Tag Archives: simu

Game Bora za kucheza kwenye simu 2026

Kadri teknolojia ya simu inavyozidi kukua, ndivyo pia mobile games zinavyozidi kuwa bora zaidi kwa upande wa graphic, gameplay na ushindani wa online.

Mwaka 2025 umeleta ushindani mkubwa kwenye game za simu, hasa kwa wapenzi wa action, racing, sports na survival. Sasa baada ya mwaka huo kuisha, Katika mwaka 2026 upande wa games unajua upo vipi? Acha tukujuze.

Hapa chini tumekuorodheshea game bora za kucheza kwenye simu mwaka 2026 ambazo zimekuwa maarufu alafu zinazopendwa na wachezaji wengi duniani.

Magame ya mpira ya kucheza kwenye simu BONYEZA HAPA>>>

Game Bora za Kucheza Kwenye Simu Mwaka 2026

  1. Delta Force Mobile

Delta Force Mobile ni moja ya game za shooter za kisasa zenye graphic kali sana. Ni chaguo bora kwa wapenzi wa game za kivita na tactical shooting.
Ndani yake kuna mode tofauti tofauti ambazo hubadilika kulingana na updates mpya. Game hili linatumia internet na ni online kwa asilimia 100.
Delta Force Mobile lilitolewa rasmi mwaka 2025 na TiMi Group, na lilipokelewa vizuri sana na mamilioni ya wachezaji kutoka pande zote za dunia.

  1. PUBG Mobile

PUBG Mobile ni game maarufu sana ya battle royale ambayo bado inaendelea kutawala hata mwaka 2026. Wachezaji hadi 100 hushuka kwenye ramani moja na kupambana hadi abaki mshindi mmoja.
Ina silaha nyingi, ramani tofauti na modes mbalimbali. PUBG Mobile ni online game inayohitaji internet muda wote wa kucheza. Lakini pia Kuna toleo dogo la game hili ambao ni maalum kwa simu zenye uwezo mdogo na mtandao usio mzuri(poor internet). Toleo hili linaitwa “PUBG Lite”.

  1. Call of Duty Mobile

Call of Duty Mobile ni game ya shooter yenye ushindani mkubwa sana katika ulimwengu wa game za kivita za simu. Ina modes kama Multiplayer, Ranked na Battle Royale.
Game hili lina graphic nzuri, silaha za kisasa na gameplay nzuri sana. Ni online game kwa asilimia 100 na linafaa kwa watu au wachezaji wanaopenda challenge ya kweli.

  1. EA SPORTS FC  Mobile

EA SPORTS FC Mobile ni game ya mpira wa miguu inayokuwezesha kuunda timu yako mwenyewe, kusajili wachezaji maarufu na kushindana na wachezaji wengine duniani.
Ina modes nyingi na graphic nzuri. Ili kufurahia ushindani wa online, game hili linahitaji internet.
EA SPORTS FC Mobile zamani ilikua nitaitwa FIFA lakini walibadili jina baada ya “FIFA” kumaliza makubaliano na EA ambao ndio wenye game hilo. Kwaiyo kama uliwahi kusikia game la “FIFA”, fahamu kuwa ndio hili hili.

  1. Need for Speed: No Limits

Need for Speed No Limits ni game ya mbio za magari yenye kasi kubwa na mashindano ya kusisimua. Unaocheza ukiwa kama dereva wa magari na unafanya mashindano katika sehemu na ramani mbalimbali.
Inakupa uwezo wa kubadilisha magari (customization) na kushindana kwenye racing tofauti. Baadhi ya modes zinaweza kuchezwa offline, lakini online races zinahitaji internet.

  1. Truck Simulator: Europe

Truck Simulator: Europe ni game ya simulation inayokupa uzoefu wa kuendesha malori kwenye barabara za Ulaya. Game za mtindo huu zimekua nyingi na vinapendwa na watu wengi. Kama ni moja watu ambao hupenda game za Truck, basi hii ni chaguo zuri kama utataka kucheza game hizo kwenye simu.
Ni game imetulia, inafaa kwa wachezaji wanaopenda realism na safari ndefu. Inaweza kuchezwa offline, lakini baadhi ya features zinahitaji internet.

  1. 8 Ball Pool

8 Ball Pool ni game rahisi lakini linakupa ushindani mkubwa katika kucheza mchezo wa pool. Unacheza pool dhidi ya wachezaji wengine kutoka sehemu mbalimbali za dunia.


Ni online game inayohitaji internet na inafaa kwa wachezaji wa rika zote. Unaweza cheza pool na rafiki zako toka sehemu mbalimbali za dunia na mukafurahi pamoja.

  1. LifeAfter

LifeAfter ni game ya survival yenyewe inakutupa kwenye dunia iliyojaa zombies. Unapaswa kutafuta chakula, silaha na kujilinda huku ukijenga maisha yako mapya.
Ni online game yenye story nzuri sana ya zombies na graphic nzuri pia.

  1. Vector

Vector ni game ya parkour inayohusisha kukimbia, kuruka na kuepuka vizuizi au vikwazo. Unaocheza kama mtu aitwae “Vector” anaekimbizwa ili kukamatwa na kundi linaloitwa “Big Bother”.
Ina gameplay rahisi lakini yenye changamoto zinazoweza changamsha sana akili. Inaweza kuchezwa offline na zuri hata simu zenye uwezo ndogo.


