Tag Archives: Love

Namna ya kuchati na mpenzi wako

Siku hizi kuchati tunaweza sema ndio moja ya vitu watu hufanya sana kwenye simu. Katika muhusiano, mawasiliano ni muhimu sana kati ya wapenzi wanaopenda. Watu wengi wakiwa Katika mahusiano kuchati ndio huwa mawasiliano yao. Kuna watu kwenye mahusiano hutumia app kama WhatsApp,Telegram au huduma za sms za kawaida, kuchati na wapendwa wao. Yote ni sawa na kuchati ni jambo zuri maana huwaweka wapenzi karibu hatakama wako mbali. Kwa namna nyingine tunaweza sema kuchati huimarisha mahusiano ya mapenzi.

Hapa The bestgalaxy tunaenda kukufungua juu ya namna ya kuchati na mpenzi wako akiwa ni wakiume au wakike. Lakini unapaswa kufahamu kuwa hakuna namna moja ya kuchati na mpenzi, upo huru kuchati na mpenzi wako vile mnavyoona inafaa na inawapa furaha. Ila kama utaona inapendeza au unahitaji msaada, unaweza pia soma yafuatayo ili kujua jinsi au namna nzuri ya kuchati na mpenzi wako.

Maneno ya kumwambia mpenzi wako usiku BONYEZA HAPA>>>

Namna ya kuchati na mpenzi wako (Mwanamke/Mwanaume)

Weka utaratibu wa kumjulia hali


Salamu au kujuliana hali ni muhimu katika mahusiano na ukiwa unachati na mpenzi wako ni vema ukiwa umeweka utaratibu wa kumsalimia na kumjulia hali. Hii itamfanya mpenzi wako kujua unamjali na umemuweka akilini mpaka unakumbuka kutaka kujua yupo kwenye hali gani.
Unaweza kuwa na tabia ya kumjulia hali mida ya Asubuhi, mchana au muda wowote baada ya kuwa kimya kwa muda. Sio lazima iwe ni kila mara na sio lazima umjulie hali mara chache pia, kikubwa usimsumbue tu.

Maswali au maoini yanaweza kurefusha maongezi

Fahamu mbinu za kurefusha maongezi maana maongezi kuna muda yanaweza kuwa magumu kuyaendeleza. Mnapochati alafu mukafika hatua ambayo maongezi ni magumu kuyaendeleza, Kumbuka kuwa maswali au maoini yanaweza kurefusha maongezi yenu. Muulize maswali kuhusu yeye, vitu anavyopenda na kuhusu mambo mengine. Hii itamfanya awe anajieleza na kufanya maongezi yenu kurefuka. Pia na wewe usiwe mvivu kutoa maoni kwenye majibu yake ili kwenda nae sawa.

SMS za kumbembeleza mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

Usiwe serious sana mtaishiwa mada

Ukiwa unachati na mpenzi wako, unaweza kuwa na mada nyingi ambazo unaweza ongeanae ili mada hizi ukiwa serious, utaziona hazina maana au zinakera. Kiufupi ikiwa kila unapochati na mpenzi wako unakua serious sana, mambo ya kuongelea yanakua machache sana kiasi ambacho unaweza ukashindwa pata mada kabisa.
Kwaiyo ni vema ukawa haupo serious sana ila mada ziwe zinatiririka kwenye maongezi yenu. Sehemu ya kucheka chekeni, sehemu ya kutaniana tanianeni, sehemu ya kubembelezana bembelezaneni, sehemu za kuongelea ujinga jifanyeni wajinga na kwenye sehemu ya mambo ya msingi ndio kueni serious.

Acha kuchati kabla hamjachoka kuchati

Kama unamtindo wa kuchati sana na mpenzi wako, hakikisha unakua na ujanja huu ili usimkere mwenza wako. Hakikisha ukichatinae sana unaacha kuchati kabla hamjafika hatua ambayo kila mtu amechoka kuchati. Tumia muda wako kuchati na mpenzi wako ila ukiona tu anaelekea kuchoka, acha kuchati nae. Unaweza katisha maongezi kwa kusema “nitakutafuta baadae kidogo mpenzi wangu” au ukatafuta kisingizio kingine. Kama atakua anataka kuendelea kuchati, kunajinsi anaweza endeleleza mwenyewe maongezi.

Usitume sms nyingi sana anapokua kimya

Ni kawaida kuwa na hali ya kushindwa kujizuia kutuma sms pale mwenza wako anapokua kimya. Ila Hali hii inabidi isikusukume kuwa kero kwa mwenza wako. Ni vema ukiwa kwenye hali hii ukahakikisha hautumi sms nyingi zisizo na maana kwa mpenzi wako. Tuma sms chache zenye kueleweka alafu kama atakua anasoma, atakuelewa na kukujibu.

