Mahusiano mara nyingi huanza kwa msukumo wa hisia kali. Yani kila mmoja anajihisi kuwa na haja kubwa ya mwenzake. Kila jambo linaonekana kuwa jipya na lenye kuvutia, Wapenzi wote wanajitahidi kwa hali na mali kuhakikisha wanampendeza au kumfurahisha mwingine. Lakini, kadri muda unavyoenda, hali hii inaweza kubadilika, na baadhi ya watu huanza kuhisi kama hakuna mapenzi ya dhati kama awali.
Hii ni hali inawakumba watu wengi, hata walio kwenye ndoa za muda mrefu. Kuna wakati mtu anajikuta anaendelea kutoa upendo, lakini mwenzake haonyeshi kujali au kuonyesha hisia zozote za kurudisha upendo huo. Hali kama hii inaweza kumkatisha tamaa, kuleta Mawazo na kumfanya mtu ahisi vibaya, hasa pale anapokuwa amejitolea sana kwa ajili ya uhusiano hayo.
Katika Hali hii, kabla ya kuchukua hatua yoyote, ni muhimu kujua kwamba yapo mambo ambayo unaweza kufanya ili kuboresha hali hii na kufufua tena mapenzi kwenye uhusiano wenu. Katika makala hii, tutazungumzia mambo unayoweza kufanya ili kurekebisha hali hii ikiwa imekutokea ghafla kwenye mahusiano yako.
Mambo ya kufanya kwa Mpenzi asieonesha kukupenda katika Mahusiano
Kuwa mpya au tofauti kwake
Kuna wakati mpenzi wako anaweza kuwa ameacha kukuzingatia kwasababu amekuzoea. Yani anaweza kuwa anaona vitu unavyofanya kwake au ukiwa nae ni vitu ambayo vinajitudia mpaka anakuona hauna cha kushangaza. Hapa nazungumzia vitu kama, jinsi unavyoongea nae, muda unaangeanae, zawadi zako, sehemu mnazoenda, ahadi unazoahidi na mambo mengine kama hayo. Ikiwa tatizo ni ili, basi utatakiwa kuwa mtu mpya kidogo kwake. Yapindue mambo ambayo unamfanyia au mnafanya kwa pamoja. Na usiyapindue kwa ubaya, fanya baadhi ya mambo mzuri kwa kumjali lakini iwe ni tofauti na alivyozoea. Kufanya hivyo kwa mpenzi asieonesha kukupenda katika Mahusiano kunaweza mfanya aanze kukuzingatia kwa upendo.
Tafuta tatizo upande wako na wake
Kama kutokukuzingatia kwake kunaonekana kuwa ni jambo zaidi ya kukuzoea, basi jaribu kutafuta sababu ya hali hiyo. Kwanza kabisa jaribu kufikilia kama wewe ndie tatizo maana kuna mambo unaweza kuwa umemfanyia ndio maana hakuzingatii. Fanya kufikilia vitu alivyowahi kukuonya au ambayo unajua kabisa viko upande wako lakini yeye humchukiza. Ukipata tatizo upande wako, fanya kuliweka sawa. Ukikuta upande wako hakuna sababu yoyote ya yeye kuwa hivyo, fanya kuhamia upande wake sasa. Jaribu kufikilia na kudadisi ni kitu gani kimembadilisha hivyo. Tafuta sababu ili ujue uitaweka vipi hali vizuri.
Ukifanikiwa kupata tatizo linalomfanya mpenzi wako asikuoneshe kukupenda, jaribu kuliweka sawa ikiwezekana hata kwa kumshirikisha.
Kaeni muongelee hilo tatizo kwa pamoja
Njia rahisi ya kumaliza matatizo ni hii maana inafanya wote mufunguke yanayofanya musiwe sawa na kujadili mfanye nini ili hali iwe sawa. Fanya kukaa na mpenzi wako muongelee tatizo ambalo unaliona kwenye mahusiano yenu. Hakikisha unamtafuta mida mizuri ya kuongelea mambo haya ili aweze kufungua yaliomo moyoni kwake.
Usipokaanae muda sahihi, anaweza kukuficha yaliopo moyoni mwake. Kama ni mume au mke wako, unaweza ongea nae muda wa kulala au mkiwa metulia baada ya kucheza michezo yenu. Kama ni wapenzi tu, unaweza tafuta muda wenu mzuri wenye utulivu kama mida hiyo nilioiieleza. Usitumie simu kuongea, kutaneni ana kwa ana muongee ndio mtaweza elewana vizuri.
Mwisho; Ningependa kukukumbusha kuwa usisahau thamani yako. Kuna mambo mengi ya kuvunja moyo katika Mahusiano yanaweza kukuvunja moyo ila usisahau kuwa kuitambua thamani ni muhumu. Ikiwa unaona dalili za kuwa mpenzi wako hataki tena mahusiano na wewe, ni sawa kuheshimu maamuzi yake. Unaweza muacha alafu ukamtafuta mtu mwingine anaeijua thamani yako.
Kila mtu anatamani kuwa na mpenzi mwaminifu na anayejali, kwani uaminifu ndio msingi wa mahusiano yenye furaha na utulivu. Si mwanaume wala mwanamke, wote wanapenda huwa na mahusiano na mtu asiewasaliti. Hisia za upendo na kuaminiana, hujenga mahusiano imara ambayo hutoa faraja na usalama wa moyo kwa wapenzi wote wawili. Hakuna anayependa kuwa na mashaka au wasiwasi kuhusu tabia za mwenzi wake, hasa linapokuja suala la kuwa na mpenzi mwingine. Hii ndio maana mwanzo wa mahusiano wapenzi husisitiza sana kutosalitiana kwa kuambiana maneno kama “Nitakupenda milele… Sina mwingine zaidi yako… Siwezi kukusaliti”.
Lakini wakati mwingine, hali ya kusalitiwa hujitokeza, na hii inaweza kuwa ngumu sana kwa aliesalitiwa kukubaliana nayo. Watu wengi hujawa na maumivu makubwa wanapogundua kwamba wamechezewa au kudanganywa na mtu alieshika furaha ya moyo wao. Hupata hisia zinazovunja moyo na kuumiza, na mara nyingi hisia hizi humfanya mtu kujiuliza kama anapaswa kuendelea na uhusiano huo au kuachana nao kabisa.
Uamuzi wa kumwacha mpenzi kwa sababu ya usaliti ni jambo zito maana ni kuharibu kabisa uhusiano uliokuwepo bila kujali mmetoka wapi. Ni muhimu kufikiria kwa makini kabla ya kuchukua hatua yoyote ili kuhakikisha kuwa unafanya uamuzi sahihi maana sio kila kusalitiwa kunatakiwa kuwa mwisho wa Mahusiano. Katika makala hii, tutaangazia mambo ya kujiuliza au kufikiria kabla ya kuchukua uamuzi wa mwisho.
Mambo ya kufikiria kabla ya kumuacha mpenzi kwa kukusaliti
Ni kweli?
Kuna mambo au matukio yanaweza kukufanya uamini kuwa mpenzi wako anakusaliti au amekusaliti lakini ikawa sio kweli. Ni ngumu kuamini kuwa mpenzi wako hajakusaliti wakati umeyaona mazingira ya kukusaliti. Watu wengine huwa Wanaamini kuwa wamesalitiwa hata kwa kuambiwa tu au kusikia maneno ya watu. Unachotakiwa kujua ni kwamba kuna wakati inaweza kuwa sio kweli.
Ni vema kabla ya kufanya uamuzi wa kumuacha kipenzi cha Roho yako, ukathibitisha ni kweli amekusaliti au hajakusaliti. Usije muacha mpenzi wako sahihi kwa vitu vya kuhisi au kusikia. Ukiona mambo yanakuchanganya, unaweza kukaa nae mukaongea kuhusu unachohisi au ulioyasikia kisha ukaangalia anayachukuliaje hayo mambo na yeye.
