Tag Archives: Mahusiano

Kijana hizi ni athari za Wanawake wakubwa sana (Majimama/Mishangazi)




Wakati baadhi ya vijana Wakiume wanaongelea na hata kutafuta kabisa Majima au Mishangazi, hebu tunangalie athari zake. “Mishangazi” au “Majimama” ni majina ambayo kuna watu hutumia wakiwa na maana “Wanawake wakubwa wanaoingia kwenye mahusiano na vijana wadogo.” wanawake hawa wapo katika jamii zetu na kumekua na simulizi nyingi za vijana kujihusisha nao kimapenzi.

Mahusiano kati ya wanawake wakubwa na vijana yanaweza kuwa ni upendo toka moyoni kabisa. Yani wanaweza kuanza kwa mazoea ya kuwa karibu alafu mwisho, wakajikuta kwenye penzi zito. Ila kwakua wanasema, Mapenzi hayana umri, tunaweza sema ni jambo lisiloshangaza sana.

Lakini pia baadhi ya mahusiano ya namna hii huwa ni kama wanabadilishana pesa au maisha mzuri kwa mpenzi. Yani hapa Kijana wa kiume anawezakua anatoa mapenzi huku Mwanamke mkubwa akitoa pesa au maisha mzuri kwa Kijana. Kwaiyo Kuna namna Kijana wa kiume anaweza faidika hapa.

Pamoja na yote ambayo kijana wa kiume anaweza pata au kufaidika kwenye mahusiano ya namna hii, Bado sio Mahusiano salama. Kijana anaweza pata athari mbaya kubwa kwenye maisha yake anapokua na majimama au Mishangazi. Athari zinazo zungumziwa hapa ni zifuatazo:

Kijana hizi ni athari za Wanawake wakubwa sana (Majimama/Mishangazi)

Magonjwa



Kama tunavyo fahamu, magonjwa kama vile HIV huwa yanaweza ambukizwa kwa kushariki Ngono zembe. Ngono zembe ni kushiriki tendo la ndoa bila Kinga yoyote.

Kama upo kwenye mahusiano na mwanamke mkubwa, Tendo hili linaweza kuwa ni tendo la kawaida sana. Mnaweza zingatia kinga siku ya kwanza lakini ya pili mukazitupia mbali kwa kuamini haziwafurahishi kwenye tendo.

Sasa ikiwa mmeamua kutotumia Kinga Kuna hatari kubwa ya kuambukizana virusi ya ukimwi na magonjwa mengine.


Kuwachukulia poa wanawake wengine



Kijana wa kiume anapoingia kwenye mahusiano na mwanamke mkubwa anaweza jikuta anaanza kudharau mwanamke wa umri wake. Yani anaweza anza wachukulia poa sana mwanamke wa umri wake maana tayari anaoneshwa au kufanyiwa vitu vingi ambayo wanawake wengine hawafanyi.


Hali hii inaweza kumfanya huyo Kijana ajiamini sana anapokua na Mwanamke wengine. Lakini kujiamni huko ni matokeo ya kugundua kuwa mwanamke wengine hawajui mapenzi.

Kugeuka tegemezi


Kijana wa kiume akipata mwanamke mkubwa anaempa pesa kisa mapenzi, kuna hatari kubwa ya huyo Kijana kuwa tegemezi kwenye maisha yake. Anaweza fikia wakati hata akiachwa na jimama anaona maisha yake yameharibika.


Kwa kawaida mwanaume anatakiwa kubeba Majukumu, kujitegemea na kutegemewa. Huyo mwanaume akizoeshwa kutegemea mwanamke, inakua ni ngumu kwake kuchukua Majukumu, kujitegemea na kutegemewa tena. Huo kwake unakua ni mzigo mkubwa sana.

Kuingia kwenye migogoro



Baadhi ya wanawake wanaoitwa “Majimama” au “Mishangazi” ni wake za watu au Mama za watu. Kutokana na hili, pamoja na yote wanayofanya, Bado ni wanawake ambao wana ndungu na jamaa kwenye maisha yao.

Kijana anaweza ingia kwenye migogoro ya kifamilia bila kujua. Ukiwa kama kijana, unaweza kuwa chanzo cha mke na mume kukosana, unaweza chukiwa na watoto wake au ndungu. Mongogoro mingi inaweza kuibuka hapa.

MZIGO WA WAKUBWA 01  (Simulizi ya Kusoma)




Tulikua tupo mimi na rafiki yangu Samsoni kwenye chumba chetu tunacholala ambacho watu huita Geto. Ilikua mida ya kama saa moja au mbili usiku hivi alafu muda huo rafiki yangu alikua ananihadithia mechi ya mpira ambayo imetoka kumalizika saa 2 zilizo pita na sikwenda kuiangalia kwenye vibanda vya mpira siku hiyo kutokana na mawazo. Mawazo yalifanya kichwa changu kiwe vibaya sana muda huo kiasi kwamba nilikua naonekana kumsikiliza Samsoni lakini kiukweli nilikua hata simuelewi japo nilikua nacheka kila akicheka na kuitikia “Ebwana ee” ili asigundue kua akili yangu haipo kabisa kwenye anayonisimilia.

Katikati ya hadithi zake za mpira tukasikia simu imeanza kuita katika kisehemu tunachozichaji simu kilichokua pembeni kidogo ya dirisha la chumba hicho. Simu yangu na ya Rafiki yangu Samsoni, zote zilikua zipo chaji alafu simu yangu niliichomeka chaji ikiwa imezimwa. Hivyo simu iliokua ikiita muda huo ilikua ni ya rafiki yangu na tuliigeukia wote ilipokua inaita maana ilitushtua kwa kupiga kelele katikati ya maongezi. Baada ya hapo Samsoni  alinyanyuka huku akijisemesha “Sijui nani huyu… itakua watu wa mpira hawa” alafu akaenda kuichukua ile simu mimi nikiwa namuangalia tu. Alipoishika simu na kusoma jina, nilimsikia akasema “Ah wewe Mpenzi wako huyu ananipiga huku. Sijui umekifanya nini tena kitoto cha watu”

Mimi nikashtuka kidogo alafu nikamuuliza “Ni Sabrina?” Samsoni alijibu “Ndio” alafu akasema tena “Ngoja nipokee nimsikilize” huku akiipokea simu na kuiweka sikioni. Mimi muda huo nilitaka nimwambie asipoke ila alikua ameishapokea kabla hata sijanyanyua mdomo kumwambia. Baada ya Samsoni kupokea simu, nilimsikia akisema “Halo Dada… niambie” alafu nikasikia kisauti kidogo cha Sabrina akasema “mambo vipi?” Samsoni akaitikia “kama kawa, vipi huko?”  Sabrina akasema “safi. Mbona rafiki yako hapatikani kwenye simu? Upo nae hapo?”. Mimi kusikia hivyo nikashtuka, nikamwambia kwa ishara rafiki yangu Samsoni asiseme yupo na mimi.

