Magari ya umeme yameonekana kuwa ni future katika teknolojia ya magari.
Kumekua na mipango mikubwa ya kuwezesha magari kuifikia sehemu ambayo magari ya diesel na petrol yameifikia. Na sio kuyafikia tu, Magari ya umeme yaenda kuwa mbadala wa Magari hayo ili kusimamisha uchafuzi wa hali ya hewa unaotokana na uchomaji wa diesel na petrol hapa Duniani.
Hapa The bestgalaxy tumekuandalia mambo matano kuhusu magari haya ya umeme. Kama wewe ni mtu unaependa kujua mambo kuhusu magari ya umeme, basi chukua muda wako kuyasoma hapa chini.
Mambo 5 kuhusu magari ya umeme
Betri ni moja ya vitu vya gharama sana kwenye magari haya
Kama tunavyo fahamu, magari huwa yananunuliwa, yatumika na katika kutumika huwa tunabadilisha sehemu za magari zilizochoka na kuweka mpya. Karibu kila sehemu tunayobadilisha kwenye gari hughalimu pesa. Sasa katika magari ya umeme ukihitaji kubadili betri, huwa inagharimu pesa nyingi kuliko sehemu zote. Betri ya sehemu ya gharama sana katika magari ya umeme.
Unashauriwa kuangalia vituo vya kuchaji kabla haujanunua
Kutokana na magari haya kuonekana future, unaweza kuwa na shauku ya kufanya kila liwezekanano ili kununua. Lakini unapaswa kujua kuwa, kumiliki magari haya ya umeme katika sehemu iso na miundombinu mizuri kwajili ya magari ya umeme ni kitu unachoweza jutia. Unashariwa kuangalia zaidi upatikanaji wa vituo vya kuchaji katika mazingira yako kabla ya kuchaji magari haya ili usiteseke kupata chaji unapoishiwa ukiwa njiani.
Unaweza kuyachaji magari ya umeme nyumbani
Kutokana na Magari haya kutumia umeme, kunauwezekano wa kuyachaji nyumbani tu kwa umeme wa nyumbani. Lakini unapaswa kufahamu kuwa chaji zinazoweza kuwekwa nyumbani huwa hazina nguvu ya kujaza betri kwa haraka ukilinganisha na chaji zinazopatikana kwenye vituo maalum. Hivyo umuhimu wa vituo vya kuchajia upo pale pale.
Wamiliki wameonekana kupata changamoto katika baridi
Katika msimu wa baridi, watu wanaomiliki magari ya umeme waishio nchi ambazo hukumbwa na theluji wamekumbana na changamoto katika kutumia magari haya. Changamoto hizi ni pamoja na kuchelewa kujaa kwa betri za magari na kupungua kwa “Range” (Umbali ambao gari linaweza kutembea kabla haujalipeleka kuchaji tena).
Yanaendelea kushuka bei
Watu wengi wanaotupia macho magari ya umeme huwa wanaishia kuyatupia macho magari ya kifahari au Luxuly cars zinazouzwa ghari sana na kusahau kuwa kuna magari ya umeme ya kawaida yasio na bei ya juu sana japo ni bado inaweza kuwa dharama sana kwa baadhi ya watu. Ujio wa magari ya umeme ni mapinduzi yanayogusa watu wote na kila siku zinavyozidi kwenda kunajisi bei zinaenda kuwa rafiki.
Unawazo gani kuhusu mapinduzi haya ya magari? Sawa, asante sana kwa muda wako. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mambo mengine.