Mambo ya kuepuka katika mahusiano BONYEZA HAPA>>>

Mwisho; usisahau kutumia maneno mazuri kwenye kuchati kwenu. Kama muko kwenye mahusiano ni vema mkawa mnachati kama wapenzi na sio marafiki. Kuna muda unatakiwa kuziweka mbali hizo “wewe” “Oya” na kuanza kuzitumia “mpenzi” “mke” “mme” na maneno mengine kama hayo.
Ni hayo tu tulio kuandalia katika ukurasa huu The bestgalaxy, usisahau kuwa karibu na sisi ili kufahamu mambo mengine mengi.

Picha zenye maneno mazuri ya mapenzi

Mawasiliano ni jambo la msingi katika mahusiano na siku hizi watu hutumia mitandao ya kijamii kuwasiliana na wapenzi wao. Mitandao hii ya kijamii itaweza kutumika kutuma jumbe za maandishi na sauti. Mbali na vitu hivyo, Video na picha ni kati ya vitu ambayo watu wanaweza tumiana kupitia mitandao ya kijamii.

Kutokana na mitandao ya kuwezesha watu kutumiana picha, kunawatu hupendelea kutuma picha zenye ujumbe au maneno mazuri kwa wapenzi wao katika mahusiano. Jambo hili ni zuri sana na linapendeza maana ni njia nzuri ya kuelezea upendo. Kama na wewe ni moja wa watu hawa, basi hapa kunaweza kuwa na kitu kizuri kwaajili yako.

Hapa chini tumeweka picha zenye maneno mazuri ya mapenzi ambazo unaweza zitumia ikiwa wewe ni moja wa watu waopenda kutumia picha hizi. Unaweza chagua inayoendana na hali yako ya mahusiano na kuitumia.

Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze Kila mala BONYEZA HAPA>>>

Picha zenye maneno mazuri ya mapenzi 

Ujumbe wa picha hii: Penzi lako hunifanya niwe ninafuraha kila nikikutazama na kutabasamu kila nikikuwaza… Nakupenda sana.

Ujumbe wa picha hii: Wewe ndio sababu ya mimi kujua upendo ni nini. Najifuza mengi toka kwako… Umekua kipenzi cha moyo stamani upunguze penzi lako.

Ujumbe wa picha hii: Katika Dunia hii nakupenda wewe.

Ujumbe wa picha hii: Neno nakupenda halitoshi kuelezea ninavyokupenda. Uwepo wako maishani mwangu ni kama mwanga… Nakuhitaji mpenzi nahisi bila wewe siwezi songa.

Ujumbe wa picha hii: Hakuna Penzi lililodumu kwa kusikiliza sana maneno ya watu. Ila kuna watu hudumu kwenye mapenzi kwa kusikilizana.

Nafikili katika picha hizi, unawezakua umepata unayoweza kutumia. Kama unatatizo katika kuidownload picha unayoitaka hapa, unaweza jaribu kuipakua kwa kugusa kwa muda wa sekunde chache alafu chagua “Download image” kwenye chaguzi zitakazojitokeza.

Kuwa mjanja! Tufuate kwenye akaunti zetu mpya za kijamii ; Instagram na Facebook

SMS za kumfanya mpenzi wako afurahi BONYEZA HAPA>>>

Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze kila mara

Baadhi ya watu wamekua wakijiuliza ni jinsi gani wanaweza wafanya wapenzi wao wawawaze kila mara au mara kwa mara. Kuna muda wazo hili humjia mtu baada ya kuona anapuuzwa kiasi flani na mpenzi wake au akiwa na hitaji la kumuweka mpenzi wake karibu zaidi.

Kama ni moja kati ya watu ambao wanataka kujua juu ya hili kwasababu hiyo au sababu nyingine tofauti. The bestgalaxy inakupa mwanga kidogo juu ya hili hapa chini. Tunaenda kuangalia vitu vichache unavyoweza jaribu kumfanya mpenzi wako akuwaze mara kwa mara.

Sms za kumfanya mpenzi wako afurahi BONYEZA HAPA>>>

Mambo ya kufanya mpenzi wako akuwaze mara kwa mara (Mwanamke au mwanaume)

Uwe msaada na mshauri wake mzuri

Mukiwa kwenye mahusiano mpenzi wako anaweza kuwa na matatizo ambayo huitaji umshauli au umsaidie kwanjia nyingine. Endapo utakua msaada na mshauri mzuri kwake basi utakua kichwani mwake kila mara maana tukiwa kama binadamu hua mara nyingi tunahitaji msaada. Hakikisha haupuuzi matatizo yake na hata yakikushinda fanya kumshauri kwa maneno mazuri. Na usiwe msaada kwenye matatizo tu, hata kwenye nyakati za furaha kuwa nae. Kusaidia kunaweza jumuisha kumpa pesa maana vitu vingi kwenye maisha ya sasa huitaji pesa .

