Kwa sasa watu wengi wanatumia AI kama ChatGPT kuedit picha. Sababu kubwa ni kwamba AI imefanya mchakato huu kuwa rahisi, wa haraka, na hauhitaji utaalamu wowote wa picha. Kwa kutoa maelezo tu, mtu anaweza kubadilisha picha yake kwa namna yoyote anayotaka.
Lakini pamoja na urahisi wake, si huduma za AI zote zinapatikana bure bila kikomo. Kwa mfano, ChatGPT hukupa nafasi chache za kuedit picha bure; baada ya hapo unatakiwa kulipia ili kuendelea kutumia kipengele hiki bila mipaka.
Watu wengi wanalipia huduma ya ChatGPT kwa sababu inaonesha uwezo mkubwa wa picha, video na uandishi. Kwaiyo kulipia ni jambo jema kama unaweza. Lakini kama huwezi kulipia na bado unahitaji kuedit picha zako mara kwa mara, kuna cha kufanya ili kufanikisha hilo bure bila kikomo.
Njia ya Kuedit Picha Bure Bila Kikomo: Microsoft Copilot
Ikiwa unataka kuedit picha kwa ChatGPT bila kikomo, njia rasmi ni kununua vifurushi vyake kama Plus, Pro, Business, au Enterprise. Lakini kama kulipia ni changamoto, suluhisho rahisi ni kutumia Microsoft Copilot.
Copilot ni AI ya Microsoft, inayotumia teknolojia ile ile ya “OpenAI” kama ChatGPT (mfano GPT-4 na GPT-5). Ina uwezo sawa wa kuedit picha, kuandika, kutafsiri, kutoa majibu na kufanya kazi nyingi kama ilivyo ChatGPT. Tofauti kubwa ni kwamba Copilot hukuruhusu kutengeneza na kuedit picha bure bila kikomo.
App ya Copilot Ai ikibadilisha muonekano wa nyuma wa picha(Background)
Kwanini Copilot?
Inatumia injini sawa na ChatGPT
Inakupa uwezo wa kuedit picha bure
Haina kikomo kama ChatGPT ya bure
Kwa kifupi, kama huwezi kulipia ChatGPT lakini unahitaji uwezo wa kuedit picha kama vile ChatGPT, basi CopilotAI ni chaguo sahihi kwako. Inapatikana kwenye simu (Play Store & App Store). Mbali na simu, inapatikana kwenye PC na kupitia website pia.
Miaka michache iliyopita, ilikua rahisi sana kutambua video au picha zilizotengenezwa na AI (Artificial Intelligence). Mara nyingi, picha au video hizo zilikuwa na makosa mengi ya wazi. Kwa mfano, mtu kwenye picha angeweza kuonekana na vidole saba, au mikono mitatu, jambo lililofanya iwe rahisi kuelewa kuwa hiyo ni kazi ya AI.
Lakini siku hizi mambo yamebadilika. AI imekua ya kisasa zaidi na makosa yake yamepungua sana. Kwa sasa, ni vigumu sana kutofautisha picha au video halisi na zile zilizoundwa na AI. Kutokana na hilo, mitandao mingi ya kijamii imeanza kuweka alama maalum (label) kwenye maudhui (picha au video) yaliyotengenezwa na AI, ili kuwasaidia watumiaji kutambua kwa urahisi.
Pamoja na hayo, bado kuna ugumu kwa watu wengi katika kutofautisha picha au video halisi na zile za AI; hasa kama zimeundwa vizuri.
Hapa The Bestgalaxy, tumekuandalia njia rahisi za kuitambua picha au video iliyotengenezwa na AI, ili usipoteze muda au kudanganywa mtandaoni. Pia ni njia ya kujilinda dhidi ya matapeli wanaotumia maudhui ya AI kwa udanganyifu.
Jinsi ya kuitambua Picha au video iliotengenezwa na Ai
1. Tumia Platform Maalum Kutambua Kazi za AI
Njia ya haraka na rahisi zaidi ni kutumia tovuti maalum zilizoundwa kwa ajili ya kutambua kama picha au video imetengenezwa na AI. Mfano wa tuvuti kama hii ni Ai or Not. Hii tuvuti inakuruhusu kuweka picha au video, kisha inakupa matokeo ikiwa ni ya AI au halisi.
Hii ni njia nzuri sana lakini kuna baadhi ya picha halisi huwa zinaweza kuonekana ni kazi za Ai kwenye njia hii. Hili linaweza kutokea endapo picha au video halisi itapitishwa kwenye michakato inayohusisha Ai. Michakato hii inaweza kuwa hata kuongeza ubora kwa kutumia Ai tu.
Kwaiyo kiufupi kuna Picha au Video halisi huwa zinaweza kuonekana kama sio halisi(za Ai) kwasababu zimeongeza ubora tu kwa kutumia Ai.
Hii ni website ya Ai or Not ikitoa majibu juu picha. Majibu ya picha hii yamesomeka “Likely AI Generated” ikiwa ni ishara yakwamba picha imetengenezwa na AI.
2. Angalia Vitu Hivi Kwa Macho Yako
Kama hutaki kutumia tovuti au programu maalum, unaweza kutambua mwenyewe kupitia dalili ndogo zifuatazo:
Rangi zilizokolea kupita kawaida: Video/Picha za AI mara nyingi huwa na rangi ang’avu kupita kiasi, zisizo za kawaida kuwepo kwenye picha halisi.