Chazo ni wewe, yeye au mtu mwingine?
Wengi likitokea jambo la kusalitiwa huwa tunaona mbaya ni aliesaliti lakini kuna wakati mtu mbaya unaweza kuwa ni wewe uliesalitiwa au akawa mtu mwingine tu mbali na nyie. Ukiwa na uwezo au moyo mkubwa, unaweza jiuliza nini chanzo cha usaliti uliofanyiwa. Kuna watu wengi tu huwa wanasalitiana kwenye mahusiano lakini baadae wanagundua nini chanzo, wanarekebisha walipokosea alafu wanaendelea na mahusiano. Unaweza gundua kuwa wewe ndio umesababisha yeye kufanya hivyo au Kuna mtu mwingine ameamua kuwavuruga.
Jambo hili limejitokeza kwenye simulizi fupi iitwayo “SIRI NA SHEMEJI” na inaweza kuwa vizuri sana kama utafuatilia simulizi hii.
Bado anakupenda na anajutia kukusaliti?
Kuna watu wanasema “Usimwamini au kuendelea na mwanamke au mwanaume aliekusaliti”. Lakini kiukweli kwenye jamii zetu mambo ya kusalitiwa hutokea kwasababu mbalimbali na watu husameheana na kuendelea kujenga mahusiano yao kama hakuna kilichotokea. Kabla ya kumuacha au kumsaheme mpenzi aliekusaliti ni vema ukajiuliza “Bado anakupenda?” na pia usisahau kujiuliza kuwa “Anajutia kukusaliti?”. Kama unaona kabisa mtu bado anakupenda sana na hataki kukupeteza kwenye maisha yake, kumsamehe unaweza kuwa uamuzi mzuri. Ila inabindi ujilidhishe kabisa ili usijejutia uamuzi wa kumsaheme.
Pia Jambo limejitokeza kwenye simu fupi iitwayo “SIRI NA SHEMEJI” na inaweza kuwa vizuri sana kama utafuatilia simu hii ili kuelewa zaidi.
Unaweza kusahau na kumpenda bila kujali?
Baada ya mpenzi wako kukusaliti, angalia moyo wako kama unaweza sahau yote na kuendelea kumpenda. Kama unaona kabisa hauwezi kumsamehe au kusahau alichofanya, ni vema ukamuacha tu maana ulionayo moyoni yanaweza pelekea kufanya jambo baya kwake kama kisasi.
Kwaiyo ni vema ukajipima kwanza kama unaweza sahau yote na kuendelea kupendana nae kama hakufanya kitu kibaya kwako. Yani kama umemsaheme, usije waza mabaya yake tena.
Hautakua wakwanza kufanya hivo, watu wengi hufanya kwa wapenzi wao, waume zao au mwake zao. Lakini ukiona hauwezi, jiweke mbali nae maana kuna siku moyo unaweza kukusukuma kumfanyia mabaya.
Ni hayo tu katika ukurasa huu wa The bestgalaxy, lakini kama ni mtu anaependa kuelewa zaidi, unaweza soma Simulizi ya “SIRI NA SHEMEJI” ili kuburudika huku ukiongeza uelewa kuhusu swala hili.
Simu imekuwa sehemu muhimu sana katika mahusiano ya siku hizi. Kupitia simu, wapenzi wanaweza kuwasiliana kwa urahisi, kubadilishana mawazo, na kueleza hisia zao bila kujali umbali uliopo kati yao. Kutopokea simu au kutokutafutwa na mpenzi wako kwa muda mrefu kunaweza kuleta wasiwasi, hasa katika mahusiano yenye mawasiliano ya mara kwa mara.
Kwa kuwa mazungumzo kupitia simu ni njia rahisi ya kutunza uhusiano, ni jambo la kawaida kwa mpenzi kujisikia vibaya au kutokuwa na amani mpenzi wake anapokaa muda mrefu bila kupiga simu. Kutozungumza kwa muda mrefu kunaweza fanya mtu kujihisi kutothaminiwa kwenye mahusiano yake ya mapenzi au kuhisi jambo jingine baya limeingia kwenye mahusiano.
“Kutokupigiwa simu na mpenzi” hali inayoweza kuwa na sababu nyingi na pia inaweza ikatokea kwa namna nyingi. Lakini badala ya kuwa na wasiwasi au kuchukia, kuna mambo kadhaa unaweza kufanya ili kuiweka sawa. Ikiwa mpenzi wako hakupigii simu kwa namna yoyote na haujui nini Cha kufanya, hapa chini kuna jinsi tumeeleza mambo unayoweza kufanya.
Mambo ya kufanya mpenzi akiwa kakupigii simu au kukutafuta
Tengeneza tabia ya kumpigia sana wewe alafu ghafla uiache kwa muda
Unaweza kufanya Jambo hili kama mpenzi wako mpya anatabia ya kutokukupigia simu lakini ukimpigia, mnaongea vizuri tu na mahusiano yenu yametulia. Utachotakiwa kufanya hapa ni kuzidisha kumjali na kumpigia simu za mara kwa mara alafu unaamua kutulia bila kumpigia ghafla. Jambo hili linaweza mfanya akupigie kujua ni nini tatizo maana sio kawaida yako. Akikupigia kwa mara ya kwanza, inaweza kuwa ndio tabia yake ya kukupigia imeanzia hapo.
Kuna watu muda huu, hawakupigii kwasababu hakuna jambo la kuongelea. Inaweza kuwa hivyo pia kwenye mahusiano. Mpenzi wako anaweza kuwa hakupigii simu mara kwa mara kwasababu mnakosa vitu vizuri vya kuongelea. Kuna watu wengi tu huwa wanashindwa kuongea vizuri na wapenzi wao kwenye simu. Na baadhi ya wanaoongea, huwa hawaongei mambo mazuri ya kuvutia kiasi kwamba mpenzi awe anatamani kupiga simu na kuongea tena.
Kama unapitia jambo la kutopigiwa simu kwa namna hii, basi fanya kutengeneza uwezo wa kuongea na mpenzi wako kwenye simu mpaka awe anatamani kukupigia ili muongee.
Onana nae mzungumzie mahusiano yenu vizuri
Ikiwa hakupigii simu na hataki kuongea na wewe kwa namna yoyote ile kama mtu aliepandwa na hasira, basi hakikisha unamtafuta muonane ana kwa ana. Unaweza kumfuata mahari alipo na ukaongea nae kuhusu mahusiano yenu vizuri ili kujua nini tatizo. Kama utakua mbali nae, unaweza watumia ndungu au marafiki kumuuliza kuhusu tatizo linalomfanya asitake kuwasiliana na wewe.
La kumaliza ni kwamba, Kuna muda mtu anaweza kuwa hakupigii simu wala kupokea simu yako kwasababu ana matatizo yaliomkuta au yupo mazingira yasiomrusu. Hivyo uwe unafikilia upande huu pia kwa mwanamke au Mwanaume wako. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy.
Natumaini unafahamu kuwa kutuliza akili na kutuma ujumbe wa mapenzi kwa umpendaye inaweza kuonekana kama jambo la kitoto lakini ni muhimu sana kwenye mahusiano. Ujumbe wa maneno ya upendo unaweza kuwa na uzito mkubwa kuliko tunavyodhani. Na hii ndio maana mara nyingi The bestgalaxy tunakuandalia makala zinazohusu mambo yanayohusu ujumbe wa mapenzi.
