Tag Archives: ai

Jinsi ya kutengeneza Pesa kwa AI za kuunda Picha

Al za kutengeneza au kuunda picha zipo nyingi sana sasa na hata watumiaji wake ulimwenguni wapo wengi pia. Kuna AI ambazo huunda picha kutokana na maelezo ya maneno inayopata na nyingine huwa zinaweza kuunda picha mpya kutokana na picha iliopewa. Yote hii ni kumuwezesha Kila mtu kuwa na uwezo wa kutengeneza picha anayoifikilia au kuihitaji. Kiufupi wanasema AI hizi zinakusaidia kugeuza wazo au unachofikilia kuwa katika picha.
Watu huzitumia AI za kutengeneza au kuunda picha katika mambo mbalimbali ikiwemo kutengeneza pesa.

Kunawatu mpaka kufikia sasa AI kwa ujumla imewasaidia kutoka sehemu moja kwenda nyingine kibiashara au chumi na mambo mengine, ikiwemo hizi za kuunda picha. Kwaiyo kutengeneza pesa kupitia AI za kuunda picha ni jambo liliofanywa na watu na linawezekana pia. Hapa Kwenye ukurasa huu the bestgalaxy tunakufungua juu ya namna gani mtu unaweza ingiza pesa au kutengeneza pesa kupitia hizi AI za kuunda picha.

AI za kutengeneza picha kwa kutumia maneno BONYEZA HAPA>>>

Jinsi ya kutengeneza Pesa kwa AI za kuunda Picha.

Kuprint nguo ya picha za AI na kuuza

Unajua kwamba kuna nguo zina picha zinauzwa madukani na zinapendwa na watu kutokana picha hizo lakini ukifuatilia utagundua picha hizo zimeundwa na AI? Unaweza fanya hivi pia kama unataka kutengeneza pesa kwa AI za picha. Unaweza tafuta nguo uka print picha zuri ya kuvutia iliotengezezwa na AI, hasa T-shirt. Alafu baada ya hapo ukaziuza kwa bei inayoendana na muonekano wake. Kama picha itakua nzuri na kuvutia, unaweza uza sana nguo za mtindo huu. Lakini hii ni nzuri kuijaribu kama una Duka la nguo au unajihusisha na maswala ya nguo ili usipate shida mambo yakiyumba kwenye mauzo.

Mfano wa nguo ni hii T-shirt nyeusi yenye picha iliotengenezwa na AI

Kukuza page ya picha za AI na kuimonetize

Kwenye mitandao ya kijamii inayojihusisha na picha, kama vile Facebook au Instagram, unaweza tengeneza pesa kwa AI. Utakachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unaposti picha nzuri kwenye ukurasa(page) wa Facebook au Instagram bila kuchoka mpaka utakapo pata watu wengi wanaoungana na wewe kwenye kurasa yako. Huo ukurasa inabidi ujihusishe na kitu jambo ambalo unalielewa sana kwenye maisha yako na unaweza wasaidia wangine kwenye jambo hilo. Na picha utakazokua unapost utakua unatengeneza kwa Al alafu zinatakiwa kuwa zinahusu mada moja ulioichagua. Kama unataka kujihusisha na magari, basi picha unazotengeneza inabidi ziwe za kuhusu magari. Unapoziposti unaweza ziwekea maelezo ambayo yatamvutia mtu kusoma au kujifunza.
Kama utafanikiwa kuwa na watu wengi unaweza anza toa huduma kwa watu au kuuza vitu ili upate pesa. Unaweza kuwa unalipwa pia kama na watu wengine kwa kuonesha matangazo.

Kutengeneza video kwa picha na kwenye platform zinazolipa

Kama ni mtu wa kutengeneza video, AI za kutengeneza picha zimekuja kukukomboa kwa kiasi kikubwa sana. Kuna aina za video huwa haziitaji vitu vingi katika kuzitengeneza, zinahitaji sauti na picha. Sasa AI kama inaweza kukupa picha kirahisi basi kutengeneza video za namna hii kwako inakua nirahisi kuliko kutumia picha zenye copyright. Na jambo hilo likiwa rahisi kwako inamaana unaweza tengeneza video za mtindo huo na kupelekea kwenye platform kama YouTube, Facebook au YouTube alafu ukapambana ukalipwa. Hata ukishindwa kulipwa na hizo platform unaweza tengeneza mfumo wako wa biashara utakao kulipa.

Kutengeneza watu matangazo ya biashara

Kama ni Graphics designer unaeweza tengeneza matangazo ya biashara, AI za picha zinaweza kukufanya uingize pesa pia. Kupitia AI unaweza tengeneza picha ya mtu au vitu vingine unavyohitaji kwenye kuunda tangazo la biashara. Kuna baadhi ya makampuni kwasasa yanapeperusha matangazo yalioundwa Graphics designer kwa msaada ya AI. Yani unawezamuona mtu kwenye tangazo lakini mtu huyo ametengenezwa na AI.
Hii ni njia hai kabisa na inatumika mpaka sasa na Graphics designers wengine kuweka kazi zao kwenye hali ya juu na kutengeneza pesa kirahisi. Kikubwa ni usitumie AI kukupa inachotaka, Itumie AI kupata unachotaka ili uendelee kuwa creative.

Mwisho ningependa kukukumbusha kuendelea kuwa karibu na mambo ya AI ili uelewe jinsi ya kuzitumia. Ni muhimu sana kwa mtu kuelewa AI katika miaka hii ili usije achwa nyuma kibiashara na kwenye mambo mengine.

AI za kutengeneza picha kwa maneno (Akili bandia)

Inaweza kuwa sio mara ya kwanza kusikia neno “Akili bandia”. Akili bandia kwa kiingereza inaitwa AI na kirefu chake ni “Artificial intelligence”. Hii ni Teknolojia ambayo imeleta na inaendelea kuleta mabadiliko makubwa kwenye sehemu mbalimbali katika ulimwengu. Tumeisha zungumzia kuhusu hili kwenye makala za nyuma na hapa tunaenda kuangalia upande wa kutengeneza picha kwa kutengeneza AI.

AI ni nini na inamatokeo gani katika Ulimwengu? BONYEZA HAPA>>>


Kuna AI zenye uwezo wa kutengeneza/kuunda picha kulingana na maelezo yako tu ambayo huitwa “prompts”. Yani unaweza inambia AI ikutengenezee picha ya paka mweupe anaemkimbiza panya alafu AI ikaelewa ulichoeleza na kutengeneza picha inayoonesha tokio hilo. Maelezo yako ndio hufanya hizo AI zitoe picha au matokeo unayohitaji na AI nyingi hutaka uandike maelezo kwa kiingereza lakini kunanjia ya kulishinda hili ntakupa mwishoni. Kuna AI nyingine haziitaji utoemaelezo sana, unaweza zipa picha ya mfano alafu zikakutengenezea picha nyingine kama hiyo.


Kuna mambo mengi ya kuzungumzia kuhusu upande huu wa AI lakini tusipoteze muda, hebu tunangalie AI hizi za kutengeneza picha.

AI za kutengeneza picha kwa kuandika maneno (Akili bandia)

DALL-E 3

DALL-E 3 ni AI inayoweza badili maneno au maelezo inayopewa kuwa picha. Inauwezo mkubwa sana katika upande wa kutengeneza picha kwa maneno. Inaweza kutambua vizuri maelezo inayopewa na kutoa matokeo au picha zenye ubora wa hali ya juu ukilinganisha na baadhi ya huduma na model za Al nyingine.
DALL-E 3 imetengenezwa na kampuni ya OpenAI ambayo imetengeza Chatbot maalufu iitwayo ChatGPT. Ukihitaji kuitumia DALL-E 3 kwasasa utahitaji kujiunga na ChatGPT alafu ulipie “ChatGPT Plus” ambayo inaweza kukuchukua kama Tsh 49,000 kwa mwezi.

Jinsi ya kuongeza ubora wa picha zako za zamani kwenye simu BONYEZA HAPA>>>

Capilot image generator

Capilot ni AI inayomilikiwa na Microsoft na AI hii inajihusisha na kufanya mambo mengi ikiwemo kutengeneza/kuunda picha. Kuna kipingele cha Capilot kinakuruhusu mtumiji wake kutengeneza picha kwa kuandika maelezo ya picha anayohitaji. Kipengele hiki kimewezeshwa na DALL-3 ambayo tumeizungumzia hapo juu hivyo unaweza tumia hii badala ya DALL-3 moja kwa moja.
Microsoft waimeiweka Capilot image generator kama kipengele cha Bing search. Ukihitaji kuitumia Capilot image generator kirahisi na Bure unaweza ingia Bing kwenye kipengele cha Bing image generator ukaitumia kutengeneza picha bure. Unaweza tumia hata kiswahili katika kuelezea picha unayohitaji ila inaweza isilete matokeo mazuri.

Muonekano wa capilot image generator katika bing unapotengeneza picha.

Midjourney

Midjourney ni moja ya AI maarufu sana katika Ulimwengu wa content creation. AI hii haijihusishi na kutengeneza picha kwa maneno tu, inajihusisha mambo mengine yanayohusu kutengeneza content kama vile video. Kipindi cha nyuma kulikua na uwezekano wa kutumia midjourney Bure lakini kwasasa hakuna nafasi hiyo.
Ukitaka kuitumia kwa sasa utatakiwa kuingia kwenye tuvuti yao kujisajili na kuchagua kifurushi/plans kati ya vifurushi vyao visivyojumuisha “Bure”.

Adobe Firefly

Adobe imejikita katika AI pia na kwasasa unaweza tumia huduma zake nyingi zikiwa zimewezeshwa na AI. Kiufupi haijabaki nyumba katika Teknolojia ya akili bandia na katika picha inakuwezesha kutengeneza picha kwa maneno kupitia “Adobe Firefly”. Adobe Firefly ni moja ya AI nzuri katika kubadirisha maneno kuwa picha. Unaweza ielezea jinsi unavyo hitaji picha iwe na ikakuletea matokeo mazuri ya picha. Inaruhusu pia kuijaribu bila malipo kwenye tuvuti yao ila idadi picha utazo tengeneza bure zinakikomo kwa mwezi na alama ya “Adobe Firefly” itakuepo kwenye hizo picha. Ukihitaji kupata uhuru zaidi basi itabidi uhusishe malipo kwenye kupata huduma yao.

Fotor

Hii Fotor pia ni AI ambayo inaweza elewa maelezo unayoipa na ikakutengenezea picha kutokana na maelezo unayoipa. Ipo vizuri sana inatoa nafasi ya kuijaribu bila malipo ingawa kuna kikomo pia. Unapewa nafasi hiyo baada ya kufungua akaunti mpya kupitia app au tuvuti yao. Inasifika zaidi kwa kutengeneza picha za michoro au kuchora japo unaweza tumia kutengeneza picha za mitindo mingine pia.

Ni hizo tu tulizokuandalia hapa ila fahamu kuwa kuna nyingine nyingi nzuri. Tumeorodhesha hizi kwenye ukurasa huu kwakua ni katika ya AI hizo nzuri.

Kama kiingereza ni kinakushinda katika kuelezea picha unayohitaji, tumia translator kubadirisha maelezo yako ya kiswahili kwenda kiingereza alafu paste maelezo hayo ya kiingereza kwenye AI. Usiache kuendelea kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mambo mengine zaidi.

Jinsi ya kutengeneza Pesa kwa AI za kuunda Picha BONYEZA HAPA>>>