Tag Archives: pesa online

Mambo 5 ya kuzingatia katika safari ya kuanza kuingiza pesa na Facebook monetization

Baada ya Facebook kufungua rasmi njia ya kuingiza kipato kupitia program ya Content monetization, watu wengi wameanza safari ya kutafuta njia ya kufanikisha ndoto ya kupata kipato kupitia content/maudhui wanazopost.

Lakini pamoja na nafasi hiyo kubwa, sio kila mtu anafanikiwa kuipata. Wengi hushindwa kutokana na kutozingatia mambo ya msingi ambayo yanaweza kusababisha kuchelewa au hata kushindwa kabisa kufikia malengo yao.
Ili kuepuka changamoto hizo, haya chini ndio mambo 5 muhimu unayopaswa kuzingatia.

Jinsi ya kutengeneza Pesa na Facebook monetization BONYEZA HAPA>>>

Mambo 5 ya Kuzingatia unapotaka Content Monetization katika Facebook

  1. Sheria za Facebook

Unapoanza safari ya kutafuta Facebook monetization, jambo la kwanza ni kuhakikisha kuwa hauvunji sheria za Facebook. Kumbuka kuwa Facebook ina sheria na miongozo mingi ambayo ni lazima izingatiwe.

Kuvunja sheria kunaweza kukusababisha usikubaliwe kuingiza pesa hata kama una followers/wafuasi wengi. Wengine huenda mbali zaidi na kufungiwa kabisa akaunti zao. Hivyo, kabla hujapiga hatua kubwa, hakikisha unazisoma na kuelewa vizuri sheria hizo ili kukusaidia kubaki salama na kuepuka matatizo ya baadaye.

  1. Aina ya Content Unazojihusisha Nazo

Kabla ya kuanza, jiulize: “Nataka nitengeneze content gani au muundo gani?” Facebook inaruhusu content za aina nyingi kama video, picha na makala za maandishi. Lakini kwa sasa njia rahisi zaidi ya kupata monetization ni kupitia video fupi (Reels). Reels hukupa nafasi ya kuongeza Followers kwa haraka, kupata views nyingi na kuongeza uwezekano wa kulipwa.

Kwa hiyo, chagua aina ya content unayoamini utaweza kuifanya kwa ubora na kwa mtindo unaoleta matokeo mazuri kwenye upande wa views.

  1. Engagement Katika Post Zako

Engagement ni jinsi watu wanavyoshirikiana na post zako. Hii inajumuisha mambo kama; Likes, Comments, Shares, Saves na hata Followers wapya.

Kadri content zako zinavyopata engagement kubwa, ndivyo Facebook itakavyotambua thamani ya kazi zako. Engagement ya juu inarahisisha safari yako ya kufikia monetization kwa haraka na hata kukua.
Kiufupi, jitahidi kutoa maudhui yanayogusa hisia, kufundisha, kuburudisha au kusisimua ili kuwaleta watu karibu zaidi na kazi zako.

  1. Usalama wa Akaunti Yako

Akaunti za Facebook mara nyingi hulengwa na wadukuzi (hackers). Hebu Fikiria umepambana mpaka umefikia vigezo vya kulipwa katika Facebook, lakini ghafla akaunti yako imechukuliwa na hacker…. maumivu yake ni makubwa sana si ndio? Sasa hii inaweza kukukuta endapo akaunti yako haitakua salama alafu ukawa unaendelea kuitumia kutafuta monetization.

Ili kulinda mambo yako kwenye akaunti, hakikisha unafanya kuwasha, Two-factor authentication, Tumia Password ngumu alafu kuingia kwenye akaunti na vifaa visivyo salama.

Kwa kufanya hivyo, utaendelea kuwa salama na kufurahia matunda ya kazi zako bila hofu ya kupoteza kitu.

  1. Usikate Tamaa

Safari ya kufanikisha kitu mtandaoni mara nyingi si rahisi. Wakati mwingine utapost maudhui yako lakini matokeo hayataridhisha moyo wako. Hapo ndipo wengi hukata tamaa.

Lakini kumbuka: kutoacha kufanya ndio msingi wa kufanikiwa. Badala ya kukata tamaa, jifunze kutokana na changamoto, tafuta mbinu mpya, na endelea kusonga mbele. Mafanikio yanahitaji uvumilivu hata huku mtandaoni.

Facebook monetization ni nafasi nzuri sana unayoweza kuitumia kuingiza kipato kupitia content zako. Lakini ili kufanikisha safari ya kumfikia hapo, zingatia sheria za Facebook, chagua content sahihi, ongeza engagement, linda akaunti yako na usikate tamaa kwenye ufanyayo.

Facebook inalipa kiasi gani kwa kutazamwa mara 1000 (1k views)?



Facebook ni mtandao unaomilikiwa na kampuni ya meta. Katika Facebook kuna kipengele unachoweza kukiita “Facebook Ads” au “Meta Ads”. Kipengele hiki katika Facebook ni kwaajili ya makampuni au watu wanaohitaji kutangaza matangazo(Ads) kwenye mtandao wa Facebook. Kuna makampuni na watu wengi sana huwa wanailipa pesa hapo ili kuonesha matangazo kwenye mtandao wa Facebook.