Wanawake na wanaume, wote hufurahia sana wanapopokea ujumbe wa mapenzi, haijalishi wana umri gani. Hata watu wenye umri mkubwa wanapoona maneno machache ya upendo kutoka kwa watu au wapendwa wao, hufurahi na kuhisi kuthaminiwa.
Mtu unaweza mtumia umpendae Ujumbe wa aina hii hatakama tayari mupo kwenye ndoa. Kikubwa ujumbe huo uwe mzuri na umpate mke au mume wako kwenye wakati mzuri atakao furahia.
Katika ulimwengu wa sasa, ujumbe mfupi ndio mzuri kuliko Ujumbe mrefu sana. Ujumbe wa maneno machache ya upendo unatosha kufikisha hisia zako na kumfurahisha bila kuhitaji maneno mengi. Ni njia bora ya kuonyesha kuwa unamjali mtu bila kutumia muda mwingi. Lakini hii haina maana kuwa ujumbe mrefu hauna umuhimu, bado unaumuhimu mkubwa sana. Kama unapenda kumtumia mpenzi wako ujumbe au sms ndefu za upendo, basi isiwe kila muda au mara kwa mara.
Ujumbe wa mapenzi kwa umpendae
Nikikwambia “Nikinywa maji nakuona kwenye glasi” najua utanicheka na hautaniamini. Lakini hiyo sentensi huwa inaana “Nakuwaza kila wakati”. Na ni kweli na kuwaza kila wakati kwasababu nakupenda sana kipenzi.
Umenipa Raha ya ajabu. Umeniacha sina usemi kama bubu. Ladha sio Sukari, sio Asali na ni zaidi ya “Tamu”.
Yani muda huu nimetulia hapa, watu wanaweza sema nawaza hela. Kumbe nakuwaza wewe kipenzi cha Roho yangu. Vipi Hali yako we malaika?
Jinsi ninavyokupenda ni kama nilikuweka ndani ya moyo wangu alafu funguo za moyo nimepoteza. Siwezi ingiza tena mtu na huwezi toka bila maumivu mpenzi, UMENIWEZA!
Moyoni ni nakupenda, akilini naamini kuwa tunapendana. Mambo ni mengi sana ya kufanya tusiwe sawa. Ila unapo lala au kuamka, usisahau kuwa nakupenda sana.
Ukisema “Nakupenda” nahisi furaha sana moyoni. Ukiwa karibu, huwa staki uende mbali. Wewe ni kile chakula naweza shiba na nikaendelea kukitamani.
Wanasema “Mtu hauwezi kuiona raha ya Dunia bila kuwa na furaha”. Mimi nasema siwezi kuiona raha ya Dunia bila wewe. Kwasababu wewe ndie furaha yangu, nakupenda kuliko unavyo fikilia.
Nakushukuru kwa kila tabasamu, kila kumbatio, na kila neno zuri uliloniambia. Nakuona kama ni zawadi ambayo kila siku inanikumbusha thamani yangu. Nakupenda sana na naomba usije choka kunipenda.
Nahisi umenizamisha kwenye usingizi mzito sana. Najiona kama naota ndoto tamu na ndoto hii, ni kuwa na wewe kipenzi. Ikiwa kweli hii ni ndoto, basi iwe hivi milele maana nikiamshwa nitaumia.
Nikikwambia “Siwezi kuishi bila wewe” unaweza nicheka kwa kuhisi ni uongo. Lakini mimi nakwambia hivyo nikiwa na maana “Siwezi kuishi maisha ninayotaka bila wewe”. Mimi nataka niishi maisha ya kupendana na wewe milele. Sasa nitawezaje kuyaishi bila wewe?
Nikikukumbuka sana, moyo wangu hunipa masharti ya kutimiza ili nipate FURAHA. Sharti la kwanza ni kuwa karibu yako na ikishindikana, basi nikupigie simu nisikie sauti yako. Uwe unapokea simu sasa mpenzi, utaniua mwenzako.
Binadamu tumeumbiwa makosa mpenzi, huenda kunakitu nakosea maana mimi si malaika. Lakini kumbuka nina Moyo, mpenzi. Na huo moyo unamapenzi ya dhati na wewe.
Upendo wako ni amani katika Dunia iliojaa vurugu na kelele nyingi juu ya MAPENZI. Wakati watu wangine wanatafuta wapenzi wanaojua mapenzi, mimi nasherekea kukupata kipenzi changu.
Nakupenda sana mpenzi. Yani hata kama wewe ungekua ni Mti alafu mimi ni ndege nilietua kwenye Mti kwa bahati mbaya katika matembezi. Bado ninge hamia kwenye mti huo mazima maana unakila ninachotaka.
Ni jumbe hizo tu katika ukurasa huu ila kuna makala nyingi unaweza soma katika The bestgalaxy ili kupata sms au Jumbe nyingi zaidi za mapenzi. Endelea kuwa karibu na sisi na pia usisahau kufuatilia mambo mengine ikiwemo simulizi.
Mtandao umekuwa daraja linalounganisha watu kutoka pembe zote za dunia na kuzalisha uhusiano wa kirafiki au kimapenzi. Kupata mpenzi au rafiki kutoka nchi au bara tofauti, kunaweza kuwa ni jambo zuri sana linalowezeshwa na Teknolojia kwa sasa. Unaweza pata mtu Toka marekani, uingereza na sehemu nyingine ulimwengu kwa kutumia simu yako tu.
Pamoja na uzuri wa jambo hilo, kama ilivyo kwa mambo mengine, kuna pande mbili za kuzijua. Kuingia kwenye uhusiano wa mtandaoni kunaweza kuwa na faida nyingi kama vile kujenga urafiki wa kawaida, kujifunza lugha mpya, na hata kupata fursa za kusafiri au kazi. Lakini pia kuna changamoto na hatari zake. Uaminifu wa mtu unaekutana nae mtandaoni unaweza kuwa mgumu kujua upo vipi, na kuna visa vya watu wengi kudanganywa au kuibiwa pesa kwa kupitia uhusiano wa namna hii mtandaoni. Ni muhimu kuwa makini na kuchukua tahadhari kabla ya kuweka hisia zako kwenye mahusiano haya ya mitandaoni.
Kwa hiyo, kama unafikiria au kutamani kupata mpenzi au rafiki wa kizungu mtandaoni, unapaswa kuziangalia faida bila kusahau hasara zake pia. Mtandao unatoa fursa nzuri za kukutana na watu wapya, lakini vilevile, unahitaji kuwa makini ili kuepuka matatizo.
Katika makala hii, tutajadili njia rahisi ambazo watu hutumia kujenga uhusiano na wazungu wa kiume au wakike mtandaoni kwasasa.
Njia za kupata Mpenzi au Rafiki wa kizungu Mtandaoni
Tuvuti za Uchumba na Urafiki
Hii ndio njia kuu na maalumu kwa mahusiano ya namna hii. Kuna tuvuti ambazo zinawakutanisha watu wanaohitaji mahusiano na watu wengine. Tuvuti hizi tunakusanya watu toka pande mbalimbali za Dunia.
Unaweza zitumia tuvuti hizi kuanzisha mahusiano ya Urafiki au mapenzi hata kama akiwa mbali na nchi uliopo. Unaweza pata mzungu kupitia tuvuti hizi na akawa Rafiki yako au Mpenzi wako kabisa. Mfano wa tuvuti hizi ni Tinder. Tinder Ina app akabisa ambayo unaweza iingiza kwenye simu yako ili kuitumia kirahisi.
Magemu ya kucheza watu wengi mtandaoni
Kwasasa Kuna game nyingi zinakusanya watu toka nchi mbalimbali na wanacheza kwa pamoja mtandaoni(Hasa game za battle Royale). Sasa hizi game zinaweza kuwa chazo cha kukutana na watu toka nchi nyingine na kuanzisha uhusiano nao. Katika game ili upate Marafiki kirahisi inabindi uwe ni mtu unaejua kucheza game vizuri na unakua msaada kwao. Yani inabidi unacheza nao tofauti mpaka wasipo kuwa na wewe, wanakukumbuka.
Ukiwa hivyo kwenye game za mtandaoni, unaweza jizolea marafiki ikiwemo wazungu maana inaweza kifika kipindi wanakutafuta kwenye simu ucheze nao. Na hapa kuzijua lugha na kuwa mchangamfu kidogo ni kitu muhimu.
Ukiachana na magroup ambayo mtu unaweza jiunga kwa kubonyeza link katika mitandao, fahamu kuwa kuna magroup ya kulipia ambayo yanakusanya watu toka pande mbalimbali za Dunia. Magroup haya mara nyingi yanakua chini ya watu maalufu mitandaoni na huwa ni kwaajili ya elimu au mambo mengine muhimu. Mfano kwenye YouTube; kuna watu huwa wanaanzisha group hizi kwaajili ya kuwafundisha watu wao kwa ukaribu zaidi. Ukijiunga kwenye group hizi, utaona watu huwa watulivu sana humo ndani maana wamelipia kuwa humo. Mbali na kuwa watulivu, huwa wanakua wanajidili na kushilikiana kwenye mambo yaliowaleta humo.
Sasa katika kujadiliana na kushirikiana, unaweza jikuta umekua na marafiki wa nchi nyingine au kizungu ambao mnaongeo kuhusu maswala flani tu. Mahusiano ya mapenzi yanaweza kuanza hivyo pia lakini inaweza kuwa baada ya kuzoeana sana maana. Hii ni kama vile mtu unaenda shule kwaajili ya Kusoma lakini unajikita kwenye mahusiano na mwanafuzi mwenzako.
Unapohitaji kupata Mpenzi au Rafiki wa kizungu Mtandaoni, njia hizo ni njia mbazo tunaweza ziita rahisi kuzitumia. Na pia fahamu kuwa kupata mwanamke au Mwanaume wa kizungu inawezekana ila unatakiwa kuwa makini sana. Epuka kuwasumbua sana watu wa nchi nyingine maana huwezi jua wanauchukuliaje usumbufu wako. Jambo linaweza kuwa sawa kwako lakini lisichukuliwe sawa kwao.
Kuanza uhusiano mpya ni jambo zuri ambalo huambatana na furaha, lakini pia mwanzo wa mahusiano ni wakati kufahamiana vizuri. Tunafahamu kuna watu ambao huanza mahusiano wakati wameisha fahamina vizuri, lakini pia kuna watu wengine huanza kufahamina vizuri baada ya kuingia kwenye mahusiano(katika hatua za awali).
Katika hatua hizo za awali za mahusiano, mazungumzo yanakua na nafasi kubwa ya kujenga msingi wa mawasiliano bora. Watu huulizana maswali ambayo yatasaidia kufahamiana zaidi na kuelewa malengo, matamanio, na mawazo ya kila mmoja. Maswali yanaweza kuwa njia bora ya kuanzisha mazungumzo na kuchunguza ikiwa mnalingana kihisia, kiakili na hata kimaisha.
Kila mtu huwa na mambo yake tofauti anayotaka kujua kwa mpenzi mpya, lakini kuna mambo ya msingi ambayo kila mtu anapaswa kujua kuhusu mwenzi wake mpya ili kujenga mahusiano imara na hata kuepeka baadhi ya mambo mabaya. Mwanaume au mwanamke kujua tabia, malengo, na mtazamo wa mpenzi wake kunaweza kusaidia kuunda uhusiano imara zaidi na kuepuka mambo mabaya yanayoweza jitokeza mbeleni.
Mara nyingi, watu huingia kwenye mahusiano bila kuzungumza masuala muhimu mwanzoni na baadae hupata changamoto nyingi kwenye mahusiano yao. Kuuliza maswali mwanzoni kunaweza kufungua mambo mbalimbali juu ya mahusiano ulioyaanzisha.
Kati ya maswali muhumu sana kumuuliza mpenzi mpya kwa kipindi hiki ni yafuatayo hapa chini:
Maswali ya kumuuliza Mpenzi wako Mpya (mwanamke au mwanaume)
Una Mpenzi?
Baadhi ya watu huona kumuuliza mpenzi mpya “Una Mpenzi?” ni jambo baya lakini si kweli. Mara nyingine kuuliza swali hili, kunaweza kukufanya utambue uko kwenye mahusiano nae kama mtu pekee au Kuna mtu unamuibia mpenzi wake. Ni Bora ukauliza tu na hatakama atakwambia hana mpenzi wakati anae, hofu na wasi wasi vitakua kwake na sio kwako.
Na akikwambia anae mpenzi, basi unaweza kuwa makini huku ukipambana kuonesha upendo wako ili kumfanya asigeuke nyuma. Kama utashindwa, pia ni sawa kuheshimu maamuzi yake. Ila fahamu tu kuwa, kujua jambo hili litakufanya uepukane na migogoro ya mapenzi. Na pia hatakama ikitokea amekusaliti na kwenda kwa mpenzi wake, moyo wako utakua kuna jinsi upo vizuri kidogo maana ulikua unajua.
Ndoto yako kubwa katika maisha ni ipi?
Kuuliza kuhusu ndoto za mpenzi wako mpya, kutakufanya umfahamu kwenye upande wa maisha. Mara nyingi watu tunaishi tukikimbiza ndoto zetu na ni ngumu sana kumuelewa mtu anavyopambana kama haujui anakimbiza ndoto gani.
Swali hili linaweza kukufanya uelewe mpenzi anapambania nini maishani. Hii itafanya ukimuona anapambana, utakua unajua ni kitu gani anafanya na hata kumsaidia ikiwezekana. Kama ataongelea ndoto za kuwa na familia, basi huo ndio wakati mzuri wa kupanga mipango yenu ya kuwa pamoja.
Umewahi kupima HIV?
Swala la HIV (Virusi vya Ukimwi) ni jambo muhimu kama unajali afya yako na ya mpenzi wako. Kama hauna HIV, ni vema ukamuuliza mpenzi wako mpya kuhusu kupima HIV ili ujue hata analichukuliaje ilo swala. Mara nyingi huwa watu hawasemi ukweli lakini kitendo cha kumuuliza kutafanya hata akiwa na HIV awe makini au afikilie mara mbili anaposhiriki tendo na wewe. Kama wewe ndie una HIV, Bado kunaweza kuwa na umuhimu wa kuuliza maswala ya haya ili ikitokea bahati mbaya umempatia HIV, aelewe kuwa lengo lako ilikua ni kumuokoa asipate.
Umejifunza nini kutoka kwenye mahusiano yako ya zamani?
“Mahusiano ya zamani” yamefanya watu wawe na mitazamo mingi sana mibaya kuhusu Mapenzi. Yani, kuna watu mahusiano yao ya zamani yamewafunza kutopenda tena, kutomwamini mtu kwenye mapenzi, kuamini mapenzi ni pesa tu na hata kuamini kuwa wanatakiwa kuacha kabla hawajaachwa maana mapenzi ni maumivu tu.
Sasa swali hilo linaweza kukufanya uelewe mpenzi wako mpya anamtazamo gani kuhusu Mapenzi. Kama atakua na mtazamo mbaya, unaweza mfanya abadilishe mtazamo wake kwa kumuonesha upendo wako wa tofauti huku ukimwambia mapenzi hayapo jinsi anavyofikilia.
Wengi ukiwaonesha mapenzi ya kweli huwa sawa kabisa na hubadilisha mitazamo yako ikawa mizuri mpaka mwisho.
