi zina maneno mazuri ya siku ya kuzaliwa kwa rafiki na hata mpenzi. Unaweza zitumia bure kwa mpenzi wako mwanaume au mwanamke au rafiki. Kikubwa uchague ipi ni sahihi kuitumia kwa upande wako.

Kuwa mjanja! Tufuate kwenye akaunti zetu mpya za kijamii ; Instagram na Facebook.

sms za mapenzi kiingereza na kiswahili

Mapenzi ya siku hizi huwa yanahusisha sana sms kwasababu watu wengi kipindi hiki huwa wanawasilina kwa sms(ujumbe). Mara nyingi hapa The bestgalaxy tumekua tukizungumzia sms za mapenzi na hapa Kwenye ukurasa huu pia tunaenda kuangalia upende huu huu wa sms za mapenzi lakini tunajikita katika sms za mapenzi katika lugha mbili. Lugha hizi ni Lugha ya kiingereza na kiswahili. Yani tunaenda kuangalia sms za mapenzi kwa kiingereza na kiswahili.

Kuna sababu zinaweza kufanya ukawa unatumia lugha ya kiswahili lakini ukataka kumtumia mwenza wako sms ya mapenzi ya lugha ya kiingereza (English). Unaweza fanya hiyo ili kuonesha utofauti tu unapochati na mpenzi wako, unaweza kufanya hivyo pia kwasababu mpenzi wako ni mtu asie elewa kishwahili sana au anapenda kiingereza tu.

Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze kila mara BONYEZA HAPA>>>

Kama upo vizuri katika lugha ya kiingereza, unaweza tuliza kichwa na kusuka sms itayo ugusa moyo wa mpenzi wako ikiwa katika kiingereza/English. Lakini kama haupo vizuri sana au unataka kutunza muda, unaweza tumia hizi chini kwa mwanamke au mwanaume.

Ujumbe/SMS za mapenzi 5 za Kiingereza na Kiswahili

Every time I’m with you I feel like my dream has come true. I cherish you always.
Kila wakati ninapokuwa na wewe nahisi ni kama ndoto yangu imetimia. Nakupenda daima.

I love you so much. In your arms, I have found my home. You complete my life in ways I never imagined. I don’t need to lose you in my life my love.
Nakupenda sana. Katika mikono yako, nimepata nyumba yangu. Wewe unanikamilisha maisha yangu katika njia ambazo sikuwahi kufikiria. Sihitaji kukupoteza kwenye maisha yangu mpenzi wangu.

Dalili za mahusiano yanataka kuvunjika na jinsi ya kuokoa BONYEZA HAPA>>>>

Your love is the melody that fills my heart with joy. Thank you for your love honey . I love you.
Mapenzi yako ni melody(wimbo) inayojaza moyo wangu na furaha. Asante kwa upendo wako honey. Nakupenda.

With you, every day is an adventure. Loving you is the greatest journey of my life. I enjoy having you in my life.
Nikiwa na wewe, kila siku ni safari. Kukupenda ni safari kubwa zaidi ya maisha yangu. Nafurahia kuwa na wewe maishani.

Honey, i need you to know that you are the reason I believe in love. Your presence lights up my world.
Honey, nataka ujue kuwa wewe ndiye sababu ya kuamini katika mapenzi. Uwepo wako unang’arisha ulimwengu wangu.

Mwisho; Ni hayo tu tuliokuandalia hapa. Lakini kabla ya kutuma sms za kiingereza unashauriwa kufikilia kama mwenza wako hupendelea kiingereza au laa. Maana kwa watu waliozoea kiswahili hata wakiwa wanajua kiingereza kunaweza kuwa na ugumu wa maneno ya kiingereza kuugusa moyo wake. Yani wanaweza wanajua kiingereza lakini wakasisimuka zaidi wakiambiwa “Nakupenda” kuliko “I love you”.

