Katika ulimwengu wa sasa unaweza angalia movie kwenye simu yako ya kiganjani ukiwa popote ulimwenguni. Mara nyingi watu wakitaka kuangalia movie huwa wanatembelea website/tuvuti zinajihusisha na movie/filamu au hutumia app zinazojihusisha na filamu ili kupata huduma ya movies. Kuna baadhi ya tuvuti au app hukuwezesha kupata huduma ya movie bure na nyingine huwa zinakuhitaji ulipie. Huduma za kulipia huwa ni bora zaidi na zinausalama zaidi ukilinganisha na baadhi ya huduma za bure japo zote ni nzuri.
Hapa Tha bestgalaxy leo tunakupa orodha ya app chache kati ya app nyingi unazoweza tumia kuangalia movie kwenye simu yako mtandaoni(online).
App za kuangalia movies online(mtandaoni)
Netflix
Hii ni app ya kampuni ya kimalekni, Netflix ambayo inayotoa huduma ya kuangalia movies/filamu kupitia Internet. Unaweza ingiza kwenye simu yako ya mkononi na kuanza kufurahia filamu kiganjani pako. Unaweza kuangalia filamu nyingi nzuri na maalufu duniani kupitia app hii. Lakini unachotakiwa kujua ni kwamba app hii ya netflix huwa haitoi huduma bure. Inaweza kukugharimu Tsh 7000 mpaka 23000(Makadilio).
ShowMax
ShowMax ni app inayotoa huduma ya kuangalia movies(filamu), michezo, vipindi vya TV na mambo mengine mengi, kiganjani pako. App hii inaweza kutumika kuangalia movie katika simu ya mkononi lakini sio bure pia. kufurahia huduma za app ya ShowMax utatakiwa kulipia kila mwezi. Kuna filamu nyingi unaweza angalia na pia kama ni mdau wa michezo, unaweza furahia michezo katika app hii. Kifurushi vyake vinaweza kugharimu Tsh 7800 mpaka 46000 kwa mwezi(Makadilio).
Youtube
Youtube ni app ambayo watu hutumia kuangalia video mbalimbali ambazo huwa zinapostiwa kwenye channel. Katika Youtube kuna channel ambazo hutuma filamu na unaweza angalia filamu hizo bure kabisa. Ukiachana na channel za filamu pia kuna kipengele cha Youtube kinachojihusisha na filamu tu(filamu za bure na kununua}. Kipengele hicho cha Youtube hakipatikani katika baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania kwa sasa ila unaweza soma maelezo ya kukuiona hapa chini.
App hii inaitwa “Amazon Prime Video” lakini kwa kifupi unaweza kuiita “Prime Video”. Ni moja ya app zinazoweza kukufanya ufurahie kuangalia movies na hata vipindi vya Tv pia kiganyani pako. Prime Video sio app ya bure lakini inakupa uwanja mpana unaofanana kiasi na netflix hivi katika filamu, unaweza angalia filamu nyingi maaalufu. Maelezo ya kiasi utakachotakiwa kulipa kwa mwezi yaliopo katika tuvuti yao yametaja kiasi kuwa ni USD 5.99 ambayo ni kama Tsh 14000 ivi…
~Viasi vya malipo vilivyo tajwa kwenye makala hii ni makadilio tu.
Katika matumizi yako ya simu za Smartphone unatakiwa kuelewa kwamba vifaa hivi vinaweza kudukuliwa na mtu mwingine na kufanya mdukuzi au huyo mtu apate uwezo wa kuona vitu vilivyomo au vitu unavyofanya kwenye simu yako bila yeye kuigusa simu yako. Mbali na kuona vitu unavyofanya au ulivyohifadhi, Mtu aliedukua simu yako pia anaweza kuwa na uwezo wa kuitumia simu yako bila kuigusa… Mfano wa vitu anavyoweza kuvifanya ni kuitumia simu yako kutuma sms kwa mtu mwengine, kuitumia camera yako kuangalia unachokifanya, kuvujisha vitu vyako au kukuzuia kufanya baadhi ya vitu kwenye simu yako.
