Tag Archives: cryptocurrency

Cryptocurrency: Jinsi ya kupata zaidi ya “100 USDT” bila kutoa pesa zako

Cryptocurrency ni aina ya sarafu ya kidijitali (digital currency) ambayo hutumika kama njia ya malipo au uwekezaji mtandaoni. Mfano wa cryptocurrency ni Bitcoin (BTC), Ethereum (ETH), Binance Coin (BNB), Solana (SOL), na Tether (USDT).
Tofauti na pesa tulizozoea kama Shilingi au Dola, cryptocurrency haipo katika mfumo wa karatasi (yote ipo kidigitali).

Njia ya haraka zaidi ya kupata cryptocurrency ni kununua au kubadilisha (exchange) kwa kutumia pesa zako za kawaida. Thamani ya sarafu hizi hubadilika kulingana na soko.
Kwa mfano, USDT (Tether) ni moja ya cryptocurrency zenye thamani inayofanana na Dola ya Marekani.
1 USDT ≈ Tsh 2,400, kwa hiyo ukiwa na 100 USDT unakua na thamani ya takriban Tsh 240,000.

Lakini je, unaweza kupata zaidi ya 100 USDT bila kutoa hata senti kutoka mfukoni mwako?

Habari njema ni kwamba, inawezekana!

Jinsi ya Kupata Zaidi ya “100 USDT” Bila Kutoa Pesa Zako

Njia rahisi na halali ya kupata USDT bila kutumia pesa yako ni kupitia platform zinazokupa USDT kwa kufanya jambo fulani.
Mfano mzuri kwa sasa ni Opera News Hub, ambayo ni platform/jukwaa linalomilikiwa na kampuni ya Opera.

Kwenye Opera News Hub:

  • Unaandika au kutengeneza content (habari au makala).
  • Ukifanya vizuri, unapewa USDT kupitia MiniPay Wallet.
  • Baada ya hapo unaweza kuamua kutunza USDT kama mali (asset) au kuibadilisha kuwa pesa za kawaida.

Kwa kifupi:

  1. Tafuta platform inayolipa kwa kukupa USDT (mfano: Opera News Hub).
  2. Fanya kazi inayohitajika (andika au tengeneza content bora).
  3. Pokea USDT wanazokupa kwenye wallet yako.
Wallet ya MiniPay

Kuna maplatform mengi duniani yanayolipa kwa kwa kukupa cryptocurrency, lakini Opera News Hub ni rahisi zaidi kuelewa na kutumia ukiwa Afrika Mashariki.
Hata kama utakua ukipata kiasi kidogo, ukijituma na kutunza USDT zako, unaweza kufikisha zaidi ya 100 USDT baada ya muda bila kutumia pesa zako za kawaida.

Disclaimer: This article is for education only and is not financial advice. Always do your own research before making any decisions.

Jinsi ya kutengeneza Pesa katika Opera news hub BONYEZA HAPA>>>

Unataka kujua Cryptocurrency ni nini? Jifuze hapa



Kiufupi Cryptocurrency ni sarafu au pesa ya kidigitali ambayo mtu anaweza kutuma au kuipokea mtandaoni lakini huwa ipo huru kwa kutokua chini ya Benk kuu au serikali. Ni watu tu huamini na kuanza kuitumia au kuacha kutumia. Na hauwezi kuigusa kama pesa za kawaida maana ipo mtandaoni tu.

Sarafu hii ya kidijitali (digital currency) inatumia mbinu za usalama za kisasa (cryptography) ili kuhakikisha miamala (transactions) ni salama na kudhibiti uundwaji wa sarafu mpya(bandia. Unaweza kuzituma pesa hizi kwa mtu kama malipo au ukazipokea na kuzitunza kama ilivyo kwenye pesa za kawaida.

Cryptocurrency(pesa za mtandaoni) huwa zipo nyingi na zina majina tofauti. Mfano wa cryptocurrency maalufu duniani ni:

  1. Bitcoin (BTC)
  2. Ethereum (ETH)
  3. Binance Coin (BNB)
  4. Tether (USDT)

Unatunza vipi Cryptocurrency?



Cryptocurrency huwa zinatunzwa katika mfuko maalum wa pesa za kidigitali. Mfuko huu huitwa  “digital crypto wallet” na hufanya kazi kama sehemu unayoweza kutunza pesa zako kidigitali au kufanya miamala. Mtu alieweka cryptocurrency kwenye digital crypto wallet ni sawa mtu alieweka pesa za kawaida katika Bank au akaunti nyingine za pesa kama Mpesa.

Kuna platform nyingi mtandaoni huwa zinakuwezesha mtu kufungua akaunti na kumiliki mfuko wako wa kuwekea Cryptocurrency Bure kabisa. Mfano wa platform hizo ni Binance.

Mtu alieweka cryptocurrency kwenye digital crypto wallet kama Binance ni sawa mtu alieweka pesa za kawaida katika Bank au akaunti nyingine za pesa kama Mpesa.

Jinsi ya kutengeneza Pesa mtandaoni kwa kuandika BONYEZA HAPA>>>

Unawezaje kupata Cryptocurrency?





Kama na wewe unahitaji kuwa na pesa za crypto, utahitajika kuwa na mfuko kwanza wa kutunzia(crypto wallet). Baada ya hapo unaweza tumia njia hizi mbili za kupata Cryptocurrency kwenye mfuko wako:



Njia ya kwanza ya kupata Cryptocurrency ni kuzinunua kwa pesa zako za kawaida. Yani unatumia pesa yako ya kawaida kuinunua pesa ya mtandaoni (cryptocurrency) alafu unaitunza kwenye mfuko wako wa crypto. Hii tunaweza kuiita “kubadilishana na pesa za kawaida”, yaani exchange. Mfano; Ukitaka kupata USDT moja (1), utatakiwa kuwa na kama Tsh 2600 (makadilio). Ukitaka BITCOIN moja (1), unaweza kuipata kwa Tsh milioni 200 na zaidi.

Thamani za huwa zinatofautiana alafu pia huwa zinapanda na kushuka. Mbali ya hilo, fahamu tu kuwa Kuna zenye thamani ndogo  na kuna zenye thamani kubwa pia.

Njia ya pili ni kutoa huduma au kufanya huduma itakayokupa au kukulipa kwa cryptocurrency. Kuna huduma unaweza kutoa mtandaoni alafu ukapewa cryptocurrency kama malipo bila kutumia pesa yako ya kawaida. Mfano wa huduma hizi ambayo ni rahisi kabisa ni huduma ya Opera news hub ambayo tumeizungumzia sana kwenye Makala za The Bestgalaxy.

Watu wengi wanatumia cryptocurrency kulipia vitu au kufanya biashara mtandaoni kwa sasa lakini Teknolojia yake ipo kwenye hatua ya ukuaji na maboresho. Huwa inaaminika kuwa cryptocurrency inaweza kuwa ndio pesa zitakazokua zinatumiaka katika miaka ijayo badala ya kutumia pesa za kawaida.

Mambo gani muhimu ya kujua kuhusu cryptocurrency?





Pamoja na yote, Kuna changamoto ambazo kila mtu anapaswa kujua kabla ya kuingia kwenye ulimwengu wa crypto. Kati ya Changamoto kubwa ni zifuatazo:

Usalama wa crypto ni mdogo kuliko pesa za kawaida. Usipokua na kuelewa mzuri, unaweza kutapeliwa kirahisi kutokana na wingi wa matapeli katika upande huu.


Cryptocurrency zinaweza kushuka thamani muda wowote. Yani unaweza kutuza cryptocurrency zako Leo zenye thamani ya milioni 1, alafu kesho ukaamka na kukuta zimeshuka thamani kutokana na jambo flani, zomekua ni laki 5. Kwaiyo kwenye ulimwengu huu unatakiwa kuwa mtu unaweza ku-manage risk.


Cryptocurrency huwa haiwezi kulipia vitu vingi sana kwenye maisha ya kawaida. Kuna huduma nyingi ambazo Bado hazijaitambua cryptocurrency katika malipo kwasababu mbalimbali.

Disclaimer: This article is for education only and is not financial advice. Always do your own research before making any decisions.