Tag Archives: internet

Jinsi ya kuongeza speed ya internet kwenye simu

Unasumbuliwa na speed ndogo ya internet? Usiwe na wasi tena! Hapa The Bestgalaxy tunakufungua juu ya nini unachoweza kukifanya kufurahia internet nyenye kasi kwenye simu yako ya smartphone.


Moja ya vitu ambavyo huudhi katika katika matumizi ya internet ni speed/ kasi ndogo. Speed ndogo ya internet sio tu huudhi bali pia hupoteza muda wa mtu anaetumia internet kwasababu kitu ambacho alitaka kukifanya kwa dakika 1 kwenye internet kinaweza mchukua mpaka dakika 5 ikiwa speed ya internet itakua ni ndogo. Watu wengi wanao thamini muda huchukizwa na swala hili.


Lakini tukirudi kufikilia kahusu historia ya internet utagundua internet imebadilika Sana na huwezi fanananisha na kipindi cha nyuma. Hata internet ya sasa isumbue vipi kwenye speed lakini huwezi ilinganisha na zamani maana huko nyuma internet ilikua haina kasi kabisa kama ya sasa. Kudownload nyimbo Moja tu yenye Mb 5 ilikua inaweza kukuchukua mpaka saa 1. Kama ni mtumiaji wa muda mrefu wa internet unaweza kuwa unajua kuhusu hili.

Yafuatayo ni mambo ambavyo Unaweza fanya kuongeza speed ya internet kwenye simu yako (hayahusishi matumizi ya WiFi)

WhatsApp yako inatatizo? Jifunze jinsi ya kutatua hapa>>>>

Namna ya kuongeza speed ya internet kwenye simu

1. Hakikisha unatumia laini ya 4G au 5G na Simu 4G au 5G

Kwasasa ukitaka kufurahia kasi nzuri ya internet basi inatakiwa iwe ni kuanzia kasi ya 4G. Ukitaka kufurahia kasi hii ya internet kwenye simu yako ya smartphone inatakiwa iwe na laini ya 4G na pia simu yako iwe ni ya 4G au 5G. Mbali na havyo pia ni vema “preferred network type” yako ikaiseti kwenye “Auto“. Kuiset preferred network type kwenye simu yako nenda kwenye “settings” ingia kwenye na uende katika “Network & internet” alafu ingia kwenye “SIM cards” kisha ingia kwenye “Mobile network“. Baada ya hapo gusa “Preferred network type” na uchague “Auto“.

2. Hamia kwenye mtandao wa simu wenye huduma ya internet yenye kasi.

Kuna muda mtu anaweza kuwa unakumbana na changamoto ya kasi ndogo ya internet katika matumizi ya internet kutokana na mtandao wa simu unaokupa huduma ya internet kutokua vizuri katika maeneo uliopo. Jaribu kufanya utafiti kwa watu uwalio kuzunguka ili kujua mtandao wanotumia kupata internet na speed yake ya internet iko vipi. Unaweza tu kuwaambia watu “Mimi ninatumia mtandao flani kupata huduma ya internet lakini naona Kama haupo vizuri Sana katika speed kwenye maeneo haya… Ivi ni mtandao gani nyinyi mnautumia na upo vizuri?”

Fanya haya kabla simu yako haijaibiwa ili kuipata ikiibiwa GUSA HAPA>>>


Kama kutakua na mtandao wanao sema upo vizuri basi jaribu na uangalie kama utakua vizuri kwako pia. Unaweza pia wasiana na watu wanao husika na mtandao wako wa simu na kuwataalifu kuhusu Jambo unalopitia kwenye eneo lako ili warekebishe. Tena bahati nzuri ni kwamba sikuizi makampuni ya mitandao ya simu ina kurasa zake katika mitandao ya kijamii na Unaweza watumia ujumbe kule na wakakujibu.

3. Boost speed ya internet kwa kuwasha “Flight mode” na kuizima.

Kama speed yako ya internet inasubua subua wakati unaitumia unaweza kuwa unaiboost kwa kuwasha “Flight mode” na kuizima. Flight mode huwakilishwa na kialama Cha “ndege ya usafiri” na hupatikana katika kisehemu Cha simu unachokifuata pindi unapo washa Data kwaajili ya kuanzia kutumia internet.

4. Tumia app zinaweza ongeza Speed ya internet.

Kuna baadhi ya app za VPN zinaweza ongeza speed ya internet. Hii inaweza onekana zaidi unapo download vitu au ku-stream vitu online ukiwa unatumia VPN. Lakini app za VPN zipo maalum kwaajili ya kuufanya muunganiko wako wa internet uwe salama na si kuongeza speed. Na pia sio kila unapotumia VPN utapata internet yenye kasi, VPN zinaweza pia kupunguza kasi kabisaa.

Mbali na app za VPN pia Kuna app zinazohusisha zaidi DNS zinaweza kuongeza kikasi Cha internet unapotumia. Mfano mzuri ni app iitwayo WARP… Unaweza ijaribu kwuingiza kwenye simu yako ya Android kwa lugusa hapa au iPhone kwa kugusa hapa

Njia 3 za kutumia intaneti bila malipo kwenye simu ya Android au iPhone

Katika mabilioni ya watu wanaotumia internet ama mtandao kila mwaka na watu wengi kati yao wanaotumia Simu. Na siku hizi, watumiaji wengi wa simu wanatumia simu za Android na iOS. Mambo mengi ambayo watumiaji wa simu za Android au iOS wanapenda kufanya kwenye simu zao yanahusisha kutumia intaneti.

Wanatumia intaneti kwenye mambo kama vile kushiriki habari, kujifunza, kuendesha biashara zao, kupata burudani na zaidi. Kwa vile sote tunajua kwamba mtandao sio bure, inagharimu watumiaji kiasi cha pesa kununua bando za internet au kulipia huduma za internet. Lakini bado kuna nini cha kufanya ili kutumia wa internet bure kwenye simu.

Ukiona dalili hizi Jua Account yako ya Facebook  imedukuliwa na si salama GUSA HAPA>>>>

Pata BAND0 kubwa la internet Kwa Bei rahisi GUSA HAPA>>>

Ikiwa wewe ni mmoja wa watu wanaotumia simu yoyote ya Android au iPhone na unahitaji kutumia intaneti bila malipo basi hapa chini kuna kinachoweza kufanya ili kupata intaneti bila malipo.

Njia za kupata intaneti ya Bure kwenye simu ya Android na iPhone


  1. Unaweza unganisha simu yako Kwenye huduma za Wifi za bure zinazopatikana kwenye mazingira yako… unaweza tafuta sehemu zilizio na huduma ya WiFi kitahisi kwa kutumia App yako ya Facebook. App ya Facebook inakipengele kinachokuonesha maeneo yenye huduma za WiFi katika eneo ulilopo.
  2. Unaweza pata ofa au zawadi za interneti ambazo hutolewa bure na kampuni inayokupatia huduma ya internet (mfano Tigo: Ukituma neno “BURE” au “Social bonus” kwenda Namba 15166 unaweza zawadiwa Mb za internet BURE..
  3. VPN pia inaweza tumika kupata internet bila malipo… lakini njia hii imewekwa hapa Kwa lengo la elimu tu na si vinginenyo. Unaweza soma moja ya makala zetu zinazohusisha njia hii HAPA>>>>>

Magroup ya WhatsApp ya kujiunga bure GUSA HAPA>>>

Kwanini bando lako la wiki la internet huisha ndani ya siku Moja/mbili?

Kwasasa katika dunia matumizi ya internet yameongezeka. Na inaonesha yatazidikuongezeka zaidi ya hapa maana baadhi ya huduma na vitu vilivyokua havihusiani na internet vimekua vinategema internet Kwa sasa. Mfano mzuri ni magari ya kisasa yanayotoka kipindi hiki. Mengine yanatumia internet kukupa huduma ya redio na vitu vingine. Yani huwezi sikiliza redio ya gari bila internet. Hebu tuachane na ulimwengu na tuingie Tanzania Sasa.

Ni wazi kuwa Kuna watu wanatumia sana internet na vifurushi vya internet Kwa hapa Tanzania vinaweza kukughalimu hata za zaidi ya 2000 Kwa GB 1(inategemea na kifurushi). Katika kununua vifurushi na kutumia internet, Kuna baadhi ya watu hununua vifurushi vya internet vya wiki lakini huvimaliza kabla ya wiki na hawajui ni Kwanini. Hiki sio kitu kukubwa kama hakikuumizi kwenye sawala la pesa lakini kama kinakuumiza basi hapa ntakujuza ni kwanini ipo hivyo na hatua gani unaweza kuchukua.

Jinsi ya kufanya simu isiishe chaji haraka GUSA HAPA>>>

Pata bando za internet Kwa Bei rahisi (Tigo & Halotel) GUSA HAPA>>>>

Kwanini bando la wiki la internet linawahi kuisha kabla ya wiki?

Kiufupi ni kwamba kitu kinacho maliza bando mara nyingi ni “matumizi”. Ukiwa na Mb 50 ikiingia kwenye internet na kutumia au zikatumika Mb 50, utabakiwa na Mb 0 hata kama ulipewa zikae mwezi. Ni mahesabu tu.

Ukiwa unamatuzi ya internet yanayotumia Mb nyingi basi utahitaji Mb nyingi ili uzitumie sio sinazokaa sana. Hata ununue bando la mwaka mzima, kama matumizi yako ni makubwa kuliko hilo bando au Mbs ulizonazo, utamaliza kabla ya huo mwaka kuisha.

Jinsi ya kufanya simu ijinunulie bando la internet (usichome pesa zako kununua bando) GUSA HAPA>>>

Kwani watu hutumia bando kiasi gani?

Kwa watumiaji wa Smartphone (Tz) wengine wanaweza kutumia Mb 200 kwa siku na kunawatu hufia hadi Gb 1, G 2 au zaidi. Hii hii pia hutegeana na “matumizi” ya mtu.
Kuna watu ambao hutumia internet kuangalia movies, kucheza magemu (cloud games) au wapo internet kikazi. Watu hawa hata GB 2 mbili zinaweza kuwa ndogo kwao Kwa siku.
Mbali na watu hao kunawatu wanamatumizi ya kawaida tu. Inawezakua wanatumia kupata nyimbo mpya, habari, matokeo ya michezo na vitu vingine kama hivyo. Watu wanye matumizi haya wanaweza kutumia chini ya Mb 500 japo wanaweza vuka hapo pia.

Nifanye nini ili kutomaliza bando la internet Kwa haraka?


Kama unataka usimalize bando lako la internet Kwa haraka basi inabidi uanze kujichunga kwenye matumizi maana maranyingi matumizi ndio hulimaliza bando.
Kama ni mtu wa movies basi punguza kuangalia movies au videos unazoangalia kwa siku.
Jizuie kutumia internet sana kama bando linaumiza pesa yako.
Ingiza vitu kama offline games au vichekesho na vitu vingine ambayo vitakua vinakufurahisha kwenye simu yako bila kuwasha data. Mfano wa vitu vingine ni Simulizi. Unaweza ukawa unanunua simulizi za kusoma kwenye simu yako alafu unakua unasoma kidogo kidogo ukiwa na muda.
Hayo ni machache niliokuandalia kwenye makala hii inayohusu internet. Tutakutana kwenye makala nyingine Lakini usiache kufuatilia The Bestgalaxy ili kujifunza mengi zaidi.