Tag Archives: mengineyo

Epuka kukopa pesa kama unatabia hizi ndani yako

Kuna uwezekanao wa kuwa na mambo mengi sana yanayoweza kusukuma mtu kukopa pesa za watu wengine au taasisi mbali mbali za kifedha. Na kukupa ni jambo zuri sana maana kuna muda mtu unaweza kukwama kifedha kwa kukumbana na jambo linalohitaji pesa ambayo hauna lakini ukalimudu kupitia mkopo.

Kuna watu hukopa pesa ili kurekebisha mambo yao yalioenda vibaya na kuna hata ambao hukopa ili kulifanikisha jambo lisilo na ulamazima sana. Kukopa kwasababu yoyote ile ni uamuzi mzuri lakini itakua uamuzi mzuri zaidi kama umefanikiwa kwenye jambo lako na kuulipa mkopo wako. Kama haujakamilisha jambo lako au umefanikisha lakini haujafanikiwa kulipa deni la mkopo wako, uamuzi wa kukopa unaweza kuwa mbaya kwako. Na endapo hali yakushindwa kulipa itakua inakuandama kila mara unapokopa ni vema ukaanza kujiweka mbali kidogo na mikopo.

Hapa The bestgalaxy tunakupa tabia ambazo mara nyingi zikiwa ndani yako basi mikopo huwa karibu sana na pia huwa ni ngumu kuilipa. Sio kila mtu mwenye madeni au anaeangukia kwenye madeni anatabia hizi. Ni baadhi ya watu tu ndio huwa na tabia tunazoenda kuzielezea hapa. Niwesema hivyo maana wengine husukumwana na vitu vilivyo nje kabisa na uwezo wao  au sababu myingine mabali na tabisa hizi.

Mambo unayotakiwa kujua kuhusu simu za mkopo BONYEZA HAPA>>>

Epuka kukopa pesa kama unatabia hizi ndani yako

Kushindwa kuzirudisha pesa zako mwenyewe

Kama ni mtu mwenye malengo na huwa unajiwekea pesa kwaajili ya mambo mbalimbali basi kuna muda unaweza kuwa unajikopa mwenyewe. Yani unachukia pesa ulizojiwekea kwaajili ya jambo flani na kuzitumia kwenye jambo lingine tu huku ukiwaza kichwani “Nitazirudisha”. Ikiwa unatabia hiii na unakua na msimamo wa kuzirudisha tena hizo pesa basi unaweza usiteseke sana kulipa hata ukikopa kwa watu wengine. Lakini kama huwa haurudishi pesa hizo na ni tabia yako, kunaweza kuwa na ugumu pia unapokopa kwa wengine. Ni vema ukajaribu kujiimarisha ndani yako kabla ya kukopa kwa wengine. Hakikisha unapambana sana kurudishia pesa sehemu zako za dani ukichukua pesa.

Jinsi ya kupata Mkopo kwenye simu BONYEZA HAPA>>>

Kuhairisha mipango yako ulioianza

Kuna baadhi ya watu huwa na mipango ya biashara na Mambo mengine yanayoweza kuhitaji pesa ili kuingiza pesa. Kukopa kunaweza kuwa ni wazo la haraka kwa mtu mwenye mipango ya namna hii lakini hana mtaji au pesa inayohitajika.
Kukopa sio kitu kibaya kama umekusudia kuanza kupambana kutimiza mpango uliojiwekea. Lakini kama ni mtu unaempenda kuhairisha mipango ulioianza, kukopa kunaweza kuumiza.
Ukichukua Mkopo kwaajili ya mpango flani lakini ukahairisha na kwenda tofauti na mpango huo, kunakua na hatari kubwa ya kupoteza pesa hiyo. Pesa ikiisha bila kufanya kitu kilichosababisha ukope, unaweza jilaumu kuliko ungefanya na kushindwa.
Kama haujaweka vizuri mipango yako au haupo tayari kuipambania kwa asilimia 100, basi usikope pesa kwanza.

