Tag Archives: nguvu za kiume

Kwanini mwanaume anashindwa kusimamisha? Sababu hizi hapa

Kuna sababu nyingi zinazoweza pelekea kutokea kwa tatizo la mwanaume kushindwa kusimamisha yaani, kushindwa kuwa na uwezo wa kuamsha uume wake na kuwa imara na mgumu wakati wa tendo la ndoa . Kuna wanaume hukumbana na tatizo hili kwa muda mfupi au kuwa tatizo la kudumu. Hali hii anaweza kumbana nayo mwanaume wa umri wowote(Mzee au Kijana).

Fanya haya ili uchelewe kupiga bao BONYEZA HAPA>>>

Sababu za mwanaume kushindwa kusimamisha

Sababu zinazoweza sababisha mwanaume kushindwa kusimamisha zinaweza kuwa za kisaikolojia, afya ya mwili, mtindo wa maisha, magonjwa ya zinaa au umri. Hebu tuangaliae zaidi mambo au sababu hizi:

Saikolojia.

Mwanaume akiwa na mfadhaiko, wasiwasi, msongo wa mawazo, au hofu ya kutofanya vizuri wakati wa tendo, anaweza jikuta kashindwa kusimamisha. Yani kama mwanaume hajiamini au mawazo yapo mbali na tendo anaweza kumbana na tatizo hili.

Afya ya mwili.

Tatizo la kushindwa kusimamisha kwa wanaume wengine linaweza kusababishwa na masuala ya afya ya mwili. Mwanaume akiwa na mwili wenye ugonjwa wa kisukari, shinikizo la damu, matatizo ya moyo, unene uliopitiliza, au ugonjwa wa tezi dume, anaweza kumbana na tatatizo la kushindwa kusimamisha.

Mtindo wa maisha.

Mwanaume pia anaweza shindwa simamisha baada ya uwezo wake wa kusimamisha kuathiliwa na matumizi ya tumbaku, unywaji wa pombe kupindukia, na matumizi ya dawa za kulevya. Pia, kutofanya mazoezi ya kutosha na kula chakula au lishe duni kunaweza kusababisha mwanaume kupata matatizo ya nguvu za kiume.

Mazoezi ya mwili yatakayo kusaidia katika mapenzi BONYEZA HAPA>>>

Magonjwa ya zinaa.

Mwanaume kuwa na baadhi ya magonjwa ya zinaa kama vile kisonono na magonjwa mengine kunaweza muathiri uwezo wake na kupelekea matatizo ya nguvu za kiume.

Umri wake.

Kwa wanaume wengi, umri huathiri uwezo wa uwezo wa kusimamisha. Mwanaume mwenye umri mkubwa anaweza jikuta amepunguza uwezo wa kusimamisha kutokana na umri wake ingawa hali hii huwakuta pia wenye umri mdogo.

Ikiwa mwanaume anasumbuliwa na tatizo hili kwa muda mrefu au mara kwa mara ni vyema kumwona daktari au mtaalamu wa afya ili kupata ushauri na matibabu sahihi yanayoweza saidia kuweka hali sawa.

Asante kwa muda wako, endelea kufuatilia The bestgalaxy, endelea kuwa karibu na The bestgalaxy.