Uwe unampa ahadi

Katika mahusiano ahadi zinaweza fanya hata mahusiano yadumu maana mnakua mnajua mnakoelekea. Ni vema sana ukawa unampa ahadi mpenzi wako na ahadi hizi zinaweza kuwa kubwa au ndogo lakini tambua kuwa ahadi ni deni kwa mpenzi wako. Unaweza huahidi mpenzi wako kuhusu vitu vya kesho, mwezi ujao, mwakani na hata maishani. Mtu anaekudai atakua anakukumbuka hata ukisahau wewe.

Ila tambua tu ahadi ni deni na kuna baadhi ya ahadi huharibu mpaka maisha ya mtu. Mfano; unamuahidi mtu mtaoana alafu anazama kwenye penzi na kukupa moyo wote  mpaka maisha alafu unaanza kumuona mjinga kisa akili yote ipo kwako na hutaki muoane tena. Ivi nafikili maisha yake utakua umeyavuruga kiasi gani?. Unaweza kuwa umewahi pewa ahadi kubwa za uongo lakini jambo hilo likufuze kuwa mkweli na sio muongo.

Mambo muhimu kufanya kwa mpenzi mwenye hasira au ukorofI BONYEZA HAPA>>>

Ukiwa nae hakikisha mnakua na furaha

Kuna nyakati nyingine kwenye mahusiano mnaweza kuwa na hasira au maugovi lakini nyakati ambazo hata mkiachana au mkiwa mbali mnaziwaza ni nyakati zile za furaha. Ukiwa kwenye mahusianao hakikisha ukiwa na mpenzi wako unakua chanzo cha furaha na sio maugomvi. Mpenzi wako anaweza kua amekufanya uchukie lakini pamoja na kuchukia kwako hakikisha  unamaliza utata na unatengeneza hali ya furaha ukiwa nae maana nyakati za furaha ndio nyakati ambazo tunaziwaza sana.

Mfano; Kuna muda unaweza chati na mpenzi wako vizuri mpaka ukarudia kusoma sms mara kumi kwa siku huku ukimuwaza. Au umeongea nae vizuri muda uliopita lakini tukio zima la maongezi yenu lipokichwani unaliwaza kila mara huku ukitabasamu.  Hii inaweza kuwa ni kwasababu mulikua kwenye nyakati inayofurahisha na Kama tunavyofahamu, hakuna mtu asiependa kuziwaza nyakati zinazofurahisha.

Pia usisahau kutumia maneno ya upendo na kumsifu ili ajisikie vizuri na kupata furaha. Pambana kutengeneza nyakati za furaha mkiwa wote alafu hizi nyakati zitatengeneza historia nzuri ya mahusiano yenu ambayo mtakua mkivutiwa kuendelea kuiandika.

Usije tumia nguvu kubwa kufanya mtu akuwaze kila mara kama hauna mpango nae kimaisha maana siku utakapomuacha unaweza kuwa na deni kubwa katika moyo wake. Asante kwa kusoma na endelea kuwa karibu na The bestgalaxy.

Mambo ya kuzingatia unapotaka kufanya Tendo (Wapenzi)

Kama ni mtu ambae upo katika mahusiano ya mapenzi na mmefikia hatua ya kutaka kucheza mchezo wa mapenzi, inaweza kuwa ni jambo zuri.
Mwanaume ikiwa umefika umri ambao unaruhurusu kufanya mchezo huu na mwanamke pia amefika umri, mnaweza kufanya mapenzi/tendo.
Lakini jambo hili linaweza kuwa zuri zaidi na salama kwenu kama mambo ambayo tunayaeleza hapa yatazingatiwa.

Mambo ya kuzingatia unapotaka kufanya tendo (mwanaume/mwanamke)

Usafi wa mwili

Usafi ni muhimu kuzingatia pale unapotaka kucheza mchezo wa mapenzi. Ikiwa wewe ni mwanaume au mwanamke, usafi unatakiwa kuuweka mbele maana uchafu unaweza mtoa mwenza wako raha ya mchezo. Hakikisha mdomo wako uko vizuri na hizo sehemu za mchezo husika siko safi pia. Epuka kuweka mdomoni vitu vyenye harufu mbaya na utumie vitu vinavyoleta harufu nzuri ili usimkere mwenza wako.

