Tag Archives: maisha

Epuka kukopa pesa kama unatabia hizi ndani yako

Kuna uwezekanao wa kuwa na mambo mengi sana yanayoweza kusukuma mtu kukopa pesa za watu wengine au taasisi mbali mbali za kifedha. Na kukupa ni jambo zuri sana maana kuna muda mtu unaweza kukwama kifedha kwa kukumbana na jambo linalohitaji pesa ambayo hauna lakini ukalimudu kupitia mkopo.

Kuna watu hukopa pesa ili kurekebisha mambo yao yalioenda vibaya na kuna hata ambao hukopa ili kulifanikisha jambo lisilo na ulamazima sana. Kukopa kwasababu yoyote ile ni uamuzi mzuri lakini itakua uamuzi mzuri zaidi kama umefanikiwa kwenye jambo lako na kuulipa mkopo wako. Kama haujakamilisha jambo lako au umefanikisha lakini haujafanikiwa kulipa deni la mkopo wako, uamuzi wa kukopa unaweza kuwa mbaya kwako. Na endapo hali yakushindwa kulipa itakua inakuandama kila mara unapokopa ni vema ukaanza kujiweka mbali kidogo na mikopo.

Hapa The bestgalaxy tunakupa tabia ambazo mara nyingi zikiwa ndani yako basi mikopo huwa karibu sana na pia huwa ni ngumu kuilipa. Sio kila mtu mwenye madeni au anaeangukia kwenye madeni anatabia hizi. Ni baadhi ya watu tu ndio huwa na tabia tunazoenda kuzielezea hapa. Niwesema hivyo maana wengine husukumwana na vitu vilivyo nje kabisa na uwezo wao  au sababu myingine mabali na tabisa hizi.

Mambo unayotakiwa kujua kuhusu simu za mkopo BONYEZA HAPA>>>

Epuka kukopa pesa kama unatabia hizi ndani yako

Kushindwa kuzirudisha pesa zako mwenyewe

Kama ni mtu mwenye malengo na huwa unajiwekea pesa kwaajili ya mambo mbalimbali basi kuna muda unaweza kuwa unajikopa mwenyewe. Yani unachukia pesa ulizojiwekea kwaajili ya jambo flani na kuzitumia kwenye jambo lingine tu huku ukiwaza kichwani “Nitazirudisha”. Ikiwa unatabia hiii na unakua na msimamo wa kuzirudisha tena hizo pesa basi unaweza usiteseke sana kulipa hata ukikopa kwa watu wengine. Lakini kama huwa haurudishi pesa hizo na ni tabia yako, kunaweza kuwa na ugumu pia unapokopa kwa wengine. Ni vema ukajaribu kujiimarisha ndani yako kabla ya kukopa kwa wengine. Hakikisha unapambana sana kurudishia pesa sehemu zako za dani ukichukua pesa.

Jinsi ya kupata Mkopo kwenye simu BONYEZA HAPA>>>

Kuhairisha mipango yako ulioianza

Kuna baadhi ya watu huwa na mipango ya biashara na Mambo mengine yanayoweza kuhitaji pesa ili kuingiza pesa. Kukopa kunaweza kuwa ni wazo la haraka kwa mtu mwenye mipango ya namna hii lakini hana mtaji au pesa inayohitajika.
Kukopa sio kitu kibaya kama umekusudia kuanza kupambana kutimiza mpango uliojiwekea. Lakini kama ni mtu unaempenda kuhairisha mipango ulioianza, kukopa kunaweza kuumiza.
Ukichukua Mkopo kwaajili ya mpango flani lakini ukahairisha na kwenda tofauti na mpango huo, kunakua na hatari kubwa ya kupoteza pesa hiyo. Pesa ikiisha bila kufanya kitu kilichosababisha ukope, unaweza jilaumu kuliko ungefanya na kushindwa.
Kama haujaweka vizuri mipango yako au haupo tayari kuipambania kwa asilimia 100, basi usikope pesa kwanza.