Kusahau shinda unapokamata pesa yoyote

Hali yako huwa inakua vipi muda ambao hauna pesa? Na hua inakua vipi ukipata pesa? Kama ukipata pesa yoyote mkononi mwako shida huwa unazisahau, unafanya matumizi na kuacha kabisa kutafuta pesa basi kukopa kunaweza kuwa kubaya kwako. Ukikopa pesa na kuishika mkononi pesa hiyo inabidi iwe kichwani kwako kuwa sio pesa yako na unahitajika kulipa. Hii inaweza kukusaidia kupata mpango wa kuilipa na kuwa makini unapozitumia pesa hizo za mkopo.
Ikiwa utaruhusu pesa hiyo ikusahaulishe shida na kuichukulia ni yako, basi unaweza kuwa ndio mwanzo wa kupuuza deni lako, kuridhika na kuanza ikiutumia pesa.
Usiache kuiona pesa ya Mkopo kuwa ni Mkopo hata ikiwa na mamilioni ya pesa.

Haupendi kudaiwa.

Kutopenda kudaiwa ni jambo zuri sana ila linakua zuri kama utakua na uwezo wa kujikumbusha mwenyewe kulipa pesa kabla haujadaiwa. Mbali na hapo ukiwa haupendi kudaiwa itabidi uanze kuepuka kukopa pesa maana kudaiwa ni lazima na ukichukia au kumfanyia vibaya anaekudai itakua ni kosa kwako tu kivyovyote maana umeshindwa kutimiza makubaliano. Wengine hufikia mpaka hatua ya kupambana kukata kulipa Kwasababu ya kudaiwa vibaya lakini hawajihukumu kwa kuchelewesha pesa muda mrefu kinyume na makubaliano.

Natumaini umesoma na kuelewa makala hii na inaweza kuwa msaada katika Maisha yako kwenye upande wa kukopa. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mambo mengine zaidi.

Mambo 5 ya kujua kuhusu Tattoo

Pamoja na kwamba watu wengi wanaonekana wanachora tottoo kipindi hiki, lakini mabaki ya binadamu walioishi miaka iliopita yanaonesha kwamba tattoo hazijaanza kuchorwa miaka hii. Totoo zilianza kuchorwa toka zamani na mpaka sasa binadamu wameendelea kuzichora.


Kwasasa tottoo huchorwa kwa kifaa maalumu kinacho tumia sindano kuingiza wino katika ngozi. Hii inaweza kuwa ni tofauti na zamani kutokana na utofauti wa kiteknolojia.
Watu ambao huusika na kuchora tatoo kwa kiingereza huitwa “tattoo artists, tattooer au tattooist”. Kuchora tattoo ni sanaa kama sanaa nyingine lakini kuchora tattoo kumekua na mitazamo mingi sana kwenye jamii.
Hapa The he bestgalaxy, tunakupa mambo machache kuhusu Tattoo au uchoraji wa tattoo. Tende pamoja kuangalia mambo haya pengine lakini utapenda kuyajua.

Mambo 5 ya kujua kuhusu Tattoo

Wino mweusi

Katika kuchora tattoo, wino wa rangi nyeusi ni wino ambao ukichorea tattoo kwenye mwili, unakua ni rahisi ukuuondoa unapoifuta. Tattoo zinaweza kufutika kwa kutumia kifaa kinachotumia mionzi kinachoitwa Laser. Lakini kufuta Tattoo huambatana na maumivu. Wino mweusi unaweza kufutika kirahisi zaidi kama itakua ni ya wino mweusi.

Sindano huchoma ngozi mara 50 hadi 3000 kwa dakika

Mashine ya kuchorea tattoo Ina sindano ambayo hutumia kuingiza wino katika ngozi. Sindano hii unapoiweka katika ngozi ili kuingiza wino, huichoma ngozi kwa haraka mara 50 hadi 3000 kwa dakika moja. Jambo hili ndio huleta maumivu flani mtu anapochora tattoo. Lakini sindano hii huishia kwenye ngozi tu, haitakiwi kuchoma zaidi mpaka ndani kabisa ya mwili.

Asilimia 23 ya watu hujutia kuchora tattoo na hujutia zaidi majina.

Katika tafiti inaonekana kuwa baadhi ya watu hujutia maamuzi yao ya kuchora tattoo. Asilimia 23 ya watu waliochora tattoo imeonekana kujutia maamuzi yao ya kuchora tattoo hasa tattoo za majina. Na hii, kama utakua ni mfuatiliaji wa watu maalufu mtandaoni, unaweza kuwa tayari umeisha kutana taharifa za wasanii au watu maharufu wakijutia maamuzi ya kuchora tattoo kama hizo.

Tattoo ya thamani kubwa kuwahi kuchorwa.