Kutumia kinga

Ikiwa mahusiano yenu yamewapeleka kucheza mchezo lakini hamjajuana vizuri, ni vema kuzingatia matumizi ya Kinga kwenye mchezo huo. Kinga ni muhimu maana huzuia mimba zisizotarajia na pia maambukizi ya baadhi ya magonjwa ikiwemo virusi vya Ukimwi. Ngono zembe inaweza kumpa mwenza wako au kukupatia wewe athari bila kujali wewe ni mwanaume au mwanamke. Ndio maana mtu anashauriwa kutumia mpira wa Kondom ambao ni Kinga unapokutana kimwili na mtu usiemjua kiundani.

Mazoezi ya mwili ambayo husaidia katika tendo BONYEZA HAPA>>>

Kuchukua tahadhari ya matukio mabaya

Kama mazingira ambayo mmekubaliana kucheza mchezo huu ni mageni kwako, ni vema ukachukua tahadhari. Hakikisha unakua makini ili vitu vyako visiibiwe, kuwa makini katika vitu unavyoweka mdomani ili usipewe dawa, kuwa makini pia usije kurekodiwa video na watu wabaya. Usiache kuzingatia jambo hili kama hata huyo mwenza wako hamjajuana vizuri maana baadhi ya watu huwa na nia mbaya tofauti na mapenzi.

Elewa mipaka yako na kuheshimu

Watu hucheza mchezo wa mapenzi na kila mtu huwa na mipaka yake katika mchezo huu. Sasa ni vema ukaelewa na wewe mipaka yako ni ipi na kuisimamia pale utakapokua ukicheza mchezo bila kumtoa mchezoni mwenza wako. Pia Kama mwenza wako atakua na mipaka, jiweke tayari kuiheshimu mipaka hiyo bila kutoka mchezoni. Na Kama mtavunja mipaka yenu basi ile kwa makubaliano.

Kuondoa woga wa kupita kiasi


Woga ukipita kiasi katika mchezo wa mapenzi, unaweza ushindwe hata kucheza mchezo vizuri. Baadhi ya wanaume wamekua wakishindwa kusimama uanaume wao kutokana na kuogopa. Ni vema kuondoa woga na kujiamini ukiwa Kama mwanaume au mwanamke ili ucheze katika nafasi yako vizuri na kumfurahisha mwenza wako.

Mambo hayo machache na yanaweza kuwa marahisi kuyapuuza, lakini ni mambo muhimu kuzingatia unapotaka kukutana kimchezo na mwenza wako hata ikiwa ni mara ya kwanza.

Jinsi ya kutunza mahusiano ya mbali

Kuwa na mahusiano ya mbali ni jambo la kawaida kipindi hiki. Kuna mambo mengi katika maisha yanaweza fanya ukaanzisha mahusiano na mtu aliembali na wewe au ukaenda mbali na mtu ulie na mahusiano nae. Umbali katika mahusiano unaweza sababisha mahusiano kuwa katika hali ya kuvunjika kwa urahisi endapo hakutakua na mambo ambayo husaidia kutunza mahusiano. Unataka kujua mambo haya ni mambo gani? Sawa, hebu soma hapa chini.

Mambo ambayo hutunza mahusiano ya mbali (Mwanaume na Mwanamke)

Mawasiliano ni muhimu.

Mawasiliano ni jambo muhuimu lisilotakiwa kukosekana kwenye mahusiano ya mbali. Mawasiliano huwaunganisha wapenzi hata mukiwa mbali. Ni vema kufanya mawasiliano mara kwa mara na mtu ulienae kwenye mahusiano ili kulinda mahusiano yenu. Jisukume kumjulia hali mapenzi wako na kuzungumzane karibu kila siku mpaka mufikie ile hali ya kuhisi muko pamoja japo mupo mbali.

Uaminifu na uvumilivu

Katika mahusiano ya mbali, kupoteza uaminifu na uvumilivu ni rahisi sana. Uaminifu na uvumilivu ukipotea kwenye mahusiano ya mbali unaweza pelekea mahusiano kuvunjika. Ni vema kila mtu kwenye mahusiano hayo ya mbali akawa mvumilivu na kuonesha uaminifu kwa kuwa muaminifu kwa mwenzake. Mara nyingi mtu ukishaanza kutokua muaminifu kwa mwenzako aliembali, utaanza kubadili tabia zako kwake bila wewe kujijua. Hii inaweza pelekea mpenzi wako wa mbali kuanza kutokukuamini, kuumia na kushindwa kuvumilia au kukusaliti.  

Kuongea kuhusu mambo yajayo na mipango ya mbele bila kujali umbali.

Unapokua unawasiliama na mtu ulienae kwenye mahusiano na mnaongelea kuhusu mambo yajayo au mipango ya mbele mnajenga picha ya Future ya mahusiano yenu pamoja na kwamba muko mbali. Ongeanae kuhusu kesho, wiki ijayo, mwezi ujao, mwaka ujao na maisha yenu ya mbele kiujumla. Weka nae mipango, ongelea matukio yanu yanayokuja, wekeaneni ahadi ndogo na kubwa mtazo mtazokua mkiishi kuzitimiza, Ulizaneni kususu vitu mtavyo fanya kesho au mwisho wa wiki.

SMS nzuri kwa Mpenzi aliembali BONYEZA HAPA>>>

Kuonesha kuwa unampenda, unamjali na unatamani muwe karibu.

Muoneshe kuwa unampenda kwa kumwambia vitu vizuri, kumfanyia vitu vizuri vitakavyoonesha unamjali hata kama upo mbali. Kama amekwambia hayuko vizuri, usipuuze kisa muko mbali. Jaribu kuwa msaada kwake kwa njia itakayowezekana. Jali maneno yake na hisia zake pia alafu usisahau kuonesha kuwa unatamani muepamoja. Mwambie vitu vizuri unavyotamani toka kwake ukiwa huko mbali, muoneshe kua yeye ndie alieuteka moyo wako huko uliko na utamani awekaribu yako hata sasaivi.

Ni hayo tu tumekuandalia katika mengi unayoweza Fanya kutunza mahusiano ya mbali. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy na usinchukie kutembelea Kila mara.

jinsi ya kuwa romantic kwa mpenzi wako

Kumwambia mpenzi wako nakupenda na kuchezanae mchezo inaweza kuwa ni jambo zuri lakini tambua kuwa bado unaweza onekana sio romanic. Kuwa romantic kumekusanya mambo mengi sana katika mahusiano. Kiufupi kuwa romantic ni kuonyesha mapenzi kwa mpenzi wako, kumuonesha kuwa unamthamini na kumjali kwa kusema na kufanya matendo yanayogusa hisia zake. Hapa The Bestgalaxy tunafungua ubongo kwa kuelezea mambo machache ya kufanya ili kuwa romantic kwa mpenzi.

SMS za kumbembeleza mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

jinsi ya kuwa romantic kwa mpenzi wako (Mwanaume au mwanamke)

Mwambie maneno matamu na yakuvutia

Kama uko pamoja nae mnaongea au unazungumza nae kupitia simu, hakikisha unamwambia maneno matamu na yakuvutia. Ongea na mpenzi wako kwa hali ya utulivu alafu mwambie maneno ya upendo toka moyoni yatakayo ugusa moyo wake na kumfanya ajue jinsi gani unampenda. Funguka mwambie moyo wako unahisi vipi juu yake au msifu kwa maneo matamu.

Mzawadie zawadi zitakazo mfurahisha

Mpe zawadi ambazo unahisi atazipenda. Zawadi sio lazima iwekubwa au sio lazima iwe pesa. Unaweza mzawadia mpenzi wako vitu vidogo sana na akafurahi mpaka ndani ya moyo wake. Unaweza mzawadia mpenzi wako hata pipi ya kijiti tu na akafurahi ila inategemeana na namna ulivyomzawadia au muko katika hali gani. Mbali ya vitu kama pipi unaweza mzawadia vitu vingine unavyoona anapenda au anahitaji ila hajakwambia.

Mpe muda wako muwe pamoja

Ni wazi kuwa kama unampenda mwanamke, unatamani akupe muda wa kuwa nea na hivyo hivyo hata mwanamke akimpenda mwanaume anatamani apate muda wa kuwa na mpenzi wake. Kutumia muda wako kuwa na mwenzako ni jambo linaloweza kufanya uwe romantic. Unaweza kutumia muda na mpenzi wako mukiwa mnaogea, mnacheza michezo ya upendo, kutembea, kuangalia vitu, kusikiliza  au kusoma vitu.

Mtu akikublock WhatsApp Fanya hivi kuchati nae BONYEZA HAPA>>>

Mshawishi mwili

Kumbusu mpenzi wako, Kumshika mikono na kumkumbatia au kumgusa kwa ujumla ni mambo muhimu sana katika mahusiano maana ni vitu ambavyo vinaweza kukufanya uonekane romantic kwa mpenzi wako. Mchokoze kimwili mpezi wako na kama atakua na mahitaji ya kimwili ni vema ukaheshimu hisia zake. Siku hizi unaweza mchokoza hata kwenye simu kwakuongelea vitu vitakavyo msisimua kidogo.

Msikilize, thamini mawazo yake na tatua migogoro kwa upendo na amani

Msikilizea anachokwambia na uoneshe kuyathamini mawazo yake. Usipuuze mawazo yake anayoyasema maana atakuona humueshimu au kumjali. Kama kuna mgogoro umejitokeza kati yenu usiwe mwepesi wa kumjia juu kumfokea au kumtukana. Tafuta njia ya amani na upendo ya kutatua mgogoro huo. Sehemu ya kuomba msamaha muombe msamaha, Sehemu ya kubembeleza mbembeleze na sehemu ya kumsamehe msamehe.

