Tag Archives: pesa mtandaoni
Mambo 5 ya kuzingatia katika safari ya kuanza kuingiza pesa na Facebook monetization
Baada ya Facebook kufungua rasmi njia ya kuingiza kipato kupitia program ya Content monetization, watu wengi wameanza safari ya kutafuta njia ya kufanikisha ndoto ya kupata kipato kupitia content/maudhui wanazopost.
Lakini pamoja na nafasi hiyo kubwa, sio kila mtu anafanikiwa kuipata. Wengi hushindwa kutokana na kutozingatia mambo ya msingi ambayo yanaweza kusababisha kuchelewa au hata kushindwa kabisa kufikia malengo yao.
Ili kuepuka changamoto hizo, haya chini ndio mambo 5 muhimu unayopaswa kuzingatia.
Jinsi ya kutengeneza Pesa na Facebook monetization BONYEZA HAPA>>>
Mambo 5 ya Kuzingatia unapotaka Content Monetization katika Facebook
- Sheria za Facebook
Unapoanza safari ya kutafuta Facebook monetization, jambo la kwanza ni kuhakikisha kuwa hauvunji sheria za Facebook. Kumbuka kuwa Facebook ina sheria na miongozo mingi ambayo ni lazima izingatiwe.
Kuvunja sheria kunaweza kukusababisha usikubaliwe kuingiza pesa hata kama una followers/wafuasi wengi. Wengine huenda mbali zaidi na kufungiwa kabisa akaunti zao. Hivyo, kabla hujapiga hatua kubwa, hakikisha unazisoma na kuelewa vizuri sheria hizo ili kukusaidia kubaki salama na kuepuka matatizo ya baadaye.
- Aina ya Content Unazojihusisha Nazo
Kabla ya kuanza, jiulize: “Nataka nitengeneze content gani au muundo gani?” Facebook inaruhusu content za aina nyingi kama video, picha na makala za maandishi. Lakini kwa sasa njia rahisi zaidi ya kupata monetization ni kupitia video fupi (Reels). Reels hukupa nafasi ya kuongeza Followers kwa haraka, kupata views nyingi na kuongeza uwezekano wa kulipwa.
Kwa hiyo, chagua aina ya content unayoamini utaweza kuifanya kwa ubora na kwa mtindo unaoleta matokeo mazuri kwenye upande wa views.
- Engagement Katika Post Zako
Engagement ni jinsi watu wanavyoshirikiana na post zako. Hii inajumuisha mambo kama; Likes, Comments, Shares, Saves na hata Followers wapya.
Kadri content zako zinavyopata engagement kubwa, ndivyo Facebook itakavyotambua thamani ya kazi zako. Engagement ya juu inarahisisha safari yako ya kufikia monetization kwa haraka na hata kukua.
Kiufupi, jitahidi kutoa maudhui yanayogusa hisia, kufundisha, kuburudisha au kusisimua ili kuwaleta watu karibu zaidi na kazi zako.

- Usalama wa Akaunti Yako
Akaunti za Facebook mara nyingi hulengwa na wadukuzi (hackers). Hebu Fikiria umepambana mpaka umefikia vigezo vya kulipwa katika Facebook, lakini ghafla akaunti yako imechukuliwa na hacker…. maumivu yake ni makubwa sana si ndio? Sasa hii inaweza kukukuta endapo akaunti yako haitakua salama alafu ukawa unaendelea kuitumia kutafuta monetization.
Ili kulinda mambo yako kwenye akaunti, hakikisha unafanya kuwasha, Two-factor authentication, Tumia Password ngumu alafu kuingia kwenye akaunti na vifaa visivyo salama.
Kwa kufanya hivyo, utaendelea kuwa salama na kufurahia matunda ya kazi zako bila hofu ya kupoteza kitu.
- Usikate Tamaa
Safari ya kufanikisha kitu mtandaoni mara nyingi si rahisi. Wakati mwingine utapost maudhui yako lakini matokeo hayataridhisha moyo wako. Hapo ndipo wengi hukata tamaa.
Lakini kumbuka: kutoacha kufanya ndio msingi wa kufanikiwa. Badala ya kukata tamaa, jifunze kutokana na changamoto, tafuta mbinu mpya, na endelea kusonga mbele. Mafanikio yanahitaji uvumilivu hata huku mtandaoni.
Facebook monetization ni nafasi nzuri sana unayoweza kuitumia kuingiza kipato kupitia content zako. Lakini ili kufanikisha safari ya kumfikia hapo, zingatia sheria za Facebook, chagua content sahihi, ongeza engagement, linda akaunti yako na usikate tamaa kwenye ufanyayo.
