Mukiwa katika mahusiano ya mapenzi mnaweza kuwa mnatumia muda mwingi kuongea au kuwasiliana kipindi cha usiku. Hii inaweza kuwa ni mmepigiana simu, mnatumiana sms(kuchati) au mupo sehemu moja mnaongea. Hapa chini kuna kuna orodha ya maneno ya kumwambia Mpenzi wako usiku pindi unapoishiwa maneno ya kuongea. Maneno haya yanaweza saidia kuanzisha mada nyingine usiku huo na kumfanya mpenzi wako afurahi au ajisikie vizuri kuwa na wewe usiku huo. Endelea kuwa karibu na The Bestgalaxy.
Maneno ya kumwambia Mpenzi wako usiku (Mwanaume au Mwanamke)
Bebi ivi umeliona giza la usiku wa leo huko nje? Maisha yangu yanaweza kuwa zaidi ya hivyo bila wewe… sitamani utoke maishani mwanagu, nakupenda sana.
Yani natamani tungelala wote leo, natamani kuona macho yako mazuri ukiyafumba,natamani kusikia sauti za chini za ndoto zako za ucku huku nikiwa nimekukumbatia dear.
Ukiniambia nitaje vitu ninavyopenda toka kwako naweza anza kuvitaja usiku huu mapaka asubui na nisimalize.
Huku niliko ni baridi sana natamani nipate kumbato lako muda huu.
Ukihesabu nyota zote angani alafu idadi ya hizo nyota uizidishe mara milioni 100 ndio idadi ya sababu za moyo wangu kukupenda wewe.
Leo ukitaka kulala niambie mimi ntaendelea kuwa macho kukulinda mpenzi wangu.
Hapa sina usingzi, natamani nije nikukiss ndipo nilale.
Unaupa furaha moyo wangu usiku huu mpaka nashindwa kuelezea huraha hii.
Anaesoma ujumbe huu ni mtu ninaempenda sana na moyo wangu hudunda kwa furaha “Pah!” kila nikiona simu au sms toka kwake.
Sisi ni binadamu, Kuna muda huwa tunapatia na kuna muda tunakosea… Moja ya vitu vikubwa ambavyo nimepatia hapa duniani ni kukupenda wewe mpenzi.
Mtu anaesoma ujumbe huu ni mtu pekee ninaempenda katika maisha yangu. kunamuda nawaza nimwambie neno gani zaidi ya “Nakupenda” ili ajue nampenda sanaaa ila nakosa jibu, unaweza nisaidia kumwambia?
Nikiamka nikakuta hii ni ndoto nitafanya chochote ili nilale tena maana ninafuraha sana kuwa na wewe muda huu. Nahisi nipo ulimwengu mwingine.
Kumekuwa na mahusiano mengi ambayo huanzishwa lakini hayafiki mbali kama lilivyo lengo kuu la mahusiano yao. Hali hii inafanya wanawake wengi wawe na wasiwasi katika mahusiano. Wamekua wakifikilia “Je, atanifanya niwewake wa maisha?” Lakini wanasahau kujiweka tayari kwaajili ya kuwa wanawake wa maisha. Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo vinaweza mfanya mwanaume akuweke moyoni na akufikilie kuwa wewe ni wake wa maishani. Hebu tumia muda wako kuvisoma hapa chini.
Mambo humfanya mwanaume akupende sana na kukuchagua maishani
Tabasamu.
Kama unahitaji mwanaume avutiwe na wewe basi tambua kitu muhimu kufanya unapokuanae ni kutabasamu na kucheka. Usionyeshe uso usio na urafiki. Kuwa kama mtu anayependeza, mwenye urafiki, na mchangamfu. Ukijitahidi kuwa mtu mwenye furaha kuliko maugomvi. Onensha sura ya tabasamu kuliko makasiliko. Mapenzi yenu yanaweza kuwa na furaha pia na hakuna mwanaume asiependa mapenzi yenye furaha.
Wanaume kwa ujumla wanapenda wasichana wenye ucheshi ambao wanaweza kuwafanya wajisikie vizuri. Kuna muda mwambie hadithi za kufurahisha na usiogope kucheka. Kumbuka usizidi kupita kiasi hadi uonekane kama mchekeshaji. Ni vizuri kuwa na mwenzi ambaye anafurahisha, lakini ni watu wachache sana wanamawazo ya kuishi na mchekeshaji.
Toa kuliko kuchukua.