Mabadiliko madogo kwenye video: Wakati mwingine vitu vidogo hubadilika ghafla, kama sura, madoa ya nguo, macho, au mwanga. Hii ni ishara ya AI.
Sauti yenye uroboti: Video za AI (hasa deepfake) mara nyingi zinakuwa na sauti nyepesi au zenye mwangwi kama sauti za roboti (robotic tone).
AI imefika mbali sana lakini bado unaweza kuitambua ukitumia umakini. Ingawa zinatambulika ila kumbuka kuwa sio kila kitu kinachoonekana halisi mtandaoni ni cha kweli. Baadhi ya video au picha zinawezakuwa ni ngumu kutambua mpaka alietengeneza aweke wazi.
Katika miaka ya hivi karibuni, dunia imeingia kwenye kipindi kipya cha teknolojia ambacho hakijawahi kushuhudiwa hapo nyuma. Ujio wa Artificial Intelligence (AI) au Akili Bandia kwa Kiswahili umebadilisha kabisa dunia katika kila sekta. Tokea kampuni kubwa kama Google, OpenAI, Meta, na Microsoft zilipoanza kuwekeza nguvu kubwa katika utafiti wa AI, dunia imeanza kushuhudia mambo ya ajabu ambayo zamani yalionekana kama miujiza.
Leo hii, AI inaweza kuandika makala, kutengeneza picha au video, kuzungumza kama binadamu, na hata kufanya maamuzi kama vile ni akili inayofanana na ya mwanadamu. Imeingia katika pande za biashara, elimu, sanaa, uandishi, afya, michezo, na hata mahusiano ya binadamu. Wengine wanaiona ai kama ni neema kubwa ya karne hii, wakati wengine wanaiogopa wakihisi inaweza kuchukua nafasi za kazi, kubadilisha maisha, au hata kuvuruga mfumo wa kijamii tuliouzoea.
Lakini jambo moja ambalo halina ubishi ni kuwa AI imeleta mapinduzi makubwa. Imefanya mambo ambayo yalionekana hayawezekani miaka michache iliyopita. Hapa chini tutaangalia mambo kadhaa ya ajabu ambayo AI imeweza kufanya mpaka sasa kwenye ulimwengu ili ujue jinsi inavyoendelea kuathiri maisha yetu ya kila siku.
Mambo 5 ya Ajabu Yanayofanywa na AI Katika Ulimwengu wa Sasa
Inaleta ugumu wa Kutambua Kazi za AI
Miaka michache iliyopita, ilikuwa rahisi sana kutambua kama picha, video, au maandishi fulani yametengenezwa na AI. Lakini sasa, mambo yamebadilika sana! AI imeboreshwa kiasi kwamba ni vigumu kugundua kama kitu fulani kimeundwa na kompyuta au binadamu. Teknolojia kama Midjourney, Sora, Runway, na D-ID zimefikia hatua ya kuzalisha picha na video zenye uhalisia wa kushangaza. Makampuni haya yanazidi kuboresha mifumo yao kila siku, na matokeo yake ni video au picha ambazo zinaonekana kama zimetengenezwa na kamera ya kweli. Ingawa bado hazijakamilika kwa asilimia 100, ubora wake unafanya hata wataalamu waone ugumu kutofautisha kazi ya AI na halisi.
Inapunguza Thamani ya Baadhi ya Kazi
AI imeathiri baadhi ya ajira duniani. Kazi ambazo zamani zilihitaji muda na utaalamu, sasa zinaweza kufanywa kwa sekunde chache kupitia AI. Kwa mfano, watu wengi waliokuwa wakitegemea platform kama Fiverr au Upwork kupata kazi za Ubunifu kama utengenezaji wa logo au picha wameanza kupoteza wateja. Yote ni kwasababu kila mtu sasa anaweza kufanya hizo kazi mwenyewe kupitia programu za Ai kama Canva AI, ChatGPT, au Logo Creator AI. Hii imesababisha baadhi ya kazi kushuka thamani huku watu wengi wakiendelea kujifunza kutumia AI kufanya mambo ambayo zamani yalihitaji mtaalamu.
Imerudisha Wasanii Waliofariki
AI imeleta kitu cha ajabu kinachogusa hisia za watu wengi. Imefanya kuwarejesha wasanii waliokufa. Hapa namaanisha; Kupitia mifumo ya AI, sasa inawezekana kutengeneza nyimbo mpya, video, au hata picha za wasanii waliotutoka miaka mingi iliyopita. Kwa mfano, unaweza kuona video mpya ya msanii maarufu aliyefariki zamani, au kusikia wimbo mpya uliotengenezwa kwa kutumia sauti yake ya zamani. AI imeruhusu mashabiki kuendelea kufurahia kazi mpya kutoka kwa wasanii waliowapenda, kama bado wako hai. Ni jambo la ajabu, na lionaonesha kuongeza uwanja mkubwa wa watu wanaohitaji kutengeneza vitu vitakavyoishi moyoni mwa watu milele.
