Tag Archives: ajira

TikTok na Instagram zinakusaidia vipi kutafuta Ajira unayoitaka?

Katika dunia ya sasa, teknolojia imeleta mabadiliko makubwa katika njia tunazotumia kutafuta ajira. Mitandao ya kijamii imebadilika kutoka kuwa sehemu ya burudani tu hadi kuwa nyenzo muhimu kwa watu wanaotafuta kazi.

Watu wengi bado hawatambui kuwa nafasi za ajira hazipatikani tu kupitia barua pepe au matangazo ya kampuni. Kwa kutumia mitandao ya kijamii vizuri, unaweza pata nafasi ya kazi unayotafuta. Kinachohitajika ni kuelewa tu mbinu sahihi za kuitumia kwa faida yako.

Kabla hujaanza kutuma maombi ya kazi kila mahali bila mafanikio, ni vema kujua kuwa TikTok na Instagram imekupa nafasi za kurahisisha michakato ya kutafuta ajira. Na kama unataka kujua ni kwa namna gani, soma yafuatayo.

TikTok na Instagram zimekupa nafasi hizi katika kutafuta ajira

1. Kukutana na mamilioni ya waaajiri

TikTok na Instagram ni sehemu ambayo mtu anaetafuta ajira anaweza itumia kukutana na waajiri wengi sana. Hii ni mitandao ya kijamii ilio wakusanya watu na kampuni mbalimbali ambazo zinaweza kumuajiri mtu. Yani kwenye TikTok au Instagram, unaweza kutana kurasa za maduka makubwa ya nguo, makampuni ya simu na hata usafirishaji. Na unaweza tuma ujumbe au kuuliza mambo mbalimbali kirahisi kabisa.

Kwaiyo kama unatafuta ajira, fahamu kuwa mitandao hii (TikTok na Instagram) tayari imekuwekea karibu sehemu nyingi unazoweza kuomba ajira. Tena bila mipaka maana unaweza kuwa nje ya Dar lakini ukawa karibu na maduka au kampuni zilizo Dar.

2. Kuonesha ujuzi au uzoefu wako ili kuvutia waajiri

Nafasi ya pili unayopewa na TikTok na Instagram katika kutafuta ajira ni uwezo wa kuonesha ujuzi au uzoefu wako kwa waajiri wako. Hii ni nafasi nzuri sana unayoweza itumia na ukapata ajira.

Wote tunafahamu kuwa ajira zimekua ni chache kuliko wahitaji. Na ajira nyingi zinazo jitokeza katika kipindi hiki, muajiri huitaji mtu Bora, mwenye ujuzi wa hali ya juu au mzoefu kabisa.


Sasa ukiwa kama mtu unatafuta ajira, unaweza kuonesha ujuzi wako au uzoefu kwako kupitia video za TikTok au Instagram. Wengine hutumia video kuchekesha wengine, au kujipost wakicheza. Hili sio jambo baya lakini ni muhimu kufahamu kuwa video zinaweza kutumika kuonesha ujuzi flani pia. Video zako za ujuzi zinaweza kuangaliwa na mamilioni ya watu. Kati ya mamilioni ya watu huo, Kuna watu wengi wanaoweza kukuajiri.


Kwaiyo hii ni nafasi nzuri ya kuonesha ulichonacho kwa watu watakao kuajiri. Lakini katika kutengeneza video, unatakiwa kuwa mbunifu sana.

3. kujiajiri wakati ukiendelea kutafuta ajira

Nafasi ya tatu ambayo TikTok na Instagram imekupa mtu unaetaka ajira ni kujiajiri huku ukitafuta ajira unayoihitaji. Unaweza kujiajiri na ukawa unaingiza pesa kwa kutumia mitandao hii.

Sio lazima ikulipe moja kwa moja kwenye akaunti yako ya Bank, unaweza itumia kutangaza huduma yako inayokuingizia kipato kwa kipindi ambacho unasubiri ajira.

Jinsi ya kutafuta nafasi za ajira/kazi kwa kutumia simu mtandaoni

Kama ni mmoja kati ya watu wanaotafuta nafasi za kazi basi hapa kunakitu kidogo unahitaji kuwanacho kichwani katika miaka hii ukiwa katika mchakato wa kutafuta ajira. Unachotakiwa kujua ni kwamba teknolojia kupitia internet/mtandao imerahisisha mchakato wa kutafuta ajira na kuufanya uweze kufanyika katika kiganja chako kwa kutumia simu yako(Smartphone).

Unaweza tumia simu yako kuangalia nafasi za ajira unayoihitaji zilizojitokeza katika sehemu mbalimbali za dunia (Ndani na nje ya nchi). Na kama utapply au kufuata maelezo ya kuipata iyo nafasi na kubahatika kuipata, utakua ni mmoja wa mamilioni ya watu waliopata na wanaoendelea kupata nafasi za kazi kwa msaada wa internet. Kama unataka kutafuta nafasi za ajira/kazi kwa kutumia simu mtandaoni lakini haufahamu ni jinsi gani unaeza fanya hivyo, basi hapa chini nakupa mwanga juu ya hili kwa njia 3. Lakini kabla ya yote ni vema ukajua kwamba kunabaadhi ya nafasi za kazi au ajira ziwekwa na matapeli mtandaoni na maranyingi humuitaji mtaka nafasi atoe pesa ili kupata nafasi ya ajira… kuwa makini ni ajira za mtindo huo ili usije tapeliwa.

Njia za kutafuta nafasi za ajira/kazi zilizojitokeza kwa kutumia simu mtandaoni

Tafuta nafasi za kazi kupitia Google search

Watu tu hutumia google search kutafuta vitu mbalimbali kirahisi mtandaoni na imekua msaada mkubwa kwa watu wengi, nafikili hata wewe unaweza kuwa mmoja wa watumiaji wake mzuri. Mtu unaweza tumia Google kupata vitu vinavyokufurahisha, vitu vitakavyo kuelimisha na vitu vingine muhimu ikiwemo nafasi za ajira zilizojitokeza sehemu mbalimbali (Ndani na nje ya Tzanzania). Na nirahisi sana… kiufupi utatakiwa kuandika maneno yanayomaanisha nafasi za kazi, aina ya kazi na mahali(kwa kingereza ili kupata matokeo mazuri). Yaani unawezakwenda Google na kuandika “””””Aina ya kazi unayoitaka + jobs in + sehemu“”””” kisha ukitafuta na kwenye matokeo utapata orodha ya nafasi za kazi kulingana ulichokiandika. Kwamfano ukiwa unataka kazi ya “Customer care service” hapa Tanzania, utaandika “Customer care service jobs in Tanzania” kwenye matokeo utapata orodha ya nafasi za kazi za customer care zilizojitokeza Tanzania. Baada ya google ikukupa nafasi za kazi itakua ni kazi kwako kusoma maelezo ya kazi hizo ili kuzielewa zaidi na kuapply ikiezekana. Lakini unapotumia njia hii inatakiwa kufahamu kuwa Google ni search engine tu, hivyo huwa haina nafasi za kazi, inakupeleaka sehemu ilipopostiwa kazi…

Jiunganishe na blog zinazohusiana na mambo ya nafasi za ajira

Kuna blog ambazo hujihusisha zaidi na kutoa tahalifa kwa watu juu ya nafasi za ajira zilizojitokeza. Maranyingi huwa zinapost tahalifa za nafasi za ajira au habari zinazohusiana na mambo hayo hayo. Mfano mzuri ni Ajiraleo.com au Ajirampya360.com. Sasa kwakua na wewe unahitaji nafasi za kazi basi unaweza anza kuwa karibu na blog za mtindo huu ili wakitoa tu tahalifa za nafasi za ajira zilizojitokeza, zikupate kwa wakati na kuanza mchakato wa kuzichangamkia. Unaweza kuwa nazo karibu kwa kuzifuata blog hizo au kurasa zao katika mitandao ya kijamii ili kupata vitu wanavyopost.

Tumia LinkedIn

Linkedin ni mtandao kama vile Facebook au twitter lakini mtandao huu unakusanya wataalamu wa mambo mbalimbali na umejikitia katika zaidi maswala ya biashara na ajira. jiunga kwenye mtandao Linkedin bure kabisa na kwenye profile yako utatakiwa kujaza taalifa sahihi kuhusu wewe na utaalamu wako. Mambo unayotakiwa kuyafanya ndani ya mtandao huu ni vema yakawa yanaendana na utaalamu wako na jambo zuri ni kwamba unaweza kupata ajira kupitia mtandao huu… kurahisisha zaidi mchakato wa kutafuta nafazi za kazi, kunakipengele cha mtandao huu kinauruhusu kutafuta nafasi za kazi zilizojitokeza kulingana na uhitaji wako na kuapply.

Mbali na njia hizo tatu, kuna njia au vitu vingine zaidi unaweza fanya kupata taalifa za nafasi za kazi zilizojitokeza lakini huenda tutazungumzia katika sehemu nyingine, hapa tumekupa mwanga kwa hayo machache. Na ni vema kuendelea kutafuta nafasi za kazi nje ya mtandaoni pia. Ishi kwa kutangaza utaalamu wako. Endelea kufuatilia The bestgalaxy.