Kusahau shinda unapokamata pesa yoyote

Hali yako huwa inakua vipi muda ambao hauna pesa? Na hua inakua vipi ukipata pesa? Kama ukipata pesa yoyote mkononi mwako shida huwa unazisahau, unafanya matumizi na kuacha kabisa kutafuta pesa basi kukopa kunaweza kuwa kubaya kwako. Ukikopa pesa na kuishika mkononi pesa hiyo inabidi iwe kichwani kwako kuwa sio pesa yako na unahitajika kulipa. Hii inaweza kukusaidia kupata mpango wa kuilipa na kuwa makini unapozitumia pesa hizo za mkopo.
Ikiwa utaruhusu pesa hiyo ikusahaulishe shida na kuichukulia ni yako, basi unaweza kuwa ndio mwanzo wa kupuuza deni lako, kuridhika na kuanza ikiutumia pesa.
Usiache kuiona pesa ya Mkopo kuwa ni Mkopo hata ikiwa na mamilioni ya pesa.

Haupendi kudaiwa.

Kutopenda kudaiwa ni jambo zuri sana ila linakua zuri kama utakua na uwezo wa kujikumbusha mwenyewe kulipa pesa kabla haujadaiwa. Mbali na hapo ukiwa haupendi kudaiwa itabidi uanze kuepuka kukopa pesa maana kudaiwa ni lazima na ukichukia au kumfanyia vibaya anaekudai itakua ni kosa kwako tu kivyovyote maana umeshindwa kutimiza makubaliano. Wengine hufikia mpaka hatua ya kupambana kukata kulipa Kwasababu ya kudaiwa vibaya lakini hawajihukumu kwa kuchelewesha pesa muda mrefu kinyume na makubaliano.

Natumaini umesoma na kuelewa makala hii na inaweza kuwa msaada katika Maisha yako kwenye upande wa kukopa. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mambo mengine zaidi.

Mguso Wa Dhahabu (Simulizi ya Sauti)

Karibu katika simulizi fupi ya sauti unayoweza sikiliza hapa The bestgalaxy. Simulizi hii inahusu Mfalme mpenda Dhahabu aliwahi hitaji kuwa mtu mwenye utajili kuliko watu wote Dunia.

“The Bestgalaxy” ni jukwaa maarufu linalotoa simulizi za sauti pia. Simulizi hizi zimeandaliwa kwa umahiri mkubwa. Kupitia The bestgalaxy wasikilizaji wanapata fursa ya kuingia katika dunia za kufikirika na kushuhudia matukio ya kusisimua, ya kichekesho, na hata ya kuhuzunisha. Mbali na kusikiliza, msikilizaji anaweza soma simulizi na kufurahia muda wake. Tunaweza sema The bestgalaxy inafanya iwe rahisi kwa mtu yeyote mwenye simu au vifaa vingine kufurahia burudani bora bila matatizo.

Jinsi ya kulinda Ndoto zako Maishani zisife

Katika maisha, kila mtu ana ndoto ambazo anatarajia kutimiza akiwa hai. Ndoto hizi zinaweza kuwa kuhusu elimu, familia, au mambo mengine . Mara nyingi, safari ya kuelekea kutimiza ndoto inaweza kuwa na changamoto nyingi zinazohitaji uvumilivu na mapambano ili kuzitimiza. Wengi hukata tamaa na kushindwa timiza ndoto zao wakiwa bado waopo hai. Ni muhimu kufahamu mambo ya kufanya ili kulinda ndoto zako na kuhakikisha unafanikiwa kutimiza pamoja na changamoto nyingi utakazopitia njiani.

Kuna muda mtu unapokimbiza ndoto zako unakua na nguvu ya kuendelea kuzifuata. Lakini katika safari hiyo, Kuna muda mtu unaweza fikia hauna nguvu tena ya kuendelea kuikimbiza ndoto kutokana na mambo unayokutana nayo safarini. Inaweza fikia wakati mtu unaamu kupuuza ndoto yako kwa kuamini kuwa “haiwezi kuwa kweli” na kujiona mjinga kwa hatua zote ulizopiga ili kufikia.

Kama unandoto na unahitaji kutimiza, Hapa The bestgalaxy tunaenda kukupa mambo machache muhimu yatakayo ilinda ndoto yako isife kama ndoto za watu wengine.

Mambo matano yanayoweza kukusaidia kufanikiwa Maishani BONYEZA HAPA>>>

Jinsi ya kulinda ndoto zako Maishani zisife

Vutiwa na mafanikio ya wengine bila kuchukia


Unapokimbiza ndoto yako unaweza kuwa unaona watu wengi wakitimiza ndoto zao wakati wewe bado. Kushuhudia wengine wakipata unachokosa inaweza kuwa ni jambo gumu kwa moyo. Unaweza jihisi vibaya na hata kuanza kuwachukia waliofanikiwa kwenye jambo ambalo wewe linakuumiza na haufanikiwi.
Ili kuzilinda ndoto zako ni vema ukavutiwa na kufurahia mafanikio ya wengine. Ukifanya hivyo itakua rahisi hata kujifunza mambo ambayo waliofanikiwa wameyafanya ili kufanikiwa. Lakini ukiwachukia utakua huoni la kujifunza na ukionawanaendelea kufanikiwa, utaumia na kupoteza muelekeo wako.

Unayoyapitia yanakuandaa kwa yajayo

Kila magumu unayopitia kwenye kuikimbiza ndoto yako, yanakuandaa kwaajili ya kutimiza ndoto unayoikimbilia. Hivyo haina haja ya kukata tamaa unapopitia magumu. Ukidondoka au kuumizwa, nyanyuka futa machozi, jiulize jambo hilo limekufunza nini kisha songa mbele. Kuna watu wanasema “hauwezi kuiona thamani ya kitu muhimu maishani ulichopata kama haujapata shida kukitafuta”. Vitu vingi vya thamani vinakua na ugumu kuvipata na huo ugumu ndio thamani yake.

Chagua mtazamo mzuri juu ya kifo

Upande wa kifo ni upande ambao watu wachache huuongelea linapokuja swala la kutimiza ndoto maishani. Watu wengi wanapokua wanaona Matukio kuhusu kifo katika mazingira yaliowazunguka, ndoto zao huyeyuka. Huwa wanakosa nguvu ya kuendelea kukimbilia ndoto zao huku moyoni wakijisemea “Duniani Tunapitia”. Hatugusii upande wa kidini ila Kama unandoto na upo hai jambo hilo lisiwe kisingizio cha kutotimiza ndoto yako. Amini vyovyote ila usitupe ndoto zako ukiwa hai maana ndoto zako zinaweza kuwa ni zaidi ya uhai wako. Mungu anaweza kuwa anataka hata kizazi chako kukibadilisha ila ni baada ya wewe kutimiza ndoto. Ndoto ya mtu inaweza kuwa ni kubwa kuliko hata Dunia ndio maana kuna ndoto watu walizikimiza wakajikuta wamebadilisha Dunia.

Kuwa na Sababu kubwa kuliko wewe ya kutimiza ndoto zako

Ili ndoto yako iwe imara na isije kufa kizembe, unganisha ndoto hiyo na mambo makubwa kuliko wewe. Unapofikilia Sababu za kuikimbiza ndoto yako, weka sababu kubwa ya kutimiza ndoto yako na sio vitu vidogo kama gari au nyumba. Fikilia kuhusu maisha ya watoto wako, familia yako na vitu vingine vikubwa na vya muhimu kama hivyo.

Fahamu hakuna binadamu anaona ndoto yako kama uionavyo

Hakuna binadamu anaeona vitu unavyoona au kufikilia. Hivyo hivyo hakuna mtu anaeona ndoto unayoikimbiza kama jinsi unavyoona wewe. Hivyo ukimuona mtu anakucheka, anakukatisha tamaa au kukudharau, usikate tamaa maana hakuna analojua kuhusu wewe na ndoto yako. Ndoto yako inakuhusu wewe hivyo unaiona wewe pekeako alafu watu wengine wanaona matokeo tu. Usihangaike na watu wanaokudharau, kuogopesha au kukukatisha tamaa, wewe endelea kufanywa kinachotakiwa kufanywa ili uwe unapotakiwa kuwa kwenye maisha yako.

Natumaini makala hii itakua msaada katika Maisha yako na huu ndio mwisho lakini The bestgalaxy inavitu vingi kwaajili yako. Endelea kuwa karibu nayo kwa mengine zaidi.

Kwanini haufanikiwi kimaisha? Sababu hizi hapa

Kila mtu unaweza kumsikia akiongelea kuhusu mafanikio lakini unapaswa kujua kuwa watu hawana maana sawa ya mafanikio. Hata ukiwauliza “Mafanikio ya kimaisha ni nini kwako?” watu huwaza vitu ambavyo hutegemeana na jinsi mafanikio yana maana gani kwao.

Kiufupi Mafanikio ya kimaisha tunaweza sema ni hali au matokeo ya kuweza kufikia lengo au malengo fulani maishani. Tunaweza pia kusema mafanikio ni kufikia au kuzidi matarajio, malengo, au viwango fulani vya utendaji katika maeneo mbalimbali ya maisha kama vile kazi, elimu, biashara, mahusiano au maendeleo binafsi.

Watu hukutana na changamoto nyingi katika kuyakimbiza mafanikio ya kimaisha. Hapa The bestgalaxy tumeisha zungumzia kuhusu mambo muhimu ili kufanikiwa pamoja na changamoto nyingi njiani. Katika ukurasa huu tunaenda kuangalia upande mwingine ambao ni mambo yanayoweza fanya mtu asifanikiwe.

Mambo yanayoweza fanya usifanikiwe

Kutojua mafanikio kwako ni nini na yanapatikana upande gani

Kama tulivyoeleza hapo juu, Kila mtu kuna jinsi ambayo mafanikio yanaonekana kwake. Sasa unapaswa kwanza kujiuliza wewe unahisi mafanikio ni nini kwako. Ni elimu ambayo itakupatia kazi? Ni biashara ambayo itafanya vizuri mpaka itabadili maisha yako? Usiwe na vitu vingi kichwani, fahamu mafanikio unayoyataka hapa Duniani na fikilia utayapata upande gani.


Kuna mtu aliulizwa “Unata kufanikiwa kivipi?” Akajibu “Kama msanii diamond… Yani nyumba kali, gari Kali na watoto wazuri kama wote… Alafu navimba kama kwenye nyimbo yake moja hivi. Yani nikisimama watu wote shangwe” akaulizwa “kwani wewe ni msanii?” Akajibu “hapana” akaulizwa tena “Unaimba mziki?” Akajibu “ah amna hata siwezi. Na sijikufanya kabisa hizo mambo”
Huyu jamaa kitu anachotamani maishani au mafanikio anayoyatamani ni ya mtu ambae ni msanii. Sio kitu baya, lakini yanaweza timia vipi ikiwa haupo kwenye upande ambao yanapatikana?. Hapa ukizidi kutamani, utapata msongo wa mawazo.


Ni vema kujua mafanikio kwako ni nini na yanapatikana upande gani. Kama mafanikio yako unahisi yatapatikana kwenye biashara, kuwa upande wa biashara, bana upande huo ata uwe msaidizi tu. Tambua kitu unachokihitaji alafu usicheze nacho mbali, pambana kukisogelea.

kubadirisha au kuyakatia tamaa malengo yako

Kujiweka malengo ni hatua nzuri ya kuanza safari ya mafanikio. Lakini mara nyingi malengo huwa na changamoto zake katika kuyatimiza. Unaweza kukumbana na vitu vingi sana katika safari ya kuyatimiza. Lakini unatakiwa kuwa makini sana linapokuja wazo la kubadirisha au kuyakatia tamaa malengo uliojiwekea. kubadirisha au kuyakatia tamaa malengo uliojiwekea inaweza kuwa ndio mwanzo wa kupotea na kushindwa kufikia mafanikio unayoyahitaji. Ni vema kupambana na kuwa msimamo wa kutimiza malengo yako ili uweze pata mafanikio unayoyahitaji.

Kukosa utayari wa kuwa unaetakiwa kuwa au kuacha vinavyo rudisha nyuma.

Inasemekana kwamba kunawatu huwa wana mipango mikubwa kwenye vichwa vyao, tena inayoweza kuwatoa waliopo. Watu hawa wanajua kila kitu kinachohitajika kufikia pale wanapotamani kuwa kimaisha. Sio hayo tu, wanajua mpaka kinachowafanya wasifikie mafanikio lakini hawapotayari kubadirika au kuacha vinavyo zuia kufanikiwa.


Ukitaka kufanikiwa mara nyingi inabidi uwe ni mtu unaweza badirika, kujifunza vitu vipya na kuwa na utayari wa kuacha mambo unayoona kabisa yanakuzuia. Usipo chukua hatua kwenye kufanya mambo hayo, unaweza jikuta unayaona mafanikio unayoyataka mbele yako lakini huyafikii.

Woga wa kushindwa au kuwa tofauti

Kama mafanikio unayoyataka yanahitaji ufanye kitu ili kuyafikia lakini unahisi woga basi tambua kwamba baada ya miaka kadhaa unaweza jutia kuogopa kwako. Wengi tukitaka kufanya bishara au vitu vya maandeleo vitakavyo boresha maisha yetu, huwa tunaogopa kudondoka au kuogopa ndugu, majirani, marafiki na watu wengine waliotuzunguka. Lakini jambo hili watu hujutia baada ya kutambua kuwa walitaka kufanya vitu vizuri ila walishindwa kutokana na kuogopa au kuwawaza watu ambao hawajaungana na maisha yao. Kama umefuatilia simulizi ya utamu wa jumla unaweza nielewa zaidi hapa.


Njia rahisi ya kuondoa woga wakufanya kitu unachotaka kukifanya ni kuingia wenye mazingira yanayohusiana na unachokitaka kukifanya. Kama unataka kuwa mfanya biashara wa samaki, Tafuta marafiki wanaojihusisha na mambo hayo, au naenda kwenye mazingira ya hayo mambo.

Kuwa mjanja! Tufuate kwenye akaunti zetu mpya za kijamii ; Instagram na Facebook

Uzazi wa mpango ni nini?

Karibu The bestgalaxy. Hapa unaenda kupata maaelezo yatakayo kufungua kidogo ubongo juu ya “Uzazi wa mpango. Uzazi wa mpango ni mpango au uamuzi wa mtu au watu katika kuzaa watoto .Lengo kuu la uzazi wa mpango ni kuruhusu wazazi kuchagua ni lini na idadi gani ya watoto wanataka kuwa nayo, kwa kuzingatia rasilimali walizo nazo zao, hali ya maisha, na malengo yao katika maisha. Kuna njia au hatua zinazochukuliwa na watu au jamii ili kudhibiti idadi ya watoto wanazozaa au kuepuka mimba zisizo tarajiwa.

Kuna njia mbalimbali za uzazi wa mpango na hapa chini tunaenda kuangalia njia 6:

Njia za uzazi wa mpango

1. Dawa za Kuzuia Mimba(Njia ya kisasa): Hizi zinaweza kuwa dawa za kumeza au sindano ambazo zinaweza kuzuia ujauzito. Mwanamke anaweza kwenda kwenye kituo cha afya akachomwa sindano ya kuzuia mimba au akameza vidonge vya kuzuia mimba.

2. Kondomu(Njia ya kisasa): Kondomu ni mipira amayo huvaliwa katika tendo kuzuia mimba na kujikinga dhidi ya magonjwa ya zinaa. Mwanaume kuvaa kondomu katika tendo kunaweza fanya mwanamke asipate mimba. Lakini pia kuna kondomu za kike ambazo mwanamke anaweza vaa kumsaidia asipate mimba.

3. Vitanzi(Njia ya kisasa): Hivi ni vifaa vinavyowekwa ndani ya mfuko wa uzazi na huweza kuzuia mimba kwa muda mrefu.

4. Vipandikizi(Njia ya kisasa): Hivi ni vijiti vyenye ukumbwa kama njiti ya kiberiti ambavyo huwekwa katika mkono wa mwanamke kwa lengo la kuzuia mimba.

5. Upasuaji wa Kuzuia Mimba(Njia ya kisasa): Kwa wanaume, upasuaji wa kufunga mirija ya uzazi (vasectomy) unaweza kutumika kuzuia mimba. Kwa wanawake, upasuaji wa kufunga mirija ya fallopian (tubal ligation) ni njia nyingine.

6. Kufuatilia mzunguko wa hedhi au kutumia kalenda(Njia ya asili): Pia unaweza zuia mimba zisizotarajiwa kwa kufuatilia mzuguko wa hedhi kisha kuepuka kufanya tendo katika siku za hatari.

Uzazi wa mpango unaweza kusaidia kudhibiti idadi ya watoto na kuboresha afya na ustawi wa wazazi na familia kwa kutoa fursa ya kuchagua lini na jinsi ya kupata watoto. Lakini unapawa kutambua kuwa njia nyingi za uzazi wampango za kisasa zimekuwa zilieta madhara kwa watumiaji. Ni vema kufika katika kitua cha afya na kupewa muongozo zaidi juu ya njia za kisasa za uzazi wa mpango. Njia ya Kufuatilia mzunguko wa hedhi au kutumia kalenda ni njia ya asili isio na madhara kwa mtumiaji ila ina hitaji umakini sana.

Mambo matano yanayoweza kusaidia kufanikiwa maishani

Kufikia mafanikio katika maisha yako kunaweza kuwa lengo linalohitaji juhudi na muda. Hapa kuna mambo matano unayoweza kufanya ili kuboresha nafasi zako za kufanikiwa:

  1. Jiwekee Malengo Maalum. kama unataka kufanikiwa nivema ukaanza kujiwekea malengo. Fahamu unataka kufanya nini na nini maaana ya mafanikio kwako. Jiulize lengo lako ni lipi, Unataka kufikia wapi na kwanini.
  2. Kuwa tayari kujifunza vitu au ujuzi mpya. Usijifunge kwenye kujifunza unapotaka kufanikiwa maana unapokua katika safari ya mafanikio unaweza kutana na vitu vingi sana na karibu vyote huwa vimelenga kukufundisha na kukukomaza kufikia pale unapopahitaji. Pia wewe mwenyewe unatakiwa kuwa ni mtu ambae unatafuta kujifunza vitu usivyovijua. Fanya utafiti na jifunze kutoka kwa wataalamu katika eneo unalotaka kufanikiwa. Jiunge na kozi, semina, au programu za kujifunza ili kuboresha ujuzi wako na kujiendeleza.
  3. Usiache Kujituma au kujisukuma kwa Bidii. Kuwa tayari kufanya kazi kwa bidii na kujitolea kufikia malengo yako. Kufanikiwa mara nyingi kunahitaji juhudi za ziada na uvumilivu. Kisukume kuendelea kufanya kazi kwa bidii hata wakati wa changamoto.
  4. Jenga mahusiano na watu waliofanikiwa au wanaoweza kukusaidia. Jiweke karibu na watu wenye uzoefu na wanaoweza kukusaidia kufikia malengo yako. Watu hawa wanaweza kutoa fursa za kujifunza, kushirikiana, na kujenga uhusiano ambao utarahisisha wewe kufikia malengo yako.
  5. Usiogope kuwa mbunifu au tofauti. Usiogope kufikiria nje ya box na kutafuta njia za ubunifu za kutatua matatizo ili kufikia malengo yako. Usiogope kuwa tofauti katika mambo yako maana sio kila kilicho tofauti hakipo sahihi.

Kumbuka kwamba mafanikio yanaweza kutofautiana kwa kila mtu na yanaweza kuwa na maana tofauti. Ni muhimu kuwa na uvumilivu na kujifunza kutokana na changamoto zinazojitokeza kwenye safari yako ya kufikia mafanikio.