Samsoni alinielewa akamjibu “Sipo nae. mimi niko mbali kidogo muda huu”. Sabrina alipoambiwa hivyo, akasema “Sawa, ukionana nae mwambie namtafuta” Samsoni akajibu “sawa” kisha simu ikakatwa. Baada ya hapo rafiki yangu alirudisha simu kwenye chaji huku akisema “Haya si umesikia? Eti anakutafuta. Sauti yake tu inaonekana mmezinguana nyie. Huu ugomvi siingilii” mimi nikacheka kwanza kidogo alafu nikasema “nitamcheki baadae”.

Baada ya hapo Samsoni aliniaga kuwa anatoka kidogo hivyo mimi nilibaki mule ndani nikiwa nimetulia tu ila kichwani kwangu mawazo ni mengi sana. Wakati akiondoka alisema pia “Alafu nilipokua anaangalia mpira, Tino alinipigia akaniambia amekutafuta hakupati hivyo umpigie” mimi nikaitikia “Ah sawa”.

Nilipokua pekeangu mule ndani, Mawazo yalinituma ninyanyue godolo tunalolatila maana Samsoni alikua anatabia ya kuweka pesa huko. Nilipofanya hivyo, nilizikuata pesa zake nyingi kiasi na nikazichukua maana niliona kama zinaweza nisaidia katika hali niliokuanayo kwenye wakati huo. Nilikua ni kama na muibia Rafiki yangu kabisa ili tu niweze kukimbia tatizo linalonipa Mawazo.


Mawazo niliokuanayo siku hiyo yalikua yamesababishwa na matokeo ya mimi kuanza kuzifungua kurasa za mapenzi katika maisha yangu. Nakumbuka miaka michache iliopita kambla ya siku hiyo nilikua nasoma sekondari kidato cha tatu na nilikua nasoma shule za kutokea nyumbani. 

Tangu nilipoanza sekondari nilikua sijawahi jihusisha au kuwaza kuwa na mpenzi shuleni japo nilikua natamani. Hii ilikua ni kutokana na mambo mengi ikiwemo sheria za shule zilizokua zikikumbushwa kila siku na walimu. Na pia nilikua nawaogopa wazazi wangu kuniona nimejiingiza kwenye maswala ya mapenzi. Mbali na hayo, nilikua naogopa sana jinsia tofauti. Kuwasogelea na kuongea nao kulikua ni mthihani mkubwa sana kwangu kipindi hicho, hasa akiwa ananivutia.

Kwenye mambo ya kufanya vizuri shuleni kwa bahati mbaya nilikua siko sana huko. Uwezo wangu katika madaftari na mithihani ulikua wa kawaida sana. Nakumbuka darasani nilikua nakaa viti vya nyuma sana. Huko nyuma nilikua nakaa na rafiki zangu wawili ambao mmoja wapo ndio huyo  anaitwa Samsoni, alafu kuna mwingine alikua anaitwa Tino. Kwaiyo tulikua kama tuna kikundi cha watu watatu nyuma ya Darasa. Darasa letu lilikua lina viti vinavyo ruhusu kukaa wawili na kiti nilichokua na kaa mimi, tulikua tunakaa mimi na Samsoni ila mwalimu akitoka tu, Tino alikua anakuja kwenye kiti kile, tunajibana watatu, tunapiga stori. Tino alikua anakaa kiti cha pembeni yetu ambacho kilikua karibu sana na sisi.

Tino alikua ni mwenzetu ila mambo yake yalikua mengi mno. Alikua ni msumbufu sana kiasi kwamba kila mtu alikua anamjua kwa usumbufu wake hapo shuleni. Watu walianza kumjua baada ya kuletwa na mzazi wake shuleni na kupigwa kutokana na kutolala kwao pamoja na kutokuja shule kwa siku 5 mfululizo katika kidato cha kwanza.

Tulikua tuna shirikiana sana Tino lakini usumbufu wangu haukufikia usumbufu wa Tino. Samsoni nae  alikua kama mimi tu, hakumfikia usumbufu Tino hata kidogo. Ila katika mambo ya kwenye vitabu, wote tulikua hatufanyi vizuri sana japo hatui wamwisho Darasani. 

Kuna siku asubuhi tulikua watatu Darasani kule nyuma ya Darasa tunapiga stori kwa kujiachia lakini ghafla akaingia mwalimu. Alivyoingia tu, tukafunga midomo alafu kila mtu kati yetu alikaa vizuri anapokaaga kisha watu wote darasani tukasimama kumsalimia Mwalimu. Baada ya kumsalimia, akaturuhusu tukae alafu nikakuta tu anasema “Nyie watatu uko nyuma hebu simameni”. Mh alivyosema hivyo nikawa nawaza “Anaongelea mimi na rafiki zangu au? Mbona anaangalia huku nyuma?” wakati najiuliza nikakuta mwalimu anasema tena “Nyie muliokua mnapiga kelele mpaka darasa zima mnasikika nyie huko nyuma simameni kabla sijawafuata.” Basi mimi nikaona huenda anatuongelea sisi, nikasimama na bada ya mimi kusimama, nikakuta na Rafiki zangu wawili wanasimama.


Baada ya hapo mwalimu akaanza kufoka “Hivi nyie mna matatizo gani? Inamana hapa shuleni mmekuja kupiga makelele au?” baada ya kusema hayo akaninyoshea mkono na kusema “Wewe hapo wewe inaonekana msumbufu maana hata Nywele haujanyoa. Hizo nywele ni siku ya ngapi nakwambia sitaki kuziona? Hebu sogea hapa mbele” mimi nikiwa mnyonge sana nilisogea taratibu pale mbele ya Darasa. Mwalimu aliniuliza “Unataka ni kupige ndio uanze unijibu?” mimi nikiwa naogopa sana nikamjibu “Hapana, samahani mwalimu nilitaka kunyoa jana ila umeme walikata”. Baada ya kumjibu mwalimu alifikilia alafu akasema “Kesho nisione hizo nywele, sawa!?” nikamjibu “Sawa” alafu nikakuta ananiambia “Na kule nyuma unakokaa, uhame. Kabebe madaftari yako kule nyuma uyalete hapa mbele kwenye hiki kiti ambacho hakina mtu”.

Baada ya mwalimu kusema hivyo nilishtuka maana nilikua sijazoea kukaa viti vya mbele ya Darasa, nikamwambia “Mwalimu hapo wanakaa watu wawili, itakua wameitwa nje”. Mwalimu akasema “Hatakama wakija hao wanao kaa hapa, waambie mimi ndio nimekuweka hapa. Kwanzia leo utakua unakaa hapa mbele. Nawakija hao, waambie wachukue kiti kingine wakae sehemu nyingine ila sio hapa”. Dah nilikua mnyonge sana siku hiyo, nikachukua vitu vyangu nyuma ya Darasa na kuhamia mbele ya darasa huku mwalimu akiniangalia.


