Tag Archives: mapenzi

Sababu 5 za kukataliwa na Wanawake

Kukataliwa na wanawake ni jambo linaloweza kumkuta mwanaume yeyote, na mara nyingi linaweza leta huzuni na kuchanganyikiwa kabisa. Katika mambo mwanaume huogopa katika Maisha yake, kukataliwa na mwanamke ni moja wapo. Mwanaume anaweza mzawadia zawadi ya thamani mwanamke bila kumwambia anampenda kwasababu ya woga wa kukataliwa tu.


Kipindi cha nyuma baadhi ya wanaume wasio amini kuwa kuna maisha ya furaha baada ya kukataliwa na mwanamke, walikua wanajitupa hata kwenye maamuzi mabaya baada ya kukataliwa. Lakini kwa sasa watu wengi wameelimika na wanaamini kuna maisha yanaendelea baada ya kukataliwa na mwanamke.


Sababu za mwanaume kukataliwa ni nyingi na huwa tofauti. Na sio kila mwanamke husema Sababu ya kumkataa mtu, wengine huficha.
Katika Sababu hizo tofauti, kuna mambo au sababu huwa zinajirudia na wanaume wengi hukataliwa kwasababu hizo. Kama ni mtu ambae upo katika kipindi cha kutafuta mwenza wako, itakua vizuri kuzihafamu sababu hizi.


Kuzifahamu au kuzijua hizi sababu kunaweza kusaidia kuboresha mbinu zako za kumpata mwanamke unaempenda maishani. Katika makala hii ya The bestgalaxy, tunaenda zungumzia baadhi ya sababu zinaweza kusababisha mwanaume kukataliwa.

Sababu 5 za kukataliwa na Wanawake

Usafi au kutojipenda

Inasemekana kuna wanawake wengi wanavutiwa na mwanaume msafi anaejipenda. Kati yao, wanawake wengine huwa wanafikili mwanaume msafi ana anaejipenda anaweza kuwajali kama anavyojijali. Hapa ndio mara nyingi wanaume wanaoitwa “Mabishoo” huwa juu.


Usipo kuwa msafi na unaejipenda, unaweza kukumbana na changamoto za kukataliwa sana na wanawake. Mwanamke anaweza asikwambie moja kwa moja, lakini tatizo au sababu ya kukataa ikawa ni hiyo.

Kumuhitaji sana


Mwanamke anaweza sema anamtaka mwanaume anaempenda na kumjali lakini akawa na Wanaume wengi wanaomkata na wanapambana kumpata kwa kumfanyia vitu vingi vya kumjali ili awakubalie lakini anawakataa. Cha kushangaza, mwanaume ambae anaweza uteka moyo wa mwanamke wa namna hii anaweza kuwa ni mwanaume asieonesha kumuhitaji sana kama wengine.


Kiufupi baadhi ya wanawake hawataki mwanaume aoneshe uhitaji sana. Wanataka mwanaume anaewapa muda, anaewapa vimashaka mashaka kidogo lakini anaupendo wa kweli.
Kuonesha kumuhitaji sana mwanamke, kunaweza kufanya uonekane mjinga kwake na ukakataliwa.

Kutokujiamini

Wanawake wengi huvutiwa na mwanaume anaejiamni. Kujiamini kwenye maisha na mambo yako ukiwa kama mwanaume, kunaweza fanya wanawake wengi kuvutiwa na wewe alafu wakakukabari.
Usiwe ni mtu unaeonesha kutokujiami mbele ya wanawake. Kuna wanawake huchukizwa sana na mwanaume ambae hajiamni hata kwakuongea kinyonge tu kunaweza mchukiza.


Ukiwa ni mwanaume unaejiamni, mwanamke anaweza kukukubali na kuamini katika wewe. Kiufupi ukijiamni, wanawake watakuamni. Lakini katika kujiamni kwako hakikisha unaepuka kujisifu sana kwake.

Muelekeo wa maisha

Mwanaume anaweza mtongoza mwanamke bila kufikilia mbali kuhusu mahusiano na maisha. Lakini mwanamke anaweza mkubali mwanaume baada ya kufikilia mbali sana kuhusu maisha na mahusiano.


Mwanaume mwenye maisha mazuri au anaeweza kupambana kupata maisha mazuri anakua na nafasi kubwa ya kukubaliwa na wanawake. Unaweza mwanaume usiwe na pesa nyingi lakini upambanaji wako wa Maisha na muelekeo wako ukawa ni mzuri kiasi, utakubaliwa kirahisi.

Kukata Tamaa ya jibu zuri


Kuna wanaume hukata tamaa ya kuendelea kumfuata mwanamke ambae amekataa kuwa nae mara moja tu. Ukiwa ukiwa Mwanaume unaekata tamaa kwa kukataliwa mara moja, utakosa wanawake wengi sana wanaokupenda kwa dhati.


Baadhi ya wanawake hukataa unapowajia mara ya kwanza na kuwaambia hisia zako lakini moyoni mwao wanakupenda. Huwa wanakataa ili kukupima tu kama unaupendo wa kweli au unawajaribu. Yani wanawake wengine wanaweza kukubali baada ya kuwaelezea zaidi ya mara tatu.

Michezo ya kuchati na Mpenzi wako (Hufurahisha na kurefusha Maongezi)

Kuchati na mpenzi kwenye simu ni njia nzuri ya kuimarisha uhusiano na kujenga hisia za ukaribu kati yenu. Katika ukurasa huu, The bestgalaxy inaenda kukupa michezo michache ambayo mnaweza kucheza pamoja katika kuchati na Mpenzi. Michezo hii itasaidia kurefusha maongezi, kuburudisha na kuongeza furaha katika uhusiano wenu.

Kuna muda wapenzi mnaweza kosa kabisa mambo ya kuchati na hii hutokea mara nyingi. Lakini kama mmoja kati yenu atakua anauelewa juu ya michezo ya kuchati, mnaweza ianzisha na kufanya maongezi yaendele katika kuchati kwenu. Michezo hii ya kuchati ni mbinu nzuri ya kufanya maongezi yaendele katika kuchati kwa wapenzi. Kwa kiingereza michezo hii inaitwa “Texting Games” na ipo mingi sana japo hapa tutaangalia michezo michache tu.

Michezo hii michache ni rahisi na inahitaji muda mchache kumuelewesha mpenzi wako kama haijui unapotaka mcheze. Haina haja ya kuwa na vifaa maalum au kuwa pamoja kimwili ili kueleweshana. Endelea kusoma ili kuijuia na kuielewa michezo hii ya kuchati.