Mambo humfanya mwanaume akupende sana na kukuchagua maishani BONYEZA HAPA>>>

Aibu yako isikuzuie kuonyesha mapenzi, kumuonesha kuwa unamthamini na kumjali kwa kusema na kufanya matendo yanayogusa hisia zake. Pia majukumu au kazi isiwe sababu ya kushindwa  kuonyesha mapenzi kwa umpendae, kumuonesha kuwa unamthamini na kumjali kwa kusema na kufanya matendo yanayogusa hisia. Ukishindwa kufanya hivyo mpenzi wako anaweza kuona sio romantic na wengine wanaweza wakakuacha kabisa maana hawafurahii mahusianio.

Unataka kumuumiza mwanaume anae kutesa unampenda? Soma hapa

Kuna mwanaume ambae uponae kwenye mahusiano na unampenda lakini anakutesa? Unataka kufanya kitu kitakacho muumiza? Ni kitu gani unahisi ukikifanya kitamuumiza? Mh sawa ila kabla haujafanya maamuzi yoyote, hapa The bestgalaxy tunakujuza vitu vichache kuhusu hili.

Ni mara nyingi watu huangukia kwenye mahusiano ambayo huanza kwa kuwapa furaha lakini baadae hubadilika na kupoteza furaha kutokana na wenza wao kubadilika na kuanza kutojali hisia zao.Hali hii katika mahusiano inaweza kubadilika na kuwa nzuri au inaweza kuendelea kuwa mbaya zaidi na kupelekea kuvunjika kwa mahusiano kabisa.

Unapokua kwenye mahusiano alafu mwenza wako akabadilika ghafla na kuanza kukutesa au kutojali hisia zako ni vema ukajaribu kwanza njia mbali mbali kubaini nini tatizo na kurekebisha mahusiano yenu. Jaribu kuvumilia huku ukiongea na mpenzi kwa uwazi kabisa nakumuuliza  nini shida na mutafanya nini ili muwe sawa.

Uvumilivu ni jambo zuri sana pale mahusiano yanapoyumba ila kama mahusiano yanayumba na kugeuka mateso yasioisha mtu anaweza shindwa kuvumilia na kuanza kutafuta njia za kumuumiza anaemuumiza na hata kuondoka kwenye mahusiano kabisa. Kumuumiza mtu anaekuumiza kwenye mahusiano ni jambo baya sana maana linaweza pelekea ukajiumiza mwenyewe. Mfano; kuna dada moja alikua akiteswa kimapenzi na mwanaume wake. Akaamua kumuumiza mwanaume wake kwa kujiingiza kwenye mapenzi na rafiki wa mwanaume wake. Baade alipewa mimba na huyo rafiki alafu akapata na magonjwa pia kisha akatelekezwa. Unafikili uamuzi wa huyo dada ulimuumiza nani?

Ukiwa kama mwanamke, kuliko kufanya maamuzi yatakayo kuathiri hata wewe ni unaweza ukafanya yafuatayo.

Mambo muhimu kufanya kwa mpenzi mwenye hasira au ukorofI BONYEZA HAPA>>>

Mambo unayoweza fanya badala ya kufanya maamuzi mabaya

Jipende kuliko alivyokuzoea.

Kuna muda unaweza mzingatia sana mtu anaekutesa kiasi kwamba unasahau hata kujipenda. Unasahau thamani ulionayo na kujiweka hovyo hovyo. Ukiwa kwenye hali hii ni vema kuikumbuka thamani yako na kuanza kujipenda. Jipende bila hata kuambiwa unapendwa alafu jijali kwenye kila kitu. Vaa vizuri, pendeza, uwe msafi na ujiamini katika uwanamke wako ila usiwe na kiburi au dharau. Tambua kwamba wewe ni wa thamani na hata ukiambiwa “Sikupendi” bado thamani yako iko pale pale.

Usiingie kwenye mahusiano mengine kwa msukumo wa kuumiza mtu.

Ukiwa kwenye mahusiano ambayo mwenza wako anakutesa, kuna muda unaweza waza kutafuta mpenzi mwingine wa haraka haraka ili tu kumuumiza mweza wako. Wazo hili ni wazo baya sana maana linaweza kukufanya usiwe makini katika kuingia kwenye mahusiano. Jambo hili linaweza pelekea uingie kwenye mahusiano yatakayokupa shida na hata kukuacha katika hali mbaya zaidi.  

Usioneshe tena kuwa unaumizwa na mambo yake.