Lakini kuna mwingine baadae ataanza kuendeshwa na mitazamo yake mibaya juu ya mapenzi na mpaka ukashindwa kumweka sawa. Huyu utajua tu kuwa tatizo ni mahusiano yake ya zamani.
Vitu au mambo gani haupendi na nini unapenda?
Ni muhumu kumuuliza mpenzi wako mpya maswali ambayo yatakufanya ujue mambo au vitu gani anaependa. Ni vema kumuuliza vitu au mambo gani huwa hapendi. Katika upande wa “Kupenda”, Unaweza kumuuliza kuhusu chakula, sehemu anazopenda kutembelea, nyimbo anazopenda kusikiliza, filamu anazopenda kuangalia, mchezo anayopenda na mambo mengine. Katika upande wa “Kutopenda” unaweza muuliza mambo kama Tabia, vyakula na mambo mengine unayotamani kujua anayapenda au vipi.
Tukitimiza mwaka 1 wa kuwa pamoja tufanye nini kusheherekea penzi letu?
Swali hili limekaa kama ahadi ya utani hivi. Lakini mara nyingi huwa linafanya muwekeane ahadi ya kulituza penzi lenu jipya mpaka lifikie mwaka. Kama mnapendana kweli, basi mtasafiri kimawazo na kuyaona mahusiano yenu yakidumu zaidi ya mwaka pamoja hatakama sasaivi ni mapya.
Katika mwaka kunaweza kuwa na misukosuko mingi sana lakini wazo la kwamba umekubaliana kuafnya kitu flani baada ya mwaka, ilaweza wafanya mshikamane.
Hii ni njia nzuri sana ya kuweka matumiani ya kuwa pamoja. Watu wengi ambao hawajaoana huwekeana ahadi ya Ndoa, lakini ndoa inaweza chukua muda kutimia. Ila hii njia ya kufurahia kila mwaka inakua inawapa matumaini huku mukiendelea kusubiri siku ya ndoa. Mnaweza kuwa mnafurahia kwa kupeana zawadi au kwenda matembezi ya pamoja kwenye sehemu tofauti. Sio lazima utumie gharama sana au kuwashirikisha watu siku hiyo.
Maswali hayo tulioyazungumza hapo juu, ni mzuri sana kwa mwanamke na Wanaume pia. Hivyo, usisite kumuuliza mwenza wako mpya kama utapata nafasi inayomuhusu kuyauliza. Mbali na maswali hayo ukuna maswali mengine hapa chini ambayo hatujayapa maelezo ila unaweza muuliza mpenzi wako mpya.
Unapenda kufanya nini ukipumzika?
Mahusiano mazuri kwako yana maanisha nini?
Ni kitu gani kinaweza kukufurahisha hata ukiwa hauna furaha?
Kuna kitu chochote unatamani nifahamu kuhusu wewe mpenzi?
Hivi mpenzi, nikifungua moyo wako ndani yake unahisi nitaona nini?
Ni hayo tu katika ukurasa huu ulioletwa kwako na The bestgalaxy. Usiache kutembelea The bestgalaxy kila mara unapo pata nafasi ili kujifunza mambo mengi kuhusu mahusiano na Mengineyo. Usisahau pia kuchukua simulizi ya Mapenzi ya SUKARI YA DADA ambapo utapewa na simulizi nyingine kama zawadi.
Nilihamia kwenye nyumba moja nzuri nikiwa napambana na maisha. Nilipata chumba kizuri sana, cha kisasa, lakini bei ya kulipia ilikuwa ndogo mno. Jambo Hilo ndio lililonivutia na nilivutiwa zaidi na utulivu wa nyumba yenyewe na upatikanaji wa huduma pia. Wenye nyumba walikuwa ni mume na mke, wakikaa peke yao bila mtoto yeyote. Kwa miezi michache, niliishi pale kwa amani bila shida yoyote, tukiheshimiana na wenye nyumba.
Siku moja, mtoto wao wa kike, Doris, alirudi kutoka masomoni. Hakuwa akiishi nao hapo muda mrefu kwa sababu alikuwa akisoma chuo, lakini alikuwa kwenye likizo kipindi hicho. Kabla hajaja nilikuwa nimesikia wazazi wake wakimzungumzia mara kadhaa, lakini sikuzingatia sana.
Aliporudi, mara ya kwanza kumwona nilishtuka kidogo. Doris alikuwa anamwili mdogo kiasi alafu mzuri wa kuvutia. Nilijikuta nashindwa kutomwangalia kila tulipokua tukipishana hapo nyumbani. Siku za mwanzo tulikuwa tukisalimiana tu kwa kifupi sana alafu bila mazungumzo hasa pale wazazi wake walipokuwapo karibu. Kuna wakati tulikuwa tunapitana kama hatuonani kabisa, kila mmoja anakua na mambo yake.
Siku moja, nilikuwa sokoni nikinunua mahitaji yangu ya kila siku. Wakati narudi, mvua ndogo ilianza kunyesha taratibu, lakini haikuchukua muda mvua ikaanza kuongezeka. Niliona ni heri nikimbilie nyumbani kabla haijawa kubwa kabisa. Wakati nakimbia, nilimuona Doris mbele yangu akitembea taratibu, akiwa amejifunika na mwamvuli. Bila kufikiria sana, niliamua kumkimbilia ili nijiunge naye chini ya mwamvuli wake.
Aliniona nikimkaribia, akaniangalia kwa haraka kisha akaniwekea mwamvuli vizuri ili utukinge wote. Nikiwa hapo, niliamua kufungua mazungumzo nea kwa kusema “Bora ulikuja na mwamvuli! Ulijuaje kama mvua itanyesha?” huku tukitembea.
Alitabasamu kisha akasema, “Niliona mawingu yanakusanyika, nikaona ni bora nijipange mapema kwa kuja na mwamvuli.” Sauti yake ilikua ya kuvutia sana. Nilijikuta nikiendelea kuongea nae kwa kumwambia, “Dah asante kwa kuniokoa. Huenda hua unaongea na Mungu wewe.” Tulicheka pamoja, na mazungumzo yaliendelea kuwa mazuri sana. Safari ya kurudi nyumbani, ilionekana kama hitaisha haraka hivi… Na hatukutaka ifike mwisho. Doris alikuwa na harufu nzuri, na jinsi alivyoongea, nilivutiwa naye sana siku hiyo. Baada ya maongezi mazuri, alinionyesha kuwa anaweza kuwa rafiki na akanipa mpaka namba yake ya simu ili tuendelee kuchati kuwasiliana nae.
Tulipofika nyumbani, tulitengana kama hatukua wote. Kila mtu aliendelea na shughuli zake, lakini ndani yangu, moyo uliacha kuzingatia kazi yake ya kusukuma Damu, ukaanza kumpenda sana Doris.
Kwanzia siku hiyo, urafiki wetu uliendelea kukua. Nilianza kuwa mjanja, kila niliposikia wazazi wake wamemtuma sehemu fulani, nilihakikisha na mimi natoka kwa wakati huo ili tutoke pamoja. Hali ilifika mahali nilishindwa kuvumilia, nilimwambia kuwa na mpenda na nahitaji awe wangu.
Hakunisita hata kidogo, alikubali maana na yeye alikua ananipenda, na hapo uhusiano wetu wa siri ukaanza rasmi. Tuliendelea kuonana kisirisiri kila tulipopata nafasi. Tulikua tukitumia muda mwingi nje ya nyumbani ili kuepuka macho ya wazazi wake. Lakini kama unavyojua, hakuna siri inayodumu ikionwa na majirani. Majirani walianza kutusema, kwa wazazi wake Doris alafu wazazi walianza kututazama kwa macho ya mashaka. Walijaribu kutuchunguza lakini hawakuwa na ushahidi wa moja kwa moja, hivyo wakawa wanafikiria tu.