Meta inatengeneza mabilioni ya pesa kwa mwaka kupitia watu wanaotangaza matangazo katika Facebook. Katika pesa hizo, huwa inachukua kiasi flani walizotengeneza na kuwalipa Content creator wa Facebook. Ili content creator kuanza kulipwa, anatakiwa kuingia katika program yao maalum kwanza(content monetization).


“Content creator” wa Facebook ni mtu ambaye huunda na kutoa maudhui (content) kwenye  Facebook ili kuwavutia, kuwaburudisha, kuwafundisha au kuhamasisha watazamaji. Na Maudhui au content zinazozungumziwa hapa ni Video, Picha na hata Makala za maandishi.

Ujuzi utakao kuwezesha kuingiza pesa mtandaoni BONYEZA HAPA>>>

Facebook inalipa kiasi gani kwa views 1000 za video?



Ukiwa kama content creator unaejihusisha na video katika Facebook, utalipwa pesa pale video zako zinapopata views (zinapoangaliwa na watu). Lakini fahamu kuwa Facebook haina kiwango maalum itakachokulipa kwa kupata views 1000 kwenye video zako. Facebook huwa inalipa kutokana na mfumo unaoitwa Cost Per Mille (CPM). Hii ina maana unalipwa kiasi kutokana na kiasi walicholipa watangazaji (watu walio lipa matangazo yanayooneshwa kwenye video zako). Yaani kama matangazo yanayooneshwa kwenye video zako hulipiwa pesa nyingi na watangazaji, basi unaweza kuingiza pesa nyingi pia ukiwa kama content creator.

Screenshot ukionesha jinsi Facebook ilivyomlipa moja ya Content creator wa India kwa video 1 fupi (Reel).


Lakini pia kiasi unacholipwa Facebook creator kinaweza kuathiliwa na mambo mengine kama nchi ya mtazamaji, sekta unayojihusisha nayo na hata tabia za watu wako katika Ads wanazoangalia.

  • Nchi ya watazamaji wako (mfano Marekani na Ulaya CPM huwa kubwa kuliko Afrika).
  • Mada/sekta ya content zako (mfano video za biashara, fedha, teknolojia hulipa zaidi kuliko utani au burudani tu).
  • Tabia za watazamaji kwenye Ads(watazamaji wakiwa wanajihusisha na Ads kwa kuziangalia au kubonyeza).

Muhimu kujua: katika Facebook kuna aina mbili za video. Video ndefu na video fupi ambazo huitwa “Reels”. Malipo hati ya aina hizo za video huwa yanatofatulia kabisa. Ukijihusisha na Reel unaweza ulipwe pesa ndogo sana kwa views 1000 ila uzuri ni kwamba huwa zinaweza kufika views milioni 1 kirahisi kuliko video ndefu.

Reels zinaweza kulipa $0.20 – $1.00+ kwa views 1000 (kutegemeana na nchi au mengineyo). Alafu video ndefu zinaweza kuwa $1 – $10+ kwa views 1000, hasa kwenye niche za biashara, fedha au teknolojia.

Jinsi ya kuuza Beats za Muziki Mtandaoni (Online)

Watu wengi(Music Producers) wana kipaji cha kutengeneza beats za muziki lakini changamoto kubwa inabaki kuwa jinsi ya kuziuza na kupata kipato. Kwa sasa, teknolojia imerahisisha sana upande huu, unaweza kuuza beats zako kwa wasanii bila hata kuwa na studio kubwa. Tena unaweza kuwafikia watu Toka nchi mbalimbali wakawa Wateja wako.

Hapa chini kuna njia tatu bora za kuuza beats zako mtandaoni. Unaweza zitumia ikiwa wewe ni producer unahitaji kutengeneza Pesa mtandaoni kupitia Beats zako.

Njia 3 za kuuza beats zako mtandaoni:

  1. Tumia Platform Maalum kwa Uuzaji wa Beats

Kuna tovuti nyingi ambazo zimetengenezwa mahsusi kwa wauzaji wa beats. Hizi platform zinakuwezesha ku-uproad kazi zako na kuziuza moja kwa moja kwa wasanii kutoka sehemu mbalimbali duniani. Baadhi ya mifano ni:

BeatStars

Airbit

Traktrain

Unachohitaji ni kufungua akaunti(inaweza kuhitaji kulipia ili kuanza kuitumia), kuweka bei zako, na ku-uproad beats zako. Hii ni njia rahisi na salama kwa sababu wateja wengine watatoka ndani ya hiyo hiyo platform ana watalipia kupitia mfumo wanaoujua, na wewe unapokea malipo yako.

