Ni sehemu nyingine tena tunaangalia Magemu mazuri unayoweza kucheza kwenye simu. Kwenye makala hii tutajikita kwenye magemu ya “battle royale” ambayo kwenye kuyacheza yanahusisha kutafuta ufalme wa vita. PUBG, COD au Free Fire ni moja magemu maalufu ya battle royale lakini ukachana magemu hayo, kuna magemu mengi sana ya muundo huu katika ulimwengu wa magemu… Na mengine yanaendelea kutoka karibu kila mwaka.
Hapa The bestgalaxy tumekuandalia orodha ya magemu machache ya Battle royale ambayo ni ya online(unatumia internet kuyacheza). Unaweza angalia orodha hii hapo chini na hata kujaribu gemu litakalo kuvutia. Ila tumejikita kwenye Andoid.
WhatsApp yako inatatizo? Jifunze jinsi ya kutatua hapa>>>>
Magemu ya ufalme wa vita ya kucheza Online/mtandaoni kwa simu za android
Rules of Survival

Rules of Survival ni gemu aina ya battle royale ambalo lilitengenzwa na kampuni ya NetEase Games. Gemu hili ni moja ya magemu kama PUBG,COD au Fire. Lilitolewa kwa simu za Android pamoja na iOS. Linakutupa katika uwanja wa mapambano/vita wenye wachezaji wengine wa gemu hilo Online/mtandaoni.
Katika gemu la Rules of Survival, Ukiwa kama mchezaji wa gemu hili unaweza cheza ukiwa pekeako au kuwa katika timu. Unapoanza unaruka kutoka kwenye ndege na kushuka taratibu katika kwenye uwanja wa mapigano ukiwa huna silaha yoyote. Silaha utakua unazitafuta na kuzikuta kwenye uwanja huo huo wa mapigano huku ukiendelea kujitetea dhidi ya wachezaji wengine.
~Game hili kwa sasa limeondolewa ila kunatetesi kuwa linaweza kurudi.
Knives Out

Hili ni moja ya magemu mazuri ya online/mtandaoni ambayo huchezwa na watu zaidi ya moja. Gemu hili ni battle royale, hukusanya watu au wachezaji katika eneo moja kubwa na kutakiwa kupigana na kujitetea wakiwa kama timu au mtu mmoja mmoja. kufika haraka unapokwenda unaweza tumia gari.
Ni gemu bomba lililotolewa mwaka 2017 na waliolitoa gemu hili ni kampuni ya NetEase Games. Mpaka sasa gemu hili mamilioni ya wachezaji katika sehemu mbalimbali ulimwenguni na wechzaji hulicheza simu mpaka pc.
FARLIGHT84

Hili ni gemu ambalo linahusisha uongo wa kisayansi na ni moja ya magemu mzuri kaika ulimwengu wa magemu ya battle royale. Linakutupa katika mazingira ya ulimwengu wazi yaliyojaa sayari mbalimbali, vituo vya anga na viumbe vingine vya anga. Kiufupi gemu hili lina mazingira tofauti sana, vitu unavyokutananavyo katika gemu hili ni vya kisanyansi na mambo mengine ya uchunguzi wa anga.
Game la FARLIGHT84 limetolewa mwaka 2023 na mpaka sasa lina mamilioni ya wachezaji toka nchi au sehemu mbali hapa ulimwenguni. Kwa maana nyine tunaweza kusema gemu hili linapendwa na watu wengi.