Siku moja, Mchana, Doris aliniambia usiku niache mlango wangu wazi, kuna jambo la kuniambia. Sikutaka kumuuliza sana, lakini nilihisi alitaka kufanya ninachokitamani kufanya nae lakini nakosa mbinu. Usiku ulipofika na watu wakiwa wamelala, nilihisi mlango wangu ukisukumwa, kisha nikaona anaingia Doris.
Basi utulipiga stori humo ndani kwa visauti flani ya chini chini mwisho tukaanza kutamani kushikana. Ndani ya muda mchache tukawa tayari tunaucheza mziki humo ndani. Huo mziki Doris alikua anataka sana na Kila nikibandika alikua analalamika lakini hataki nibandue. Doris alionekana kuwa na kiu ya kucheza na nami mziki mpaka ananivuta kwake. Niliendelea kufurahia kuwa naye huku nikiwa na hofu ya wazazi wake kujua. Nilikua najitahidi sana mziki usisikike nje usiku mpaka tukamaliza kucheza, akarudi kwao.
Hiyo ilikua ni siku ya Doris kutoroka kwao na kuja kwangu lakini hakuishia hapo, alikua akipata nafasi usiku anakuja kila mara.
Baada ya kuja mara kadhaa, wazazi wake walijua wazi kuwa kuna kitu kinachoendelea kati yetu. Walichukia sana na wakanipandishia bei ya chumba ghafla ili nihame. Walifikiri ningeshindwa kumudu kodi mpya na kuondoka, lakini mimi niliendelea kuishi pale…
Doris, kwa upande wake penzi lilimchanganya mpaka alifikia hatua ya kukataa kurudi chuo. Alianza kuwajibu wazazi wake vibaya kila walipomwonya kuhusu mimi na nilikua nasikia kabisa. Kila mara walipojaribu kunizungumzia vibaya, Doris alikuwa anatetea sana. Aliwahi hata kuwatishia kujiua kama watajaribu kututenganisha. Kwa kweli, nilianza kuwa na hofu kwa jinsi uhusiano wetu ulivyokuwa unazidi matarajio yangu. Mimi nilijua yatakuwa mahusiano ya kawaida tu alafu tutakuja kuachana baadae kama mahusiano yangu mengine ya huko nyuma.
Wakati hayo yote yakiendelea, siku moja Doris aliniambia kwamba ana ujauzito. Hapo ndipo moyo wangu ulianza kudunda kwa kasi sasa. Sikutarajia habari kama hizo kwa wakati ule alafu yeye alikua anataka azae kabisa. Nilihisi kama maisha yangu yakuwa yenye majukumu makubwa. Niliona kabisa kwenye maisha nitateleza na kuanguka na huyu Doris ni utelezi utakaoniangusha. Katika hayo Mawazo, wazo la kumkimbia lilinijia maana niliona ndio njia sahihi ya kujiokoa muda huo. Nilianza kupanga kimya kimya jinsi nitakavyohama na kuanza maisha mapya sehemu nyingine. Nikapata chumba mbali na hapo alafu nikaanza kuhamisha vitu kwa Siri Kila usiku unapoingia.
Baada ya kuhamisha baadhi ya vitu vyangu muhimu kwa siri, niliondoka ghafla bila kumwambia. Nilihamia mbali ila sio sana. Nilikua nikifikiria kwamba pengine nikiwa huko nitakua na nguvu ya kumkataa Doris na ujauzito wake alafu nitaanza upya maisha yangu. Lakini usiku huo huo wa kwanza baada ya kuhama, nilikosa usingizi. Nilijikuta nikiwaza sana kuhusu Doris na jinsi alivyokuwa tayari kufanya kila kitu kwa ajili ya upendo wetu. Moyoni mwangu nilihisi kama nilikuwa napanga kufanya kosa kubwa.
Nilikua nikikumbuka jinsi alivyokua anavimba kwa wazazi wake kwaajili yangu, jinsi alivyonipenda, alivyoacha upendo wake kwangu umuendeshe bila kujali chochote kiasi kwamba wazazi wake walifikiri nimemloga. Moyoni mwangu, nilihisi kumwacha Doris kwa sababu ya ujauzito ingekuwa dhambi kubwa sana. Maumivu ambayo niliona naenda kumpa nilihisi kabisa hata mungu awezi nisamehe. Hivyo niliamua kupuuza maamuzi yangu.
Usiku huo huo nilimwandikia ujumbe Doris atoroke kwao aje sehemu niliopo. Baada ya kuja nilimshawishi tuanzishe maisha yetu pamoja. Na kweli, Doris alikubali japo alikua anaogopa kidogo. Tulikio yafanya sio mzuri sana lakini ndio tulianzakuishi pamoja kama mke na mume, ingawa hatukuwa tumehalalisha uhusiano wetu.
Wakati tuliendelea na maisha yetu, wazazi wake walianza kuachana na chuki zao kwangu. Waliniona nikijitahidi na kumtunza binti yao mpaka wanakosa sababu ya kunichukia . Hatimaye walinipa baraka zao, na nikamfanya Doris kuwa mke wangu rasmi.
Sasa tunaishi kwa furaha kama familia. Maisha ya kuishi pamoja Kuna muda yakuwa ni magumu kama haujajipanga lakini namshukuru mke wangu Doris kwa kuwa na mimi mpaka sasa tunamaisha mazuri kidogo.
Watu wengi huamini katika mapenzi ya kweli, ambayo mpenzi anakukubali na kukupenda jinsi ulivyo, pamoja na mapungufu yako. Yani kila mmoja anakua anajua kuwa hakuna aliye mkamilifu. Na haya mapenzi ya kweli yanahitaji uvumilivu, heshima, na kujitolea kwa pande zote mbili. Huu ni Upendo hadimu sana na pindi unapopata aina hii ya upendo, unapaswa kuthamini na kuulinda kwa juhudi zote.
Ni kweli, hakuna uhusiano wa mapenzi unaoweza kuwa na watu wakamilifu wa asilimia mia moja maana sisi sote ni binadamu wenye makosa. Unaweza kufanya jambo baya au kuwa na tabia fulani bila kujua ambazo, zinamkera au kumuumiza mwanamke wako au mwanaume wako. Wakati mwingine, hata kama mpenzi anakupenda kwa dhati, mambo haya yanaweza kufikia hatua ya kumfanya ajisikie kutaka kujiondoa kwenye Mahusiano.
Katika makala hii, tutaangalia mambo machache ambayo yanaweza kumfanya mpenzi wako aachane na wewe, hata kama bado anakupenda. Ni muhimu kuelewa kuwa maneno, au maamuzi fulani yanaweza kuathiri mapenzi na kupelekea kuvunjika kwa uhusiano. Kufahamu haya kutakusaidia kuboresha au kauyaokoa mahusiano yako pindi yatakapokua kwasababu hizi.
Mpenzi anaekupenda anaweza kukuacha kwasababu hizi
Kutokujali kuhusu yeye au upendo wake
Awe ni mwanamke au mwanaume, usipoonesha kumjali, hatakama anakupenda anaweza kukuacha. Watu huonesha upendo lakini kama hautawajali wao na upendo wao, basi huondoka zao. Akiona anakutafuta, anakuzingatia na kukuoesha moyo wake unavyokupenda lakini wewe hauoneshi kuzingatia au kujali kwa chochote, kuna siku anaweza kuacha. Anaweza fanya hivyo hatakama moyo wake bado unakupenda. Ni vema kutambua kuwa kila wanaotuonesha upendo huwa wanahitaji kuzingatiwa pia. Mioyo ya watu wanao tukumbuka na kutupenda hujisikia vizuri tunapo onesha kujali pia.