Baada ya kukaa mbele mwalimu alianza kufundisha somo lake maana ndio ulikua muda wake huo. Mimi pele mbele nilikua sina amani kabisa maana sijazoea kukaa hapo alafu mbali na hilo, Daftari la mwalimu huyo nilikua sina. Lakini mwalimu alipoanza kufundisha nilichukua kidaftari flani cha ajabu, nikakiweka pale mbele ili kuzuga.

Nakumbuka baada ya kama dakika 10 hivi Mwalimu alipoanza kufundisha, alikuja mwalimu Mkuu akiwa ameambatana na wanafunzi kama watano hivi na mwanafunzi wa kike alikua mmoja. Darasa zima tulijikuta tunavutiwa kumuangalia yule mwanafuzi wa kike. Mwalimu mkuu alianza mazungumzo na Mwalimu aliekua Darasani na mazungumzo yao yalikua ni kwamba hao wanafunzi watano ni wageni na kwanzia siku hiyo watakua wanasoma humo Darasani. Walimu walipomaliza kuzungumza, wale wanafunzi wakaingia ndani ya Darasa alafu yule Mwalimu aliekua Darasani akawaambia watafute nafasi za kukaa mule Darasani. Kabla hata hawajapiga hatua sana, nikakuta mwalimu ghafla anamwambia yule mwanafuzi mgeni wa kike “Wewe usiende huko. Kaa hapa na huyu”. Mimi moyo ulishtuka sana maana alikua anamuelekeza yule Mwanafunzi wa kike akae na mimi kwenye kiti kimoja. Kiukweli mimi nilikua naogopa kukaa na jinsia tofauti hasa wakiwa wazuri ndio napoteza uhuru kabisa yani. Na Mwalimu alikua anamzingatia yule mwanafuzi wa kike kwa kiasi flani, kama ni ndugu yake hivi.

Nakumbuka yule mwanafunzi alikaa na mimi pele huku akiwa na viaibu aibu vya ugeni alafu na mimi wakati huo nina viaibu vya kumuogopa.  Tukiwa tumekaa  pale mwalimu aliwauliza jina wageni wote waliokuja na nilisikia yule Mwanafunzi wa kike akijitambulisha kuwa anaitwa Zuwena.  Basi baada ya hapo mwalimu aliendelea kufundisha na mimi nikawa kama namsikiliza  hivi ingawa akili yangu ilikua inahama. Yani nikua nikitupa jicho langu mara moja moja kwa yule Mwanafuzi wa kike kumuangalia jinsi alivyo. Japo nilikua naogopa, ila alikua anavutia sana kumuangali alafu alikua msafi sana. Kuna muda nilimtupia macho tukagongananae alafu akaona viaibu. Mimi nilipogongananae macho nilishtuka na nikaingiwa na woga zaidi ila woga ulipungua nipowaza “ Inamaana na yeye ananiogopa huyu. Dah ila mzuri mpaka raha. Ingawa naogopa ila hapa nijitahidi niwe hata rafiki yake tu. Sina hata rafiki wakike ujue”. Nakumbuka niliwaza mambo mengi sana kuhusu huyo mgeni bila kujua kuwa ndio namuingiza moyoni hivyo mtoto wa watu.

Baadae, mwisho wa kipindi cha mwalimu aliekua akifundisha ulifika na mwalimu alituachia maswali ya kufanya nyumbani tuyaandike alafu akasema anaondoka. Lakini kabla hajaondoka akasema “Nyie muliofika leo hakikisheni munaazima madaftari Kwa wenyeji ili muandike vitu vyote vya nyuma. Wewe Zuwena utachukua Daftari kwa huyo uliekaanae hapo, sawa!?”. Nikiwa pembeni ya Zuwena nikamsikia Zuwena akiitikia “Sawa” huku nikiwa nimeshtuka mno maana Daftari wanalo liongelea sina. Kichwani nikaanza kuwaza “Hapa mbona kama naenda kuumbuka kwa mgeni sasa. Huyu mwalimu na huyu mgeni wanajua Daftari ni hili lililopo Mezani lakini ukweli ni kwamba sina Daftari. Nikijieleza kwa huyu mgeni kuwa sina daftari, nitaonekana mjinga sana kwake na naweza shindwa kuwa rafiki yake. Dah tena anaonekana anaakili sana huyu, ntaumbuka leo.”



INAENDELEA…

Ujumbe mzuri kwa Mke au Mume aliye mbali na wewe

Katika maisha ya ndoa, kuna nyakati ambazo wanandoa wanalazimika kuwa mbali kwa sababu mbalimbali kama vile kazi, masomo, au majukumu mengine ya maisha. Ingawa umbali unaweza kuwa changamoto, ni muhimu kuendelea kudumisha mawasiliano na kuonyesha upendo na kujaliana hata mkiwa mbali. Kwa bahati nzuri, ujumbe wa maandishi ni njia rahisi na ya haraka ya kufikisha hisia kwa mke au Mume, huku ukimpa moyo na kumhakikishia kuwa yupo akilini kila wakati.

The Bestgalaxy, katika makala hii tumekusudia kutoa mifano ya ujumbe mzuri kwa mke au mume aliye mbali. Ujumbe huu unaweza kumtia moyo, kumfariji, au hata kumpongeza kwa kukuweka moyoni, bila kujali umbali uliowatenganisha. Maandishi haya madogo lakini yenye maana kubwa yanaweza kuimarisha uhusiano wenu na kumfanya mwenzako ajisikie kupendwa na kuthaminiwa hata akiwa maili nyingi kutoka kwako.

Mambo ya kuzingatia katika kuwasiliana na mpenzi aliye mbali BONYEZA HAPA>>>

Ujumbe mzuri kwa Mke au Mume aliye mbali na wewe

  • Tupo mbali ila unavyonionesha upendo ni kama nipo karibu na wewe. Nakupenda na sitoacha kukupenda maana nililiandika Jina lako kwenye moyo wangu kwa wino usiofutika milele.


  • Kwenye familia yangu wewe ni malkia, mama watoto wangu na ndio familia yangu kiufupi. Kila nikikumbuka unavyonipenda, kunipa furaha, kunisaidia na kusimama nami, najiona nimekupata kama bahati. Ni maisha tu yananiweka mbali nawe ila nakupenda na natamani nirudi.

  • Nipo mbali kwasasa ila tambua Moyo na Mawazo yangu vipo kwako. Kila siku yangu ya huku haiwezi kuwa sawa bila kajua hali yako. Nakupenda sana na nakuahaidi kutunza penzi letu mpaka tutakapo onana.


