Matatizo ya kifamilia, mahusiano, kazi au matatizo ya kiafya yanaweza kuwa sababu ya watu kuingia kwenye msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo ni jambo linalowatokea watu wengi katika maisha na hutofautina viwango. Watu wenye msongo wa mawazo mara nyingi wanahisi uzito wa mawazo yasiyowezekana, wasiwasi, au hali ya kukosa amani ya akiil zao. Na hali hii ikizidi huwa inaleta athari kubwa tu. Ni vema kuchukua hatua ya kapambana na msongo wa mawazo pele unapoona unataka kukuzidi.
Kushugulisha mwili, Kufanya mazoezi ya mwili, Kubadilishana mawazo na watu au marafiki waliokuzunguka, Kufanya vitu vinavyokupa furaha na kuonana na wataalam/madaktari ni baadhi ya mambo au njia nzuri unazoweza kutumia kupambana na msongo wa mawazo.
Ukiachana na mambo hayo, hapa chini The Bestgalaxy tunakufungua juu ya jinsi simu yako inaweza kukusaidia kidogo katika kupambana na msongo wa mawazo. Tunaenda kuanagalia vitu vichache unavyoweza kuvifanya kwa wakati falani kwenye simu yako ili kupunguza au kupambana na msongo wa mawazo. Lakini kabla ya yote ningependa ufahamu kuwa baadhi ya vitu hivi sio vizuri sana na nitakwambia ni kwanini.
Jinsi ya kupunguza msongo wa mawazo kwa kutumia simu
Tafuta ufumbuzi wa tatizo lililopelekea msongo wa mawazo
Simu janja au smartmphone huwa zinakupa uwezo mkubwa kiganjani pako. Unaweza tumia simu hizi kujifunza jinsi ya kutatua mambo mbali mbali kwa kusoma au kuangalia video za mafunzo. Unaweza tumia mtandao kama Youtube au Google kuuliza na kujifunza jinsi ya kutatua tatizo linalopelekea wewe kuwa na msongo wa mawazo. Ufumbuzi au usaidizi utakao upata utakufanya upunguze msongo wa mawazo.
Ungana au zungumza na watu watakao kupa furaha
Simu huwa zinampa mtu uwezo wa kufanya mazungumzo na watu walio mbali nae. Mtu anaweza fanya mazungumzo na familia, marafiki na hata kuungana na watu asio wajua. Kufanya mazungumzo na watu wanaokupa furaha au kukushauri, husaidia kupunguza msongo wa mawazo.
Cheza magemu
Kwenye simu,unaweza cheza magemu ya aina nyingi. Kucheza magemu sio njia nzuri sana ya kupunguza msongo wa mawazo ila inategemeana na hali iliokukuta. Kabla ya kutumia njia hii ni vema ukatambua kuwa njia hii huwa inatumika kukimbia uhalisia au kukusahaulisha uhalisia tu ila haitibu tatizo lilikuletea msongo wa mawazo. Unaweza cheza gemu na ukasahau kabisa uhalisia au hali ulionayo. Lakini baada ya kucheza unaweza kuwa unahisi furaha na nguvu ya kukabiliana tena na jambo linalokupa msongo wa mawazo au unaweza maliza kucheza gemu ukukuta tatizo liko palele na msongo wa mawazo ukakujia tena. Ni vema pia kuepuka kutumia muda mwingi kwenye kucheza gemu bila kutatua tatizo au kufanya mambomengine ya msingi maana hilo ni tatizo jingine pia.
Kuangalia na kusikiriza vitu vitakavyokupa furaha
Kupitia simu yako, unaweza kuangalia video zinakupa furaha au kusikiliza audio zinazokupa furaha. Kama unapenda vichekesho, filamu na video za burudani nyingine basi unaweza kuangalia video zote kwenye simu yako. Mbali na video unaweza pia kusikiliza nyimbo unazojipenda au simulizi. Lakini ni vema kufahamu kuwa kutumia muda mwigi kuangalia video huwa si uamuzi mzuri wa kupuguza msongo wa mawazo.