Lilitolewa rasmi mwaka 2013 lakini Bado ni moja ya game mzuri sana unazoweza kucheza mwaka huu kama haujawahi kucheza.

  1. Shadow Fight 2

Shadow Fight 2 ni game ya mapigano inayojulikana kwa mtindo wake wa kivuli. Kama unapenda game za kupigana, basi unaweza jaribu kucheza hii maana imekua chaguo la wengine kwa miaka kadhaa sasa.
Ina mapigano ya kuvutia, silaha mbalimbali na story nzuri nyuma ya mapigano hayo. Inaweza kuchezwa offline, huku baadhi ya features zikihitaji internet.

Ni game hizo tu katika Makala hii ndio tumeziongelea lakini fahamu kuwa Kuna game nyingine nyingi nzuri unaweza kucheza na ukafurahi. Hizo ni baadhi tu ya game Bora.
Chagua inayokufaa kulingana na aina ya games unazopenda.

MUHIMU: Game zote hizi zinapatikana kwa simu za Android na hata ukitafuta kwa iOS zinapatikana pia(iPhone)

Jinsi ya kukopa Pesa katika Mixx by yas (Kwenye simu)

Watu wengi wanaotuma na kupokea pesa kwenye simu zao hapa Tanzania huwa wanatumia huduma za kifedha za mitandao ya simu ikiwemo Mixx by yas kutoka Yas(Tigo).
Mixx by yas imekua moja ya njia nzuri za kutuma na kupokea pesa toka miaka nyuma ambayo ilikua inaitwa “Tigo Pesa”.


Mbali na kutumika kutuma na kupokea pesa, Mixx by yas huwa ina huduma nyingine ndani yake zinahusisha fedha. Katika huduma hizo, kuna huduma ambazo zimelenga kumsaidia au kumuwezesha mtumiaji wao.
Katika Makala hii, tutajikita katika huduma yao ya mikopo inayomuwezesha mtu kukopa pesa zinazoweza kumsaidia kwenye mambo mbalimbali. Ikiwa unahitaji kujua namna ya kukopa pesa katika akaunti yako ya Mixx by yas, basi hapa ndio mahali pake.

Mambo ya kuzingatia unapochukua Mkopo kwenye app za mikopo BONYEZA HAPA>>>

Kukopa Pesa katika akaunti ya Mixx by yas

Kama unahitaji kukopa pesa katika akaunti ya Mixx by yas na uwe huru kuitumia kwenye mambo mbalimbali basi utatakiwa kutumia huduma yao ya “Nivushe plus“. Nivushe plus ni huduma ya Mixx by yas inayokuwezesha mtumiaji kukopa kiwango flani cha pesa na kukilipa katika muda uliochagua kurejesha. Unapewa uhuru wa kuchagua ni muda gani utarejesha(inaweza kuwa baada ya wiki kadha au mwezi mmoja kabisa).

Kama ilivyo mikopo mingine, Nivushe plus pia huwa ina riba ingawa ni kiwango kidogo sana ukilinganisha na baadhi ya huduma za mikopo. Ukiachilia mbali kuwa na riba kidogo, Nivushe plus ni huduma ya haraka sana ya Mkopo kwa watumiaji wa Yas (Tigo).

Jinsi ya kukopa pesa Nivushe plus

Njia rahisi ya kukopa pesa katika Nivushe plus ni kupitia app ya “Mixx by yas“. Kama una app hii kwenye simu yako, fanya yafuatayo:

  • Fungua app ya Mixx by yas
  • Chagua kipengele Cha “Mikopo” kinachoandikwa “Loans” kwa lugha ya kiingereza.
  • Baada ya hapo, chagua “Nivushe plus” kwenye chaguzi zitakazokuja.
  • Ukishachagua, utapelekwa kwenye ukurasa maalum wa kuchukua, kuangalia na kurejesha mikopo.
Ukurasa wa Nivushe plus katika app ya Mixx by yas

Kwenye ukurasa huo unaweza kukopa Mkopo na kuangalia taalifa nyingi za mikopo. Taalifa hizo ni pamoja na Salio la deni, kiwango chako Cha kukopa na hata historia ya malipo yako.

Kiwango unachoweza kukopa katika Nivushe plus huwa kinaongezeka kutoka na mambo kama miamala unavyofanya kwenye akaunti yako na uaminifu katika kurejesha mikopo. Mara nyingi mtu muaminifu na mwenye miamala mikubwa huwa anakua na kiwango kikubwa cha kukopa. Lakini kitu muhimu zaidi ni uaminifu. Ukiwa vizuri unaweza kukopa hadi milioni 2 (Tsh 2,000,000)

Kuna faida ya kuchelewa kununua toleo jipya la simu?



Karibu kila mwaka, makampuni ya simu huwa yanatoa matoleo mapya ya simu. Makampuni haya ya simu huyatoi tu matoleo ya simu, bali huwa yanashindana kutoa simu zenye maboresho na Teknolojia mpya ilio Bora kwa watumiami.
Watu wengi huwa wanaumiza kichwa sana namna gani wanaweza kupata matoleo haya mapya.