  • Wanasema “Umbali si kitu kwenye mapenzi ya kweli”. Umenifanya niamini hivyo kwasababu haujapunguza penzi lako kwangu. Umekua na mimi kwa simu kila moyo unapohitaji, tumekua wanandoa ambayo ni marafiki kwenye kila hali. Nakupenda sana na asante kwa kuwa nami.
  • Huwa nakuona kwenye ndoto zangu. Na hata nikifumbwa macho kwenye maisha siku hizi sioni giza, nakuona wewe mwanga wangu. Asante kwa kuwa rafiki na mshauri na mzuri kwangu. Usijesahau kuwa nipo mbali ila nakupenda sana.

  • Ni wanawake wengi huitaji mahusiano ila wachache hukubali kuwa Mama. Asante kwa kukubari kuwa mama watoto wangu. Pia ni wanawake wechache huvumilia mume anapokua mbali lakini wewe unafanya hivyo. Asante kwa kuniheshimisha na sichoke kuniheshimisha. Nakupenda sana mke wangu.


  • Mungu akulinde huko uliko mume wangu. Unapambana sana juu ya maisha yetu. Naweza kuwa sipo vizuri katika kukushukuru kwa kila jambo ila tambua nakupenda na kukuombea kwenye kila unalofanya. Nakupenda sana mme wangu.

  • Nakukumbuka kila mara Mme wangu. Siku ya kuonana na wewe naiona kama ipo mbali sana ila kamwe siwezi punguza upendo wako. Naomba kwa mungu nafasi zetu ziwe pamoja milele, na akusaide kwenye kila jambo lako kipenzi.

Unapomtumia ujumbe mzuri mke au mume wako aliye mbali unamkumbusha kuwa unampenda, unamjali na haujamsahau. Kwaiyo jambo hili ni muhimu sana katika Mahusiano.

Zingatia haya ili usichokwe na Mpenzi wako

Kuchokwa na mpenzi wako ni mojawapo ya changamoto kubwa ambazo watu wengi hukutana nazo katika mahusiano ya kimapenzi. Wakati mwingine, bila hata kugundua nini sababu ya kuchokwa, mtu anajikuta tu amechokwa. Hili si jambo la kushangaza, kwani mahusiano yanahitaji juhudi, uelewa, na ubunifu ili yaendelee kuwa yenye afya nzuri kwa pande zote mbili(Upande wa Mwanamke na Mwanaume).

Ni kawaida kwa watu kupuuza umuhimu wa mambo madogo yanayochangia uimara wa mahusiano alafu mahusiano yanayumba. Muda mwengine, mambo hayo tukiyafanya kwa kuzidi, yanafanya watu wachokwe kwenye mahusiano.
Kwa bahati nzuri, kuna mambo muhimu ya kuzingatia ili kufanya usichokwe kirahisi kwenye mahusiano. Baadhi ya mambo hayo ni yafuatayo;

Ujumbe wa mapenzi kwa umpendae BONYEZA HAPA>>>

Mambo ya kuzingatia ili usichokwe na mpenzi wako

Kuwa chanzo cha furaha na Amani kwake

Hapa Duniani tukiwa binadamu huwa tunapenda sana kuwa kwenye nyakati za Amani na furaha. Mara nyingi huwa tunapenda na kuwakumbuka sana watu wanaotupa Amani na furaha maishani. Na ni ngumu sana kumchoka mtu anaekupa furaha na Amani maishani, hivyo kuwa mtu huyo kwake. Kuwa mtu ambae anajua kabisa akiwa na wewe anapata amani na furaha.
Hakikisha kunamuda ukiwa nae unaweka lawama, kesi na matatizo pembeni alafu mnafanya mazungumzo ya furaha na Amani.

Mfanye akukose kwa muda flani (Akumiss)


Ni sawa kwa na mpenzi wako pamoja kwa muda mrefu lakini isiwe ni kila mara. Kuna muda inabidi ujiweke mbali nae kidogo ili akukumbuke na kujua umuhimu wako. Wataalam huwa wanasema kitu ambacho huonekana au kupatikana kirahisi hupunguza thamani. Na kwenye mahusiano hii inawezatokea pia.

Kuna muda jiweke busy na mambo yako, usipatikane kirahisi mpaka akutafute. Hii isiwe ni ugomvi, fanya kama kumkumbusha umuhimu wako kidogo kwa kuwa mbali nae alafu jirudi tena kwake kama kawaida. Kwa lugha nyingine tunaweza sema mfanye “Akumiss” kidogo kwa muda alafu kuwa nae karibu tena. Ukiwa unafanya hivi inaweza kuwa ngumu kwa mpenzi wako kukuchoka.

Kuwa na tabia ya kumfanyia asivyotarajia

Kama upo kwenye mahusiano alafu mambo yote unayomfanyia mpenzi wako ni yanayojirudia au yamezoeleka, basi kuna siku unaweza chokwa.
Ni vema ukawa na tabia ya kufanya baadhi ya vitu bila yeye kutarajia.

Usitabilike kwenye baadhi ya mambo katika Tendo au katika Maisha ya kuishi nae kawaida.

Kutengeneza nae mambo yajayo(future)

Mahusiano ya mapenzi bila future, yanawezekana ila huwa yanafika sehemu mnachokana. Yani kama ni Tendo tu ndio huwakutanisha pamoja na mpenzi wako, basi tambua tu kuna siku unaweza chokwa au wewe mwenyewe ukamchoka mwenzako.


Mahusiano ya mapenzi ni pamoja na kuwa pamoja au kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kimaisha. Na ili usichokwe, ni vema ukawa na tabia ya kupanga mambo mtayofanya pamoja mbali na tendo. Mfano, naweza panga na mpenzi wako kwenda kwenye sharehe pamoja, kuishi nyumba moja, kununua kitu flani pamoja na hata kukutana tu mupige stori.

Ukizingatia hayo yote, unaweza fanya iwe kungumu kwa mpenzi wako mwanamke au mwanaume kukuchoka. Anaweza kuwa anatamani kila siku uzidi kwa nae kwenye maisha yake.

SMS za kumiss Mpenzi wako (Mwanamke au Mwanaume)

Katika maisha ya mahusiano ya kimapenzi, kuna nyakati ambapo hisia za kumkumbuka mpenzi wako zinakuwa nyingi sana. Hali hii hutokea pale mnapokuwa mbali au hata wakati mnakuwa karibu lakini shughuli za kila siku zinawazuia kuwa pamoja. Kumkosa mtu unayempenda kwa muda ni huleta hali ngumu sana hata mnapokua na mapenzi ya dhati. Lakini ni jambo zuri ni kwamba, kuieleza hali hiyo kwa mpenzi wako hufanya ajue umuhimu wake kwako na hata kukupenda zaidi. Yani unaweza kumtumia hata ujumbe wa sms mzuri wa kumueleza jinsi gani umemiss na akafurahi na kujua unamuhitaji.