Kama kuna vitu mweza wako huwa anafanya kwa dharau ili kukuumiza na umejaribu kila mbinu kumzuia au kumwambia aache lakini anaendelea kufanya, acha kuonesha kuwa unaumia alafu kuwa kimya. Pengine anahitaji kukuumiza ndio maana anaendelea kufanya. Acha kumuonesha kuwa unaumia ili ajue amekuumiza mpaka umechoka. Kama atakua ni mtu anaejari, ataanza kuwaza mabadiliko yako.

Kubaliana hali halisi na ujipumzishe.

Ikiwa umevumilia na kujaribu kila njia ya kuokoa mahusiano yako lakini imeshindikana, kubaliana na hali halisi. Usilazimishe sana huwa kwenye mahusiano ambayo yanahatalisha mpaka maisha yako. Jaribu kurekebisha na ikishindikana kabisa, futa machozi alafu jipumzishe kwenye mahusiano hayo. Usifanye maamuzi yoyote mabaya.

Sms za mapenzi motomoto (Mahaba niue)

Kuna muda ukiwa kwenye mahusiano, unaweza tamani kumwambia maneneo ya mahaba moto moto mpenzi/mme/mchumba wako kwa njia ya ujumbe. Hili ni jambo hufanyiana wapenzi hasa mukiwa na upendo wa kweli kati yenu alafu munatumia sana simu kuwasiliana. Watu wengi wanapopokea jumbe au sms za mahaba toka kwa wawapendao, hufurahi.

Kama unataka kumtumia mpenzi wako sms za mapenzi motomoto basi hapa The bestgalaxy tunakupa sms za mapenzi motomoto ambazo unaweza mtumia mpenzi wako bila kuumiza kichwa sana. Kama utaona ni nzuri na zinaendana na mahusiano yako ya mapenzi, uaweza zitumia.

Maneno ambayo hautakiwi kusema kwa mwenza wako BONYEZA HAPA>>>

Sms za mapenzi motomoto (Mwanaume na Mwanamke)

  1. Siku hizi nanenepa kutokana na matunda unayo nipatia. Kila nikila nazidi kukung’ang’ania. Nafikiri wewe ndie mungu alinishushia maana umenipatia dear.
  2. Napenda kugusa ngozi yako laini kila nikiwa karibu yako. Kila ninapoigusa nahisi raha na msisimko. Hakika umeumbwa vizuri wewe mtoto, hahaha.
  3. Natamani unikumbatie nipate joto hapa nilipo. Natamani vitu vingi toka kwako japo siwezi sema. Nimekukumbuka sana mpaka nahisi siwezi hema.
  4. Natamani kusikia sauti yako mpenzi wangu. Unasauti nzuri inayougusa moyo wangu na kuulipua kwa furaha. Natamani tuishi pamoja ili niwe naisikia kila mara. Wewe ni tulizo la moyo wangu nakupenda sana.
  5. Natamani niwe na wewe kila siku,kila saa na kila dakika. Penzi lako moto naliitaji mpaka mwisho wa maisha. Nilikua naona mapenzi mabaya ila wewe kunakitu umenifundisha. Nakupenda zaidi ya sana.
  6. Ningerudi nyuma na kupewa nafasi ya kuchagua tena mtu ninaempenda, anaenifanya niwe na furaha na kunipa penzi linalo gusa moyo wangu bado ningekuchagua wewe. Nakupenda sana mpenzi wangu.
  7. Kukupata wewe kunanifanya nijione mwenye bahati sana katika dunia. Sijui sana kuhusu moyo wako ila tambua moyo wangu umeishazama katika penzi mpaka naogopa. Umeishaniteka sijiwezi mpenzi.
  8. Kuna watu niliwakaribisha kwenye maisha yangu wakanifanya nione mapenzi mabaya. Penzi lako nimefanya nione mapenzi matamu na sitamani niamshwe kwenye hii ndoto. Nakupenda sana.
  9. Nimeacha vitu vingi sana kwaajili yako na siwezi jutia maana unanipa furaha mpenzi wangu. Atuwezi kuwa sawa kila siku ila tambua nazidi kukupenda kila siku. Wewe ndie nimekuchagua moyoni na ndie daktari unaeweza tibu maradhi yangu. Wewe ni mtu wa thamani maishani mwangu.
  10. Penzi lako tamu, haliishi hamu. Upendo wangu kwako ni moto usiozima. Moyo wangu unalidunda jina lako na kila mara natamani kuwa karibu yako. Sijawahi penda kama hivi.

Mambo ya kushangaza usioyajua kuhusu Wanawake na Wanaume BONYEZA HAPA>>>

SMS nzuri kwa mpenzi aliembali(mapenzi ya mbali)

Ni kawaida sana kuona  wapenzi wanaopendana kukutana na sababu mbalimbali zinazopelekea wapenzi hao kuwa mbali. Sababu hizi zinaweza kuwa ni kazi, masomo na mambo mengine katika maisha. Wapenzi ambao wako mbali au  wanaoishi mbali ni vema wakazingatia sana mawasiliano na kuonyeshana upendo katika mawasiliano. 

Hapa The Bestgalaxy leo tunakupa orodha ya jumbe fupi za mapenzi ya mbali zinazoweza kutumika katika kuwasiliana. Kama mahusiano yapo kwenye hali hii basi unaweza tumia jumbe hizi:

Jinsi ya kuwa romantic kwa mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

sms za mapenzi ya mbali

1. Umbali wowote kati yetu hauwezi kuuzima upendo wangu kwako Mpenzi. Kila siku nakuwaza na nazidi kukupenda tu huku natamani sana uwekaribu yangu.

2. Kukaa mbali na wewe ni kazi ngumu sana mpenzi wangu. Kuna muda natamani nije huko uliko niwe na wewe ila nikikumbuka kuwa kuna siku tutaonana, napata amani kidogo, Nakupenda sana.

3. Hata kama tuko mbali kimwili, moyo wangu daima uko nawe huko uliko. Nakupenda sana.

4. Napenda tunanyowasiliana, unanifanya nijisikie karibu nawe japo tuko mbali. Kichwa changu na moyoni mwangu bado upo wewe mpaka tutakapokutana tena.

5. Kuna malaika wa upendo nimenitokea na kuniambia kuwa penzi letu linapendeza. Umbali hauwezi kututenganisha mpenzi wangu, tuendele kuwa pamoja milele.

6. Usiruhusu shetani atumie mwanya wa sisi kuwa mbal,i kuua penzi letu. Penzi letu ni kubwa kuliko umbali wetu. Siwezi kukuona au kukugusa huko uliko ila tambua moyo wangu wote upo kwako.

Jinsi ya kutunza mahusiano ya Mbali BONYEZA HAPA>>>

7. Sikuizi nakosa joto lako tamu unalonipa pindi nikigusa mwili wako. Lakini bado nakupenda kwa nguvu zote. Jina lako limeandikwa ndani ya moyo wangu na haliwezi futika milele. Unaeweza fanya niumie au niendelee kufurahi ni wewe.

8. Moyo angu hulipuka kwa furaha kila tunapowasiliana. Hii ni kwasababu nakupenda na siku zinavyozidi kwenda, nazidi kukupenda leo kulio jana. Sipati picha nitakavyokua tukikutana.

9. Moyo wangu uko nawe, hata kama mwili wangu uko mbali na wewe. Umbali hauwezi yumbisha penzi langu  kwako. Nikishindwa kuvuilia nipo tayari kukufuata na sio kukuacha kipenzi changu.

10. Jukumu la kulinda penzi letu ni langu mimi na wewe mpenzi. Tunapokua mbali au karibu ni vema tukakumbuka jukumu letu mpenzi. Tusije ruhusu walioharibu mapenzi yao waalibu na yetu. Nakupenda sana.

Jumbe au sms kama hizi zinaweza kusaidia kuimarisha uhusiano wenu wa mbali na kumfanya mpenzi wako ajisikie kuthaminiwa na kupendwa. Pia ni vema kukumbuka kuwa mawasiliano ya mara kwa mara na jitihada za kukutana zinaweza kuwa na mchango mkubwa kwenye uhusiano wa mbali.

UTAMU WA JUMLA 🔞 (Simulizi ya sauti)

Simulizi ya UTAMU WA JUMLA ni simulizi yenye uhusiano kidogo na simulizi ya SUKARI YA DADA. Unaweza sikiliza simulizi hii ukiwa ndani ya The Bestgalaxy Bure kabisa na pia unaweza ipakua na kufurahia kwenye simu au kifaa chako. Sikiliza simulizi hii katika mazingira tulivu yatakayo ruhusu kuielewa kirahisi.

Katika kuisikiliza ukiwa kama msikilizaji hakikisha unazingatia umri maana simulizi hii haitakiwi kusikilizwa na mtu mwenye umri chani ya miaka 18.

kama umebonyeza na inachelewa kuanza basi huenda ni tatizo la mtandao wako. Jaribu mara kadhaa kwa kusubiri.

Sehemu ya 1
Sehemu ya 2
Sehemu ya 3
Sehemu ya 4
Sehemu ya 5
Sehemu ya 6
Sehemu ya 7
Sehemu ya 8
Sehemu ya 9
Sehemu ya 10
Sehemu ya 11 (mwisho)

Kupata taharifa ya simulizi mpya na mambo mwengine, hakikisha unatembelea The bestaglaxy kila mara na pia unaweza jiunga kwenye group letu la Whatsapp Bure.