Jinsi ya kum-surprise au kumshangza mpenzi wako bila kutumia Pesa BONYEZA HAPA>>>

Michezo ya kuchati na Mpenzi wako wa kiume au wakike

Kwasababu nakupenda

Mchezo huu unachezwa na wapenzi ambao mnapendana alafu mmetulia mnachati kwa sms. Wapenzi mnatakiwa kuwa mnatumiana sms zenye ujumbe unaojumuisha maneno “Kwasababu nakupenda”.

Kwamfano; unaweza mwambia mpenzi wako “Nimekupa moyo wangu wote kwasababu nakupenda”. Huu ni mfano tu lakini mnatakiwa kutumiana sms za muundo huo zinazogusa mioyo yenu na kuelezea hisia zenu. Mchezo wa “Kwasababu nakupenda” unaweza kuwafurahisha na vilevile mtakua mnajenga mahusiano yenu kwa kuambiana mambo mazuri mnayoweza kufanya,mlio yafanya na mnayotaka kufanya Kwasababu ya upendo.

Maliza au taja wimbo

Mchezo mwingine ni huu unaitwa “Maliza au Taja wimbo”. Wapenzi katika mchezo huu mnakua manatajiana mistari ya nyimbo za mapenzi alafu kila anaetajiwa atatakiwa kumalizia mstari au kutaja jina la nyimbo aliotajiwa.

Kutuma mistari mitamu ya kisisimua, kutamfurahisha zaidi mpenzi unaechati nae kwenye mchezo huu.
Kwenye mchezo huu mnatakiwa kuwa ni watu mnaosikiliza na kufuatilia nyimbo za mapenzi. Kama ni watu wa namna hiyo, basi mnaweza furahia zaidi mchezo.

Jinsi ya kulinda Ndoto zako Maishani zisife BONYEZA HAPA>>

Kisia nilipo

Mchezo huu unachezwa na wapenzi na wanaucheza kwa kukisia mazingira ambayo wapo. Yani unaweza anza kwa kukisia sehemu alipo, anachokifanya na hata vitu vilivyo mzunguka. Yeye atakua anakwambia kama umekosea au umepatia.

Mtakua mnapokezana pale mmoja wenu anapopatia kukisia. Mchezo huu wa kukisia unakua mzuri zaidi kama watu wote ni wakweli alafu mnapendana kiasi cha kuweza kuumiza kichwa kufikilia na sio kutaja tu mnachojiskia. Kila mchezaji anatakiwa kufikilia jibu kulingana na anavyomjua mwenza wake.

Nishawishi tulale

Katika michezo, mchezo mzuri sana wa mapenzi katika kuchati ni huu. Mchezo wa “Nishawishi tulale” ni mchezo unachezwa wakati wa usiku unapochati na mpenzi.
Unachezwa kwa kuahidiana kuwa hamtalala na mtachati pamoja mpaka asubuhi. Kama mmoja anataka kulala kabla ya asubuhi, tatatakiwa kumshawishi mweza wake walale kwa kufanya au kumwambia jambo lolote litakalomshawishi mwenza wake.
Mtu anaetaka kulala aweza ahidi zawadi, akatoa maneno mtamu au jambo lolote litakalo mfanya mpenzi asietaka kulala, alale. Wachezaji wote mnatakiwa kujali sheria za mchezo na kutimiza ahadi zenu.

Mpelelezi

Machezo wa “Mpelelezi” ni mchezo wa kuchati ambao unahusu kuulizana maswali. Wapenzi mnakua mnapeana maswali kwa kupokezana na kila swali linatakiwa kujibiwa.

Idadi ya maswali inaweza kuwa 5 kwa kila mtu na hata 20 mkipenda. Kikubwa hapa ni kuulizana maswali mazuri yatakayo wafurahisha wote wawili.
Mchezo huu wa kuchati unaweza fanya watu mnaopendana mjuane zaidi ya mnavyojuana kwenye mambo mbalimbali. Ukipata nafasi ya kucheza mchezo huu, kuuliza maswali ya kusisimua na kujenga mahusiano yenu ni muhimu sana.

Michezo yote hii tulioiweka hapa ni rahisi sana kumfurahisha mpenzi wako wa mwanamke au mwanaume. Na huwa inafaida kubwa kwenye kujenga umahusiano ya wapenzi wanapenda kuchati. Unaweza ucheza na mume wako, mke wako bila tatizo lolote. Unaweza pia mtumia mwenza wako makala hii ili kuokoa muda wa kumulelezae ingawa ni vizuri kumuelekeza mwenyewe.

Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy!

Unajuaje kama Ex wako anakupenda? Dalili ni hizi

Mahusiano ya mapenzi yanaweza kuwafanya watu waamini kuwa watakua pamoja milele lakini sio kila mahusiano hufikia huko. Baadhi ya watu hushindwa kufikia malengo ya mahusiano yao baada ya kukumbana na mambo ambayo hutikisa au kuvunja mahusiano. Lakini pia sio kwamba Mahusiano yanayodumu huwa hayapitii mambo kama hayo, hupitia mambo magumu. Kuna watu huvunja mahusiano kabisa na kuitana “ex” lakini baada ya muda hurudiana tena na kuendelea kuwa pamoja. Kiufupi kurudiana na mpenzi wa zamani ni jambo la kawaida ambalo watu hufanya.

Kama bado mpenzi wako wa zamani unampenda, kujaribu kumuelewa mpenzi wako wa zamani inaweza kuwa ni changamoto. Wakati mwingine, mpenzi wako wa zamani anaweza kutoa dalili za kukupenda lakini kichwani kwako ukawa unawasiwasi na hauzielewi. Hapa katika The bestgalaxy, tutazungumzia kuhusu dalili za mpenzi wa zamani(ex wako) kukupenda. Kujua dalili hizi husaidia kumuelewa au kujua kama bado mpenzi wako anakupenda na kuna nafasi ya kurudisha upendo wenu ikiwa na wewe Bado unampenda.

Kujua dalili hizi kunaweza kukupa uwezo wa kujua hisia zake na kusaidia kufanya maamuzi sahihi kuhusu kurudisha uhusiano wenu. Wakati ukifanya hayo, ni vema kufahamu kuwa maamuzi ya kurudisha na mpenzi wa zamani yanaweza kuwa maamuzi mabaya pia kama hautafanya utafiti vizuri juu ya lengo lake kwako.