Mfano; Ujumbe mdogo wa “Nimekukumbuka mpenzi wangu, natamani niwe karibu na wewe” unaweza kubeba uzito wa hisia zako zote na kuonyesha jinsi gani unamuhitaji mpenzi wako. Wakati mwingine, huenda mpenzi wako anajihisi mpweke au hana uhakika wa hisia zako ila akiwa anapata ujumbe wako wa kummiss, anaweza kuwa ni faraja anayoihitaji. Ni jambo dogo kulifanya lakini lenye nguvu ya kuimarisha uhusiano na kuonyesha kwamba unamjali.

Mambo yasiofaa kuwambia marafiki kuhusu Mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

Katika makala hii, tumekusanya orodha ya SMS bora ambazo unaweza kumtumia mpenzi wako kumjulisha jinsi unavyomkumbuka. Unaweza zitumia bura kuleta furaha kwenye mahusiano wako.

SMS za kumiss mpenzi wako

  • Nipo hapa nimetulia ila kila nikifikilia jinsi nafurahia nikiwa karibu yako, natamani nikufuate ulipo. Nakumiss sana mpenzi, natamani niwepo ulipo.
  • We ni ile tamu waliosema “haionjwi” kwasababu mtu akionja hunogewa. Tangu nilipo onja ukaribu wako, nautamani kila mara. Nakumiss sana.
  • Upo mbali mpenzi wangu, lakini moyo haujawahi punguza upendo wako. Bado nahitaji wewe uwe wangu, na Bado nahitaji niendelee kuwa wako.
  • Unauzuri wa kushangaza kama nyota angani. Nikiangalia nyota na vitu vingine vyenye uzuri wa kushangaza, huwa nakukumbuka sana wewe.
  • Kuna muda unaweza waza eti nitakuacha na maumivu niende mbali. Huko mbali nafika vipi bila wewe? Moyo unakuhitaji kila dakika. Hata sasa nimekumiss nakuwaza wewe…
  • Nakupenda sana. Tafadhali njoo unijaze furaha ya uwepo wako Kipenzi. Moyo wangu umemiss zile hisia za kuwa karibu yako.
  • Huku Moyo uliokupenda unanisumbua kuhusu wewe. Umekukumbuka sana mpenzi wangu, natamani uje useme nao kwa ukaribu. Umechoka, uhitaji kukuona wewe Tabibu.
  • Njoo niyaone yale macho yako mazuri Mpenzi. Njoo unilishe kile chakula mimi hupenda. Nimekumiss mpaka onaona giza, siioni furaha bila ya wewe ninaekupenda.
  • Kile na hitaji nikiwa na huzuni, ni wewe. Na hata kile nile nahitaji nikiwa na furaha, ni wewe. Kiufupi, maisha yangu nayaona ni mzuri nikiwa na wewe. Nimekumiss mpenzi wangu.
  • Nakupenda na ninakutaka karibu nami zaidi ya kitu chochote ulimwenguni. Nakuhitaji zaidi ya chupa ya maji jangwani. Uko wapi mpenzi?

Sms hizi za kumiss ni nzuri kwa walio kwenye ndoa (Mume au mke) na hata kwa wasio kwenye ndoa (Wapenzi). Kikubwa unatakiwa kuchagua sms au ujumbe unapenda na hali yenu. Na pia ni muhimu kujua ni wakati gani wa kumtumia sms huyo umpendae.

Movie gani ni nzuri kuiangalia ukiwa na Mpenzi wako?

Katika vitu hufurahisha zaidi, kutazama filamu/movie nzuri ukiwa na mpenzi ni moja wapo. Unakua ni wakati mzuri wa kujenga uhusiano wenu kwa pamoja huku mkifurahia hadithi zinazovutia na kugusa nyoyo. Kuangalia movie pamoja kunawapa wapenzi nafasi ya kufurahia na kutathimini mahusiano au maisha kutokana na wahusika wa movie na kujifunza mengi kupitia wahusika hao.

Movie nzuri za kutazama na mpenzi wako hazihitajika kuwa na hadithi za kuvutia. Lakini pia zinapaswa kuwa zinakugusa hisia na zenye maudhui ambayo yanawaweka nyinyi wawili kwenye safari nzuri ya mahusiano. Unapo chagua movie za kuangalia pamoja unatakiwa kuwa makini sana kwa sasa maana sio kila movie unapaswa kuangalia mukiwa pamoja. Mnachokiangalia pamoja ni vema kikawa kinaziweka hisia zenu pamoja, kuwajenga kwenye mahusiano na kuwaburudisha.

Katika makala hii, tunaangalia orodha ya filamu/ movie ambazo ni bora kutazama ukiwa na mpenzi wako Mwanamke au Mwanaume. Movie hizi zitaamsha hisia, kuleta furaha, na kufanya mufurahie muda wenu wa pamoja.

Unaweza angalia movie itakayo kifaa zaidi alafu akaitafuta, kuiangalia kwenye platform mbalimbali za movie mtandaoni.

Jinsi ya kuangalia movie Bure mtandaoni BONYEZA HAPA>>>

Movie nzuri kutizama ukiwa na mpenzi

  1. Rapunzel (Katuni/Animation)

Hii ni movie/filamu ya Tangled (2010) ya Disney. Ni hadithi ya kifalme inayomuhusu muhusika Rapunzel mwenye nywele ndefu za kichawi, anayetoka kwenye mnara wake kwa msaada wa mwizi aitwaye Flynn Rider. Ni mchanganyiko wa vichekesho, mapenzi, na adventure.

  1. Titanic

Titanic (1997), iliyoongozwa na James Cameron, ni filamu ya mapenzi na drama ya kihistoria. Inahusu kuzama kwa meli ya Titanic mwaka 1912. Wanaigiza Leonardo DiCaprio (Jack) na Kate Winslet (Rose), kama wapenzi kutoka tabaka tofauti wanaokutana na kupendana kwenye meli hiyo.

  1. No Hard Feelings

Filamu hii ya vichekesho ya mwaka 2023 inamshirikisha Jennifer Lawrence. Inahusu Maddie, mwanamke anayekodiwa na wazazi matajiri kumfundisha kijana wao mwenye aibu (Percy) jinsi ya kuwa na ujasiri kabla ya kuanza chuo. Ni mchanganyiko wa vichekesho, mapenzi na mafunzo ya maisha.

  1. Subservience

Filamu hii ya kisayansi (sci-fi thriller) inahusu madhara ya teknolojia ya AI (akili bandia). Nyota wake ni Megan Fox na Michele Morrone. Hadithi inazungumzia AI ya nyumbani inayogeuka na kusababisha matatizo makubwa.

  1. What the Peeper Saw

Filamu hii pia inajulikana kama Night Child (1972). Ni thriller ya kisaikolojia kuhusu mvulana anayetuhumiwa kuhusika na kifo cha mama yake na uhusiano wake wa ajabu na mama wa kambo. Ni hadithi ya hofu na hila za akili.

Mbali na movie hizi, Kuna movie au filamu nyingine nyingi sana zinawoza kufa ukiwa na mpenzi wako. Kama una movie nyingine kichwani, unaweza andika hapo kwenye sehemu ya maoni ili kuwasaidia wengine.

Sms za kumwambia mpenzi wako kuwa unampenda BONYEZA HAPA>>>

Vitu vya kufuatilia ili kujenga Imani ya Mapenzi tena (Wengi wameipoteza)





Imani ya mapenzi ya kweli, tunaweza sema ni imani, uaminifu, na matumaini yaliyowekwa katika mahusiano ya mapenzi ya dhati kati ya watu wawili. Ni hali ya kuamini kwamba mapenzi yanaweza kustahimili changamoto, misukosuko, na majaribu ya maisha bila kuvunjika. Kwa upande mwingine inaweza kuwa ni imani inayofanya uamini kuwa mnapendana, mtapendana na mtaendelea kuwa pamoja.

Imani hii ya mapenzi watu huwa nayo mwanzoni katika maisha ikiwa iko vizuri tu. Lakini baada ya kukutana na maumivu ya mapenzi, wengi huipunguza au kuipoteza kabisa. Yani unaweza kuta mtu alikua na mpenzi wake wa kwanza akiamni watakua pamoja milele lakini jambo flani baya linatokea, wanaachana akiamini hakuna mwanamke au mwanaume yoyote mwenye mapenzi ya kweli. Maumivu ya mapenzi hufanya watu wafikilie tofauti kabisa kuhusu mahusiano ya mapenzi.

Kuondoa au kupunguza Imani katika mapenzi sio jambo baya maana husaidia kuwa makini kwenye mahusiano yajayo lakini kukizidi kunaweza kuwa kubaya. Mfano; kuna watu wanaimani ndogo sana juu ya mapenzi kasi kwamba hawawezi tulia kwenye mahusiano na hata wakiingia, hayadumu kwasababu hawayazingatii wala kuwa na malengo. Hapa ndio utasikia mtu anakwambia “Sina imani na Wanawake kwenye mapenzi” au “Siamini mwanaume yoyote mwenye mapenzi”. Na kunatabia nyingi mbaya zinaweza kuzaliwa baada ya Imani ya mapenzi ya kweli kupungua au kuondoka.

Baadhi ya watu huwa kwenye hali mbaya ya kutoamini katika mapenzi mpka hutamani hata kupata msaada utakaofanya wawe na imani tena. Yani wanatamani wampende mtu mmoja kwa dhati huku wakiwa na malengo yalionyooka.

Jambo la kurudisha Imani sio jepesi sana maana hutegemena na kilichoiondoa au kuipunguza. Lakini hapa chini The bestgalaxy tumejaribu kuweka vitu vya kufuatilia ili kuongea Imani ya mapenzi ya kweli. Ni vitu vidogo sana ila vinaweza kujenga imani ya mapenzi ya kweli kwa kiasi kikubwa.

Jinsi ya kupata Mpenzi mtandaoni BONYEZA HAPA>>>

Vitu vya kufuatilia ili kujenga imani ya mapenzi ya kweli tena

Simulizi za mapenzi



Baadhi ya simulizi za mapenzi huwa zinajenga Imani ya mapenzi ya kweli unapozifuatilia. Zinaweza kuwa za sauti, maandishi na hata video lakini unapozifuatilia zinakushawishi kuingia kwenye mahusiano na kuamini yatadumu.
Kupitia simulizi hizi, unaweza jifunza mambo mbalimbali ambayo yatakusaidia kuwa mvumilivu tena, mwenye mapenzi ya dhati na kuamini kuwa mahusiano yako yatadumu. Unaweza hata kufunguka ubongo na kujua mbinu mbalimbali za kutatua changamoto ili kudumu kwenye mahusiano yako.

Mfano wa simulizi nzuri za namna hii ni simulizi iitwayo SUKARI YA DADA na UTAMU WA JUMLA.

Nyimbo za mapenzi



Nyimbo huwa zinaimbwa na watu wengi sana hapa Duniani na katika mapenzi watu haimba mambo tofauti tofauti. Baadhi ya nyimbo za mapenzi hinaweza kukusaidia kuamini tena kwenye mahusiano ya mapenzi ya kweli. Sio kila nyimbo huwa zinakua hivyo ila Kuna nyimbo nyingi chanya za mapenzi zinazoweza kukujenga kiiimani kwenye mahusiano.

Mambo ya Dini



Dini za kikriso na kiislam huwa zinamuongonzo juu ya mapenzi na hakuna inayoelezea mambo ya muumizana au kutoaminiana. Dini zote nimewaka wazi nini cha kufanya mnapopendana ili kuwa pamoja na zinahitaji muwepamoja milele. Uvumilivu heshima na mambo yote ya msingi katika kuwa pamoja kwenye mahusiano ni mambo ambayo huelezwa wazi kwenye dini.

Kwaiyo kufuatilia dini yako kunaweza kuijenga Imani na hata kukusaidia kuishi maisha na mazuri na mpenzi wako.

Mwisho ningependa kukushauri kuwa katika kufuatilia mambo haya ili kujenga Imani, ni vema ukamuhusisha na mpenzi wako. Yani mshawishi na mpenzi wako kufuatilia mambo haya ili muijenge imani kwa Pamoja.

Jinsi ya kurudiana na mpenzi wako wa zamani (Ex)

Kurudiana na mpenzi wako wa zamani inaweza kuwa hatua kubwa inayohitaji fikra za kina na maandalizi mazuri. Watu wengi hupitia hali ya kutaka kurudiana baada ya uhusiano kuvunjika. Lakini sio jambo la kukurupuka tu; kuna masuala mengi ya kuzingatia kabla ya kuchukua hatua yoyote.

Katika makala hii, tutajadili hatua muhimu unazoweza kufuata ili kurudiana na mpenzi wako wa zamani kwa njia yenye mafanikio. Kila hatua imeundwa kukusaidia kufikiria kwa kina na kuimarisha uhusiano wenu unapofanikiwa kuurudisha kwenye uhai. Lengo ni kuhakikisha kuwa kurudiana kwenu kunaleta furaha na uimara badala ya maumivu ya zamani. Endelea kusoma ili uione njia bora ya kurudisha mahusiano kwenye hali nzuri.

Mambo ya kufanya kwa Mpenzi asieonesha kukupenda BONYEZA HAPA>>>

Jinsi ya kurudiana na mpenzi wako wa zamani

Fikilia maamuzi yako kabla ya hatua

Kwanza kabisa; Fikilia maamuzi unayotaka kufanya kama ni sahihi au si sahihi. Na tena ufikilie kuwa kama maamuzi ni sahihi kwasasa ila yataonekana kawa mabaya baadae, hautajilaumu sana.
Kwenye mapenzi, kuna baadhi ya watu huachana na mtu alafu hupata mtu alie sahihi, na pia kuna watu hurudiana na mtu alie sahihi. Sasa unahisi utakua ni yupi kati ya hawa watu? Hebu fikilia vizuri kwanza maamuzi yako.

Angalia kama kuna upendo kati yenu

Upendo ni kitu kigumu kukificha kikiwepo kati yenu hatakama mumeachana. Na kama mumeachana ila kuna upendo kati yenu, kunakua na uwezekano wa kurudiana. Kwaiyo kama unataka kurudiana na mpenzi wako, angalia kwanza kama kuna upendo kati yenu.


Unaweza utambua upendo kirahisi kwa kujaribu kuwa karibu nae. Angalia kama anawivu na wewe, angalia kama anakuwekea milango ya mumuingia, angalia kama uwepo wako karibu nae anautambua au kuukupenda kabisa.

Mfano mzuri; kwenye simu unaweza kuta alikublock lakini baada ya muda kaondoa block. Au kama sio kwenye simu basi anaweza hata kuwa mara nyingi anakuja katika sehemu unazoweza kumuona kirahisi na kuanza kuongea nae.

Jenga uaminifu upya

Kama mlitengana kwasababu iliopelekea asikuamini, basi unatakiwa kufanya kazi kubwa sana ya kujenga uaminifu. Mfano; Ikiwa ulimsaliti ndio mkaachana, utakua na kazi ya kumfanya aamini kuwa unajutia kosa lako, hautamsaliti tena na hauhitaji kumpoteza kwenye maisha yako. Tena kwa vitendo zaidi na sio maneno tu.


Kujenga uaminifu kunaweza kuchukua muda sana ila hakikisha unazingatia sana swala hilo maana asipokuamini, kunakua na uwezekano mkubwa wa kuvutiwa na wengine anaohisi wanamapenzi ya dhati kulio wewe. Hii ni kwasababu kosa lako limekua kama ishara ya kuwa hauna mapenzi ya dhati kwake.

Anzisha mahusiano ya mapenzi rasimi kwa uangalifu

Mwisho, fanya kuanzisha mahusiano ya mapenzi rasimi. Unaweza anza kufanya hivi kwa kumwambia bado unampenda na kuomba nafasi ya kuwa nae. Akikubari, utakua tayari umeingia nae kwenye mahusiano. Lakini usiishie kujiachia tu, jaribu kuwa muangalifu kwenye mambo mbalimbali kati yenu. Zingatia kuendelea kujenga uaminifu na kufanya mahusiano yenu yawe imara zaidi.

Wakati ukifanya yote hayo, epuka kulazimisha mpenzi au mtu ulieachananae kurudiana tena. Yani ukiona dalili za yeye kutotaka murudiane kivyovyote, acha kumfuatilia kabisa maana hata baada ya kurudiana unaweza kuteswa kihisa.

Sababu zinapelekea mtu kutodumu kwenye mahusiano

Kunazisha mahusiano ya mapenzi na mtu, kunaweza kuwa ndio safari ya kuishi mukiwa pamoja mpaka mwisho wenu. Lakini Safari hiyo, watu wengi hutengana na kuivuruga kabisa. Yani kwasasa sio kila mahusiano yanayoanza yanafika mbali, wengi huanzisha mahusiano ambayo hayadumu. Na asilimia kubwa ya mahusiano ambayo hayadumu ni mahusiano yanayohusha watu wenye umri wa 19-29. Watu wanaweza kuingia hata kwenye ndoa lakini Bado wasidumu.

Kwaiyo tatizo la kutodumu kwenye mahusiano ni jambo linalowagusa watu wengi sana. Hapa Duniani kuna wanawake na Wanaume wengi kwasasa wanajiuliza “Kwanini sidumu kwenye mahusiano” bila kupata majibu. Hivyo, ukiwa ni mmoja wa watu woanojiuliza kuhusu hili, basi tambua haukopekeako katika ulimwengu, kuna watu wengi sana.

Mahusiano yako yanaweza kuwa hayadumu kwasababu flani lakini ni gumu moja kwa moja kusema sababu hiyo. Ni ngumu maana kuna sababu nyingi zinazopeleake mtu kutodumu kwenye mahusiano. Hapa chini tumejaribu kuzungumzia sababu chache ili kusaidia mtu yoyote anaepitia tatizo hili kwasababu hizo. Kujua haya kunaweza kukusaidia katika Mahusiano utayopata au ulionayo.

Jinsi ya kupata Mpenzi mtandaoni BONYEZA HAPA>>>

Sababu zinapelekea mtu kutodumu kwenye Mahusiano

Woga wa kuumizwa

Kuna watu waliweka moyo katika Mahusiano ambayo yaliwaumiza sana. Na kama tunavyojua, Ukimpenda mtu sana au ukizama kwenye mahusiano nae sana, basi hata kuumizwa utaumizwa sana. Jambo hili likitokea kwa mtu, linaweza mfanya asidumu kwenye mahusiano mengine mapya tena kwasababu anakua anaogopa kuumizwa. Anaweza jitahidi kupenda lakini akikumbua maumivu au akiona dalili za kuumizwa, anajikuta anajiweka mbali na mahusiano.

Ikiwa unaona unashindwa kudumu kwenye mahusiano kwasababu hii, basi unatakiwa kujipa nafasi ya kupenda tena. Amini kuwa yaliopota yalikuumiza kwakua haukua na mtu sahihi tu kisha mpende anaekupenda. Tengeneza nae malengo bila woga maana woga utakufanya upoteze hata mtu sahihi kwako.

Matarajio makubwa

Asilimia kubwa ya watu (hasa vijana) huwa na matarajio makubwa juu ya wapenzi wao. Baada ya kuona wanachotajia hakipo, wanaona kama hawapendwi au hawana bahati ya kupata mahusiano wanayohitaji. Yani unaweza kuta mwanaume au mwanamke anatamani apate mpenzi mwenyewe maisha kama ya kwenye TV au mambo anayowaza yeye tu kichwani mwake. Akikutana na mtu anaehisi anafanana na huyo anaemuhitaji, basi anategemea kwenye mahusiano au kwenye maisha halisia atakua hivyo hivyo, jambo ambalo ni gumu kutokea.


Mambo mengi unayotarajia kuyapata kwa mpenzi wako au mahusiano yako, unaweza kuyakosa au ukayapa alafu baada ya muda yakapotea. Hivyo, ni vema ukapunguza mambo unayotarajia kwenye mahusiano au kwa mtu unaeingia nae kwenye mahusiano ili udumu nae. Usitege mpenzi wako atakua sahihi Kila wakati, atakua na hela kila wakati, atakua anakuzingatia sana wewe tu kila wakati au kufanya mambo mengine kama hayo.

Kutokutana na mtu sahihi

Wakati mwingine unaweza pitia kwenye hali ya Kila mahusiano kuvunjika na tatizo lisiwe kwako moja kwamoja. Tatizo linaweza kwa ni bado haujakutana na mtu sahihi atakae weza kuunda muhusiano na wewe yasiovunjiaka. Sio Kila mahusiano yanayovunjiaka yanavunjia kwa bahati mbaya, mengine huwa ya Bahati nzuri inayokupeleka kwa mtu atakae kupenda na kukuthamini.
Ili upate mtu sahihi, ni vema ukawa mtu sahihi pia. Kuwa mtu ulietayati kwa mahusiano yasiovunjiaka ili ukikutana na mwanaume au mwanamke atakaekupenda kwa dhati, ujione anabahati kukutana kukupata wewe.

Kukosa uvumilivu

Ukiwafuta wazee waliofanikiwa kuishi wakiwa pamoja kama mke na mume, na kuwaliza Siri ya kudumu wakiwa pamoja, watakuambia mengi ikiwemo “Uvumilivu”.
Ni ngumu kudumu kwenye mahusiano na binadamu mwenzio bila kuwa mvumilivu. Hii ni kwasababu kuna mambo mengi hutokea kwenye mahusiano ili kuharibu mahusiano na hakuna njia ya kuyashinda zaidi ya kuvumilia.

Tabia yako

Tabia yako inaweza kuwa chanzo cha mahusiano yako ya mapenzi kutodumu. Kuna tabia ambazo unaweza kuwa nazo na hauzizingatii lakini ndio hufanya mahusiano yako kuvunjika. Mambo kama Kiburi, dharau, uchafu, uvivu, kutoaminika, kuwa na wapenzi wengi au mambo mengine kama hayo.

Kama ni mpenzi wa simulizi, unaweza fuatilia simulizi ya UTAMU WA JUMLA ili kupata mwanga kwenye tabia zinavyoweza haribu mahusiano. Kwenye sehemu ndogo simulizi hiyo, kuna mtu alikua hadumu kwenye mahusiano kwasababu ya tabia yake.

Ni hayo tu katika ukurasa huu, Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy

Ujumbe mzuri kwa mpenzi wako

Kuna wakati unaweza tulia na kuamua kumfurahisha mpenzi wako kupitia simu. Kuna mambo mengi sana unaweza mfanyia kupitia hiyo simu na akafurahi. Inaweza kuwa ni unampigia mnaongea mambo mazuri, unamtumia picha na hata ujumbe tu wa maandishi.

Na tena sio lazima muwe mnaishi mkiwa mbali mbali ndio mtumie simu kumfurahisha. Unaweza mfurahisha mpenzi wako kupitia simu hata kama mnaishi nyumba moja. Kumtumia ujumbe mzuri asio utarajia kwenye simu yake ni jambo unaloweza fanya kama utani ila linaweza kufanya afurahi sana hatakama mnaishi pamoja.

The bestgalaxy tumekua mstari wa mbele kuhakikisha hauumizi kichwa sana kwenye mambo ya mahusiano. Katika ukurasa huu, tumekuandalia orodha ya ujumbe mzuri kwa mpenzi wako. Kama unahitaji kumtumia mweza wako ujumbe unaoeleza hisia za upendo ulionao kwake, basi unaweza chukua itayokufaa hapa.

Sms za kumwambia mpenzi wako kuwa unampenda BONYEZA HAPA>>>

Ujumbe mzuri kwa mpenzi wako (Mwanaume au Mwanamke)

  • Unahisi kuna mwanaume anaependa mwanamke mzuri hivyo amkukose kisa mimi? Au wanawake wengine wanapenda unavyo kuwa na mimi? Hapana, hawapendi kuona tukipendana hao. Kuwa pamoja ni pigo letu kwao.
  • Penzi lako hunisukuma kutaka nikuulize “Nikupatie nini hapa Duniani ufurahi?” lakini nakumbuka siwezi kupa kila kitu. Ila ningekua na wezo, ningekupa tu kama nilivyokupa huu moyo wangu wa pekee uwe nao wewe mpenzi.
  • Sauti tamu ninayopenda kuisikia masikioni mwangu bila kuchoka ni Sauti yako. Mtu pekee ninaempenda bila kuchoka ni wewe. Kitu pekee ninachoweza pokea bila kuchoka ni penzi lako.
  • Waliopita walinifundisha kuwa mapenzi ni maumivu na nisiamini mtu. Wewe umenifundisha maana sahihi ya mapenzi na radha yake hadimu. Umenifanya niwasahau mazima, nimekupenda na nakukuona wewe tu.
  • Umenizamisha kwenye hisia za mapenzi mpaka najiona mimi na wewe tu kwenye Dunia. Na naogopa ila kwasababu nakuamini, naendelea. Nakupenda na naamini popote nikwa na wewe, sijapotea.
  • Nashindwa kuelezea jinsi nakupenda ila hebu fikiria; kila nyota angani ingekua inawakilisha jinsi ninavyokupenda. Unahisi ningekua nakupenda kiasi gani?
  • Niende nikaombe nini kwa jirani? Nikaombe Maji ili nikate kiu? Hapana, wewe tayari umeiweza kiu yangu. Siwezi hata kuiomba Asali kwao maana natosheka na vitamu unavyonipa malkia wangu.
  • Kuna muda huwa nakosa kabisa furaha na Sababu za kufurahia maisha yangu. Ila nikikumbuka nina wewe maishani, furaha humwagika kama maji ya mvua moyoni.
  • Usijiuze nakupendea nini mpenzi wangu. Utauchosha bongo wako Bure. Ninasababu nyingi sana za kukupenda wewe. Na hata ukiziondoa, bado nahisi Moyo wangu uliumbwa kukupenda wewe.
  • Kabla ya kukutana na wewe, nilitamani kukutana na mtu kama wewe nimpende maishani. Sasa nimekupata, nakupenda na kwenye maisha umekua kama Nuru gizani.
  • Najua kunamuda tunagombana au hatuelewani. Lakini tambua sijutii kukupata Ila najutia kuwa nawe mapema hapa Duniani. Moyo wangu unakupenda na umejaa mpaka akilini.

Katika orodha hii, Kuna ujumbe unaoweza kutuma kwa mwanamke na hata Mwanaume pia. Kwaiyo hii ni kwa watu wa jinsi a zote. Kikubwa hakikisha unatambua muda amambao utakua mzuri kwa mpenzi wako kupokea. Angalia na maana sahihi ya ujumbe ili mpenzi wako aelewe unacho maanisha unapomtumia.

Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy