Kama ni shabiki mzuri wa mpira wa miguu unaweza kua ni mmoja wa watu wanopenda kufuatilia matokeo ya mechi mbalimbali katika ulimwengu wa kabumbu. Teknolojia imeisharahisisha mambo mengi sana katika soka. Kupitia simu yako ya mkononi unaweza kuangalia mechi live na ukafurahia, kiganjani pako!.. Mbali na nakushuhudia mechi live kiganjani pako, unaweza pia kuangalia matokeo ya mechi zilizochezwa au zinazoendelea kuchezwa hapo hapo kiganjani pako. Hii inasadia sana maana unaweza kua hauna muda wa kutulia na kuangalia mechi lakini lakini ukawa unajua mechi katika upende wa scoles ziko vipi.
Kuna njia zaidi ya moja zinaweza kutumika kuangalia matokeo ya mpira kwenye simu na watu huzitumia kila siku yaani kuangalia matokeo ya mechi za leo, jana na siku zaidi hiyo. Hapa The bestgalaxy tunaweka wazi njia 3 unazoweza kuzitumia kuangalia matokeo ya mpira kwenye simu yako ya mkononi.
Njia 3 za kuangalia matokeo ya mechi za mpira kwenye simu
1. App na site/tuvuti maalum kwaajili ya kuangalia matokeo
Unapotaka kujua matokeo ya mechi mbalimbali kwenye simu yako, tambua kuna app za simu ambazo ni maalum kaajili ya matokeo ya mechi za mpira wa miguu na michezo mingine. Unaweza ingiza moja ya app za muundo huu kwenye simu yako na ukawa unatumia kuangalia matokeo ya mechi unazozihitaji kwenye simu. Uzuri wa app hizi ni kwamba nyingi huwa zinakua zinatoa huduma ya kukupatia matokeo bure kabisa japo kila utakapotaka kuzitumia utatakiwa kutumia internet. Mfano wa app hizi ni app iitwayo “LiveScore” na pia hii nyingine inaitwa “GOAL Live Scores”. Mbali na app izo kuna App ningine nyingi sana unaweza tumia kuangalia Scores. kwenyewe app hizi unaweza pia kufurahia vipengele vingine kama vile habari za michezo na ratiba za michezo.
Ukiachana na uwepo wa app, pia kuna websites/tuvuti unaweza tumia kuangalia matokeo ya mechi. App nyingi zinazojihusisha a matokeo ya mechi huwa ni za websites. mfano mzuri ni hii appp ya LiveScore; kuna website inatwa “LifeScore” na hiyo website ndio inaapp iitwayo “LiveScore”. kwahiyo hapo unakua uamuzi wako kuangalia matokeo mechi zako kupitia website au app.

2. Angalia matokeo ya mpira kupitia Google search
watu wengi hutumia google search kupata taharifa mbalimbali kwa haraka. Kunavitu ukivitafuta google unawezeza kuvipata kwa shida lakini sio matokeo ya mechi(hasa kama mechi inatambulika). Google inaweza kukupa matokeo moja kwa moja ya mechi ilioisha unayoihitaji bila mizungusho mingi. Na kitu kizuri ni kwamba kupitia Google unaweza pata taalifa nyingine kuhusu mechi kirahisi sana na bila kupoteza muda wala kutumia bando sana kama baadhi ya njia nyingine. Unaweza tumia njia hii kuangalia matokeo ya mechi za simba na yanga bila utata.
3. Angalia scores kwenye app au tuvuti za kubeti
Ukiachana na njia hizo mbili ambazo unaweza tumia kuangalia scores, njia ya tatu ni kucheki scores kupitia app au tuvuti za kubeti. Kama wewe ni mtu unaebeti kupitia simu, hainaaja ya kujitesa kuangalia matokeo ya mechi zinanoendelea kuchezwa. Unaweza kuangalia kirahisi kupitia kipengele cha “LIVE” katika website au app ambayo unaitumia kubeti. Kipengele hiki huwa kinakupa taalifa za mechi zinazochezwa muda huo na Moja ya taalifa utakazo zipata ni pamoja na magoli. Kipengele hiki ni kwaajili ya kubeti lakini unaweza kukitumia kuangalia scores za mechi unazozijitaji.