Mambo ya kuepuka baada ya kuachana na mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

Dalili za mpenzi wa zamani kukupenda

Kuweka ugumu katika mawasiliano

Kuna watu mkiachana huwa wanakata njia za mawasiliano haraka na kukuwekea ugumu wa kuwapata lakini moyoni wanaokua bado wanakupenda. Mtu hufanya hivyo kwa msukumo wa hasira tu au ili aone unamtafuta na ajiridhishe kuwa anamuhitaji. Anaweza kublock kwenye simu na kukuwekea ugumu wa kukutananae lakini siku akiona umepambana na kukutananae mkaogea, atajisikia vizuri kuliko kawaida.

Mara nyingi hii hutokea endapo wewe ndio chanzo cha mahusiano kuvunjika. Adhabu anayokupa ni kuwa mbali na wewe kwa kukata ukaribu ili angalau uone umuhimu wake na kutambua makosa yako. Kupambana kumtafuta kunaweza fanikisha kurudisha uhusiano wenu.

Kukutafuta au kufungua njia za mazungumzo

Mpenzi wa zamani anaweza kuwa anakutafuta kwa njia mbalimbali na kufungua njia za mazungumzo kati yenu. Hii inaweza kuwa dalili ya mpenzi wa zamani kutamani murudiane. Anaweza kuwa anafanya hivi baada ya kukumbuka ukaribu wako na Mapenzi yenu kwa ujumla.


Kukupigia simu, kukutumia sms, kukuondolea block kwenye simu au kutafuta vinjia vingine vya kufanya maongezi na wewe ni ishara za kutaka murudiane. Wengine huwa wanashindwa kuficha kabisa hisia zao na kutaka mzungumzie mambo ya mahusiano yenu. Hapa ndio utasikia akisema mambo kama “Ulienae kwa sasa anafaidi… Umenifanya mapenzi niyaogope… Msalimie mpenzi wako” ili tu muongelee mahusiano yenu.

Wivu unapokua karibu na watu wengine

Njia rahisi ya kujua ex wako anakupenda au hakupendi ni wivu. Ni ngumu sana kwa mpenzi wa zamani kukuficha wivu wake anapo kuona na watu wengine. Kama hakupendi, anaweza asiwe na wivu ila kama anakupenda, moyo wake hauwezi muacha salama pindi unapooneka upo karibu na watu wengine. Anaweza kukosa amani au kufanya jambo lingine linaloonesha anawivu na wewe. Kama ni mtu wa “WhatsApp Status” basi wivu juu ya jambo aliloliona kwako atauweka kwenye Status yake kwa maneno ya kukuumiza au kuonesha ameumizwa.

Yupo makini sana na wewe au mambo yako

Ex anaekupenda anaweza igiza kukupuuza lakini hawezi kukupuuza kirahisi. Unapoongea nae anaweza igiza kukupuuza lakini huwa anazingatia kila neno. Mkiwa sehemu moja anaweza igiza kutokukuzingatia lakini macho na akili yake inakua kwako. Kuna muda unaweza gongana nae macho akiwa anakuangalia alafu akazuga kufanya mambo mengine. Yote ni kwasababu anakupenda na upo kwenye akili yake.

Ni hayo tu katika makala hii ya The bestgalaxy, kama utapenda unaweza Endelea kusoma makala nyingine. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mambo mengine zaidi huku ukijiunga nasi kwenye mitandao ya kijamii.

Kuchepuka kuna faida ila hizi ni hasara zake

Kuchepuka, au kumsaliti mpenzi wako(mume/mke), ni jambo ambalo limekuwa na athari kubwa sana. Ingawa inaweza kuonekana kama jambo la siri na linafaida, lakini ukweli ni kwamba kuchepuka kunaweza kuwa na madhara makubwa na yakudumu maishani mwawahusika.


Sababu za kuchepuka zinaweza kuwa ni mtu kutoridhika na mahusiano ya mapenzi alionayo na kutafuta furaha ya muda mfupi pembeni. Mbali na Sababu hiyo, kuna sababu nyingine nyingi zinawezapelekea mtu kuchepuka. Kuchepuka kuna faida zake na moja ya faida ni kupunguza msongo wa mawazo hasa kama mpenzi wako hakujali.

Watu wengi huenda kwenye michepuko kupata amani ya moyo au kujipumzisha kwenye mahusiano walionayo kwasababu mbalimbali. Pamoja na jambo hili kuwa na faida lakini haina maana ni jambo zuri. Na kuna baadhi ya watu hufanya hivyo lakini kiundani ni hawapendi kuchepuka.

Madhara ya kuchepuka yanaweza kuonekana katika pande mbalimbali za maisha, zikiwemo afya ya kiakili na kimwili, mahusiano ya kifamilia, na hata nafasi ya mtu katika jamii. Watu wanaochepuka hawafikirii matokeo ya muda mrefu ya vitendo vyao, na hivyo kujikuta wakisababisha maumivu na matatizo ambayo hayawezi kutatulika kwa urahisi.

Katika makala hii, tutajadili kwa undani hasara chache zinazoweza kutokana na kuchepuka. Tunafanya hivi kutoa mwanga juu ya jinsi gani vitendo hivi vinaweza kuathiri maisha yetu na wale tunaowapenda.

Jinsi ya kumtuliza mpenzi wako mkikosana BONYEZA HAPA>>>

Hasara za kuchepuka kwa mwanamke au mwanaume

Kupata magonjwa

Kuwa na mchepuko ni kufungua mlango wa magonjwa kwenye mwili wako na familia yako pia. Kuna magonjwa mengi mtu unaweza pata kwa mchepuko na kumpelekea mpenzi wako pia. HIV na magonjwa mengine ya zinaa yanaweza kumpata kirahisi mtu mwenye mchepuko na kuiathiri familia yake pia.
Kama ni mtu useihitaji magonjwa haya na unataka kujikinga basi unashauriwa kutochepuka. Kuwa mwaminifu kwa mpenzi wako ni njia ya kujikinga na magonjwa kutoka nje ya mahusiano yenu.

Kumuumiza mpenzi wako au familia

Watu wengi wanapochepuka huwa wanahisi endapo mpenzi atatambua kuwa anachepuka ndipo ataumia. Lakini ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya watu wakianza kuchepuka huanza uonesha tabia tofauti kwa wapenzi wao. Tabia hizi tofauti huwa zinaanza kumuumiza kabla haya ukweli haujajulikana.


Kama mpenzi wako anakupenda na anakujua vizuri, ni ngumu sana kumficha unapopata mchepuko. Tabia na baadhi ya mambo yako mengi yatabadilika japo hautajitambua. Hali hii itamuingiza kwenye mawazo na maswali mengi ya kumuumiza.
Tabia hizi zinaweza fikia hatua ya kuidharau familia na kufanya mambo mabaya bila kujitambua.