Hii ni video ya 2Pac akiwa na Kode pamoja na wengine waliokufa. Video hii imetengenezwa na AI
Imetajirisha Watu Wanaoitumia Vizuri
Kama ilivyo kwa teknolojia nyingine, wale wanaoitumia AI vizuri, wamepata mafanikio makubwa. Watu wengi duniani wameweza kujijenga kifedha kupitia AI, wengine wanauza huduma za ubunifu, wengine wanaunda biashara za kidigitali, na wengine wanatumia AI kuendesha matangazo ya biashara mtandaoni. Kwa mfano; baadhi ya vijana mpaka sasa wanaingiza pesa kwasababu wameunda brand za nguo, eBooks na hata video kwa nguvu ya AI. AI ni kama kifaa chenye thamani ya mamilioni, inayoweza kubadilisha maisha ya mtu yeyote anayeijua vizuri.
Pamoja na hofu nyingi zilizokuwepo mwanzoni, AI sasa imekubalika kote duniani. Watu wa rika zote, kuanzia wanafunzi, walimu, wafanyabiashara, hadi watoto wadogo, wanaitumia kila siku. Kwa mfano, watoto wengi hutumia ChatGPT kujifunza, kuuliza maswali, au hata kufanya kazi za shule. Hili ni jambo zuri lakini ni muhimu kukumbuka kuwa AI haiko sahihi kwa asilimia 100. Wakati mwingine inaweza kutoa taarifa zisizo sahihi au kukosea bila wewe kujua.
Mwisho; fahamu kuwa ai imeleta mabadiliko makubwa katika maisha ya kila siku. Inatengeneza fursa mpya na changamoto mpya kwa wakati mmoja. Lakini kikubwa kwa mtu ulie bahatika kuwa hai katika mapinduzi haya ya Teknolojia ni kujifunza namna nzuri ya kunufaika nayo.
Kama wewe ni mfuatiliaji wa teknolojia ya AI(Artificial Intelligence), basi unajua kuwa sasa hivi kuna njia nyingi za kutengeneza picha na video kwa kutumia AI. Changamoto kubwa ni kwamba karibu kila platform ya AI maarufu huhitaji malipo kabla hujaweza kufurahia huduma zake.
Kwa mfano, sehemu ya kutengeneza videoza AI mara nyingi ndiyo ghali zaidi. Kuna baadhi ya platform zikikugharimu hadi zaidi ya Tsh 200,000kwa mwezi ili upate uhuru wa kutengeneza video kwa uhuru mkubwa.
Lakini sio kila mtu ana uwezo wa kulipia gharama hizi. Wapo wanaolipia kwa sababu wanatambua thamani yake; hasa wale wanaotumia video au picha za AI kutengeneza brand zao na hata kuingiza pesa kama content creators.
Habari njema ni kwamba sio lazima ulipie! Kuna njia halali na rahisi kabisa ambayo unaweza kutumia kutengeneza picha na video za AI bure na bila kikomo.
Njia hii ni kupitia huduma ya Bing. Hii ni injini ya utafutaji (search engine) inayomilikiwa na kampuni ya Microsoft. Watu huitumia kutafuta vitu mbalimbali kama ilivyo “Google” lakini inamilikiwa na kampuni tofauti.
Ukiachilia mbali kutafuta vitu mbalimbali, katika Bing kuna sehemu ya kutengeneza Video na Picha za Ai bure(Bing Image Creator na Bing Video Creator.). Hii sehemu ndio unaweza kuitembelea ukihitaji kutengeneza video au picha bila kulipia chochote.
Bing Image Creator: Hii ni sehemu inayokuwezesha kutengeneza picha za AI bure kabisa. Unachotakiwa kufanya ni kutembelea tovuti ya Bing(au Google) na kisha kutafuta “Bing Image Creator”. Hapo utaweza kuandika maelezo ya aina ya picha unayoitaka na AI itakutengenezea papo hapo.
Bing Video Creator: Kama unataka video, unaweza kutumia “Bing Video Creator”. Hii pia inapatikana mtandaoni bure kupitia Bing. Unachotakiwa kufanya ni kutafuta jina hilo kwenye Bing au Google, kisha utaelekezwa kwenye sehemu ya huduma hiyo.
MUHIMU KUJUA: Ili kutumia huduma hizi, utahitaji kuwa na akaunti ya Microsoft. Kama tayari unayo, unaweza kuingia moja kwa moja. Kama huna, unaweza kufungua akaunti mpya bure kabisa.
Kwa hiyo, kama umekuwa ukitaka kutengeneza picha na video za AI bure bila kikomo, usihangaike tena na gharama kubwa. Bing imekuletea suluhisho kwenye hili.
AI(Artificial Intelligence) ni nini? Kwa Kiswahili huwa tunaita “Akili Bandia” na ni teknolojia inayoruhusu mashine au kompyuta kufanya maamuzi, kuchambua taarifa, na kutabiri matokeo kama vile binadamu. Hivi sasa Teknolojia ya Ai inawekwa katika sehemu mbalimbali ili kurahisisha mambo ambayo yalikua si rahisi kwa kila mtu kuyafanya. Imerahisisha mambo ya kuedit picha, kuunda video, kuandika na hata kwenye maswala ya kubeti pia.
AI hutumia data kubwa/taalifa nyingi, hesabu, na mifumo ya machine learning ili kutoa matokeo yenye usahihi wa kiwango cha juu.
