Tag Archives: simu

Jinsi ya kutuma picha, video au sauti kwenye app ya sms za kawaida (Android RCS)

Kama unatumia simu ya smartphone ya Android, unapaswa kufahamu kuwa unaweza tumia app ya sms za kawaida zaidi ya ilivyozoeleka. Unaweza tuma jumbe za maandishi, sauti na hata kutuma video au kupokea vitu hivyo kwa watu wengine. Kama ilivyo kwenye app ya WhatsApp au Telegram ndivyo app yako ya sms za kawaida inaweza tumika. Hapa The bestgalaxy unaenda kujuzwa kuhusu jinsi ya kufanya hivyo ila kabla ya yote hebu tuelewe maana ya “RCS messaging” kwanza.


“RCS messaging” (Rich Communication Services) ni njia mpya ya kutuma na kupokea jumbe kati ya simu za smartphone. Njia hii hua inatumia data(internet) badala ya SMS za kawaida kwenye Lain yako. Kupitia huduma au njia ya RCS messaging, watu wanaweza tumiana vitu vingi ikiwemo video, picha na Audio. Kwa watu wa iPhone jambo kama hili walikuanalo kwenye app ya iMessages japo kuna utofauti.

Jinsi ya kutuma picha, video, sauti au kwenye app ya sms za kawaida (Android)

Unaweza kutuma picha, video au sauti kwenye app ya sms za kawaida kupitia RCS messaging. Kufanya hivi ukiwa na simu ya android utahitajika kutumia app ya sms ya Google). App hii inaitwa “Google messages”, inapatikana playstore. App hii kwenye baadhi ya simu inakuepo tu bila kuiiingiza(kuiinstall). Lakini kwenye simu nyingine inakua haipo hivyo, tutatakiwa kuingiza mwenyewe kutoka Playstore.
Kama unataka kuingiza app ya Google messages au kuanza kutumia RCS messaging kwa ujumla, unaweza fuata hatua zifuatazo;

  • Ingia Playstore utafute app inayoitwa “Google messages” kisha iingize kwenye simu. Kama tayari unayo fanya ku-Upate tu.
  • Baada ya hapo ifungue na kukubali Sheria za RCS messaging kwakubonyeza “Agree”. Kama itakuomba nafasi ya kuwa “Default SMS app” utatakiwa kukubali pia.
  • Baada ya yote kuwa sawa app ya Google messages, app hiyo inaweza kukuomba namba ya simu kwaajili kuanza kutumia RCS messaging. Jaza namba ya simu na baada ya hapo ukiwa na namba ya mtu ambae pia ameset RCS kwenye simu yeke, mtafurahia kutumiana video, picha na video kupitia app hiyo.
  • Kama haujaletewa sehemu ya kujaza namba, gusa profile au icon inayopatikana juu upande wa kulia kwenye app ya Google messages. Baada ya hapo ingia kwenye kipengele cha Settings cha app ya Google messages kisha changua RCS Chats na uiwashe RCS. Katika kuiwasha utaulizwa namba ya simu. Baada kuweka sawa namba ya simu utakua tayari umeanza kuitumia RCS messaging kwenye simu yako.


Faida za kutumia RCS messaging ni kupata uwezo wa kutuma na kupokea picha na video zenye ubora wa juu, Kuona mtu anapo andika ujumbe “Typing”. Mbali na hayo, mtumiaji utaona SMS ulizotuma kama zimefika au kusomwa(Delivery receipts). Unaweza kuunda magroup pia.

Kama utakua unahitaji mwanga zaidi katika hili, unaweza wasiliana na The bestgalaxy ukasaidiwa.

Jinsi ya kupata namba zilizofutika kwenye simu BONYEZA HAPA>>>

Mambo unayotakiwa kujua kuhusu Simu za Mkopo

Siku hizi hauhitaji kujiumiza sana kupata simu Janja au smartphone maana kuna mpaka simu za Mkopo. Simu hizi zinasaidia sana watu katika kuingia kwenye ulimwengu wa kisasa na kufurahia matunda ya Teknolojia.

Kuna mambo mwengi mtu anaweza ya kosa akiwa hana simu hizi za kisasa. Na pia Kuna vitu vingi mno mtu anaweza nufaika navyo kupitia simu hizi. Ukiwa kama mtu unaeishi ulimwengu wa hivi sasa, smartphone ni kitu muhimu usichotakiwa kukikosa japo faida au umuhimu hutokana na matumizi yako.

Kuna watu wengi kwa sasa wanatumia simu za smartphone za Mkopo na zimekua msaada mkubwa kwao huku wakiendelea kulipa Mkopo kidogo kidogo. Pia kuna watu wameisha maliza malipo ya Mkopo na wanaendelea kufurahia simu wakiwa na umiliki wa simu hizi kwa 100%.

Unaweza ukawa ni mtu unaetumia au unahitaji simu hizi za Mkopo. Hapa The bestgalaxy, tunajaribu kukupa mwanga kidogo kuhusu simu za Mkopo kwa kuangalia mambo machache kuhusu simu hizi. Unaweza kupitia mambo haya kwa makini hapa chini.

Katika matumizi yako ya simu usifanye mambo haya BONYEZA HAPA>>>

Mambo unayotakiwa kujua kuhusu simu za Mkopo

Ni njia rahisi ya kupata simu mpya unayohitaji ukiwa na pesa ndogo

Kupitia huduma za Mikopo ya simu unaweza kupata simu mpya unayohitaji ukiwa hauna pesa ya kutosha kuinunua. Unaweza usiwe na shilingi laki 500,000 kamili mkononi lakini ukapata simu mpya yenye thamani ya pesa hiyo kwa Mkopo baada ya kutoa posa kidogo tu kama kianzio. Hivyo ni njia nzuri kama unatamani kupata simu mzuri mpya bila kuwa na pesa ya bei yake kamili.

Kikubwa unatakiwa kuwa na pesa ya kianzio tu ambayo mara nyingi hutegemeana na bei ya simu unayokopa na hata sehemu unayopata huduma ya Mkopo huo. Kama unakopa simu ya bei kubwa kianzio nacho huwa kinakua kikubwa.

Sio chaguo zuri kama hauna pesa ya uhakika ya kila siku

Kama unaona kabisa hautakua na pesa ya uhakika ya kulipia kila siku, simu hizi zinaweza kuwa sio chaguo zuri kwako. Simu hizi zinahitaji mtu alipie au awe amelipia malipo ya siku ili atumie. Kama mtu hatalipia, simu hua inajifunga na kumnyima mtumiaji nafasi ya kutumia mpaka atapo lipia.

Sasa ukiona hali yako ya pesa inaweza kufanya ukose pesa ya kulipia mpaka unafungiwa kwa muda mrefu, hili sio chaguo zuri sana. Ni vema ile pesa unayopanga kuweka kwenye kianzio ukachagua kununua simu used ya bei ndogo ambayo hautatakiwa kutoa pesa nyingine kuitumia. Kama hauna pesa za kulipia simu hizi unaweza kuona kero zinapojifunga wakati ni haki yao kukufungia.

Unaweza pata simu za mkopo kwenye Makampuni ya mawasiliano ya simu

Ukihitaji kupata huduma za simu za Mkopo, unaweza zipata toka kwenye maduka maalumu kwa mikopo hiyo yaliopo sehemu mbalimbali hapa Tanzania. Lakini pia hii mitandao ya mawasiliano ya simu kama Tigo na Vodacom, imejiingiza kwenye utoaji wa huduma za mikopo ya simu.

Unaweza kukopa simu kwenye mtandao wa simu unaotumia kama Vodacom au Tigo alafu ukawa unalipwa kidogo kidogo huku ukiendelea kuitumia. Unaweza wasiliana na mtandao wako wa simu kupata maelezo juu ya jambo hili. Uzuri wa kukopa katika mitandao ya simu ni kwamba unapewa OFA za vifurushi kwenye Laini ya simu. Lakini pia sehemu nyingine za kukopa simu zipo vizuri pia.

Taalifa za malipo hutunzwa

Unapotumia simu ya Mkopo ni vema ukajua taalifa zako na malipo yako mara nyingi huwa zinatunzwa ili kukusaidia pale unapokwama au usumbufu unapojitokeza. Taalifa hizi zinaweza kuwa ni namba uliotumia kulipia na hata kiasi.

Ni jambo zuri sana kama ni muaminifu lakini kama sio muaminifu kuna uwezekano wa kutafutwa kupitia taalifa hizo japo wengi hawafikii hatua hiyo. Na hata ukiibiwa taalifa za malipo anayotoa mtu anaelipia na kuitumia baada ya kuibiwa zinaweza tumika kujua simu ipo kwa nani.

Ni hayo machache katika ukurasa huu, Endelea kuwa nasi na usisahau kwa simu za mikopo ni msaada mkubwa kwa watu katika kipindi hiki. Hazina usumbufu wa kukunjana mashati na kuaibisha wakati wa kukudai.

Sehemu za kuuza bidhaa zako zilizotumika Mtandaoni (Vitu used)

Unaweza kuwa hata sio mtu unaefanya bishara kama sehemu kuu ya kupata pesa lakini ukawa na vitu vyako unavyotamani kuuza. Vitu hivi vinaweza kuwa ni Simu yako ya zamani, PC, Tv, Redio na hata magari. Watu wengi wana vitu kama hivyo na wanatamani kuviuza lakini kwakua sio watu waliojikita kwenye bishara basi wanashindwa kupata sehemu ya kuviuza hivyo vitu na hata muda wa kufanya hivyo wanaweza kosa.


Teknolojia kupitia mtandao (internet), unamuwezesha kila mtu mwenye bidhaa anayotaka kuiuza akutane na watu wanaweza kununua bidhaa mtandaoni. Kupitia simu yako yenye uwezo wa internet au kifaa kingine cha internet, utaweza ukauza vitu vyako used kwa watu wengine. Njia ya kuuza vitu used kupitia mtandao, inaweza kuokoa muda wako muuzaji kwa kufanya kitu au bidhaa used unayouza ionekane kwa watu wengi wanaweza kuinunua huku ukiwa unaendelea na shudhuli zako nyingine.

Kwenye ukurasa huu, The bestgalaxy tumekuandalia orodha ya app chache zinazokuwezesha kuuza vitu used mtandaoni kupitia simu yako. Katika orodha hii, hatujaangalia upande wa Dunia, ila tumengalia katika upande wetu huu tu hivyo usishangae kutoziona platform kama eBay na Amazon.

Mambo ya kuzingatia unaponunua bidhaa mtandaoni (Online) BONYEZA HAPA>>>

App za kuuza bidhaa zako zilizotumika Mtandaoni (Vitu used)

Facebook

Kuna mtu anaweza jiuliza “Facebook inakujaje kwenye orodha ya app za kuuzia vitu used?” hebu tuanze na hili. Facebook inaingizwa kwenye orodha ya app za kuuzia vitu used kwasababu inakipengele kiitwacho “marketplace”. Kipengele cha Facebook marketplace kinakuruhusu mtumiaji wa Facebook kuuza na kununua bidhaa, ikiwemo used. Ukiwa na akaunti ya Facebook, utaweza kuweka picha na maelezo ya kitu unachouza pale alafu wanunuzi wakakutafuta kwaajili ya kununua. Zamani walikua wanaruhusu kuweka hadi namba ya simu lakini kwasasa hawaruhusu kwasababu za kiusalama.

Kupatana

Kupatana ni app rasmi kwaajili ya kuuza na kununua bidhaa mtandaoni. Mtu unaweza itumia kuuza vitu na pia unaweza itumia kununua vitu kutoka kwa wengine. Inatumika na watu wengi hivyo inaweza kuwa rahisi kumpata mnunuzi wa bidhaa yako used au kupata mtu anaeuza bidhaa unayohitaji. Inaruhusu kuweka picha na maelezo ya bidhaa yako ili anahitaji aelewe vizuri unachouza kabla hajakutafuta.

Jiji

Hii JiJi ni app nyingine kubwa ya kuuza na kununua bidhaa ambayo unaweza itumia kuuza vitu vyako used. Haina watumiaji wachache, wengi tu huuza na kununua vitu used kupitia app hii hivyo utakua sio mtu wa kwanza kuuza vitu used ndani yake. Ukiweka picha, maelezo ya bidhaa yako na mawasiliano yako vizuri, unaweza pata mnunuzi ndani ya app hii bila kupoteza muda sana maana watumiaji wapo wengi. Ni nzuri zaidi kwenye bidhaa za kielekroniki na magari alafu pia imepewa nyota 4.5 kati ya nyota 5 katika playstore.

Tisitano

Tisitano pia ni app kwaajili ya kuuza na kununua bidhaa. Inawakutanisha wauzaji wa vitu au bidhaa na wanunuzi wa vitu au bidhaa hizo. Inaweza tumika kuuza vitu vyako used kupitia simu yako ya mkononi bila kupoteza muda wako sana. Unaweza iweka bidhaa yako ndani ya app hii na ikaonwa na watu wengi kama app ya Kupatana au JiJi. Kuna maelfu ya watu huitumia app kwenye maswala ya kuuza na kununua vitu mtandaoni.

Mwisho, tunapenda kukukumbusha umakini unapouza na kununua bidhaa mtandaoni kupitia app hizi. Fahamu kuwa unaweza kutana na matapeli au watu wenye nia mbaya pia. Lakini hii isikuzuie kufurahia njia hii ya kuuza vitu used mtandaoni maana watu kama hawa wapo pia kwenye maisha yetu ya kila siku. Endelea kufuatilia The bestgalaxy kwa mambo mengine zaidi.

Jinsi ya kutengeneza au kurekodi Nyimbo kwa kutumia Simu

Kutengeneza nyimbo kwa kutumia simu inawezekana? Ndio, inawezekana na nyimbo unayotengeneza kwa kutumia simu inaweza kuwa na mafanikio makubwa tu kama nyimbo za Studio rasmi. Kipindi cha nyuma, ukiwa kama msanii wa Muziki ilikua ni lazima uhusishe vyumba vya Studio rasmi vinavyomilikiwa na maproduser ili kufanya mazoezi ya nyimbo na kurekodi nyimbo zako. Lakini kwa sasa, hakuna ulazima sana wa kwenda huko kama hauna uwezo. Unaweza tumia simu yako ya mkononi kufanya mazoezi ya kurekodi nyimbo zako na hata kurekodi kabisa ukiwa nyumbani tu.

Jinsi ya kutengeneza au kurekodi nyimbo kwa kutumia simu

Unaweza tengeneza au kurekodi nyimbo iliokamilika kwenye simu ila utatakiwa kuwa na app maalumu kwa kazi hiyo. App zipo nyingi na kati ya app hizo kuna app ngumu kutumia, pia kuna app rahisi kidogo zisizo hitaji mambo mengi kwenye kuzitumia. Moja ya app ambazo ni rahisi kutumia ni app iitwayo “Voloco”. Inapatikana katika Playstore kwa simu za Android na hata Appstore kwaajili ya watu wa iPhone au vifaa vya iOS kwa ujumla.

App ya Voloco inahusiana zaidi na kuweka Voco kwenye Beat. Unaweza ingiza Beat lako mwenyewe au ukadownload humo humo ndani Beat zilizotengenezwa na watu wengine. Ni ngumu kukuelezea kila kipengele cha app hii kwa maandishi ili uweze kuitumia ila tumejaribu kukuelezea hapa chini kwa msaada wa picha vitu vya muhimu kuvijua utakapo fungua app hii.

Kutengeneza nyimbo ni project na kwenye app hii kitu cha kwanza utakachotakiwa kukifanya ni kutengeneza au kufungua project mpya. Ukisha fungua project mpya unaweza weka Beat unalotaka kuliimbia kwenye project hiyo alafu ukaanza kurekodi sauti au voco zako. Uzuri ni kwamba Ina Autotune hivyo kunajinsi sauti au voco zako zinaboreshwa.

Unashauriwa kuvaa Earphone unaporekodi voco zako. Baada ya kumaliza kila kitu kwenye project hiyo, unaweza itunza project yako kwenye app hiyo.


Ukihitaji kuitoka kama audio za kawaida unaweza ingia kwenye project ulizo tunza alafu ukabonyeza vidoti vitatu vilivyo kwenye project yoyote unayoyahitaji alafu ukaugusa “Download” ili kuidownload nyimbo uliotengeneza iwe kwenye simu yako. Utakua na chaguo la kutunza iyo nyimbo kama Audio au video. Nyimbo yoko itakua tayari lkuisikiliza japo unaweza pia kuipitisha kwenye software nyingine ili kuiweka kwenye ubora zaidi au kuibadilisha kuwa mp3 kama utahitaji.

Tofauti kati ya Simu za Waterproof na simu za Water resistance

Linapokuja swala la simu kuingia maji, inaweza kuwa ni moja ya vitu watu hawapendi litoke hata kidogo. Ila kutokana na kazi tunazofanya au mazingira ambayo mtu upo, jambo hili linaweza tokea. Na simu ikiingia maji wote tunajua kinachoweza kutokea ni kuharibika kwa simu pamoja na kupoteza vitu vya muhimu vilivyo kwenye simu.
Ili kuzuia jambo hilo lisitoke, Makampuni ya simu huwa yanatoa simu ambozo zinasifa ya kuzuia maji kuingia kwenye simu. Simu hizi mara nyingi hutangazwa kuwa ni “Waterproof” au “Water resistance”. Na watu wengi wakiwa wanataka kununua simu wakiona imetajwa kuwa ni “Waterproof” au “Water resistance” huwa wanajua ni simu zisizo ingia maji.

Kitu muhimu kujua hapa ni kwamba kuna utofauti kati ya Simu zinazosemwa kuwa ni “Waterproof” na simu zinazosemwa kuwa ni “Water resistance”. Na hapa chini The bestgalaxy tunaenda kukufungua kitu muhimu juu ya utofauti huo.

Tofauti kati ya Simu za Waterproof na simu za Water resistance

Simu za waterproof na simu za water resistance zina tofauti katika jinsi zinavyozuia maji. Simu za waterproof zina uwezo wa kuzuia maji kuingia ndani yake kabisa. Lakini simu za water resistance zinakua na kiwango cha kuzuia maji kwa kiasi flani au namna flani.

Kiufupi simu hadi imeitwa “Waterproof” ni haiwezi ruhusu maji kupenya ndani kabisa. Lakini simu ikiitwa “Water resistance” huwa inaweza kuzuia maji lakini inategemeana na wingi wa maji, joto la maji, aina ya maji, muda iliokaa ndani ya maji au kina cha maji. Na unapotumia simu za Water resistance haushauliwi kuziweka kwenye maji makusudi maana zinaweza kuingia maji. Kuzuia maji kwake kuna kunailinda simu yako isiharibike pale unapo idondosha kwa bahati mbaya kwenye maji au sababu nyingine zisizo za makusudi.

Inasemekana kwamba simu nyingi huwa ni Water resistance na sio Waterproof. Na Kuna Makampuni yanaweza kuziita simu zao Waterproof kwa lengo la kibiashara lakini zikawa zinastahili kuitwa Water resistance na sio Waterproof. Kutokana na jambo hili, haushauriwi kujiamini sana kiasi cha kuiweka weka kwenye maji simu yako hovyo baada ya kuambiwa ni Waterproof.

Simu za Waterproof na Water resistance huwa zinawekwa vimipira na gundi kwenye nafasi ambazo maji yanaweza kupita. Mara nyingi simu za muundo huu huwa ni ngumu kuzifungua zinapotaka kurekebishwa kifundi na pia zikifunguliwa tu, huwa zinapoteza uwezo wake wa kuzuia maji. Mbali na jambo hil, simu hizi zinaweza poteza uwezo wa kuzuia maji baada ya kudondoshwa chini na kujigonga au kutumia kwa muda mrefu.

Ingress protection ratings (IP ratings) ni kipimo cha uwezekano wa kifaa cha kielectric ikiwemo simu zuia maji(vimiminika) na vumbi. Mfano wa IP rating ni “IP68” na imetajwa kuwa samsung galaxy s24 ultra inauwezekano huo. Namba ya kushoto “6” ni uwezekano wa kuzuia vumbi alafu namba “8” ni uwezekano wa kuzuia maji. Simu hii inafahamika kama ni “Waterproof” kutokana na uwezekano huo japo bado haushauriwi kujiachia nayo kwenye maji au vimiminika. Mwisho ningependa ufahamu kuwa Samsung Galaxy S24 ultra ni simu ya kwanza toka Samsung iliojikita kwenye Ai (akili bandia).

Jinsi ya kupata Namba zilizofutika kwenye Simu

Kwenye simu huwa tunatuza namba na siku hizi Smartphone huturuhusu kutunza katika Email mbali na kuzitunza katika Laini na Simu yenyewe. Mara nyingi mtu unashariwa utunze namba za simu kwenye simu yako katika Email. Email ni sehemu nzuri ya kutunza namba zako maana huwa Inazitunza namba in cloud na kuzifanya iwe rahisi kuzipata hata utakapo ibiwa au kupoteza simu. Yani hata kama umeibiwa simu, ukiwa na taalifa za Email yako uliotunzia namba tu, unaweza ingiza email hiyo kwenye simu yako nyingine na ukapata namba za simu ulizotunza. Taalifa za Email tunazoziongelea ni Email yenyewe na Password yake tu.

Ukiona dalili hizi ujue akaunti yako ya Facebook si salama BONYEZA HAPA>>>


Katika ukurasa huu wa The bestgalaxy, hatuta zungumzia kuhusu utunzaji wa namba za simu zaidi ya hapa. Ila tunaenda kueleza jinsi ya kupata Namba za simu zilizofutika.

Jinsi ya kupata Namba za simu zilizofutika

Ikiwa umefuta namba yoyote kwenye simu yako na haipo tena kwenye Lain, Email na hata katika simu yenyewe, tambua bado unanafasi ya kuipata namba hiyo. Namba iliofutika kwenye simu inaweza kuwa katika akaunti yako ya Facebook iliopo kwenye app ya Facebook ya simu yako.

Ukiwa na app ya Facebook kwenye simu yako, huwa wanaomba ruhusa ya kuchukua namba za simu ulizotunza kwenye simu yako ili wazitumie kuiweka akaunti yako ya Facebook karibu na watu unaowajua. Hii ni moja ya sababu ambazo hupelekea kuwaona watu unaowajua kwenye Facebook.
Ukiruhusu ruhusu Facebook ichukue namba za simu kwenye simu yako, hata zikifutika kwenye simu, bado zitakuepo ndani ya akaunti yako ya Facebook. Kama uliiruhusu Facebook kuchukua namba za simu, unaweza fuata yafuatayo ili kupata Namba zilizofutika kwenye Simu yako.

  • Ingia katika Facebook na ubonyeze vimistari vitatu gusa “Settings”
  • Ingia kwenye settings alafu nenda kwenye “Accounts center”.
  • Ingia kwenye “Your Information and permissions” na ubonyeze kwenye “Upload contacts”
  • Chagua account yako ya Facebook utakayoiona Pele alafu utapelekwa kwenye ukurasa uliona orodha ya majina ya namba ambazo Facebook imeyatunza.
  • Baada ya hapo utakua ukigusa tu majina ili kuona namba. Kwenye orodha ya namba hizo unaweza kuziona namba ya simu iliofutika kwenye simu yako.

Kama haukuiruhusu Facebook kuchukua namba za simu kwenye simu yako, unaweza usiikute namba ambayo unaihitaji. Ni hayo tu tulio kuandalia hapa ila usiache kutembea The bestgalaxy.

Matumizi ya simu ya zamani unaponunua mpya (usiiuze au kuidharau)

Mara nyingi watu, hutumia simu walizonunua alafu hununua nyingine mpya baada ya muda flani. Sababu za kununua hutofautiana maana kila mtu huwa na jambo lake liliomsukuma kutoa pesa yake na kunua simu mpya. Kuna watu hununua simu mpya baada ya kuona simu ya zamani imeharibika kabisa, wengine hununua baada ya kupoteza simu, pia kuna wengine huwa wananuanua simu mpya kutokana na kuichoka simu ya zamani au kutamani kubadilisha simu tu.

Kama unatabia ya kununua simu mpaya ili kubadilisha simu au kwenda na wakati ni jambo zuri. Simu mpya huwa zinakuja na maboresho pamoja vitu vingine vizuri kwa huo wakati zinaotolewa. Hivyo kwenda na wakati katika upande wa simu ni jambo zuri. Lakini unaponunua simu, mpya simu ya zamani huwa unafanya nini?
Kama haujui matumizi ya simu yako ya zamani unapo nunua simu mpya, soma hapa chini ili kufahamu jinsi wanavyoweza itumia.

Matumizi ya simu ya zamani unapo nunua mpya

Badili kuwa kifaa cha games

Simu yako ya zamani kama ipo vizuri na inaweza kuwekwa games za kucheza, basi ibadili kuwa kifaa cha games. Kuna games nzuri sana ambazo unaweza zijaza kwenye simu hiyo alafu ukitulia ukawa unazicheza. Sio lazima iwe wewe tu unacheza, hata ukiwapa watoto inaweza kuwa vizuri pia.

Ifanye WiFi ya nyumbani

Simu za smartphone huwa zina WiFi ambayo unaweza unganisha vifaa vingine vinavyotumia internet alafu vikatumia internet kupitia simu hiyo. Sasa endapo itakua na simu ya zamani na laini ya simu usioitumia, unaweza weka bando la kutosha kwenye hiyo laini alafu ukiingiza kwenye simu kisha ukawa unaitumia iyo simu kama WiFi ya nyumbani kwako. Kama unatumia internet kwenye PC au simu yako, hii inaweza kuwa nzuri kwako maana utakua unaiunganisha kifaa chako kwenye simu hiyo ya zamani ili kupata internet.

Iweke kuwa simu ya nyumbani

Unasimu ambayo ukiwa mbali na nyumbani ukiipiga mtu yoyote aliopo nyumbani anaweza ipokea? Mh sawa. Ni vema kuwa na simu ya nyumbani ili ukipata dharura au wakipata dharaura watu alioko nyumbani muwasiliane. Kama hauna simu ya zamani, unaweza ibadili kuwa simu ya nyumbani kwa kuiwekea laini na kuwaambia wanaoshinda nyumbani waitumie kama simu ya nyumbani tu.

Badili kuwa kifaa Cha Muziki na video

Kama unapenda kusikiliza nyimbo na kuangalia filamu, basi simu yako ya zamani inaweza kukufurahisha kwenye hilo. Unaweza ijaza nyimbo zote ambazo huwa ukitulia unazisikiliza sana bila kuchoka au ukajaza filamu unazozipenda sana. Baada ya kufanya hivyo ukipata muda utakua unachukua iyo simu na kusikiliza nyimbo au filamu zako bila Kuigusa simu yako mpya na kumaliza betri.

Tunzia file usizotaka kutembea nazo au zipotee

Simu yako ya zamani pia inaweza tumika kama kifaa cha kuhifadhia vitu vyako. Unaweza ingiza mafaili ambayo hautaki yapotee au hautaki yawe kwenye simu yako mpya. Ukishaingiza, unaweza ficha hiyo simu sehemu ambayo unahisi ni salama. Kama ni mtu unaekumbuka password, basi unaweza weka na password kwenye simu hiyo.

Unaponunua simu mpya, usisahau kuwa thamani ya simu ya zamani bado ipo. Kikubwa ujue jinsi gani utaitumia simu ya zamani baada ya kupata simu hiyo maana usipojua hautaiona thamani yake.

Mbali na yote, kuiuza au kuigawa ni jambo zuri pia maana unakua ni kama unawasaidia watu wengine kupata simu na kuwaonesha upendo.

Jinsi ya kupata simu janja/smartphone bila kuwa na pesa nyingi

Karibu The bestgalaxy na asante sana kwa kuwa hapa muda huu. Katika ukurasa huu tumekuandalia maelezo ya kukufungua ubongo juu ya jinsi ya kumiliki simu janja/smartphone bila kuwa na pesa nyingi. Maelezo haya yamelenga watu ambao hawatumii smartphone/simu janja mpaka sasa wakiamini hawawezi miliki simu hizi za kisasa kwasababu hawana pesa nyingi.

Ukweli ni kwamba usipokua unatumia simu janja kipindi hiki, unakuwa unapitwa na mambo mengi sana ambayo ungeyapata kiganjani kwako. Mfano mzuri ni kutumia app ya Whatsapp; kuna baadhi ya watu katika kazi zao wanashindwa kutuma au kutumiwa video,picha na vitu vingine kwasababu tu hawatumii app ya Whatsapp na sio kwamba hawapendi bali ni simu zao haziwezi.

Kuendelea kutumia hizo simu ndogo ni jambo zuri lakini kuanza kutumia simu janja kunaweza kuwa jambo zuri zaidi hasa ukijua matumizi mazuri na chanya kwako. Kama unataka kuanza kutumia simu janja lakini unauwezo mdogo sana kipesa unaweza fanya yafuatayo kupata simu janja kwa huo huo uwezo ulionao.

Jinsi ya kumiliki simu janja/smartphone bila kuwa na pesa nyingi.

Pata simu za mkopo na anza kulipa kidogo kidogo.

Moja kati ya vitu ambavyo watu hufanya sasaivi ni kuchukua simu za mikopo. Kuna makampuni huwa yanajihusisha na kutoa simu janja za mikopo. Unatakiwa kuwa na kiwango kidogo sana cha pesa ambacho utawapa alafu watakupa simu. Kiasi hicho cha pesa kinafahamika kama “kianzio” na kinaweza kuwa hata chini ya elufu 80 kwa baadhi ya simu(Ukubwa wa kianzio huwa kinategemeana na Thamani ya simu unayokopa). Baada ya kupewa hiyo simu utaanza kuitumia kama kawaida ila utatakiwa kuwa unalipia kiasi kidogo sana cha pesa kila siku mpaka utakapo maliza deni lako. Kiasi cha kulipa kila siku mara nyingi huwa kinakua ni chini ya Tsh 2000. Usipolipia simu hizi hua inajifunga na kukukumbusha kulipia ili uendelee kuitumia. Simu za mikopo ni nzuri sana kama hauna pesa nyingi za kununua simu ila unauhakika wa kupata pesa ndogo ya kulipia kila siku.

Nunua simu za ofa toka kwenye mitandao ya simu.

Mitandao ya simu kama vile Vodacom au Tigo huwa inakua na simu ambazo mtu unaweza zinunua kwa bei rahisi sana ukilinganisha na kuzinunua simu hizo kwenye maduka ya kawaida. Mara nyingi huwa mitandao hii inawaambia wateja wake kuwa watembelee katika maduka yao ili wajipatie simu za ofa. Ukienda katika maduka hayo utapata simu mpya za bei rahisi ambazo huwa zinakua mpaka chini ya 100000. Baada ya kununua simu hizo unaweza pewa bando la internet la kutumia mwaka mzima na pia huwa wanahitaji utumie mtandao wao kama mtando mkuu kwenye simu hizo. Hii ni njia nzuri ya kupata simu kwa bei rahisi hasa kama haupendi kuwa na deni.

Chukua simu zilizo tumika na mtu mwingine.