Kuwa mtumwa wa Siri

Kuwa na mchepuko ni Siri ambayo inaweza kukufanya uwe mtumwa kwenye maisha yako. Siri ya kuwa na mchepuko inaweza zaa Siri nyingine inayoweza kufanya usiwe huru kwa mpenzi wako. Kuna watu hutamani mpaka kuiacha michepuko yao lakini wanashindwa kutokana na kuwa watumwa wa siri. Mchepuko unaweza kukujia juu na kutishia kufichua Siri kwa namna mbalimbali ili tu uendelee kuwa mtumwa.


Mbali na hayo, kuwa na mchepuko kunaweza pelekea mtu kupata mtoto wa nje na kuwa mtumwa wa Siri hiyo. Kiufupi Siri ya kuwa na mchepuko inaweza zaa Siri nyingine nyingi zitazokufanya mtumwa unaepambana kufunika vitu ulivyofanya gizani kila siku.

Mfano mzuri wa jambo hili upo katika simulizi ya WEUSI WEUPE, wanawake wengi kwenye simulizi hii waligeuka watumwa wa siri.

Kupata msongo wa Mawazo

Wakati mwingine msongo wa Mawazo unaweza tulizwa na mchepuko lakini sio nyakati zote. Kuwa na mchepuko kunaweza ongeza au kuleta msongo mwingine wa Mawazo. Kuna mambo mengi sana kutoka kwa mchepuko yanaweza kukueletea mzongo wa Mawazo. Mambo kama magonjwa, fumanizi na hata ujauzito unaweza tokea na kukupa msongo wa Mawazo.

Kuyumba kiuchumi au kusahau maendeleo yako

Uchumi wako unaweza athiriwa na mambo yako ya mahusiano ya mapenzi. Mchepuko unaweza kukufanya utumie pesa vibaya au kukupumbaza usifanye mambo ya maendeleo na mpenzi wako. Kuna wanaume hujikuta wanapeteza pesa nyingi za maendeleo kwa michepuko. Na pia kuna wanawake hujikuta wamepoteza pesa au mali za familia kutokana na michepuko.

Kiufupi michepuko inaweza onekana mizuri lakini matokeo yake ni mabaya. Na ubaya mambo ya Siri ni kwamba yakienda vibaya yanakua makubwa sana.
Ni hayo tu katika The bestgalaxy, Endelea kuwa nasi.

Mambo madogo ya kuzingatia katika kuwasiliana na mpenzi aliembali

Kuwasiliana na mpenzi aliembali kunaweza kuwa na changamoto, lakini ni jambo muhimu linaloweka mahusiano katika hali nzuri. Umbali unaweza kuwa ni Sababu ya mahusiano mengi ya mapenzi kuvunjika. Kuna watu hujikuta wamepoteana kabisa na wapenzi wao baada ya kuwa mbali kwa muda mrefu.


Lakini sio kila mahusiano yanaweza vunjwa na umbali, Kuna watu hudumu pamoja hata wakiwa mbali. Na jambo hili linawezekana mkipendana.
Kuna mambo madogo ambayo yanaweza kusaidia kuimarisha uhusiano wenu na kuhisi kama mnaishi pamoja. Katika kurasa hii, tutazungumzia mambo hayo madogo ambayo yanaweza kufanya tofauti kubwa katika mawasiliano na mpenzi aliembali.


Mambo haya yanaweza kusaidia kupunguza kuuhisi umbali kati yenu na kuhakikisha kwamba uhusiano wenu unakua vizuri. Lengo la kufanya hivi ni kusaidia watu waliopo kwenye hali hii kujisikia wapo karibu pamoja na hata kuyalinda mahusiano.

Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze kila mara BONYEZA HAPA>>>

Mambo madogo ya kuzingatia katika kuwasiliana na mpenzi aliembali

Kuuliza alipo mnapowasiliana na anacho kifanya

Unaweza sikia mara nyingi kuwa watu hawapendi kuulizwa “upo wapi sasaivi?” lakini usiache kumuumiza mpenzi wako swali hilo. Ni muhimu kufahamu mpenzi wako yupo sehemu gani hatakama mahali alipo ni sehemu usiozo zijua vizuri. Mbali na mahali alipo, unaweza muuliza na kitu anacho kifanya pia.

Ukiwa na tabia hii unapowasiliana na mpenzi aliembali itakusaidia kuelewa maisha anayoishi na pia mizunguko yake. Kupata picha ya mizunguko au maisha yake kunaweza fanya muwe kama muko pamoja mnapo wasiliana. Tabia hii ni kama inaunganisha ulimwengu wenu hivi. Inaweza kufika mahali mnapiga stori kuhusu mambo anayoyaona, sehemu alipo, sehemu anayoelekea na hata changamoto anazokutananazo alafu mnaelewana.

Hali ya kutafutana


Umbali unaweza fanya mahusiano kufifia lakini mawasiliano yanaweza kudumisha mahusiano. Watu wengi hutumia simu kama njia ya mawasiliano na wapendwa wao waliombali.


Endapo kutafutana kwenye simu kutafifia na hakuna njia nyingine ya mawasiliano, basi mahusiano yanaweza kuwa hatarini sana.
Ni vema kuzingatia hali ya kutafutana na kuhakikisha ipo vizuri kati yenu maana kufifia ni dalili mbaya. Hakikisha unamtafuta mpenzi wako na pia usisahau kufanya mambo yanayofanya asikusahau.

Kutumia maneno mazuri ya upendo

Kuwasiliana na mpenzi wako na kuzungumza kama mafiki sio jambo baya ila usinisahau kuwa unahitajika kuongea nae kama mpenzi wako. Unahitajika kutoa maneno mazuri yatakayo ugusa moyo wake. Kumkumbusha kuwa unampenda, mwambie maneno yatakayo msisimua mpaka akuite “romantic”. Usipofanya hivyo kuna mtu wa karibu yake anaweza fanya hivyo na kuuteka kirahisi moyo wa mpenzi wako aliembali. Akisifiwa au kuchokozwa kidogo vile ambayo wewe haumchokozi, anaweza kukuweka pembeni utulie na mazungumzo yako ya kirafiki.

Sms za kumsifia mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

Kufanya vitu zaidi ya mawasiliano

Mawasiliano yanaweza kuwashikilia mnapo kuwa mbali na mpenzi wako lakini ni muhimu kufanya vitu zaidi ya mawasiliano pia. Mnaweza fanya vitu kama kutumiana zawadi, pesa na kufanya mambo mengine ambayo mtu unaweza kusema “Mpenzi wangu aliembali amenifanyia” mbali na maneno maneno.