Kuwa mjanja! Tufuate kwenye akaunti zetu mpya za kijamii ; Instagram na Facebook

Sms za kubembeleza mpenzi wako

Kubembeleza mpenzi wako sio kuwa mjinga. Ni moja katika ya mambo muhimu kufanya unapokua kwenye mahusiano ya mapenzi na mtu anaekupenda. Na kubembeleza hua kuna nyakati zake na sio kila wakati. Unaweza hitajika kumbembeleza mpenzi wako baada ya tukio lililomuumiza hisia zake, baada ya kuchukizwa, kuonesha hali ya kukataa jambo unalohitaji au unapohitaji kumtuliza moyo wake na kumuweka sawa katika penzi lenu.
Kuna baadhi ya watu husema “mimi sjui kubembeleza kwenye mapenzi” au “mimi siwezi kubembeleza kwenye mapenzi” lakini unapaswa kufahamu kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kubembeleza hawaujui.

Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze kila mara BONYEZA HAPA>>>


Kubembeleza mpenzi wako huonyesha upendo na kujali kwako kwake. Yani kunajinsi anahisi unamjali. Kubembeleza mpenzi wako pia kunaweza kuimarisha uhusiano wenu kwa kufanya muwe na maelewano ya amani. Kubembeleza mpenzi wako kunaweza kusaidia kukuza uhusiano wa kimwili na kihisia kati ya wewe na mpenzi wako. Kubembeleza mpenzi wako kunaweza kusaidia kujenga imani kati yenu pia.
Huo ni muhimu wa kubembeleza katika mahusiano ya mapenzi ila kabla hatujaendelea, ukizidi sana kubembeleza inaweza kuwa sio jambo zuri tena. Lakini katika ukurasa huu tunaenda kuangalia sms za kubembeleza mpenzi.
Kutokana na utandawazi, watu hutumia sms kuwasiliana na wapenzi wao. Sasa ukiwa mmoja wa watu hawa, kuna sms ambazo mtu unaweza mtumia mpenzi kubembeleza kwenye mambo mbali mbali kwenye mahusiano yenu. Sms hizo unaweza tulia na kuziandika mwenyewe au unaweza angalia sms zitakazo kufaa hapa chini na kuzitumia.

Maneno ambayo hautakiwi kusema kwa mwenza wako BONYEZA HAPA>>>

Sms za kubembeleza mpenzi wako

  • Wewe ndiye wangu mahabuba unaejua kunipa huba. Mwanamke ambae moyo umeushika. Nitabaki na wewe milele, sitochoka kukupenda malaika.
  • Kuna muda nakaa nawaza jinsi gani naweza fanya ili nioneshe moyo wangu unakupenda kiasi gani ili tu uondoe mashaka juu ya upendo wangu kwako kipenzi. Natamani hata kukupeleka kwa wangu wazazi. Nakupenda sana mpenzi.
  • Usije choka kunipenda honey. Na mimi siwezi choka kukupenda pia. Siwezi hata kuelezea jinsi nafurahi kuwa na wewe dear. Ninapokwambia “nakupenda” moyo wangu ndio unanituma kukuambia.
  • Amini kuwa mimi nakupenda wewe japo wanaonitamani ni wengi. Moyoni mwangu kuna chumba chako wewe, sina vyumba vya wengi na humo upo wewe tu mpenzi.
  • Tumekua hatuelewani sana katika siku hizi. Yawezekana ni shetani amekuja kutuchezea. Hebu tumshinde kwa kuanza siku ya leo vizuri kipenzi. Pamoja na yote tunayopitia, tambua sitamani kukupoteza. Moyo wangu bado unakupenda.
  • Nisikupende wewe ili nimpende nani kwenye hii Dunia? Kuwa na wewe ni ndoto niliokua nasubiri kutimiza hapa chini ya jua. Hakuna anaeweza kuniamsha kwenye ndoto hii zaidi yako. Na sitamani itokee maana nakupenda sana.
  • Ivi katika maisha yako umewahi ona penzi lililodumu kwa kusikiliza sana maneno ya watu? Mimi sijawahi, ila nimeona watu wanaodumu kwa kusikilizana tu. Hebu tupuuze ya watu twende mbele mpenzi wangu, nakupenda wewe tu.
  • Nyakati za usiku wewe hua mwezi na wakati wa mchana wewe unakua jua langu. Kiufupi umekua msaada kila wakati ili nisipote kwenye giza. Nakupenda sana mpenzi.
  • Wewe ni wapeke maishani na ninakupenda, sifikirii kukusaliti na wala sifikirii kukutenda. Nakuomba tuendelee kupendana kila siku siku habbity wangu.
  • Unataka kuondoka kwenda wapi? Unataka kunicha na nani mwenzio? Unataka kuniumiza kweli? Atatibu nani majeraha unayota kuniachia? Hebu tumia dakika chache kufikilia tulipotokea. Kumbuka kuwa nakupenda sana mpenzi wangu.