Muda huu kuna watu wanaziuza simu zao kwasababu mbali mbali na wamekosa wateja. Kuna watu wanauza simu laki 1 na waliinunua laki 3. Kuna watu wamezichoka simu zao wapotayari kuziuza hata chini ya laki. Unaweza pata simu nzuri tu toka kwa watu wanaoziuza simu zao ila utakiwa kuwa makini sana na simu hizi maana zinaweza kukupeleka pabaya. Ni vema ukikutana na mtu anaeuza simu ukamuuliza kwanini anauza, ametumia kwa muda gani inatatizo gani na kufuata taratibu zitakazo kuokoa pindi simu hiyo itakapokua imehuswa na tukio baya.

Ukitaka kupata simu inayouzwa mtaani kwako, tangaza kwa watu kuwa unahitaji simu ili hao watu wakisikia mtu anauzwa simu, wamlete muuzaji kwako. Kama hautaki kununua simu za mtaani kwako, unaweza tumia app kama Jiji au app ya Kupatana ila umakini unahitajika sana.

Jinsi ya kujua kama simu inafuatiliwa/inachunguzwa na mwingine(anaona bila kuigusa)

Katika matumizi yako ya simu za Smartphone unatakiwa kuelewa kwamba vifaa hivi vinaweza kudukuliwa na mtu mwingine na kufanya mdukuzi au huyo mtu apate uwezo wa kuona vitu vilivyomo au vitu unavyofanya kwenye simu yako bila yeye kuigusa simu yako. Mbali na kuona vitu unavyofanya au ulivyohifadhi, Mtu aliedukua simu yako pia anaweza kuwa na uwezo wa kuitumia simu yako bila kuigusa… Mfano wa vitu anavyoweza kuvifanya ni kuitumia simu yako kutuma sms kwa mtu mwengine, kuitumia camera yako kuangalia unachokifanya, kuvujisha vitu vyako au kukuzuia kufanya baadhi ya vitu kwenye simu yako.

Lakini ukiwa kama mtumiaji wa smartphone wa miaka hii, hutakiwi kuwa na hofu sana juu ya hili kwani kunaviashilia vya kuangalia kwenye simu yako ili kujua upo salama au vipi. Hapa The beestgalaxy tutakupa mwanga juu ya jinsi ya kuangalia simu yako ya Android kama imedukuliwa na inafuatiliwa/inachunguzwa na mwingine.

WhatsApp yako inatatizo? Jifunze jinsi ya kutatua hapa>>>>

Jinsi ya kuangalia kama simu yako inafuatiliwa/inachunguzwa na mwingine

katika matumizi ya simu watu huwa wanapenda kuingiza apps nyingine mbali mbali ukiachana na zile ambazo huwa wanazikuta tayari zipo kwenye simu. Kitu unachotakiwa kujua hapa ni kwamba kuna Program au apps ambazo unaweza kuingiza kwa bahati mbaya au ukaingiziwa kwenye simu yako na zikiwa kwenye simu yako zinakua zinatumika na mtu mwingine huona au kufanya vitu kwenye simu yako bila kuigusa.

Endapo katika simu yako kutaingizwa apps hizi kwa makusudi au bahati mbaya, simu yako itakua sio salama tena maana vitu. Lakini kitu kizuri ni kwamba kwenye sikuizi kwenye simu za Android kuna program inaitwa “Google play protect”. Program hii inamilikiwa na google na kazi yake kubwa kwenye simu ni kukulinda dhizi ya apps hatari unazoziingiza kwenye simu yako. Kama kuna app yoyote inayoweza kuwa hatari umeiingiza, Google play protect huwa inatoa taharifa na kukushari cha kuifanya. Unaweza kuitumia Google play protect kuangalia kama angalia kama simu yako ni salama au si salama. Unachotakiwa kufanya ni kufuata hatua hizi chini.

  • Chukua simu yako na uingie katika app ya Play store
  • Baada ya hapo, gusa kiduara cha profile yako na uchague “Play protect
  • Bonyeza kitufe kilichoandikwa “Scan” na baada ya hapo Google play protect itaanza kuangalia kama kuna app zozote hatari kwenye simu yako alafu itakupa majibu.
  • Kama kutapatikana app yoyote hatari utaonyenshwa app hiyo alafu utashauriwa kuiondoa kwenye simu yako kwa kugusa kitufe cha “Uninstall“.

Google play protect ni njia nzuri na rahisi ya kuangalia kama simu iko salama ukiwa kama mtumiaji wa kawaida lakini huwa haikuhakikishii usalama kwa 100%.

Google play protect ikiwa “Active” kwenye simu yako huwa inatafuta na kulinda hii ya app hatari. Na endapo itakuta app harari imeingizwa au unataka kuiingiza kwenye simu yako, itakupa taharifa.

Mbali nna kutumia Google play protect kuangalia kama simu yako iko salama unaweza pia kujua kuwa simu kwa kuangangalia kama kwenye simu yako kuna vitu vifuatavyo.

Angalia orodha ya app zinazotumia sana internet na kama utakuta app ambayo haieleweki na hauitumi lakini ipo juu kwenye matumizi ya bando, inawezakua ni app hatari. Kama kamera ya simu yako ukiifungua inakuandikia “Camera is being used by another application” au “You cannot use more than one application that uses camera” au “Camera may be in use by another application” hiyo inaweza kuwa ni ishara ya kwamba simu yako sio salama. Mbali na hayo, kukuta vitu ambanyo haujavifanya lakini vimefanyika kunaweza kuwa kiashiria cha hatari pia.