Katika historia ya kuchora tattoo, tattoo ya thamani kuwahi kuchorwa ni yenye thamani ya Dola 924,000 za kimarekani. Hii ilikua ni tattoo ya muda mfupi iliochorwa kwa kujumuisha vipande vya almasi. Lakini tattoo hii iliochorwa kwa lengo la kuwa kama tangazo. Kampuni ya Shimansky ndio ilihusika na jambo hilo na aliechorwa tattoo hii alikua ni mwanamke model aitwae Minki van der Westhuizen.

Kuchangia damu.

Kuchora Tattoo hakukuzuii kuchangia damu kama utakua umekidhi vigezo vya kuchangia damu. Kumekua na baadhi ya watu wamekua wakijua kuwa ukichora tattoo hautaweza changia damu maishani mwako. Jambo hilo sio kweli, unaweza kuchangia damu bila shida kama utakua umekidhi vigezo vya kiafya vinavyohitajika kuchangia damu. Ila ukichora tattoo unatakiwa kukaa kwa miezi 3 au 6 ndipo ufanyiwe vipimo, uchangie damu.

Kuchora Tattoo sio jambo lisilo hitaji utaalamu. Kama umefikia uamuzi wa kuchora tattoo, unashauriwa kuwatumia wataalamu wa jambo hilo na sio kuchora hovyo tu. Hii ni Kwasababu kunavitu muhimu visipo zingatiwa unaweza jiwekea kwenye hatari zaidi kiafya kuliko tattoo yenyewe. Usalama usipo zingatiwa kwenye sindano, unaweza ambukizwa magonjwa. Pia Kuna wino wa tattoo huwa unapigwa marufuku kwasababu za kiafya lakini mtu asie mtaalamu wa mambo ya tattoo anaweza tumia wino huo kisa sio gharama kwake. Ukiachana na uliopigwa marufuku, wino mwekundu wa tattoo sio mzuri sana maana unaweza sababisha upere japo sio kwa wote. Nafikili umefurahia kujua mambo haya, usiache kufuatilia The bestgalaxy.

Mambo matano yanayoweza kusaidia kufanikiwa maishani

Kufikia mafanikio katika maisha yako kunaweza kuwa lengo linalohitaji juhudi na muda. Hapa kuna mambo matano unayoweza kufanya ili kuboresha nafasi zako za kufanikiwa:

  1. Jiwekee Malengo Maalum. kama unataka kufanikiwa nivema ukaanza kujiwekea malengo. Fahamu unataka kufanya nini na nini maaana ya mafanikio kwako. Jiulize lengo lako ni lipi, Unataka kufikia wapi na kwanini.
  2. Kuwa tayari kujifunza vitu au ujuzi mpya. Usijifunge kwenye kujifunza unapotaka kufanikiwa maana unapokua katika safari ya mafanikio unaweza kutana na vitu vingi sana na karibu vyote huwa vimelenga kukufundisha na kukukomaza kufikia pale unapopahitaji. Pia wewe mwenyewe unatakiwa kuwa ni mtu ambae unatafuta kujifunza vitu usivyovijua. Fanya utafiti na jifunze kutoka kwa wataalamu katika eneo unalotaka kufanikiwa. Jiunge na kozi, semina, au programu za kujifunza ili kuboresha ujuzi wako na kujiendeleza.
  3. Usiache Kujituma au kujisukuma kwa Bidii. Kuwa tayari kufanya kazi kwa bidii na kujitolea kufikia malengo yako. Kufanikiwa mara nyingi kunahitaji juhudi za ziada na uvumilivu. Kisukume kuendelea kufanya kazi kwa bidii hata wakati wa changamoto.
  4. Jenga mahusiano na watu waliofanikiwa au wanaoweza kukusaidia. Jiweke karibu na watu wenye uzoefu na wanaoweza kukusaidia kufikia malengo yako. Watu hawa wanaweza kutoa fursa za kujifunza, kushirikiana, na kujenga uhusiano ambao utarahisisha wewe kufikia malengo yako.
  5. Usiogope kuwa mbunifu au tofauti. Usiogope kufikiria nje ya box na kutafuta njia za ubunifu za kutatua matatizo ili kufikia malengo yako. Usiogope kuwa tofauti katika mambo yako maana sio kila kilicho tofauti hakipo sahihi.

Kumbuka kwamba mafanikio yanaweza kutofautiana kwa kila mtu na yanaweza kuwa na maana tofauti. Ni muhimu kuwa na uvumilivu na kujifunza kutokana na changamoto zinazojitokeza kwenye safari yako ya kufikia mafanikio.