Facebook inalipa kiasi gani kwa kutazamwa mara 1000 (1k views)?
Facebook ni mtandao unaomilikiwa na kampuni ya meta. Katika Facebook kuna kipengele unachoweza kukiita “Facebook Ads” au “Meta Ads”. Kipengele hiki katika Facebook ni kwaajili ya makampuni au watu wanaohitaji kutangaza matangazo(Ads) kwenye mtandao wa Facebook. Kuna makampuni na watu wengi sana huwa wanailipa pesa hapo ili kuonesha matangazo kwenye mtandao wa Facebook.
Meta inatengeneza mabilioni ya pesa kwa mwaka kupitia watu wanaotangaza matangazo katika Facebook. Katika pesa hizo, huwa inachukua kiasi flani walizotengeneza na kuwalipa Content creator wa Facebook. Ili content creator kuanza kulipwa, anatakiwa kuingia katika program yao maalum kwanza(content monetization).
“Content creator” wa Facebook ni mtu ambaye huunda na kutoa maudhui (content) kwenye Facebook ili kuwavutia, kuwaburudisha, kuwafundisha au kuhamasisha watazamaji. Na Maudhui au content zinazozungumziwa hapa ni Video, Picha na hata Makala za maandishi.
Ujuzi utakao kuwezesha kuingiza pesa mtandaoni BONYEZA HAPA>>>
Facebook inalipa kiasi gani kwa views 1000 za video?
Ukiwa kama content creator unaejihusisha na video katika Facebook, utalipwa pesa pale video zako zinapopata views (zinapoangaliwa na watu). Lakini fahamu kuwa Facebook haina kiwango maalum itakachokulipa kwa kupata views 1000 kwenye video zako. Facebook huwa inalipa kutokana na mfumo unaoitwa Cost Per Mille (CPM). Hii ina maana unalipwa kiasi kutokana na kiasi walicholipa watangazaji (watu walio lipa matangazo yanayooneshwa kwenye video zako). Yaani kama matangazo yanayooneshwa kwenye video zako hulipiwa pesa nyingi na watangazaji, basi unaweza kuingiza pesa nyingi pia ukiwa kama content creator.

Lakini pia kiasi unacholipwa Facebook creator kinaweza kuathiliwa na mambo mengine kama nchi ya mtazamaji, sekta unayojihusisha nayo na hata tabia za watu wako katika Ads wanazoangalia.
- Nchi ya watazamaji wako (mfano Marekani na Ulaya CPM huwa kubwa kuliko Afrika).
- Mada/sekta ya content zako (mfano video za biashara, fedha, teknolojia hulipa zaidi kuliko utani au burudani tu).
- Tabia za watazamaji kwenye Ads(watazamaji wakiwa wanajihusisha na Ads kwa kuziangalia au kubonyeza).
Muhimu kujua: katika Facebook kuna aina mbili za video. Video ndefu na video fupi ambazo huitwa “Reels”. Malipo hati ya aina hizo za video huwa yanatofatulia kabisa. Ukijihusisha na Reel unaweza ulipwe pesa ndogo sana kwa views 1000 ila uzuri ni kwamba huwa zinaweza kufika views milioni 1 kirahisi kuliko video ndefu.
Reels zinaweza kulipa $0.20 – $1.00+ kwa views 1000 (kutegemeana na nchi au mengineyo). Alafu video ndefu zinaweza kuwa $1 – $10+ kwa views 1000, hasa kwenye niche za biashara, fedha au teknolojia.

Jinsi ya kuuza Beats za Muziki Mtandaoni (Online)
Watu wengi(Music Producers) wana kipaji cha kutengeneza beats za muziki lakini changamoto kubwa inabaki kuwa jinsi ya kuziuza na kupata kipato. Kwa sasa, teknolojia imerahisisha sana upande huu, unaweza kuuza beats zako kwa wasanii bila hata kuwa na studio kubwa. Tena unaweza kuwafikia watu Toka nchi mbalimbali wakawa Wateja wako.
Hapa chini kuna njia tatu bora za kuuza beats zako mtandaoni. Unaweza zitumia ikiwa wewe ni producer unahitaji kutengeneza Pesa mtandaoni kupitia Beats zako.
Njia 3 za kuuza beats zako mtandaoni:
- Tumia Platform Maalum kwa Uuzaji wa Beats
Kuna tovuti nyingi ambazo zimetengenezwa mahsusi kwa wauzaji wa beats. Hizi platform zinakuwezesha ku-uproad kazi zako na kuziuza moja kwa moja kwa wasanii kutoka sehemu mbalimbali duniani. Baadhi ya mifano ni:
Unachohitaji ni kufungua akaunti(inaweza kuhitaji kulipia ili kuanza kuitumia), kuweka bei zako, na ku-uproad beats zako. Hii ni njia rahisi na salama kwa sababu wateja wengine watatoka ndani ya hiyo hiyo platform ana watalipia kupitia mfumo wanaoujua, na wewe unapokea malipo yako.

- Kuwa na Website Yako ya Kuuza Beats
Kama unataka kuwa na brand yako binafsi, basi kuwa na website ni muhimu. Kupitia website yako, Wateja wataona beats zako zote kwa mpangilio mzuri. Unaweza kuweka mfumo wa malipo (Card, Crypto, Skrill, M-Pesa, n.k).
Inakusaidia kujenga jina lako kama producer professional.
Website yako inaweza pia kuwa sehemu ya kuonyesha huduma nyingine unazotoa kama mixing & mastering, au hata tutorials za muziki.
- Uza Kupitia Mitandao ya Kijamii
Mitandao ya kijamii ni soko kubwa la bure. Tumia Instagram, TikTok na Facebook kuonyesha vipande vya beats zako. Unaweza ku-uproad video fupi za beats alafu wasanii watakao lipenda beat, wanakua wanakutafuta inbox kwaajili ya maelewano ya kibiasha.
Unaweza pia kutumia captions nzuri na kutoa challenge mbalimbali kwa wasanii juu ya Beats zako ili kupata Wateja zaidi.
Mitandao ya kijamii hukusaidia kufikia watu wengi bila gharama kubwa, ila unahitaji kuwa consistent na ubunifu kwenye content unayoshare.
Kuuza beats mtandaoni siyo kazi ngumu kama ukipanga vizuri mfumo wako. Unaweza kuanza na platform za kuuza beats, kisha kujenga website yako, na hatimaye kutumia nguvu ya mitandao ya kijamii kupata wateja zaidi. Yani mfumo wako ukiwa vizuri, unaweza tumia njia zote tatu kama ulimwengu wa kuuza beats zako.
Unataka kujua Cryptocurrency ni nini? Jifuze hapa
Kiufupi Cryptocurrency ni sarafu au pesa ya kidigitali ambayo mtu anaweza kutuma au kuipokea mtandaoni lakini huwa ipo huru kwa kutokua chini ya Benk kuu au serikali. Ni watu tu huamini na kuanza kuitumia au kuacha kutumia. Na hauwezi kuigusa kama pesa za kawaida maana ipo mtandaoni tu.
Sarafu hii ya kidijitali (digital currency) inatumia mbinu za usalama za kisasa (cryptography) ili kuhakikisha miamala (transactions) ni salama na kudhibiti uundwaji wa sarafu mpya(bandia. Unaweza kuzituma pesa hizi kwa mtu kama malipo au ukazipokea na kuzitunza kama ilivyo kwenye pesa za kawaida.
Cryptocurrency(pesa za mtandaoni) huwa zipo nyingi na zina majina tofauti. Mfano wa cryptocurrency maalufu duniani ni:
- Bitcoin (BTC)
- Ethereum (ETH)
- Binance Coin (BNB)
- Tether (USDT)

Unatunza vipi Cryptocurrency?
Cryptocurrency huwa zinatunzwa katika mfuko maalum wa pesa za kidigitali. Mfuko huu huitwa “digital crypto wallet” na hufanya kazi kama sehemu unayoweza kutunza pesa zako kidigitali au kufanya miamala. Mtu alieweka cryptocurrency kwenye digital crypto wallet ni sawa mtu alieweka pesa za kawaida katika Bank au akaunti nyingine za pesa kama Mpesa.
Kuna platform nyingi mtandaoni huwa zinakuwezesha mtu kufungua akaunti na kumiliki mfuko wako wa kuwekea Cryptocurrency Bure kabisa. Mfano wa platform hizo ni Binance.
Mtu alieweka cryptocurrency kwenye digital crypto wallet kama Binance ni sawa mtu alieweka pesa za kawaida katika Bank au akaunti nyingine za pesa kama Mpesa.
Jinsi ya kutengeneza Pesa mtandaoni kwa kuandika BONYEZA HAPA>>>
Unawezaje kupata Cryptocurrency?
Kama na wewe unahitaji kuwa na pesa za crypto, utahitajika kuwa na mfuko kwanza wa kutunzia(crypto wallet). Baada ya hapo unaweza tumia njia hizi mbili za kupata Cryptocurrency kwenye mfuko wako:
Njia ya kwanza ya kupata Cryptocurrency ni kuzinunua kwa pesa zako za kawaida. Yani unatumia pesa yako ya kawaida kuinunua pesa ya mtandaoni (cryptocurrency) alafu unaitunza kwenye mfuko wako wa crypto. Hii tunaweza kuiita “kubadilishana na pesa za kawaida”, yaani exchange. Mfano; Ukitaka kupata USDT moja (1), utatakiwa kuwa na kama Tsh 2600 (makadilio). Ukitaka BITCOIN moja (1), unaweza kuipata kwa Tsh milioni 200 na zaidi.
Thamani za huwa zinatofautiana alafu pia huwa zinapanda na kushuka. Mbali ya hilo, fahamu tu kuwa Kuna zenye thamani ndogo na kuna zenye thamani kubwa pia.
Njia ya pili ni kutoa huduma au kufanya huduma itakayokupa au kukulipa kwa cryptocurrency. Kuna huduma unaweza kutoa mtandaoni alafu ukapewa cryptocurrency kama malipo bila kutumia pesa yako ya kawaida. Mfano wa huduma hizi ambayo ni rahisi kabisa ni huduma ya Opera news hub ambayo tumeizungumzia sana kwenye Makala za The Bestgalaxy.
Watu wengi wanatumia cryptocurrency kulipia vitu au kufanya biashara mtandaoni kwa sasa lakini Teknolojia yake ipo kwenye hatua ya ukuaji na maboresho. Huwa inaaminika kuwa cryptocurrency inaweza kuwa ndio pesa zitakazokua zinatumiaka katika miaka ijayo badala ya kutumia pesa za kawaida.

Mambo gani muhimu ya kujua kuhusu cryptocurrency?
Pamoja na yote, Kuna changamoto ambazo kila mtu anapaswa kujua kabla ya kuingia kwenye ulimwengu wa crypto. Kati ya Changamoto kubwa ni zifuatazo:
Usalama wa crypto ni mdogo kuliko pesa za kawaida. Usipokua na kuelewa mzuri, unaweza kutapeliwa kirahisi kutokana na wingi wa matapeli katika upande huu.
Cryptocurrency zinaweza kushuka thamani muda wowote. Yani unaweza kutuza cryptocurrency zako Leo zenye thamani ya milioni 1, alafu kesho ukaamka na kukuta zimeshuka thamani kutokana na jambo flani, zomekua ni laki 5. Kwaiyo kwenye ulimwengu huu unatakiwa kuwa mtu unaweza ku-manage risk.
Cryptocurrency huwa haiwezi kulipia vitu vingi sana kwenye maisha ya kawaida. Kuna huduma nyingi ambazo Bado hazijaitambua cryptocurrency katika malipo kwasababu mbalimbali.
Disclaimer: This article is for education only and is not financial advice. Always do your own research before making any decisions.

Jinsi ya kutengeneza Pesa katika channel ya WhatsApp kwa kutumia Opera news hub
Mtandao wa WhatsApp unaweza kufanya uungane na kuwasiliana watu mbalimbali. Lakini katika mtandao huu unaweza pia ukaingiza pesa na kuwa moja ya watu wanaotumia mtandao vizuri.
Watu wengi huwa wanatamani kujua ni jinsi gani mtu anaweza kuingiza pesa mtandaoni. WhatsApp ni moja ya mitandao ambayo mtu anaweza kujifunza kuutumia kutengeneza Pesa na akawa amefanikiwa kuitwa mtu anaetengeneza pesa mtandaoni. Kwaiyo ikiwa wewe ni mmoja wanaotaka kujua namna ya kutengeneza Pesa mtandaoni, mtandao huu unaweza kuwa upande mzuri.
Jinsi ya kutengeneza Pesa kwa kucheza games mtandaoni BONYEZA HAPA>>>
Kwenye Makala hii, unaenda kujifunza namna ya kutengeneza Pesa kwenye Channel ya WhatsApp(WhatsApp channel) na tutatumia Opera news hub kufanya hivyo. Tuanze kwa kufahamu vitu hivi viwili kwanza;
- Channel ya WhatsApp(WhatsApp channel): Hiki ni kipengele cha WhatsApp ambacho kina kuwezesha mtumiaji wa WhatsApp kuwa na Followers/wafuasi. Unaweza kuwatumia wafuasi Picha, Makala na kushiri nao mambo mbalimbali kama ilivyo kwenye kurasa za Instagram au Facebook. Kila mtumiaji wa WhatsApp anaweza kumiliki channel yake bila shida yoyote.