Natumaini hayo yanaweza kuwa msaada kwako kama upo katika hali ya umbali na mpenzi wako wa kiume au wa kike. Ukiwa mwanamke au mwanaume mambo haya ni muhimu kuyajua maana kuwa mbali na mtu unaempenda kunaweza tokea kwasababu nyingine zisizozuilika.

Maneno matamu kwa mpenzi wa kiume

Maneno matamu yanaweza kuwa silaha yenye nguvu sana ya kuimarisha uhusiano wa mapenzi. Maneno ya upendo au mahaba yanaweza kumfanya mpenzi wako mwanaume ajisikie vizuri, ahisi kuthaminiwa na kupendwa zaidi.

Katika makala hii, tunaenda kukupa baadhi ya maneno matamu ambayo unaweza kumwambia mpenzi wako wa kiume ili kumfurahisha na kuimarisha uhusiano wenu.

Ingawa wanaume wanaonekana kama wapenda kujali sana wanawake lakini ni kama wanawake, wanahitaji kuhakikishiwa upendo na kuthaminiwa pia. Maneno matamu yanaweza kuwa njia nzuri ya kugusa hisia zako na kumfurahisha mpenzi wako wa kiume. Jinsi mwanamke unavyompenda na kumthamini, huisi uhisi vizuri pia.
Furaha katika uhusiano wenu inaweza changiwa na kumwambia mwanaume wako maneno mazuri na matamu ya upendo. Maneno haya yanaweza kuwa faraja kubwa katika Maisha yake na kuimarisha muunganiko wenu wa kihisia.

Kusema maneno matamu kunahitaji ubunifu na kujua ni nini hasa kinachoweza kumgusa moyo mpenzi wako. Sio maneno yote matamu yanaweza onekana mazuri kwa kila mtu, hivyo ni muhimu kujua tabia na matamanio ya mpenzi wako. Katika orodha ifuatayo, tutakupa mifano ya maneno matamu ambayo unaweza tumia kugusa moyo wa mpenzi wako wa kiume na kumfanya ajisikie unampenda kila siku.

Sms za kumwambia mpenzi wako unampenda BONYEZA HAPA>>>

Maneno matamu kwa mpenzi mwanaume

  • Mapenzi yananiendesha sana siku hizi, lakini napenda yanavyoniendesha. Kukupenda wewe, kukujali, kukuwaza kila mara ni vitu hata mimi mwenyewe nafurahi kuvifanya.
  • Mimi ubovu wangu ni mapenzi yako. Nahisi Raha na furaha hata nikikuwaza tu. Umejaa kwenye hii akili na kutoka moyoni Nakupenda.
  • Wewe ni mwanaume Bora kuliko wanaume wote katika Ulimwengu wangu. Nahisi bahati kuwa na wewe na sijawahi jutia chaguo langu.
  • Kwenye ulimwengu wa mapenzi wewe ni kila kitu kwangu. Nikiwa na kiu, maji ni wewe. Nikitaka Furaha kwako ni tele. Unakua daktari nikiota upele. Ni Mwanaume ulienijulia mpaka nawaza kuwa pamoja milele.
  • Nakukumbusha kuwa wewe ndie ulieniambia “Nakupenda” mara ya kwanza. Lakini moyo wangu ulikupenda hata kabla haujaniambia hivyo. Nakupenda na nakupenda jinsi ulivyo.
  • Umeniaminisha kuwa sukari, asali na tende sio vitu vitamu kuliko vyote Duniani. Kwasasa naamini penzi lako ndilo tamu na pia muhimu maishani. Asante kwa upendo wako, nakupenda sana honey.
  • Tuko mbali ila kabla sijalala nakuwaza, nikilala usingizini nakuota, nikiamka nakuwaza tena. Yote sababu nakupenda na natamani kufanya chochote tuwe pamoja tena. Nimekumiss sana.
  • Kuupa mmea adhabu ya kuota na kustawi bila maji ni sawa na mimi kuishi bila upendo wako. Nguvu yangu na dhaifu wangu ni wewe mpenzi wangu, nakupenda sana.
  • Nikuite jina gani utambue wewe ni mwanaume pekee ninaempenda hapa Duniani? Nakupenda mpaka naogopa mpenzi wangu. Yani najihisi ni mwanamke niliekamilika kwasababu ya penzi lako.
  • Najua kuna wakati nakukosea mpenzi. Inaweza kuwa ni ngumu kwenye nyakati hizo kuamini kuwa nakupenda. Nisamehe kwa yote, usisahau kuwa nakupenda na nitakupenda daima.
  • Nakuombea kila linalokupa furaha na mambo mema kwa mungu. Furaha yako ni amani kwangu kipenzi, nakupenda sana.
  • Katika mambo na penda toka kwako ni vile unanisikiliza mpenzi wako. Napenda sana na najua na wewe moyo wako una mengi kipenzi, hebu niambie chochote Leo wangu.
  • Kila mwanamke ana ndoto ya kupata mwanaume anaempenda Maishani. Natamani kurusha maua juu na kuiambia Dunia kuwa wa ndoto nimekupata. Wewe ni mwanaume wa ndoto zangu, nakupenda zaidi ya unavyofikilia.
  • Kila siku ambayo nipo kwenye mahusiano ya mapenzi na wewe ni siku yenye baraka kwangu. Kila dakika ambayo nipo karibu na wewe ni dakika ya thamani kwangu. Wewe ni muhimu kuliko muda wangu, nakupenda.
  • Nitatumia kila dakika ya maisha yangu nikiwa nakupenda kutoka moyoni. Najivunia kuwa na wewe moyoni, unanipa raha.
  • Popote ulipo tambua unatembea na moyo wangu. Nitahisi maumivu ukiuumiza, nitakua na furaha ukiulinda. Yote ni upendo mme wangu. Nimekupa moyo kwasababu Nakupenda.

Huu ni mwisho wa orodha yetu ya maneno matamu ya mapenzi lakini ndani ya The bestgalaxy Kuna makala nyingine za maneno ya mapenzi. Endelea kuwa karibu na The Bestgalaxy kwa makala nyingine kama hizi.

Maswali ya mwanamke yanayohitaji umakini kujibu (Fikilia kwanza)

Mwanamke anaweza kuwa na maswali mengi ukiwa nae kwenye mahusiano. Maswali haya yanaweza kutokea kutokana na hali mbalimbali zinazomkabili, ikiwa ni pamoja na masuala ya afya, mahusiano, kazi, na hata utani tu. Sio kila swali analouliza mwanamke ulienae kwenye mahusiano lina umuhimu au linahitaji umakini. Laini baadhi ya maswali hayo yanahitaji kufikiriwa kwa kina ili kutoa majibu yanayofaa.

Ukiwa kama mwanaume ni muhimu kuwa na uelewa wa kutambua maswali muhimu toka kwa mwanamke. Mwanamke ulienae kwenye mahusiano akikuuliza maswali usijibu vyovyote unavyojisikia tu, jaribu kufikilia kabla haujajibu. Baadhi ya maswali yanaweza kuwa kama mepesi lakini ndio yakawa ni mazito kuliko mahusiano yenyewe.

Mwanamke anaweza kukuwinda mwezi mzima ili akuulize swali dogo sana kwako lakini jibu lako linaweza kuwa na maana kubwa kwake. Usipo mridhisha na majibu yako anaweza kukujia tena na swali hilo hilo au akaliuliza kwa mtindo mwingine.

Katika makala hii, tumechambua maswali machache ambayo mwanamke anaweza kuwa nayo, maswali ambayo yanahitaji umakini katika kuyajibu. Kujua haya inaweza kukusaidia mwanaume kijana katika mahusiano ya mapenzi na mwanamke.

Jinsi ya kujua mpenzi ulienae anakupotezea muda BONYEZA HAPA>>>

Maswali ya mwanamke yanayohitaji umakini kuyajibu

Unamalengo gani na mimi?



Mara nyingi wanawake ukiwanao kwenye mahusiano wanaweza uliza Swahili na huwa zito sana japo ni kama jepesi. Mwanamke mpaka kafikia hatua ya kukuuliza swali hili tambua amejiuliza vitu vingi sana kichwani kuhusu mahusiano yenu na anataka uyajibu wewe kwa hilo jibu utakalo litoa. Ukijibu jibu ambalo litamuonesha hauna mpango mzuri nae basi mahusiano kwanzia hapo yanaweza anza kukata muda wowote.


Huwa mara nyingi wanauliza swali hilo ili kujua mahusiano mulioyaanzisha ni yakudumu au laa. Kama ataona umejibu kama hauna mpango nae basi anaweza anzisha mahusiano yoyote mapya muda huo. Unaweza kuta tu hata ameolewa ghafla na hajakwambia.

Unafanya kazi gani?



Wanaume wengi huwa wanajibu swali hili kirahisi lakini ni swali ambalo ukikosea kujibu mahusiano yako yanaweza kuwa magumu. Mwanamke ambae hajui kazi yako akikuuliza kuhusu kazi unayoifanya, usikurupuke kutaja kazi nzuri sana ili tu akupende. Ni bora utaje ya kawaida au usitaje kabisa.


Unapomwambia mwanamke kazi yako kuna jinsi kichwani anafikilia atakavyoishi na wewe na maisha yatakuaje. Ukiwa mtu mwenye kipato kidogo na anakupenda basi kunajinsi anaweza kuwa anajibana kimatumizi na kukuomba pesa ndogo kwenye shida.


Ukimwambia unafanya kazi nzuri na ina pesa, usishangae akianza kukuomba viasi vikubwa vya pesa na kukuletea matatizo yanayohitaji pesa nyingi. Sio wanawake wapo hivi ila wengi baada ya kujua kazi huwa hivyo. Kiufupi huwa wanapenda kuwa wanawake wa kiwango chako na ukidanganya kiwango, kunajinsi uweza shindwa kufurahia mahusiano maana atakua amejiweka kwenye kiwango kisicho chako.

Unanipenda kweli?



Hata ukiamshwa usingizi na mpenzi wako unaempenda, hakikisha unajibu vizuri hili swali. Mara nyingi mwanamke akikuuliza “Unanipenda kweli?” Anaweza kuwa anataka kuondoa wasiwasi moyoni mwake juu ya upendo wako kwake.

Inaweza kuwa sio kila anapokuuliza swali hili anawasiwasi ila kumjibu huwa kunaufanya moyo wake ujimwage zaidi kwako.
Kuna muda swali hili pia huwa na jambo kubwa nyuma yake. Lakini uzuri ni kwamba sura yake inaweza kukuambia kama ni jambo baya au zuri.

Umenipendea nini?



Mwanamke kukwambia “Umenipendea nini?” ni jambo la kawaida sana na mwanaume wengi husema “Nakupenda jinsi ulivyo tu”. Mwanaume ni bora ujibu hivyo kuliko kujibu vingine ukajichanganya.


Kuna wanawake huwa wanatafuta mwanaume anaewapenda kweli jinsi walivyo na sio kuwatamani. Ukikutana na mwanamke ambae yupo hivi alafu akajibu mambo kama “Shepu” au “Macho” na vingine bila kumwambia kwanza umempenda jinsi alivyo, anaweza kuweka kwenye kundi la waliomtamani.
Ni vema ukamwambia kwanza umempenda jinsi alivyo alafu akataja na vitu vingine vinavyokuvutia zaidi au unavyo vitamani.



Maswali haya machache ni ya msingi na mara nyingi yanakua na machango mkubwa kwenye kuimarisha mahusiano. Kila swali lina maana yake na uzito wake, na unatakiwa kuyajibu kwa uangalifu. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy.

Jinsi ya kumtuliza mpenzi wako mkikosana au kutoelewana

Kutokuelewana na kufanyiana makosa ni mambo ya kawaida na hutokea mara nyingi sana. Hakuna anaependa mambo hayo yatokee lakini mara nyingi hutokea bila kutarajia.


Kutokuelewana au kufanyiana makosa kunaweza fanya mahusiano ya mapenzi kutikisika na hata kuvunjika kabisa. Lakini hii inategemeana na jambo lililofanya wapenzi mufikie hatua mbaya na maamuzi au hatua muliochukua baada ya kukoseana au kutoelewana.


Katika mambo muhimu kujua katika Mahusiano ni jinsi ya kufanya mnapokoseana au kutoelewana na mpenzi wako. Ni muhimu Kwasababu kukosana na kutoelewana ni kama hakupingiki kwenye mahusiano, hutokea tu. Lakini ukiwa na ufahamu wa jinsi gani ufanye, itakusaidia kwenye kuweka sawa mahusiano kwenye hali hiyo.

Katika makala hii, tutajadili jinsi ya kumtuliza mpenzi wako mnapokosana au kutoelewana. Kwa kuelewa na kufuata mbinu sahihi, unaweza kusaidia kurejesha amani na kuimarisha uhusiano wenu bila shida.

SMS za kumfanya mpenzi wako afurahi BONYEZA HAPA>>>

Mambo ya kufanya kumtuliza mpenzi wako mkikosana au kutoelewana

Muombe msamaha

Baada ya kukosana au kutokuelewana kulikosababishwa na wewe ni vema ukamuomba msamaha mpenzi wako. Neno “Samahani” linaweza muweka sawa mpenzi wako na kumrudishia katika hali ya kwaida. Neno hili ni moja ya maneno yenye nguvu za kurekebisha hisia za mtu na kumuweka sawa mnapokua mmekosana.
Ukimkosea mtu bila kumuomba msahama anaweza kuwa na mawazo mengi sana. Wengine usipo waomba msamaha huwa wanakupangia vitu vingi kichwani ili kukulipizia. Lakini ukiomba msamaha baada ya kukosea inaweza fanya mwenza wako asifike mbali sana kimawazo.

Muache peke yake kwa muda

Kuna baadhi ya watu wakikosewa au wakitokewa na kutokuelewana huwa wanahitaji kuwa peke yao kwa muda ndipo watarudi sawa. Usipo mpa muda wa kuwa peke yake hata msamaha wako hawezi kuuelewa.
Sio kila mtu yupo hivyo ila kama ukiwa kwenye mahusiano na watu wa namna hii basi uwe unaheshimu muda wake wa kuwa peke yake pale ambapo hamuelewani au mmekosana. Unaweza ukamuacha peke yake wa muda alafu ukaanza kujisogeza tena kidogo kidogo.
Hii inaweza kuwa sio njia ambayo mtu unaweza fikili kuitumia kwa haraka haraka ila ni njia muhumu ya kuweka sawa kiakili baadhi ya watu mnapokosana.

Mzawadie kitu anachokipenda

Baada ya kukosana au kutokuelewana unaweza muweka mpenzi wako kwenye hali ya furaha kwa kumpa zawadi. Tafuta zawadi nzuri unayohisi anaweza ifurahia alafu mpatie.
Wote tunajua hakuna asiependa au kufurahia kupewa zawadi za gharama Duniani, lakini zawadi sio lazima iwe ya gharama. Zawadi nzuri inaweza kuwa kitu chochote kizuri kinachoweza ugusa moyo wa mtu. Kwaiyo jaribu kufikilia kitu chochote kizuri kitakacho ugusa moyo wa mwanamke au mwanaume umpendae. Kama ukikipata cha bei ndogo au kubwa, fanya kumpatia ili kumtuliza au kumuweka sawa.

Jinsi ya kum-surprise au kumshangza mpenzi wako bila kutumia Pesa BONYEZA HAPA>>>

Mwambie maneno mazuri ya upendo

Kwenye mahusiano ya mapenzi maneno ya upendo huwa yananguvu sana. Neno moja au mawili mazuri ya upendo yanaweza upasua moyo kwa furaha. Hasira na makasiriko baada ya kutoelewana au kukosana, vinaweza tulizwa na maneno matamu ya upendo.
Ukikosana na mpenzi wako au kutoelewana nae, unaweza tumia maneno mazuri au matamu kumuweka sawa. Unaweza mkumbusha jinsi gani unampenda, umuhimu wake kwako, uzuri wake na mambo mengine ya kuvutia au kugusa moyo.

Ni hayo tu katika makala hii, natumai unaweza kuwa umeelewa jinsi gani unaweza mtuliza mtu wako mnapokua hamko sawa. Napenda kusisitiza kwamba watu tupo tofauti hivyo ni vema kufikilia kidogo kama njia unayataka kuitumia inamfaa mwanamke au mwanaume umpendae.

Mwanaume usimfanyie mwanamke mambo haya katika Mahusiano (Fikilia kwanza)

Ni muhimu kuzingatia na kuheshimu hisia na mahitaji ya mwenzi wako. Hili lina umuhimu mkubwa zaidi kwa wanawake, ambao mara nyingi wanahitaji uangalifu maalum ili kuhisi kuthaminiwa na kuungwa mkono ndani ya mahusiano na hata maisha kiujumla. Hapa The bestgalaxy ukurasa huu unaenda kukujuza mambo ambayo si vema ukayafanya kwa mwanamke unapokua nae kwenye mahusiano. Makala hii inaweza onekana imelenga mwanaume lakini kila mtu anaweza isoma. Mbali na hayo kuna makala nyingine tutakuja lenga wanawake pia na itaweza somwa na yoyote.

Katika Mahusiano mnaweza kutana na watu wenye tabia tofauti, mkaelewana na kuwa pamoja. Kuwa pamoja kama wapenzi kunaweza kuwa na mambo mengi sana mnafanya au kufanyiana. Mambo mengine yanaweza onekana mazuri na mengine yakaonekana wazi kuwa mabaya. Mengine yanaweza kuonekana mazuri au ya kawaida lakini ni mabaya baada ya muda.

Jinsi ya kumfurahisha mwanamke katika Mahusiano BONYEZA HAPA>>>

Mambo mwanaume kumfanyia mwanamke si vizuri

Usitoe siri au mambo mabaya ya mwanamke wako kwa wengine

Unaweza ukawa na mpenzi mwanamke mwenye mambo ambayo si vema kuyaonglelea kwa watu. Yanaweza kuwa ni mambo yanayofanya mtu amshushe thamani na kumchulikia vibaya.

Ikiwa unatabia ya kuongea mambo hayo kwa watu na bado upo nae kwenye mahusiano hata wewe unaemuongelea unakua unajichafua pia. Itakua ni vizuri kama utakua unatabia ya kutomuongelea vizuri mwanamke wako maana thamani yake ikiwa kubwa kwa watu na wewe unaonekana wathamani pia. Ni bora usimuongelee kabisa kuliko toa Siri au kumuongelea vibaya mtu ulienae kwenye mahusiano.

Usimshawishi kufanya mambo hatari kupinga ujauzito

Kama unampenzi na hamjafikia hatua ya kukubaliana kuzaa, basi hakikisha ukiwa kama mwanaume unakua mungalifu pia kwenye kuzuia ujauzito. Usiwe ni mtu ambae unaenda mara kwa kama hauoni au kuelewa mwanamke anatumia njia zipi alafu anakua makini kusisitiza mwanamke atumie njia hatari kuzuia matokeo ya uzembe.

Njia hatari zikizidi zinaweza msababishia mwanamke matatizo ya kizazi. Sasa unaweza muelewa kirahisi pindi atakapo patwa na matatizo hayo na kushindwa kupata ujauzito?


Ukiona mwanamke wako haelewi au anatumia sana njia za hatari bila kukushirikisha, hakikisha unamsaidia na kumuelimisha. Sio Kila mwanamke anaufahamu mzuri juu ya mambo ya uzazi. Fanya hivyo ili muuzuie ujauzito kwa njia salama na awe vizuri mpaka mtakapo amua kupata mtoto.

Jinsi ya kum-surprise au kumshangza mpenzi wako bila kutumia Pesa BONYEZA HAPA>>>

Usimpuuze bila kumsifia au kumpa maneno mazuri baada ya tendo

Baada tu ya tendo hasa la mara ya kwanza kwa mwanamke anaweza kuwa na mawazo mengi ya kutaka kujua kama yupo vizuri kwako au laa. Ukiendelea na mambo yako na kuondoa ukaribu baada ya tendo Hilo unaweza kumfanya mwanamke ahisi vibaya juu yake mwenyewe.

Kama ni mpenzi wako, hakikisha haumuachi kwenye Mawazo hayo kila mara. Jitahidi kukumbuka kumtafuta na kumpa maneno mzuri juu ya alicho kufanya na wewe. Hii pia inaweza kumfanya ajiamini au kuwa huru anapokutana na wewe tena kwenye tendo.

Epuka mahusiano ya muda marefu kama haunampango wa kumuoa

Kati ya mwanamke na mwanaume, mahusiano yakianza mara nyingi anaewaza mbali kuhusu mahusiano ni mwanamke. Anaweza waza kuhusu familia na hata watoto kipindi mahusiano hayajafikia hata kuishi pamoja. Hili sio jambo baya maana ni moja ya ndoto zao.


Unapokua na mwanamke kwenye mahusiano ya muda mrefu anaweza kuwa anawekeza sana akili yake kwako na kufanya amini utakua nae milele. Sasa kama hauna mpango wa kumuoa au kuwa nae maishani basi ni wazi mahusiano ya muda marefu ni maandalizi ya kumuumiza tu. Ikiwa hautaki kumuumiza mwanamke usie na mpango nae, mahusiano ya muda mrefu ni yakuyaepuka sana ili usimuuze. Usipofanya hivyo unaweza uumiza na kumpotezea muda wa kumtafuta atakae mpenda milele au kumuoa.


Mambo tuliozungumzia hapo juu yanaweza kuwa marahisi kusahau au kupuuza lakini ni mambo muhimu. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy na useache kuwa nasi.

Sms za kumwambia mpenzi wako kuwa unampenda

SMS inaweza kuwa njia nzuri ya kueleza hisia za upendo na mapenzi kwa mwanamke au mwanaume umpendae. Sms kama sms zinamchango mkubwa katika mahusiano ya sasa maana ndio mara nyingi huunganisha wapenzi wakiwa mbali.

Katika makala hii, tumekuangalia jumbe mbalimbali za SMS ambazo unaweza kumtumia mpenzi wako kumwambia kuwa unampenda. Kuonyesha upendo kupitia maneno kunaweza kuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha uhusiano na kuongeza ukaribu kati yenu. Kunaweza mkumbusha jinsi gani unampenda na unahitaji.

Kwenye mahusiano ya mapenzi, maneno ni kitu kikubwa sana. Maneno yanaweza yumbisha mapenzi na hata kuyaweka sawa pia. Soto tunajua kwamba wakati mwingine mnaweza kuwa kwenye mahusiano lakini yakawa yanayumba. Kumwambia maneno mpenzi wako ya jinsi gani unampenda kunaweza mkumbusha mpenzi wako kushikamana na kuwa pamoja kwenye mahusiano. Na pia kuna muda mpenzi anaweza kuwa na kiu ya maneno mazuri toka kwako lakini akashindwa kusema maana na yeye haelewi.

SMS za kumsifia mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

Sms za kumwambia mpenzi mwanamke/mwanaume unampenda

  • Yule mtu anaeweza ufurahisha au kuuvunja moyo wangu ni wewe. Kuwa nawe ni furaha ya moyo wangu, sitamani kuwa mbali na wewe.
  • Kama kukupenda ni ujinga basi nakubari kuwa hivyo. Penzi lako limeushika moyo wangu mpaka naogopa. Ukiona chozi langu la maumivu ya mapenzi limenidondoka jua ni wewe. Na ikitokea hivyo naomba usije sahau kuwa hata wakulifuta pia ni wewe. Nakupenda sana.
  • Nakupenda Toka moyoni, Ukaribu wako huichemsha damu. Kuwa na Wewe ni Ndoto yangu tamu, staki kukatishwa mpenzi maana hainiishi hamu.
  • Penzi lako limenipeleka kwenye ulimwengu wa mapenzi ambao sikuwahi jua upo. Unanipa Raha, nakua na furaha kama mtoto.
  • Zawadi kubwa ninayotamani kuendelea kupata toka kwako ni upendo wako. Moyo wangu umeisha lidhia kuwa na wewe maishani, na wewe ukibadilika tu, jua unaniumiza mwanzako.
  • Duniani karibu kila mtu ana anae mpenda kwa dhati toka moyoni na yupo akili kila mara. Katika Maisha yangu mtu huyo ni wewe!
  • Wanaweza kuwa wamekwambia au umesikia maneno mengi kuhusu mimi. Ila naomba upuuze na usikilize moyo wangu unasema nini sasaivi. Moyo wangu usema unakupenda wewe!
  • Nimekua nikipenda kuangalia vitu vizuri na vyakupendeza ili nifurahi. Tangu nilipokutia machoni sina haja ya kuangalia chochote kizuri mbali na wewe ili nifurahi. Macho na kila kitu toka kwako hunivutia.
  • Ninapomaliza kuongea na wewe kwenye simu hua nakata simu lakini natamani kuendelea kuisikia sauti yako tena. Sijawahi kuichoka sauti yako maana ni faraja ya moyo wangu. Nakupenda sana.
  • Sijawahi jihisi mpweke nikiwa karibu na wewe mpenzi. Naweza umia kwa kupoteza vingi maishani ila nitaumia zaidi nikikupoteza wewe kipenzi. Maana nanipa sababu ya kufurahia maisha.
  • Moyo wangu hupitia mambo mengi maishani. Lakini dawa yake kila mara huwa ni wewe. Unajua jua kuugusa bila kuushika. Unagusa sehemu wajinga hawawezi fika. Nitakupenda mpaka mwisho wa Maisha.
  • Siri ya furaha yangu ni kuwa na wewe. Najiona wa thamani kwasababu yako. Moyo wangu umenitoraka, upo kwako. Umeuvuta kwa Raha za penzi lako. Nakupenda sana Mpenzi.

SMS hizi ni nzuri kwako? Kama ni nzuri unaweza tumia Bure kwa unaempenda. Usisahau kuangalia sms nyingine za mapenzi ndani ya The bestgalaxy na useache kuifuatilia pia. Asante sana kwa muda wako ulioutoa kusoma makala hii.