Mwisho; Sms hizi zinaweza tumika na wanawake au wanaume. Kikubwa unapotumia, hakikisha inaendana na hali yenu ya mahusiano au mazungumzo.

sms za mahaba kwa mume au mke

Kuitwa Mume au mke haimaanishi hauitaji kumwambia mwenza wako unampenda au maneno mazuri ya upendo na mahaba.Watu wengi huisha ingia kwenye hatua ya kuitana mume au mke huwa wanasahau kuambiana maneno mazuri kiasi kwamba wanaweza kuyumbishwa kwenye mahusiano kwa kuanguka kimapenzi na mtu wa nje kisa anawaambia maneno mazuri na kuwasifia.

Kumwambia mke au mume wako maneno ya upendo ni jambo linaoweza mpa furaha na kuona unamjali haijalshi unatumia sms au unaongea moja kwa moja. Kama unataka kumtumia mke au mume wako sms za mahaba,hapa chini kuna orodha ya sms za mahaba kwa mume au mke ambazo unaweza tumia bure kabisa. Chagua zinazoendana na hali yako ya mahusiano ndio utumie.

Maneno ambayo hautakiwi kusema kwa mwenza wako BONYEZA HAPA>>>

sms za mahaba kwa mume au mke 

Umeuweza moyo wangu mpaka nahisi umeniloga. Unaupa raha moyo wangu nikikukosa pembeni yangu napata homa. Pezi lako ni tamu na kila siku linazidi kunoga. Kwako nimefika vya wengine siwezi onja.

Salamu yako ni nusu ya uhai wangu na kuikosa nisawa na kuidhulumu nafsi. Ukweli ni kwamba nikipata salamu yako huwa najisikia faraja moyoni mwangu, Nakupenda sana wangu.

Kuishi na wewe  ni raha sana. Penzi lako ni zawadi niliopewa na mungu katika maisha maana linanifanya nione thamani ya kuishi dear. Nitakupenda milele bila kujutia.

Mazoezi ya mwili ambayo husaidia katika tendo BONYEZA HAPA>>>

Umenifanya nijione wa thamani toka pale uliponichagua kuwa wako maishani. Kwenye milima na mabonde umepambana mpaka sasa umekuwa na mimi. Asante kwa upendo huu honey, nitakupenda milele maishani.

Wewe ndie mfalme wangu, Mwanaume ninaekupenda kwenye dunia hii, Mtu ninaejivunia kuwa nae maishani na natamani popote alipo ajue kuwa pamoja na yote tunayopitia kwenye maisha, bado ameteka hisia zangu.

Acha leo nikwambie ukweli. Thamani ya penzi unalonipa ni kubwa kwangu na siwezi fananisha na chochote kwenye hii dunia. Namshukuru mungu kwa kunikutanisha mpenzi mwema unaejali hisia za moyo wangu, Nakupenda sana mpenzi, usichoke kunipenda.

Wewe ndie malaika wangu, Fundi wa raha zangu, Msaidizi niliepewa na mungu, Mwanamke mzuri ninaempenda kwenye ulimwengu mpaka nikaamua kumchagua yeye tu maishani mwangu na sasa natamani ajue kuwa sijawahi jutia kuwa nae maishani, upendo wake unanipa furaha isio na kifani.

Penzi letu haliwezi kuvutia kuila mtu hapa duniani. Natamani uzibe sikio la kusiliza wengine na unisikilize mimi tu. Ninaposema nakupenda nasema toka moyoni. Usisikilize ya watu mpenzi mimi nakupenda wewe tu hapa duniani.

Sms za mapenzi motomoto (Mahaba niue)

Kuna muda ukiwa kwenye mahusiano, unaweza tamani kumwambia maneneo ya mahaba moto moto mpenzi/mme/mchumba wako kwa njia ya ujumbe. Hili ni jambo hufanyiana wapenzi hasa mukiwa na upendo wa kweli kati yenu alafu munatumia sana simu kuwasiliana. Watu wengi wanapopokea jumbe au sms za mahaba toka kwa wawapendao, hufurahi.

Kama unataka kumtumia mpenzi wako sms za mapenzi motomoto basi hapa The bestgalaxy tunakupa sms za mapenzi motomoto ambazo unaweza mtumia mpenzi wako bila kuumiza kichwa sana. Kama utaona ni nzuri na zinaendana na mahusiano yako ya mapenzi, uaweza zitumia.

Maneno ambayo hautakiwi kusema kwa mwenza wako BONYEZA HAPA>>>

Sms za mapenzi motomoto (Mwanaume na Mwanamke)

  1. Siku hizi nanenepa kutokana na matunda unayo nipatia. Kila nikila nazidi kukung’ang’ania. Nafikiri wewe ndie mungu alinishushia maana umenipatia dear.
  2. Napenda kugusa ngozi yako laini kila nikiwa karibu yako. Kila ninapoigusa nahisi raha na msisimko. Hakika umeumbwa vizuri wewe mtoto, hahaha.
  3. Natamani unikumbatie nipate joto hapa nilipo. Natamani vitu vingi toka kwako japo siwezi sema. Nimekukumbuka sana mpaka nahisi siwezi hema.
  4. Natamani kusikia sauti yako mpenzi wangu. Unasauti nzuri inayougusa moyo wangu na kuulipua kwa furaha. Natamani tuishi pamoja ili niwe naisikia kila mara. Wewe ni tulizo la moyo wangu nakupenda sana.
  5. Natamani niwe na wewe kila siku,kila saa na kila dakika. Penzi lako moto naliitaji mpaka mwisho wa maisha. Nilikua naona mapenzi mabaya ila wewe kunakitu umenifundisha. Nakupenda zaidi ya sana.
  6. Ningerudi nyuma na kupewa nafasi ya kuchagua tena mtu ninaempenda, anaenifanya niwe na furaha na kunipa penzi linalo gusa moyo wangu bado ningekuchagua wewe. Nakupenda sana mpenzi wangu.
  7. Kukupata wewe kunanifanya nijione mwenye bahati sana katika dunia. Sijui sana kuhusu moyo wako ila tambua moyo wangu umeishazama katika penzi mpaka naogopa. Umeishaniteka sijiwezi mpenzi.
  8. Kuna watu niliwakaribisha kwenye maisha yangu wakanifanya nione mapenzi mabaya. Penzi lako nimefanya nione mapenzi matamu na sitamani niamshwe kwenye hii ndoto. Nakupenda sana.
  9. Nimeacha vitu vingi sana kwaajili yako na siwezi jutia maana unanipa furaha mpenzi wangu. Atuwezi kuwa sawa kila siku ila tambua nazidi kukupenda kila siku. Wewe ndie nimekuchagua moyoni na ndie daktari unaeweza tibu maradhi yangu. Wewe ni mtu wa thamani maishani mwangu.
  10. Penzi lako tamu, haliishi hamu. Upendo wangu kwako ni moto usiozima. Moyo wangu unalidunda jina lako na kila mara natamani kuwa karibu yako. Sijawahi penda kama hivi.

Mambo ya kushangaza usioyajua kuhusu Wanawake na Wanaume BONYEZA HAPA>>>

SMS nzuri kwa mpenzi aliembali(mapenzi ya mbali)

Ni kawaida sana kuona  wapenzi wanaopendana kukutana na sababu mbalimbali zinazopelekea wapenzi hao kuwa mbali. Sababu hizi zinaweza kuwa ni kazi, masomo na mambo mengine katika maisha. Wapenzi ambao wako mbali au  wanaoishi mbali ni vema wakazingatia sana mawasiliano na kuonyeshana upendo katika mawasiliano. 

Hapa The Bestgalaxy leo tunakupa orodha ya jumbe fupi za mapenzi ya mbali zinazoweza kutumika katika kuwasiliana. Kama mahusiano yapo kwenye hali hii basi unaweza tumia jumbe hizi:

Jinsi ya kuwa romantic kwa mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

sms za mapenzi ya mbali

1. Umbali wowote kati yetu hauwezi kuuzima upendo wangu kwako Mpenzi. Kila siku nakuwaza na nazidi kukupenda tu huku natamani sana uwekaribu yangu.

2. Kukaa mbali na wewe ni kazi ngumu sana mpenzi wangu. Kuna muda natamani nije huko uliko niwe na wewe ila nikikumbuka kuwa kuna siku tutaonana, napata amani kidogo, Nakupenda sana.

3. Hata kama tuko mbali kimwili, moyo wangu daima uko nawe huko uliko. Nakupenda sana.

4. Napenda tunanyowasiliana, unanifanya nijisikie karibu nawe japo tuko mbali. Kichwa changu na moyoni mwangu bado upo wewe mpaka tutakapokutana tena.

5. Kuna malaika wa upendo nimenitokea na kuniambia kuwa penzi letu linapendeza. Umbali hauwezi kututenganisha mpenzi wangu, tuendele kuwa pamoja milele.

6. Usiruhusu shetani atumie mwanya wa sisi kuwa mbal,i kuua penzi letu. Penzi letu ni kubwa kuliko umbali wetu. Siwezi kukuona au kukugusa huko uliko ila tambua moyo wangu wote upo kwako.

Jinsi ya kutunza mahusiano ya Mbali BONYEZA HAPA>>>

7. Sikuizi nakosa joto lako tamu unalonipa pindi nikigusa mwili wako. Lakini bado nakupenda kwa nguvu zote. Jina lako limeandikwa ndani ya moyo wangu na haliwezi futika milele. Unaeweza fanya niumie au niendelee kufurahi ni wewe.

8. Moyo angu hulipuka kwa furaha kila tunapowasiliana. Hii ni kwasababu nakupenda na siku zinavyozidi kwenda, nazidi kukupenda leo kulio jana. Sipati picha nitakavyokua tukikutana.

9. Moyo wangu uko nawe, hata kama mwili wangu uko mbali na wewe. Umbali hauwezi yumbisha penzi langu  kwako. Nikishindwa kuvuilia nipo tayari kukufuata na sio kukuacha kipenzi changu.

10. Jukumu la kulinda penzi letu ni langu mimi na wewe mpenzi. Tunapokua mbali au karibu ni vema tukakumbuka jukumu letu mpenzi. Tusije ruhusu walioharibu mapenzi yao waalibu na yetu. Nakupenda sana.

Jumbe au sms kama hizi zinaweza kusaidia kuimarisha uhusiano wenu wa mbali na kumfanya mpenzi wako ajisikie kuthaminiwa na kupendwa. Pia ni vema kukumbuka kuwa mawasiliano ya mara kwa mara na jitihada za kukutana zinaweza kuwa na mchango mkubwa kwenye uhusiano wa mbali.