Vijana ambao huwa wanamtindo wa kuhitaji kujaribu vitu vipya, huwa wanahitaji matoleo mapya. Kujaribu vitu vipya ni jambo zuri sana ila ni nzuri zaidi kama liko ndani ya uwezo wako.
Ikiwa hauna uwezo wa kipesa wa kununua kila toleo jipya la simu, basi usiumize sana kichwa juu ya matoleo haya ya simu. Sababu za kutoumiza kichwa sana ni zifuatazo;

Mambo unatakiwa kujua kuhusu simu za mkopo BONYEZA HAPA>>>

Sababu za kutonunua kila toleo jipya la simu




Uzalishaji wa simu upo kibiashara




Fahamu kuwa makampuni ya simu yapo kibiashara na simu ndio moja ya bidhaa wanazouza. Kama zilivyo biashara nyingine, wanahitaji bidhaa ziuzike na wapate faida walioikusudia kisha wauze tena. Kutoa toleo jipya la simu ni sawa na kuingiza mzigo mpya sokoni ili watu wanunue. Hii ndio moja ya sababu simu hutoka kila mara na kuuzwa kama zilivyo bidhaa nyingine.

Kwaiyo endapo utakua hauna uwezo wa kununua toleo jipya la simu, usijisikie kuachwa nyuma. Nasema hivyo kwasababu wao wametoa toleo jipya kwasababu ya faida yao ya kibiashara na sio yako moja kwa moja. Yani kama bidhaa hauwezi ilimiliki, isikunyime usingizi.

Matoleo mapya hushuka bei baada ya muda



Kama umekua karibu na maswala ya kununua simu, utagundua kwasasa simu nyingi huwa zinapungua Bei kwa kasi sana baada ya mwaka moja au mwili toka zitolewe. Yani simu nyingi sana zilizouzwa bei ghali mwaka Jana na mwaka juzi unaweza zikuta kwa bei rahisi mwaka huu. Kuna watu walinunua simu kwa laki 9 kipindi hicho lakini kwa sasa simu walioinunua inapatikana kwa laki 3 tu. Na kadri siku zinapozidi kwenda ndio simu hushuka bei zaidi kutokana na matoleo mapya kuwa mengi na sababu nyingine.

Kwaiyo hapa Naweza kusema kutokimbilia matoleo mapya kunaweza kukufanya uiokoe pesa yako. Unaweza kuwa unasubiri simu mpya zishuke bei ndio ununue kwa bei rahisi.

Baadhi ya matoleo mapya ya simu huja na matatizo



Kwenye historia za simu, kuna matoleo mapya mengi sana yaliokuja na matatizo. Yani simu inaweza kutolewa kipindi hiki lakini baada ya muda mchache, watuamaji wakaanza kukumbana na matatizo ya kiufundi. Mfano wa matatizo yaliowahikutokea sana kwenye historia za matoleo ya simu ni kupata moto sana, vioo kutokwa na mistari, kuzima ghafla na mambo mengine mengi.


Kwaiyo kuchelewa kununua matoleo mapya ya simu kunaweza kukusaidia kuepuka matatizo kama haya. Yani utaona watu wanalalamika juu ya matatizo haya kabla haujatoa pesa yako kuinunua.

Matoleo mapya hayawi tofauti sana na yaliopo



Siku hizi kampuni kama Apple na Samsung huwa zinatoa matoleo kila mwaka lakini haina maana kuna ulazima wa kuchukua kila toleo jipya. Baadhi ya watu kwasasa huwa wananunua hata matoleo ya zamani ya simu za kampuni hizo kwasababu ya kuepuka bei. Mbali na bei, siku hizi kunakua na utofauti mdogo sana wa toleo jipya na toleo la zamani.


Tofauti wanazoweka kwasasa ni Teknolojia ambayo sio ya lazima sana kwa mtumiaji wa kawaida. Mfano; unawezakukuta simu toleo jipya ni bei ghali alafu inasifika kwa kamera inayozoom umbali mrefu sana… Mtumiaji wa kawaida hii itakusaidia nini? Haina umuhimu sana.

Kwa kuangalia hayo yote tuliozungumzia hapo juu, utagundua kunafaida ya kutokimbilia matoleo mapya ya simu. Matoleo mapya ni mazuri lakini kama hauna uwezo wa kununua kila toleo bila Mawazo, basi kuyaacha yapite kwa muda ni chaguo zuri pia.

Zingatia mambo haya kabla haujachukua mikopo kwenye App za Mikopo


Kupata mkopo imekuwa rahisi kuliko zamani. Kwa kutumia tu simu yako ya mkononi, unaweza kupakua app ya mikopo(Loan apps), kujisajili, na kupata pesa papo hapo. Urahisi huu umewavutia na kuwasaidia watu wengi mpka sasa, lakini pia umeambatana na changamoto zake.

Kuna mambo yameonekana kuwakumba wale wasiokuwa waangalifu katika kutafuta app sahihi za mikopo. Makala hii inakueleza mambo muhimu ya kuzingatia kabla hujatumia app yoyote ya mkopo ili kuepuka yaliowakuta wengine.

Mambo ya kuzingatia katika App za mikopo

1. Usalama wa Taarifa Binafsi


Moja ya mambo ya msingi mtandaoni ni kulinda taarifa zako. App nyingi hukusanya taarifa kama jina lako, kitambulisho, namba ya simu, na hata mawasiliano ya marafiki. Taalifa hizi zinaweza kutumia vibaya au vizuri.

Kabla ya kutumia app yoyote, hakikisha inaheshimu faragha ya mtumiaji na haijawahi kuripotiwa kwa matumizi mabaya ya taarifa.

2. Riba na Malipo ya Ziada


Ingawa unaweza kupewa mkopo kwa haraka, kumbuka kuna gharama nyuma ya pazia. Riba na ada zinazotolewa na app za mikopo hutofautiana sana. Wengine hutoza viwango vikubwa vinavyofanya urejeshaji kuwa mzigo. Ni vema kusoma masharti yao ya kifedha kabla ya kukubali kuchukua mokopo.

3. Masharti ya Marejesho


Kabla ya kuchukua mkopo wowote, hakikisha umeelewa masharti ya malipo. Je, mkopo unatakiwa kulipwa ndani ya siku ngapi? Kuna adhabu gani kwa kuchelewa? Kuwa na mpango wa malipo kabla hujachukua mkopo ili kuepuka presha isiyo ya lazima.

Jinsi ya kupata password ulioisahau kwenye akaunti yako BONYEZA HAPA>>>

4. Huduma kwa Wateja


App nzuri lazima iwe na njia rahisi za kupata msaada pale unapokwama. Tafuta app yenye huduma ya wateja inayopatikana kwa simu, barua pepe, au WhatsApp. Ukosefu wa mawasiliano ni kiashiria cha huduma duni au kutoaminika.


Kukopa si tatizo, lakini kukopa bila kuelewa kinachoendelea kunaweza kukuumiza. App za mikopo ni msaada mzuri kwa wale wanaojua kuzitumia kwa akili. Fanya kuchunguza kwa makini ndio ukope.

App ya Gamehub imerahisisha kucheza game za Xbox katika simu

Wachezaji wa games kwenye simu wanazidi kupewa njia rahisi na za kisasa za kufurahia games wanazozipenda kwenye simu. App ya Gamehub ni moja ya suluhisho jipya ambalo limeleta mabadiliko makubwa kwa wapenzi wa games. Kupitia app hii, sasa inawezekana kucheza game za Xbox moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi bila haja ya kuwa na console ya Xbox.

Kama bado haujajua ni kwamba unaweza cheza game za Xbox kwenye simu  lakini hii itakuhitaji utumie huduma ya xcloud. Xcloud ni huduma inayokuwezesha mtu kucheza game za Xbox na nyingine nyingi katika mtandao (Online). Kupitia huduma hii, unaweza cheza game nyingi kubwa kwenye simu yako bila kuwa na simu yenye uwezo sana maana. Kikubwa utakachotakiwa kuwa nacho ni internet yenye kasi tu na tulisha zungumzia juaa ya hilo kwenye makala nyingine hivyo hatauta zungumzia sana hapa.

Game la Fortnite katika Xcloud

Hapa tunakujuza tu kuwa kuna app inaitwa Gamehub imerahisisha zaidi mchakato wa kucheza game za Xbox kupitia hiyo hiyo xcloud.

Kitu kizuri ilicho rahisisha ni kuondoa uhitaji kwa kutumia VPN ikiwa upo nje ya nchi zenye huduma (kama vile US). Yani kupitia app ya Gamehub utaweza kucheza game za Xbox kupitia xcloud popote bila kutumia VPN. Utafanikisha jambo kilo kupitia kipengele cha kuchagua unataka kucheza kama upo sehemu (location). Unaweza fanya yafuatayo kujaribu hiya.

Jinsi ya kucheza game za Xbox kwenye simu kwa app ya Gamehub

Unachohitaji ni kuwa na akaunti ya Xbox, simu yenye uwezo wa kuunganisha intaneti, na app ya Gamehub yenyewe.

  • Fungua app na ujisajiri
  • Baada ya kujisajili, nenda kwenye upande Xbox kwa kubonyeza alama ya Xbox
  • Ukiwa hapo, palasa sehemu ya pembeni katika upande wa kulia, kwenda kushoto kuelekea kulia.
  • Ukifanya hivyo utaletewa sehemu ambayo utachagua location (mahali). Wewe unaweza chagua USA au UK.
  • Baada ya hayo, Chagua game unalotaka kucheza alafu ujisajiri kwa akaunti yako ya Microsoft kama kawaida kwaajili ya kuanza kucheza.

Nakukumbusha tu kuwa kama haujalipia Xbox game pass ultimate, hautaweza kucheza game zaidi ya Fortnite.

Hii ni habari njema kwa watu ambao hawana nafasi au uwezo wa kununua vifaa vya Xbox lakini bado wanatamani kufurahia michezo hiyo.

Jinsi ya kutengeneza App ya simu

Kikawaida, kutengeneza app ni mchakato unaohusisha kuandika “Code” ambazo ni maelezo katika lugha ya computer. Hivyo ukitaka kutengeneza app kwa utaalam zaidi, unapaswa kujua namna ya kuandika Code katika lugha mbalimbali za computer.

Kwa mtu unaetaka kuwa mtaalam wa kutengeneza app za simu, unaweza jifunza lugha za computer kama vile JavaScript, Kotlin, Java, Python, Java na nyinginezo. Ukiwa mtaalam wa lugha za computer na ukawa na uwezo wa kutengeneza app, alafu utaitwa “App developer”.


App developer anaweza kuingiza pesa kwa kuajiliwa sehemu mbalimbali anazoweza kufanya kazi kama “Developer”. Mfano; Kampuni ya Meta ambayo inaumiliki Instagram, Facebook na WhatsApp, huwa zina watu ambao hufaamika kama “Developer” ambao huusika na maboresho ya app hizo. Ni wachache Duniani ila huingiza pesa nyingi sana.

Mbali na kuajiliwa, App developer anaweza ingiza pesa kwa project zake mwenyewe. Yani anaweza pambana kutengeneza kitu anachokiwaza alafu kikamuingizia pesa kwa kukiuza au kukiingiza katika mifumo itakayomuingizia pesa. Mfano mzuri ni Kutengeneza game linalo muingizia pesa au kuwatengenezea watu app za kurahisisha mambo yao ya kibiashara.

Jinsi ya kutengeneza Pesa kwa kucheza games mtandaoni BONYEZA HAPA>>>

Jinsi ya kutengeneza app za simu kwenye simu za bila  kujua Code

Pamoja na hayo yote, sio lazima mtu uwe mtaalam ndio utengeneze app za simu. Mtandaoni kuna tuvuti/website nyingi ambazo zimerahisisha mchakato wa kutengeneza app za simu.

Website nyingine zinarahisisha mchakato wa kutengeneza app kiasi ambacho mtu yoyote anaweza kutulia na zitumia kutengeneza app za Simu. Unaweza usijue kabisa maswala ya lugha za computer lakini ukafanikisha kutengeneza app kupitia website hizo.

Ukizitafuta website za mtindo huu katika mtandao, utazikuta nyingi sana lakini asilimia kubwa zinahitaji ulipie pesa. Mfano mzuri ni tuvunti ya Andromo, AppMySite na Appypie. Ni kati ya website rahisi kuzitumia katika kutengeneza app za simu (Android na iOS)lakini ili kupata uhuru kwenye app yako, utatakiwa kulipia.

kutengeneza app za simu kwenye simu BURE


Lakini swala la kulipia, lisikukwamishe maana Kuna tuvuti nyingine zinakupa uhuru mkubwa kabisa bure. Mfano wa tuvuti hizo ni hii hiitwayo “Appcreator24” au tuvuti iitwayo “Appsgeyser“. Website hizi unaweza kuzitumia kutengeneza app za simu kwa urahisi sana na bila kulipia.

Hapa the bestgalaxy tunakupa mwanga wa jinsi ya kutengeneza app ya simu kupitia tuvuti ya Appcreator24. Hapa chini tumekupa hatua muhimu zakuchukua ili kutengeneza app kwenye tuvuti hiyo ila utatakiwa kuwekeza muda wako kujifunza kiundani.

  1. Ingia kwenye website ya Appcreator24 ujisajili
  2. Bonyeza “Create app” kuanza kutengeneza app
  3. Jaza taalifa za app unayotaka na uchague mtindo wake
  4. Maliza kwa Download app yako ikiwa kama Apk au AAB file

Baada ya hapo utachangua wewe kwa kuipeleka. Unaweza kuiweka kwenye simu yako au kuipeleka sehemu kama Playstore ili watu waipakue kisha upate pesa kwa kuonesha matangazo. Na kama unataka kuiboresha au kuiweka vizuri, basi utaingia kwenye hiyo website ya Appcreator24 ili kurekebisha.

Pamoja na yote hayo, fahamu kuwa website nyingi za kulipia ndio hutumia kutengeneza app nzuri zaidi. Na pia, kujua code kunaweza kufanya uwe bora zaidi katika kuzitumia tuvuti zote za kuunda app. Watu engine hutumia AI kuandika Code katika kuunda app na hufanikiwa kutengeneza app nzuri sana. Lakini sio lazima kufanya hivyo, unaweza tengeneza app bila kujihusisha na code!

Hizi ni Website nzuri kwa watumiaji wa iPhone

Ukiangalia ulimwengu wa teknolojia ya sasa, unaona iPhone inabaki kuwa moja ya vifaa maarufu na vyenye ushawishi mkubwa. Kutokana na muundo wake wa kifahari na uwezo wake, iPhone imekuwa chaguo la kwanza kwa mamilioni ya watu duniani kote. Kwa baadhi ya watu iPhone si kifaa cha mawasiliano, ni sehemu ya mtindo wa maisha.

Kila matoleo au kizazi kipya cha iPhone kinaleta ubunifu ambao si tu unarahisisha maisha, bali pia unafanya matumizi ya simu kuwa ya kuvutia zaidi. Kwa kutumia iPhone, unapata fursa ya kufurahia maelfu ya apps kwaajili ya mahitaji tofauti yanayoweza kuwa katika upande wa mawasiliano, burudani na hata uzalishaji/biashara.

Kwa upande wa kupiga picha nzuri; Kamera za hali ya juu za iPhone zinakupa uwezo wa kupiga picha nzuri sana na wengi hupenda iPhone kwaajili ya jambo hilo.