Huu ni ukurasa wa tuvuti/website ya Beatstars ukionesha Beats zinazouzwa.
  1. Kuwa na Website Yako ya Kuuza Beats

Kama unataka kuwa na brand yako binafsi, basi kuwa na website ni muhimu. Kupitia website yako, Wateja wataona beats zako zote kwa mpangilio mzuri. Unaweza kuweka mfumo wa malipo (Card, Crypto, Skrill, M-Pesa, n.k).

Inakusaidia kujenga jina lako kama producer professional.

Website yako inaweza pia kuwa sehemu ya kuonyesha huduma nyingine unazotoa kama mixing & mastering, au hata tutorials za muziki.

  1. Uza Kupitia Mitandao ya Kijamii

Mitandao ya kijamii ni soko kubwa la bure. Tumia Instagram, TikTok na Facebook kuonyesha vipande vya beats zako. Unaweza ku-uproad video fupi za beats alafu wasanii watakao lipenda beat, wanakua wanakutafuta inbox kwaajili ya maelewano ya kibiasha.

Unaweza pia kutumia captions nzuri na kutoa challenge mbalimbali kwa wasanii juu ya Beats zako ili kupata Wateja zaidi.

Mitandao ya kijamii hukusaidia kufikia watu wengi bila gharama kubwa, ila unahitaji kuwa consistent na ubunifu kwenye content unayoshare.

Kuuza beats mtandaoni siyo kazi ngumu kama ukipanga vizuri mfumo wako. Unaweza kuanza na platform za kuuza beats, kisha kujenga website yako, na hatimaye kutumia nguvu ya mitandao ya kijamii kupata wateja zaidi. Yani mfumo wako ukiwa vizuri, unaweza tumia njia zote tatu kama ulimwengu wa kuuza beats zako.

Kutengeneza au kurekodi nyimbo kwa simu BONYEZA HAPA>>>

App zinazo kupa pesa kwa kufanya kitu kidogo kwako (Unazitumia Kila siku)

Hapa chini The bestgalaxy nimekuandalia orodha ya app chache ambazo zinaweza kupa zawadi ya pesa kwa kufanya jambo flani dogo linaloweza kuwa jepesi kwako.  Lakini kabla ya yote ufahamu kuwa pesa hizi ni ndogo sana na haziwezi kukufanya upate utajiri. Pia fahamu kuwa hizi app ni app ambazo hutoa pesa kama zawadi lakini sio app rasim kwenye upande huo. Hizi ni app rasmi katika upande wa kurahisisha upatikanaji wa huduma au mahitaji kirahisi. Yawezekana unazitumia kila siku. Kuna wakati tutazungumzia kuhusu platform rasimi kwa kutengeneza pesa nyingi.

Tunaweka app kwenye simu zetu kwasababu mbalimbali na moja kati ya sababu ya kuweka baadhi ya app ni kupata huduma au amahitaji kirahisi kwa kutumia simu. Mfano, kuna app ambazo tunaweka kwenye simu ili tuweze kupata huduma za kifedha kihisi kwenye simu zetu na pia  kuna app hurahisisha manunuzi ya vitu kwa kutusogezea bidhaa tunazoweza nunua kwenye simu zetu.

App zinazo kupa pesa kwa kufanya kitu kidogo kwako (Android)

Farasi

Farasi ni moja ya app ambazo zinajihusisha na maswala ya usafili. Kwakutumia app hii unaweza pata usafiri wa kukutoa ulipo mpaka mahali unapotaka kwenda kirahisi. App hii inakutumika na watu wengi tu katika maswala ya usafiri. App hii hua inatoa zawadi kwa watumiaji wake pale wanapoitumia kupata usafiri. Kwasasa unapoanza kuitumia unapata Tsh 3000 mbali na zawadi nyingine utazopata unapotumia. Angalia app kwa KUBONEZA HAPA alafu kama utakua unajiunga usisahau kujaza namba 715233405 kwenye kibox cha referral code.

Branch app

App ya Branch ni app ya mikopo. Ni moja kati ya app nzuri sana katika upande wa app zinazokuwezesha kupata mikopo kwenye simu Tanzania. App hii inaweza kukupa zawadi ya pesa pele unaporudisha pesa kwa mara ya kwanza baada ya kuazima ila kupata zawadi hii ni lazimu uwe umealikwa. BONYEZA HAPA kupata maelezo zaidi ya app hii na zawadi zake

Tigo pesa app

App ya Tigo pesa ni app ambayo hurahisisha zaidi maswala ya kufanya miamala kwa watumiaji wa Tigo. App  hii huwa anatoa kiasi kido cha pesa kama zawadi pale unapomualika rafiki yako. Kama unarafiki ambae anatumia mtandapo wa Tigo lakini ana app, unaweza mualika huyo rafiki alafu akapatiwa zawadi ya pesa kwenye akaunti yako ya Tigo pesa. Kama hauna app ya Tigo pesa, INGIA HAPA kuipakua.

Mwisho ningependa kukukumbusa tu kuwa app hizi sio app rasimi kwa kutengeneza pesa, zinatoa pesa kama zawadi TU.