- Opera news hub: Hii ni platform ambayo huwa inalipa watu kwa kuandika Makala mbalimbali. Mtu huwa analipwa pesa kutokana makala zake zilizosomwa na watu. Wingi wa wasomaji, unaweza kuwa ndio wingi wa mapato pia. Kusoma zaidi kuhusu hii BONYEZA HAPA>>>
Jinsi ya kutengeneza pesa katika WhatsApp channels kwa kutumia Opera news hub
Iwapo mtu utafanikiwa kumili channel ya WhatsApp yenye wafuatiliaji wengi, Kuna namna unaweza kuitumia kuingia pesa kupitia Opera news hub. Utakua unaitumia channel ya WhatsApp kupata wasomaji wa Makala zako za Opera news hub ili ulipwe na Opera news hub. Utakachotakiwa kufanya ili kufanikisha hayo yote ni kufuata hatua zifuatazo tu;
- Fungua akaunti ya Opera news hub kisha utaanza kuandika Makala nzuri kwaajili ya followers wako wa Channel ya WhatsApp. Mfano; Unaweza kuandika Makala za Michezo kama channel yako ni kuhusu Michezo.
- Baada ya hapo, utakua ukizituma link za Makala katika Channel yako ya WhatsApp.
- Endapo Makala zako zitapata wasomaji wengi wanaozisoma kutoka kwenye channel yako ya WhatsApp, utaingiza pesa kwenye akaunti yako ya Opera news hub.
Kwa kufuata hayo yote, utakua umefanikiwa kuingiza pesa kwenye WhatsApp channel yako kwa msaada wa Opera news hub. Pesa ambazo unaweza kuzitengeneza, zinategemeana na watu ambao ni wasomaji wa Makala zako. Kama utakua na watu wengi wanaozisoma, pesa pia itakua ni nyingi.
Opera News Hub: Jinsi ya kufungua akaunti, kutengeneza pesa na kupokea
Opera News Hub ni platform ambayo inawezesha watu kuingiza pesa kwa kutengeneza contents (mahudhui). Kama ni muandishi, hii inaweza kuwa moja ya platform nzuri kuitumia unapokua unahitaji kutengeneza Pesa kwa kuandika ukiwa Tanzania. Kuna kipindi platform hii hilikua haipatikani kwa waandishi wa Tanzania huku baadhi ya nchi jirani wakiwa na uwezo wakuitumia. Lakini kwasasa Mwandishi, ukiwa Tanzania unaweza kufungua akaunti, kutengeneza pesa na kuzipokea bila tatizo.
Jinsi ya kufungua akaunti ya Opera news hub
Ukihitaji kufungua account ya Opera news hub, Anza kwa kutembelea tuvuti ya Opera news hub ambayo ni https://hub.opera.com/ kwenye web browser yako. Baada ya kuingia kwenye tuvuti, utatakiwa kuanza kutengeneza akaunti yako kwa Gmail au Facebook akaunti. Kutumia Gmail ni chaguo zuri zaidi maana unaweza pata matatizo kwenye akaunti yako ya Facebook kirahisi zaidi kuliko Gmail(Gmail ni salama zaidi katika kufungua akaunti).
Kwenye mchakato wa kutengeneza akaunti utatakiwa kujaza taalifa zako kama kama vile majina Kamili, nchi unayotoka na namba za kitambulisho chako na jina unalotaka kuitumia kwenye Opera news hub. Mbali na taalifa hizo kuna namba za wallet utatakiwa kizijaza. Namba hizi za wallet utazipata kwa kupakua app ya Minipay na kufungua akaunti ya Minipay kwa kutumia namba yako ya simu.
Minipay ni app ambayo inatumika kama mfuko wa kupokea hela za mtandaoni. App hii inapatikana kwenye Playstore and hata Appstore ukihitaji kuipakua. Katika ku verify namba yako kwenye Minipa, verification code zitatumwa kwenye WhatsApp hivyo hakikisha namba tunayoitumia, unatumia kwenye WhatsApp pia.
Ukishajaza namba ya wallet na vitu vingine, utafanikiwa kutengeneza akaunti yako Bure kabisa. Utakua na uwezo wa kuingia kwenye akaunti yako ya Opera news hub kwa kutumia simu yako au PC. Uzuri ni kwamba kama unahitaji app ya Opera news hub pia ipo! Unaweza ichukua Toka Playstore au Appstore.
Jinsi ya kutengeneza pesa katika Opera news hub
Katika Opera news hub, waandishi wanaweza andika Makala zao na kuzichapisha ili zisomwe na watu wengine. Endapo Makala za muandishi zitakua zikisomwa watu, pesa itakua inaingia katika akaunti ya muandishi kwakua amefanya kazi nzuri inayochaguliwa au kupendwa na watu. Hapa nazungumiza zile Makala ambazo zinapata click nyingi (Mibofyo), likes, na hata comments (maoni).
Ili kufanya vizuri zaidi kwenye Opera news hub kama muandishi, ni vema ukawa unatoa Makala za habari na vitu vinavyo trend. Hii itakusaidia kupata wasomaji wengi na kuingiza pesa zaidi. Uwe na uwezo wa kutengeneza hata Makala 5 au 10 kabisa kwa siku ili kutengeneza Pesa nzuri katika mwezi. Pesa zote utakazotengeneza kwenye Makala yako, utakua unaziona kwenye akaunti yako.

Jinsi ya kupokea pesa katika Opera news hub
Pesa ulizotengeneza kwenye Opera news hub utakua ukizipokea kila mwezi. Pesa hizo zitakua zinaingia kwenye akaunti yako ya Minipay.
Minipay ni app ambayo inatumika kama mfuko wa kupokelea hela mtandaoni. Uzuri ni kwamba tumeisha iongelea hapo juu, hivyo hatutazungumzia sana hapa.
Kwaiyo pesa zitaingia kwenye akaunti yako ya Minipay na utakua na uwezo wa kuzitoa hata kwenye simu yako tu kupitia Mpesa, Mixx by Yas, Airtel Money na hata Bank ikiwezekana.
Kwa kufanya hayo yote, utakua umefanikiwa kuingiza pesa kwa kuandika mtandaoni kupitia Opera news hub. Mwisho, ningependa kusisitiza kuwa Makala za mambo ya habari na mambo “trend” huwa zina nafasi kubwa ya kufanya vizuri. Ikiwa utakua na Makala mbali na hizo itakuhitaji uweke jitihada zaidi kwenye kuchapisha Makala mpya kila mara.
Muhimu: Maelezo haya yanajitosheleza kabisa kukusaidia wewe kuanza kuingiza pesa endapo utayafuata na kuanza kazi.
Lakini kama utahitaji msaada wa moja kwa moja wa kufunguliwa akaunti na kuunganisha kila kitu bila kupoteza muda, unaweza kutuma ujumbe WhatsApp +255 622 586 399 tukusaidie kila kitu ili kazi yako inayobaki ni kuandika Makala na kuhesabu mapato yako.
Jinsi ya kutengeneza Pesa mtandaoni kwa kuandika (Uandishi)
Unaweza kuandika kupitia PC au simu yako ya mkononi? Kama jibu lako ni “Ndio” basi tambua kuwa kuna namna unaweza tengeneza pesa mtandaoni. Kwenye mtandao kuna nafasi ya karibu kila mtu kutengeneza Pesa mtandaoni. Kitu kikubwa na muhimu ni kujua namna gani unaweza fanya hivyo.
Kwa kuandika tu mtu unaweza tengeneza zaidi 1000 $ kwa mwezi ambazo ni sawa na zaidi ya milioni mbili. Lakini pesa inayotengenezwa huwa inategemeana na njia anayotumia, nguvu ulioiweka na sehemu ulioilenga. Kwaiyo haimaanishi kila mtu anaweza tengeneza pesa nyingi kupitia uandishi mtandaoni.
Hapa chini The bestgalaxy tunajaribu kukupa mwanga wa namna gani mtu unaweza tengeneza pesa kwa uandishi. Tutaangalia njia chache mambazo ni nzuri kwa mwandishi kuitumia katika kipindi hiki. Unataka kufahamu? Basi, twende pamoja!
Ujuzi utakaokuwezesha kutengeneza Pesa mtandaoni BONYEZA HAPA>>>
Njia za kutengeneza Pesa mtandaoni kwa kuandika
1. Kutengeneza na kuuza E-books
Unaweza ingiza pesa nyingi kwa kutengeneza na kuuza E-books. E-books ni vitabu vilivyo katika mfumo wa kidigitali na huwa vinanunuliwa na watu wengi mtandaoni. Mtu unaweza kuandika kitabu chako kwa simu au PC kupitia app kama WPS office kisha ukakiuza kwa watu mtandaoni.
Wateja ya ebooks wapo karibia ulimwengu mzima hivyo unaweza kutengeneza na kuuza kitabu chako hata nje ya nchi. Lakini kama tunavyojua; mtu hawezi soma kitabu kisicho mvutia au kisicho kwenye lugha yake. Hivyo ukihitaji kupata wateja wa nchi za nje, utatakiwa kukiandika kitabu chako kwa kuwalenga wanunuzi wa nje pia.
Kama unataka kuuza E-books kwa Africa mashariki, unaweza tumia hata WhatsApp na mitandao mingine ya kijamii tunayoitumia. Lakini ukilenga watu wa nje hapo, ni vema unatumia platform maalum za kuzuia vitabu. Mfano mzuri wa platform za kuzia vitabu mtandaoni hizi ni Amazon KDP.
2. Kuandika kwenye platform zinazolipa waandishi
Unafahamu kuwa kuna platform ambazo zinakulipa moja kwa moja kwa kuandika tu? Kama haujui, basi fahamu hilo kwanzia sasa. Unaweza tengeneza pesa nyingi tu kupitia uandishi wako ingawa itakuhitaji kujitoa sana ili kuweza kuingiza hizo pesa nyingi.
Medium, mtandao wa X(twitter) na Opera news hub ni kati ya platform zinazolipa kwa kuandika. Kwenye hizi platform 3 nilizotaja hapa, Opera news hub ni platform rahisi sana kwa watu wa Africa mashariki kuanza nayo. Inagawa pesa unayoweza tengeneza ni yakawaidi lakini mfumo wa kufanya kazi na kupokea pesa yako, umenyooka zaidi kuliko hizo platform nyingine hapo (Wanalipa pesa kirahisi kupitia app yao ya Minipay).
3. Kutoa huduma za Uandishi kwenye tuvuti za freelancing
Mtindo wa kufanya kazi kwa kuajiriwa kwa muda na wateja tofauti, bila kuwa mfanyakazi rasmi huwa unafahamika kama “freelancing”. Na tuvuti za freelancing ndio sehemu maalum kwa watu wanafanya kazi kwa mtindo huu. Ni kama sehemu ya kukutana na watu wanaoweza kukupa kazi za muda mfupi na kukulipa bila kukuajiri kabisa.
Sasa kama wewe unahitaji kutengeneza Pesa kwa kuandika, basi unaweza Ingia kwenye tuvuti za freelancing ili kupata watu wanaoweza kukupa kazi za kuandika mambo mambo mbalimbali bila kukuajiri moja kwa moja. Hautakua wakwanza kufanya hivyo maana Kuna watu wengi sana Duniani wanaingiza pasa kupitia tuvuti za freelancing kama Fiverr kupata kazi fupi za Uandishi na kuingiza pesa nyingi sana.
Nadhani mpaka hapa umeisha pata picha ya namna unaweza tengeneza pesa mtandaoni kwa kuandika. Asante sana kwa muda wako lakini kabla haujaondoka, ningependa kufahamu kuwana hii sio tu Makala ya kusoma bali ni mwanzo nzuri wa kuelewa jinsi gani unaweza jiajiri mwenyewe mtandaoni.
Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy na usisahau kufuatilia simulizi ya MIAKA IJAYO ili kuiweka sawa na mambo yajayo katika ulimwengu.

Jinsi ya kutuma pesa Kenya na Tanzania (Vodacom/Safaricom)
Kutuma pesa nje ya nchi ilikua ni jambo gumu sana katika miaka ya nyuma, lakini wakati huu jambo hili ni jambo jepesi kiasi kiasi kwamba unaweza fanya kiganjani pako ndani ya dakika mbili. Hii yote ni kwasababu ya Teknolojia ambayo lengo lake ni kurahisisha maisha ya Binadamu.
Hapa The bestgalaxy tunaenda kuangalia jinsi ya kutuma pesa Kenya na Tanzania kwakuhusisha Safaricom Kenya na Vodacom Tanzania. Kama upo nchi ya Tanzania, unaweza tumia mtandao wa Vodacom kumtumia pesa mtu kwa Mpesa akiwa kenya anatumia mtandao wa Safaricom. Pia ukiwa kenya unatumia Safaricom unaweza mtumia pesa mtu kwa Mpesa akiwa anatumia mtandao wa Vodacom Tanzania.
Jinsi ya kutengeneza Logo ya biashara au Binafsi BONYEZA HAPA>>>
Kutuma pesa Kenya na Tanzania (Vodacom/Safaricom)
Unataka kujua jinsi ya kutuma? Usijali, hapa chini kuna maelezo juu ya hatua unazoweza kufuata pale unapotaka kutuma pesa ukiwa Tanzania na kenya kwakutumia mtandao wa Vodacom au Safaricom.
Kutuma pesa toka Tanzania kwenda Safaricom Kenya kwa kutumia Mpesa(Vodacom)
- Fungua App ya Mpesa na uguse sehemu ilioandikwa “Services” alafu utaletewa orodha ya huduma.
- Chagua huduma ilioandikwa “International Transfers” kwenye orodha hiyo.
- Baada ya kufanya hiyo utapelekwa kwenye ukurasa utakao takiwa kuchagua nchi unayotaka pesa iende. Utachagua Kenya kwakua ndiko unataka kutuma pesa.
- Baada ya kuchagua nchi utaletewa ukurasa wa kuchagua mtandao. Wewe utachagua mtandao wa Safaricom kwakua mtu unaemtumia anatumia Safaricom.
- Baada ya kuchagua, utapelekwa kwenye ukurasa utakao takiwa kujaza namba ya simu ya mtu unaemtumia pesa kwa mfumo wa kimataifa (254xxxx) kisha andika kiasi unachotaka kutuma. Na ukishajaza utabonyeza kitufe kilichoandikwa “Endelea” ili kuendelea na hatua nyingine za uthibisho wa kutuma pesa yako.
Sending money from Kenya to Tanzania with Mpesa (Safaricom)
- Dial *334# to open Mpesa Global.
- Select “Send Money Abroad”.
- Select “Send to Mobile Number”
- Select “Tanzania” as a county you want to send money.
- Enter Recipient Mobile Number in International Format (255xxxxxx)
- Enter Amount of Money you want to send.
- Select source of fund and purpose of Funds then confirm.
Mwisho ningependa kukukumbusha kuwa makini katika kutuma pesa yako ili kuepuka kutuma pesa kimakosa. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy na usiache kufuatilia The bestgalaxy.
App zinazo kupa pesa kwa kufanya kitu kidogo kwako (Unazitumia Kila siku)
Hapa chini The bestgalaxy nimekuandalia orodha ya app chache ambazo zinaweza kupa zawadi ya pesa kwa kufanya jambo flani dogo linaloweza kuwa jepesi kwako. Lakini kabla ya yote ufahamu kuwa pesa hizi ni ndogo sana na haziwezi kukufanya upate utajiri. Pia fahamu kuwa hizi app ni app ambazo hutoa pesa kama zawadi lakini sio app rasim kwenye upande huo. Hizi ni app rasmi katika upande wa kurahisisha upatikanaji wa huduma au mahitaji kirahisi. Yawezekana unazitumia kila siku. Kuna wakati tutazungumzia kuhusu platform rasimi kwa kutengeneza pesa nyingi.
Tunaweka app kwenye simu zetu kwasababu mbalimbali na moja kati ya sababu ya kuweka baadhi ya app ni kupata huduma au amahitaji kirahisi kwa kutumia simu. Mfano, kuna app ambazo tunaweka kwenye simu ili tuweze kupata huduma za kifedha kihisi kwenye simu zetu na pia kuna app hurahisisha manunuzi ya vitu kwa kutusogezea bidhaa tunazoweza nunua kwenye simu zetu.

App zinazo kupa pesa kwa kufanya kitu kidogo kwako (Android)
Farasi
Farasi ni moja ya app ambazo zinajihusisha na maswala ya usafili. Kwakutumia app hii unaweza pata usafiri wa kukutoa ulipo mpaka mahali unapotaka kwenda kirahisi. App hii inakutumika na watu wengi tu katika maswala ya usafiri. App hii hua inatoa zawadi kwa watumiaji wake pale wanapoitumia kupata usafiri. Kwasasa unapoanza kuitumia unapata Tsh 3000 mbali na zawadi nyingine utazopata unapotumia. Angalia app kwa KUBONEZA HAPA alafu kama utakua unajiunga usisahau kujaza namba 715233405 kwenye kibox cha referral code.
Branch app
App ya Branch ni app ya mikopo. Ni moja kati ya app nzuri sana katika upande wa app zinazokuwezesha kupata mikopo kwenye simu Tanzania. App hii inaweza kukupa zawadi ya pesa pele unaporudisha pesa kwa mara ya kwanza baada ya kuazima ila kupata zawadi hii ni lazimu uwe umealikwa. BONYEZA HAPA kupata maelezo zaidi ya app hii na zawadi zake
Tigo pesa app
App ya Tigo pesa ni app ambayo hurahisisha zaidi maswala ya kufanya miamala kwa watumiaji wa Tigo. App hii huwa anatoa kiasi kido cha pesa kama zawadi pale unapomualika rafiki yako. Kama unarafiki ambae anatumia mtandapo wa Tigo lakini ana app, unaweza mualika huyo rafiki alafu akapatiwa zawadi ya pesa kwenye akaunti yako ya Tigo pesa. Kama hauna app ya Tigo pesa, INGIA HAPA kuipakua.
Mwisho ningependa kukukumbusa tu kuwa app hizi sio app rasimi kwa kutengeneza pesa, zinatoa pesa kama zawadi TU.