Tag Archives: simulizi

USIKU SIUTAKI (Simulizi Fupi ya Kusoma)

Maisha yangu yamekuwa si rahisi. Nimekulia mtaani, na kila siku ilikuwa ni kupambana ili nipate chakula na mahitaji ya kila siku. Mara nyingi nilikuwa nafanya kazi za vibarua sehemu mbalimbali. Mtaa wetu ulikuwa na maisha ya kawaida sana, watu walijitahidi kupambana kila siku ili kuishi, wengine wakiwa na biashara zao ndogondogo. Ni kama shughuri za kuimaisha hapo mtaani nilikutana na Mama Cheupe, mama mtu mzima kidogo aliyekuwa akiuza chakula kwenye kibanda maalufu katika maeneno yetu. Alikua na mwilini mkubwa alafu anajipenda sana.

Kwanza, aliniweka kama mteja wa kawaida tu. Nilikuwa napita pale kibandani mara kwa mara baada ya kazi, nikiwa na njaa. Mama Cheupe alikuwa mkarimu sana kwangu. Kuna wakati alikukua akiniuzia chakula kwa bei ya chini au hata kunipa bure kabisa. Ilikuwa ni kama alinijali kwa namna fulani, na nami sikuchukua muda mrefu kuelewa kwamba alikuwa akinisogeza zaidi kwake maana kujali kwake kulipita kiasi.

Siku moja, aliniambia nikipata muda niende nyumbani kwake. Mume wake alikuwa safarini kwa siku mbili, na alikuwa anataka tu niwe karibu nae eti ili nimpunguzie upweke. Nikiwa kijana mdogo, nilivutiwa na nafasi hiyo, japo moyoni nilijua ni hatari lakini moyo ulikua unatamani tu bila sababu.
Kwanzia hapo, mahusiano yetu ya siri yalianza. Kila mume wake akisafiri alikua akinitafua na kuniambie niende kwake. Tulikua tukishiri mapenzi, na mara nyingine nilikua nalala mpaka asubuhi. Nilikua na hofu moyoni lakini hiyo hofu ilikua ndio kama unaongeza ladha ya penzi hivi kwa muda huo. Alikua ananisifia sana huku akimponda mme wake. Pamoja na mwili aliokua nao, vita vikianza nilikua nahakikisha yeye ndio anachoka balaa. Kwaiyo alikua haishi kunisifu na kunihitaji. Alikua anashawishi sana.

Nilijua kuwa hili jambo ni hatari sana, na haliwezi kuwa endelevu. Kuna siku ilikuwa ni usiku nipo nimelala na yule Mama. Mume wa Mama Cheupe alikuwa amesafiri tena, nami nikaenda nyumbani kwake nifurahi na Mama Cheupe na kulala huo. Tulikaa, tukala na baadaye nikalala pale kama kawaida.

Lakini usiku huo mambo yalibadilika ghafla. Nikiwa nimelala, tulisikia hatua za mtu nje ya nyumba. Mwili wangu ukakosa nguvu, moyo ukadunda kwa kasi. Tulikua tu Mume wa Mama Cheupe alikuwa amerudi ghafla. Na sisi mara moja tulihisi kuna kitu hakiko sawa nje. Aliposogea karibu na mlango, mimi nilichanganyikiwa mno lakini Mama Cheupe alikua makini sana hata kuliko mimi. Nakumbuka alionyesha mlango wa nyuma wa nyumba hiyo ambao ni mbali na ule anaotaka kuingilia Mume wake.
Basi na mimi niliamua kufanya jambo moja tu ambalo ni kukimbia. Kwa haraka niliinuka kitandani, nikavaa viatu vyangu na kwa kasi nikatoka nje kupitia mlango wa nyuma. Ile nimeisha uacha mlango nikakuta mwanga mkubwa wa tochi umenimulika ghafla. Mh nilishtuka sana nikaanza kukimbia lile eneo huku nikiukwepa ule mwanga. Wakati nikifanya hivyo nilisikia kelele za mwizi zikitoka kwa aliekua ananimulika. Nilichanganyikiwa maana ilikua ni sauti ya Mume wake Mama Cheupe na alikua akiita watu.

Nilipiga mbio nikielekea vichochoroni, bila hata kugeuka nyuma mara nyingi. Nilikuwa na hofu ya kufa, nilihisi kama ndio nakufa hivyo maana kwa usiku ule, watu wakiamka watadhani mimi ni mwizi kweli alafu wanaweza niua bila kunisikiliza. Sikuweza hata kupumua vizuri mpaka nilipokuwa mbali na nyumba ya Mama Cheupe.
Nilivyofika ninapolala, sikua nikiamini hata kama nimepona. Nilikaa chini na kufikiria vizuri jambo lililonitokea maana lilikua linaenda kuchukua uhai wangu kabisa na sikua na uwezo wa kubisha kuwa si mwizi kwa usiku ule. Ni bola hilo jambo lingenikuta mchana kuliko usiku.

Siku iliofuata niliongea na Mama Cheupe. Aliniambia Mume wake hakugundua kuwa kuna jambo lolote lilikua likiendelea kati ya mimi na yeye usiku ule. Yani alichojua yeye ni kuwa kulikua na mwizi pale nyumbani na mwizi huyo ndio mimi. Inamaana hata ningekufa usingejulikana ukweli wowote kuhusu mimi. Usiku ungeyafunika yote yaliokua yakiendelea.

Kwanzia siku hiyo niliona japokua usiku unaficha mambo mengi na kuyafanya Matamu, lakini Usiku ni hatari sana. Unawezaje kuwaelewesha watu kuwa wewe sio mwizi wakati wanakuona unakimbia maeneo yao Usiku?🤔

KASINGO MAMA 1 (Simulizi Fupi ya Kusoma)




Nilipokuwa mdogo, nilikuwa na ndoto kubwa ya kuondoka kijijini kwetu na kwenda kusoma chuo kikuu. Wazazi wangu walikuwa wakulima, na ingawa maisha yalikuwa magumu, walinipa moyo kila siku kwamba elimu yangu ingeweza kubadilisha hali ya familia yetu. Mwishowe, ndoto zangu zilianza kutimia nilipopata nafasi ya kusoma chuo kikuu. Niliondoka nyumbani nikiwa na imani kuwa kila kitu kitakuwa sawa. Nilipokua nikiwaaga wazazi wangu, walikuwa na furaha sana, lakini machozi ya huzuni yalinitiririka nilipo ona namwacha dada yangu Zena nyumbani pale nyumbani.

Zena alikuwa na mtoto mchanga ambaye alizaa mwaka uliopita baada ya kupitia kipindi kigumu kwenye maisha yake alipo safiri kwenda mbali kidogo na nyumbani. Alipewa ujauzito na mwanaume asiyemjua vizuri maisha yake. Mwanaume huyo alimtelekeza mara tu alipomwambia kuwa ana mimba. Na mbaya zaidi Zena alipata virusi vya Ukimwi (HIV) kutoka kwa huyo mwanaume. Pamoja na yote alikua ni mtu anae jipenda kuliko kawaida. Ila mimi ninaejua alioyapitia, nilipokuwa nikimwangalia Zena na kufikilia changamoto zake, nilihisi huruma sana kwa Dada yangu. Niliondoka nikiamini kuwa mafanikio yangu chuoni huenda yatakuwa muhimu kwa Dada na familia yetu kiujumla.

Nilipofika chuoni, maisha ya huko yalikuwa mapya kwangu. Nilijitahidi kwenye masomo, nikakutana na marafiki wapya, na hata nikapata mpenzi wangu wa kwanza aitwae Juma. Huyu Juma tulikuwa na urafiki mzuri na baadaye tukaanza uhusiano wa kimapenzi. Uhusiano wetu ulikuwa wa furaha na upendo. Lakini haikuchukua muda mrefu kabla ya maisha yangu kuelekea mwelekeo mwingine. Mwalimu mmoja mgeni chuoni alianza kuvutiwa na mimi na akaanza kunivutia kwa ahadi za pesa na maisha mazuri.

Mwalimu huyo alikuwa na pesa na alikuwa tayari kunipa zawadi nyingi ili nimpe nafasi ya kuwa mpenzi wangu. Kwa muda, nilijaribu kumpuuza na kumkataa, lakini alizidi kunitafuta na kunisumbua. Alianza kunisumbua kwa njia ya zawadi na pesa. Ingawa nilihisi vibaya kumpokea mwanzo lakini mwisho nilijikuta nikiwa katika uhusiano wa siri naye. Nilijihisi nikiwa nimechanganyikiwa katikati ya upendo wa Juma na tamaa za mwalimu. Mapenzi ya Juma yalikua yananipa Raha na amani lakini mapenzi ya Mwalimu yalikua yananifanya niishi vizuri hapo chuoni maana pesa alizokua akinipa zilikua zikinisaidia. Kuna muda Juma pia aliwahi saidiwa na pesa za huyu Mwalimu maana alikua na shida alafu nikampatia.



Yule Mwalimu kuna jinsi alirahisisha maisha yangu ya hapo chuoni mpaka nikawa naona aibu kumkatalia jambo lolote analohitaji. Kuna siku alinipelea sehemu tukale chakula cha mchana lakini tulivyoenda alizidisha mizunguko mpaka nikajikuta nipo nae nyumba ya wageni. Aliniomba nilale nae ili aone japo kidogo kitu ambacho nakificha Kila siku kwenye mwili wangu. Na mimi kwajinsi alivyokua ananihidumia, ilikua ngumu kutamka neno “Hapana” au “Staki” kwa jambo analoliomba muda huo. Sikua na jinsi, nilimruhusu angurume na kuguna “mmmh.. mmh” kwenye uwanja wangu huku nikiwa naisikia ile radha tamu isio na kifani.
Mbali na siku hiyo tuliendelea kufanya matukio kama hayo mengi sana huku nikiendelea kumfichia Juma asijue lolote maana nilikua nampenda alafu yupo vizuri. Niliishi chuoni nikiendelea kufurahia mapenzi kutoka kwa wanaume hao wawili, Juma na Mwalimu.



INAENDELEA…

Bonyeza kitufe kilichoandikwa “WhatsApp” hapa chini ili tukupatie simulizi hii usome mpaka mwisho BURE kabisa!

SIRI NA SHEMEJI (Simulizi fupi ya Kusoma)

Anisa alikuwa mwanamke mzuri, mwenye heshima na upendo kwa mume wake, Kevin. Ndoa yao ilikuwa changa, yenye matumaini makubwa na ndoto za baadaye. Hata hivyo, nyuma ya tabasamu zake za kila siku, Anisa alikuwa anabeba siri nzito.

Muda mrefu uliopita kabla ya kuolewa na Kevin, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na rafiki wa karibu sana wa mume wake aitwaye Marcus. Uhusiano huo ulivunjika kutokana Marcus kumuacha Anisa. Anisa alipoamua kuwa Kevin ndiye mwanaume wa maisha yake, Marcus alitambuliswa na Kelvin kuwa ameoa mwanamke aitwae “Anisa” na ndio atakua Shemeji yake. Marcus alikubari swala hilo na wala hakutaka kuuongelea uhusiano wake na Anisa kwa Kelvin. Lakini moyoni, Marcus hakuwa tayari kuachilia uhusiano wao wa zamani na Anisa. Alianza kumtafuta tena Anisa kwa njia za siri, akimtumia jumbe za kimapenzi kila mara, na kumfanya asiwe na amani.

Anisa hakutaka kumuumiza mume wake wala kuharibu urafiki wa Kevin na Marcus, hivyo aliamua kubeba mzigo huo kimya kimya. Kila wakati alipokea jumbe za Marcus, alifuta haraka, akijaribu kusahau na kuishi kama hakuna kilichokuwa kikiendelea. Lakini usumbufu huo ulianza kumkosesha amani na kumfanya kuwa na mawazo mengi.

Kevin aliona mabadiliko hayo kwa mke wake. Alianza kuhisi kuwa Anisa anaficha kitu. Tabasamu lake lilikuwa la bandia, na mara nyingi alikuwa kwenye mawazo. Moyo wa Kevin ulianza kumshuku mke wake. Alihisi kuwa huenda Anisa alikuwa anamficha jambo zito. Ili kupata ukweli, aliamua kuchunguza simu ya mke wake bila ridhaa yake.

Alishika simu ya Anisa wakati alipokuwa amelala, akafungua meseji. Ndani ya meseji hizo, aliona maneno ya kimapenzi kutoka kwa rafiki yake wa karibu, Marcus. Kevin alichanganyikiwa. Bila kujiuliza mara mbili, aliamini kuwa Anisa alikuwa amemsaliti kwakua na mahusiano ya mapenzi na rafiki yake wa karibu.

Hasira na huzuni zilimjaa Kevin na alimwambia mkewe kuhusu jambo alilolikuta kwenye simu yake. Hakutaka kusikiliza chochote maana mawazo ya kifo yalimwingia kichwani. Hakuwa na nguvu za kuongea na Anisa wala kwenda kukabiliana na rafiki yake.
Bila kumkabili Anisa au kujaribu kuelewa zaidi, aliondoka nyumbani akiwa amejaa maumivu, akitembea kwa hasira barabarani.

Alifika kwenye barabara yenye magari mengi, moyo wake ukiwa umevunjika kabisa. Alitamani maumivu hayo yaishie haraka, na hakuhisi tena thamani ya kuendelea kuishi. Ghafla, gari lilikuja kwa kasi na kumgonga Kevin, likamrusha pembeni.

Anisa, akiwa ndani ya nyumba, alihisi kuna jambo baya lililokuwa limetokea. Aliposhindwa kumtafuta Kevin kwa simu, moyo wake ulijawa na hofu. Baada ya muda, alipokea simu kutoka hospitali: “Mume wako amepata ajali mbaya, anahitaji matibabu ya haraka.”

Anisa alikimbilia hospitali, machozi yakimtiririka, moyo wake ukiwa umejaa wasiwasi. Alipofika, aliambiwa kwamba Kevin alikuwa hajafa, lakini alikuwa katika hali mbaya sana, hawezi kuzungumza, wala kuutikisa mwili wake. Ajali ile ilimwacha na majeraha ya ndani yaliyoathiri uwezo wake wa kufanya mambo.

Anisa alilia kwa uchungu, akijilaumu kwa kilichotokea. Alijua tu kuwa Kevin alikuwa kwenye hali hiyo kwa sababu ya tukio la kuona Jumbe za Marcus kwenye simu yake. Alijaribu kumjulisha hayo Marcus kuhusu ajali hiyo na kile kilichosababisha Kevin apate ajali. Marcus, aligopa sana jambo hilo, aliamua kukimbia mji haraka, akiacha kila kitu alichokua akifanya. Hakutaka kukabiliana na matokeo ya vitendo vyake.

Siku zilibadilika kuwa wiki, na wiki zikawa miezi. Anisa hakukata tamaa. Aliendelea kumtunza Kevin, akihakikisha anapata huduma bora zaidi hospitalini. Kila siku, alikuwa pale akimshika mkono, akimuombea apone na kurudi kuwa yule mume aliyempenda. Ingawa Kevin hakuweza kusema wala kutikisa mwili wake, macho yake yalimuonyesha mazuri yote aliokua anafanya Anisa kwa wakati huo.

Baada ya miezi mitatu ya mapambano ya kiafya ya muda mrefu, Kevin alianza kuonyesha dalili za kupona. Polepole, alianza kupata nguvu za kuzungumza na kutikisa mwili wake tena. Aliona upendo ambao hakuutarajia kutoka kwa Anisa, aliyeendelea kumhudumia licha ya hali ngumu waliyopitia. Kila siku, Anisa alimwomba msamaha kwa kile kilichosababisha maumivu yote hayo, akimweleza ukweli kuhusu Marcus na jinsi alivyojaribu kutaka awe nae bila mafanikio.

Kevin, akiwa sasa na akili iliyotulia na moyo uliopata nafuu, alitafakari upendo wa Anisa na kujitolea kwake. Ingawa aliumizwa na yaliyotokea, aliweza kuona kuwa Anisa hakumsaliti ila alikuamejaribu kumlinda kwa Siri tu. Aliamua kumsamehe mke wake, akifahamu kuwa mapenzi yao yalikuwa na nguvu ya kustahimili dhoruba hiyo nzito.

Mwisho, walirudi nyumbani pamoja wakiwa na upendo zaidi ya sana. Waliahidi kutokuwa na siri tena, wakifahamu kwamba kusikilizana na uaminifu ndiyo msingi wa ndoa yao.

Umejifunza nini kupitia simulizi hii? Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy.

KAMA WEWE (Simulizi ya Sauti)

Simulizi ya “KAMA WEWE” ya kiswahili ni simulizi inayopatikana katika The bestgalaxy na unaweza sikiliza Bure kabisa. Simulizi hii ni fupi sana lakini imebeba ujumbe mzuri kuhusu maisha na mafanikio katika hayo Maisha.

Simulizi ya Sauti ya kama wewe

Hii ni moja ya simulizi nzuri sana kuisikiliza kama Burudani huku ukijifunza. Sote tuna jua kuwa mtu unapojifunza kupitia hadithi za watu wengine, tunapata mwanga juu ya mbinu walizotumia kukabiliana na changamoto.

WEUSI WEUPE (Simulizi ya Sauti)

Hapa The bestgalaxy tumekuletea simulizi iitwayo “WEUSI WEUPE”. Simulizi ya WEUSI WEUPE ni Simulizi inayoelezea kuhusu viumbe wa ajabu wanaweza kuishi katikati ya binadamu. Ni moja kati ya Fiction stories fupi na nzuri zilizo katika Lugha ya Kiswahili. Unaweza furahia kusikiliza simulizi hii, hapa chini.

Sehemu ya 1
Sehemu ya 2
Sehemu ya 3 (Mwisho)

Kusikiliza hadithi(simulizi) ni muhimu sana katika maisha yetu kwa sababu kunatusaidia kujifunza na kuelewa masomo ya maisha kutoka kwa wengine. Hadithi zinabeba maarifa, busara, na maadili ambayo yanaweza kutusaidia kufanya maamuzi bora na kushinda changamoto mbalimbali. Kwa kusikiliza hadithi, tunapata fursa ya kujifunza kupita maisha ya wengine, kujua mbinu walizotumia kukabiliana na matatizo, kuepuka makosa waliyoyafanya na hata kuburudika tena. Hii inatufanya tuwe na ufahamu mkubwa zaidi wa maisha na kutuwezesha kuboresha mienendo yetu.

Mguso Wa Dhahabu (Simulizi ya Sauti)

Karibu katika simulizi fupi ya sauti unayoweza sikiliza hapa The bestgalaxy. Simulizi hii inahusu Mfalme mpenda Dhahabu aliwahi hitaji kuwa mtu mwenye utajili kuliko watu wote Dunia.

“The Bestgalaxy” ni jukwaa maarufu linalotoa simulizi za sauti pia. Simulizi hizi zimeandaliwa kwa umahiri mkubwa. Kupitia The bestgalaxy wasikilizaji wanapata fursa ya kuingia katika dunia za kufikirika na kushuhudia matukio ya kusisimua, ya kichekesho, na hata ya kuhuzunisha. Mbali na kusikiliza, msikilizaji anaweza soma simulizi na kufurahia muda wake. Tunaweza sema The bestgalaxy inafanya iwe rahisi kwa mtu yeyote mwenye simu au vifaa vingine kufurahia burudani bora bila matatizo.

MIAKA IJAYO (Simulizi ya sauti)

Teknolojia imekua na msaada mkubwa sana katika maisha ya binadamu na imemuwezesha kufanya vitu vingi sana.

Wananadamu wamekua wakiiendeleza Teknolojia Kila siku kiasi kwamba inasemekana inaweza fikia wakati maisha ya binadamu yanaweza kuwa ya ajabu kuliko hivi sasa.

Sikiliza makala hii sehemu ya kwanza mpaka ya mwisho kupata picha ya maisha ya binadamu yanavyoweza kuwa kutokana na technology.

Miaka Ijayo: Sehemu Ya 1
Miaka Ijayo: Sehemu Ya 2
Ifahamu zaidi Simulizi ya MIAKA IJAYO

INAENDELEA…



Simulizi ya “MIAKA IJAYO” kutoka The Bestgalaxy ni simulizi ya sauti inayochunguza jinsi teknolojia inavyoendelea kubadilisha maisha ya binadamu na matarajio ya maisha ya baadaye. Unaposikiliza Simulizi hii, unapelekwa moja kwa moja katika ulimwengu wa baadae kwakua inatoa taswira ya dunia itakavyokua maendeleo ya kiteknolojia yatakapofika mbali. Inahimiza wasikilizaji kufikiria jinsi maisha yatakavyokuwa kutokana na maendeleo haya ya teknolojia.

Simulizi hii ilichapishwa kwa mara ya kwanza katika 2024 na inapatikana kwa mfululizo (series). Unaweza kuisikiliza bure katika tuvuti hii ya The Bestgalaxy.

NITAKUPA PESA NYINGI (Simulizi ya sauti)

“NITAKUPA PESA NYINGI” ni simulizi fupi ya sauti unayoweza isikiliza au kuipakua bure ndani ya The Bestgalaxy. Simulizi hii ya sauti imetolewa ili kusikiliza Bure kabisa hivyo unaweza anza sikiliza hapa hapa au baada ya kuipakua kwenye kifaa chako bila malipo.

Ni vema kusikiliza simulizi ya NITAKUPA PESA NYINGI ukiwa umetulia ili kuielewa zaidi katika fani na maudhui yake. Usisahau pia kufuatilia simulizi kali zaidi za sauti zilizo ndefu kuliko hii.

UTAMU WA JUMLA 🔞 (Simulizi ya sauti)

Simulizi ya UTAMU WA JUMLA ni simulizi yenye uhusiano kidogo na simulizi ya SUKARI YA DADA. Unaweza sikiliza simulizi hii ukiwa ndani ya The Bestgalaxy Bure kabisa na pia unaweza ipakua na kufurahia kwenye simu au kifaa chako. Sikiliza simulizi hii katika mazingira tulivu yatakayo ruhusu kuielewa kirahisi.

Katika kuisikiliza ukiwa kama msikilizaji hakikisha unazingatia umri maana simulizi hii haitakiwi kusikilizwa na mtu mwenye umri chani ya miaka 18.

kama umebonyeza na inachelewa kuanza basi huenda ni tatizo la mtandao wako. Jaribu mara kadhaa kwa kusubiri.

Sehemu ya 1
Sehemu ya 2
Sehemu ya 3
Sehemu ya 4
Sehemu ya 5
Sehemu ya 6
Sehemu ya 7
Sehemu ya 8
Sehemu ya 9
Sehemu ya 10
Sehemu ya 11 (mwisho)

Kupata taharifa ya simulizi mpya na mambo mwengine, hakikisha unatembelea The bestaglaxy kila mara na pia unaweza jiunga kwenye group letu la Whatsapp Bure.