Mbali na Kamera mtumiaji hufurahia huduma za kipekee kama Siri, iCloud, na FaceTime ambazo hufanya utumiaji wa iPhone kuwa wa tofauti na simu nyingine.

Katika makala hii, tutaangazia website au tovuti chache ambazo ni kwaajili ya watumiaji wa iPhone. Hizi ni zile tuvuti ambazo zinaweza rahisisha zaidi baadhi ya mambo kwa mtumiaji wa iPhone.

YouTube channel za kuangalia Movies Bure BONYEZA HAPA>>>

Website/Tuvuti nzuri kwa watumiaji wa iPhone

Apple Support

Apple ni mahali ambapo mtumiaji wa iPhone anaweza kupata suluhu za matatizo mbalimbali ya kifaa cha iPhone. Kupitia Apple support, mtu unaweza badili password ya akaunti ya Apple, kuupdate kifaa chako ili kupata maboresho na mambo mengine.
Apple Support imeletwa na kampuni ya Apple ili kusaidia watumiaji wa bidhaa za Apple kama iPhone na hata bidhaa mbali na iPhone.

Tubi TV

Kwa wapenzi wa movie wanaonatumia iPhone, hii inaweza kuwafaa zaidi. Tubi TV ni tuvunti ambayo inawezesha watu kuangalia Movie bure katika Internet. Kupitia iPhone yako, unaweza itumia tuvuti ya Tubi TV kuangalia maelufu ya movie bila kulipia chochote(Bure).
Huduma hii ya movie inapatikana USA hivyo ukiwa nje ya sehemu husika, hautaweza ipata bila kutumia VPN.

Kwaiyo utatakiwa kupata VPN hata ya Bure kwenye iPhone yako alafu utaunganisha kwenye server za USA kisha ndio utaingia kwenye Tuvuti ya Tubi TV.com
Ukishaingia katika tuvuti, utatakiwa kuifungua tena tuvuti hiyo katika “Desktop view mode”(Washa kipengele cha “Request Desktop view”) ili isikulazimishe kudownload app ya Tubi TV. Usipofanya hivyo, hautafanikiwa kuangalia Movie hata moja.

MacRumors

Hii tuvuti ya MacRumors, inajihusisha na taalifa mbalimbali zinazohusu bidhaa za Apple. Kwakua iPhone ni bidhaa ya kampuni ya Apple, basi habari zake mpya huwa zinapatikana katika MacRumors. Mfano wa taalifa unazoweza kupata kupitia MacRumors ukiwa kama mtumiaji wa iPhone ni mabadiliko yaliofanywa katika iOS, Ujio wa iPhone mpya na mengineyo.
MacRumors sio sehemu pekee unayoweza kupata habari za simu za iPhone lakini ni moja ya sehemu bora za kupata habari muhumu kuhusu simu za iPhone na vifaa vingine vya kampuni ya Apple.

iPhone Photography School

Website ya iPhone Photography School inakuwezesha kunielewa zaidi Kamera ya iPhone. Kwenye tuvuti hii, unaweza pata masomo ya kuitumia kamera ya iPhone kwa ustadi mkubwa.


Wengi huwa tunatumia kamera za simu zetu bila kuzingatia vipengele vya upigaji mzuri wa picha. Katika iPhone, watu wanaweza piga picha nzuri sana lakini wengi kati yao hawajui kwa upana kamera ya iPhone. Kiufupi watu hutumia Kamera ya iPhone kwa mazoea lakini inamambo mengi sana na yanahitaji mtu utenge muda wa kuelewa kila kipengele na kukitumia.

Ni hayo tu katika orodha hii. Unadhani ni tuvuti gani nyingine nzuri kwa watumiaji wa iPhone? Tuandikie kwenye sehemu ya maoni ili kusaidia wengine.

Play Store inakataa kuingiza app na games kwenye simu (Can’t install)

Kama ni mtumiaji wa simu za Android na huwa unatumia Playstore kuingiza games au apps nyingie kwenye simu yako, kuna muda unaweza kumbana na matatizo katika kutumia playstore. Na moja ya matatizo unayoweza kukumbana nanaoyo ni hili la kushindwa kudownload au kupakua vitu na kuingiza kwenye simu.

Unaweza ukawa unatafuta app unayoitaka kwenye Playstore, unabonyeza kitufe cha “Install” ili kuipakua lakini badala ya kuanza kuingia kwenye simu, play store inazunguka kwa muda mrefu na app haiingi kwenye simu. Na ukiisubiri wa muda mrefu zaidi inakuja na ujumbe wenye neno “Can’t install”. Ikiwa unakumbana na tatizo hili, fuata maelezo hapa chini kutatua tatizo hili.

AI za kutengeneza Video kwa picha tu BONUS>>>

Jinsi ya kutatua tatizo la “Play store kukataa ku download app na games kwenye simu”

Unapopata tatizo hili kitu cha kwanza kufanya ni kuangalia kama Storage ya simu yako imebaki kidogo au ipo ya kutosha. Simu ikiwa imebakiza nafasi ndogo ya kuifadhi vitu, unaweza kumbana na tatizo hili. Hivyo utatakiwa kuwa na nafasi ya kutosha ili kuingia app au game unalohitaji.


Ukiona nafasi ya kuifadhi vitu ipo sawa, angalia kama muunganiko wa internet upo vizuri kwenye simu yako maana internet ikiwa inasumbua tatizo hili linaweza kukukumba pia.

Kama vyote viko sawa na bado tatizo linaendelea, Jaribu kuclear/kufuta data za app ya playstore kwa kufuata hatua zifuatazo:

  • Nenda kwenye orodha ya app za kwenye simu yako na utafute app ya Play store.
  • baada ya hapo, ishikilie app hiyo kwa sekude chache alafu kunachaguzi zitatokea.
  • kwenye hizo chaguzi zilizo tokea, chagua sehemu ilio andikwa “Application details” lakini inaweza kuwa imeandikwa “Application info” au “App info”.
  • Baada ya kufanya hvyo, utapelekwa kwenye ukurasa ambao utatakiwa kutafuta sehemu palipo andikwa “Storage” na kupabonyeza.
  • Ukisha fanya hivyo, utapelekwa kwenye ukurasa mwengine na kwenye kurasa huo, utatakiwa kubonyeza sehemu walipoandika “Clear Data” na kuchagua “Ok” kwenye swali utakalo ulizwa na simu yako baada ya kufanya hivyo. (Sehemu hiyo inaweza kuandika “Clear Storage” pia)

Baada ya kufanya hayo, utakua tayari umefuta data za playstore na utatakiwa kwenda playstore yako na kuanza kuitumia kama mwanzo… Itakua ipo vizuri na haina tatizo tena.

Ikiwa umefanya yote yaliopo hapa na haujafanikiwa, huenda kunaweza kuwa na tatizo katika app unayotaka kuingia kwenye simu. Baadhi ya app huwa zina matatizo yalionje ya uwezo wako. Ila unaweza njia mbadala ya ingiza app unayohitaji ikiwa kama Apk file.

Jinsi ya kutafuta simu iliyopotea au kuibiwa

Kupoteza simu ni jambo ambalo linaweza kumtokea mtu yeyote na linaweza kuwa na athari mbaya katika maisha yetu. Simu zetu zimejaa taarifa muhimu, picha za kumbukumbu, na mawasiliano ya shughuri zetu nyingine muhimu. Wakati simu inapopotea au kuibiwa, inaweza kuleta hasara kubwa, si tu kwa kwenye akili bali pia kwa taarifa binafsi na usalama wa mwenyewe simu.



Kuna mamilioni ya simu hupotea kila mwaka Duniani Kwasababu mbalimbali na wengi huwa hawazipati simu zao. Simu inapopotea, mtu anaweza kuingia kwenye hatari za kupoteza taarifa binafsi kama vile akaunti za benki, chats muhumu, na Akaunti za mitandao ya kijamii. Bila simu, tunaweza kupoteza mawasiliano na marafiki, familia, na hata kazi tunazofanya. Hali hii inafanya tukio la kupoteza simu kuwa na athari ya kufika mpaka kujaribu maisha ya mtu.



Katika ukurasa huu, tutaangalia njia mbalimbali ambazo zinaweza kukusaidia mtu kupata simu iliyoibiwa au kupotea. Njia hizi ni rahisi kufuata na zinaweza kusaidia kupunguza hasara na kurejesha mawasiliano yako haraka iwezekanavyo.

Game zenye muonekano mzuri za Online Battle Royale BONYEZA HAPA>>>

Njia za kutafuta simu iliyopotea au kuibiwa

Kuipigia au kutuma ujumbe kwenye namba iliopo kwenye simu

Njia ya kwanza unayoweza itumia kupata simu yako iliopotea na kuitumia ujumbe au kuipigia namba ya Laini (Sim card) iliopo kwenye simu. Kupiga simu kutafanya uongee na mtu alie na simu yako kama bado haijazimwa. Kama itakua haipatikani, tuma ujumbe au sms kwenye namba hiyo ili laini ikirudi hewani, upokee taalifa ya kuwa sms imefika (Delivered report) na kujua simu yako ipo imewashwa.

Hii ni njia nzuri na rahisi kuitumia kuitafuta hata simu ya batani ilioibiwa au kupotea.

Kutumia Find My Device kujua simu ilipo

Google Find My Device ni huduma ya Google ya Bure kabisa ambayo inawezesha watu kutambua simu zao zilipo kwa kuzionesha katika Ramani. Huduma hii inampa mtu nafasi ya kuifunga simu iliopotea au kufuta vitu vilivyomo ili visionwe na mtu mwingine.


Kutumia njia hii kupata simu iliopotea utatakiwa kudownload app iitwayo “Google Find My Device” kwenye simu nyingine. Baada ya hapo, utaifungua app hiyo na kujaza Email iliopo kwenye simu ulioibiwa kisha utaletewa taalifa za simu yako na sehemu iliopo.

Kama hiyo simu iliopotea itakua imeunganishwa kwenye internet alafu imewashwa Location, utafanikiwa kuiona ilipo na kuifuatilia. Lakini kama hivyo vitu vitakua vimezimwa, hautafanikiwa kuona simu yako ilipo.

Kwa watu wa iPhone, Find My Device ya Google haiwezi wasaidia maana ni maalumu kwa simu za Android. Ukiwa na iPhone utahitaji kutumia huduma kutoka Apple inaitwa “Find My” au “iCloud Find My Devices“.

Muonekano wa app ya Find My Device katika kuitafuta simu ya Infinix Hot 8 Lite iliopotea(Mfano).

Kutumia IMEI kupata Simu ilioibiwa

Utapatikanaji wa Simu iliopotea au kuibiwa ni ngumu kufanywa na mtu binafsi kwa njia hii. Jambo hili linahitaji uhusishe polisi na utatakiwa kuwa na Sababu ya kufanya hivyo maana police au vyombo vya usalama hawatakusaidia kama umeipoteza wewe mwenyewe kwa uzembe wako au umesahau ulipoweka. Ni vema kuwa na Sababu ya msingi na inayopelekeaa kuwahusisha polisi au vyombo vya usalama.

Mwisho ningependa kusisitiza swala la kuweka vitu vyako ikiwemo simu, katika hali ya usalama. Epuka kuweka simu yako mbali na mifuko yako au mikononi mwako unapokua mbali na nyumbani.

App nzuri za simu katika kufanya mazoezi ya mwili

Kuna app nyingi ambazo tunaweza ziingiza kwnye simu zetu na zikawa msaada kwenye vitu au mambo tunayofanya kwenye maisha. Hapa kwenye ukurasa huu The bestgalaxy tumekusanya app chache zinazoweza saidi katika upande wa mazoezi ya mwili. Nadhani wengi tunajua umuhimu wa mazoezi ya mwili katika maisha ya mwanadamu, hasa katika kipindi hiki chenye mambo mengi yanayohatarisha afya ya mwili wa binadamu.

Binadamu wa sasa tumezungukwa na vyakula pamoja na tabia nyingi zisizo rafiki kwa Afya zetu, ukiwa kama mwanadamu wa kipindi hiki unashauriwa kufanya mazoezi ili kuuweka mwili sawa na kuepuka baadhi ya magonjwa. Kabla ya kwenda moja kwa moja kuangalia app hizi, nakukumbusha kuijenga na kuendelea kuilinda tabia ya kufanya mazoezi maana ni jambo la maana usiloweza kujutia maishani.

Home workouts app: credit

App nzuri za simu katika kufanya mazoezi ya mwili(Android na iOS)

Home workouts

Hii app ni maarufu sana katika upande wa app za mazoezi za simu. App ya Home workouts imejikita zaidi katika kusaidia watu wanaotaka kufanya mazoezi ya mwili wakiwa nyumbani. Inakupa mbinu za mazoezi ya kufanya ili kuweka misuli ya mwili vizuri, kupunguza uzito au kupunguza mwili. Inakuonesha jinsi unavyoweza fanya yote hayo ukiwa nyumbani bila kwenda GYM zilizo mbali na ulipo. Inaweza simama kama mwalimu au msimamizi wako wa mazoezi ya nyumbani ukiwa kama Mwanamke au Mwanaume unaempenda mazoezi.

Workout for Women

Hii app ni kwaajili ya mwanawake unaehitaji kufanya mazoezi. Kama wewe na mwanamke unaetaka kufanya mazoezi ya mwili lakini unakosa muda wa kutoka ulipo na kuelekea GYM, basi app hii inaweza kuwa masada zaidi kwako. App ya Workout for Women inasimama kama mwalimu wa nyumbani wa mazoezi ya kuweka mwili sawa. Inakupa mazoezi ya kupungiza tumbo, kuongea makalio na kufanya ujihisi mwepesi. Workout for Women inakupa mbinu za kufanya mazoezi hata ukiwa kitandani hivyo itakua ni juu yako tu kutenga dakika chache kujiweka sawa kila siku.

Strava

Strava ni app maalumu kwa watu wanaopenda kufanya mazoezi lakini mazoezi haya sio ya sehemu moja. Hii ni kwaajili ya mazoezi kama kukimbia au kuendesha baisikeli. Wengi hufanya mazoezi haya asubuhi au jioni ili kuwema miili yao sawa. App hii inasidia mtu kupima umbali anaokimbia kila siku na kujua anakimbia kutoka wapi kwenda wapi.

Inaweza kuunganishwa na saa za kidigitali zinazofahamika kama “Smartwatch” japo sio zote. Inasaidia kuangalia maendeleo katika mazoezi yako hirahisi kwenye simu. Unaweza angalia hata Hali ya mapigo yako ya moyo unapofanya mazoezi (Hii itakuitaji utumie Heart rate monitor au Smartwatch).

GYM DONE

App hii imejikita zaidi kwenye upande wa mazoezi ya GYM. Ni app inayoweza kukuongoza unapofanya mazoezi kwenye chumba Cha GYM kwakutumia vifaa mbalimbali. Kwenye app ya GYM Done unaoneshwa mbinu au namna ya kutumia vifaa vya GYM kuweka vizuri misuli ya sehemu tofauti za mwili. Mtumiaji unaweza pia kujiweka mipango yako ya mazoezi ili kukamilisha malengo yako.

App za mazoezi ya mwili zimekua zikitumika na mamilioni ya watu wanapofanya mazoezi na zimekua msaada mkubwa katika kujenga afya ya mwili. Ni app hizo tu katika orodha yetu lakini fahamu kuwa kuna app nyingi nzuri kwa mazoezi ya mwili. Endelea kuwa nasi kwa mambo mengine zaidi.