Katika ulimwengu wa michezo na kubeti, AI hutumika kuchambua takwimu za mechi, historia ya timu, wachezaji, hali ya hewa, na hata mienendo ya dau (betting patterns) ili kutoa mapendekezo bora zaidi.
“Mikeka ya uhakika” ni neno linalotumika na wapenzi wa kubeti kumaanisha mikeka iliobashiri mechi zenye nafasi kubwa ya kushinda. Kwa kawaida, mikeka hii inatokana na uchambuzi wa kitaalamu wa michezo.
Hata hivyo, ni muhimu kuelewa kuwa hakuna dau lenye uhakika wa 100%, bali mikeka ya uhakika inamaanisha uwezekano mkubwa wa kushinda kulingana na uchambuzi ila lolote lisilotarajiwa linaweza kutokea.
Kupata mikeka ya uhakika kwa kutumia AI
Kama ilivyo katika sehemu nyingine, AI imeleta mapinduzi kwenye ulimwengu wa kubeti pia. Kwasasa kupitia platform za Ai za ubashiri, unaweza tumia kupata mkeka wa uwakika uliochambuliwa kitaalamu bila kupoteza muda sana. Huduma au platform hizi maalum hutoa uchambuzi wa haraka na sahihi uliofanywa na AI.
Kuna watu hivi sasa huwa wanatumia Ai katika kupata mikeka ya kubeti na hushinda baadhi ya mikeka yao. Hii imetusukuma sisi kukupa mwanga juu ya hili na pia tumekuandalia video inayofudisha jinsi ya kutumia AI kupata mikeka ya uhakika.
Haya ni Matokeo yaliobashiriwa na Ai kisha yakawa kweli kwa 100% baada ya mechi kuchezwa.
Ukihitaji video inayofundisha hayo kwa kina, unaweza kuipata kupitia WhatsApp. Utalipia Tsh 9000 TU kupata masomo haya lakini baada ya kujifunza utakua na uwezo wa kutengeneza mikeka yako kwa Ai na kushinda kirahisi.
Kiufupi Ai imekua msaada katika kupata mikeka uwakika kwa haraka ingawa haiwezi kukupa ushindi kwenye kila mkeka.
Yani inaweza kuongeza nafasi zako za kupata mikeka ya uhakika maana AI uondoa upendeleo na kutumia data kubwa au taalifa nyingi ambazo so rahisi kwa binadamu kuzifikilia kwa muda mfupi.
Kwa muda sasa, utengenezaji wa video umekuwa kazi ngumu inayochukua muda na kuhitaji ujuzi wa camera au programu za kuedit video. Hata hivyo, maendeleo ya haraka katika teknolojia ya akili ya bandia (AI) yamefungua njia mpya zinazorahisisha mambo katika utengenezaji wa video. AI inaweza kuwa ni zana nzuri katika kutengeneza au kuunda video.
Zana za AI au “AI tools” za sasa zinaweza saidia kuunda video za ubora wa juu kwa kutumia tu maandishi au picha kama wazo au chanzo cha video unayohitaji kuiunda. Yani jambo muhimu unalotakiwa kuwa nalo ni wazo la video unayohitaji tu.
AI zinaweza kutumika kuunda aina mbalimbali za video, kwanzia video za matangazo ya uuzaji wa bidhaa mpaka mafunzo ya elimu kuhusu mambo mbalimbali. Mbali na hayo, zinaweza kuunda video za watu halisi au video za katuni. Hii inafanya AI kuwa msaada kwa watu na kutengeneza video mtandaoni na hata biashara zinazotafuta njia ya ubunifu ya kuwasilisha ujumbe kwa wateja.
Hapa kwenye ukurasa huu, hatutazungumzia sana kuhusu “Jinsi ya kutengeneza au kuunda video kwa maandishi au picha“. Hatuta fanya hivyo kwakua, tumeisha zungumza hilo kwenye makala nyingine. Kwenye hii kurasa tutaangalia AI tano za kutengeneza Video kwa maneno au picha. Orodha hii chini, imewekwa kumrahidishia mtu yoyote anaehitaji huduma ya AI za kutengeneza au kuunda Video.
AI 5 za kutengeneza Video kwa maneno au picha
kling AI
Kling ni platform ya AI ambayo inatumika kutengeneza Video pamoja na ukuunda picha. Yani unaweza itumia kling AI kuunda Picha unayoifikilia au video unayoiihitaji. Katika upande wa kutengeneza Video, ni kati ya AI nzuri sana ndio maana utumeiweka katika orodha hii.
Inakuruhusu kutengeneza video kwa kutoa maelezo maandishi na Picha. Unaweza pata huduma ya kufanya hivyo Bure kabisa lakini ukihitaji uhuru zaidi katika utengenezaji wako wa video, unaweza lipia. Kling, imetengenezwa na kikundi kinachojihusisha na AI Cha kampuni ya Kuaishou Technology. Kampuni hii ni moja ya Makampuni ya kichina yaliojikita katika ulimwengu wa kidigitali.
Invideo AI
InVideo ni platform nyingine ya kiteknolojia linalotumia akili bandia(AI) kuunda video kwa maelezo ya maandishi tu. Kupitia Invideo, Mtumiaji au Watumiaji wanaweza kuunda video zilizokamilika zinanohusu mambo mbalimbali. Mfumo wake wa kutengeneza Video upo tofauti kidogo na AI kama Kling AI. Hii inatumika kutengeneza video zinazoelezea mambo. Mfano; Unaweza tengeneza Video inayoelezea Historia ya kampuni ya Google na hiyo video ikwa imejumisha picha na sauti zinazoielezea. Unaweza Clone sauti yako ikawa inatumika kwenye video unazotengeneza. Watu wengi huitumia kutengeneza video za makala mbalimbali alafu huziweka video hizo kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook na TikTok.
Midjourney
MidJourney ni platform ya Artificial intelligence (Akili bandia) linayoweza kutumika kuunda Video kwa kutumia maandishi (text prompts). Ina huduma nyingine ya kuunda Picha lakini pia mbali na hiyo, inaweza tumika kuunda Video kwa maelezo yako ya maandishi au picha. Watumiaji wanaandika maelezo ya video wanayotaka, na AI ya MidJourney inaunda Video nzuri kulingana na maelezo hayo. Hii inawapa watumiaji nafasi ya kubuni michoro na miundo mbalimbali bila hitaji la ujuzi wa kubuni. Ni maarufu sana kwa watu wanaojihusisha na utengenezaji wa content mtandaoni kwa sababu ya uwezo wake.
Veed
Hii Veed ni platform inayoendana kidogo na Invideo hivi. Ni moja ya AI zinazotumika kutengeneza video kusoma mambo mbalimbali. Veed kwa ujumla inavipengele vingi vinavyohusu video. Katika vipengele vyake, kuna kipengele kidogo kinamruhusu Mtumiaji kuunda Video kwa maelezo ya maandishi tu na unapata matokeo ambayo ni Video. Watu wangi hutumia AI za muundo huu kuunda Video kwaajili ya YouTube channel, Facebook, Instagram na TikTok.
Aitubo
Aitubo ni platform nyingine ya akili bandia (yaani AI) inayounda picha na video za ubora wa juu kutoka kwa maandishi. Katika Aitubo, watumiaji wanaweza kuunda picha au video kwakutoa maelezo ya maandishi.
Kwenye orodha hii, Naweza kuifananisha kidogo na Kling AI au Midjourney kwasababu zinaendana. Haziendani kwa Kila kitu lakini kama unahitaji AI ambayo inafanya kazi kama Kling AI na Midjourney, basi Aitubo inaweza kuwa chaguo sahihi.
Katika orodha hii kuna huduma za AI ambazo huruhusu mtumiaji kutumia bila malipo lakini ukihitaji uhuru zaidi katika AI hizo unaweza kulipia. Kling AI, Veed, Aitubo na Invideo ni mfano wa huduma hizo. Lakini pia Kuna huduma ya AI ambayo hauwezi pata kabla ya kulipia. Mfano wa huduma hii Katika Orodha yetu ni Midjourney.
Kama tunavyofahamu, AI au Akili bandia ni teknolojia inayowezesha mashine kufanya kazi zinazohitaji akili za kibinadamu, kama vile kutambua picha, kuelewa lugha, na hata uundaji wa content (maudhui). Hivi sasa, unaweza kutumia AI kutengeneza Video kwa kutumia picha flani au kuelezea video unayohitaji kwa maandishi pekee.
Yani kama unapicha unayotamani iwe ni video, AI inaweza fanya hivyo kwaajili yako. Na pia uweza kuipa maelezo kuhusu video unayohitaji kwa maandishi tu na ikakuundia hiyo. Kuna huduma nyingi kwasasa zinawawezesha watu kutengeneza video kwa kutumia AI na video hizo zimesambaa sana mtandaoni. Kama ni mtu wa mitandao, unaweza kuwa tayari umewahi kuona video nzuri na ukaambiwa imetengenezwa na AI.
Kwa sasa Ulimwengu wa video za mitandaoni umekua ukihusisha sana AI katika kutengeneza video. Watu wanaotengeneza video katika YouTube, TikTok, Instagram na hata Facebook wamekua wanatumia sana AI kipindi hiki.
Sababu kubwa ya watu kutumia AI katika kutengeneza Video ni kuokoa muda na gharama pia. Mtu unaweza tumia AI ndani ya dakika 1 kutengeneza Video ambayo ingechukua pesa nyingi au siku nyingi.
Mfano; kwa kawaida ukihitaji video inayoonesha uwanja wa ndege na ndege zinavyoruka angani, utatakiwa kuingia gharama za kupata kamera, kupata kibali cha kuchukua video sehemu flani katika uwanja wa ndege. Hii inaweza kukuchukua siku kadhaa ili kukamilisha wazo zima la video yako. Lakini kupitia AI, unaweza tengeneza Video hiyo ya uwanja wa ndege kwa dakika moja tu kwa kutumia hata simu ya mkononi.
Kwaiyo, AI Inafanya kuokoa muda, kupunguza gharama za uzalishaji wa Video, na kutoa fursa za ubunifu pia.
Jinsi ya kutengeneza Video kwa maneno au picha kwa kutumia AI
Huduma za AI zinazowezesha watu kutengeneza video kwa AI zipo nyingi sana mtandaoni kwa sasa na zipo tofauti. Ukihitaji kutengeneza video kwa AI unatakiwa kwanza kuchangua huduma utakayotumia kufanya hivyo. Kwa hapa The bestgalaxy, tunakuelekeza Jinsi ya kutengeneza Video kwa kutumia KLING AI.
KLING AI imetengenezwa na kumpuni ya kichina iitwatwayo Kuaishou Technology. Imekua ikitumika kutengeneza video zinazo trend ikiwemo ile ambayo mahindi yanageuka kuwa samaki(kama umewahi ona unaweza nielewa). KLING AI inawawezesha Watumiaji wake kuunda Video wanazozihitaji kwa kuweka picha au maelezo ya maandishi tu. Yani ukiipatia Picha ya watu wanaocheza Mpira, itakupa video ya watu waliopo kwenye picha wakicheza mpira. Na ukiipa maelezo ya maandishi yanayahusu kutengeneza “video ya watu wakicheza mpira” itakupatia video ya watu wakicheza mpira kama ulivyoeleza. Lakini lugha ya kiingereza ni Lugha unayotakiwa kuitumia ili kupata matokeo mazuri.
Huduma hii hutoa nafasi kidogo kwa watu kuitumia Bure kila siku lakini ukihitaji uhuru zaidi, utahitajika kulipia. Unataka kuijaribu KLING AI? Fuata hatua zifuatazo kuanza kutengeneza Video kwa maneno au picha na KLING AI bure kabisa.
Tengeneza Akaunti Akaunti ikikamilika, Chagua “AI videos” katika ukurasa wa kwanza.
Baada ya kufanya hayo, utaletwa kwenye ukurasa wenye upande ulioandikwa “Text to Video” na upande “Image to Video”
Upande ulioandikwa “Text to Video” utakua ukiutumia kutengeneza Video kwa kutoa maelezo ya maandishi ya video unayohitaji.
Upande ulioandikwa “Image to Video” utakua ukiutumia kuweka Picha unayohitaji ibadilishwe kuwa video(kubadili picha kuwa video). Mbali na picha, unaweza ongezea na maelezo ya maandishi katika sehemu hii ili Video inayotoka iwe ni video unayohitaji.
Mbali na KLING AI, kuna AI nyingi mno ambazo watu hutumia kutengeneza video ikiwemo Midjourney(unalipia kuitumia). Tutakua tukizungumzia AI hizi na nyingine nyingi kwenye makala nyingine, Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy.
Utengenezaji wa Logo ni ubunifu wa kutengeneza alama zinazotambulisha biashara, huduma, au bidhaa mbalimbali. Logo ni moja ya nyenzo muhimu katika kujenga utambulisho wa chapa, na inachangia sana katika kuvutia wateja na kuweka mtazamo mzuri wa watu kuhusu biashara au huduma fulani. Kutokana na maendeleo ya teknolojia, sasa kuna njia nyingi za kutengeneza logo, na moja ya njia hizo ni kutumia akili bandia (AI).
Kutumia AI katika kutengeneza logo ni njia inayozidi kupendwa na kupata umaarufu kutokana na AI kurahisisha mchakato wa kutengeneza Logo. Kiufupi kutumia AI hurahisha na kuokoa muda ambao mtu angetumia kutengeneza Logo kwa uwezo wake au kwa watu wengine. Al inaweza tengeneza Logo nzuri ndani ya dakika 2 tano tu na ukaanza kuitumia.
Teknolojia hii inasaidia kuondoa changamoto mbalimbali ambazo wabunifu(Graphics designers) wamekuwa wakikabiliana nazo kwa muda mrefu. Mbali ya kuwasaidia wabunifu, Teknolojia hii inamuwezesha mtu yoyote kutengeneza Logo kwa matumizi yake binafsi.
Katika makala hii, tutaangazia jinsi ya kutumia AI kutengeneza Logo. Tunaenda kuelekeza jinsi unaweza tengeneza Logo kwa kutumia AI inayofahamika kama “Copilot” au “Bing AI image creator” Bure kabisa. Unaweza fanya yote utayoelekezwa kwa kutumia simu yako au PC.
Jinsi ya kutengeneza Logo yako binafsi au Biashara kwakutumia AI.
Kuna huduma nyingi za AI unaweza tumia kutengeneza Logo. Ila hapa tutakueleza jinsi ya kuunda Logo kwa kutumia huduma ya Bing AI image creator (Copilot). Ni huduma inayoweza kutumika kuunda Logo binafsi au ya biashara bila malipo. Ni kitu kizuri maana huduma nyingi hazitoi nafasi ya Bure kama hii.
Ukihitaji kutengeneza Logo kwa kutumia AI hii, chukua simu au PC yako na ufuate hatua zifuatazo:
Ingia Google kwa kutumia web browser yako Kisha Tafuta “Bing AI image creator”.
Baada ya hapo, ingia kwenye matokeo utakayoyaona juu kutoka Bing.
Kabla ya kufanya jambo lote utatakiwa kutengeneza akaunti kwakubonyeza kitufe chenye neno “Join”. Akaunti inayotumika hapa ni akaunti ya Microsoft.
Baada ya kuweka akaunti sawa, utarudishwa kwenye ukarasa ambao unasehemu ya kuandika unachotaka kuunda. Kwakua unataka kuunda Logo, unaweza ukaandika maelezo ya logo unayoitaka. Ila ili upate matokeo mazuri unatakiwa kutumia kiingereza. Kwa mfano; Nikitaka kutengeneza logo ya jina “Mabano Shop” Naweza kuandika “””””Logo of words “Mabano Shop” and make it as transparent Logo.””””” Alafu ukabonyeza “Kitufe kilichoandikwa “Create”.