Ili kuongeza nafasi zako za kukupenda lazima utoe kuliko kuchukua. Mwanaume anaweza kutofautisha kwa urahisi kati ya msichana ambaye anataka kitu kutoka kwake na yule anayemjali. Nadhani unajua kuna wasichana wengi ambao wanafuata pesa na wameweka mbele pesa kuliko mahusiano. Wanaume wengi wanao wafuata wanawake wa mtindo huu huwa hawana mpango nao wa maisha maana huona kama wananunua upendo hivi… Jitofautishe na wauzaji na aone unavutiwa naye kwa upendo wake na sio pesa yake au kitu kingine chochote. Yani hata akitanguliza gari mbele usishoboke nalo sana kuliko kumpenda yeye maana baadae anaweza anza kulisifu gari kwa kukukamata wewe na mbaya zaidi inaweza kuwa ni wanawake wengi walinaswa na gari hilo hivyo, haunajipya.
Mpenafasi ya kufanya kazi, Mshauri na kumtia Moyo.
Unaweza sikiliza hii
Katika maisha Mwanaume maranyingi huzungukwa na vitu vinavyomkatisha tamaa na kumuumiza lakini anatakiwa ajikaze tu kwasababu ni “Mwanaume”. Hii inaweza kuwa kazini, kwenye familia na maeneo mengine. Endapo mwanaume anaejielewa atapata mwanamke ambae anamsikiliza mambo yake magumu, anamshauri, anamtia moyo na kumsukuma kufanya maamuzi mazuri na maendeleo hata kwenye mambo madogo kwenye maisha, hawezi kumuacha mwanamke huyo aondoke maishani mwake. Kuna familia huwa zinainuka na kuwa na mafanikio kwasababu ya jambo hili, hasa zikiwa na mambo ya kidini ndani yake.
Kama muko kwenye mahusiano na mwanaume na anaonekana kuwa busy sana na kazi mpaka anafikia kuwa mbali na wewe, Usimfikilie tofauti moja kwa moja na kuanza vurugu. Mruhusu mwanaume afanye kazi kidogo ili kufanya maendeleo kisha vumilia pindi anapokua mbali na wewe ila usijisahau kumuonesha upendo sana.
Hili ni jambo ambalo linaweza kuongeza sana nafasi zako za kushinda upendo wake. Wanawake wegi wanakata tamaa na kumuacha mwanaume wanapoona yupo busy Sana na maisha… huzani kuwa hawana nafasi tena lakini jua kuwa wakati huo ndio wakati mzuri wa wewe kuongeza upendo wake kwako.
Muoneshe kuwa bado yupo moyoni wako, muoneshe kuwa unajua anachokifanya na ukipata muda muulize maswali au kumshauri, muoneshe kuwa bado unamjali hii itamfanya akuweke katika fikila zake za kimaisha. Usijekosa maisha mazuri anayokupambania kwa kukata tamaa.
Lakini unapo mruhusu afanye kazi mbali na wewe hakikisha unafanya vitu vya upendo ambavyo vitamfanya aanze waza kukuweka karibu yake au kuja karibu yako(kama atakua na uwezo huo). Ukipata nafasi pia mtembelee au fanya mautundu akutembele.
#Muvumilie anaejali upendo na uvulilivu wako tu, Wanaume wengine hukimbia mazima.
Usimmiliki sana kuliko kumuonesha upendo.
Wanawake wengi hufanya makosa ya kumiliki sana mwanaume na wakati hata hawamuoneshi upendo. Unaweza kujaribu kumlinda sana asiende kwa wanawake wengine ili abaki kuwa na wewe pekee katika maisha yake lakini je anao wafuata wanamvuta kama jinsi unavyo fanya wewe?. Ni wazi kuwa wanamvuta kwa upendo na vitu vingine vizuri… hivyo na wewe kuwa mbunifu na kwenye kumuonesha upendo ambao utamvutia zaidi kisha mruhusu aamue kuchagua kinachomfaa. Ikiwa wewe ndiye wa kwake, hakika atakupenda.
Maadili mazuri ni lazima katika kumshawishi mwanaume akupende zaidi na aweke moyo wote kwako maishani. Hakuna mtu anayetaka kujihusisha na mtu ambaye haeleweki,hasikii au hana nidhamu. Bila shaka kila mtu husita kumpa moyo mtu ambae hana maadili mazuri. Wanaume wanapenda wanawake ambao wana nidhamu. Hivyo basi muheshimu na pia uwevizuri nae ataona unafaa kuwa wake maishani. kuna mambo unawezasikia rafiki au mwanawake wa mitandaoni Eti “Ukinichiti nakuchiti” “Wanaume wote ni Mbwa” “Siwezi kuwa na mwanaume mwenye gari au pesa” “Siwezi olewa kwa sasa mimi ni mzuri” na mengine mengi kama hayo. Ukileta mambo hayo kwenye maisha yako unaweza angukia pua, ni vema kutula kuwa na maadili yatakayomkaribisha mtu kuwa na wewe maishani. Onesha heshima kwa Mwanaume hata wakikuita mshamba. Kuwa msafi, vaa vizuri na marafiki wastaarabu.
Katika mahusiano wapenzi mnaweza ongea au kuwasiliana mpaka ikafika wakati mkakosa cha kuzungunzia, hasa kama hakuna mmoja kati yenu mwenye uwezo wa kuendesha mazungumzo. Ukiwa kwenye hali hii, unaweza ingizia maneno na vimaswali vilivyopo hapa chini kurefusha mazungumzo yenu, kumchekesha na hata kukusaidia kumjua vizuri mpenzi wako. Unaweza kuyatumia kama sms, au kuyaongea unapokua nae karibu au kwenye simu. Lakini unapotumia maneno na maswali haya hakikisha hamupo kwenye hali ambayo itamfanya mpenzi wako aone kero. Endelea kuwa karibu na The Bestgalaxy.
Maneno na maswali ya kurefusha maongezi na mpenzi wako
Kuna watu walikua wanamsifia dada flani hivi kuwa anamacho mazuri, nilivyomwangalia yule dada nikajiuliza “Mh hivi wanamjua mpenzi wangu hawa? hahaha” Unamacho mazuri sana alafu nayapenda.
Hivi hilo kovu ulifanya nini?, au ulikua cha utundu utotoni?
Kama kuna zawadi ambayo ulipanga kumpa mtu atakae kupenda kwa dhati maishani mwako nipe tu maana nakupenda sana mpenzi, sitamani utoke maishani mwangu unanipa furaha mwenzio. Stamani niamke kwenye hii ndoto.
Kwa mfano umeshida Milioni 80 sasa hivi, utanipa shingapi au utafanyia nini?
Kukupenda ndio kitu ninachoweza kukifanya bila kuchoka duniani mpenzi wangu. Sijui niwe nakuita jina gani ili usije sahau kuwa nakupenda na usinitende…
Ulivyo kuwa mdogo ulitaka ukiwa mkubwa uwe nani?
Hebu fumba macho tuone… Hahaha Unamacho mazuri… ivi unajua kwamba una macho mazuri hivyo?
Kwaiyo umelala peke yako? huogopi?
Wiki ijayo nikumbushe nikwambie kitu… Ntakwambia kitu kizuri
Kitu gani unapenda utimize kabla siku zako za kuishi duniani hazijaisha?
Bebi, ivi nikikwambia utaje vitu vitano tu unavyo penda duniani utataja vitu gani?
Unapenda mbwa au paka?
Ivi katika maisha yako unaogopa nini?
Ulifikiria nini mara ya kwanza nulipokwambia nakupenda?
Niambie vitu vitatu tu ambavyo hauvipendi?
Ivi umenipendea nini? au unapenda nini toka kwangu mpenzi?
Ninavyokugusa huwa najiskia vizuri sana ivi wewe unahisi vipi?
Unafanya nini sasa hivi?
Upo na nani hapo kipenzi?
Natamani nije hapo japo kukubusu tu lips zako nzuri hizo
Ukichukia unapenda kufanya nini ili kutuliza hasira zako?
Alafu usiku nilikuota
Ivi umeishawahi poteza hela? ilikua kiasi gani?
Niambie maneno matatu mazuri toka moyoni mwako
Unapenda kuangalia filamu? unapenda filamu gani?
Hahaha… nitakwambia kesho… au nipe zawadi nikwambie leo
kwenye familia yenu wewe ni mtoto wa ngapi kuzaliwa?
Ivi bebi Unapendelea zaidi kula chakula gani?
Ugali kwa kiluga chenu munauitaje?
Ukipewa nafasi ya kutembelea nchi tatu duniani ambazo hauja wahi tembelea, utachaguza zipi?
Asubuhi ni mwanzo wa siku na kuianza siku vizuri kunaweza kuwa ni pamoja na kupokea sms ya maneno ya upendo toka kwa watu tunaowapenda. Kumpa maneno mazuri ya upendo mpenzi wako wa moyoni anaekupenda kunaweza kufanya aifurahie siku nzima na pengine kufanya aendele kukuamini kwamba unamjali, upo yupo kichwani mwako na unamuwaza huko uliko. Hivyo kama unataka kufanya jambo hili, tambua kuwa hizo ni kati ya faida zake katika mahusiano. Na kama unahitaji sms za maneno mazuri za asubuhi zitakazo mgusa roho mpenzi wako, unaweza ukoa muda kwa kuangalia sms fupi ziliopo hapa chini zitakazo endana na hali ya penzi lenu.
Asubuhi njema… Natamani siku ya leo tungeamka kitanda kimoja na wewe. Tena sikufichi, huku niliko nakosa vitu vingi sana kwasababu niko mbali na wewe mpenzi wangu… Ila nikikumbuka kuwa unanipenda na pia nakupenda, moyo wangu unatulia kidogo na kusubilia siku tutakayoonana ingawa naona kama nachelewa kukutana na wewe malaika wangu, nakupenda sana.
Upendo ni zawadi ya pekee sana mungu aliyoiweka ndani ya mioyo yetu bure na mimi nimeitumia vema sasa zawadi hii kwa kukupenda wewe. Nakupenda sana na sijawahi jutia kukupenda mpenzi wangu. Asubuhi njema wangu.
Kuna mtu mmoja mzuri, anaakili sana, mkarimu na nampenda saaaana, yupo anaisoma sms hii niliomtumia pekeyake asubuhi hii. Ameuteka moyo wangu na sihitaji kuunasua maana anaupa raha kwa penzi lake, Asubuhi njema kwake.
Natumai ulikuwa na usingizi mzuri sana. Tafadhali amka sasa kwa sababu asubuhi yangu haiwezikamilika kujua hali yako wewe. Habari ya asubuhi mpenzi!
kila siku huwa nawaza kukusu wewe na mapenzi yetu kiujumla… nimegungua najifunza vitu vingi sana toka kwako, pia upendo wako unaboresha maisha yangu na kunifanya niishi kwa furaha sana. Asante kwa kuwa mimi, nimekuweka moyoni, nakupenda na nazidi kukupenda kila siku mpenzi wangu, Asubui njema kwako.
Natumai umelala kama malkia. Sasa tafadhali amka kama nyota na utawale ulimwengu wangu kwa siku ya leo tena. Habari za asubuhi!
Katika penzi letu kunamuda tunagombana alafu tunapatana. Hii isije kukufanya uamini kuwa sikupendi. Kama jinsi jua linavyo chomoza asubuhi hii na kuleta mwanga palipo na giza ndivyo uwepowako unaleta furaha kwenye maisha yangu. Nakupenda sana na najivunia kuwa na wewe…. Nakutakia asubuhi njema wangu.
Tunapitia vitu vingi katika penzi letu lakini sijawahi jutia kukupenda wala kuwa na wewe kwenye penzi. Mimi huwa naamini mimi ni Mfalme na wewe ni Malkia katika safari ya maisha na penzi letu, naamini unanipenda na nakupenda sana. Nakutakia asubuhi njema na siku yenye furaha.
Leo nimeamka nikiwa na mawazo yako tu akilini mwangu. Huwezi amini nilivyo kumiss hapa. Siezi kufurahia asubuhi hii nzuri bila wewe mpenzi wangu. Amka!
Najisikia kubarikiwa sana kila asubuhi ya maisha yangu ninapojua hali yako ni salama. Umeamka poa?
Mara nyingi wanawake warembo na wenye mvuto wa kumvutia kila mwanaume huishia kuzisikia ndoa kwa wenzao tu kutokana na sababu mbalimbali.
Wengi huwa na tabia ambazo huudhi na huwaogopesha wanaume wanaowahitaji bila wao wenyewe kujijua.
Ivi unaweza kuchagua kuwa na kitu chenye muonekano mzuri maishani mwako kitakachokupa shida na maumivu milele?
Ikiwa watu hushindwa kuvumilia kuishi na vidonda vinavyowapatia nyumba, magari na pesa, unafikiri urembo/uzuri unaweza kuwa na nini cha ajabu kwenye maisha?
Wanaume huwa sio wajinga na katika asilimia kubwa ya wanawake wanaoolewa huwa ni wanawake wa kawaida sana ukiwaangalia kwa macho jinsi walivyo, mpaka unakuta wengine wanajiuliza “mbona kamchagua mwanamke wa kawaida sana pamoja na malizote zile?”
Ukiwa mrembo/mzuri utapendwa na wanaume wengi ila watakupenda kwa lengo la kupata Penzi tu, baada ya hapo utakuwa wa kuchezewa na baadhi ya sababu zinazopelekea wanaume kufanya hivyo ni zifuatazo;
Tabia
Wanawake kama hao huwa na tabia mbaya na nikiongelea tabia mbaya basi najumuisha uvaaji, ukaaji, viwanja vya starehe, lugha zisizo nzuri na marafiki pia. Vitu hivyo humtenganisha mwanamke mzuri na wanaume wa oaji. Labla akutane na mtu wa tabia yake lakini asilimia kubwa ya wanaume wenye tabia hizo huwa wanatafuta wanawake waliotulia huku wakiendelea wanawake warembo wasio tulia. Wanaume wengi huwa hawapendezwi na tabia za aina hiyo hata mwanamke awemrembo kiasi gani.
Kuwa na maringo sana
Unakuta mwanamke ameweka kucha ndefu, nzuri,za kuvutia na anamaringo kiasi kwamba mwanaume mwenye mpango wa kuoa akimuona anajiuliza
“Sasa kwa hizi kucha atanifuliaje nguo?… Anamaringo sana sijui itakuaje tukipishana?… Anaanzaje kuosha vyombo?… Ivi atakubali kutulia na kulea mtoto?.. Inaonekana hata kupika hajui”
Mwisho mwanaume anaona hafai wala haoneshi tabia zozote za mwanamke ambae anatakiwa kukaa katika nyumba.
Wanawake warembo huwa ghali kuwatunza kwa sababu wamejiwekea dhana kuwa wanafaa kupelekwa katika hoteli kubwa kubwa na maeneo yaliyo na bidhaa ghali. Huwa hawalegezi msimamo hasa kuhusu mahitaji yao na wanakotaka kwenda kununua bidhaa.
Mwanaume akipiga hesabu za haraka haraka kuhusu ghalama ambazo anatumia kipindi cha ambacho yupo na mwanamke mrembo anaependa kulidhishwa kwa kufanyiwa mambo makubwa huwa anagundua kumuoa ni sawa na kubeba mzigo mzito sana kichwani.
Ni wabinafsi
Wanawake wa aina hiyo huishi wakifikiria dunia ni yao na kwamba wanafaa kuabudiwa na kila mwanamume. Wanaume wengi hupenda kuwa katika mahusiano nao na hii ndio sababu kubwa ya wanawake hawa kujiona wa hali ya juu sana.
Wasichojua ni kuwa wanaume huwatumia tu na kuwaacha kutokana na tabia zao ili kutafuta mwanamke mzuri wa kuoa. Kibaya zaidi ni kwamba, wanawake hawa huendelea kutiwa moyo na uzuri wao huku wakisahau kuwa umri walionao hauwasubiri.
Hawataki kuwa wazazi
Wanawake hao hupenda kusalia wakiwa wanapendeza, hivyo huwa wanaogopa kuzaa wasipate mikunjo, wasinenepe au kuwa na matiti kulegea. Kwa kawaida, hakuna mwanamume anayependa kuoa mwanamke ambaye hawezi kumzalia, hasa kwa sababu ya utamaduni wa Kiafrika.
wavivu kutatua changamoto za mahusiano
Kuna wanawake ni warembo na wazuri sana kiasi ambacho wanaume huwafananisha au huwasifu kuwa ni kama malaika. Kutokana na kusifiwa sana hujiona wazuri sana na hupenda kuwa kama yai kwenye mahusiano. Ukweli ni kwamba hata uwe mzuri vipi, kuna changamoto utakutananazo kwenye mahusiano. Nikizungumzia changamoto inaweza kuwa umekuta mweza wako kabadilika ghafla au kunajambo limetokea katiyenu na linafanya musielewane. Wanawake wazuri wanapokutana changamoto hizi huwa hawajisumbui kutatua changamoto…. Wanaona bora kubadilisha mwanaume kuliko kutafuta njia inayoweza rekebisha mahusiano yao hatakama wao ndio chanzo cha kuyumbisha mahusiano. Hali hii inawafanya wawewanabadilisha tu wanaume na hawafikii hatua ya ndoa… Na hata wakiingia kwenye ndoa huwa sio wavumilivu maana ndoa inachangamoto nyingi zaidi.
Sasa kama una sifa za aina hiyo, huenda ni wakati wako kubadilika ikiwa unataka kupata mume.
Mpira wa kondomu hutumika katika tendo la kujamiiana ili kuzuia mimba na vile vile hutumika kwa lengo la kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa.
Katika utumiaji wa mipira ya kondomu kupasuka kwa kondomu hutokea mara nyingi Sana bila kutarajiwa. Mara nyingi kitendo hiki husababisha mimba zisizotarajiwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Hapa kuna hatua nne unazoshauriwa kuzifuata iwapo kondomu imepasuka:
1. Kuwa mtulivu na tafuta kondomu hiyo iliopasuka.
Mara nyengine kwa mwanamke vipande vya mpira huo wa kondomu vinaweza kuingia ndani ya mwili.
Ingiza vidole vyako ndani ya mwili, vishike na kuvitoa nje.
Mipira ama vipande vya kondomu vinavyosalia ndani ya mwili wa binadamu vinaweza kusababisha hasara hivyobasi ni muhimu kuangalia na kuhakikisha kuwa umetoa kondomu yote.
2. Tumia dawa za kuzuia kushika mimba iwapo hamjakubaliana kupata mtoto(Kwa mwanamke)
Dawa hizi zinapaswa kutumiwa katika kipindi cha saa 72 tu. Zinauzwa madukani yaani zinapatikana katika maduka ya dawa.
Iwapo huna mpango mbadala unaweza kutumia dawa za kupanga uzazi.
3. Kupimwa magonjwa ya zinaa hususan HIV iwapo hujui hali ya mwenzako
Nenda katika kituo cha dharura karibu nawe na umwambie daktari yaliofanyika.
Pia unaweza kuchukua dawa aina ya Post Exposure Prophylaxis (PEP) katika kipindi cha saa 72.
PEP ni mchanganyiko wa dawa za kukabiliana dhidi ya virusi vya ukimwi ambazo zinakuzuiwa kutoambukizwa HIV iwapo mwenzako ni mwathiriwa.
Kumbuka kwamba kila ugonjwa wa zinaa una muda wake wakati unapoambukizwa na wakati utakapoonyesha unapopimwa.
Unashauriwa kufanyiwa vipimo zaidi vya vya magonjwa ya zinaa baada ya mwezi na baada ya miezi sita ili kujua hali yako.
4. Jiulize kuhusu kilichosababisha na usirudie kosa.
Wapenzi wengi huruka hatua hii bila kujua kuwa hayo ni makosa makubwa, kwa sababu utakapoelewa ni kwa nini mpira huo ulipasuka ndipo unaweza kujiweka vizuri katika mchezo mwingine. Hivyobasi jiulize kuhusu hilo.
Ukiwa kwenye mahusiano Unaweza kufanyia vitu vingi kwema kwa mweza wako ili kuonesha unamjali. Kutumia ujumbe wa mapenzi mpenzi wako ni Moja ya Jambo linaloonesha kujali pia… Mukiwa ni wapenzi mulio mbali hii inaweza kuwa ni kitu muhimu kinachojenga mahusiano kuliko hata kutuma tuma pesa.
Zifuatazo ni SMS au meseji za kumtakia mchana mwema mpenzi wako. Kama unahitaji Unaweza chagua zinazoendana na mahusiano yako kwa sasa kisha ukazitumia kwa umpendae. Endelea kuwa karibu na The Bestgalaxy kwa mambo mengine mazuri zaidi.
SMS za mchana mwema kwa mpenzi wako
Upendo wangu kwako huongezeka kila wakati ninapokutazama. Hautafifia wala kuisha kwa sababu hauna mwisho. Kila mara kumbuka kuwa Nakupenda sana na kwa muda huu nakutakia mchana mwema kipenzi changu.
Mpenzi, muda huu nakukumbusha tu kuwa wewe ndio chaguo langu. Yaani naomba ujue kuwa wewe ni Mfalme wa kasri langu na kwamba moyo uliokaa kifuani mwangu utalidunda jina lako. Ninakupenda zaidi ya ninavyoweza kusema nakupenda. Mchana mwema mpenzi wangu.
Nakutakia mume/mke mtamu zaidi ulimwenguni siku njema. Hakuna mtu katika ulimwengu mzima anaweza kuwa mpenzi wa maisha yangu kwa sababu nafasi hiyo tayari imechukuliwa na wewe, mume/mke wangu mpendwa. Nakupenda Saana na napenda kukupenda.
Asante kwa kupenda kila kitu changu, pamoja na kutokamilika kwangu. Mungu alinipa zawadi isiyo na kifani maishani mwangu pale alipokuumba wewe mpenzi wangu. Nakupenda sana kuliko ujuavyo.
Tambua kuwa wewe ni mtu pekee katika ulimwengu wote ambaye hufanya maisha yangu kuwa kamili kabisa na maridadi. Mpendwa, asante kwa kuleta joto na mwangaza katika maisha yangu. Sijawahi jutia kukupenda.
Nina nafasi moyoni mwangu ambayo hakuna mtu anayeweza kuchukua kwa sababu hakuna mtu mwingine anayeweza kunifanya nifurahi kama unavyonifanya. Nakutakia mchana mwema.
Wewe ni damu ambayo hupitia mishipa yangu. Wewe ndiye kipande muhimu ambacho hufanya roho yangu ikamilike. Siwezi kamwe kuishi katika ulimwengu huu bila wewe, mpenzi wangu wa thamani. Kuwa na siku mchana mwema huko uliko!
Kuangalia machoni pako kunanipeleka kwenye ulimwengu wenye zaidi ya maelfu ya furaha. Penzi lako hufanya nijihisi Niko paradiso. Umeniweza sasa, naomba kokote uendako usisahau kuwa nakupenda mpenzi wangu. Mchana mwema kwako.
Kila nikiona simu au SMS toka kwako moyo wangu hudunda kwa furaha… Kiufupi nakupenda na natamani kuelezea upendo wangu zaidi ya kukuambia “nakupenda” ili tu utambue na usije kuniumiza. Tambua hilo kipenzi changu… Nakutakia mchana mwema.
Mazoezi ni kitu muhimu sana katika maisha ya mwanadamu kwa sababu huuweka mwili vizuri na huuepusha na baadhi ya magonjwa pia. Mazoezi pia yamethibitika kusaidia katika kuuweka mwili mwili vizuri katika upande wa tendo la kujamiiana/kufanya mapenzi kwa jinsia zote mbili. Lakini unatakiwa kujua kuwa si mazoezi yote huwa na faida katika upende wa kufanya mapenzi bali ni mazoezi ya Kigel ndio huwa na faida katika upande huu.
Kigelni aina ya mazoezi rasmi yalioandaliwa kwaajili ya kuimarisha misuli ya nyonga na viungo vilivyopo chini kwa mwanaume na mwanamke. Mazoezi haya husaidia viungo vilivyopo chini ya nyonga kuboresha mawalisiliano, kuboresha udhibiti wa kibofu cha mkojo na pia huimarisha uwezo wa kufanya tendo/mapenzi
Jinsi ya kufanya mazoezi ya kigel Kitu kizuri kuhusu mazoezi haya ni hayahitaji gharama zaidi ya muda wako maana unaweza yafanya hata ukiwa nyumbani. Mazoezi haya hufanywa na wanaume au wanawake. Tafuta sehemu yenye hewa safi na nafasi ya kutosha pia iweinaruhusu wewe kulala chini (chini pawe pasafi au weka kitambaa), inaweza kuwa ni chumbani, sebleni na ikiwezekena nenda katika vyumba maalumu vya kufanyia mazoezi. Baada ya hapo unaweza fanya mazoezi yafuatayo;
Zoezi la kwanza;
Lala chali katika sakafu ilionyooka, kunja magoti kisha pandisha kiuno juu kabisa kama picha iliopo juu inavyoonesha. Baada ya kufanya hayo anza kupandisha kiuno hicho na kukishusha. Endelea kufanya hivyo kwa muda usiopungua dakika tano.
Zoezi la pili;
Jilaze katika sakafu ukiwa umenyooka na umeangalia chini, kisha unyanyue mwili wako kwa kutumia miguu yako na mikono yako kama jinsi picha inavyoonesha. Kaa kwa kuganda kama ulivyo na hakikisha wiliwako unanyooka kama rula kutoka miguuni hadi kichwani. Endelea kukaa kwa muda usiopungua dakika tano.
Zoezi la tatu;
Lala chali ukiwa umeinyoosha miguu alafu nyanyua mikono na miguu juu kisha kunja magoti miguu ikiwa bado ipo hewani. Anza kuushusha mguu wa upande mmoja wakati huohuo hukishusha mkono wa upende tofauti na uliopo mguu kisha rudisha tena mguu na mkono juu. Rudia kitendo hicho kwa mguu na mkono mwingine. Endelea kurudia rudia tena tendo hilo kama picha inavyooneshwa katika picha inavyooneshwa hapo juu kwa muda usiopungua dakika tano.
Hayo ni baadhi tu ya mazoezi ya kigel ambayo unaweza fanya kila siku ili kuuweka mwili wako uwe vizuri katika tendo la kujamiiana. Sasa tuangalie baadhi ya faida ambazo mtu anaefanya mazoezi haya huzipata.
Faida kwa mwanaume
Huongeza uwezo wa kujizui kumaliza tendo kwa haraka
Huimarisha misuli katika sehemu zake
Huongeza uwezo wa kubana mkojo
Faida kwa mwanamke
Huimarisha misuri ya nyonga na kuifanya iwe fanisi
Huongeza hamu ya kufanya mapenzi
Hufanya mzunguko wa damu ufanyike vizuri katika sehemu zake.
Natumaini mpaka hapa umejifunza kitu na nakusihi endelea kuwa na The Bestgalaxy hakikisha upo na sisi kila wakati ili uendele kupata vitu vizuri.
Kipindi cha mwisho wa mwaka ni kipindi kizuri sana cha wapenzi kutumia muda wao pamoja. Sasa kama unampenzi basi katika ukaribu wenu wa kipindi hiki unaweza kumtumia mpenzi wako ujumbe mzuri utakao mfurahisha na kujiona wa peke katika maisha yake. Hapa tume kuandalia jumbe nzuri unazoweza mtumia mpenzi wako katika kipindi cha Krismasi. jumbe hizo ni zifuatazo;
~~~~Tulikutana, tukapambana ili tubaki pamoja, tukashinda na tulikua na nguvu katika changamoto zote tulizokabiliana nazo mpaka kufika hapa. Nafikili penzi letu litazidi kuwa imara zaidi. Nimependa kutumia Christmas hii kukukumbusha kuwa, nakupenda sana mpenzi wangu.~~~~
~~~~~~Penzi lako ni zawadi bora ambayo ninaweza kuifurahia zaidi! Krismasi njema, mpenzi!~~~~
~~~~Siku zinakwenda, masaa yana kwenda mimi bado nipo na wewe. Unaona naishi kwa furaha, naona kuishi ni raha lakini tambua sababubu kubwa ni wewe. Tafadhari usije sahau kuwa nakupenda na moyo wangu umetekwa na wewe.~~~~~~
~~~~~Krismasi inakuja mara moja kwa mwaka, lakini tafadhali jua kwamba ninakuenzi kila siku, bila kujali umbali kati yetu. Christmas njema mapenzi wangu.~~~~~
~~~~Nakutakia Christmas njema mme/mke wangu… Nakupenda Sana na ningependa popote ulipo utambue una nusu ya moyo wangu na nusu niliobakinayo yote inakupenda wewe.~~~~
~~~~Penzi letu ni changa bado lakini upendo wangu kwako upo zaidi ya unavyoweza kufikilika, nakupenda Sana na nafurahi kila nikikuona mbele ya macho yangu hakika umeteka hisia zangu. Nakutakia furaha msimu huu wa sikukuu na nitafurahi zaidi tukitumia wote siku ya Christmas.~~~
~~~~~Wewe ni ua zuuri lililoota katika bustani ya moyo wangu, tena ni ua pekee la thamani, linalonipa furaha katika maisha yangu. Nakupenda Sana na najivunia kuwa na wewe malaika wangu. Kuwa na furaha tele katika msimu huu wa sikukuu, kipenzi changu!~~~~~~
~~~~~Hakuna raha kama kupendwa na wewe na sijawahiona karaha kuwa na we. Kama moyo wangu ungekuwa wazi, ungejiona ukiwa peke yako na ukobusy kunipa furaha. Nakupenda Sana na nakutakia furaha katika msimu huu!~~~~~
~~~~Katika Christmas hii nitapenda niwe na furaha, na nikae na mtu ninaempenda na anipae furaha. Vyote hivyo vitakamilika endapo tutatumia siku hiyo pamoja maana utanipa furaha na vile vile nitakuwa na wewe nikupendae na unapae furaha. Mpenzi, tutakua wote si ndio?~~~~
~~~~~Wanasema furaha haiwezi kupimwa kwa maneno halisi, Ni kweli. Tambua kuwa Krismasi hii inatukumbusha kwamba upendo, furaha, na nia njema ndio vitu halisi vinavyoinua maisha yetu. Asante kwa furaha unayoniletea tangu nilipokutana na wewe, mpenzi wangu.~~~~~
Kutuma sms au ujumbe wenye maneno mazuri kwa mpenzi wako, ni kitu muhimu sana katika mapenzi. Unapotuma ujumbe/message moja kwa moja unakua umeonesha kumjali na pia kumkumbusha kuwa yeye ni wamuhimu kwako. Leo nakupa sms ambazo unaweza zituma kwa mpenzi wako kwaajili ya kumtakia usiku mwema na akajisikia vizuri. Chagua ujumbe unaoendana na hali ya mahusiano yako Kwa sasa hapa chini na umtumie. Lakini kumbuka kuwa sio pazima umtumie ujume kama ulivyo andikwa hapa. Unaweza ubadilisha badilisha.
SMS za mapenzi za kumtakia usiku mwema mpenzi wako
# 1: Natamani usiku wa kwanza ambao tutakua pamoja. Natumai unafikiria juu yetu kama mimi. Daima kumbuka kuwa nakupenda mpaka mwisho wa wakati. Ulale vizuri mpenzi.
# 2: Mpenzi wangu mtamu, nadhani siku yako imekuwa nzuri kama wewe. Lala na upumzike vizuri, ili uweze kuamka mchanga na mwenye nguvu kwa siku ya kesho. Usiku mwema.
# 3: Maneno hayawezi kuelezea jinsi ninavyokupenda na kukuthamini. Tumekuwa na moja ya siku bora za maisha yetu na ni maombi yangu tutakuwa na siku kama hizo kwa maisha yetu yote. Usiku mwema, mwanamke mzuri
# 4:Natumai leo imekuwa nzuri kwako. Nimekuwa nikifikia niwezaje pata furaha usiku huu. Nikakumbuka kuwa kumtakia usiku mwema mpenzi aliekatika moyo wangu hunipa kutanipa furaha. Usiku mwema.