Tag Archives: iOS

App za kuangalia Movies/Filamu mtandaoni kwa simu

Katika ulimwengu wa sasa unaweza angalia movie kwenye simu yako ya kiganjani ukiwa popote ulimwenguni. Mara nyingi watu wakitaka kuangalia movie huwa wanatembelea website/tuvuti zinajihusisha na movie/filamu au hutumia app zinazojihusisha na filamu ili kupata huduma ya movies. Kuna baadhi ya tuvuti au app hukuwezesha kupata huduma ya movie bure na nyingine huwa zinakuhitaji ulipie. Huduma za kulipia huwa ni bora zaidi na zinausalama zaidi ukilinganisha na baadhi ya huduma za bure japo zote ni nzuri.

Hapa Tha bestgalaxy leo tunakupa orodha ya app chache kati ya app nyingi unazoweza tumia kuangalia movie kwenye simu yako mtandaoni(online).

App za kuangalia movies online(mtandaoni)

Netflix

Hii ni app ya kampuni ya kimalekni, Netflix ambayo inayotoa huduma ya kuangalia movies/filamu kupitia Internet. Unaweza ingiza kwenye simu yako ya mkononi na kuanza kufurahia filamu kiganjani pako. Unaweza kuangalia filamu nyingi nzuri na maalufu duniani kupitia app hii. Lakini unachotakiwa kujua ni kwamba app hii ya netflix huwa haitoi huduma bure. Inaweza kukugharimu Tsh 7000 mpaka 23000(Makadilio).

ShowMax

ShowMax ni app inayotoa huduma ya kuangalia movies(filamu), michezo, vipindi vya TV na mambo mengine mengi, kiganjani pako. App hii inaweza kutumika kuangalia movie katika simu ya mkononi lakini sio bure pia. kufurahia huduma za app ya ShowMax utatakiwa kulipia kila mwezi. Kuna filamu nyingi unaweza angalia na pia kama ni mdau wa michezo, unaweza furahia michezo katika app hii. Kifurushi vyake vinaweza kugharimu Tsh 7800 mpaka 46000 kwa mwezi(Makadilio).

Youtube

Youtube ni app ambayo watu hutumia kuangalia video mbalimbali ambazo huwa zinapostiwa kwenye channel. Katika Youtube kuna channel ambazo hutuma filamu na unaweza angalia filamu hizo bure kabisa. Ukiachana na channel za filamu pia kuna kipengele cha Youtube kinachojihusisha na filamu tu(filamu za bure na kununua}. Kipengele hicho cha Youtube hakipatikani katika baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania kwa sasa ila unaweza soma maelezo ya kukuiona hapa chini.

Jinsi ya kuona kipengele cha movies cha YouTube Gusa hapa>>>>

Prime Video

App hii inaitwa “Amazon Prime Video” lakini kwa kifupi unaweza kuiita “Prime Video”. Ni moja ya app zinazoweza kukufanya ufurahie kuangalia movies na hata vipindi vya Tv pia kiganyani pako. Prime Video sio app ya bure lakini inakupa uwanja mpana unaofanana kiasi na netflix hivi katika filamu, unaweza angalia filamu nyingi maaalufu. Maelezo ya kiasi utakachotakiwa kulipa kwa mwezi yaliopo katika tuvuti yao yametaja kiasi kuwa ni USD 5.99 ambayo ni kama Tsh 14000 ivi…

~Viasi vya malipo vilivyo tajwa kwenye makala hii ni makadilio tu.