Lakini ukiwa kama mtumiaji wa smartphone wa miaka hii, hutakiwi kuwa na hofu sana juu ya hili kwani kunaviashilia vya kuangalia kwenye simu yako ili kujua upo salama au vipi. Hapa The beestgalaxy tutakupa mwanga juu ya jinsi ya kuangalia simu yako ya Android kama imedukuliwa na inafuatiliwa/inachunguzwa na mwingine.
Jinsi ya kuangalia kama simu yako inafuatiliwa/inachunguzwa na mwingine
katika matumizi ya simu watu huwa wanapenda kuingiza apps nyingine mbali mbali ukiachana na zile ambazo huwa wanazikuta tayari zipo kwenye simu. Kitu unachotakiwa kujua hapa ni kwamba kuna Program au apps ambazo unaweza kuingiza kwa bahati mbaya au ukaingiziwa kwenye simu yako na zikiwa kwenye simu yako zinakua zinatumika na mtu mwingine huona au kufanya vitu kwenye simu yako bila kuigusa.
Endapo katika simu yako kutaingizwa apps hizi kwa makusudi au bahati mbaya, simu yako itakua sio salama tena maana vitu. Lakini kitu kizuri ni kwamba kwenye sikuizi kwenye simu za Android kuna program inaitwa “Google play protect”. Program hii inamilikiwa na google na kazi yake kubwa kwenye simu ni kukulinda dhizi ya apps hatari unazoziingiza kwenye simu yako. Kama kuna app yoyote inayoweza kuwa hatari umeiingiza, Google play protect huwa inatoa taharifa na kukushari cha kuifanya. Unaweza kuitumia Google play protect kuangalia kama angalia kama simu yako ni salama au si salama. Unachotakiwa kufanya ni kufuata hatua hizi chini.
Chukua simu yako na uingie katika app ya Play store
Baada ya hapo, gusa kiduara cha profile yako na uchague “Play protect“
Bonyeza kitufe kilichoandikwa “Scan” na baada ya hapo Google play protect itaanza kuangalia kama kuna app zozote hatari kwenye simu yako alafu itakupa majibu.
Kama kutapatikana app yoyote hatari utaonyenshwa app hiyo alafu utashauriwa kuiondoa kwenye simu yako kwa kugusa kitufe cha “Uninstall“.
Google play protect ni njia nzuri na rahisi ya kuangalia kama simu iko salama ukiwa kama mtumiaji wa kawaida lakini huwa haikuhakikishii usalama kwa 100%.
Google play protect ikiwa “Active” kwenye simu yako huwa inatafuta na kulinda hii ya app hatari. Na endapo itakuta app harari imeingizwa au unataka kuiingiza kwenye simu yako, itakupa taharifa.
Mbali nna kutumia Google play protect kuangalia kama simu yako iko salama unaweza pia kujua kuwa simu kwa kuangangalia kama kwenye simu yako kuna vitu vifuatavyo.
Angalia orodha ya app zinazotumia sana internet na kama utakuta app ambayo haieleweki na hauitumi lakini ipo juu kwenye matumizi ya bando, inawezakua ni app hatari. Kama kamera ya simu yako ukiifungua inakuandikia “Camera is being used by another application” au “You cannot use more than one application that uses camera” au “Camera may be in use by another application” hiyo inaweza kuwa ni ishara ya kwamba simu yako sio salama. Mbali na hayo, kukuta vitu ambanyo haujavifanya lakini vimefanyika kunaweza kuwa kiashiria cha hatari pia.
Mpira wa miguu ni mchezo maarufu zaidi duniani. Hapa tutajadili kuhusu magemu ya mchezo huu maarufu. Katika ulimwengu huu, mbali na kutazama mechi ya moja kwa moja za mpira wa miguu, kuna watu wengi wanaopenda kucheza magemu ya mpira au Kandanda. Kuna ambao wanapenda kucheza magemu kupitia vifaa vya kucheza magemu kama vile, Playstation . Na watu wengine hutumia simu kucheza magemu ya mpira wa miguu.
Unaweza pia kuwa mmoja wa watu wanaotumia simu kwenye michezo ya mpira wa miguu ndio maana uko hapa. Ikiwa wewe ni mmoja wao basi hapa ni sahemu nzuri kwako. Tunakupa orodha ya gemu 5 bora za Mpira unazoweza kucheza kwenye simu (Android) Bila kupoteza muda wako, sasa twende moja kwa moja kwenye orodha ya magemu bora ya mpira au soka kwa simu ya Android.
FIFA Mobile ni mojawapo ya magemu bora ya Soka ya Android kwa mashabiki wa soka. Gemu hili limetolewa na EA. Huchezwa Kwa kutumia Data, yaani huitaji internet. Katika gemu hili unaweza kujenga timu yako ya ndoto na kuanza safari ya soka. Na unaweza kuijenga kwa kusajili superstars unaopenda katika soka. Linakuruhusu kucheza au kushindana na watu wengine mtandaoni.
Gemu hili hapo awali ulilitwa “PES” lakini sasa ni “eFootball“. Kwa hivyo, ikiwa wewe ni moja ya watu ambao tayari umecheza magemu ya PES, basi hii pia ni PES lakini PES imebadilishwa jina kuwa eFootball. Kwenye orodha hii ya mgemu bora ya mpira ya simu za Android, tunaongeza gemu hili kwasababu ni gemu nzuri. Muonekano kwenye gemu hili ni mzuri. Ili kucheza gemu la eFootball kwenye simu ya Android unahitaji kutumia intaneti. Kwa maneno mengine tunaweza kusema gemu hili hutumika Data japo ni bure kupakua na kucheza. Simu yako lazima iwe na zaidi ya 2G RAM, Android 7 na 3.3GB ya nafasi ili kuwa na gemu la eFootball bila matatizo. Pia ikiwa na CPU 1.5 GHz au zaidi itaifanya ifanye kazi vizuri zaidi.
3. Dream league Soccer.
Dream league Soccer (DLS) ni gemu lingine la mpira au soka linaliweza kucheza kwenye simu simu. Gemu hili lilitolewa na First Touch games limited. Katika gemu hili unaweza kuunda timu yako ya ndoto na kusaini wachezaji wako unaowakubali wa mpira wa miguu kwenye timu yako. Internet huitajika ili kucheza gemu hili kwa sababu ni DSL ni gemu linalihitaji data kulicheza. Lakini kulipakua na kuicheza ni bure ingawa ukihitaji, unaweza kununua baadhi ya vitu ndani ya gemu kwa pesa halisi.
Total Football ni gemu lililotolewa mwaka 2022 (Beta). Gemu hili huchezwa Kwa kutumia Data/internet japo ukiwa Haina data unaweza kunavitu unaweza kuvifanya kwenye gemu na vikakufurahisha. Studio Vega Private Limited ndio wamelitoa gemu hili. Kwenye gemu hili unaweza kuunda timu yako, kusaini wanasoka mashuhuri kisha kuipeleka timu yako kileleni. Jumla ya mchezo wa Kandanda ni mzuri sana na ni bure kuucheza na Kupakua kwenye simu ya Android.
5. Pro League Soccer.
Ikiwa unataka gemu zuri la Android ambao haliwezi hata kuchukua nafasi kubwa ya simu, gemu hili ni kwa ajili yako. Pro League Soccer ni gemu la simu la mpira was miguu ambalo ni dogo kuliko tulioyataja juu. Unaweza kuona gemu hili ni tofauti na magemu kama vile FIFA au eFootball lakini inafurahisha sana kulicheza. Linakuruhusu kuandika majina ya wachezaji na hata kutengeneza Jezi unavyotaka. Mojawapo ya jambo zuri ni kwamba, gemu la hili linaweza kuchezwa bila internet.
Hivi ndivyo tunamaliza orodha hii. Lakini kumbuka kuwa kuna zaidi ya magemu ma 5 bora ya mpira kwa simu za Android ingawa tume orodhesha magemu matano pekee.
Ikiwa unataka kujua zaidi kuhusu magemu ya simu na vitu vingine basi usisahau kutembelea tovuti hii kila siku. Daima tuko hapa kukufahamisha mambo mengi.
Tukizungumzia magemu ambayo watu hupenda kuyacheza basi hatuwezi acha kuyataja magame ya magari. Magemu ya magari yamekua yakipendwa na watu wengi sana Duniani kwakua ni magemu mazuri Sana na humfanya mchezaji afurahie uchezaji wake. Hapa nimekuandalia orodha fupi ya magemu mazuri ya magari unayoweza kuyacheza kwenye simu yako ya Android.
1. Real Racing 3
Kama unapenda magemu mazuri na bora ya magari hakikisha haukosi game la Real Racing 3 katika simu yako. Gemu hili huchezwa Online na Offline yaani unaweza cheza kwa kutumia data au bila data. Ukitumia data(Online) utakua ukishindana na watu halisi wanao cheza gemu hilo muda huo katika nchi mbalimbali hivyo kila gari utakaloliona humo jua linaendeshwa na mtu alieshika simu kama wewe. Kama ilivyo kawaida ya magemu ya online, gemu hili linamuonekano mzuri sana uliobeba uhalisia wa mashindano ya magari. Kuna aina nyingi sana za magari mazuri na yenye kasi Sana. Linakupa uwezo wa kubadili kamera utakavyo. Real Racing 3 ni moja ya magemu yapatikanayo playstore na hupatikana kwa MB 40 tu lakini ukishalipakua na kulifungua utatakiwa ulisubiri lipakue data zake na inashauriwa uwe na nafasi isiopungua Gb2.5. Unaweza kulipakua kirahisi kwa kugusa INSTALL
Ni gemu zuri sana la magari lililochini ya Gameloft. Gemu hili limetengenezwa likiwa kama ni muendelezo wa magemu ya Asphalt.Katika orodha ya magemu ya magari yenye ubora wa hali ya juu katika muonekano, hauwezi acha kuliweka gemu hili kwakua linamuonekano mzuri Sana.Gemu hili huchezwa Online yaani kwa kutumia data pia huchezwa offline nikiwa na maana bila kutumia data.Ukitumia data(Online) utakua ukishindana na watu halisi wanao cheza gemu hilo muda huo katika nchi mbalimbali.Gemu la Asphalt 8 airborne hupatikana playstore kwa GB 1.6 na unaweza kulipata kirahisi kwa kugusa INSTALL
3. Drift Max Pro
Ni gemu la magari ambalo mpaka sasa linachezwa na zaidi ya watu milioni 50 ulimwenguni. Gemu hili linahusu mashindano ya kuyaburuza magari. Pia lipo vizuri kwenye upande wa ubora wa muonekano ukilinganisha na baadhi ya magemu mengine ya magari.Kama unapenda kushindana online na watu toka sehemu mbalimbali za dunia basi gemu hili pia linakupa nafasi ya kucheza na watu wengine online. Hupatikana kwa MB 361 katika Playstore na unaweza kulipata kirahisi kwa kugusa INSTALL
GT Racing 2 ni gemu lingine toka Gameloft ambalo unaweza kulicheza bure kabisa na bila kutumia data (Offline) lakini pia kama utahitaji kushindana na watu wengine toka sehemu mbalimbali za dunia kutika kuendesha magari basi utalazimika kutumia data. Gemu hili mpaka sasa limechezwa na watu wengi sana hapa duniani na wamelisifu kuwa ni lenye muonekano mzuri na linawafanya wahisi uhalisia wa mchezo wa magari.Linapatikana playstore kwa GB 1.1 na unaweza kulipata kirahisi kwa kugusa INSTALL
5. Asphalt 9 Legends
Hili ni gemu toka kwa watiotengeneza gemu la Asphalt 8 airborne na limetengenezwa kama muendelezo wa magemu ya Asphalt. Linaweza chezwa na kila mtu kwasababu lina Controls nyepesi kiasi ambacho hata mtoto mdogo anaweza kuzielewa. Katika gemu hili kuna gari za nyingi na zenye kasi sana. Mpaka sasa linachezwa na watu zaidi ya milioni 50 na wengi hulipenda kwasababu linamuonekano bora.Huchezwa kwa kutumia data na linakukutanisha na watu toka sehemu mbalimbali za dunia ili kushindana katika kuendesha magari. Hupatikana playstore na unaweza kulipata kirahisi kwa kugusa INSTALL
Wengi tumekua tukitumia WhatsApp katika kuwasiliana na ndugu na jamaa zetu kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Pia tumekua tukijiunga katika Magroup (Vikundi) ambavyo nia na madhumini yake ni kutujumuisha kwa pamoja ili tuweze kujadili au kubadilishana mambo mbalimbali. Kuwa na group si tatizo ila tatizo huja pale group linapokuwa na watu wengi wanaochati kipindi wewe hauna muda wa kuchati kutokana na sababu mbalimbali na kukupelekea kuona sms za wengine kuwa kero kwakua huingia kwa kelele mfululizo. Kama unagroup ambalo husababisha kelele kutokana na message zake, unaweza lifanya yafuatayo ili kulifanya liingize message kimya kimya;
Nenda katika ukarasa wako wa WhatsApp kisha lishikilie group lenye kelele kwa muda usiopungua sekunde tatu Kama inavyooneshwa hapo chini.
Ukishikilia kwa muda wa sekunde tatu group litajipiga tiki na maeneo ya juu ya WhatsApp kutatokea chaguzi: katika chaguzi hizo utaona alama ya spika iliokatwa. Alama hii inamaanisha kulikarisha kimya group hivyo utaigusa alama hiyo kama picha inavyokuonesha hapa chini.
Baada ya kuigusa alama hiyo utaletewa chaguzi uchague group hilo liwekimya kwa muda gani kwaiyo utachagua masaa8, wiki 1 au milele kisha utagusa neno “Ok” kama inavyooneshwa katika picha.
Baada ya kufanya hayo utakua umetatua tatizo la kelele maana sms za group hilo zitakua zinaingia kimya kimya. Na unachotakiwa kujua ni kwamba kama utachagua masaa8 basi baada ya masaa8 group litakua linaingiza sms kwa kelele kama kawaida na hata ukichagua wiki, wiki likiisha kelele zitakua palepale ila ukichagua milele hutaskia kelele za group hilo mpaka utakapo lishikilia tena group hilo na kugusa kialama cha sipika isiokatwa ili kuliweka huru. Kama ni mtu ambae unamagroup mengi au unamagroup ya ajabu ajabu unaweza tumia njia hii kuepuka kelele na kulifanya group lisije kuleta taalifa za sms za ajabu ajabu.
Kama ni mpenzi wa muda wa kuangalia mpira wa miguu wa nje ya nchi, nadhani umeshawahi kosa kuangalia mechi ulioipania kwasababu mbalimbali ikiwemo kuwa mbali na Tv. Teknolojia inazidi kukua kila siku na kuturahisishia mambo. Sasa unaweza angalia mechi Kali za mpira wa miguu kupitia simu yako mubashara(Live) ukiwa popote. hapa tutakujuza jinsi ya kuangalia mpira wa nje karibu mechi zote kwenye simu yako BURE.
Ikiwa unahitaji kuangalia mpira live kwenye simu yako, utahitajika kuwa na app maalumu kwaajili ya kuangalizia mpira. App hizi zipo nyingi sana katika playstore(Android) lakini mimi nakushauri uchukue app nyepesi na isiokula sana Mbs iitwayo Live Football Tv.
App ya Live Football Tv ni app ya kuangalia mpira live kwenye simu yako. Mpaka Sasa inatumiwa na zaidi ya watu Milioni ulimwenguni na wanaisifu kwa kuonesha mipira mingi bila matatizo. Mbali na kukuonesha mechi live(mubashara), huwa inakupa matokeo na video za matukio muhimu ya mechi zilizomalizika kwaiyo Kama haukua na bando la kutosha kuangalia mpira mzima, unaweza angalia video ya goli lilivyofungwa tu. Pia inakupa nafasi ya kuangalia vipindi vingine vya kimichezo bure toka Ptv sports.
App hii ya kuangalia mpira live haipatikani Playstore kwasasa ila unaweza kitafuta Google na kuipakua. Pia Unaweza ipakua kirahisi kwa kugusa hapa>>> INSTALL. Na baada ya kuipakua, hauitajiki kujisajili au kufanya Jambo lolote la kujiunga ili kuitumia. Ni kuifungua na kuinjoi…
Fahamu kuwa: App nyingi zinazowezesha kuangalia mpira bure huendelewa Playstore kutokana na Kuvunja sheria za Playstore. Ikiwa app nilioitaja nayo itaondelewa basi unaweza ipakua app nyingine nje ya Playstore Kwa kugusa HAPA>>>
Je, ni Mbs ngapi zinahitajika kuangalia mpira mzima(Dk90) kwenye simu?
Hili ni swali ambalo wengi hujiuliza, wanapohitaji kuanza kuangalia mpira kupitia simu. Ukweli ni kwamba, kadri video inavyokua na muonekao mzuri ndivyo Mbs huwa zinalika nyingi. Itakua ni vizuri zaidi Kama hautakua na chini ya Mb900 ili kutokua na wasiwasi wa bando kuisha.
Kama wewe ni mpenda magemu na unatumia simu yako ya Android kucheza magemu basi hapa tumekuandalia orodha ya magemu machache ambayo unaweza ya cheza na ukafurahia zaidi muda wako wa kucheza magemu kwenye simu yako. Kama ndio kwa Mara ya kwanza unataka kujifunza au kuanza kucheza magemu ya Android basi ni vema ukaangalia magemu yalio katika orodha hii na ukaangalia linalo kufaa kisha ukalipakua.
Call of Duty mobile
Hili ni gemu zuri sana la kivita ambalo limetolewa na Activision. Gemu la Call of Duty mobile ni gemu lililochezwa na watu Wengi na Mpaka sasa linaendelea kuchezwa na mamilioni ya watu ulimwenguni. Kama unapenda magemu ya kivita basi gemu hili unaweza kulifulahia zaidi lakini unachotakiwa kujua nikwamba game hili ni la Online. Kwa lugha nyingine tunaweza kusema gemu hili linahitaji internet ili kulicheza. Kitu kizuri kuhusu magemu hili ni kwamba unaweza kucheza na watu wengine na pia Kuna mode ningine za kucheza zinazoweza kufanya usichoke kulicheza. Ili kulipata kirahisi gusa HAPA
Bus Simulator Indonesia ni moja ya magame ambayo huchezwa na watu wengi sana na mpaka sasa limechezwa na watu wasiopungua Milioni 50 na wengi hulifahamu kwa jina lake la BUSSiD. Ni game lililotolewa mwaka 2017. Game hili ni la Online yaani ili kulicheza utahitajika kutumia data. Kama nimpenzi wa game za muundo huu basi hakikisha unapakua game hili maana ni game zuri sana.Kitu unachotakiwa kukifahamu ni kwamba mazingira na magari yalio katika game hili yanayofana na mazingira ya Indonesia ndiomana likawa na jina Indonesia.Linaweza kuchezwa na watu zaidi ya mmoja (Online). Linapatika playstore kwa MB zisizopungua 272. Unaweza kulipakua kirahisi kwa kugusa HAPA
Traffic Rider
Kama ni mtu unaependa magame mazuri na unavutiwa zaidi na game za pikipiki basi game la Traffic Rider ni game litakalokufurahisha zaidi. Game hili mpaka Sasa limechezwa na watu zaidi ya Milioni 7 ulimwenguni na asilimia kubwa ya watu hao wamelipenda. Linamuonekano mzuri, Sauti zenye uhalisia na majira yenye uhalisia maana kuna hadi mission za usiku. Kadr unavyoendesha kasi pikipiki na kuovertake magari ndivyo unavyojiongezea idadi ya Scores. Lina missions zaidi ya 70 na kuna zaidi ya pikipiki 20 tofauti tofauti.Traffic Rider ni game lipatikanalo Playstore na lina MB90 tu. Hukubali mpaka katika simu zenye RAM 1 bila shida yoyote. Kama utahitaji kulipata kirahisi game hili gusa HAPA
Ni gemu ambalo unalicheza ukiwa Kama mtu ambae upo kwenye mji uliochafuka na kila mtu naeishi katika mji huo anaishi kwa hofu kubwa kutokana na uwepo wa wafu wanaotembea yaani Zombies na baadhi ya viumbe vingine visivyo na urafiki na binadamu. Ni moja ya magame mazuri yanayopatikana kwa Mbs chache katika playstore. Lina nyumba zinaingilika na unawachezesha wahusika zaidi ya mmoja katika mji huo. Unaweza kulipata kirahisi game hili kwa kugusa HAPA
EA Sports UFC
Unapenda magemu ya kupigana? Kama Unapenda magemu ya kupigana basi gemu la EA Sports UFC ni game ambalo halitakiwi kukoswa kwenye simu yako. Gemu hili ni moja ya magemu mazuri sana ya kupigana. Lina muonekano mzuri mno ambao utakufanya ufurahie kulicheza. Linahusu kupigana kwa kutumia ngumi na mateke.
Limekusanya wapiganaji wengi maalufu duniani ambao utatakiwa kuwafungua kutokana na uchezaji wako. Gemu hili linaweza kuchezwa Offline na Online. Ukiwa unacheza Online unakua na uwezo wa kucheza na watu wengine toka sehemu mbalimbali za dunia na utatakiwa kupambana nao na kufanya wapoteze dira kwa vitasa(ngumi) na mateke ya mitindo mbalimbali ili uibuke mshindi. Unaweza lipata katika playstore kwa kugusa HAPA
Overkill 3
Hili ni gemu zuri sana la Action ambalo mpaka sasa limechezwa na watu zaidi ya milioni 5. Linamuonekano mzuri na watu wengi wanalipenda kutokana na muonekano wake unaofanana na Caver Fire. Gemu hili huchezwa bila data (Offline) pia linaweza kuchezwa na watu zaidi ya mmoja kwa kutumia data (Online).Inashauriwa anaecheza gemu hili awe na miaka 16 na kuendelea. Overkill 3 ni gemu lipatikanalo Playstore kwa kama MB 401 ivi na unaweza kulipata kirahisi kwa kugusa INSTALL
Takashi Ninja Worriror: Shadow of last samurai
Hili ni moja ya magemu mazuri sana ambayo kwa sasa yako trend katika playstore. Gemu hili ni la kijapani na linamuhusu kijana Takashi ambae anaingia katika kulipa kisasi kutokana na watu wake kufanywa vibaya. Ukilipakua utaweza kulicheza muda wowote na bila kukugharimu chochote maana gemu hili huchezwa bila data (Offline) pia hupatikana kwa MB chache sana zisizopungua MB 87. Unaweza kulipata kirahisi katika playstore kwa kugusa INSTALL
Modern Strike Online
Ni moja ya magemu bora ya kivita ambayo huchezwa Online tu. Limechezwa na watu wengi sana wasio pungua Milioni hamsini(50).Gemu hili ni moja ya magemu yanayofanana na gemu la Call of duty hivyo kama unapenda magemu ya jamii ya Call of duty, usiache kucheza game hili. Katika game hili unaweza cheza na marafiki zako Online kwa kiunda timu ya kuwaangamiza maadui au mukashindana kuua maandui ili atakaewaua maadui wengi awemshindi. Modern Strike Online ni gemu lipatikanalo Playstore kwa MB zisizopungua MB 494. Unaweza lipata kirahisi kwa kugusa INSTALL
Kama ni wewe ni mpenzi gemu za mashindano ya pikipiki basi real moto linaweza kuwa bora sana kwako. Game hili huchezwa bila kutumia data yaani ni gemu la Offline. Limechezwa na zaidi ya watu Milioni kumi(10). Utaweza kutunza kumbukumbu zote za gemu hilo kwenye email yako ili simu ikipotea uendelee kucheza palepale ulipoishia kucheza gemu hilo pindi utakapopata simu nyingine na kuiingiza email yako. Gemu hili hupatikana playstore kwa MB 143. Unaweza kulipata kirahisi sana kwa kugusa INSTALL
Garena Free Fire
Garena Free Fire linatumia data na lipo hivi; Unamchagua mtu wako utakaemchezesha kisha unatupwa katika eneo moja na wenzako 49 wanaocheza gemu hilo muda huo duniani ili mupigane na uwemzima. Kwaiyo kila mtu utakaemuona katika gemu hili ni mtu anaepambania maisha na anaecheza kama wewe. Zaidi ya watu Milioni 500 ulimwenguni wanalicheza Gemu hili kupitia vifaa vyao vya Android. Ni gemu linalopendwa na watu wengi kutokana na kuwa dogo kuliko magemu mengine ya muundo huu ambayo ni PUBG na CODM. Unaweza kulipakua katika playstore kwa MB 674 pia unaweza rahisisha upatikanaji wake kwa kugusa INSTALL
Kama unapenda gemu za magari usiache kupakua gemu hili lenye utofauti mkubwa na magemu ya magari yanayotamba kila mwaka. Game hili ni moja kati ya magame yanayopendwa na watu na mpaka Sasa limepakuliwa na zaidi ya watu Milioni 50. Linauhalisia wa kufurahisha wa mashindano ya Rarry. Ukiachilia mbali muonekano wa game hili kuwa mzuri pia game hili linawezwa chezwa na mtu mmoja Offline au zaidi ya moja Online.Lina chukua kama MB 120 kulipakua na linapatikana katika playstore. Unaweza lipata kirahisi kwa kugusa INSTALL
eFootball
Ukiongelea gemu kali za mpira wa miguu katika mwaka huu huwezi acha game hili. Gemu hili limepakuliwa na watu wengi sana hapa duniani na hii ni kwasababu liko vizuri. Kama umeshawahi cheza magemu ya PES basi tambua kuwa “eFootball” ni lile lile PES ila wamebadilisha jina tu.
Linachezwa Online na inashauriwa kuwa na mtandao usiosumbua ili uweze kulifaidi gemu hili bila usumbufu.Hupatikana playstore kwa GB 1.6 pia unaweza kulipata kirahisi sana kwa kugusa INSTALL
Hili ni gemu la mchezo wa ngumi ambalo mpaka sasa limechezwa na watu wasiopungua Milioni 10 ulimwenguni. Lipo vizuri sana kwanzia muonekano hadi sauti za vitasa(Ngumi). Kama ni mpenzi wa magemu ya kupigana, usikubali kuliacha gemu hili maana ni gemu lenye uhalisia wa mchezo wa kupigana wa Boxing. Inashauriwa anaecheza game hili asiwe na miaka chini ya kumi na sita (16+). Game la Real Boxing hupatikana playstore kwa kama MB 291 ivi na unaweza kulipata kirahisi kwa kugusa INSTALL
Jumanji: Epic run
Kama unaijua vizuri filamu ya Jumanji au gemu la Tempo Run basi unaweza kulipenda zaidi hili gemu maana limeundwa kutokana na filamu ya Jumanji na muundo wake unafanana na gemu maarufu liitwalo Tempo Run.Ni gemu ambalo hujezwa bila data na mpaka Sasa linachezwa na zaidi ya watu million 10 duniani. Mchezaji wa gemu hili anatakiwa kuwa na umri usiopungua miaka 12.Linapatikana playstore kwa MB 154 na unaweza kulipata kirahisi kwa kugusa INSTALL