Dharau
Kwa mwanamke, dharau zinaweza fanya uachwe hatakama una uzuri wa hali ya juu. Kwa wanaume, dharau zinaweza fanya wanawake wajitoe kwenye mahusiano pia. Dharau ina athari kwenye mambo mengi sana hapa Duniani na ndio maana watu wote wanasisitizwa kuwa na heshima.
Kuonesha dharau kwenye mahusiano ya mapenzi, kunaweza mfanya mwanamke au mwanaume wako asiuone thamani yake. Kila mtu anatamani kuwa sehemu ambayo anathaminiwa au kuheshimiwa na sio sehemu anayodharauriwa. Kwaiyo, itafika wakati anaweza jitoa kwenye mahusiano hatakama bado anakupenda.
Kukosa uaminifu
Kama jinsi ilivyo ngumu kufanya kazi au biashara na mtu asie muaminifu, ndivyo ilivyo kwenye mahusiano. Watu wengi hujiingiza kwenye mahusiano wakiwa na matumiani ya kupata mtu ambae watamuamini kumkabidhi Moyo. Na hakuna mtu ambae anatamani kumpenda kwa moyo wote mtu ambae haaminiki kwenye mahusiano.
Endapo utakua na tabia nyingi za kukosa uaminifu kwa mpenzi wako, unaweza mpoteza hata kama anakupenda. Watu huweka mioyo yao sehemu iliotulia na wanayoiamini. Ni vema sehemu hiyo ikawa ni wewe.
Muelekeo wa maisha
Ukiwa kama Mwanamke au mwanaume, kuna umri ukifika ni vema unawa tayari unaelewa maisha yako, unajua muelekeo wa maisha yako na sehemu unahitaji kukifika au mambo unataka kupata. Ukiwa unaishi bila kuujali muelekeo wa maisha yako au unaelekea pabaya, unaweza poteza mpenzi wako hatakama anakupenda sana.
Kuepuka hili, tengeneza vizuri Maisha yako, kuwa mtu unaewaza mambo mazuri na kujiwekea mipango mizuri kuhusu maisha yako. Ukifanya hivyo, mpenzi wako atajiona mwenye bahati kuwa na mwanaume au mwanamke anaejielewa kama wewe. Na hata tamani kukupoteza maishani.
Uchafu au kutojipenda
Ni ngumu mpenzi wako kukuambia “Acha uchafu” au “Haujipendi, upo hovyohovyo” lakini wengi wanapenda usiwe hivyo. Kuwa mchafu na Haujipendi ni mambo ambayo yanaweza fanya mpenzi wako kukuacha na kuvutiwa kuwafuata wengine anaoamini wapo tofauti.
Kuzuia hilo ni vema wewe mwenyewe ukawa msafi wa mwili na mambo yako yote unayofanya. Hakikisha unaweka mwili katika hali nzuri, ondoa harufu na kujipenda kwa kujiweka katika muonekano mzuri kila mara. Kuzoeana na mpenzi wako kusifanye usahau kuwa msafi na kujipenda ni muhumu.
Ni hayo tu muhimu katika makala hii na natumaini yanaweza kuwa msaada kwako ukiwa kama mpenzi, mke au mume wa mtu. Lakini kabla haujaondoka katika ukurasa hii, fahamu kuwa kutomlidhisha mpenzi wako katika tendo, inaweza sababisha kuachwa pia. Kwaiyo hakikisha upo vizuri upande huu pia. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy.
Kutafuta mpenzi au wachumba mtandaoni(Online) imekuwa njia maarufu sana katika Maisha ya sasa maana teknolojia imegusa hata kwenye upande huu pia na upande huu unaitwa “Online Dating”. Katika miaka ya hivi karibuni, kuna watu wengi ambao wamepata wake au waume wao wa maisha kupitia mitandao. Yani walianza uhusiano mtandaoni na wakafikia hatua ya kufunga ndoa kabisa.
Lakini pamoja na mafanikio yanayopatikana kwa baadhi ya watu, kuna changamoto nyingi zinazowakabili wale wanaotafuta wapenzi au wachumba mtandaoni. Watu wengi wanazama mtandaoni kutafuta wenza lakini wanajikuta katika mikono ya watu wabaya.
Si kila mtu unayekutana naye mtandaoni anakuwa na nia nzuri. Kuna wale ambao wanadanganya kuhusu utambulisho wao, huku wengine wakiwa na nia ya kujinufaisha tu. Hali hii inaweza kusababisha watu kuogopa kujihusisha na uhusiano wa mtandaoni kwa kuhofia kuvunjwa moyo au kudhulumiwa.
Mbali na changamoto za namna hiyo, Kuna watu ambao wanatamani kujua jinsi gani wanaweza fanya ili kutafuta au kupata Mpenzi mtandaoni lakini hawajui. Kutojua jambo hili vizuri, imekua ni changamoto kubwa kwao.
Hapa katika makala hii tunatoa mwanga juu ya mbo hilo ili kusaidia kila mtu kuelewa vizuri na kuanza kufurahia matunda ya Teknolojia Katika upande huu. Hii ni kwa Wanaume na Wanawake pia.
Namna ya kupata au kutafuta Mpenzi mtandaoni
Njia maalufu Duniani ya kupata au kutafuta wapenzi online ni mtandaoni wa Tinder. Tinder ni mtandao unaowakutanisha watu wanaotafuta wapenzi katika sehemu mbalimbali hapa ulimwenguni. Mtandao unamfanya mtumiaji awe karibu na watu wengine wanaotaka wapenzi uwaliopo karibu.
Kuna mitandao mingi sana hufanya hivi lakini Tinder ni mtandao maalufu sana katika ulimwengu wa kutafuta wapenzi. Tinder ina mamilioni ya watu wanao iamini na kuitumia.
Ukihitaji kutumia Tinder kirahisi, unaweza ipakua App ya Tinder kwenye simu yako kwanza. Baada ya kuiweka app ya Tinder kwenye simu yako, fuata maelezo yafuatayo;
Ifungue na uanze kujisajili.
Katika kujisajili utatakiwa kuandika taalifa zako ikiwemo jina, picha zako zaidi ya moja na Namba yako ya simu.
Akaunti ikikamilika, utakua na uwezo wa kuanza kuitumia app hii kuona watu wanahitaji wapenzi. Lakini kwenye simu, yako app itakuhitaji uwashe “Location” ili upate kirahisi watu waliokaribu na wewe.
Utakua unaziona picha za watu alafu una-Like kwa kubonyeza alama ya moyo kama utampenda mwenye picha hizo. Ikiwa na yeye ata-Like zako, mnaweza anza mazungumzo.
App ya Tinder
Jambo la muhimu kujua hapa ni kwamba App hii inaonekana kama kuitumia ni Bure hivi ila sio bure. Ili kuifurahia bila vikwazo, unatakiwa kulipia na unaweza lipia hata kwa wiki tu. Ukilipia unapata uhuru zaidi katika kutafuta mpenzi na kuchati na watu. Na katika kuitumia Bado umakini unahitajika maana unaweza kutana na watu wabaya wakakuingiza mjini.
Njia nyingine rahisi za Bure za kutafuta wapenzi Online
Mbali na mitandao kama Tinder, unaweza itumia mitandao ya kijamii hii tulioizoea. Facebook au WhatsApp inaweza kuwa katika ya mitandao unayaweza kutana na watu lakini pia unaweza jipatia mwenza kupitia kwenye magroup ya mahusiano au mijadala mbalimbali. Kama ni mtumiaji wa WhatsApp, unaweza fuata hatua zifuatazo kutafuta mpenzi mtandaoni kirahisi;
Fuatilia magroup ya WhatsApp yanayokusanya watu wa mtaani kwako, mkoa wako, kazini, kanisani au shule yako alafu ujiunge nayo.