Je, wajua haya kuhusu Kondomu na Ukimwi? soma hapa

Kondomu ni kifuko kinachotumiwa na wanaume tangu zamani kuzuia mimba na maambukizi ya maradhi ya zina. Siku hizi kuna kondomu ya kike pia.

Kondomu zinatengenezwa kwa ngozi ya mnyama, siku hizi hutengeneza kwa kutumia mpira.

Utengenezaji hufanyika katika mazingira ya baridi ili kuhifadhi uimara wa mpira.

Zinaunganishwa ngozi nyembamba mbili ili matundu ya ngozi ya kwanza yazibwe na ile ya pili na matundu ya ngozi ya pili yazibwe na ile ya kwanza.

Kisha kupimwa, kondomu huwekewa dawa ya kuzuia isiharibike: dawa hiyo ina madhara kwa afya.

Pamoja na kutumika kwa ajili ya kuzuia mimba kwa mafanikio makubwa (ingawa si 100%), mpira huo unatangazwa sana kama kinga imara dhidi ya virusi vya UKIMWI.

Lakini katika utafiti uliofanywa na shirika la Sexuality Information and Education Council la Marekani kwa majozi 122 ambapo mmojawao alikuwa mwathirika, wenzao 12 waliambukizwa (10%) ingawa walifanya ngono kwa kutumia kondomu kila mara na kwa usahihi.

Shirika la Human Life International lilifanya utafiti kwa aina mbalimbali za ngono. Kati ya waliotumia vizuri kondomu, mwaka wa kwanza waliambukizwa: 11% za waliofanya ngono ya kawaida, 30% za waliofanya ulawiti. Mwaka wa pili wakafikia 21% na 51%. Mwaka wa tatu wakawa 30% na 66%.

Kwa maneno mengine ni kwamba kondomu haizuii moja kwa moja, bali inaahirisha maambukizi: kama si leo, inaweza tokea kisababu kesho ukapata japo ni kwa uwezekano mdogo sana, hasa kama ukiwa muangalifu katika taratibu za utumiaji. Pamoja na yote hayo, huwezi kulinganisha hata kidogo kutumia kondomu na kutotumia kabisa. Bado kondomu ni kitu kinachozuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa asilimia kubwa sana ukilinganisha na kutoitumia. Ndio maana watu hushauriwa kutumia kondomu ili kuzuia maambukizi wanaposhirikiana kimwili bila kujua hali zao. Na endapo mtu akipata virusi vya ukimwi ni vema akajikubali, akeelewa kuwa sio mwisho wa maisha na pia kuwatu wengi katika Dunia au mazingira yake wanahali kama yake waishi kama kawaida.

Mazoezi ya kupunguza tumbo au kitambi (rahisi unafanya hata nyumbani)

Tumbo au kitambi imekua ni tatizo ambalo baadhi ya wanaume na wanawake hukumbananalo katika miili yao. Tukitungunzia kitambi katika mwili wa mwanadamu ni mafuta ambayo hujikusanya katika maeneo ya tumbo na kulifanya tumbo kuonekana limeongezeka ukubwa. Mara nyingi kitambi huibuka katika mwili wa mtu kutokana na mlo wa mtu mwenyewe au staili ya maisha yake kiujumla. Mazoezi ni njia salama na ya bure ya kuepukana au kuondokana na kitambi.

Kunawatu huwa wanashindwa kutumia njia hii na kufanikiwa kupunguza kitambi kutokana na kutarajia matokeo ndani ya siku moja au mbili. Ukiwa na mawazo hiyo kichwani hautaweza kufanikiwa kupunguza kitambi kwa njia ya mzaoezi maana matokeo huwa yanachukua muda. Yanaweza kuaanza kuonekana zaidi baada ya siku 30(mwezi).

Ukitaka kufanikiwa kirahisi, kichwa chako kiwe kinaelewa kwamba mazoezi unayoanza kufanya hayapunguzi tumbo tu, yanakufanya uweunacheza mchezo wa kitandani vizuri na kwakuchangamka, utachangamka pia katika shughuli zako nyingine tena utaepukana baadhi ya magonjwa. Ukifanya mazoezi vizuri kwa siku 7 tu unaweza anza kuona faida hizo nyingine hatakama tumbo halijapungua. Ni vema ukafanya mazoezi kuwa ni tabia yako tu ili faida zake uwe unazifurahia kila siku katika maisha yako.

Hapa chini tunashusha mazoezi matatu tu ambayo unaweza kuanza kuyafanya kila siku ili kupunguza kitambi au tumbo. Mazoezi haya ni kwaajili ya wanawake na wanaume pia. Yanaweza fanyawa hata nyumbani tu na kama hauna muda maalum wa mazoezi unaweza tafutiza dakika chache kila siku kabla haujaingia kuoga, ukayafanya. kwasiku za mwanzo unaweza pata maumivu kutokana na mwili kutozoea mazoezi lakini usikate tamaa, endelea kufanya tu maana maumivu huisha na hukuacha ukiwa imara zaidi.

Mazoezi matatu ya kupunguza Tumbo au kitambi (Mwanawake na Mwanaume)

Zoezi la kwanza

Tafuta sehemu nzuri na safi ambayo itakuruhusu kulala chali bila tatizo. Nenda katika sehemu hiyo kisha ulale chali. Nikisema “kulala chali” namaanisha kulala kwa kuangalia juu. Baada ya kulala chali hapo chini, kishike kichwa chako kwa mikono yako yote miwili alafu ukiwa hivyo hivyo, anza kujinyanyua kiwiliwili na kichwa juu alafu unarudi chini. Endelea kwenda juu na chini, juu chini bila kuibandua miguu yakochini. Angalia mfano katika picha hii;

Image:Giphy

Zoezi la pili

Katika zoezi hili, hatua ya kwanza ni kuchuchumaa chini. Baada ya kuchuchumaa nyoosha mikono yako mbele alafu shika chini katika sakafu. Baada kufanya hivyo, anza kuitegua na kuivuta miguu yako yote miwili kwa nyuma bila kiwili wili kugusa chini alafu irudishe tena miguu kama ilivyokua. Endelea kuifanya hivyo miguu kama inavyoonekana katika picha hii.

Image:Giphy

Zoezi la tatu

Kwenye zoezi hili utatakiwa kuanza kwa kulala chali kama katika zoezi la kwanza. Lakini baada ya kulala chali utatakiwa kuwa unanyanyua miguu yako yote miwili, wa kushoto na wakulia na kulileta juu kwa pamoja alafu unairudisha Tena chini. Endelea kufanya hivyo kwa kurudia kwenda juu na chini. Unaweza angalia picha ili kuelewa zaidi.

Image:Giphy

Mbinu 6 zitakazo kusaidia katika mapishi yako

Moja ya jambo muhimu sana kwa mtu anaependa kupika vyakula vizuri ni ubunifu. Kwaiyo kama unaependa kuwa mtu unaepika chakula kizuri basi zingatia zaidi katika ubunifu wa mapishi na kujua jinsi ya kukianda chakula katika mitindo mbalimbali. Na mara nyingi hii katika kukipika chakula ndio huwatofautisha wapishi na kuamua nyupi ni bora zaidi na kama ni mama wa nyumbani basi tambua kuwa mapashi ya kibunifu na mitindo mbalimbali yanaweza ifanya familia ikifurahie chakula na kujenga afya pia. Tukiachana na maswala ya hayo, hapa tumekuandalia mbinu au mambo unayoweza kuyafanya ili kurekebisha mapishi yako yanapokua vibaya au kurahisisha upishi wako.

Mbinu 6 zitakazo kusaidia katika mapishi

1. Mchuzi ukizidi Maji na kuwa mwepesi, kwangua kiazi mviringo kwenye kikunio cha nyanya weka katika mchuzi wako ili kuufanya uwemzito.

2. Chumvi ikizidi kwenye chakula weka kiazi mviringo kilichomenywa katika chakula ili kupunguza chumvi.

3. Laza maharage yanayochelewa kuiva kwenye chupa ya chai yenye maji ya moto kisha asubuhi chemsha kwa dakika 30 tu yatakuwa tayari yameiva (yataiva haraka)

4. Ukimaliza kuosha vyombo kwa kutumia Still Ware,itunze still ware kwa kuiweka kwenye Maji ili isiharibike na ifae kwa matumizi ya kesho.

5. Ukiunguza wali kata kitunguu maji nusu kisha weka kwenye wali na ufunike kwa dakika tano. Kitunguu maji kinasaidia kutoa harufu ya moshi

6. Mchuzi wa maini ukitaka uwe rost nzito au mchuzi wowote na hauna nyanya za kutosha… Weka kijiko kimoja cha chakula cha unga wa ngano ukoroge na maji kidogo alafu weka kwenye mchuzi kisha acha uchemke dakika 5

Katika Matumizi yako ya simu usifanye vitu hivi (Unaweza juta!) GUSA HAPA>>>