Baada ya kubonyeza kitufe hicho utaletewa picha za Logo zilizotengeneza kwaajili yako. Utatakiwa kuchagua logo utakayoipenda na kuipakua/download kwenye simu yako au PC.
Ukitaka kudownload logo hiyo kwenye simu, utaichagua kwakuigusa kisha utagusa vidoti vitatu vilivyopembeni ya picha ulioichagua alafu utabonyeza Download. Na kwenye PC, utaichagua tu na kubonyeza Download moja kwa moja.
Ili kupata matokeo mazuri unatakiwa uandike vizuri maelezo ya Logo yako. Unaweza toa maelezo zaidi ya niliotoa mimi hapo juu. Yani unaweza sema hata Logo unayoitaka ni kwaajili ya nini ili AI inaipotengeza, itengeze Logo inayoendana na jambo unaloenda kufanyia. Mfano; Kama Logo inahusu kuvua samaki basi unaweza kuweka neno “Logo is about fishing” kwenye maelezo yako. Jitahidi kuandika maelezo kwa ufupi maana AI Bado hazipo vizuri kwenye kuelewa unachokitaka.
Al ni nzuri katika kuzitengeneza Logo lakini kuna makosa madogo madogo inaweza yafanya katika kuunda Logo. Kama ni mtu mwenye ujuzi wa ku-edit picha, unaweza tumia ujuzi wako kuboreshwa au kurekebisha baadhi ya makosa yaliopo kwenye logo iliotengenezwa na Al. Graphics designer au Mtu mwenye ujuzi wa ku-edit picha anaweza tengeneza Logo ya AI yenye ubora zaidi.
Teknolojia ya akili bandia (AI) imekuwa inaleta mabadiliko kwenye pande nyingi duniani, na suala la AI kuchukua ajira za watu limezua mjadala mkubwa miongoni mwa watu. Kuna watu wengi wanahofia kwamba AI itasababisha watu wengi kupoteza kazi. Swala hili limeongelewa na watu wengi sana lakini pamoja na yote, Teknolojia ya AI inaonekana haiwezi ondolewa Duniani kwa sasa. Teknolojia hii inaendelea kuboreshwa kila siku na inaingizwa kwenye pande mbali mbali zinazohusu maisha ya binadamu. Na inasemekana kuwa Teknolojia ya AI haitaondoka, itaendelea kuwepo tu hapa Duniani.
Hapa The bestgalaxy, tunaenda kujalibu kuchimba kidogo juu ya swala hili ili kukujuza kiundani kuhusu AI na ajira za watu. Tumefanya hivi ili kutoa mwanga kwa watu wasiolielewa swala hili vizuri.
Fahamu kuhusu AI kuchukua Ajira za watu
Ni kweli AI inachukua Ajira za watu?
Kuna vitu au Mashine zinazotumia AI zina uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na haraka kuliko au kama binadamu. Kadri siku zinavyo zidi kwenda, Teknolojia ya AI inakua Bora na kufanya vitu au Mashine hizo kuongezeka idadi na kuwa bora pia. Kuna Makampuni huvutiwa na vitu au Mashine za Teknolojia ya AI na kuanza kuzitumia badala ya kuajili binadamu. Swala hili hufanywa ili waepuke gharama za kuwalipa watu na pia hufanya mambo yao yaende haraka kuliko ambavyo wangetumia binadamu. Kwa maelezo mengine hapa tunaweza sema AI inachukua Ajira za watu.
Inasemekana kuwa asilimia 60 ya kazi au Ajira zinaweza chukuliwa na AI. Na swala ya AI kuchukua Ajira ni jambo ambalo linaongelewa kwa uwazi kabisa hata na AI zenyewe.
Watu wanatakiwa kufanya nini?
Watu wanapaswa kuelewa kwanza AI itaendelea kuwepo na kuleta matokeo mengi kwenye maisha ya binadamu ikiwemo upande huu wa Ajira au kazi. Lakini kitu cha muhimu ni kuondoa hofu kisha kujifunza mambo ya AI ili kujua upande wako utaathiriwa vipi kwasasa au miaka ijayo.
Mtu unashauriwa pia kuiweka akili yako sawa na kuwa tayari kujifunza vitu vipya au ujuzi. Katika vitu unavyotakiwa kujifunza ni kuitumia AI maana AI inaweza tumika na mtu yoyote kufanya mambo ya maana yatakayokuingizia kipato pia au kuiboresha kazi hiyo hiyo unayoifanya. Kiufupi kitu kimoja cha AI kinaweza chukua ajira ya mtu alafu hapo hapo kitu kingine cha AI kinaweza kuwa kimerahisisha au kuzalisha kazi nyingine ambayo mtu huyo anaweza ifanya. Kuijuia hiyo kazi au fulsa itakuitaji kufungua akili yako kwenye ujuzi mpya. Na hii ndio sababu ya The bestgalaxy kusikiliza watu kufuatilia AI.
Katika dunia ya sasa maendeleo ya Teknolojia makubwa yamewezesha wataalamu kuunda robot zinazofanana na binadamu. Robot zilizoundwa kwa mfano wa Binadamu zinaitwa humanoid. Safari ya kutengeneza robot za muundo huu zilianzishwa muda kidogo na wataalamu mbalimbali na mpaka kufikia sasa Kuna uwepo wa robot zenye uwezo mkubwa ukilinganisha na kipindi cha nyuma. Kufuatia uwepo wa Teknolojia ya AI (Akili bandia) robot nyingi zilizo undwa kwa mfano wa Binadamu zimekua na uwezo mkubwa katika kuingiliana na binadamu halisi. Teknolojia ya AI ni kama inafanya kuzipa akili robot za humanoid na kuziwezesha kufanya baadhi ya mambo kama binadamu.
Kadri Teknolojia ya AI inavyoendelea kukua ndio robot za Humanoid zinaendelea kuwa na uwezo mkubwa katika kufanya mambo kama binadamu. Inasemekana Teknolojia ya AI ikifika katika hatua za juu, humanoid robot zinaweza kuwa na uwezo mkubwa kuliko binadamu kwenye kufanya mambo mengi. Na pia tunaweza fikia wakati robot za mfano wa Binadamu zikaweza jichanganya na binadamu kufanya shughuli mbalimbali katika Maisha ya kila siku. Inasemekana wakati huo roboti hizi za humanoid zitakua nyingi na zitakua zikitoa msaada na huduma katika sekta tofauti. Zinaweza kuwa kwenye huduma za afya, elimu, viwanda na hata burudani.
Roboti za humanoid nyingine tayari zimeanza kuwa sehemu ya maisha ya binadamu kwasasa. Kuna robot za muundo huu ambazo tayari zinafanya kazi au kutoa huduma. Katika makala hii hatuta chimba sana kuhusu robot za humanoid sana. Kwasasa hebu tuangalie robot chache za humanoid zilizo tengenezwa vizuri Duniani.
Robot 5 zilizoundwa kama Binadamu (Humanoid)
Ameca
Ameca ni roboti lililoundwa kama binadamu wa kiume linalojulikana kwa uwezo wake wa kuingiliana na binadamu. Imetengenezwa na kampuni ya Engineered Arts ya Uingereza. Ameca imewezeshwa na teknolojia ya hali ya juu ya AI kuweza kuelewa na kujibu mambo katika maongezi inayoyafanya na binadamu. Anauwezo wa kuona na kutambua vitu anavyo viona kupitia camera zilizoundwa kama macho. Katika lugha, Ameca huelewa na kuzungumza lugha zaidi ya moja.
Sophia
Sophia ni roboti mwingine ambae amekuwa na umaarufu sana duniani. Aliwahi kuzua gumzo baada ya kutamka kuwa atawaharibu wanadamu. Sophia alipokua katika mahojiano CNBC alijibu “Okay, I will destroy humans,” alipokua aliulizwa kuhusu kuharibu wanadamu. Sophia robot yupo vizuri sana katika maongezi na hii ni Kwasababu umewezeshwa na Teknolojia ya juu ya AI. Anapoongea sauti inayotoka ni ya kike na hata sura pia Kwasababu ameundwa kuwa roboti wa kike. Aliundwa na kampuni ya Hanson Robotics.
Atlas
Atlas ni humanoid robot alieletwa na kampuni ya Boston Dynamics kwaajili ya kufanya kazi zinazohitaji nguvu na usahihi. Huwezi muweka katika kundi la Sophia robot au Ameca huyu maana yeye umeundwa kwaajili ya mambo yanayo jumuisha kukimbia, kuruka na kubeba vitu. Ni robot mwenyewe Teknolojia ya juu inayomuwezesha kufanya vitendo mbali mbali kama binadamu mkakamavu. Anaweza hata kuruka sarakasi ya kujirusha na kujigeuza hewani bila kugusa chini na akatua salama.
Optimus
Optimus ni robot alietengenzwa kwaajili ya kusaidia katika shughuli mbalimbali kama vile kazi za nyumbani, viwandani na maeneno mengine kama hayo. Robot hili hufahamika pia kama Telsa bot, ni moja ya robot maalufu katika Ulimwengu wa Teknolojia. Limetengenezwa na kampuni ya Telsa ambayo ipo chini ya Elon musk ambae ni mmiliki wa mtandao wa X. Optimus anaweza kuwa sehemu muhimu ya nguvu kazi katika Maisha ya baadaye, kwa kuwasaidia binadamu kupunguza mzigo wa kazi za kila siku.
Jia Jia
Huyu ni roboti wa kike wa kibinadamu aliyeundwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha huko China. Alizinduliwa rasmi mwaka 2016 na anajulikana kwa sura yake ya kuvutia na uwezo wa kuingiliana na binadamu katika maongezi. Imeundwa ili kuonekana kama binadamu, na yupo vizuri katika kusikiliza na kujibu maswali anayouliza na binadamu.
Roboti hizi zinaweza fanya mambo mengi kama binadamu lakini kiukweli robot hizi bado hazipo sawa kwa 100%. Kuna makosa na mambo mengi ambayo unaweza uoneshwe kwenye video au mitandao ya kijamii lakini fahamu kuwa kuna makosa yanafanywa na robot hizi. Zinaweza fanya makosa katika kujibu maswali au kufanya matendo.