Ukijiunga, kwenye group hizo utakua karibu na watu wanaoweza kukujua au vutiwa na wewe. Kuwa mtu unae chati ili watambue uwepo wako kwenye group.
Jaribu kujenga mahusiano na watu unaovutiwa nao kwenye group hizo alafu kuzeni uhusiano huo mpaka muanze kuchati inbox alafu muwe wapenzi.
Njia hii ni njia nyepesi sana ya kupata Mpenzi mtandaoni. Na naweza kusema ni njia salama zaidi maana unakutana wa watu halisi waliokaribu na wewe. Hata kama hauwajui vizuri, Bado ni ninja rahisi kwakua mnaweza kukutana kirahisi kutokana na ukaribu. Lakini endapo utajiunga kwenye group za watu wasiokaribu na wewe na hamjuani kabisa, inaweza kuwa rahisi kuibiwa au kutapeliwa.
Pamoja na changamoto nyingi, bado kuna nafasi ya kupata mapenzi ya kweli mtandaoni(kwenye internet). Kufanikiwa kunategemea jinsi unawasiliana, uvumilivu, na uwezo wa kuchunguza vizuri kuhusu mtu unaemuhitaji. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy.
Anisa alikuwa mwanamke mzuri, mwenye heshima na upendo kwa mume wake, Kevin. Ndoa yao ilikuwa changa, yenye matumaini makubwa na ndoto za baadaye. Hata hivyo, nyuma ya tabasamu zake za kila siku, Anisa alikuwa anabeba siri nzito.
Muda mrefu uliopita kabla ya kuolewa na Kevin, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na rafiki wa karibu sana wa mume wake aitwaye Marcus. Uhusiano huo ulivunjika kutokana Marcus kumuacha Anisa. Anisa alipoamua kuwa Kevin ndiye mwanaume wa maisha yake, Marcus alitambuliswa na Kelvin kuwa ameoa mwanamke aitwae “Anisa” na ndio atakua Shemeji yake. Marcus alikubari swala hilo na wala hakutaka kuuongelea uhusiano wake na Anisa kwa Kelvin. Lakini moyoni, Marcus hakuwa tayari kuachilia uhusiano wao wa zamani na Anisa. Alianza kumtafuta tena Anisa kwa njia za siri, akimtumia jumbe za kimapenzi kila mara, na kumfanya asiwe na amani.
Anisa hakutaka kumuumiza mume wake wala kuharibu urafiki wa Kevin na Marcus, hivyo aliamua kubeba mzigo huo kimya kimya. Kila wakati alipokea jumbe za Marcus, alifuta haraka, akijaribu kusahau na kuishi kama hakuna kilichokuwa kikiendelea. Lakini usumbufu huo ulianza kumkosesha amani na kumfanya kuwa na mawazo mengi.
Kevin aliona mabadiliko hayo kwa mke wake. Alianza kuhisi kuwa Anisa anaficha kitu. Tabasamu lake lilikuwa la bandia, na mara nyingi alikuwa kwenye mawazo. Moyo wa Kevin ulianza kumshuku mke wake. Alihisi kuwa huenda Anisa alikuwa anamficha jambo zito. Ili kupata ukweli, aliamua kuchunguza simu ya mke wake bila ridhaa yake.
Alishika simu ya Anisa wakati alipokuwa amelala, akafungua meseji. Ndani ya meseji hizo, aliona maneno ya kimapenzi kutoka kwa rafiki yake wa karibu, Marcus. Kevin alichanganyikiwa. Bila kujiuliza mara mbili, aliamini kuwa Anisa alikuwa amemsaliti kwakua na mahusiano ya mapenzi na rafiki yake wa karibu.
Hasira na huzuni zilimjaa Kevin na alimwambia mkewe kuhusu jambo alilolikuta kwenye simu yake. Hakutaka kusikiliza chochote maana mawazo ya kifo yalimwingia kichwani. Hakuwa na nguvu za kuongea na Anisa wala kwenda kukabiliana na rafiki yake. Bila kumkabili Anisa au kujaribu kuelewa zaidi, aliondoka nyumbani akiwa amejaa maumivu, akitembea kwa hasira barabarani.
Alifika kwenye barabara yenye magari mengi, moyo wake ukiwa umevunjika kabisa. Alitamani maumivu hayo yaishie haraka, na hakuhisi tena thamani ya kuendelea kuishi. Ghafla, gari lilikuja kwa kasi na kumgonga Kevin, likamrusha pembeni.
Anisa, akiwa ndani ya nyumba, alihisi kuna jambo baya lililokuwa limetokea. Aliposhindwa kumtafuta Kevin kwa simu, moyo wake ulijawa na hofu. Baada ya muda, alipokea simu kutoka hospitali: “Mume wako amepata ajali mbaya, anahitaji matibabu ya haraka.”
Anisa alikimbilia hospitali, machozi yakimtiririka, moyo wake ukiwa umejaa wasiwasi. Alipofika, aliambiwa kwamba Kevin alikuwa hajafa, lakini alikuwa katika hali mbaya sana, hawezi kuzungumza, wala kuutikisa mwili wake. Ajali ile ilimwacha na majeraha ya ndani yaliyoathiri uwezo wake wa kufanya mambo.
Anisa alilia kwa uchungu, akijilaumu kwa kilichotokea. Alijua tu kuwa Kevin alikuwa kwenye hali hiyo kwa sababu ya tukio la kuona Jumbe za Marcus kwenye simu yake. Alijaribu kumjulisha hayo Marcus kuhusu ajali hiyo na kile kilichosababisha Kevin apate ajali. Marcus, aligopa sana jambo hilo, aliamua kukimbia mji haraka, akiacha kila kitu alichokua akifanya. Hakutaka kukabiliana na matokeo ya vitendo vyake.
Siku zilibadilika kuwa wiki, na wiki zikawa miezi. Anisa hakukata tamaa. Aliendelea kumtunza Kevin, akihakikisha anapata huduma bora zaidi hospitalini. Kila siku, alikuwa pale akimshika mkono, akimuombea apone na kurudi kuwa yule mume aliyempenda. Ingawa Kevin hakuweza kusema wala kutikisa mwili wake, macho yake yalimuonyesha mazuri yote aliokua anafanya Anisa kwa wakati huo.
Baada ya miezi mitatu ya mapambano ya kiafya ya muda mrefu, Kevin alianza kuonyesha dalili za kupona. Polepole, alianza kupata nguvu za kuzungumza na kutikisa mwili wake tena. Aliona upendo ambao hakuutarajia kutoka kwa Anisa, aliyeendelea kumhudumia licha ya hali ngumu waliyopitia. Kila siku, Anisa alimwomba msamaha kwa kile kilichosababisha maumivu yote hayo, akimweleza ukweli kuhusu Marcus na jinsi alivyojaribu kutaka awe nae bila mafanikio.
Kevin, akiwa sasa na akili iliyotulia na moyo uliopata nafuu, alitafakari upendo wa Anisa na kujitolea kwake. Ingawa aliumizwa na yaliyotokea, aliweza kuona kuwa Anisa hakumsaliti ila alikuamejaribu kumlinda kwa Siri tu. Aliamua kumsamehe mke wake, akifahamu kuwa mapenzi yao yalikuwa na nguvu ya kustahimili dhoruba hiyo nzito.
Mwisho, walirudi nyumbani pamoja wakiwa na upendo zaidi ya sana. Waliahidi kutokuwa na siri tena, wakifahamu kwamba kusikilizana na uaminifu ndiyo msingi wa ndoa yao.
Umejifunza nini kupitia simulizi hii? Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy.