Kama ni mtumiaji wa simu za smartphone unatakiwa kuwa makini sana katika matumizi yako ya smartphone maana ukiitumia smartphone yako vibaya unaweza kujikuta jela au unaweza kuwa kwenye wakati mgumu kwa kupoteza vitu vyako vya msingi na heshima kwa jamii. Leo nimekuandalia baadhi ya vitu ambavyo unapaswa kuvizingalia katika kutumia smartphone yako. Tutazungumzia vitu vichacheche tu, vingine tutaangalia katika makala nyingine. Lakini Kabla ya yote ningependa kukushukuru Kwa kufuatilia “The Bestgalaxy” na nakusihi usiache kufuatilia ili kujifunza vitu vingi zaidi.
Jinsi ya kupata mkopo kwenye simu GUSA HAPA>>>>
Bila kupoteza muda hebu tuangalie ni vitu gani usifanye katika matumizi ya simu yako…
1. Usijichukue picha za utupu na kutunza kwenye simu yako.

Kama ni mtu unaependelea kujichukua picha za utupu kwa makusudi na kuzitunza basi hakikisha unajiweka tayari kiakili kuwa hata zikivuja hazita kushtua wala kukuumiza. Kumekua na uvujaji mkubwa wa picha/video za utupu na ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya watu wenye picha au video hizo hawajui ni kwanini picha hizo zimetoka nje ya simu zao. Kitu muhimu kukijua ni kwamba si vizuri kuweka picha au video hizo kwenye simu maana kunavitu vingi sana ambavyo vinaweza pelekea kuvuja kwa vitu vyako.
2. Usiingize app nje playstore hovyo hovyo.

Wengi tumezoea kuingiza app tunazozipenda kupitia playstore lakini kuna baadhi huwa tunaingiza tu yaani mtu katuma kwenye group la WhatsApp, basi unajaribu kuiingiza au umesearch Google bila kuangalia ata site inaaminika vipi, unaiingiza kwenye simu yako.
Kitu muhimu cha kujua ni kwamba kuna app ambazo ukiingiza kwenye simu yako tu huwa zinabeba taarifa zako kwenye simu na kuzituma kwa huyo mtaka taharifa za watu tena kwa kutumia bando lako bila wewe kujua. App hizi hupatikana nje ya Playstore hivyo basi katika kuingiza app nje ya Playstore hakikisha sehemu unayotoa app unaiamini na inaaminika pia.
Jinsi ya kufanya simu ijinunulie bando la internet (usichome pesa zako kununua bando) GUSA HAPA>>>
3. Usisambaze taarifa au link usizozijua kiundani.
Kama ni mtumiaji mzuri wa simu na mitandao nadhani umewahi fanya kitendo cha kusambaza link au ujumbe flani ili upata kituflani lakini mwisho ukagundua ni uongo. Sasa unadhani uliowasambazia walikuchukuliaje? na ulichokisambaza kingekua kinahusisha utapeli, unadhani tapeli wa hao uliowasambazia angekua ni nani kama si wewe?
Usipendelee kusambaza ujumbe au tahalifa usizo na uhakikanazo na wala usiwe na tamaa na vitu vya bure mitandaoni, utaibiwa alafu unaonekana wewe ndio mwizi.
4. Usisahau taarifa za Email yako wala kuzigawa.
Wewe ni mmoja kati ya watu wasio jua Email zao au password zakuingilia katika email zao?
Naweza kusema, kwasasa Email ni kitu cha msingi kuliko simu unayotumia. Email yako ni utambulisho wako katika sehemu mbalimbali pia email husaidia kupata vitu vyako vya msingi vilivyopo kwenye simu endapo simu yako itaibiwa au kuhalibika ghafla. Kwakutumia email yako utaweza itafuta simu yako ikipotea na kutambua mahali ilipo.
Email hurahisisha sana mambo maana unaweza ukawa umeibiwa simu au imezimwa ghafla lakini ukawa unavitu vyote muhimu kama picha zako,video na majina ya simu kwa kushika Email yako na password yake kichwani mwako (Kama uliseti hivyo).
Tambua kuwa ni muhimu kujua Email yako na password yake na kamwe usimpatie mtu password maana utakua umempa tahalifa zako na akiwa mjanja atakupekua mpaka vitu unavyo search Google na kujua uwezo wako unaishia wapi.
Download na kuangalia movie zote bure kwenye simu GUSA HAPA>>>