Jinsi ya kutafuta nafasi za ajira/kazi kwa kutumia simu mtandaoni

Kama ni mmoja kati ya watu wanaotafuta nafasi za kazi basi hapa kunakitu kidogo unahitaji kuwanacho kichwani katika miaka hii ukiwa katika mchakato wa kutafuta ajira. Unachotakiwa kujua ni kwamba teknolojia kupitia internet/mtandao imerahisisha mchakato wa kutafuta ajira na kuufanya uweze kufanyika katika kiganja chako kwa kutumia simu yako(Smartphone).

Unaweza tumia simu yako kuangalia nafasi za ajira unayoihitaji zilizojitokeza katika sehemu mbalimbali za dunia (Ndani na nje ya nchi). Na kama utapply au kufuata maelezo ya kuipata iyo nafasi na kubahatika kuipata, utakua ni mmoja wa mamilioni ya watu waliopata na wanaoendelea kupata nafasi za kazi kwa msaada wa internet. Kama unataka kutafuta nafasi za ajira/kazi kwa kutumia simu mtandaoni lakini haufahamu ni jinsi gani unaeza fanya hivyo, basi hapa chini nakupa mwanga juu ya hili kwa njia 3. Lakini kabla ya yote ni vema ukajua kwamba kunabaadhi ya nafasi za kazi au ajira ziwekwa na matapeli mtandaoni na maranyingi humuitaji mtaka nafasi atoe pesa ili kupata nafasi ya ajira… kuwa makini ni ajira za mtindo huo ili usije tapeliwa.

Njia za kutafuta nafasi za ajira/kazi zilizojitokeza kwa kutumia simu mtandaoni

Tafuta nafasi za kazi kupitia Google search

Watu tu hutumia google search kutafuta vitu mbalimbali kirahisi mtandaoni na imekua msaada mkubwa kwa watu wengi, nafikili hata wewe unaweza kuwa mmoja wa watumiaji wake mzuri. Mtu unaweza tumia Google kupata vitu vinavyokufurahisha, vitu vitakavyo kuelimisha na vitu vingine muhimu ikiwemo nafasi za ajira zilizojitokeza sehemu mbalimbali (Ndani na nje ya Tzanzania). Na nirahisi sana… kiufupi utatakiwa kuandika maneno yanayomaanisha nafasi za kazi, aina ya kazi na mahali(kwa kingereza ili kupata matokeo mazuri). Yaani unawezakwenda Google na kuandika “””””Aina ya kazi unayoitaka + jobs in + sehemu“”””” kisha ukitafuta na kwenye matokeo utapata orodha ya nafasi za kazi kulingana ulichokiandika. Kwamfano ukiwa unataka kazi ya “Customer care service” hapa Tanzania, utaandika “Customer care service jobs in Tanzania” kwenye matokeo utapata orodha ya nafasi za kazi za customer care zilizojitokeza Tanzania. Baada ya google ikukupa nafasi za kazi itakua ni kazi kwako kusoma maelezo ya kazi hizo ili kuzielewa zaidi na kuapply ikiezekana. Lakini unapotumia njia hii inatakiwa kufahamu kuwa Google ni search engine tu, hivyo huwa haina nafasi za kazi, inakupeleaka sehemu ilipopostiwa kazi…

Jiunganishe na blog zinazohusiana na mambo ya nafasi za ajira

Kuna blog ambazo hujihusisha zaidi na kutoa tahalifa kwa watu juu ya nafasi za ajira zilizojitokeza. Maranyingi huwa zinapost tahalifa za nafasi za ajira au habari zinazohusiana na mambo hayo hayo. Mfano mzuri ni Ajiraleo.com au Ajirampya360.com. Sasa kwakua na wewe unahitaji nafasi za kazi basi unaweza anza kuwa karibu na blog za mtindo huu ili wakitoa tu tahalifa za nafasi za ajira zilizojitokeza, zikupate kwa wakati na kuanza mchakato wa kuzichangamkia. Unaweza kuwa nazo karibu kwa kuzifuata blog hizo au kurasa zao katika mitandao ya kijamii ili kupata vitu wanavyopost.

Tumia LinkedIn

Linkedin ni mtandao kama vile Facebook au twitter lakini mtandao huu unakusanya wataalamu wa mambo mbalimbali na umejikitia katika zaidi maswala ya biashara na ajira. jiunga kwenye mtandao Linkedin bure kabisa na kwenye profile yako utatakiwa kujaza taalifa sahihi kuhusu wewe na utaalamu wako. Mambo unayotakiwa kuyafanya ndani ya mtandao huu ni vema yakawa yanaendana na utaalamu wako na jambo zuri ni kwamba unaweza kupata ajira kupitia mtandao huu… kurahisisha zaidi mchakato wa kutafuta nafazi za kazi, kunakipengele cha mtandao huu kinauruhusu kutafuta nafasi za kazi zilizojitokeza kulingana na uhitaji wako na kuapply.

Mbali na njia hizo tatu, kuna njia au vitu vingine zaidi unaweza fanya kupata taalifa za nafasi za kazi zilizojitokeza lakini huenda tutazungumzia katika sehemu nyingine, hapa tumekupa mwanga kwa hayo machache. Na ni vema kuendelea kutafuta nafasi za kazi nje ya mtandaoni pia. Ishi kwa kutangaza utaalamu wako. Endelea kufuatilia The bestgalaxy.